WAISLAMU WAHAMASISHWA KUCHINJA WANYAMA WALIONONA SIKUKUU YA EID AL-ADHA




Na Marco Maduhu,SHINYANGA

WAUMINI wa Dini ya Kiislamu wametakiwa katika kusherehekea Sikukuu ya kuchinja ya Eid al-Adha, wakachinje Wanyama walionona na wenye rangi nzuri.
Hayo yamebainishwa leo Juni 29, 2023 na Sheikh wa Wilaya ya Shinyanga Soud Kategire kwenye Swala ya Eid al-Adha iliyofanyika katika viwanja vya Sabasaba Manispaa ya Shinyanga.
Amesema katika kusherekea Sikukuu ya kuchinja ni vyema Waislamu wakachinja Wanyama walionona na wenye rangi nzuri, pamoja na kusherehekea sikukuu hiyo kwa Amani na kumcha mwenyezi Mungu.

“Katika kusheherekea sikukuu hii ya kuchinja Eid al-Adha nendeni mkachinje Wanyama walionona na wenye rangi nzuri,”amesema Sheikh Kategire.
Naye Sheikh wa Mkoa wa Shinyanga Ismail Makusanya, amewataka Waumini wa Kiislamu katika kusherehekea sikukuu hiyo, wakafurahi na watu wenye uhitaji, wakiwamo Yatima, Wajane, Wazee, watoto wenye Ualbino na majirani kwa kula nao chakula cha pamoja, na siyo kuitumia siku hiyo kwa kufanya Maasi.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post