MWIJAKU ADAI KUVAMIWA NA MABAUNSAMasaa kadhaa baada ya Chama cha Bouncers na Bodyguards nchini (BBT) kutoa onyo kali kwa Socialite na Mtangazaji, Burton Mwemba kwa tuhumiwa za kuwavunjia heshima baada ya kuwashika shika kifuani wakiwa kazini, @mwijaku aibuka na kuwataka wakaripoti kituo cha Polisi.


Kupitia twitter, Mwijaku amedai kuwa alivamiwa na Mabaunsa usiku nyumbani kwake na kujaribu kuua Mbwa wake kwa sumu ila hawakufanikiwa.


"Wapeni salamu hawa MABAUNSA wakaripoti Polisi harakaa kabla hatuja watafuta. Jaribio lao la kutaka KUNIUA jana halikubaliki. Na niwambie KUNIUA HAWAWEZI".


"Mabaunsa walio kuja usiku kwangu na kujaribu kunivamie jiandaeni Kisaikolojia. Mmejaribu kuua Mbwa kwa sumu mmeshindwa sasa sheria itafuata mkondo wake ndio mtanijua kwa nini nimetokea KIGOMA".

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post