SERIKALI YAPONGEZA MGODI WA BARRICK BULYANHULU KUENDESHA SHUGHULI ZAKE KWA VIWANGO VYA KIMATAIFA

Picha ya pamoja ya Maofisa Waandamizi kutoka Wizara ya Madini na Wafanyakazi wa Barrick Bulyanhulu wakati walipofanya ziara mgodini hapo
Ujumbe wa Maofisa Waandamizi kutoka wizara ya madini wakipatiwa maelezo ya uendeshaji wa shughuli katika vitengo mbalimbali kutoka kwa wafanyakazi wa Barrick wakati ulipotembelea mgodi wa Barrick Bulyanhulu.
Wafanyakazi wa Barrick wakiongoza ujumbe wa Maofisa Waandamizi wa Wizara ya Madini kutembelea maeneo mbalimbali ya uzalishaji wakati walipofanya ziara katika mgodi wa Barrick Bulyanhulu
Ujumbe wa Maofisa Waandamizi kutoka wizara ya madini wakipatiwa maelezo ya uendeshaji wa shughuli katika vitengo mbalimbali kutoka kwa wafanyakazi wa Barrick wakati ulipotembelea mgodi wa Barrick Bulyanhulu.
Ujumbe wa Maofisa Waandamizi kutoka wizara ya madini wakipatiwa maelezo ya uendeshaji wa shughuli katika vitengo mbalimbali kutoka kwa wafanyakazi wa Barrick wakati ulipotembelea mgodi wa Barrick Bulyanhulu.

***
Wizara ya Madini imetoa pongezi kwa Mgodi wa Barrick Bulyanhulu, uliopo katika Halmashauri ya wilaya ya Msalala mkoani Shinyanga kwa kuendesha shughuli zake za uchimbaji wa madini kwa kuzingatia viwango vya juu ya kimataifa.

Pongezi hizo zimetolewa na Mjeolojia Mwandamizi kutoka Wizara ya Madini,Mhandishi Deograthias Oreku, aliyeongoza ujumbe wa Maofisa waandamizi wa Wizara hiyo ulipofanya ziara mgodini hapo na kutembelea vitengo mbalimbali vya uzalishaji sambamba na kufanya mkutano na viongozi wa mgodi huo.

Alisema mgodi huo unaendesha shughuli zake kwa viwango vikubwa vya ubora wa kimataifa sambamba na kutumia teknolojia za kisasa za shughuli ya uchimbaji ambazo zinatumika katika migodi mikubwa duniani “ Kwa kweli tumefurahishwa na ziara hii ya kikazi ambapo tumeweza kuona shughuli za mgodi ambao ni mfano mzuri wa uwekezaji katika sekta ya madini”,alisemaMhandisi Oreku, ambaye alimwakilisha Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini katika ziara hiyo.

Ujumbe huo pia ulitembelea bwawa la kuhifadhia tope sumu katika mgodi na kufurahishwa kwa jinsi lilivyojengwa kitaalamu kuhakikisha uendeshaji wa shughuli za mgodi hauleti madhara kwenye mazingira na wananchi wa maeneo ya jirani.

Maofisa hao kutoka Wizara ya Madini walielezwa kuwa kampuni ya Barrick itaendelea kushirikiana na Serikali kuhakikisha inafanikisha miradi ya kuboresha jamii zinazozunguka katika maeneo ya migodi yake kwa mujibu wa sera za nchi kupitia fedha za Uwajibikaji kwa jamii (CSR).

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post