Picha : MAHAFALI YA 40 YA WANACHUO WA HATUA YA TATU VETA SHINYANGA YAFANYIKA...DC SAMIZI AVUTIWA FANI YA MADINI YA VITO

Na Kadama Malunde – Malunde 1 blog

Mahafali ya 40 ya Chuo cha Ufundi Stadi Shinyanga yamefanyika ambapo jumla ya wanafunzi 79 kati yao wasichana 35 na wavulana 44 wamehitimu Elimu ya Mafunzo ya Ufundi Stadi Daraja la Tatu (III) katika fani za Umeme, Bomba, Ujenzi, Uhazili na TEHAMA na Fani ya Ufundi wa Mitambo mikubwa.

Mahafali ya 40 ya Wanachuo wa Hatua ya Tatu Chuo cha VETA Shinyanga yamefanyika leo Ijumaa Juni 9,2023 ambapo mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi.

Akizungumza wakati wa Mahafali hayo, Samizi amesema lengo la serikali ni kuimarisha vyuo vya ufundi stadi VETA hivyo kuwepo kwa vyuo vya VETA ni sehemu ya suluhisho la ajira kwa vijana kwani vyuo hivyo vinawezesha vijana kujiajiri na kuajiri wengine.

“Tunatarajia vijana hawa mara baada ya kumaliza mafunzo wakajiajiri na waajiri wengine. Nitoe wito kwa chuo muendelee kubuni fani tofauti tofauti. Matarajio yetu ni Chuo hiki kiwe chachu ya uanzishaji wa viwanda vidogo, tuwe sehemu ya waanzishaji wa viwanda vidogo”,amesema Samizi.

“Haya yote ni utekelezaji wa ilani ya uchaguzi CCM. Kumaliza kwenu masomo isiwe mwisho wa kujifunza na kujiendeleza zaidi kielimu. Undeni vikundi kwa ajili ya kupata mikopo”,ameongeza.

Mkuu huyo wa wilaya amewasihi wazazi mkoa wa Shinyanga kutumia chuo cha VETA kwa kuwapeleka vijana wakapate ujuzi.

Mkuu huyo wa wilaya ametoa wito kwa wafanyabiashara na taasisi mbalimbali kuchangamkia fursa ya kujenga hosteli/mabweni kwa ajili ya kupangisha ili kuongeza udahili wa wanafunzi wanaotoka nje ya Manispaa ya Shinyanga.
Akiwa katika chuo cha VETA kwenye karakana ya ukataji na ung’arishaji madini ya vito, Mkuu huyo wa Wilaya ameeleza kufurahishwa zaidi na Fani ya Ukataji, Ung'arishaji na Uchongaji wa madini ya vito (Gemstone cutting, polishing and carving).

“Nimepita kwenye karakana ya ukataji na ung’arishaji madini ya vito. Hongereni sana VETA kwa fani hii. Nimepewa cheni ya Rubi ,karakana hii ni nzuri na mkoa wetu ni mkoa wa kimadini. Karakana hii ina uwezo wa kuongeza thamani ya madini, tutawatangaza vijana hawa ili wakafanye kazi ya kuongeza thamani za madini yanayopatikana katika mkoa wa Shinyanga mikoa mingine”,amesema Samizi.

Kaimu Mkuu wa Chuo cha VETA Shinyanga, Magu Mabelele amesema hadi leo VETA Shinyanga inahudumia mkoa mzima wa Shinyanga hivyo kutokana na majukumu hayo bado wanakabiliwa na changamoto kadhaa ili kuwafikia wateja wake ipasavyo.

“Changamoto kubwa kuliko zote ni miundombinu ya chuo kuweza kuwahudumia wananchi wa Shinyanga katika wilaya ya Kahama na Kishapu na Shinyanga kwa sababu ya ufinyu wa mabweni tuliyonayo kwani mabweni tuliyonayo yanachukua wanafunzi 170. Hata hivyo kwa kutumia wanafunzi wetu na walimu tumefanikiwa kukarabati bweni moja na kuongeza nafasi za bweni 100 kwa ajili ya wanafunzi wa kozi za muda mfupi”,amesema Mabelele.
Kaimu Mkuu wa Chuo cha VETA Shinyanga, Magu Mabelele.

Amesema pia kuna changamoto ya upungufu wa vyumba vya madarasa, kuharibika kwa uzio wa chuo pamoja kukosekana kwa usafiri wa uhakika kutoka katikati na pembezoni mwa Manispaa ya Shinyanga ambayo huwafanya wanafunzi wa kutwa kutofika kwa wakati na mara nyingine kuwafanya kuwa watoro wa mara kwa mara hivyo kuomba wafanyabiashara ya usafirishaji abiria kuanzisha safari za daladala ili kuwarahisisha wanafunzi kutoka Mjini kwenda chuoni kwa urahisi.

“Licha ya kuwa na changamoto, chuo cha VETA Shinyanga kimekuwa mdau mkubwa wa maendeleo ya wananchi wa Manispaa ya Shinyanga kwa kushiriki katika kazi mbalimbali za kijamii ikiwemo kupanda miti,kukarabati na kusawazisha barabara, kutengeneza samani za shule na vyuo hivyo kuunga mkono juhudi za Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kuwahudumia Watanzania kikamilifu. Mfano ni huu wa leo tumekabidhi madawati 20 yenye thamani ya shilingi Milioni 1.6 kwa ajili ya wanafunzi wa shule za msingi Kolandoto na Kizumbi ambayo yatatumiwa na wanafunzi 60”,ameongeza Mabelele.

Kuhusu Fani ya vito, Mabelele amesema karakana iliyopo katika chuo hicho inaweza kusaidia kupunguza utoroshaji wa madini vito.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi akikabidhi cheti kwa Mhitimu Elimu ya Mafunzo ya Ufundi Stadi Daraja la Tatu (III) katika chuo cha VETA Shinyanga.

Naye Mratibu wa Mafunzo katika Chuo cha VETA Shinyanga, Jamary Mayala amesema Chuo cha VETA Shinyanga kinatoa mafunzo ya kozi za muda mrefu 10 na fani za muda mfupi 27.

Amesema mpaka sasa Chuo kina wanafunzi 436 wa kozi za muda mrefu kati yao 275 ni wavulana na 161 ni wasichana na wanafunzi waliodahiliwa kuanzia Januari hadi Juni 2023 wa kozi za muda mfupi ni 644 kati yao 368 ni wavulana na 276 ni wasichana.

“Chetu kimekuwa na mafanikio kadha wa kadha mfano Wanachuo wetu ngazi ya tatu waliofanya mitihani yao Juni 2022 walifaulu kwa 99.3%. Tumeshiriki utengenezaji wa samani za vyuo vipya vya wilaya za Kwimba na Kishapu na tumeshiriki miradi ya ujenzi wa vyuo vipya vya VETA vya wilaya za Kishapu na Igunga. Pia tumeweka mfumo wa Gesi kwa ajili ya kupikia chakula cha wanachuo wetu wa bweni”,amesema Mratibu huyo wa mafunzo.

Akisoma Risala kwa niaba ya wahitimu wenzake,Janeth Paul amesema wamefanikiwa kupata mafunzo ya ufundi stadi na wanaondoka chuoni wakiwa na ujuzi wa kutosha, wakijiamini kwa kufanya kazi kwa weledi bila kusimamiwa na mtu yeyote kwa ukaribu.

“Tumefanikiwa katika miradi ya ujenzi wa vyuo vya VETA wilaya za Kishapu na Igunga na hivyo kutujengea umahiri katika ujuzi wetu. Lakini pia tumeshiriki katika kazi mbalimbali za kijamii zilizofanyika katika Manispaa ya Shinyanga kama vile upandaji miti. Hali kadhalika tumeshiriki katika michezo mbalimbali ndani na nje ili kujenga afya zetu”,amesema Paul.

ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Mgeni rasmi Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi akizungumza wakati Mahafali ya 40 ya Wanachuo wa Hatua ya Tatu Chuo cha VETA Shinyanga leo Ijumaa Juni 9,2023 ambapo jumla ya wanafunzi 79 kati yao wasichana 35 na wavulana 44 wamehitimu Elimu ya Mafunzo ya Ufundi Stadi Daraja la Tatu (III) katika fani za Umeme, Bomba, Ujenzi, Uhazili na TEHAMA na Ufundi Mitambo. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mgeni rasmi Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi akizungumza wakati Mahafali ya 40 ya Wanachuo wa Hatua ya Tatu Chuo cha VETA Shinyanga leo Ijumaa Juni 9,2023
Mgeni rasmi Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi akizungumza wakati Mahafali ya 40 ya Wanachuo wa Hatua ya Tatu Chuo cha VETA Shinyanga leo Ijumaa Juni 9,2023
Kaimu Mkuu wa Chuo cha VETA Shinyanga, Magu Mabelele akizungumza wakati Mahafali ya 40 ya Wanachuo wa Hatua ya Tatu Chuo cha VETA Shinyanga leo Ijumaa Juni 9,2023
Kaimu Mkuu wa Chuo cha VETA Shinyanga, Magu Mabelele akizungumza wakati Mahafali ya 40 ya Wanachuo wa Hatua ya Tatu Chuo cha VETA Shinyanga leo Ijumaa Juni 9,2023
Wahitimu wakisoma risala wakati Mahafali ya 40 ya Wanachuo wa Hatua ya Tatu Chuo cha VETA Shinyanga leo Ijumaa Juni 9,2023
Mratibu wa Mafunzo katika Chuo cha VETA Shinyanga, Jamary Mayala akizungumza wakati Mahafali ya 40 ya Wanachuo wa Hatua ya Tatu Chuo cha VETA Shinyanga
Mratibu wa Mafunzo katika Chuo cha VETA Shinyanga, Jamary Mayala akizungumza wakati Mahafali ya 40 ya Wanachuo wa Hatua ya Tatu Chuo cha VETA Shinyanga
Diwani wa kata ya Kizumbi, Reuben Kitinya akizungumza wakati Mahafali ya 40 ya Wanachuo wa Hatua ya Tatu Chuo cha VETA Shinyanga
Awali Wanafunzi 79 kati yao wasichana 35 na wavulana 44 waliohitimu Elimu ya Mafunzo ya Ufundi Stadi Daraja la Tatu (III) katika fani za Umeme, Bomba, Ujenzi, Uhazili na TEHAMA na Ufundi Mitambo wakiingia ukumbini kwa kucheza

Awali wahitimu Elimu ya Mafunzo ya Ufundi Stadi Daraja la Tatu (III) katika fani za Umeme, Bomba, Ujenzi, Uhazili na TEHAMA na Ufundi Mitambo wakicheza muziki
Wanafunzi wa Fani ya Upishi (Food Production) wakitoa burudani wakati Mahafali ya 40 ya Wanachuo wa Hatua ya Tatu Chuo cha VETA Shinyanga
Vijana wa kundi la sanaa maarufu Kambi ya Nyani wakitoa burudani wakati Mahafali ya 40 ya Wanachuo wa Hatua ya Tatu Chuo cha VETA Shinyanga
Vijana wa kundi la sanaa maarufu Kambi ya Nyani wakitoa burudani wakati Mahafali ya 40 ya Wanachuo wa Hatua ya Tatu Chuo cha VETA Shinyanga
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi (kulia) akiwa kwenye karakana ya Ukataji, Ung'arishaji na Uchongaji wa madini ya vito katika chuo cha VETA Shinyanga. 
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi (kulia) akiangalia cheni ya madini ya Rubi kwenye karakana ya Ukataji, Ung'arishaji na Uchongaji wa madini ya vito katika chuo cha VETA Shinyanga. 
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi (kulia) akiangalia cheni ya madini ya Rubi kwenye karakana ya Ukataji, Ung'arishaji na Uchongaji wa madini ya vito katika chuo cha VETA Shinyanga. 
Mwalimu katika chuo cha VETA Shinyanga akimwelezea Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi kuhusu Fani ya Ukataji, Ung'arishaji na Uchongaji wa madini ya vito (Gemstone cutting, polishing and carving)

Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi akikipongeza chuo cha VETA Shinyanga kuanzisha Fani ya Ukataji, Ung'arishaji na Uchongaji wa madini ya vito (Gemstone cutting, polishing and carving)
Mwalimu wa chuo cha VETA Shinyanga (Madam Judy) akimwelezea Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi (katikati) kuhusu fani ya Urembeshaji na Mapambo (Salon annd Decoration)
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi (kulia) akizungumza na mwanafunzi anayesomea fani ya Urembeshaji na Mapambo (Salon annd Decoration)
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi (katikati) akiwa katika darasa la Fani ya Uhazili na TEHAMA katika chuo cha VETA Shinyanga
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi (wa pili kulia) akiwa katika darasa la Fani ya Uhazili na TEHAMA katika chuo cha VETA Shinyanga
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi (kulia) akiwa katika darasa la Fani ya Umeme katika chuo cha VETA Shinyanga
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi (aliyevaa kiremba cha bluu) akiwa katika darasa la Fani ya Ubunifu, Ushonaji na Teknolojia ya nguo katika chuo cha VETA Shinyanga
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi (aliyevaa kiremba cha bluu) akiangalia begi la kibunifu lililotengenezwa  katika darasa la Fani ya Ubunifu, Ushonaji na Teknolojia ya nguo katika chuo cha VETA Shinyanga

Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi (aliyevaa kiremba cha bluu) akiwa amebeba begi la kibunifu lililotengenezwa  katika darasa la Fani ya Ubunifu, Ushonaji na Teknolojia ya nguo katika chuo cha VETA Shinyanga

Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi (aliyevaa kiremba cha bluu) akikabidhi madawati 10 kwa ajili ya shule ya Msingi Kolandoto yaliyotolewa na chuo cha VETA Shinyanga
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi (aliyevaa kiremba cha bluu) akikabidhi madawati 10 kwa ajili ya shule ya Msingi Kizumbi yaliyotolewa na chuo cha VETA Shinyanga

Sehemu ya madawati 20 kwa ajili ya shule ya Msingi Kizumbi na Kolandoto yaliyotolewa na chuo cha VETA Shinyanga
Wanafunzi wa Fani ya Ukataji, Ung'arishaji na Uchongaji wa madini ya vito wakionesha kikombe cha ajabu walichotengeneza ambacho kinabadilika rangi kutoka nyeusi kuwa nyeupe na kuonesha picha baada ya kuwekewa kimiminika cha moto

Wahitimu Elimu ya Mafunzo ya Ufundi Stadi Daraja la Tatu (III) katika fani za Umeme, Bomba, Ujenzi, Uhazili na TEHAMA na Ufundi Mitambo wakiwa kwenye mahafali ya 40 ya chuo cha VETA Shinyanga.
Wahitimu Elimu ya Mafunzo ya Ufundi Stadi Daraja la Tatu (III) katika fani za Umeme, Bomba, Ujenzi, Uhazili na TEHAMA na Ufundi Mitambo wakiwa kwenye mahafali ya 40 ya chuo cha VETA Shinyanga.
Wahitimu Elimu ya Mafunzo ya Ufundi Stadi Daraja la Tatu (III) wakiwa kwenye mahafali ya 40 ya chuo cha VETA Shinyanga.

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi akikabidhi cheti na zawadi kwa Mhitimu Elimu ya Mafunzo ya Ufundi Stadi Daraja la Tatu (III) katika chuo cha VETA Shinyanga.

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi akipokea zawadi kutoka kwa Wanafunzi Fani ya Ubunifu, Ushonaji na Teknolojia ya nguo 
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi akipokea zawadi ya keki kutoka kwa Wanafunzi Fani ya Upishi
Wageni waalikwa wakiwa kwenye Mahafali ya 40 ya Wanachuo wa Hatua ya Tatu Chuo cha VETA Shinyanga
Meza kuu wakiwa kwenye Mahafali ya 40 ya Wanachuo wa Hatua ya Tatu Chuo cha VETA Shinyanga
Wanafunzi wakiwa kwenye Mahafali ya 40 ya Wanachuo wa Hatua ya Tatu Chuo cha VETA Shinyanga
Meza kuu wakiwa kwenye Mahafali ya 40 ya Wanachuo wa Hatua ya Tatu Chuo cha VETA Shinyanga
Walimu wa VETA wakiwa kwenye Mahafali ya 40 ya Wanachuo wa Hatua ya Tatu Chuo cha VETA Shinyanga
Wanafunzi wakiwa kwenye Mahafali ya 40 ya Wanachuo wa Hatua ya Tatu Chuo cha VETA Shinyanga
Wanafunzi wakiwa kwenye Mahafali ya 40 ya Wanachuo wa Hatua ya Tatu Chuo cha VETA Shinyanga

Meza kuu wakiwa kwenye Mahafali ya 40 ya Wanachuo wa Hatua ya Tatu Chuo cha VETA Shinyanga
Wazazi na waalikwa mbalimbali kiwa kwenye Mahafali ya 40 ya Wanachuo wa Hatua ya Tatu Chuo cha VETA Shinyanga

Mahafali ya 40 ya Wanachuo wa Hatua ya Tatu Chuo cha VETA Shinyanga yakiendelea
 Mahafali ya 40 ya Wanachuo wa Hatua ya Tatu Chuo cha VETA Shinyanga yakiendelea
Meza kuu wakiongozwa na Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi (akiyevaa kiremba rangi ya bluu) wakipiga picha ya kumbukumbu na wageni mbalimbali wakati wa Mahafali ya 40 ya Wanachuo wa Hatua ya Tatu Chuo cha VETA Shinyanga
Meza kuu wakiongozwa na Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi (akiyevaa kiremba rangi ya bluu) wakipiga picha ya kumbukumbu na wahitimu Fani ya Umeme wakati wa Mahafali ya 40 ya Wanachuo wa Hatua ya Tatu Chuo cha VETA Shinyanga
Meza kuu wakiongozwa na Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi (akiyevaa kiremba rangi ya bluu) wakipiga picha ya kumbukumbu na wahitimu Fani ya Bomba wakati wa Mahafali ya 40 ya Wanachuo wa Hatua ya Tatu Chuo cha VETA Shinyanga
Meza kuu wakiongozwa na Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi (akiyevaa kiremba rangi ya bluu) wakipiga picha ya kumbukumbu na wahitimu Fani ya Uhazili na TEHAMA wakati wa Mahafali ya 40 ya Wanachuo wa Hatua ya Tatu Chuo cha VETA Shinyanga
Meza kuu wakiongozwa na Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi (akiyevaa kiremba rangi ya bluu) wakipiga picha ya kumbukumbu na wahitimu Fani ya Ufundi wa Mitambo mikubwa wakati wa Mahafali ya 40 ya Wanachuo wa Hatua ya Tatu Chuo cha VETA Shinyanga
Meza kuu wakiongozwa na Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi (akiyevaa kiremba rangi ya bluu) wakipiga picha ya kumbukumbu na wahitimu Fani ya Ujenzi wakati wa Mahafali ya 40 ya Wanachuo wa Hatua ya Tatu Chuo cha VETA Shinyanga
Meza kuu wakiongozwa na Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi (akiyevaa kiremba rangi ya bluu) wakipiga picha ya kumbukumbu na watumishi katika chuo cha VETA Shinyanga wakati wa Mahafali ya 40 ya Wanachuo wa Hatua ya Tatu Chuo cha VETA Shinyanga
Meza kuu wakiongozwa na Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi (akiyevaa kiremba rangi ya bluu) wakipiga picha ya kumbukumbu na wazazi wakati wa Mahafali ya 40 ya Wanachuo wa Hatua ya Tatu Chuo cha VETA Shinyanga.

Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post