Picha : WADAU WA MASUALA YA JINSIA WAKIFUATILIA MUBASHARA HOTUBA YA BAJETI YA TAIFA 2023/2024

Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) umewakutanisha wadau wa masuala ya jinsia katika Mjadala na Uchambuzi wa Bajeti ya Taifa ya Mwaka wa Fedha 2023/2024 maarufu ‘Kijiwe cha Kahawa’ ili kuwapa fursa kufuatilia mubashara Taarifa ya Hali ya Uchumi kwa mwaka 2022 na Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa mwaka 2023/2024 pamoja na Hotuba ya Bajeti ya Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 ikiwasilishwa Bungeni Jijini Dodoma na Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Soma pia : 

TGNP YAKUTANISHA WADAU KATIKA KIJIWE CHA KAHAWA KUFUATILIA MUBASHARA TAARIFA HALI YA UCHUMI NA BAJETI YA TAIFA

Wadau wa masuala ya Kijinsia wakiwa katika Ukumbi wa TGNP Mabibo Jijini Dar es salaam leo Alhamisi Juni 15,2023 wakifuatilia mubashara Hotuba ya Bajeti ya Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 ikiwasilishwa Bungeni Jijini Dodoma na Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post