Tazama Picha : DC JOHARI SAMIZI AONGOZA MAHAFALI YA 17 SHULE YA AWALI NA MSINGI HOPE SHINYANGA

Na Mwandishi wetu - Malunde 1 blog

Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi ameongoza Mahafali ya 17 ya Shule ya awali na msingi Hope
'Hope English Medium Nursery & Primary School' iliyopo Mjini Shinyanga ambapo jumla wanafunzi 79 wamehitimu elimu ya darasa la saba mwaka 2023.

Akizungumza wakati wa Mahafali hayo yaliyofanyika Septemba 23,2023 Mgeni rasmi Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi ameipongeza shule hiyo kuwa kuendelea kufanya vizuri kitaaluma.

Mhe. Johari ametumia fursa hiyo kuwakumbusha wazazi na walezi kuhakikisha wanawalinda watoto na watumie Teknolojia kwa maendeleo endelevu na siyo kusababisha mmomonyoko wa maadili.

“Ulimwengu huu wa digitali una fursa mbalimbali endapo ukitumika vizuri kwa maendeleo endelevu, lakini ukitumika vibaya ndiyo chanzo kikuu cha mmomonyoko wa maadili kwa watoto.

 Kutokana na utandawazi na Teknolojia iliyopo kwa sasa isitufanye watoto wetu kuwa huru kupitiliza, ukishindwa kumdhibiti mtoto utakuwa unatengeneza bomu la baadaye katika taifa letu hivyo sisi kama wazazi na serikali kwa ujumla hatutakua tayari kuandaa bomu la baadae kwa maana na sisi tumelelewa na wazazi ndiyo maana mnatuona tuko hivi na nchi imetulia",amesema Mkuu huyo wa wilaya.

Naye Mwalimu Mkuu wa Shule ya awali na msingi Hope, Aphonce John amewaomba wazazi kutumia fursa ya kuwaleta watoto wao katika shule hiyo 'Hope English Medium Nursery & Primary School' pamoja na Shule ya Sekondari Hope kwani shule hiyo inatoa elimu bora na imekuwa ikifanya vizuri katika mitihani ya kitaifa.

Amesema Shule ya Hope imekuwa ikifanya vizuri kitaaluma ambapo kiwilaya ya Shinyanga imekuwa ikishika nafasi ya kwanza pamoja na kuendelea kufanya vizuri pia kimkoa na kitaifa hivyo kuwaomba wazazi wawapeleke watoto wao kupata elimu bora shuleni hapo.

"Shule ya Hope ni shule ya Wanashinyanga na mikoa jirani kwa ujumla hivyo hakuna sababu ya kumpeleka mtoto mbali. Tunatoa elimu ya awali, msingi na tuna shule nyingine ya Sekondari (Hope Extended Excellence Secondary).
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi akizungumza wakati wa Mahafali ya 17 ya Shule ya awali na msingi Hope 'Hope English Medium Nursery & Primary School' iliyopo Mjini Shinyanga

Mwalimu Mkuu wa Shule ya awali na msingi Hope, Aphonce John akizungumza wakati wa Mahafali ya 17 ya Shule ya awali na msingi Hope 'Hope English Medium Nursery & Primary School' iliyopo Mjini Shinyanga

Mwanafunzi akisoma risala wakati wa Mahafali ya 17 ya Shule ya awali na msingi Hope 'Hope English Medium Nursery & Primary School' iliyopo Mjini Shinyanga
Wahitimu wakiingia ukumbini wakati wa Mahafali ya 17 ya Shule ya awali na msingi Hope 'Hope English Medium Nursery & Primary School' iliyopo Mjini Shinyanga

Zoezi la kukata keki likiendelea wakati wa Mahafali ya 17 ya Shule ya awali na msingi Hope 'Hope English Medium Nursery & Primary School' iliyopo Mjini Shinyanga

Mwanafunzi akimlisha keki Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi wakati wa Mahafali ya 17 ya Shule ya awali na msingi Hope
Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post