DMI YASHIRIKI BONANZA LA SHIMIWI


*****************

Chuo cha Bahari Dar es Salaam (DMI) kimeungana na Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi katika Bonanza la Uzinduzi wa Michezo ya shirikisho la Michezo ya Wizara na Idara za Serikali Tanzania'SHIMIWI' ambayo hufanyika Kila mwaka.

Uzinduzi wa Bonanza hilo ni maandalizi ya Michezo ya SHIMIWI inayotarajiwa kufanyika mwezi Septemba 2023 limebebwa na Kauli mbiu isemayo "Michezo hujenga afya Bora kwa wafanyakazi" limefanyika leo Jijini dodoma ambapo Mhe. Balozi Dkt. Moses Mpogole Kusiluka, Katibu Mkuu Kiongozi alikuwa mgeni rasmi.

Watumishi kutoka Chuo cha Bahari Dar es Salaam wakiongozwa na Mwalimu wa Michezo (DMI) Ndg. Mansour Likamba na Mwalimu wa Riadha (Wizara ya ujenzi na Uchukuzi) Ndg. Samweli Pununter walipata fursa ya kuungana na watumishi wa Wizara mbalimbali na Taasisi za Serikali katika Bonanza hilo

Mwalimu wa Michezo DMI Ndg Mansour Likamba (Wa pili kulia) akiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post