TALGWU YATOA MAFUNZO KWA WAAJIRI HALMASHAURI ZA WILAYA MKOA WA SHINYANGA KUBORESHA MAZINGIRA YA WAAJIRI NA WAAJIRIWA

Mwenyekiti wa TALGWU na Rais wa Chama Cha Wafanyakazi Tanzania (TUCTA, Tumaini Nyamhokya

Na Kadama Malunde – Malunde 1 blog

Chama cha Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa Tanzania (TALGWU) kimetoa mafunzo kwa Waajiri wa Halmashauri za Wilaya Mkoa wa Shinyanga kwa ajili ya kuwajengea uwezo kuhusu masuala mbalimbali ya Vyama vya Wafanyakazi.

Semina hiyo ya siku moja imefanyika leo Jumatano Septemba 20,2023 Mjini Shinyanga na kukutanisha pamoja viongozi wakuu wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa Tanzania (TALGWU) na Waajiri wa Halmashauri za Wilaya (Wakurugenzi wa Halmashauri na Wakuu wa Rasilimali watu kutoka Halmashauri za wilaya Mkoani Shinyanga.

Akizungumza wakati akifungua Semina hiyo, Mgeni rasmi Kaimu Katibu Tawala Msaidizi Sehemu ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu Mkoa wa Shinyanga, Manyama Katikiro  amesema mafunzo hayo yatasaidia kuongeza mahusiano mazuri baina ya TALGWU na waajiri ili kuboresha mazingira ya waajiriwa.

“Mafunzo haya yanasaidia kuimarisha mahusiano baina ya vyama vya wafanyakazi na waajiri ili kuleta tija katika utoaji wa huduma kwa jamii”,amesema Katikiro.
Kaimu Katibu Tawala Msaidizi Sehemu ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu Mkoa wa Shinyanga, Manyama Katikiro.

“Tunataka ustawi wa watumishi siyo kudumaza watu, naomba tuendelee kushirikiana na kushikamana ili kufikia malengo ya kuleta tija katika taifa letu tukitawaliwa na hekima na busara badala ya mihemko”,ameongeza Katikiro.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa TALGWU na Rais wa Chama Cha Wafanyakazi Tanzania (TUCTA, Tumaini Nyamhokya  amesema mafunzo hayo yatasaidia kupunguza migogoro baina ya waajiri na waajiriwa.
    
“TALGWU imejitahidi sana kupunguza migogoro baina ya waajiri na waajiriwa, tunaendelea kutengeneza mazingira mazuri kwa wafanyakazi ikiwa ni pamoja na kuhakikisha maslahi yao yanaboreshwa. Naomba tuendelee kushirikiana na kushikamana ili twende pamoja”,amesema.

“Mafunzo haya yanaimarisha mahusiano yetu Chama na Waajiri. Sisi ni wamoja hatutakiwi kutengana bali tunapaswa kujenga ili kutatua changamoto za wafanyakazi lengo kubwa pia  ni kupunguza migogoro kati ya waajiri na waajiriwa”,ameongeza Nyamhokya.
  Naye Katibu Mkuu wa TALGWU,  Rashid Mohamed Mtima amesema wametoa semina kwa Wakurugenzi wa Halmashauri na Wakuu wa Rasilimali watu kutoka Halmashauri za wilaya ili waweze kufahamu masuala mbalimbali ya Vyama vya Wafanyakazi kwa sababu wao ndiyo wasimamizi wa wafanyakazi katika maeneo ya kazi kwenye Halmashauri.

“Mafunzo haya yameanzia katika mkoa wa Shinyanga na tutatoa mafunzo kwenye mikoa mingine nchini kuhusu vyama vya wafanyakazi ili kuweka mazingira salama kwenye maeneo ya kazi kwa kuimarisha mahusiano mazuri baina ya waajiri na waajiriwa”,ameongeza.

Nao washiriki wa mafunzo hayo akiwemo Mkurugenzi wa Halmashauri ya Msalala,Hamis Katimba na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Kishapu, Emmanuel Johnson wamesema mafunzo hayo yamewajengea uwezo kuhusu namna ya kushughulikia masuala ya wafanyakazi ili kupunguza migogoro kwenye maeneo ya kazi.

ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Kaimu Katibu Tawala Msaidizi Sehemu ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu Mkoa wa Shinyanga, Manyama Katikiro akizungumza wakati akifungua mafunzo kwa Waajiri wa Halmashauri za Wilaya Mkoa wa Shinyanga kwa ajili ya kuwajengea uwezo kuhusu masuala mbalimbali ya Vyama vya Wafanyakazi leo Jumatano Septemba 20,2023 Mjini Shinyanga. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Kaimu Katibu Tawala Msaidizi Sehemu ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu Mkoa wa Shinyanga, Manyama Katikiro akizungumza wakati akifungua mafunzo kwa Waajiri wa Halmashauri za Wilaya Mkoa wa Shinyanga kwa ajili ya kuwajengea uwezo kuhusu masuala mbalimbali ya Vyama vya Wafanyakazi

Mwenyekiti wa TALGWU na Rais wa Chama Cha Wafanyakazi Tanzania (TUCTA, Tumaini Nyamhokya akizungumza wakati wa mafunzo kwa Waajiri wa Halmashauri za Wilaya Mkoa wa Shinyanga kwa ajili ya kuwajengea uwezo kuhusu masuala mbalimbali ya Vyama vya Wafanyakazi

\Mwenyekiti wa TALGWU na Rais wa Chama Cha Wafanyakazi Tanzania (TUCTA, Tumaini Nyamhokya akizungumza wakati wa mafunzo kwa Waajiri wa Halmashauri za Wilaya Mkoa wa Shinyanga kwa ajili ya kuwajengea uwezo kuhusu masuala mbalimbali ya Vyama vya Wafanyakazi
Mwenyekiti wa TALGWU na Rais wa Chama Cha Wafanyakazi Tanzania (TUCTA, Tumaini Nyamhokya akizungumza wakati wa mafunzo kwa Waajiri wa Halmashauri za Wilaya Mkoa wa Shinyanga kwa ajili ya kuwajengea uwezo kuhusu masuala mbalimbali ya Vyama vya Wafanyakazi
Katibu Mkuu wa TALGWU,  Rashid Mohamed Mtima akizungumza wakati wa mafunzo kwa Waajiri wa Halmashauri za Wilaya Mkoa wa Shinyanga kwa ajili ya kuwajengea uwezo kuhusu masuala mbalimbali ya Vyama vya Wafanyakazi

Naibu Katibu Mkuu wa TALGWU,  Wandiba Kongolo akizungumza wakati wa mafunzo kwa Waajiri wa Halmashauri za Wilaya Mkoa wa Shinyanga kwa ajili ya kuwajengea uwezo kuhusu masuala mbalimbali ya Vyama vya Wafanyakazi
Mafunzo kwa Waajiri wa Halmashauri za Wilaya Mkoa wa Shinyanga yaliyoandaliwa na TALGWU kuhusu masuala mbalimbali ya Vyama vya Wafanyakazi yakiendelea

Mada zikiendelea kutolewa wakati Mafunzo kwa Waajiri wa Halmashauri za Wilaya Mkoa wa Shinyanga yaliyoandaliwa na TALGWU kuhusu masuala mbalimbali ya Vyama vya Wafanyakazi 
Viongozi wa TALGWU wakipiga picha ya kumbukumbu na Waajiri wa Halmashauri za Wilaya Mkoa wa Shinyanga.

Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post