WAFANYABIASHARA WAMETAKIWA KUCHANGAMKIA FURSA UWEKEZAJI ENEO MACHIMBO YA BUZWAGI, KAHAMA KUWA DUBAI NDOGO

 

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme akizungumza na Wafanyabiashara mkoani Shinyanga.

Na Marco Maduhu, SHINYANGA

MKUU wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme, amewataka Wafanyabiashara mkoani Shinyanga, kuchangamkia fursa za uwekezaji katika eneo lililokuwa la Machimbo ya dhahabu Buzwagi ambalo limegeuzwa kuwa kitovu cha uchumi(Samia Special Economic zone) na kuinuka kiuchumi.

Mndeme amebainisha hayo leo Juni 20,2023 Wakati akizungumza na wadau wa Biashara, Viwanda na Wawekezaji, kikao kilichofanyika kwenye ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa huo wa Shinyanga.

Amesema Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia, inatambua na kuthamini mchango Mkubwa wa Wafanyabiashara katika kukuza uchumi wa Nchi, ndiyo maana imeendelea kuwatengea maeneo ya uwekezaji, likiwamo na eneo lililokuwa la Machimbo ya Mgodi wa Buzwagi lenye ukubwa wa Hekta 1,333.

"Wafanyabiashara karibuni muwekeze katika eneo hili lililokuwa la Machimbo ya Buzwagi na kuongeza thamani ya mazao, tayari kuna wawekezaji kutoka Ndani na Nje ya nchi wameshakuwa na nia ya kuwekeza hapo, hivyo na nyie hapa Shinyanga changamkieni fursa hii,"amesema Mndeme.

"Pia kwenye lilileshimo ambalo lilikuwa likichimbwa madini tunakaribisha wawekezaji wa Utalii, hivyo tumemieni pia fursa hii kuwekeza Mahoteli ya Kitalii tunataka Kahama iwe Dubai ndogo ya Tanzania," ameongeza Mndeme.

Amesema pia wilaya ya Kahama wametenga pia eneo lenye ukubwa wa Hekali 2,000,ambalo litajengwa Bandari Kavu eneo la Nyanshimbi, na hivyo Shinyanga kuwa na Bandari mbili ikiwano ya Isaka, na kuifanya Shinyanga kuwa kituo cha uchumi na kupanua wigo wa ajira kwa vijana.

Aidha, amewahakikishia Wafanyabiashara mkoani humo kuwa Serikali ipo pamoja nao, na wale ambao wanataka maeneo ya Uwekezaji watapewa maeneo bila ya Urasimu wowote, na kuwataka wachangamkie fursa za uwekezaji ikiwa maeneo yapo na yana miundombinu yote.

Katika hatua nyingine Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, amewataka wafanyabiashara hao, kumuunga Mkono Rais Samia katika utendaji wake kazi wa kutumikia Watanzania, na kupuuza maneno ya upotoshaji juu ya Mkataba wa Bandari ya Dar es salaam na Dubai.

Amesema katika Mkoa huo Rais Samia ndani ya Utawala wake, ameshatoa kiasi cha fedha zaidi ya Bilioni 600 kwa ajili ya utekelezaji wa Miradi mbalimbali ya Maendeleo, ukiwamo na ukarabati wa Uwanja wa Ndege, ambao ni kilio kikubwa cha wafanyabiashara.

Nao baadhi ya Wafanyabiashara akiwamo Salumu Khamis ambaye ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Jambo, wameipongeza Serikali kwa kuleta mabadiliko ya kimaendeleo katika Mkoa huo wa Shinyanga, na kuomba ujenzi wa ukarabati wa Uwanja wa Ndege ukamilishwe haraka sababu wanapoteza muda mwingi wa kibiashara.

Akizungumzia issue ya Bandari, amesema Wafanyabiashara ndiyo waathirika, na wanawashaghaa watu ambao wamekuwa wakipinga Mkataba huo wa Bandari sababu siyo Waathirika, na kubainisha kuwa wanaiunga Mkono Serikali juu ya uwekezaji wa Bandari na kuomba wasihusishwe na Wanasiasa.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme akizungumza na Wafanyabiashara.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme akiendelea kuzungumza na Wafanyababiashara.
Kikao cha wafanyabiashara kikiendelea.
Mfanyabiashara Maarufu mkoani Shinyanga Salum Khamis (JAMBO) akichangia hoja kwenye kikao hicho.
Wafanyabiashara wakiendelea na kikao.
Mfanyabiashara mkoani Shinyanga Gillitu Makula akichangia hoja kwenye kikao hicho.
Wafanyabiashara wakiendelea na kikao.
Wafanyabiashara wakiendelea na kikao.
Wafanyabiashara wakiendelea kuchangia hoja kwenye kikao hicho.
Wafanyabiashara wakiendelea na kikao.
Wafanyabiashara wakiendelea na kikao.
Wafanyabiashara wakiendelea na kikao.
Wafanyabiashara wakiendelea na kikao.
Wafanyabiashara wakiendelea na kikao.
Wafanyabiashara wakiendelea na kikao.
Wafanyabiashara wakiendelea na kikao.
Wafanyabiashara wakiendelea na kikao.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Kahama Anderson Msumba (kulia) akiwa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Saimon Berege kwenye kikao hicho.
Wafanyabiashara wakiendelea na kikao.
Wafanyabiashara wakiendelea na kikao.
Wafanyabiashara wakiendelea na kikao.
Wafanyabiashara wakiendelea na kikao.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Kahama Anderson Msumba (kulia) akiwa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Saimon Berege kwenye kikao hicho.
Wafanyabiashara wakiendelea na kikao.
Wafanyabiashara wakiendelea na kikao.
Wafanyabiashara wakiendelea na kikao.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post