WATU 10 WAMEFARIKI KWENYE AJALI KILIMANJARO
Watu 10 wamefariki dunia na mwingine mmoja kujeruhiwa baada ya Lori la Polisi kugongana na gari la mizigo Kirikuu katika eneo la Datch Conner Siha mkoani Kilimanjaro.

Mkuu wa Wilaya ya Siha Christopher Timbuka amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo.

Amebainisha kuwa katika ajali hiyo walifariki ni wanawake 6 wanaume 4, na Majeruhi wapo katika Hospitali ya Siha na Maiti zimehifadhiwa katika Hospitali ya Kibong'oto na kwamba taratibu za kutambua waliofariki zinafanyika.


Ametaja Chanzo cha ajali hiyo ni kuyumba kwa Kirikuu, baada ya kupata hitilafu kwenye Gurudumu la kulia na kusababisha kugongana uso kwa uso na Lori la Polisi.


SOMA HAPA ZAIDIChanzo ITV.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post