RAIS WA MAREKANI AANGUKA JUKWAANI

Ikulu ya Marekani ‘White House’ imesema Rais Joe Biden yuko sawa baada ya kujikwaa na kuanguka kwenye jukwaani alipokuwa kwenye sherehe za kuhitimu za Chuo cha Jeshi la Wanaanga huko Colorado Marekani.

Bw Biden, ambaye ndiye rais mkongwe zaidi wa taifa hilo anayehudumu akiwa na umri wa miaka 80, alisaidiwa kusimama na alionekana kuwa hajadhurika.


Rais alikuwa amesimama kwa takriban saa moja na nusu kupeana mikono na kila mmoja wa wanafunzi 921 waliohitimu.


Awali, mkurugenzi wa mawasiliano wa Ikulu ya White House alisema kuwa "yuko sawa".


"Kulikuwa na mfuko wa mchanga kwenye jukwaa alipokuwa akipeana mikono," Ben LaBolt aliandika kwenye Twitter baada ya kuanguka siku ya Alhamisi.


"Nilipata mchanga," rais huyo aliyetabasamu alitania waandishi wa habari alipokuwa akirejea Ikulu jioni hiyo.


Ripoti ya waandishi wa habari wa Ikulu ya White House hapo awali ilisema Bw Biden alijikwaa kwenye mfuko mweusi wa mchanga alipokuwa akipanda jukwaani.


Picha za tukio hilo zinaonyesha Bw Biden akionekana kuelekeza moja ya mifuko miwili ya mchanga iliyotumiwa kuinua kifaa chake cha teleprompta huku akisaidiwa na afisa wa Jeshi la Wanahewa na washiriki wawili wa huduma yake ya siri.


Alionekana akirudi kwenye kiti chake bila kusaidiwa na baadaye akikimbia kurudi kwenye msafara wake sherehe ilipokamilika muda mfupi baada ya ajali hiyo.


Mwandishi huyo aliongeza kuwa rais hakujibu maswali aliporejea kwenye ndege yake.


Katibu wa waandishi wa habari wa Ikulu ya White House, Karine Jean-Pierre alisema Bw Biden alikuwa akijihisi "mwenye afya kabisa" na alipanda ndege hiyo akiwa na "tabasamu kubwa".


Wakosoaji wamesema Bw Biden ni mzee sana kuwania muhula wa pili kama rais.


Kura za hivi majuzi zinaonyesha kuwa wapiga kura wengi wa Marekani wana wasiwasi kuhusu umri wake mkubwa.


Atakuwa na umri wa miaka 82 mwanzoni mwa muhula wa pili ikiwa atashinda.


Kuanguka huku, pamoja na kujikwaa hapo awali kutoka kwa baiskeli yake na njiani akipanda ngazi za Air Force One, kunaweza kuongeza wasiwasi huo.


Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump, mtangulizi wa chama cha Republican atachuana na Bw Biden katika uchaguzi wa Ikulu ya Marekani 2024, na alizungumza juu ya kisa hicho kutoka kwa hafla ya kampeni huko Iowa, akisema "mambo yote ni balaa tupu".


"Natumai hakuumia," alisema Bw Trump, 76, ambaye mara nyingi amekuwa akidhihaki umri wa Bw Biden. "Hiyo haileti msisimko."


"Lazima uwe mwangalifu kuhusu hilo kwa sababu hutaki - hutaki hilo. Hata ikibidi uelekeze njia panda," akaongeza Bw Trump, akionekana kurejelea matembezi yake ya uangalifu kutoka kwa jukwaa ambako kuligonga vichwa vya habari. mwaka 2020.


Alisema wakati huo njia panda katika Chuo cha Kijeshi cha Marekani huko West Point, New York, ilikuwa ya utelezi, na akapuuza maswali ya vyombo vya habari yaliyofuata kuhusu afya yake kama habari za uwongo.


Gavana wa Florida Ron DeSantis, mgombea mwingine wa uteuzi wa Republican 2024, pia alijibu tukio hilo la kuanguka wakati wa hafla ya kampeni huko New Hampshire: "Tunatumai na tunamtakia Joe Biden ahueni ya haraka kutokana na majeraha yoyote ambayo huenda amepata.


"Lakini pia tunaitakia Marekani afueni ya haraka kutokana na majeraha ambayo imeyapata kwa sababu ya Joe Biden na sera zake."


Uchunguzi wa mwisho wa Bw Biden ulifanyika mnamo Februari.


Daktari wa Ikulu ya Marekani Dkt Kevin O'Connor aliandika wakati huo: "Rais bado anastahili kuhudumu, na anatekeleza kikamilifu majukumu yake yote bila udhuru yoyote ya kila mara."


Dkt O'Connor aliongeza kuwa Bw Biden anatembea sio akiwa wima hasa "akitembea kwa kasi", kwa kiasi kikubwa, kunasababishwa na uchakavu wa uti wa mgongo na uharibifu wa mishipa kwenye miguu yake, lakini hali yake ilikuwa haijabadilika kutoka hapo awali mnamo Novemba 2021.


Bwana Biden sio kamanda mkuu wa kwanza kupoteza msimamo wake mbele ya kamera.


Rais Barack Obama alijikwaa kwa kupanda ngazi katika hafla ya 2012, wakati Rais Gerald Ford alianguka chini ya ngazi za Air Force One mnamo 1975.

 Via BBC SWAHILI

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post