RC MNDEME AMWAGIA SIFA, PONGEZI KAMANDA WA POLISI MKOA WA SHINYANGA

Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme, amempongeza Kamanda wa Polisi wa mkoa huo ACP Janeth Magomi kwa juhudi kubwa alizozifanya katika kudumisha amani na utulivu mkoani Shinyanga.

Mhe. Mndeme ametoa pongezi hizo leo wakati wa ziara ya Kamishna wa Kamisheni ya Ushirikishwaji Jamii CP Faustine Shilogile alipotembelea ofisi ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga kwa lengo la kutoa salamu za shukrani kwa mkuu wa mkoa huyo kutokana na ushirikiano wake na hamasa anazozitoa kwa Jeshi la Polisi mkoani hapa Shinyanga.

Katika ziara hiyo, Mkuu wa mkoa alimueleza Kamishna Shilogile kwamba Kamanda Janeth Magomi amekuwa ni kiongozi wa kipekee na mwenye kujitoa kwa kila hali ili kuhakikisha mkoa wa Shinyanga unakuwa salama.

"Kwa muda mrefu sasa sijasikia matendo ya kutisha ndani ya mkoa wangu, mauaji yamepungua, hivi sasa kwa kweli ninapata usingizi",amesema Mhe. Mndeme

Mkuu huyo wa mkoa amemuahidi Kamanda Shilogile kwamba wameshaandaa cheti maalum cha utambuzi wa umahiri wa Kamanda Magomi.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments