JAFO AAGIZA KAMPUNI ZA MADINI KUZINGATIA UTUNZAJI MAZINGIRA, AZITAKA ZIJIFUNZE KWA GGML

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Selemani Jafo (kulia) akipokea zawadi kutoka kwa Meneja Mwandamizi anayesimamia mahusiano ya jamiii kutoka GGML, Gilbert Mworia baada ya kutembelea banda la kampuni hiyo katika maonesho ya sita ya teknolojia ya madinia Geita.
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Selemani Jafo (kushoto) akimsikiliza Meneja Mwandamizi anyesimamia mahusiano ya jamii kutoka GGML, Gilbert Mworia kampuni hiyo katika maonesho ya sita ya teknolojia ya madinia Geita alipotembea banda la kampuni hiyo katika maonesho ya sita ya teknolojia ya madinia Geita.


NA MWANDISHI WETU

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Selemani Jafo ameziagiza kampuni zote nchini zinazojihusisha na uchimbajin wa madini kuzingatia taratibu na sheria zinazohusiana na mazingira ili kuisaidia Tanzania na dunia kukabiliana na janga la mabadiliko ya tabia nchi.

Ameziagiza kampuni hizo kwenda kujifunza namna Kampuni ya Geita Gold Mining Limited (GGML) inavyotekeleza sera ya utunzaji wa mazingira kwa kuwa ndio kampuni mfano inayochimba madini na kuzingatia sheria hiyo ya utunzaji mazingira.

Jafo ametoa agizo hilo leo wakati akizungumza na waandishi wa habari baada ya kupanda miti na kutembelea mabanda ya maonesho ya sita ya teknolojia ya madini yanayoendelea katika uwanja wa Bombambili-EPZ mjini Geita.

Amesema katika nafasi yake ya uwazi katika maeneo ambayo anayafuatilia kwa umakini ili kulinda mazingira ni shughuli zinazofanywa na kampuni za madini hasa ikizingatiwa uzalishaji wa dhahabu husababisha pia uwepo wa kemikali hatari kwa mazingira.


“Lakini katika kampuni ambayo inajitahidi kuhifadhi mazingira ni GGML kwa hiyo napenda kuwatia moyo kwamba muendelee na ari hiyohiyo kuhakikisha mazingira yanatunzwa.


“Kwa sababu endapo tutakuza uchumi kupitia madini lakini tusipotunza mazingira tutapa madhara makubwa… kumbukeni mabadiliko ya tabia nchi ni janga duniani. Hakuna taifa ambalo lipo salama kutokana na mabadiliko ya tabia nchi, kiwango cha joto kinaongezeka kila kukicha,” amesema Jafo na kuongeza;


“Tuendelee kukuza uchumi lakini tulinde mazingira. GGML mmendelea kuwa wadau wakubwa na sisi serikali tunahitaji wadau kama ninyi ili kushirikiana kuhakikisha nchi inasonga mbele,” amesema.

Awali akitoa salamu za mkuu wa mkoa wa Geita, Martin Shigela, Mkuu wa wilaya ya Nyang’wale, Grace Kingalame amesema kwa mwaka huu mkoa huo umepanga kupanda miti 1500.

Amesema tangu kampeni ya upandaji miti ianze, mkoa huo umekuwa kinara katika hilo na kufanikisha kupanda miti zaidi ya milioni moja.


Kwa upande wake Waziri wa Madini, Anthony Mavunde amesema atasimamia sekta hiyo kuhakikisha shughuli zote za uchaimbaji zinaendana sera ya utunzaji ji wa mazingira.

Aidha, Meneja mazingira wa GGML, Mhando Yusuph amesema mgodi huo umeweka sera ya utunzaji wa mazingira ambayo inagusa maeneo makubwa matatu.


Ametaja maeneo hayo ambayo ni kuzuia uchafuzi wa mazingira, kufuata sheria zinazohusu mazingira na kufanya maboresho endelevu katika suala la mazingira.

“Kwa hiyo kila kitu kinachofanyika ndani ya mgodi kinazingatia utunzaji wa mazingira. Tunazingatia usimamizi wa mazingira ndani ya mgodi kwa shughuli zote za uchimbaji na kuhakikisha hatuchafui vyanzo vya maji kama mito na mabwawa yaliyo ndani ya mgodi.


“Pia katika kuhakikisha sera hii inazingatiwa, huwa tunafanya upimaji wa maji yaliyopo ndani ya mgodi. Lakini piwa kwa kuwa uchimbaji unahusisha kuondoa rasilimali za miti kunapotokea eneo halitumiki tena huwa tunapanda miti,” amesema Yusuph.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post