KAMPUNI YA WELLWORTH HOTELS AND LODGES YAFAFANUA TAARIFA ZA UPOTOSHAJI MTANDAONI KUHUSU MRADI WA LAKE MAGADI SERENGETI








********

Na Mwandishi Wetu.

Kampuni ya Wellworth Hotels and Lodges Ltd imetoa ufafanuzi juu ya taarifa za upotoshaji zilizotolewa kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter zenye lengo la kuichafua kampuni hiyo na biashara zake.


Taarifa iliyotolewa Kwa vyombo vya Habari Mei 31 2023 na Mkurugenzi mtendaji wake Zulfikar Ismail zimedai kuwa katika ukurasa huo wa Twitter unaojitambulisha kama kigogo media inc@kogogo2014 kuwa ujenzi wa mradi wa hoteli ya kitalii Lake Magadi iliyoko ndani ya Hifadhi ya Serengeti kuwa haukufuata taratibu hazina ukweli wowote bali ni upotoshaji unaopaswa kupuuzwa.


"Taarifa zilizochapishwa kwenye mtandao huo wa kijamii kuanzia tarehe 30 Mei 2023 ni ya uongo na isiyo na utafiti wowote, na imekosa uhalali wa kuheshimiwa na kupokelewa na jamii kwani imejaa maneno ya kuokoteza barabarani kwani kampuni hiyo imekua ikifuata sheria katika utekelezaji wa miradi yake na kwa muda mrefu imejijengea heshima kubwa kutokana na ubora wa hoteli zake hivyo haitakubali kuchafuliwa Kwa namna yoyote ile", imesema taarifa hiyo.


Kuhusu ujenzi wa Loji/ Hoteli inayojengwa kwenye eneo la Magadi Serengeti taarifa hiyo imesema kuwa mradi huo umefuata hatua na taratibu zote za kisheria ambapo Kwa sasa iko katika hatua za mwisho kukamilika na inatarajiwa kufunguliwa katika robo ya kwanza ya mwaka 2024.


Mradi wa hotel hiyo ya Kitalii ya nyota Tano( five star hotel) ina idadi ya vyumba 75 na ina thamani ya shilingi Bilioni 43.68 yenye uwezo wa kupokea wageni 150 Kwa wakati Mmoja.




Kuhusu Manufaa ya Mradi huo taarifa hiyo imesema ni pamoja na kutoa ajira Kwa wafanyakazi zaidi ya 180 wa Moja Kwa Moja , ajira zisizo za Moja Kwa Moja kama vile kuuza bidhaa zao kwenye hoteli hiyo, ongezeko la watalii, kuchangia pato la Taifa Kwa kulipa Kodi sambamba na utekelezaji Kwa vitendo dhana ya Royar Tour iliyofanywa na Rais Dk Samia Suluhu Hassan katika kukuza sekta ya Utalii hapa nchini.


Aidha kampuni ya Wellworth Hotels anda Lodges Ltd imeishukuru serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kwa kuendelea kuweka Mazingira bora ya uwekezaji hapa nchini kwamba wao kama wawekezaji wazawa wataendelea kushirikiana na serikali katika Kuendelea kukuza biashara hapa nchini kupitia hotel zake za kitalii.


Hata hivyo kupitia taarifa hiyo Kampuni hiyo imewaomba Watanzania wazidi kuinga mkono serikali ya Awamu ya sita nakuwapuuza wale maadui wachache wa maendeleo hapa nchini wakiwemo wale wanaotoa habari za kupotisha Kwa lengo la kuwakatisha tamaa wawekezaji wazawa.
Sambamba na taarifa ya Kampuni hiyo ,Mei 31 2023 Mamlaka ya Usimamizi wa hifadhi za Taifa (TANAPA) iliyotolewa kwa vyombo vya habari na Afisa Uhifadhi Mwandamizi Kitengo Cha Mawasiliano Catherine Mbena imesema kuwa Kampuni ya Wellworth Hotels and Lodges Ltd ilipewa eneo la Ujenzi wa Loji katika eneo la ziwa magadi Serengeti mwaka 2015 ,kwa barua kumb.Na.TNP/HQ/P.30/17 ya tarehe 04/06/2015 ,ambapo inasema mwekezaji huyo alikamilisha taratibu zote ndani ya shirika pamoja na baraza la Uhifadhi na Usimamaizi wa Mazingira (NEMC) inayomtaka mwekezaji kufanya tathmin za athari za kimazingira kabla ya kuanza ujenzi wa Loji ndani ya hifadhi ambapo ulikamilika na kupewa cheti cha Mazingira namba EC/EIS/2435 cha tarehe 16/05/2016.


Taarifa hiyo ya TANAPA inaendelea kusema kuwa kutolewa kwa cheti cha Mazingira kwa undelezaji wa eneo hilo la uwekezaji linakidhi vigezo vya kuendeleza nakuongeza kuwa ujenzi wa Loji hiyo ulianza mwaka 2017 na kuendelea hadi mwaka 2018 ambapo ujenzi ulisimama kufuatia janga la UVIKO 19 na mwaka 2021 kazi ya ujenzi wa Mradi huo iliendelea tena

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post