BENKI YA CRDB YAWAPA PUNGUZO LA BEI WATEJA SIMU ZA SAMSUNG GALAXY Z


Dar es Salaam. Tarehe 10 Agosti 2023: Benki ya CRDB imeingia ushirikiano na kampuni ya Samsung Tanzania ili kuwapa punguzo la bei wateja watakaonunua simu mpya aina ya Samsung Galaxy Z Fold5 na Galaxy Z Flip5.


Ushirikiano huo umetangazwa leo jijini Dar es Salaam na Mkuu wa Huduma za Kadi wa Benki ya CRDB, Farid Seif aliyeambatana na Mkuu wa Kitengo cha Simu cha Samsung Tanzania, Mgope Kiwanga mbele ya waandishi wa Habari.


Akizungumzia ushirikiano huo, Seif amesema kuanzia sasa, wateja wanaopenda kuzinunua simu hizo mpya wanaweza kuweka oda zao ili kuanza kufurahia huduma katika simu hizo zenye ubora wa kimataifa.
“Katika kipindi hiki, wateja wetu wataweka kuokoa kati ya shilingi 308,000 hadi shilingi 565,000 iwapo watanunua simu hizi kipindi hiki cha promosheni. Ukienda kwenye maduka ya Samsung yaliyoenea kote nchini au kwenye matawi yetu ya wateja wakubwa, utatakiwa kulipia asilimia 20 ya bei ya simu unayoitaka na ukiletewa utarudishiwa asilimia 10 ya bei uliyolipa,” amesema Seif.


Kwa aliye mbali na duka, Seif amesema anaweza kuweka oda yake kwa kuingia kwenye akaunti za mitandao ya kijamii za Benki ya CRDB katika majukwaa ya Instagram, Twitter na Facebook ambako kuna ‘link’ itakayowaunganisha na kitengo cha huduma kwa wateja cha Samsung Tanzania ambako wanaweza kuweka oda ya simu waitakayo.


“Kwa njia yoyote kati ya hizi, mteja atakayelipa kwa kutumia kadi ya Benki ya CRDB au kupitia Simbanking atarudishiwa asilimia 10 ya malipo aliyoyafanya,” amesisitiza Seif.
Kwa miaka mingi, Benki ya CRDB imekuwa ikongoza kwa ubunifu katika kuwahudumia wateja wake. Ilikuwa ya kwanza kuanzisha matumizi ya kadi zinazofahamika zaidi kama CRDB Tembocard na ikawa ya kwanza kuzindua programu ya huduma kupitia simu za mkononi almaarufu kama Simbanking ambayo inaongoza kwa kutumiwa nchini miongoni mwa programu za benki zilizopo.


Kwa Watanzania ambao hawajajiunga na huduma za Benki ya CRDB hivyo kutokidhivigezo vya kunufaika na punguzo hili, Seifa amesema wanawakaribishwa kufanya hivyo na kuwa sehemu ya mtandao mkubwa wa matawi yaliyopo kwenye halmashauri zote nchini pamoja na huduma za mawakala wengi wanaopatikana mitaani.


“Kwa sasa utaratibu umerahisishwa, mteja anaweza kujifungulia akaunti yeye mwenyewe au akaenda kufungulia kwa wakala yaani CRDB Bank Wakala au akaenda kwenye tawi letu lolote na kuanza kufuarahia huduma likiwamo punguzo la bei la simu bora za Samsung,” amesema Seif.
Kuhusu unafuu uliopo, Kiwanga amesema mteja atakayenunua simu zinazoingizwa sokoni sasa hivi atanufaika na punguzo hilo la bei, na atapata saa ya mkononi yenye thamani ya shilingi 900,000 au ‘earpods’ zinazouzwa shilingi 450,000 kutegemeana na aina ya simu atakayoinunua.


“Simu aina ya Galaxy Z Fold5 tunaiuza kwa shilingi milioni 5.65 na ile ya Galaxy Z Flip5 ni shilingi milioni 3.08. Ukiweka punguzo la asilimia 10 ambalo mteja atalipata akilipa kupitia mifumo ya Benki ya CRDB pamoja na zawadi hizi anazopewa, utaona kuwa anaipata simu hii kwa bei ndogo kuliko uhalisia wake. Nawakaribisha Watanzania kuchangamkia fursa hii kwenye maduka yetu ndani ya kipindi cha promosheni kitakachodumu mpaka mwishoni mwa mwezi huu,” amesema Kiwanga.


Simu hizi mbili, Kiwanga amesema ni mwanzo tu ushirikiano wao na Benki ya CRDB ila huko mbeleni wanatarajia kuzijumuisha bidhaa nyingine zote za kampuni ya Samsung ili kuwapa unafuu Watanzania wanaopenda kutumia bidhaa bora za kielektroniki.
Kwa sasa, kampuni ya Samsung Electronics inanadi toleo lake la tano la simu aina ya Galaxy Z ambazo zinakunjika huku zikiwa na urahisi mwingi katika matumizi yake. Zikitamblishwa kwa tarehe tofauti duniani, uzinduzi wakee nchini ulifanyika tarehe 26 mwezi uliopita katika maduka ya Sansung yaliyopo Mlimani City, Palm Village na Royal Communications jijini Dar es Salaam.


Ili kunufaika na ofa iliyopo, Kiwanga amesema maduka yao yote yapo wazi kupokea oda za wateja na akawakaribisha kwenye maduka ya F&S Electronics Mlimani City, SES Mlimani City, Gadget Masaki, SES JMall na Brandshop Palm Village ya jijini Dar es Salaam Pamoja na Samsung Brandshop na Dodoma Express ya jijini Dodoma bila kusahau duka la Benson & Company jijini Arusha.
Mkuu wa Huduma za Kadi wa Benki ya CRDB, Farid Seif (kulia) na Mkuu wa Kitengo cha Simu cha Samsung Tanzania, Mgope Kiwanga wakitangaza punguzo la asilimia 10 kwa wateja watakaonunua simu aina ya Galaxy Z Fold5 na Galaxy Z Flip5 wakilipa kupitia mifumo ya Benkiya CRDB.
Mkuu wa Huduma za Kadi wa Benki ya CRDB, Farid Seif (kulia) na Mkuu wa Kitengo cha Simu cha Samsung Tanzania, Mgope Kiwanga wakiwa kwenye picha ya pamoja na waandishi wa habari waliojishindia zawadi wakati wa kutangaza punguzo la asilimia 10 kwa wateja watakaonunua simu aina ya Galaxy Z Fold5 na Galaxy Z Flip5 wakilipa kupitia mifumo ya Benki ya CRDB.
Mkuu wa Huduma za Kadi wa Benki ya CRDB, Farid Seif (kulia) na Mkuu wa Kitengo cha Simu cha Samsung Tanzania, Mgope Kiwanga wakiwa kwenye picha ya pamoja na wafanyakazi wa taasisi hizo mbili baada ya kutangaza punguzo la asilimia 10 kwa wateja watakaonunua simu aina ya Galaxy Z Fold5 na Galaxy Z Flip5 wakilipa kupitia mifumo ya Benki ya CRDB.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post