CHATANDA AWAOMBA WANANCHI KUMCHAGUA BAHATI NDINGO MBUNGE WA MBARALI


Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania UWT, Mary Chatanda amewaomba wananchi wa Mbarali kumpa kura za ndio, Bahati Ndingo ambaye ni mwanamke msikivu ,mpenda maendeleo makubwa katika kukuza uchumi wa Mbarali mkoani Mbeya.

Mwenyekiti Chatanda amesema, 'Sisi kama wanawake Wilaya ya Mbarali tuwaombe wanaume zetu usiku na mchana katika kuunga juhudi za mwanamke kwa kumpa kura za ndio Mgombea wetu wa Ubunge Jimbo la Mbarali.

"Mwanamke ndio Jeshi la familia na niwahakikishie  mmepata mwanamke shupavu na atawaongoza kikamilifu ndani ya Wilaya yetu msifanye makosa chagua Bahati Ndingo kwa Maendeleo ya Mbarali.

"Mimi kama Mwenyekiti wetu wa Wanawake Tanzania niwaombe wananchi wa Mbarali ifikapo tarehe 19/9/2023 msifanye makosa mchague Chama Cha Mapinduzi ,mchague mgombea Bahati Ndingo awe  Mbunge wa Mbarali".

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post