Na Dotto Kwilasa,DODOMA.
MBUNGE wa Geita vijijini Joseph Musukuma ameishauri Serikali kuona haja ya kuwa na utaratibu wa kuwapeleka Waandishi wa habari kushuhudia hali na mfumo wa miradi mbalimbali inayoanzishwa nchini ili kuwa na uhalisia wa hali ilivyo na kusaidia kupeleka taarifa sahihi kwa jamii zisizoweza kuzua taharuki.
Ameyasema hayo jijini hapa Leo June 9 aliokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu uvumi ulioshika kasi hivi sasa kwenye mitandao ya kijamii ambapo baadhi ya watu wamekuwa wakisema kuwa bandari hiyo imeuzwa na wengine wakisema imekodishwa kwa mkataba wa miaka100.
Amesema,"Kama serikali iliweza kutupeleka wabunge basi ione haja pia kuwapeleka waandishi zaidi ya 100 kushuhudia hali ilivyo mbaya bandarini,"amesema
Kuhusu kuhusishwa kwenye mpango wa kupewa gari na Kampuni ya Dubai ili mambo yaende Mbunge huyo amesema,"Mimi sijahongwa,Nina mali zangu na hata hiyo gari wanayosema nimehongwa nimenunua mwenyewe na vielelezo vipo,Mimi sio kama wao,"amefafanua.
Pia amewataka Watanzania kutoyumbwisha na maneno ya watu wasioitakia mema nchi bali waunge mkono jidihada za Rais Samia Suluhu Hassan kwenye uwekezaji mkubwa wa bandari ya Dar es salaam ambao utakuwa na tija kwa wafanyabiashara nadi na nje ya nchi.
"Mimi nimefika Dubai nimejionea namna bandari za wenzetu zinavyofanya kazi, uwekezaji unaofanywa na serikali yetu inayoongozwa na Rais Samia utasaidia sisi wafanyabiashara kutuondolea malalamiko ya kucheleweshewa kupata mizigo yetu kwenye bandarini"amesema Musukuma
Akieleza hali iliyopo sasa katika bandari kwenye upokeaji wa mizigo Mbunge huyo amesema hali ni mbaya mizigo inachukua muda mrefu na inasababisha wafanyabiashara wengi kuagiza mizigo kupitia bandari nyingine ikiwemo bandari ya Mombasa.
"Rais ni taasisi siyo mtu mmoja inawatu wengi sio kwamba wanavyozungumza mitandaoni hakuna tafiti zilizofanyika, Ikulu imefanya utafiti na sisi wabunge baadhi tulienda kuona na kuona ni kuamini, na sio wanaozungumza mitandaoni wanauwezo mkubwa sana sio kweli unaweza uakawa na uwezo mukubwa wa kuzungumza mitandaoni lakini hujui,"amesema
Vile vile aliwataka watanzania kuunga mkono azimio hilo na kama kunamapunguvu yatasimama kwenye mkataba kwani kwa sasa kinachojadiliwani ni makubaliano ya nchi na nchi na hakuna aliyeuona mkataba huo.
"Nawahakikishia watanzania maneno yanayoandikwa kwenye mitandao sio ya kweli kwasababu hata Rais Samia atastaafu na yeye ataishi maisha kama ya kwetu si kweli kama ataenda kusaini mkataba ambao hauna maslahi kwa Taifa hili labda yeye kama iwe akistaafu anahama Tanzania lakini hapana tusikatishane tamaa,"amesisitiza
Hata hivyo ameeleza watanzania wamekuwa na tabia ya kuzusha taarifa za uongo na kueleza kuwa hakuna mkataba wa kimkakati ambao umewahi kufanyika kwenye awamu zote bila kuwa na kelele na kelele ambazo zinatengenezwa na watu wasiiitakia mema nchi .
"Hata kwenye uongozi wa serikali ya awamu ya tano chini ya Hayati Rais Magufuli, alipotaka kuanza ujenzi wa bwawa la kufua umeme Rufiji wapo waliopiga kelele lakini serikali haikukatishwa tamaa,wakati ule watu walipiga sana kelele kuliko hata hizi lakini Magufuli alijenga bwawa la Rifiji na hivisasa bwawa hilohilo watu wanaliombea kura wakati wa uchaguzi,"amesema.