UJENZI MABWENI YA WASICHANA UMETAJWA MKOMBOZI KUTIMIZA NDOTO ZA MTOTO WA KIKE

 

Ujenzi Mabweni ya wasichana umetajwa mkombozi kutimiza ndoto za mtoto wa kike

Na Marco Maduhu, GEITA

WANAFUNZI ambao wanasoma katika Shule ya Sekondari Msalala Halmashauri ya Nyang’hwale mkoani Geita, wamesema ujenzi wa mabweni ya wasichana katika shule za Sekondari umekuwa na msaada mkubwa kwa wanafunzi wa kike kutimiza ndoto zao.
Bweni la Wasichana shule ya Sekondari Msalala Halmashauri ya Nyang'hwale mkoani Geita.

Wanafunzi wa kike wa kidato cha Nne katika shule hiyo ambao hawajafunga shule, wamebainisha hayo jana wakati wakizungumza na waandishi wa habari, walipotembelea shule hiyo kuona ujenzi wa Mabweni, Vyumba vya Madarasa na Bwalo la Chakula, yaliyojengwa na Mgodi wa Barrick Bulyanhulu kupitia fedha za CSR.
Mwanafunzi Leonida Daniel akizungumzia umuhimu wa Mabweni ya wasichana shuleni.

Mmoja wa wanafunzi hao Leonida Daniel, amesema mtoto wa kike kusoma umbali mrefu na shule imekuwa kikwazo kikubwa kwao katika kutimiza ndoto zao, sababu hukumbana na vishawishi njiani kwa kurubuniwa na wanaume, na mwisho wa siku ana angukia kwenye mapenzi na kuambulia ujauzito.
Mwanafunzi Tusajigwe Geogre akizungumzia umuhimu wa Mabweni ya wasichana shuleni.

“Uwepo wa Mabweni ya wasichana hapa shuleni kwetu umekuwa mkombozi mkubwa kwa wanafunzi wa kike kutimiza ndoto zetu, na pia tumekuwa na muda mwingi wa kujisomea na kufanya vizuri kitaaluma,”amesema Leonida.

Makamu Mkuu wa shule hiyo ya Sekondari ya Msalala Johnmary Stephen, amesema ujenzi wa mabweni ya wasichana shule hapo umesaidia kupunguza utoro kwa wanafunzi pamoja na mimba za utotoni, ambapo kwa mwaka mzima zilikuwa zikitokea zaidi ya mimba Tano.
Makamu Mkuu wa shule ya Sekondari Msalala Halmashauri ya Nyang'hwale Johnmary Stephen.

Mrakibu kutoka Idara ya Mahusiano ya Jamii Mgodi wa Barrick Bulyanhulu William Chungu, amesema katika Wilaya hiyo ya Nyang’hwale wamekuwa wakitoa fedha za (CSR), na kutekelezwa miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwamo sekta ya elimu.
Mrakibu kutoka Idara ya Mahusiano ya Jamii Mgodi wa Barrick Bulyanhulu William Chungu.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Nyang’hwale Husna Toni, amesema tangu mwaka 2018 hadi 2023, wameshapokea fedha za (CSR) kiasi cha Sh.bilioni 4.4 fedha ambazo zimekuwa na mchango mkubwa katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwamo ujenzi wa mabweni ya wasichana.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Nyang’hwale Husna Toni, akielezea fedha za CSR zilivyochochea maendeleo.
Muonekano wa Bwalo la chakula katika shule ya Sekondari Msalala Halmashauri ya wilaya ya Nyang'hwale mkoani Geita ambalo limejengwa kwa fedha za (CSR) kupitia Mgodi wa Barrick Bulyanhulu.
Muonekano wa vyumba viwili vya Madarasa katika shule ya Sekondari Msalala Halmashauri ya wilaya ya Nyang'hwale mkoani Geita ambavyo vimejengwa kwa fedha za (CSR) kupitia Mgodi wa Barrick Bulyanhulu.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post