SERIKALI ITAENDELEA KUBORESHA MAZINGIRA YA BIASHARA NCHINI
Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Exaud Kigahe amesema Serikali itaendelea kuboresha mazingira ya biashara kwa kuendelea kupunguza tozo na kodi zinazokua kero kwa wafanyabiashara nchini.

Mhe. Kigahe Ameyasema hayo Mkoani Mbeya alipokitembelea kikundi cha wauzaji wa mchele (Mbeya Rice Group) katika soko la SIDO Mwanjelwa kwa lengo la kusikiliza na kutatua changamoto zao.

Aidha amewataka viongozi wa kikundi hicho kuzingatia ubora katika hatua zote za uzalishaji kuanzia shambani hadi kiwandani ili mchele huo upate soko katika masoko ya Kimataifa.

"Naomba mjitahidi sana katika uandaaji wa mpunga wakati mnapoelekea kuuchakata ili kupata mchele,hakikisheni mnaanika vizuri mahali ambapo hapawezi kusababisha mchele kuwa na mchanga lakini pia mtafute mashine ambayo inayoweza kupembua mchele na chenga ili tuweze kushindana kimataifa.”amesema Mhe. Kigahe

Aidha amesema,Serikali inaendelea kuongea na Taasisi za kifedha na hasa kwenye vikundi ili wafanyabaishara hao waweze kukopesheka na benki mbalimbali ikiwemo benki ya TIB.

Aidha, kuhusiana na suala la ushuru mkubwa lililolalamikiwa na wafanyabiashara hao, Mhe. Kigahe ameiagiza Ofisi ya Katibu Tawala wa Mkoa ilichukue hilo na waone namna ya kuangalia kupunguza ushuru ili waweze kuchukua wafanyabiashara wengi zaidi na kupata fedha nyingi licha ya kukusanya kidogo kidogo lakini itaongeza uhiyari wa kulipa kodi na hivyo serikali kupata mapato mengi zaidi.

Awali Katibu Mkuu wa Mbeya Rice Group Julius Ngalawa amesema kongano hilo linawanachama 29 na wafanyabiashara 2000 na wakulima 1000 ambapo wanachakata tani 78,000 za mpunga zinazouzwa nchini na na nchu za nje kama Uganda,Zambia ,Botswana.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post