MWENYEKITI UWT TAIFA ARIDHISHWA NA UTENDAJI KAZI KITUO CHA AFYA MAILI TANOMWENYEKITI wa Jumuiya ya Wanawake Tanzania (UWT) ya Chama Cha Mapinduzi(CCM) Mary Chatanda ameridhishwa na utendaji kazi wa Kituo cha afya Maili Tano.

Chatanda ameridhishwa na kituo hicho baada ya kukitembelea leo Agosti 23, 2023 akiwa katika ziara yake ya kikazi mkoani Tabora.

Kituo cha Afya Maili Tano ambacho kilipokea Sh.milioni 400 mwaka 2018 kwa ajili ya ujenzi wa maabara, jengo la mama na mtoto, jengo la upasuaji, mochwari pamoja na Nyumba ya Mtumishi.

Aidha Kituo hiki kimepokea vifaa tiba vya kutosha katika awamu hii ya sita vikiwamo Kitanda cha upasuaji, taa ya kisasa ya upasuaji, mashine ya kusaidia wagonjwa wakati wa upasuaji pamoja na vifaa vifaa tiba ambavyo vimewezesha kituo hicho kuwa kwanza kutoa huduma ya upasuaji kwa Manispaa ya Tabora.

Akizungumza akiwa kwenye kituo hicho Chatanda amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Samia Suluhu Hassan kwa kukiwezesha kituo hicho kupata vifaa tiba hivyo kituo hicho kutoa huduma mbalimbali ikiwemo ya upasuaji.

Amesema huduma hiyo imewezesha kinamama wajawazito kupata huduma hiyo na hivyo kutekeleza kwa vitendo kampeni ya kuokoa mama na mtoto.

Akiwa katika kituo hicho ametatua changamoto ya maji baada ya kumpigia simu Naibu Waziri Marryprica Mahundi ambaye amekiri kuchimba kisima katika Kituo hicho ili kuondoa changamoto hiyo.

Chatanda amesema Kituo cha afya kinapokuwa kina uhaba wa maji wanawake wengi ndio wanapata shida hasa wakati wa kujifungua kwa kuwa wanahitaji maji mengi ili yawasaidie katika kujifungua

Hivyo amempongeza Naibu Waziri wa Maji kwa kuahidi kuitatua changamoto hii. "Maji ni uhai na muhimu kwenye taasisi zozote zile za umma kuwa na maji.Niwatake TUWASA muendelee kusambaza maji katika taasisi za umma kwani wananchi wengi wanahitaji huduma ya maji"

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post