Mkuu wa Chuo cha Bahari Dar es Salaam (DMI) Dkt. Tumaini Gurumo akitoa elimu ya uokozi melini wakati wa dharula Kwa kutumia kifaa maalun cha uokozi leo Julai 18,2023 katika Maonesho ya Vyuo Vikuu yanayoendelea kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam.
*************
CHUO Cha Bahari Dar es Salaam (DMI) kimetoa wito kwa wananchi kutembelea banda lao kwaajili ya kupata taarifa kuhusu kozi zinazotolewana DMI katika Maonesho ya Vyuo Vikuu yanyoendelea katika Viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam.
Akizungumza katika Maonesho hayo leo Julai 18,2023 Mkuu wa Chuo cha Bahari Dar es Salaam (DMI) Dkt. Tumaini Gurumo amewakaribisha watanzania wanaohitaji kujiunga na chuo hicho kuja kujisajili katika kozi mbalimbali kwenye Maonesho hayo.
DMI katika Maonesho hayo wameendelea kutoa elimu kuhusu masuala mbalimbali yanayoohusu bahari ikiwemo matumizi sahihi ya uokozi melini wakati wa dharura kwa kutumia kifaa maalum cha uokozi.
Wataalam kutoka Chuo cha Bahari Dar es Salaam wakiendelea kuwahudumia wananchi waliotenbelea Banda la DMI