KUKAMILIKA KWA MFUMO WA KUSAJILI WATOTO WAISHIO KWENYE MAKAO YA WATOTO KUTASAIDIA UPATIKANAJI WA TAKWIMU SAHIHI



Na WMJJWM, DODOMA

Kamishna wa Ustawi wa Jamii amesema kukamilika kwa Mfumo wa kusajili Watoto waishio kwenye Makao ya Watoto itarahisisha upatikanaji wa takwimu sahihi kwa ajili ya maamuzi na Mipango thabiti ya Serikali katika kuwahudumia kundi hilo ndani ya Jamii.

Akifungua Warsha ya Siku moja ya wadau wanaopitia na kutoa maoni kuhusu mahitaji ya uundwaji wa mfumo huo Agosti 29, 2023 jijini Dodoma, amesema kukamilika kwa mfumo itatoa mwanya wa kutayarisha pia afua za masuala ya Watoto.

Kamishna Nandera amesema kwa sasa nchini kote kuna zaidi ya makao elfu nne lakini uratibu na upatikanaji wa taarifa wa haraka imekuwa ni vigumu kubaini.

"Kukamilika kwa Mfumo huu utasadia kuboresha malezi kwa watoto lakini pia utarahisisha mawasiliano na utatibu wa makao hayo hivyo ujio wa mfumo tunasema ni mwarobaini wa kukabiliana na hatua mbalimbali za malezi ya watoto" amesema Nandera.

Awali, Kamishana msaidizi wa Ustawi wa Jamii anayeshughulikia watoto Baraka Makona, amesema hitaji la Mfumo limekuwa muhimu kutokana na wakati wa sasa mambo mengi kuwa kidijitali.

Naye Mdau kutoka Shirika la Both ends Believing Lightnes Aquilline, amesema wao kama wadau wa Maendeleo wanaona fahari kufanya kazi na Serikali na hususani Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum hivyo wataendelea kutoa mchango wao kwa muda wote wa ukamilishaji wa Mfumo na kuuhudumia.

Kukamilika kwa Mfumo huo, kutasadia kuwa na kanzi data itakayowezesha kuwajua mahali walipo na hatua mbalimbali wanazopitia katika makuzi yao.

Wadau mbalimbali wamehudhuria warsha hiyo ikiwemo wamiliki wa Makao, Maafisa Ustawi wa Jamii wa Halmashauri za Mkoa wa Dodoma, shirika la PACT Tanzania pamoja na Wizara za kisekta.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post