KUNDO ASHIRIKI KAMPENI ZA UDIWANI KATA YA UNAMHALA,AWAONYA WANAOTOA VITISHO KWA WAPIGA KURA

 

Mbunge wa Jimbo la Bariadi Mhandisi Kundo Mathew akizungumza kwenye 
 uchaguzi mdogo wa udiwani unaotarajiwa kufanyika tarehe 12 Julai 2023 katika kata Bunamhala.



Na Mathias Canal, Bariadi-Simiyu

Wakazi wa Kijiji cha Giriku Wilaya ya Bariadi Mkoani Simiyu wametakiwa kujitokeza kwa wingi kupiga kura katika uchaguzi mdogo wa udiwani unaotarajiwa kufanyika tarehe 12 Julai 2023 katika kata Bunamhala.

Uchaguzi huo utafanyika ili kukamilisha safu ya uongozi kufuatia kifo cha aliyekuwa diwani wa kata hiyo marehemu Mhe Nhola Samora.

Akizungumza wakati wa mkutano wa kuhitimisha kampeni za uchaguzi wa kata hiyo uliofanyika katika vijiji tofauti tofauti, Mbunge  wa Jimbo la Bariadi mkoani Simiyu Mhe Mhandisi Kundo Mathew ameonya baadhi ya wanasiasa wanaowatishia wanachi watakaojitokeza kupiga kura.

"Hawa watu ni adui wa Maendeleo yoyote anayewaambia kesho msijitokeze kupiga kura ili kumchagua diwani wenu, huyo ni adui wa maendeleo" Amesisitiza Mhandisi Kundo

Amesema "Anayezuia watu kumchagua kiongozi wao maana yake hataki maji, barabara, zahanati, umeme, kituo cha afya na dawa kwenye vituo cha afya" 

Mhandisi Kundo amesema kuwa watu wanaofanya hivyo hawatakiwi kusikilizwa kwa namna yoyote kwani Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan amesema ataendelea kuboresha huduma mbalimbali za kijamii ikiwemo upatikanaji wa dawa katika vituo vya afya.

Kuhusu changamoto ya upatikanaji wa maji katika kata hiyo Mhe Kundo amesema kuwa tayari serikali imesaini mkataba wa kuleta maji ya ziwa victoria hivyo wanachi wake mkao wa kula.

Katika uchaguzi wa nafasi ya diwani katika kata ya Bunamhala jumla ya vyama 14 vinatarajiwa kushiriki kinyang'anyiro cha nafasi hiyo katika uchaguzi utakaofanyika tarehe 12 Julai 2023.



Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post