Tanzia : MBUNGE WA MBARALI AFARIKI DUNIA


Mbunge wa Jimbo la Mbarali Mhe. Francis Leonard Mtega (59) amefariki dunia leo Julai 1,2023 kwa ajali ya kugongwa na Trekta (Power Tiller) Mbarali Mkoani Mbeya akiendesha pikipiki aina ya Boxer.

Kwa Mujibu wa Jeshi la Polisi Mbeya Mbunge huyo aligongwa na Power Tiller wakati akiendesha pikipiki na kusababisha kifo majira ya saa nane na dakika 40 mchana katika eneo la Mahango Kibaoni kata ya Chimara wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya katika barabara ya Chimara Kapungu ambapo mwendesha Power Tiller alimgonga mwendesha pikipiki huyo.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post