WATANZANIA WATAKIWA KUCHANGAMKIA FURSA ZILIZOPO BAHARINI

Waziri wa Uchumi wa Buluu na Uvuvi Zanzibar, Suleiman Masoud Makame akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kongamano la pili la Uchumi wa Buluu ambalo limeandaliwa na Chuo Cha Bahari DSM (DMI) lengo ikiwa ni kujadiliana namna gani wanazitazama au kuziona fursa zilizopo katika matumizi ya Bahari, mito na maziwa iliyopo kwaajili ya maendeleo ya uchumi na maendeleo kwa ujumla.Uzinduzi huo umefanyika leo Juni 27,2023 Jijini Dar es Salaam

*********************

Watanzania wametakiwa kuchangamkia fursa zilizopo baharini ikiwemo rasilimali kubwa ya mafuta na gesi pamoja na madini mengine yanayopatikana chini ya Bahari ili kukuza uchumi wa nchi kwani kwenye usafiri na usafirishaji, zaidi ya asilimia 75 ya yote yanayoyonekana yanasafirishwa kupitia bahari.

Hayo yalisemwa leo Juni 27,2023 jijini Dar es Salaam na Waziri wa Uchumi wa Buluu na Uvuvi Zanzibar, Suleiman Masoud Makame wakati wa uzinduzi wa Kongamano la pili la Uchumi wa Buluu ambalo limeandaliwa na Chuo Cha Bahari DSM (DMI) lengo ikiwa ni kujadiliana namna gani wanazitazama au kuziona fursa zilizopo katika matumizi ya Bahari, mito na maziwa iliyopo kwaajili ya maendeleo ya uchumi na maendeleo kwa ujumla.

"Chini ya Bahari kuna vitu vingi ambavyo bado watanzania hatujavifikia tumekazana kwenye madini mengine ya juu lakini tukifanya tafiti za kutosha chini ya Bahari kuna rasilimali nyingi za kuitoa Tanzania kwenye unyonge"

Aidha Makame alisema kuna kila sababu ya kuthamini mchango wa mabaharia ambao wamewezesha maendeleo yote duniani, kwani usafiri wa anga unatumia sehemu chache sana kufikisha maendeleo Duniani.

Kwa upande wake Mkuu wa Chuo Cha Bahari Dar es Salaam, Tumaini Gurumo alisema bado kuna uchache wa wa wataalamu katika maeneo ya uchumi wa Buluu ambapo chuo Cha Bahari Dar es Salaam ndicho chuo kinachotegemewa katika eneo la usafirishaji kwa njia ya maji hivyo amewataka vijana kuchangamkia fursa hiyo kwa kuwa na rasilimali watu ili kukuza uchumi wa Buluu kwa.

"Hali ya wataalamu katika maeneo ya uchumi wa Buluu bado si kubwa, bado tuna wataalamu wachache sana, Chuo Cha Bahari Dar es Salaam kinategemewa katika habari nzima ya kutoa wataalamu hasa katika eneo la usafirishaji kwa njia ya maji hivyo katika eneo hilo tumejipambanua tuna maeneo yote, huu uchumi wa Buluu tuna uchumi wa maji, tuna washeria wanahitajika wa masuala ya maji, wasanifu wa vyombo vya majini, utengenezaji, majini lakini hawa wote tunao wachache hivyo bado hawajatosheleza hivyo vijana wa kitanzania tunapoeleza uchumi wa Buluu lazima tuwe na rasilimali watu"

Kadhalika Gurumo alisema kwa sasan wanataka waongeze mchango wa utalii katika uchumi wa nchi kwani umezoeleka sana utalii wa kwenda mbugani ambapo upo utalii unaohusiana na maji.

"Tukipata vyombo vingi vya kutosha watu wanaweza wakapanda na kuja kutazama" Alisema Gurumo

Gurumo alisema Tanzania imejaaliwa kuwa na sehemu kubwa ya bahari, mito, maziwa makubwa nne na vyombo vikubwa vya maji ambavyo vinatumika kwa usafirishaji lakini bado havitumiwi sawasawa.

"Sehemu ya uchumi ambayo inachangiwa na haya maji tuliyonayo ni ndogo sana wakati kuna mambo mengi yanaweza kutumika katika Bahari mojawapo suala la usafirishaji kwa njia ya maji, tunazo Bandari, mabaharia ambao wanauwezo wa kuingiza fedha hata za kigeni kwani wanauwezo wa kutoka hata nje ya mipaka ya nchi hii wakafanya kazi na kuingiza fedha za kigeni wakaleta Tanzania kwaajili ya kukuza uchumi"

Kuhusu suala la uvuvi Gurumo alisema bado watanzania wanafanya uvuvi mdogomdogo kwa kutumia vyombo vidogo ambavyo haviendi mbali, hivyo wanaka kuona watanzania wengi zaidi badala ya kuwekeza katika maeneo mengine ambayo wameyazoea kwa kawaida waje katika maeneo ya Bahari au shughuli zinazohusiana na bahari zenyewe zilizokuwa na manufaa kwa Taifa zima.

"Uvuvi ni sehemu ya uchumi wa Buluu, tunapotazama uvuvi unavyofanyika kwa sasa ni kwamba ni uvuvi mdogomdogo kwa kutumia vyombo visogo ambavyo haviendi mbali , kuna maji makubwa zaidi ambayo yana samaki wakubwa zaidi na wa aina ambazo zinahitajika zaidi ulimwenguni na kwenye masoko zaidi, hivyo tunaka kuona watanzania wengi zaidi badala ya kuwekeza katika maeneo mengine ambayo tumeyazoea kwa kawaida tuje katika maeneo ya Bahari au shughuli zinazohusiana na bahari zenyewe zinamanufaa kwa Taifa zaidi"

Naye Mwenyekiti wa bodi Chuo Cha Bahari DMI, Captain Ernest Bupamba alisema wao kama DMI kazi yao ni kuwafundisha wataalam ambao watasaidia serikali katika kutekeleza malengo yake kuhusu uchumi wa Buluu na kujielekeza pia kwenye maeneo ambayo kidogo walikua nyuma.

"Kongamano hili tunajitahidi kuwaelimisha wadau pamoja na watanzania kwa ujumla kuweza kujua uchumi wa buluu ni nini, kuzijua maliasili zilizo baharini ambao ndiyo uchumi wa Buluu wenyewe"

"Kwenye usafirishaji tulikua na tatizo la ujenzi wa meli pamoja na Boti, tulikua na kiwanda kimoja Cha songolo Marine Transport ambacho kinatununulia vyombo vyetu kwenye uchumi wa Buluu lakini sasa DMI tumeanza kufundisha vijana kwaajili ya kudizaini na kujenga meli" Aliongeza

Mkuu wa Chuo Cha Bahari Dar es Salaam, Tumaini Gurumo akiwa kwenye uzinduzi wa Kongamano la pili la Uchumi wa Buluu ambalo limeandaliwa na Chuo Cha Bahari DSM (DMI) lengo ikiwa ni kujadiliana namna gani wanazitazama au kuziona fursa zilizopo katika matumizi ya Bahari, mito na maziwa iliyopo kwaajili ya maendeleo ya uchumi na maendeleo kwa ujumla.Uzinduzi huo umefanyika leo Juni 27,2023 Jijini Dar es Salaam

Mwenyekiti wa bodi Chuo Cha Bahari DMI, Captain Ernest Bupamba akiwa kwenye uzinduzi wa Kongamano la pili la Uchumi wa Buluu ambalo limeandaliwa na Chuo Cha Bahari DSM (DMI) lengo ikiwa ni kujadiliana namna gani wanazitazama au kuziona fursa zilizopo katika matumizi ya Bahari, mito na maziwa iliyopo kwaajili ya maendeleo ya uchumi na maendeleo kwa ujumla.Uzinduzi huo umefanyika leo Juni 27,2023 Jijini Dar es Salaam


Wadau mbalimbali wakifuatilia uzinduzi wa Kongamano la pili la Uchumi wa Buluu ambalo limeandaliwa na Chuo Cha Bahari DSM (DMI) lengo ikiwa ni kujadiliana namna gani wanazitazama au kuziona fursa zilizopo katika matumizi ya Bahari, mito na maziwa iliyopo kwaajili ya maendeleo ya uchumi na maendeleo kwa ujumla.Uzinduzi huo umefanyika leo Juni 27,2023 Jijini Dar es Salaam

(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post