REDESO KISHAPU YAZINDUA MRADI MPYA




Na Sumai Salum - Kishapu
Shirika lisilokuwa la kiserikali REDESO wilayani Kishapu Mkoani Shinyanga limezindua mradi wa Kuimarisha ustahimilivu wa kipato na kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi kwenye mnyororo wa thamani wa zao la mkonge Mkoani Shinyanga ambapo utakuwa katika kata tano ambazo ni Kishapu,Uchunga,Shagihilu,Lagana na Negezi.


Uzinduzi huo umefanyika leo Juni 2,2023 katika ofisi za Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Kishapu ambapo Meneja mkuu wa kitengo cha kutafuta Fedha za miradi Bi.Christina John amesema kuwa mradi huo ni wa miaka 3 na bajeti yake ni Tsh.367,718,000 ambapo Care International imepata ufadhili wa fedha kutoka kwa Tanzania Fund Friends.


Hata hivyo Meneja huyo amesema lengo hasa la kuleta mradi huo wilayani Kishapu ni kuongeza uzalishaji, lishe, kuongeza kipato, uhimilivu katika kukabiliana na mabadiliko tabianchi,usawa,ushawishi na upatikanaji wa soko la uhakika la zao la mkonge kupitia wakulima wadogo na yote hayo ni ili kurudisha hali ya mwanzo ya uzalishaji kabla ya janga la Uviko-19.


Aidha akizungumza kwenye uzinduzi huo meneja mradi REDESO Kishapu Bw. Charles Buregeya amesema kuwa wanufaika wa mradi 70% ni wanawake na 30% ni wanaume ,wanufaika wa moja kwa moja katika mradi huo ni 1,200 na wasio wa moja kwa moja ni 6000 ambapo kuna mradi wa zao la mkonge,ufugaji kuku aina ya Saso,bustani za mbogamboga kwani hii itawasaidia kupata fedha za kuendesha maisha wakati wakisubilia miaka 3 ya uvunaji mkonge.


Hata hivyo Buregeya ameongeza kuwa hadi hii leo tayari wameanza utekelezaji wa mradi wa kuku pamoja na ukarabati na ujengaji wa vitalu nyumbav(green houses) 2 katika jijini cha Mihama na Lagana ambapo wanufaika wamepanda nyanya huku vifaranga vya kuku vikiwa na zaidi ya mwezi mmoja.


Kwa upande wake Mdau wa mradi wa kuku kutokea kata ya Ukenyenge Bi. Rehema Ally amesema kuwa mradi wa ufugaji kuku ni mzuri kwani amesomesha watoto wake 7 kwenye shule binafsi wakati akiishi na kuku na sasa mradi huu utamasaidia kufuga kuku kibiashara.


Aidha Bi. Annastazia Christopher ni mdau wa kuongeza thamani (usinga) kutokea kata ya Isoso licha ya kuipongeza Care kwa kuwa mfadhili wa REDESO amesema kuwa kutafutiwa kwa masoko ya bidhaa zao itakuwa mkombozi kwao kwani itawafanya wanawake wengine kukimbilia fursa ya utengenezaji wa bidhaa hizo.


Kwa upande wake Mtendaji wa kata ya Uchunga Bw. Ignas Mpiluka amesema kuwa atahakikisha anafuatilia vema mradi huo katika vijiji vyote vya mradi wake huku akiahidi kuendelea kutoka elimu ya mikopo ya fedha kwa wanakikundi yenye riba nafuu kwa lengo la kuhakikisha uchumi wa mtu mmoja mmoja na kata unaongezeka.


Mwakilishi kutoka ofisi ya mkuu wa mkoa ambaye pia ni Afisa Maendeleo Bi. Rehema Edson amewapongeza Care kuwa mfadhili ndani ya mkoa wa Shinyanga na ametoa rai kwa watumishi wa ngazi ya wilaya,kata na vijiji kuhakikisha wanakuwa wafuatiliaji maeneo yote ya mradi kwa ajili ya kufikia Kishapu yenye hali nzuri ya kiafya na kiuchumi.


Hata hivyo mradi huo Shirika la Care INTERNATIONAL limekusudia kulenga kundi la wanawake kuwa wanufaika wakubwa kutokana na mila na desturi kandamizi zinazowafanya wanawake wawe nyuma kuchangamkia fursa za maendeleo katika jamii na taifa kwa ujumla.
Mwakilishi kutoka ofisi ya mkuu wa mkoa ambaye pia ni Afisa Maendeleo Bi. Rehema Edson akizungumza
Nkinda Kulwa mdau wa zao la mkonge na mwenyekiti SHIWAMKI
Ignas Mpiluka mtendaji kata ya Uchunga
Mwakilishi kutoka Care Tanzania akielezea mradi Bi. Christina John
Mwakilishi kutoka Care Tanzania akielezea mradi Bi.Christina John
Meneja miradi REDESO Kishapu Charles Buregeya
Meneja miradi REDESO Kishapu Charles Buregeya
Mdau wa mradi wa kuku kutoka Ukenyenge Bi.Rehema Ally
Mdau wa kuongeza thamani (usinga) kutokea Isoso Bi. Annastazia Christopher

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post