UCHAGUZI WA VIONGOZI STAND UNITED FC KUFANYIKA AGOSTI 16, FOMU KUTOLEWA KUANZIA JULAI 17

Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya Chama Cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Shinyanga (SHIREFA) akitangaza uchaguzi wa viongozi wa Klabu ya Mpira wa Miguu Stand United FC

Na Elizabeth Hassan & Kadama Malunde - Shinyanga

Kamati ya Uchaguzi ya Chama Cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Shinyanga (SHIREFA) imetangaza uchaguzi wa viongozi wa Klabu ya Mpira wa Miguu Stand United FC ‘Chama la Wana’ ya Mkoani Shinyanga unaotarajiwa kufanyika Agosti 16,2023.

Akitoa tangazo la Uchaguzi wa Viongozi wa Stand United FC leo Ijumaa Julai 14,2023, Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi SHIREFA, Mh. Thomson Mtani amezitaja nafasi zinazogombewa kuwa ni Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti, Katibu Mkuu, Katibu Msaidizi, Mweka Hazina na Wajumbe wa Kamati ya Utendaji.

Amesema gharama za kuchukua fomu kwa nafasi ya Mwenyekiti ni Tsh. 200,000/=, Makamu Mwenyekiti sh 100,000/=, Katibu Mkuu sh 100,000/=, Katibu Msaidizi sh 50,000/=, Mweka Hazina sh 50,000/= na wajumbe wa kamati tendaji sh. 50,000/=.

“Fomu zitaanza kutolewa kuanzia tarehe 17.07.2023 hadi tarehe 21.07.2023 katika ofisi za SHIREFA kuanzia saa 2:00 asubuhi hadi saa 10:00 jioni. Pesa za fomu ziwekwe akaunti ya SHIREFA (Jina la Akaunti : Shinyanga Regional Footbal Association , Namba ya Akaunti 30702302591, Benki ya NMB. Fomu zirudishwe ofisi za SHIREFA kati ya saa 2:00 asubuhi hadi saa 10:00 jioni ikiambatanishwa na hati ya malipo ya benki ”,ameeleza Mtani.

Mwenyekiti huyo wa Kamati ya Uchaguzi SHIREFA amezitaja sifa za kugombea nafasi za uongozi Stand United kuwa ni pamoja na kuwa Mwadilifu na mwanachama wa klabu hiyo.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Chama Cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Shinyanga (SHIREFA), Said Mankiligo amewataka wanachama wa Stand United kujitokeza kwa wingi kuchukua fomu za kuwania uongozi kwenye klabu hiyo.
Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya Chama Cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Shinyanga (SHIREFA) akitangaza uchaguzi wa viongozi wa Klabu ya Mpira wa Miguu Stand United FC
Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya Chama Cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Shinyanga (SHIREFA) akitangaza uchaguzi wa viongozi wa Klabu ya Mpira wa Miguu Stand United FC
Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya Chama Cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Shinyanga (SHIREFA) akitangaza uchaguzi wa viongozi wa Klabu ya Mpira wa Miguu Stand United FC
Mwenyekiti wa Chama Cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Shinyanga (SHIREFA), Said Mankiligo akizungumza wakati Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya Chama Cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Shinyanga (SHIREFA) akitangaza uchaguzi wa viongozi wa Klabu ya Mpira wa Miguu Stand United FC

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post