PPRA YATAMBULISHA RASMI MFUMO MPYA WA UNUNUZI WA UMMA

 

Mwenyekiti wa bodi ya PPRA,Dk. Leonada Mwagike akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dodoma leo June 23,2023 kuhusu kuanza kwa mfumo wa NeSt.


Na Sarah Moses, Dodoma.

MAMLAKA ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA)imetambulisha Mfumo wake mpya wa ununuzi wa Umma wa kielektroniki ujulikanao kama NeST ambao utaanza kutumika rasmi julai mosi mwaka huu ili kudhibiti ununuzi wa Umma unaozingatia  uwazi.

Akizungumza na Waandishi wa habari leo 23 Juni 2023 Jijini Dodoma Mwenyekiti wa Bodi  ya Mamlaka hiyo,Dk. Leonada Mwagike amesema mfumo huo utaanza kutumika rasmi Katika michakato ya ununuzi kwa baadhi ya Taasisi za umma ambazo tayari zimepatiwa mafunzo.

Dk.Mwagike amesema kuwa kutokana na mahitaji mapya ya teknolojia pamoja na maelekezo ya Serikali ya kuimarisha eneo la ununuzi, PPRA ilianza zoezi la kusanifu mfumo huo hali inayosaidia misingi mikuu ya kimataifa ya ununuzi kuzingatiwa.

"Mfumo huu wa NeST utakuwa mbadala wa mfumo unaotumika hivi sasa wa TANePS,unatarajiwa kutatua changamoto za kiufundi na hivyo kukidhi mahitaji ya Serikali Katika Sekta ya manunuzi,"amesema.

Hadi kufikia mwezi Juni,2023 moduli muhimu kwa ajili ya kuruhusu mfumo kuanza kutumika zimesha kamilika na kwamba mo

Akizungumza na Waandishi wa habari leo 23 Juni 2023 Jijini Dodoma Mwenyekiti wa Bodi  ya Mamlaka hiyo,Dkazi huu utahakikisha kuwa hadi ki wa Mamlaka hiyo(PPRA)Eliakim Maswi amesema mamlaka imeandaa mpango kabambe wa mafunzo ambapo hadi kufikia Oktoba 1,2023 Taasisi zote za Umma zitatakiwa kuwa zimesha patiwa mafunzo na kujisajili kuanza kutumia mfumo huo.

Amesema kuwa utaratibu umewekwa ili Taasisi ambazo hazijapatiwa mafunzo ziweze kuendesha ununuzi wake kwa kutumia mfumo uliopo kwa kipindi hiki cha mpito cha miezi mitatu . 

"Moja ya kuwa nguzo muhimu kwenye NeST ni kuwa na uwezo wa kusajili watumiaji Kwa haraka,urahisi na kwa usahihi, watumiaji watatakiwa kujisajili na kuweka taarifa zinazotakiwa kutokana na aina ya shughuli anayopanga kuifanya kwa kutumia mfumo mara moja tu,"

Hata hivyo Mkurugenzi huyo ametaja baadhi ya faida zitakazopatikana baada ya kuanza kutumika Kwa mfumo wa NeST kuwa ni pamoja na kuongezeka kwa uwazi na kuondoa mwingiliano wa kibinadamu na kuongeza uwajibikaji. 



Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post