USHIRIKISHWAJI WA TAASISI ZA UMMA KATIKA KUANDAA VIWANGO NA MIONGOZO YA E-GA


Maafisa TEHAMA kutoka katika taasisi mbalimbali za umma wameshiriki katika kikao kazi cha kuandaa na  Viwango na Miongozo ya Serikali Mtandao, ili kuhakikisha inaendana na Sheria ya Serikali Mtandao Na. 10 ya mwaka 2019.  

Lengo ni kuhakikisha Serikali inakua na Serikali mtandao yenye tija na inayoongeza ufanisa katika utendaji kazi na utoaji huduma kwa umma.

Kikao hicho kilichoandaliwa na Mamlaka ya Serikali Mtandao (e-GA), kilifanyika kwa siku 3 kuanzia Agosti 15, 2023 katika ukumbi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi jijijini Dodoma.

Viwango na Miongozo hiyo inapatikana katika Tovuti ya e-GA kupitia kiungohttps://www.ega.go.tz/standards

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post