JUBILEE YA MIAKA 10 YA SHULE YA AWALI NA MSINGI SAMUU YAFANA SHINYANGA ,MCHUNGAJI AKEMEA WANAUME KUVAA HERENI


Mchungaji wa kanisa la EAGT Kiloleli Mkoani Mwanza Dkt.Jacob Mutash  akizungumza na wageni waalikwa.

Na Amo blog Shinyanga.

Shule ya awali na Msingi Samuu 'Samuu English Medium School' ya Mjini Shinyanga leo Jumamosi Julai 15,2023 imefanya Jubilee ya miaka 10 tangu kuanzishwa kwake. 

Akitoa Taarifa ya kuanzishwa kwa Shule hiyo Mama Samaytu ambaye ni mkurugenzi wa Shule hiyo ameeleza kuwa Shule ya SAMUU ENGLISH MEDIUM SCHOOL ilianzishwa rasmi Tarehe 15/7/2013 na kuanza kutoa huduma kwa watoto wadogo, yaani “DAY CARE” ambapo mtoto mmoja alisajiliwa, na waalimu wawili wakiwa waanzilishi.


Mama Samaytu ameeleza kuwa Shule ya Awali na Msingi SAMUU imesajiliwa kwa usajili wa na. EM 17239 ipo eneo la kijiji cha Mwagala,kata ya Ibadakuli Manispaa ya Shinyanga umbali wa kilometa 5, kutoka mashariki ya mji wa Shinyanga.

Aidha Mama Samaytu amefafanua kuwa Shule ya Awali na Msingi SAMUU ni ya kutwa (Day) kwa madarasa yote ambayo ina usafiri wa kutosha unao safirisha wanafunzi kutoka nyumbani hadi shuleni na kurudishwa makwao kwa wakati kila siku.

Hata hivyo Mama Samaytu ameongeza kuwa Wanafunzi wanao soma katika Shule hiyo hupewa huduma ya uji baada ya masomo ya vipindi vya asubuhi pamoja na chakula bora na cha kutosha baada ya vipindi vya mchana hali inayo wawezesha wanafunzi kumudu masomo na kufanya vizuri darasani.

‘’Shule ina wanafunzi wa kutosha lakini kitaaluma Kutokana na uongozi makini, na Utawala madhubuti wa shule yetu, SAMUU ENGLISH MEDIUM, imekuwa ikipanda kitaaluma mwaka hadi mwaka na kufanikiwa kupata matokeo yaliyo Bora kwa wanafunzi wanaofanya mitihani mbalimbali “amesema Mama Samaytu.

Mojawapo ya matokeo hayo ni:-Mwaka 2021 (VII). Wanafunzi wote walifanya vizuri na kupata daraja Bora “A”, katika mtihani wa darasa la saba, na hivyo shule ilishika nafasi ya Pili Kitaifa, nafasi ya kwanza

Kimkoa, Kiwilaya na Kikata, :- Mwaka 2022 (VII): Ufaulu wa wanafunzi ulikuwa Daraja “A” Bora. Wanafunzi wote waliofanya mtihani darasa VII walifaulu daraja “A” na walichaguliwa kuendelea na masomo ya Sekondari katika shule mbalimbali zikiwemo shule za vipaji maalum,Sambamba na ufaulu wa kiwango cha juu kwa matokeo ya wanafunzi wa darasa la saba, lakini

Pia shule imekuwa ikifanya vizuri kwa mitihani ya wanafunzi wa darasa la nne (IV) kuingia darasa la tano (V) kwani ufaulu wao ni mzuri wa kiwango daraja “A” Bora mwaka hadi mwaka.

Kwa upande wake Mgeni rasmi katika Jubilee hiyo ambaye ni Dkt.Jacob Mutash ambaye ni Mchungaji wa kanisa la EAGT Kiloleli Mkoani Mwanza amewasihi walimu na viongozi wa Shule hiyo kuongeza bidii na kutobweteka na matokeo wanayo yapata huku akikemea vitendo vya baadhi ya vijana wa kiume wanaovaa hereni kitendo ambacho kinafaa kukemewa na kila mzazi na mlezi katika jamii .

Pia Dkt. Mutash ameiomba serikali kuwachukulia hatua kali za kisheria baadhi ya vijana wanao jihusisha na vitendo vya ushoga na usagaji katika jamii hali itakayo saidia kuwa na kizazi salama kinacho ishi misingi ya kumjua Mungu.
Burudani zinaendelea wakati wa Jubilee
Mama Samaytu ambaye ni mkurugenzi wa Shule ya Samuu akizungumza katika Jubilee.
Mama Samaytu ambaye ni mkurugenzi wa Shule ya Samuu akijipa raha wakati wa Jubilee.
Dkt. Jacob Mutash ambaye ni Mchungaji wa kanisa la EAGT Kiloleli Mkoani Mwanza akizungumza na wageni waalikwa.
Watoto wakitoa burudani.
Watoto wakiendelea kutoa burudani.
Mwalimu mkuu wa Shule ya Samuu akifanya Utambulisho.
Mama Samaytu ambaye ni mkurugenzi wa Shule ya Samuu akifanya utambulisho wa wageni
Burudani zinaendelea
Burudani zinaendelea
Mama Samaytu ambaye ni mkurugenzi wa Shule ya Samuu akizungumza kwenye jubilee
Mama Samaytu ambaye ni mkurugenzi wa Shule ya Samuu akitoa neno
Walimu ambao ni waanzilishi wa Shule wakifurahia jubilee
Mama Samaytu ambaye ni mkurugenzi wa Shule ya Samuu akisoma Risala.
Mama Samaytu ambaye ni mkurugenzi wa Shule ya Samuu akisoma Risala.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post