WAKULIMA WASHAURIWA KULIMA KILIMO CHA UMWAGILIAJI

Na Dotto Kwilasa, Malunde1 Blog, Dodoma

Afisa Mauzo wa Kampuni ya umwagiliaji ya SIMUSOLAR Hadija Seleman amewashauri wakulima kulima Kilimo Cha umwagiliaji ili kurahisisha shughuli za Kilimo na kupata uhakika wa mazao.

Akizungumza leo Aug 4,2023 Jijini Dodoma na Waandishi wa habari kwenye maonesho ya wakulima Nanenane amesema Kilimo Cha umwagiliaji ni mkombozi Kwa wakulima kwani kinampa mkulima uhakika wa mazao hata bila msimu.

Amesema ili kuhakikisha suala la Kilimo Cha umwagiliaji linafanikiwa, Kampuni hiyo umeanza kuuza na kukopesha pampu Kwa wakulima Ili kuwasaidia kupata mazao ya kutosha.

"Pampu zinazofaa Kwa Kilimo Cha umwagiliaji zinatumika kwenye mfumo wa umwagiliaji wa matone wenye ukubwa wa mita za mraba 500 Kwa bei ya ofa,"amesema

Ameongeza kuwa Kilimo Cha umwagiliaji ni mkombozi Kwa Sekta ya kilimo na salama Kwa chakula kinachopatikana .

Akieleza faida za Sola hiyo amesema ni inasaidia kuachana na matumizi ya jenereta na mafuta Kutokana na Sola hiyo kutumia mfumo wa umeme jua

"Sola hii ni ya umeme jua na inauwezo wa kuchakata nguvu ya umeme jua kwenda Mfumo wa umeme na mafuta ikiwa ni pamoja na kuwa na uwezo wa kuendesha pampu Kwa siku mzima,"amefafanua


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post