WANANCHI WATEMBELEA BANDA LA NEC MAONESHO YA NANE NANE DODOMATume ya Taifa ya Uchaguzi ipo katika Viwanja vya Nzuguni Jijini Dodoma yanapofanyika maonesho ya Wakulima maarufu kama Nane Nane kwa Kanda ya Kati Dodoma. Ushiriki wa Tume katika maonesho hayo ni kutoa Elimu ya Mpiga Kura kwa wananchi wanaotembelea maonesho hayo.

Aidha Tume inapata fursa ya kukutana ana kwa ana na wadau mbalimbali wa Uchaguzi na kuweza kuzungumza nao na kujibu maswali na hoja mbalimbali zinazowakabili. Ufafanuzi kuhusu masuala ya Ucxhaguzi pia unatolewa na maafisa wa Tume waliopo katika banda hilo la Maonesho.

Tume ya Taifa ya Uchaguzi inawakaribisha wananchi wote kutembelea banda hilo la kupata ufafanuzi juzi ya mambo yanayowatatizo.

Mkuu wa wilaya ya Dodoma mjini, Jabir Shekimweri akiwasikiliza maafisa wa Tume ya Taifa ya uchaguzi wakati Mkuu hyyo wa Wilaya alipotembelea banda la Tume katioka Maonesho ya Wakulima Nane Nane Kanda ya Kati yanayoendelea katika viwanja vya Nzuguni Jijini Dodoma.
Maofisa wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi wakiwapa maelezo wanafunzi wa Shule ya Msingi Hijra ya Jijini Dodoma wakati walipotembelea banda la Tume katioka Maonesho ya Wakulima Nane Nane Kanda ya Kati yanayoendelea katika viwanja vya Nzuguni Jijini Dodoma.

Wakuu wa Wilaya za Chamwino, Iramba na wenyeviti wa halmashauri za Dodoma leo tarehe 3 Agosti, 2023 wametembelea banda la Tume ya Taifa ya Uchaguzi kwenye maonesho ya wakulima (Nanenane) Kanda ya Kati yanayofanyika katika viwanja vya Nanenane Nzuguni Jijini Dodoma.

Wananchi mbalimbali wakipata huduma katika Banda la Tume ya Taifa ya Uchaguzi.
Wananchi mbalimbali wakipata huduma katika Banda la Tume ya Taifa ya Uchaguzi.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post