WALIMU WA SHULE YA MSINGI BUHANGIJA MANISPAA YA SHINYANGA WAPEWA MAFUNZO ELIMU JUMUISHI

Walimu wa Shule ya Msingi Buhangija Manispaa ya Shinyanga wapewa mafunzo ya elimu jumuishi

Na Marco Maduhu,SHINYANGA

WALIMU wa Shule ya Msingi Buhangija Manispaa ya Shinyanga, wamepewa mafunzo ya elimu Jumuishi na Misingi yake, ubainishaji wa watoto wenye ulemavu, ulinzi na usalama kwa watoto na uokoaji endapo yakitokea majanga ya moto tena.

Mafunzo hayo yametolewa kwa muda wa siku tatu, ambayo yamehitimishwa leo June 3,2023 kwenye ukumbi wa mikutano uliopo katika mabweni ya watoto wenye mahitaji maalumu, ambao wanasoma shule hiyo ya Msingi Buhangija Jumuishi.

Mshauri wa Mradi Elimu Jumuishi T.0. 51 Dk Ildephonce Mkama, ambao Unashirikisha Mashirika Manne ambayo ni Sense International, Tanzania Cheshire Foundation, ADD International na Light For the World, amesema elimu hiyo wanaitoa katika Shule Jumuishi 48.

Amesema Shule hizo Jumuishi 48 zinatoka katika wilaya Tatu ambazo ni Misungwi, Manispaa ya Shinyanga na Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga na wamewafikia walimu 636, wakiwamo na Maofisa elimu na wadhibiti ubora kwa lengo la kuwajengea uwezo walimu namna ya ufundishaji bora watoto wenye mahitaji maalumu.

“Mafunzo ambayo tumeyatoa ndani ya siku tatu kwa Walimu wa shule hii ya Msingi Buhangija Jumuishi, ni Elimu Jumuishi na Misingi yake, ubainishaji watoto wenye ulemavu, ulinzi na usalama wa mtoto, usalama na uokoaji,”amesema Dk.Mkama.

Naye Mgeni Afisa Elimu Kata ya Ibinzamata Manispaa ya Shinyanga Mackrine Shija akimwakilisha Katibu Tawala wa Wilaya ya Shinyanga Boniphace Chambi, amepongeza utolewaji wa mafunzo hayo, na kuwataka Walimu Maarifa ambayo wamepata wakayatumie vizuri kwa maslahi mapana ya Taifa na watoto wenye mahitaji maalumu pamoja na kuongeza ufaulu.

Aidha, mbali na utolewaji wa mafunzo hayo pia Shirika la Sense International, limetoa mkono wa pole wa vifaa vya shule kwa watoto wenye ulemavu, ambao walinusurika katika ajali ya bweni ambalo liliteketea moto, na kupoteza maisha ya watoto watatu na kunusurika 29.

Mwakilishi wa Shirika la Sense International Rajabu Mtunge ametaja vifaa vya shule ambavyo wamevitoa, kuwa ni Begi 20, Magodoro 20,Trank 20, Mashuka 20, Neti 29, Sare za shule, Madaftari 290, Boksi Nane za Kalamu pamoja na Kofia 18 za kujikinga na jua.

Mwalimu Mkuu wa Shule Msingi Buhangija Jumuishi Manispaa ya Shinyanga Fatuma Jilala, ameshukuru utolewaji wa mafunzo hayo pamoja na utolewaji wa vifaa vya shule kwa watoto ambao walinusurika katika ajali ya bweni kuteketea na moto novemba mwaka jana na kupoteza wanafunzi watatu.
Mgeni Rasmi Afisa Elimu Kata ya Ibinzamata Manispaa ya Shinyanga Mackrine Shija akimwakilisha Katibu Tawala wa Wilaya ya Shinyanga Boniphace Chambi, akizungunza kwenye uhitimishaji wa mafunzo hayo.
Afisa Elimu Taaluma Manispaa ya Shinyanga Wingwila Kitila akizungumza kwenye uhitimisha mafunzo hayo.
Afisa Elimu Maalumu Manispaa ya Shinyanga Edward Mdagata akizungumza kwenye uhitimisha mafunzo hayo.
Mshauri wa Mradi Elimu Jumuishi T.0. 51 Dk Ildephonce Mkama, akielezea utekelezaji wa mradi huo kwa walimu ambao wanafundisha Shule Jumuishi.
Mwakilishi wa Shirika la Sense International Rajabu Mtunge, akielezea namna walivyoguswa na tukio la watoto wenye ulemavu kupoteza maisha mara baada ya bweni lao kuteketea moto na kuamua kutoa mkono wa pole wa vifaa vya shule kwa watoto ambao walisalimika.

Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Buhangija Fatuma Jilala, akitoa shukrani kwa kupata mafunzo hayo, pamoja na vifaa vya shule kwa wanafunzi wenye ulemavu ambao walinusurika katika ajili ya bweni kuteketea moto.

Mkuu wa Jeshi la Zimamoto na uokoaji wilaya ya Shinyanga Ispekta Stanley Luhwago akitoa mafunzo ya usalama na uokoaji kwa walimu wa shule ya Msingi Buhangija Jumuishi, namna ya kujikinga na majanga ya moto na kuanza kuuzima wakatika akisubiri Jeshi hilo kufikia eneo la tukio.
Mkuu wa Jeshi la Zimamoto na uokoaji wilaya ya Shinyanga Ispekta Stanley Luhwago, akitoa elimu namna ya kujikinga na majanga ya moto na kuuzima moto kwa mwalimu mwenye ulemavu wa macho Elizabeth Matheo.
Mkuu wa Jeshi la Zimamoto na uokoaji wilaya ya Shinyanga Ispekta Stanley Luhwago, akitoa elimu kwa vitendo namna ya kukabiliana na majanga ya moto na kuuzima.
Walimu wakiwa kwenye mafunzo.
Mafunzo yakiendelea.
Mafunzo yakiendelea.
Mafunzo yakiendelea.
Mafunzo yakiendelea.
Mafunzo yakiendelea.
Mafunzo yakiendelea.
Mafunzo yakiendelea.
Mafunzo yakiendelea.
Mafunzo yakiendelea.
Mafunzo yakiendelea.
Mafunzo yakiendelea.
Mafunzo yakiendelea.
walimu wakiwa kwenye mafunzo.
Mafunzo yakiendelea.
Afisa Elimu Kata ya Ibinzamata Manispaa ya Shinyanga Mackrine Shija, (kushoto) akipokea vifaa vya shule kutoka kwa mwakilishi wa Shirika  Sense Internatonal Rajabu Mtunge kwa ajili ya kuvikabidhi kwa wanafunzi wenye ulemavu ambao walinusurika na ajali ya moto mara baada ya bweni kuteketea moto.
Afisa Elimu Kata ya Ibinzamata Manispaa ya Shinyanga Mackrine Shija, (kushoto) akipokea vifaa vya shule kutoka kwa mwakilishi wa Shirika la Sense Internatonal Rajabu Mtunge kwa ajili ya kuvikabidhi kwa wanafunzi wenye ulemavu ambao walinusurika na ajali ya moto mara baada ya bweni kuteketea moto.
Afisa Elimu Kata ya Ibinzamata Manispaa ya Shinyanga Mackrine Shija, (kulia) akikabidhi vifaa vya shule kwa watoto wenye ulemavu ambao wanasoma shule ya msingi buhangija Jumuishi ambavyo vimetolewa na Shirika la Sense International, (kushoto) ni Mwalimu Mkuu wa shule hiyo Futuma Jilala.

Afisa Elimu Kata ya Ibinzamata Manispaa ya Shinyanga Mackrine Shija, (kulia) akikabidhi magodoro kwa watoto wenye ulemavu ambao wanasoma shule ya msingi buhangija Jumuishi ambavyo vimetolewa na Shirika la Sense International, (kushoto) ni Mwalimu Mkuu wa shule hiyo Futuma Jilala.
Muonekano wa vifaa vya shule ambavyo vimetolewa na Shirika la Sense International
Wanafunzi wenye ulemavu mbalimbali na wenye Ualbino ambao wanasoma na kulelea katika kituo cha Buhangija wakiwa kwenye kukabidhiwa vifaa vya shule.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post