MAAFISA USHIRIKA KAGERA WATAKIWA KUSIMAMIA UTEKELEZAJI WA 'MUVU'




Mrajis Msaidizi wa Vyama vya Ushirika anayesimamia Masoko na Uwekezaji Revocatus Nyagiro akiongea na Maafisa Ushirika wakati wa kikao cha Mafunzo ya Mfumo wa Usimamizi wa Vyama vya Ushirika 'MUVU' mkoani Kagera.


Mrajis Msaidizi wa mkoa wa Kagera Robert George akisisitiza jambo wakati wa kikao cha Mafunzo ya 'MUVU'




Mkuu wa Kitengo cha TEHAMA Hermis Rulagirwa akifafanua jambo wakati wa kikao cha Mafunzo ya 'MUVU' mkoani Kagera.

Sehemu ya washiriki wakifatilia mada mbalimbali wakati wa kikao cha mafunzo ya Usimamizi wa Mfumo wa Usimamizi wa Vyama vya Ushirika kwa Maafisa Ushirika na Watendaji wa Vyama yaliyoratibiwa na Tume ya Maendeleo ya Ushirika kwa lengo la kukuza uelewa wa matumizi ya Mfumo huo kilichofanyika Bukoba Mkoani Kagera .



Na.Mwandishi Wetu

Maafisa Ushirika wametakiwa kusimamia matumizi ya Mfumo wa TEHAMA wa Usimamizi wa vyama vya Ushirika 'MUVU' kwa lengo la kuhakikisha mnyororo wa uzalishaji na ukusanyaji wa mazao unafanyika kwa usahihi na Mkulima anapata malipo sahihi na kwa wakati.

Ameyasema hayo Mrajis Msaidizi wa Vyama vya Ushirika anayesimamia Masoko na Uwekezaji, Revocatus Nyagiro, wakati wa kikao cha mafunzo ya Usimamizi wa Mfumo wa Usimamizi wa Vyama vya Ushirika kwa Maafisa Ushirika na Watendaji wa Vyama yaliyoratibiwa na Tume ya Maendeleo ya Ushirika kwa lengo la kukuza uelewa wa matumizi ya Mfumo huo kilichofanyika Bukoba Mkoani Kagera Juni 19, 2023.

Amefafanua kuwa ni wajibu wa Maafisa Ushirika kuhakikisha kuwa wanawapa watendaji wa Vyama vya Ushirika ushirikiano wa kutosha wa kutumia na kuelewa Mfumo huo wa Usimamizi katika hatua za ukusanyaji wa mazao kutoka kwa wakulima, uandaaji wa taarifa sahihi za mazao kwenye ghala, uuzaji na mkulima kupata mrejesho katika kila hatua kwa njia ya ujumbe mfupi wa Simu.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post