TAKUKURU TANGA YAWAPANDISHA KIZIMBANI WATUHUMIWA WA MAKOSA YA RUSHWA NA UHUJUMU UCHUMI

 


Na Oscar Assenga,TANGA.

TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa TAKUKURU mkoani Tanga imewapandisha kizimbani watuhumiwa wane(8)kwa makosa ya rushwa na uhujumu uchumi na kuisababisha Serikali matumizi batili ya zaidi ya shilingi milioni 28.

Waliopandishwa kizimbani ni William Nguluko Mwalimu Mkuu Shule ya Msingi Mabokweni jijini Tanga ambaye anakabiliwa na ashitaka la ubadhirifu na ufujaji kinyume na kifungu cha 28(1)(2) sharia na kuzuia na kupambana na rushwa sura ya 329 marejeo ya mweka 2022.

Kosa jingine ni kula njama , kutenda makossa ya rushwa kinyume na kifungu na kifungu 32 sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa , kuisababishia hasara serikali kinyume na aya ya 10(1) ya jedwali la kwanza na kifungu cha 57(1) na 60(2) sharia ya uhujumu uchumi sura ya 200 marejeo ya mwaka 2002.

Mshitakiwa wa pili ni Sudi Mshamu, mwalimu wa fedha katika shule hiyo , ambaye yeye anakabilwa na na makosa 31 likiwemo kosa la kughushi kinyume na kifungu cha 333,335(111) na 338,340(2)A sharia ya kanuni ya adhabu sura ya 16 marejeo ya mwaka 2022.

Kosa jingine ni kula nyama kinyume na kifungu cha 32 sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa sura ya 329 marejeo ya mwaka 2022 ikisomwa pamoja na aya ya 21 jedwali la kwanza na kifungu cha 57 (1) na kifungu cha 60(2) sharia ya uhujumu uchumi sura ya 200 marejeo ya mwaka 2020.

Mtuhumiwa wa tatu, Mwanabakari Adhumani aliyekuwa mwenyekiti wa kamati ya shule hiyo anashitakiwa kwa tuhuma ya kula njama kifungu cha 32 ,sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa sura ya 329 marejeo ya mwaka 2022.

Kosa jingine ni kuisababishia hasara serikali kinyume na aya ya 10(1) jedwali la kwanza na kifungu cha 57(1) na 60(2) sharia ya uhujumu uchumi sura ya 200 marejeo ya mwaka 2022.

Mshitakiwa wa nne ni Yusuph Mushi mwalimu wa shule ya sekondari Saruji ambaye kati ya makossa yanayomkabili ni kula nyama kinyumea na kifungu cha 32 sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa sura ya 329 marejeo ya mwaka 2022 ikisomwa pamoja na aya ya 21 jedwali la kwanza na kifungu cha 57 (1) na 60(2) sharia ya uhujumu uchumi sura ya 200 ya mwaka 2022,mshitakiwa alikiri kutenda kosa hilo.

Mbele ya hakimu wa Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Kakimu Mkazi Tanga Sophia Masati mtuhumiwa wa kwanza amekataa kutenda kosa hilo,wakati wa pili mwalimu wa fedha amekiri kutenda kosa hilo na mshitakiwa wa tatu naye amekataa kutenda kosa hilo wakati mshitakiwa wa nne amekiri kutenda kosa hilo.Washitakiwa hao wamerudishwa rumande na kesi yao itawajwa tena Julay 7 mwaka huu.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post