TBS YAZINDUA VIWANGO SPORT BONANZA


*************

Na Mwandishi wetu

UONGOZI wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS) kwa kutambua umuhimu wa michezo katika kujenga afya ya mwili na akili kwa wafanyakazi, umejenga kiwanja cha mchezo wa Pete chenye ubora wa hali ya juu.

Kiwanja hicho kimezinduli jana Makao Makuu ya Shirika, Ubungo, jijini Dar es Salaam na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TBS, Lazaro Msasalaga, hafla iliyoenda sambamba na ufunguzi wa Bonanza 2023.

Akizungumza kwenye hafla hiyo, Msasalaga, aliupongeza uongozi wa TBS kwa kutambua umuhimu wa michezo katika kujenga afya ya mwili na akili kwa wafanyakazi.

"Kwa kutambua hilo, uongozi uliona ni vema kujenga kiwanja cha michezo chenye ubora wa hali ya juu, kiwanja hiki ili kuhakikisha kuwa wafanyakazi wanapata sehemu nzuri ya kufanya mazoezi na kucheza mechi zao badala ya kwenda kucheza kwenye viwanja vya taasisi nyingine," alisema Msasalaga na kuongeza;

"Na hii itaokoa muda na kurahisisha ufanyaji wa mazoezi kila jioni." Alitumia fursa hiyo kuwahamasisha wafanyakazi kushiriki kwenye Bonanza hiyo.

Alisema katika Bonanza hiyo ya nne kufanyika tangu kuanzishwa rasmi kwa Viwango Sports Bonanza mwaka 2020, itakuwa ni ya kipekee ikilinganishwa na miaka ya nyuma.

Alisema Bonanza hiyo, ambayo ilianza Agosti 28 likitarajiwa kuhitimishwa Septemba 2, mwaka huu itashirikisha timu sita kutoka kurugenzi zifuatazo;

Kurugenzi ya Udhibiti Ubora (DOM), Kurugenzi ya Raslimali Watu na Utawala (DHRA), Kurugenzi ya Upimaji Ugezi (DTM), Kurugenzi ya Uandaaji Viwango (DSD), Timu ya watoa huduma TBS, ikihusisha wanaotoa huduma ya hakula, ulinzi na usafi.

Timu hiyo ya watoa huduma inashiriki Bonanza hiyo kwa mara ya kwanza ili kudumisha ushirikiano, kwani na wao ni wanajamii ya TBS.

Kwa mujibu wa Msasalaga, Bonanza hiyo itashirikisha michezo ya mpira wa miguu, pete, wavu, kuvuta kamba, rede na michezo ya jadi.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post