MWANAFUNZI KIDATO CHA PILI MBARONI KWA KUMWIBIA MWALIMU VITU VYENYE THAMANI YA MILIONI 8

 


Jeshi la Polisi Mkoani Morogoro linamshikila mwanafunzi miaka (15) kidato cha pili shule ya sekondari iliyopo Manispaa ya Morogoro kwa kumwibia mwalimu wake anaejulikana kwa jina la Anna Tebela vitu mbali mbali vyenye thamani ya milioni Nane.

Akizungumza na Waandishi wa habari Kaimu Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Morogoro Hassan Maya amesema tukio hilo lilitokea Julia 23 /2023 ambapo mtuhumiwa huyo alivunja mlango wa nyumbani kwa mwalimu Anna na kuiba Laptop 2 (Apple), (Toshiba) moja.

Vitu vingine ni Tv flati scrini nchi 25, Radio 2, Begi la nguo, Pasi ya Umeme, Simu 2 Huawei na Tecno, Saa ya mkononi, Chaji ya simu, Sabufa, Flash 2, USB6, Pochi 2 Klamu pamoja na Mikasi vyote vikiwa na thamani ya shilingi Milioni nane.

Aidha Kaimu Kamanda amesema kuwa mwanafunzi huyo alikamatwa Julia 25 mwaka huu na alipo hojiwa alikiri kuvunja nyumba ya mwalimu huyo na kuiba vitu hivyo .

Kamanda ameongeza kuwa mwalimu Anna ambaye ni Mkazi wa Bigwa alifika Polisi na kuvitambua vitu hivyo huku akibainisha kuwa hatua za kisheria zitafuata ikiwa ni pamoja na kumpeleka mtuhumiwa huyo Mahakamani.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments