YANGA SC YAUWASHA MOTO NBCPL, YAITANDIKA KMC FC 5-0


NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

KLABU ya Yanga imefanikiwa kuondoka na alama tatu kwa kuweza kuinyuka KMC FC 5-0, kwenye mchezo wa ligi Kuu NBC uliopigwa kwenye dimba la Azam Complex Jijini Dar es Salaam.
Katika Mchezo huo Yanga iliwaanzisha baadhi ya nyota wao akiwemo Pacome Zouzoua ambaye amekuwa nyota wa mchezo kwa kufanikiwa kufunga bao moja na kutengeneza lingine kuisaidia timu yake kuondoka na ushindi mnono.

Zouzoua ameonesha uwezo wake na kuvuta hisia za mashabiki ambao walifika uwanjani wakishangilia pindi anapogusa mpira na kupeleka mashambulizi kwa wapinzani.

Dickson Job alianza kuandika bao la kwanza kipindi cha kwanza mara baada ya kupiga shuti la kisigino kipa wa KMC na kuokoa hivyo Job akapata nafasi tena ya kufunga bao ambalo lilidumu mpaka mapumziko.

Mabao mengine ya Yanga Sc yamewekwa kimyani na Mudathir Yahya, Aziz Ki pamoja na KonKoni.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post