WATOTO WAWILI WAFARIKI KWA KUKOSA HEWA WAKICHEZEA GARI TINDE


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Janeth Magomi
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Janeth Magomi

Na Mwandishi wetu - Malunde 1 blog
Watoto wawili wanaokadiriwa kuwa na umri wa miaka kati ya 6 na 7 wamefariki dunia kwa kukosa hewa wakichezea gari katika Kitongoji Ng’ung’ula Kijiji cha Jomu kata ya Tinde wilaya ya Shinyanga.

Diwani wa kata ya Tinde, Japhar Kanolo
ameiambia Malunde 1 blog kuwa tukio hilo limetokea Jumanne Agosti 22,2023 majira ya saa 12 jioni wakati watoto wakicheza ndani ya gari likajifunga na wazazi wao hawakujua kilichokuwa kinaendelea.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Janeth Magomi amethibitisha kupokea taarifa za tukio hilo.

“Jeshi la polisi tumepokea taarifa hizi. Wazazi walitoka Mwanza wakiwa na gari lao kwenda kusalimia nyumbani kwao Tinde, walipofika pale hawafunga milango ya ile gari, na vioo vilikuwa vimefungwa”,amesema Kamanda Magomi.


“Kilichotokea ni watoto walienda kucheza kwenye lile gari, wakalikorofisha likawa likajifunga. Kwa mujibu wa Daktari watoto wale walifariki kwa kukosa hewa”,ameeleza Kamanda Magomi.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post