Mfano wa mboga ya chainizi
Jeshi la polisi Mkoa wa Mwanza linamshikilia Maneno Thomas (35) mkazi wa Chamgati wilaya ya Sengerema kwa tuhuma za kumchoma kwa maji ya moto mikono yote mtoto wake akimtuhumu kudokoa mboga ya majani aina ya chainizi.
Inadaiwa siku ya tukio mtuhumiwa alifika nyumbani akaomba apikiwe chakula ndipo aliambiwa mboga imeisha ndipo akachemsha maji kisha kumwagia mikono yote. Mboga hiyo ililiwa na mtoto huyo aitwaye Daniel Maneno.
Baada ya tukio hilo mtuhumiwa alimficha mwanae huyo katika chumba, kabla ya wananchi kupata taarifa na kusaidia kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo.