WAZIRI NDALICHAKO AWATAKA MAAFISA KAZI KUENDELEA KUSIMAMIA HAKI ZA WAFANYAKAZI NCHINI

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako akizungumza na Maafisa kazi Wafawidhi wa Mikoa kwenye mafunzo yaliyoratibiwa na ofisi hiyo kwa kushirikiana na Shirika la Kazi Duniani (ILO),leo Juni 27,2023 jijini Arusha.
Baadhi ya Maafisa Kazi wafawidhi wa walioshiriki mafunzo hayo wakimsikiliza Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako (hayupo pichani) wakati akizungumza na Maafisa kazi Wafawidhi wa Mikoa kwenye mafunzo yaliyoratibiwa na ofisi hiyo kwa kushirikiana na Shirika la Kazi Duniani (ILO),leo Juni 27,2023 jijini Arusha.

Na: Mwandishi wetu - Arusha

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako amewataka Maafisa kazi wafawidhi nchini kuhakikisha wanasimamia haki za wafanyakazi nchini.

Prof. Ndalichako amebainisha hayo leo Juni 27, 2023 wakati akizungumza na Maafisa kazi Wafawidhi wa Mikoa kwenye mafunzo yaliyoratibiwa na ofisi hiyo kwa kushirikiana na Shirika la Kazi Duniani (ILO), jijini Arusha.

Aidha, Prof. Ndalichako amesema kufanya hivyo kutawezesha uwepo wa kazi zenye staha na usimamizi mzuri wa haki za wafanyakazi, ikiwa ni dhamira ya Serikali anayoiongoza Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kuendelea kuimarisha maslahi ya wafanyakazi nchini.

Kwa upande mwengine Katibu Mkuu - Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Prof. Jamal Katundu amewasisitiza maafisa hao kufanya kazi kwa kuzingatia maadili ya taaluma zao, kuwa wabunifu, waadilifu na kufanya kazi kwa umoja.

Naye, Mkurugenzi Mkazi wa ILO Afrika Mashariki, Jealous Chirove amesema watendelea kushirikiana na Serikali na kuunga mkono juhudi za zake ili maeneo ya kazi yaendelee zingatia masuala ya haki na usawa kwa wafanyakazi.






Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post