RAIS SAMIA ATEUA VIONGOZI MBALIMBALI


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, amefanya uteuzi wa viongozi mbalimbali.

Amemteua Bw. Omar Issa kuwa Mkuu (Chancellor) wa Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela (NM-AIST).

Bw. Issa ni Mwenyekiti wa Bodi ya TANESCO na anachukua nafasi ya Mhe. Dkt. Gharib Bilali, Makamu wa Rais Mstaafu ambaye amemaliza muda wake.

Amemteua Prof. Abel N. Makubi kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Mifupa (MOI). Prof. Makubi anachukua nafasi ya Dkt. Respicious Boniface ambaye amemaliza muda wake.

Amemteua Dkt. Abdulhamid Yahya Mzee kuwa Mkuu wa Chuo (Chancellor) cha Taifa cha Ulinzi (NDC). Dkt. Mzee alikuwa Katibu Mkuu Kiongozi Mstaafu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na anachukua nafasi ya Balozi Dkt. Marten Y. C. Lumbanga aliyemaliza muda wake.

Amemteua Dkt. Edwin Mhede kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya NMB Ple kwa kipindi cha pili.
Uteuzi huu umeanza tarehe 06 Juni, 2023

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post