KATAMBI AONYA UTUMIKISHWAJI NA UNYANYASAJI WA WATOTO




Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe.Patrobas Katambi akitoa taarifa kwa umma jijini Dodoma kuhusu maadhimisho ya siku ya kimataifa ya kupinga utumikishwaji wa watoto.

Na Mwandishi Wetu, DODOMA

Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe.Patrobas Katambi amesema serikali haitavumilia kuona watoto wanakosa haki zao za msingi kwa sababu ya utumikishwaji na unyanyasaji.

Mhe.Katambi ametoa kauli hiyo Juni 12, 2023 jijini Dodoma alipokuwa akitoa taarifa kwa umma kuhusu maadhimisho ya siku ya kimataifa ya kupinga utumikishwaji wa watoto ambayo hufanyika ifikapo Juni 12 ya kila mwaka.

Amesema utumikishwaji watoto katika sekta za uchumi ikiwamo mashamba na migodini huchangia watoto kukosa haki zao za msingi za kupata elimu na makuzi katika jamii zao.

“Nitoe wito kwa jamii kuacha vitendo vya kutumikisha watoto na kutofautisha kazi ya mtoto ambazo zinawapa fursa ya kujifunza stadi za Maisha bila kuathiri maendeleo ya kielimu, kijamii na makuzi,”amesema.

Aidha, amesisitiza jamii na wadau wa maendeleo kuendelea kushirikiana na serikali katika mapambano dhidi ya utumikishwaji wa watoto na wakulima na vyama vyote vya ushirika wa mazao ya biashara vihakikishe kuwa hakuna uzalishaji wa zao lolote unaohusisha utumikishwaji wa mtoto.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post