BILIONI 40.4 ZATEKELEZA MIRADI YA MAENDELEO KISHAPU... ELIMU SEKONDARI YAFANIKIWA 100%


Mkuu wa Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga, Joseph Mkude akitoa taarifa ya tathmini ya utekelezaji miradi mbalimbali ya maendeleo
Mkuu wa Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga, Joseph Mkude akitoa taarifa ya tathmini ya utekelezaji miradi mbalimbali ya maendeleo
Mkuu wa Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga, Joseph Mkude akionesha kikombe cha tuzo ya utunzaji mazingira na upandaji miti ili kukabiliana na mabadiliko tabia nchi na kupunguza ukame Wilayani Kishapu mkoani Shinyanga

Na Sumai Salum  - Kishapu 
Jumla ya shilingi Bilioni 40.4 kwa mwaka wa fedha 2022/2023 zimetumika kutekeleza shughuli mbalimbali za miradi ya maendeleo wilayani Kishapu mkoani Shinyanga.

Akitoa taarifa ya tathmini ya utekelezaji miradi ya maendeleo mwaka wa fedha 2022/2023 na robo ya kwanza mwaka wa fedha 2023/2024 katika mkutano wake na waandishi wa habari ofisini kwake Leo Septemba 22,2023 mkuu wa Wilaya hiyo, Joseph Mkude amesema hadi sasa sekta ya elimu Sekondari imefikisha lengo la utekelezaji wake kwa asilimia 100 uliogharimu kiasi cha shilingi Bilioni 4.157.

"Tumejenga na kukamilisha ujenzi wa vyumba vya madalasa 121 na kuweka madawati 4840 katika shule ya Sekondari Ikonda,Talaga,ukenyenge,uchunga,usia,igaga,Songwa,Somagedi, Mangu,Sekeididi,Mipa,Ngofira,Mwataga,Mwamashele,Mwamala,Mwakipoya,Mwadui tech. ,Kishapu girl's,Shiteleja,Mwigumbi,Bulekela,Maganzo,Mwamadulu,lagana,Isoso,Kiloleli,Busia,Idukilo,Mwanima,Bunambiyu,Bubiki na Mwaweja, nakata zote 29 za Wilaya yetu zimefikiwa na mradi huu",amesema Mkude.

Hata hivyo Wilaya ya Kishapu imejenga na kukamilisha matundu 45 ya vyoo na kuweka miundombinu ya mji katika shule ya Sekondari Maganzo,Isoso,Kishapu na kukamilisha shule mpya moja yenye jumla ya vyumba vya madarasa 8,maabara 3,maktaba na jengo la utawala katika shule ya Sekondari Bupigi na Mwaweja.

Sambamba na hayo vyumba vya madalasa 12 vimejengwa katika shule ya Sekondari Mwataga,Talaga,Mipa,Ngofira, Somagedi, Mwakipoya na Wishiteleja na ukamilishaji ujenzi mabweni 5,nyumba za walimu 4 shule ya sekondari Ikonda.

Kwa upande wa elimu msingi wamejenga jumla ya vyumba vya  madarasa 88,madawati 1120,matundu ya vyoo 278 yenye huduma ya maji na ujenzi wa shule mpya 2 huku ujenzi wa chuo cha ufundi stadi yaani Veta Kishapu ambacho kinatoa kozi zaidi ya 5 kiligharimu kiasi cha shilingi B 2.695.

Sambamba na hayo katika sekta ya afya iliyotumika B 4.486  Wilaya imejenga na kukamilisha vituo 2 vya  afya Negezi na Mwang'arang'a katika kata ya Ukenyenge na Masanga na tayari vinafanya kazi Huku kituo Cha afya Mwamalasa kiko kwenye hatua ya ukamilishwaji.

"Tumejenga zahanati 6 na kukarabati zahanati ya Nyenze na nyumba 3 za watumishi Kalitu na tayari tumejenga matundu 24 ya vyoo na kuweka huduma ya maji Kule Uchunga,Mwamashele,Negezi pamoja na Mwadui luhumbo na pia katika hospitali yetu ya Wilaya ya Dr. Jakaya Kikwete tumejenga majengo 11 ikiwemo jengo la dharula,maabara,wodi ya wazazi,wodi ya watoto,Upasuaji,Mionzi,Stoo ya dawa,jengo la kufulia,njia za kutembelea wagonjwa,miundombinu wa jenereta wa kufuma umeme na tunaendelea na ujenzi jengo la huduma jumuishi (One Stop Center)", ameongeza Mkude.

Hivyo sekta zingine ni Mifugo na kilimo( B 1.269),Rasilimali watu na utawala bora(Mil 240), Maji (B 16.164), Maendeleo ya jamii(B 6.554) pamoja na sekta ya miundombinu ya barabara(TARURA) milioni 276 ambapo kwa mwaka wa fedha 2023/2024 Wilaya imetenga kiasi cha B 2.259 kwa ajili ya matengenezo ya Barabara,kalvati na madaraja.

Hivyo Mkude amewashukuru wananchi, asasi zisizokuwa za kiserikali pamoja na ofsi zote za serikali hasa Mkurugenzi wa halmashauri ya Kishapu Bw.Emmanuel Johnson kwa kusimamia vizuri fedha za serikali na kufikia malengo yaliyokusudiwa na serikali ya awamu ya sita ya Samia Suluhu Hassan katika utekelezaji wa ilani ya uchaguzi.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post