TOWN STARS YAPOKEA KICHAPO FAINALI YA UVCCM FOOTBALL CUP, DIWANI GULAM HAFIDH AKABIDHI MBUZI

Timu ya Town Stars imepokea kichapo cha goli 2 - 1 dhidi ya Buzuka Fc kwenye fainali ya mashindano ya mpira wa miguu kombe la UVCCM FOOTBALL CUP kata ya mjini Manispaa ya Shinyanga

Fainali hiyo ya mpira wa miguu imefanyika leo Agosti 20, 2023 kwenye uwanja wa Chuo cha Ualimu Shinyanga (SHYCOM) uliopo Manispaa ya Shinyanga.

Fainali hizo zilizoanza kutimua vumbi mnamo tarehe 17/08/2023 ikizikutanisha timu nne kutoka kata ya mjini ambazo ni timu ya St. Joseph College, timu ya Shycom,Town Stars na Buzuka Fc ambapo timu iliyoibuka mshindi wa michuano ya kombe hilo imepatiwa zawadi ya mnyama aina ya mbuzi.

Akisoma risala kwenye mchezo huo Katibu wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) kata ya Mjini Pili Makalanga amesema lengo la mashindano hayo ni kutengeneza chachu na kuibua vipaji vya vijana, kusaidia vijana kuamka, kujituma na kuachana na makundi yasiyofaa.

"Faida ya mashindano haya ni burudani kwa vijana, kutengeneza urafiki na ujamaa baina ya vijana hawa lakini pia kuleta chachu, kuimarisha umoja na ushirikiano na kuachana na makundi ya mitaani yanayopelekea kujihusisha kwenye vitendo visivyofaa ikiwemo utumiaji wa madawa ya kulevya na wizi, kubwa zaidi ni kuhamasisha vijana kujiunga na Umoja wa Chama cha Mapinduzi kwa lengo la kukipambania chama na maslahi ya vijana wa kata ya mjini, na siku ya leo tumeandaa kadi kwa vijana wa kata ya mjini", amesema Pili Makalanga.

Akizungumza mara baada ya mchezo huo aliyekuwa mgeni rasmi, diwani wa kata ya mjini Mhe. Gulam Hafidh Muqadam amepongeza Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) wilaya ya Shinyanga kwa kuandaa mashindano hayo ya mpira wa miguu kwa vijana maalufu kama UVCCM FOOTBALL CUP kwa kutekeleza ilani ya chama hicho na kukuza vipaji kupitia sekta ya michezo.

“Vijana mmecheza mpira mzuri vipaji vya vijana wetu wa kata hii ya mjini tumeviona kiukweli niwapongeze sana timu zote kwa mchezo mliouonesha ni matumaini yangu tutakapo shiriki mashindano ya kata kwa kata kwenye kombe la UVCCM ushindi utabaki kwa kata ya mjini kikosi kitakachoundwa na vijana hao kitaenda kutuwakilisha vyema”,amesema.

“Lakini pia niwapongeze Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) wilaya ya Shinyanga kwa kuandaa mashindano haya ya vijana, na kuwakumbusha vijana kuendelea kuunga mkono jitihada za Rais wetu Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan na kuendelea kutekeleza ilani ya Chama cha Mapinduzi lakini pia kuwaunganisha vijana kwa pamoja katika michezo jambo ambalo linawaepusha na vitendo viovu mitaani”, aliongeza Mhe. Diwani Gulam Hafidh.

Naye aliyekuwa Mbunge wa jimbo la Shinyanga Mjini Stephen Masele aliyefika uwanjani hapo kama mshabiki na mpenzi wa mpira wa miguu kushuhudia fainali hiyo ameahidi kutoa ushirikiano kwenye timu hiyo ya kata ya mjini na kuipongeza timu ya Buzuka FC kwa kuibuka mshindi wa fainali hiyo.


Diwani wa kata ya mjini Mhe. Diwani Gulam Hafidh akikabidhi zawadi ya mbuzi mnyama kwa washindi wa mashindanio hayo.
Diwani wa kata ya mjini Mhe. Diwani Gulam Hafidh Akizungumza baada ya fainali hiyo.
Diwani wa kata ya mjini Mhe. Diwani Gulam Hafidh Akisalimiana na wachezaji wa timu ya Town Stars.
Katibu wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) kata ya Mjini Pili Makalanga akisoma risala.
Aliyekuwa Mbunge wa jimbo la Shinyanga Mjini Stephen Masele akizungumza kwenye mashindano hayo.
Baadhi ya watazamaji waliojitokeza kutazama fainali hiyo.
Mwenyekitio wa UVCCM Shinyanga Mjini (kushoto) akikabidhi kadi za uanachama kwa wachezaji
Mwenyekitio wa UVCCM Shinyanga Mjini (kushoto) akikabidhi kadi za uanachama kwa wachezaji
Diwani wa kata ya mjini Mhe. Diwani Gulam Hafidh (kulia) akiwa pamoja na aliyekuwa Mbunge wa jimbo la Shinyanga Mjini Stephen Masele wakitazama mchezo huo ukiendelea.






Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post