ABIRIA 12 WAFARIKI DUNIA GARI LAO LIKIGONGANA NA LORI USO KWA USO


Abiria 12 wa matatu (daladala) wameripotiwa kufariki dunia kufuatia ajali mbaya iliyotokea jioni ya Alhamisi, Septemba 7,2023 kwenye barabara kuu ya Nairobi-Mombasa nchini Kenya.

Ajali hiyo ilitokea eneo la Ikanga huko Taita Taveta wakati matatu hiyo ilipogongana ana kwa ana na lori.

OCPD wa Voi Bernstein Shari alithibitisha ajali hiyo katika eneo la Ikanga huko Taita Taveta, kwenye barabara kuu yenye shughuli nyingi, baada ya matatu hiyo kugongana ana kwa ana na lori.

Picha zilizoshirikiwa na shirika la usalama barabarani la Sikika zilionyesha wananchi wakiwa wamezunguka eneo la ajali ambapo lori lilikuwa limepinduka na matatu kubomoka vibaya. 

Watu 12 walifariki katika kisa hicho, huku watatu wakikimbizwa katika hospitali ya Rufaa ya Voi wakiwa katika hali mahututi.

Miili ya marehemu pia ilihamishiwa katika chumba cha kuhifadhi maiti cha hospitali hiyo. 

Matatu hiyo inayomilikiwa na Chania Genesis Sacco ilikuwa ikielekea Mombasa wakati lori hilo lilikuwa likielekea Nairobi ajali ilipotokea. Ilitokea takriban saa kumi jioni.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post