Habari Njema!! SAFIRI KWA MABASI YA MKOMBE LUXURY KUTOKA DAR-ES SALAAM HADI AFRIKA KUSINI KWA BEI POA KABISA

Habari njema na za kufurahisha kwa sasa watanzania wanaweza kusafiri kwa raha mustaree kwa usafiri wa basii kutoka Dar-Es-Salaam hadi Johannesburg,Afrika Kusini kwa kutumia mabasi mapya kabisa aina ya kampuni ya kizalendo ya Kitanzania Mkombe Luxury Bus ambayo ina makao yake Johannesburg Afrika kusini, Kampuni hiyo kitanzania imekuja na suluhisho la kurahisisha Safari za kutoka hapa nchini Tanzania hadi Afrika Kusini.

Kwa sasa wasafiri wa Tanzania na Afrika Kusini wanaweza kutumia usafiri huo wa Mkombe Luxury Bus ambao nauli yake ni Tsh 350,000 za kitanzania kwa safari moja na wanaweza kulipia nauli ya Tsh,700,000 (laki saba) kwenda na kurudi.

Kampuni hiyo imefungua ofisi zake mtaa wa Shekilango jijini Dar-es-salaam ambapo tiketi zinapatikana pia wanapatikana kwa whatsapp +27604749717.

Wasafiri wa Tanzania na South Africa wanaweza kutumia usafiri kwa kupitia Zambia, maporomoko ya maji ya Victoria Falls, Zimbabwe hadi Johannesburg Afrika Kusini basi linachukua siku tatu hadi Afrika kusini.

Kampuni hiyo ya kizalendo Mkombe imekuja kurahisisha usafiri wa kwenda na kurudi hadi Afrika Kusini na pia wana magari ya kusafirisha mizigo. 

Safiri kwa Raha na Mkombe Luxury Bus ambayo ndani yana Choo,TV na WiFi ya internet safarini kote. Unaposafiri na usafiri huu Luxury Mkombe Bus ni Utalii Tosha.



Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post