HOTUBA YA MPANGO WA MAENDELEO WA TAIFA WA MWAKA 2023/24

 



Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), akiwasilisha Taarifa ya Hali ya Uchumi kwa mwaka 2022 na Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa mwaka 2023/2024, bungeni jijini Dodoma.



              

                 

         

Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2023/24 

          

                 

 

ORODHA YA VIFUPISHO

ASA

Agricultural Seed Agency 

ASDP II

Agriculture Sector Development Programme II 

ATC

Arusha Technical College

ATCL

Air Tanzania Company Limited 

ATMIS

Agriculture Trade Management Information System 

BRELA

Business Registrations and Licensing Agency

BTI

Beekeeping Training Institute

BTIP II

Backbone Transmission Investment Project - II

CAMARTEC

Centre For Agriculture Mechanization and Rural Technology 

COASCO

Co-operative Audit and Supervision Corporation

COSTECH

Tanzania Commission for Science and Technology  

CPB

Cereals and Other Produce Board 

DCF

Development Cooperation Framework

DIT

Dar es Salaam Institute of Technology

DITF

Dar es Salaam International Trade Fair

DMDP

Dar es Salaam Metropolitan Development Project 

DMI

Dar es Salaam Maritime Institute 

DUCE

Dar es Salaam University College of Education

EAC

East Africa Community 

EACOP

East Africa Crude Oil Project 

e-GA

Electronic Government Authority 

e-HRP

Electronic Human Resource Planning

EIA

Environment Impact Assessment 

e-OPRAS

Electronic Open Performance Review and Appraisal System

EP4R

Education Program 4 Result

ESIA

Environment and Social Impact Assessment

ETH

Engineering Technology Hubs

FETA

Fisheries Education Training Agency 

FORVAC

Forestry and Value Chain Development Programme

GePG

Government Electronic Payment Gateway 

GST

Geological Survey of Tanzania

HCMIS

Human Capital Management Information System 

HESLB

Higher Education Students’ Loans Board 

HGA

Host Government Agreement  

IDRAS

Integrated Domestic Revenue Administration System

IJA

Institute of Judicial Administration 

IMF

International Monetary Fund 

ISTA

International Seed Testing Agency 

i                           


 

JNIA

Julius Nyerere International Airport 

KIA

Kilimanjaro International Airport

LITA

Livestock Training Agency 

LNG

Liquefied Natural Gas 

LSP II

Legislative Support Project II

MMEM

Mpango wa Maendeleo ya Sekta ya Elimu ya Msingi 

MSD

Medical Stores Department 

MSM

Mamlaka za Serikali za Mitaa

MTAKUWWA

Mpango Kazi wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto

MTDS

Medium Term Debt Strategy 

MUCE

Mkwawa University College of Education  

MUSE

Mfumo wa Ulipaji Serikalini

MUST

Mbeya University of Science and Technology 

NEEC

National Economic Empowerment Council

NFRA

National Food Reserve Agency

NIDC

National Internet Data Centre

NIT

National Institute of Transport

NPMIS

National Project Management Information System

OECD

Organization for Economic Co-operation and Development 

OSC

One Stop Centre 

PFMRP

Public Financial Management Reform Programme

PPP

Public-Private Partnership 

PSSSF

Public Service Social Security Fund

REA

Rural Energy Agency

REGROW

Resilient Natural Resource Management for Tourism and Growth

SELF

Small Entrepreneurs Loan Facility 

SEZ/EPZ

Special Economic Zone/Export Processing Zone

SGR

Standard Gauge Railway 

SIDO

Small Industries Development Organization

SMMRP

Sustainable Management of Mineral Resources Project

STAMICO

State Mining Company 

SUA

Sokoine University of Agriculture 

SWIOFish

South West Indian Ocean Fisheries Governance and Shared Growth

TADB

Tanzania Agricultural Development Bank

TAEC

Tanzania Atomic Energy Commission

TAFICO

Tanzania Fisheries Corporation

TAFIRI

TALIRI

Tanzania Fisheries Research Institute Tanzania Livestock Research Institute

TAMCO

Tanzania Automobiles Manufacturing Company

TANESCO

Tanzania Electrical Supply Company 

 

TARI

Tanzania Agricultural Research Institute

 

TATC

Tanzania Automotive Technology Centre

 

TBC

Tanzania Broadcasting Cooperation

 

TBS

Tanzania Bureau of Standard

 

TCRA

Tanzania Communication Regulatory Authority 

 

TDCs

Technology Development Centres

 

TEA

Tanzania Education Authority 

 

TEMDO

Tanzania Engineering and Manufacturing Design Organization

 

TESP

Teacher Education Support Project

 

TGC 

Tanzania Gemmological Centre 

 

TIRDO

Tanzania Industrial Research and Development Organization

 

TOSCI

Tanzania Official Seed Certification

 

TPSF

Tanzania Private Sector Foundation 

 

TTCL

Tanzania Telecommunications Corporation,

 

UTT - AMIS

Unit Trust of Tanzania- Asset Management and Investor Services

 

UVIKO-19

Ugonjwa wa Virusi vya Korona - 19

 

 

YALIYOMO

 

MUHTASARI  ............................................................................................. 2

SURA YA KWANZA....................................................................................... 2

HALI YA UCHUMI........................................................................................ 2

1.1.  Utangulizi........................................................................................... 2

1.2.  Mapitio ya Hali ya Uchumi Kikanda na Kimataifa......................................... 2

1.2.1. Ukuaji wa Uchumi wa Dunia........................................................ 2

1.2.2. Uchumi wa Nchi Zilizoendelea...................................................... 2

1.2.3. Uchumi wa Nchi Zinazoendelea na Zinazoibukia Kiuchumi.................. 2

1.2.4. Uchumi wa Nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara............................ 2

1.2.5. Mwenendo wa Ukuaji wa Uchumi kwa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki na Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika....................................................................................... 2

1.3.  Mapitio ya Hali ya Uchumi wa Taifa.......................................................... 2

1.3.1. Pato la Taifa na Ukuaji wa Uchumi................................................ 2

1.3.2. Mfumuko wa Bei....................................................................... 2

1.3.3. Sekta ya Nje............................................................................. 2

1.3.4. Sekta ya Fedha......................................................................... 2

1.3.5. Deni la Serikali.......................................................................... 2

1.4.  Maendeleo ya Watu.............................................................................. 2

1.4.1. Ongezeko la Idadi ya Watu mwaka 2022........................................ 2

1.4.2. Viashiria vya Maendeleo ya Watu.................................................. 2

1.4.2.1. Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini................................... 2

1.4.2.2. Upatikanaji wa Chakula  ................................................. 2

SURA YA PILI............................................................................................. 2

MAPITIO YA UTEKELEZAJI WA MPANGO.......................................................... 2

2.1.  Utangulizi........................................................................................... 2

2.2.  Utekelezaji wa Bajeti ya Maendeleo ya Mwaka 2022/23............................... 2

2.3.  Hatua za Utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo............................................ 2

2.3.1. Miradi ya  Kielelezo.................................................................... 2

2.3.2. Kuchochea Uchumi Shindani na Shirikishi....................................... 2

2.3.2.1. Uendelezaji wa Miundombinu na Huduma........................... 2

2.3.2.3. Mapinduzi ya TEHAMA.................................................... 2

2.3.3. Kuimarisha Uwezo wa Uzalishaji Viwandani na Utoaji Huduma............ 2

2.3.3.1. Uzalishaji Viwandani....................................................... 2

2.3.3.2. Ubiasharishaji wa Mazao ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi kupitia ASDP II       2

2.3.3.3. Uchimbaji wa Madini, Vito vya Thamani na Gesi Asilia........... 2

2.3.3.4. Huduma....................................................................... 2

2.3.4. Kukuza Biashara na Uwekezaji..................................................... 2

2.3.4.1. Huduma za Biashara na Masoko........................................ 2

2.3.4.2. Kuboresha Mazingira ya Kufanya Biashara na Uwekezaji......... 2

2.3.5. Kuchochea Maendeleo ya Watu.................................................... 2

2.3.5.1. Afya............................................................................ 2

2.3.5.2. Ustawi na Maendeleo ya Jamii.......................................... 2

2.3.5.3. Elimu........................................................................... 2

2.3.5.4. Ardhi, Mipango Miji, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.......... 2

2.3.5.5. Huduma za Maji na Usafi wa Mazingira............................... 2

2.3.5.6. Hifadhi ya Mazingira na Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi 2

2.3.5.7. Usimamizi wa Maafa Nchini.............................................. 2

2.3.6. Kuendeleza Rasilimali Watu......................................................... 2

2.3.6.1. Ujuzi na Uwezeshaji....................................................... 2

2.3.7. Uwekezaji katika Taasisi na Mashirika ya Umma............................... 2

2.3.8. Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi.................................. 2

2.4.1. Ufuatiliaji wa Miradi katika kipindi cha Mwaka 2022/23...................... 2

2.4.2. Changamoto za Utekelezaji wa Mpango wa Maendeleo wa Mwaka 2022/23 2

2.4.3. Hatua Zilizochukuliwa Kukabiliana na Changamoto .......................... 2

SURA YA TATU........................................................................................... 2

MIRADI YA KIPAUMBELE KWA MWAKA 2023/24................................................ 2

3.1.  Utangulizi........................................................................................... 2

3.2.  Misingi ya Mpango na Shabaha za Ukuaji wa Uchumi.................................. 2

3.2.1. Malengo na Shabaha za Ukuaji wa Uchumi..................................... 2

3.2.2. Misingi (Assumptions) ya Mpango kwa Mwaka 2023/24.................... 2

3.3.  Miradi ya Kipaumbele kwa Mwaka 2023/24............................................... 2

3.3.1. Miradi ya Kielelezo..................................................................... 2

3.3.2. Kuchochea Uchumi Shindani na Shirikishi....................................... 2

3.3.2.1. Kuimarisha Mazingira Wezeshi ya Uwekezaji........................ 2

3.3.2.2. Mapinduzi ya TEHAMA.................................................... 2

3.3.2.3. Kuimarisha Miundombinu na Mifumo ya Kitaasisi.................. 2

3.3.3. Kuimarisha Uwezo wa Uzalishaji Viwandani na Utoaji Huduma............ 2

3.3.3.1. Uzalishaji Viwandani....................................................... 2

3.3.3.2. Kilimo, Mifugo na Uvuvi................................................... 2

3.3.3.3. Uchimbaji wa Madini, Vito vya Thamani na Gesi Asilia........... 2

3.3.3.4. Huduma....................................................................... 2

3.3.4. Kukuza Biashara na Uwekezaji..................................................... 2

3.3.4.1. Kuboresha Mazingira ya Uwekezaji na Kukuza Uwekezaji........ 2

3.3.4.2. Kukuza Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi.............................. 2

3.3.4.3. Kukuza Sekta Binafsi....................................................... 2

3.3.4.4. Huduma za Biashara na Masoko........................................ 2

3.3.4.5. Mahusiano na Nchi za Nje na Uchumi wa Kidiplomasia........... 2

3.3.5. Kuchochea Maendeleo ya Watu.................................................... 2

3.3.5.1. Afya............................................................................ 2

3.3.5.2. Ustawi na Maendeleo ya Jamii.......................................... 2

3.3.5.3. Elimu........................................................................... 2

3.3.5.4. Ardhi, Mipango Miji, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.......... 2

3.3.5.5. Huduma za Maji na Usafi wa Mazingira............................... 2

3.3.5.6. Hifadhi ya Mazingira na Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi 2

3.3.5.7. Hifadhi na Kinga  ya Jamii................................................ 2

3.3.6. Kuendeleza Rasilimali Watu......................................................... 2

3.3.6.1. Ujuzi na Uwezeshaji....................................................... 2

3.3.7. Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi.................................. 2

3.3.8. Uwekezaji katika Taasisi na Mashirika ya Umma .............................. 2

SURA YA NNE............................................................................................. 2

UGHARAMIAJI WA MPANGO WA MAENDELEO WA TAIFA 2023/24......................... 2

4.1.  Utangulizi........................................................................................... 2

4.2.  Ugharamiaji wa Utekelezaji wa Mpango wa Maendeleo wa Taifa 2023/24........ 2

4.3.  Mikakati ya Vyanzo vya Mapato ya Kugharamia Mpango  Mwaka 2023/24........ 2

4.4.  Mapato ya Ndani.................................................................................. 2

4.4.1. Mapato ya Kodi na Yasiyo ya Kodi................................................. 2

4.5.  Mikopo na Misaada............................................................................... 2

4.5.1. Mikopo ya Nje........................................................................... 2

4.5.2. Mikopo ya Ndani........................................................................ 2

4.5.3. Misaada ya Nje......................................................................... 2

4.6.  Vyanzo Mbadala na Bunifu vya Kugharamia Miradi ya Maendeleo .................. 2

SURA YA TANO........................................................................................... 2

UFUATILIAJI, TATHMINI NA UTOAJI WA TAARIFA............................................. 2

5.1. Utangulizi............................................................................................ 2

5.2. Misingi na Mbinu za Ufuatiliaji na Tathmini................................................. 2

5.3. Matokeo ya Ufuatiliaji na Tathmini............................................................ 2

5.4. Muundo wa Taarifa za Ufuatiliaji na Tathmini.............................................. 2

5.5. Mgawanyo wa Majukumu  ..................................................................... 2

SURA YA SITA............................................................................................ 2

VIHATARISHI NA MIKAKATI YA KUKABILIANA NAVYO........................................ 2

6.1.  Utangulizi........................................................................................... 2

6.2.  Vihatarishi vya Ndani na Nje na Mikakati ya Kukabiliana Navyo...................... 2

 

 

 

 

 


              

MUHTASARI

 

Mpango wa Mwaka 2023/24 ni wa tatu katika utekelezaji wa Mpango wa Tatu wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano 2021/22 – 2025/26, wenye dhima ya Kujenga Uchumi Shindani na Viwanda kwa Maendeleo ya Watu. Mpango huu ni mwendelezo wa utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025 inayotekelezwa kupitia Mpango Elekezi wa Muda Mrefu, 2011/12 – 2025/26. Mpango huu ni muhimu katika kuainisha maeneo mahsusi  ya vipaumbele kwa Wizara, Idara Zinazojitegemea, Wakala wa Serikali, Taasisi na Mashirika ya Umma, Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa kwa mwaka 2023/24.

 

Mpango wa Mwaka 2023/24 unajumuisha: Malengo na shabaha za Mpango na Bajeti kwa mwaka 2023/24; maeneo mahsusi ya vipaumbele yaliyozingatia vipaumbele vya Mpango wa Tatu wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano 2021/22 – 2025/26 na Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2020; mfumo wa ugharamiaji wa Mpango; wajibu wa sekta ya umma na binafsi na mgawanyo wa majukumu; na mfumo wa ufuatiliaji, tathmini na utoaji wa taarifa za utekelezaji wa Mpango. 

 

Aidha, Mpango wa Mwaka 2023/24 umeandaliwa kwa mujibu wa matakwa ya Ibara ya 63 (3) (c) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977 na Sheria ya Bajeti, Sura 439. Maandalizi ya Mpango wa Mwaka 2023/24  yamezingatia nyaraka za kisera za kitaifa, kikanda na kimataifa ambazo ni: Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025; Mpango wa Tatu wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano 2021/22 - 2025/26; Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi kwa Ajili ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2020; Dira ya Maendeleo ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) 2050; Dira ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika(SADC) 2050; Makubaliano ya Paris kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi; Ajenda 2063 ya Maendeleo ya Afrika; na Malengo ya Maendeleo Endelevu 2030.

 

Wadau mbalimbali kutoka Wizara, Idara Zinazojitegemea, Wakala wa Serikali, Sekretarieti za Mikoa, Mamlaka za Serikali za Mitaa, Taasisi na Mashirika ya Umma na Sekta Binafsi wameshiriki katika Mchakato wa Maandalizi ya Mpango wa Mwaka 2023/24. Vile vile, Washirika wa Maendeleo wameshirikishwa kupitia majadiliano katika maeneo mahsusi ya ushirikiano, ufadhili wa miradi ya maendeleo na programu za kisekta.

 

Katika kipindi cha utekelezaji wa Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2022/23, Mwenendo wa uchumi wa Taifa umeendelea kuimarika ambapo thamani halisi ya Pato ghafi la Taifa kwa be iza mwaka 2015 ilifikia shilingi trilioni 141.9 ikilinganishwa na shilingi trilioni 135.5 mwaka 2021, sawa na ukuaji wa asilimia 4.7, nakisi ya urari ilifikia dola za Marekani milioni 4,441.2 kwa kwa kipindi cha mwezi Julai 2022 hadi Aprili 2023, ikilinganishwa na nakisi ya dola za Marekani milioni 2,516.1 katika kipindi kama hicho mwaka 2022, mikopo kwa sekta binafsi iliongezeka kufikia asilimia 22.5 mwaka 2022 ikilinganishwa na asilimia 10 mwaka 2021. Aidha, viwango vya riba za mikopo ya benki za biashara kwa sekta binafsi kwa mwaka vimeendelea kupungua japo kwa kasi ndogo, kufikia wastani wa asilimia 15.91 mwezi Aprili 2023 kutoka ikilinganishwa na asilimia 16.31 Aprili 2022. Aidha, Katika kipindi cha mwezi Mei 2023, mfumuko wa bei nchini ulifikia wastani wa asilimia 4.0  ikilinganishwa na wastani wa asilimia 3.8 kwa kipindi kama hicho mwaka 2022, kutokana na changamoto ya mlipuko wa UVIKO – 19 na athari za vita ya Urusi na Ukraine. 

 

Kwa ujumla Mpango wa Mwaka 2023/24 umejumuisha utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwa kipindi cha mwaka 2022/23 na miradi ya kipaumbele kwa mwaka 2023/24. Aidha, utekelezaji wa Mpango kwa mwaka 2023/24 utaendelea kutoa kipaumbele kwa miradi ya kielelezo na kimkakati ikiwemo: Ujenzi wa Reli ya Kati kwa Kiwango cha Kimataifa (Standard Gauge); Kufua Umeme wa Maji wa Julius Nyerere – MW 2,115; kuboresha Shirika la Ndege Tanzania (ATCL); ujenzi wa Bomba la Mafuta Ghafi kutoka Hoima (Uganda) hadi Tanga (Tanzania); kuchakata na Kusindika Gesi Asilia kuwa Kimiminika (LNG) – Lindi; makaa ya Mawe (Mchuchuma - Njombe) na Chuma (Liganga - Njombe); na kufua Umeme wa Maji wa Ruhudji (MW 358) – Njombe.  

 

Katika kipindi cha Julai 2022 - Aprili 2023, Wizara ya Fedha na Mipango ikishirikiana na taasisi nyingine za Serikali ilifuatilia miradi na programu za maendeleo 211 kati ya miradi 300 iliyopagwa kufuatiliwa katika kipindi husika. Miradi hiyo inajumuisha miradi ya kielelezo na kimkakati katika maeneo mbalimbali nchini. Ufuatiliaji huo ulibaini hatua zilizofikiwa katika utekelezaji wa miradi, mafanikio, changamoto na mapendekezo. Ufuatiliaji na Tathmini uliwezesha kutolewa kwa maamuzi yanayoongozwa na taarifa sahihi na kwa wakati. Aidha, Serikali itaendelea kuchukua hatua za haraka katika kukabiliana na vihatarishi vitakavyojitokeza katika utekelezaji wa Mpango wa Maendeleo wa Taifa. Hatua hizo zinajumuisha kutoa elimu kwa wananchi juu ya umuhimu wa kutunza mazingira ili kudhibiti uharibifu unaotokana na shughuli za kibinadamu, kuendelea kufuatilia kwa karibu mfumuko wa bei ya bidhaa za chakula ili kutoa ruzuku ya mbolea itakayoongeza uzalishaji pamoja na kutoa ruzuku katika bidhaa za mafuta.  

 

Kitabu cha Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2023/24 kimegawanyika katika sura sita (6): Sura ya kwanza (1) ni mapitio ya hali ya uchumi; Sura ya pili (2) ni mapitio ya utekelezaji wa Mpango wa Maendeleo wa mwaka 2022/23 katika kipindi cha robo tatu; Sura ya tatu (3) inaelezea miradi na programu ya kipaumbele kwa mwaka 2023/24; Sura ya nne (4) ni ugharamiaji wa Mpango; Sura ya tano (5) inaainisha utaratibu wa ufuatiliaji, tathmini na utoaji taarifa za utekelezaji wa Mpango; na Sura ya sita (6) inaainisha vihatarishi vya utekelezaji wa Mpango na namna ya kukabiliana navyo.

 

SURA YA KWANZA

 

HALI YA UCHUMI

1.1. Utangulizi

Sura hii inaelezea mwenendo wa viashiria vya hali ya uchumi nchini, kikanda na dunia kwa mwaka 2022 pamoja na mwelekeo kwa mwaka 2023. Mwenendo wa viashiria hivyo unajenga msingi wa Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2023/24. Kwa ujumla, mwenendo wa ukuaji wa uchumi katika kipindi cha mwaka 2022 umepungua ukilinganisha na ukuaji  katika kipindi cha mwaka 2021. 

 

1.2. Mapitio ya Hali ya Uchumi Kikanda na Kimataifa

 

1.2.1. Ukuaji wa Uchumi wa Dunia 

Kwa mujibu wa taarifa ya Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) ya Aprili 2023 inaonesha kuwa, kasi ya ukuaji wa uchumi wa dunia imepungua kutoka asilimia 6.3 mwaka 2021 hadi asilimia 3.4 mwaka 2022. Upungufu huo unatokana na sababu mbalimbali ikiwemo kasi ndogo ya ukuaji wa uchumi wa China na India; madhara ya janga la UVIKO-19; vita kati ya Urusi na Ukraine; na sera za kupunguza ukwasi katika chumi za Ulaya ili kukabiliana na mfumuko wa bei. Aidha, Uchumi wa dunia unatarajiwa kupungua zaidi na kufikia ukuaji wa asilimia 2.8 mwaka 2023 kutokana na kuendelea kwa vita kati ya Urusi na Ukraine, mabadiliko ya Tabia ya Nchi na Sera za Marekani kuongeza riba.

 

1.2.2. Uchumi wa Nchi Zilizoendelea

Kiwango cha ukuaji wa uchumi wa nchi zilizoendelea kilipungua na kufikia asilimia 2.7 mwaka 2022 ikilinganishwa na asilimia 5.4 mwaka 2021. Upungufu huu umesababishwa na madhara ya vita kati ya Urusi na Ukraine inayoendelea kuyumbisha uchumi wa dunia hususan kuongezeka kwa gharama za maisha kulikosababishwa na mfumuko wa bei za nishati barani Ulaya na kuongezeka kwa bei za vyakula  katika soko la dunia. Aidha, uchumi wa nchi hizi unatarajiwa kupungua na kufikia ukuaji wa asilimia 1.3 mwaka 2023.

 

1.2.3. Uchumi wa Nchi Zinazoendelea na Zinazoibukia Kiuchumi

Kiwango cha ukuaji wa uchumi wa Nchi Zinazoendelea na Zinazoibukia Kiuchumi ulipungua na kufikia wastani wa asilimia 4.0 mwaka 2022 ikilinganishwa na asilimia 6.9 mwaka 2021. Hii  ilitokana na madhara ya vita kati ya Urusi na Ukraine ambayo yameendelea kuathiri uchumi wa  nchi hizi. Aidha, kiwango cha ukuaji wa uchumi wa Nchi Zinazoendelea na Zinazoibukia Kiuchumi za Bara la Asia, ikijumuisha China na India kilipungua na kufikia wastani wa asilimia 4.4 mwaka 2022 ikilinganishwa na asilimia 7.5 mwaka 2021.

 

 

 

 

1.2.4. Uchumi wa Nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara

Ukuaji wa Uchumi kwa Nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara ulipungua kufikia wastani wa asilimia 3.9 mwaka 2022 ikilinganishwa na asilimia 4.8 mwaka 2021. Aidha, uchumi wa nchi hizi unatarajiwa kupungua na kufikia ukuaji wa asilimia 3.6 mwaka 2023. Upungufu huo ulitokana na madhara ya vita kati ya Urusi na Ukraine iliyosababisha mfumuko wa bei za nishati ya mafuta na vyakula. Jedwali Na. 1 linaonesha mwenendo wa ukuaji wa uchumi wa dunia na matarajio.

 

Jedwali 1: Mwenendo wa Ukuaji wa Uchumi wa Dunia na Matarajio

Kundi/Mwaka

 

 

Ukuaji Halisi (asilimia)

 

 

Mataraji o

(asilimia

)

2017

2018

2019

2020

202

1

202

2

2023

Dunia

3.8

3.6

2.8

-2.8

6.3

3.4

2.8

Nchi Zilizoendelea

2.5

2.3

1.7

-4.2

5.4

2.7

1.3

Nchi Zinazoendelea na Zinazoibukia 

4.7

4.7

3.6

-1.8

6.9

4.0

3.9

Nchi Zinazoendelea na          Zinazoibukia

Kiuchumi za Bara la Asia

6.6

6.4

5.2

-0.5

7.5

4.4

 

5.3

Nchi za Afrika Kusini mwa  Jangwa la

Sahara

2.9

3.2

3.3

-1.7

4.8

3.9

3.6

Chanzo: Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF - WEO), Aprili, 2023

 

1.2.5. Mwenendo wa Ukuaji wa Uchumi kwa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki na Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika

Kiwango cha ukuaji wa Pato la Taifa kwa nchi za ukanda wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) kilikuwa cha wastani wa asilimia 4.1 mwaka 2022 ikilinganishwa na wastani wa asilimia 5.3 mwaka 2021. Aidha, ukuaji wa uchumi kwa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afirka Mashairiki (EAC) ulikuwa wa wastani wa  asilimia 5.3 mwaka 2022 ikilinganishwa na wastani wa asilimia 6.3 mwaka 2021 kama inavyoonekana  katika Jedwali Na. 2.

 

 

 

Jedwali 2: Ukuaji wa Uchumi kwa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika

Mashariki na Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika

Ukuaji wa Uchumi kwa nchi za SADC

 

 

Nchi

2020

 

2021

2022

Angola

-5.4

 

1.1

2.8

Botswana

-8.7

 

11.8

6.4

Tanzania 

4.8

 

4.9

4.7

DRC

1.7

 

6.2

6.6

Eswatin

-3.2

 

7.9

0.5

Lesotho

-6

 

2.1

2.1

Madagascar

-4.0

 

5.7

4.2

Malawi

-1.7

 

4.6

0.8

Mauritius

-15.0

 

3.5

8.3

Msumbiji

-1.2

 

2.3

4.1

Namibia

-8.5

 

2.7

3.8

Seychelles

-7.7

 

7.9

8.8

Zambia

-2.8

 

4.6

3.4

Zimbabwe

-5.3

 

8.5

3.0

Afrika ya Kusini

-6.4

 

4.9

2.0

Wastani

-4.6

 

5.3

4.1

Ukuaji wa Uchumi kwa Nchi za EAC

 

 

Burundi

0.3

 

3.1

1.8

Kenya

-0.3

 

7.5

5.4

Rwanda

-3.4

 

10.9

6.8

DRC

-1.7

 

6.2

6.6

Sudani Kusini

-6.5

 

5.3

6.6

Tanzania

4.8

 

4.9

4.7

Uganda

-1.3

 

6.0

4.9

Wastani

-1.1

 

 6.3 

 5.3

 

Chanzo: Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) toleo la Aprili 2023

 

1.3. Mapitio ya Hali ya Uchumi wa Taifa 

 

1.3.1. Pato la Taifa na Ukuaji wa Uchumi

Mwaka 2022, Mwaka 2022, thamani halisi ya Pato la Taifa kwa bei za mwaka 2015 lilifikia shilingi trilioni 141.9 ikilinganishwa na shilingi trilioni 135.5  mwaka 2021.  Aidha, kiwango halisi cha ukuaji wa pato la Taifa kilifikia asilimia 4.7 mwaka 2022 ikilinganishwa na asilimia 4.9 mwaka 2021. Kiwango hicho cha ukuaji kilitokana na: mikakati iliyochukuliwa na Serikali kukabiliana na athari za vita nchini Ukraine; uwekezaji wa kimkakati katika miundombinu ya nishati, maji, afya, elimu, barabara, reli na viwanja vya ndege; kuongezeka kwa uzalishaji wa madini, hususan makaa ya mawe; kuongezeka kwa mikopo kwa sekta binafsi iliyochachua shughuli za kiuchumi; na kuongezeka kwa shughuli za utalii. Kutokana na hatua mbalimbali zinazoendelea kuchukuliwa na Serikali, Pato ghafi la Taifa linatarajiwa kufikia dola za Marekani billioni 85.42 mwaka 2023/24 kutoka makadirio ya dola bilioni 77.41 mwaka

2022/23.                                                                                                                               

 

1.3.2. Mfumuko wa Bei 

Vita vya Urusi na Ukraine vimesababisha kupanda zaidi kwa bei ya mafuta duniani, ambayo yamechangia ongezeko la gharama za uzalishaji na usafirishaji wa bidhaa.  Mwaka 2022, mfumuko wa bei wa dunia uliongezeka kwa kiwango kikubwa kufikia wastani wa asilimia 8.7 ikilinganishwa na wastani wa asilimia 4.7 mwaka 2021. Aidha, mfumuko wa bei kwa nchi zilizoendelea uliongezeka na kufikia wastani wa asilimia 7.3 mwaka 2022 ikilinganishwa na wastani wa asilimia 3.1 mwaka 2021. Vile vile, mfumuko wa bei kwa nchi zinazoendelea za Asia uliongezeka na kufikia wastani wa asilimia 3.8 mwaka 2022 ikilinganishwa na wastani wa asilimia 2.2 mwaka 2021.  Mwaka 2022, mfumuko wa bei kwa nchi za Afrika zilizo Kusini mwa Jangwa la Sahara ulifikia wastani wa asilimia 14.5 ikilinganishwa na wastani wa asilimia 11.0 mwaka 2021. Kwa ujumla, kuongezeka kwa mfumuko wa bei kulitokana na kupanda kwa bei za nishati na vyakula kulikosababishwa na kuvurugika kwa mnyororo wa uzalishaji kutokana na vita inayoendelea nchini Ukraine pamoja na mabadiliko ya tabianchi.

 

(a)        Mfumuko wa Bei Nchini

Mfumuko wa bei nchini umeendelea kuwa ndani ya lengo la wigo wa kuwa chini ya asilimia 5. Mwaka 2022, mfumuko wa bei ulifikia wastani wa asilimia 4.3 ikilinganishwa na wastani wa asilimia 3.7 mwaka 2021. Aidha, mfumuko wa bei kwa mwaka unaoishia mwezi Mei, 2023 umebaki kama ilivyokuwa kwa mwaka unaoishia mwezi Mei, 2022 ikiwa ni wastani wa asilimia 4.0. Hali hii imesababishwa na kuongezeka kwa  uzalishaji na usambazaji wa bidhaa na huduma; na kuongezeka kwa upatikanaji wa mazao ya chakula katika baadhi ya maeneo nchini na nchi jirani kulikosababishwa na upatikanaji wa mvua katika maeneo yanayotegemea mvua.

 

Katika kipindi kilichoishia mwezi Mei mwaka 2023, mfumuko wa bei wa vyakula na vinywaji baridi uliongezeka na kufikia asilimia 8.5 ikilinganishwa na asilimia 5.5

katika kipindi kama hicho mwaka 2022. Aidha, mfumuko wa bei usiojumuisha vyakula na nishati (Core Inflation) ulifikia wastani wa asilimia 2.0 katika kipindi cha mwaka unaoishia mwezi Mei 2023 ikilinganishwa na asilimia 3.0 katika kipindi kama hicho mwaka 2022. Kupungua kwa kasi ya upandaji bei ya bidhaa zisizo za vyakula na nishati kulitokana na kuongezeka kwa uzalishaji wa bidhaa hizi nchini, ikiwemo saruji (Kielelezo Na. 1).

 

Kwa upande mwingine mfumuko wa bei wa nishati, mafuta na ankara za maji ulipungua kutoka asilimia 13.5 katika kipindi cha mwaka unaoishia mwezi Mei 2022 na kufikia asilimia hasi 1.1 kwa mwaka unaoishia mwezi Mei 2023. Hii ilitokana na kupungua kidogo kwa bei ya nishati ya mafuta katika soko la dunia, mfano; kwa mwaka unaoishia mwezi Mei 2022, bei ya dizeli ilipanda kwa asilimia 18.7, petroli asilimia 10.8 na mafuta ya taa kwa asilimia 14.2. Aidha kwa mwaka unaoishia mwezi Mei 2023, bei ya dizeli ilishuka hadi kufikia wastani wa asilimia hasi 0.3, petroli kwa asilimia chanya 1.9 na mafuta ya taa kwa asilimia hasi 2.1

 

Kielelezo 1: Mwenendo wa Mfumuko wa Bei Nchini (Kwa Mwaka Unaoishia Aprili 2021 hadi Mei 2023)

 

Chanzo: Ofisi ya Taifa ya Takwimu

 

(b)        Mfumuko wa Bei kwa Nchi za Ukanda wa Afrika Mashariki

Mfumuko wa Bei kwa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ulifikia wastani wa asilimia 11.2 mwaka 2022 ikilinganishwa na wastani wa asilimia 8.6

mwaka 2021. Kuongezeka kwa mfumuko wa bei kulitokana na kupungua kwa uzalishaji wa chakula kwa baadhi ya nchi wanachama na kuongezeka kwa gharama na mahitaji ya mafuta katika nchi hizi. Sababu nyingine ni pamoja na vita vya mara kwa mara katika nchi za Sudani Kusini na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Aidha, kwa wastani, viwango vya mfumuko wa bei kwa nchi ya Tanzania, Kenya na Uganda ndivyo pekee viliendelea kuwa ndani ya lengo la Jumuiya la mfumuko usiozidi asilimia 8 kwa mwaka.  Kwa upande mwingine, nchi za Burundi na Rwanda ndizo zilikuwa na viwango vikubwa vya mfumuko wa bei mwaka 2022 uliofikia asilimia 18.9  na 13.9 mtawalia  ambapo Tanzania ilikuwa na kiwango cha chini zaidi cha mfumuko wa bei wa asilimia 4.3.

 

Jedwali 3: Mfumuko wa Bei katika Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa Januari 2021 hadi Disemba 2022

Nchi

2021

2022

 

Mfumuko wa Bei (Asilimia)

Tanzania

3.7

4.3

Uganda

2.2

6.8

Kenya

6.1

7.6

Rwanda

0.8

13.9

Burundi

8.3

18.9

Sudani ya Kusini

30.2

17.6

DRC

9.0

9.0

Wastani kwa Afrika Mashariki

8.6

11.2

Chanzo: Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) toleo la Aprili 2023 na nchi husika.

 

1.3.3. Sekta ya Nje

Sekta ya nje imeendelea kukabiliwa na changamoto zitokanazo na vita kati nchi ya Ukraine na Urusi pamoja na kuibuka kwa maambukizi mapya ya UVIKO-19. Hali hii imesababisha usumbufu wa mnyororo wa uzalishaji na usambazaji wa bidhaa na huduma duniani na hivyo kupekelea kupanda kwa bei za bidhaa na huduma  mbalimbali katika soko la dunia.

 

(a)         Urari wa Malipo ya Kawaida 

Kwa kipindi cha mwezi Julai 2022 hadi Aprili 2023, urari wa malipo yote ya nje ulikuwa na nakisi ya dola za Marekani milioni 4,414.2. ikilinganishwa na nakisi ya dola za Marekani milioni 2,516.1 kwa kipindi kama hicho mwaka 2022 Hii ilichangiwa na kuongezeka kwa gharama za uagizaji wa bidhaa kutoka nje ya nchi kutokana na athari hasi kwenye mnyororo wa uzalishaji na ugavi wa bidhaa dunia na malipo ya Serikali nje ya nchi.

 

(b)         Mwenendo wa Biashara ya Bidhaa na Huduma

Urari wa Biashara ya Bidhaa

Urari wa biashara ya bidhaa ulikuwa na nakisi ya dola za Marekani milioni 6,065.6 kwa kipindi cha mwezi Julai 2022 hadi Aprili 2023 ikilinganishwa na nakisi ya dola za Marekani milioni 3,556.8 kwa kipindi kama hicho mwaka 2022. Hii ilitokana na kuongezeka kwa gharama ya uagizaji bidhaa kutoka nje, hususan mafuta ya petroli, mbolea, malighafi za viwandani na bidhaa za ujenzi hususan kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya kimkakati. Vile vile, vita nchini Ukraine ilisababisha kuongezeka kwa bei za bidhaa kutokana na kuvurugika kwa mnyonyoro wa uzalishaji na ugavi duniani. 

 

Urari wa Biashara ya Huduma 

urari wa biashara ya huduma ulikuwa na ziada ya dola za Marekani milioni 2,198.7  kwa kipindi cha mwezi Julai 2022 hadi Aprili 2023 ikilinganishwa na ziada ya dola za Marekani milioni 1,585.1 kwa kipindi kama hicho mwaka 2022, sawa na ongezeko la  asilimia 38.7. Hii ilitokana na kuongezeka kwa mapato yatokanayo na shughuli za utalii na usafirishaji kulikosababishwa na kuendelea kuimarika kwa uchumi wa dunia kutokana na kupungua kwa athari za UVIKO-19 pamoja na juhudi za serikali katika kuvutia watalii kutoka nchi mbalimbali duniani.

 

Urari wa Biashara ya Bidhaa na Huduma

Urari wa biashara ya bidhaa na huduma ulikuwa na nakisi ya dola za Marekani milioni 3,866.9 kwa kipindi cha mwezi Julai 2022 hadi Aprili 2023 ikilinganishwa na nakisi ya dola za Marekani milioni 1,971.7 kwa kipindi kama hicho mwaka 2022.Hii ilichangiwa zaidi na kuongezeka kwa nakisi katika urari wa biashara ya bidhaa kulikosababishwa na ongezeko la gharama za uagizaji wa bidhaa.

 

(c)        Akiba ya Fedha za Kigeni

Akiba ya fedha za kigeni imeendelea kuwa ya kuridhisha kukidhi mahitaji ya uagizaji wa bidhaa na huduma kutoka nje ya nchi. Hadi kufikia Aprili 2023, akiba ya fedha za kigeni ilikuwa dola za Marekani bilioni 4.88 ambayo inatosheleza uagizaji wa bidhaa na huduma kutoka nje ya nchi kwa kipindi cha takriban miezi 4.4. Mahitaji ya nchi kisheria ni kuwa na kiasi cha fedha za kigeni kinachotosheleza uagizaji wa bidhaa na huduma kutoka nje ya nchi kwa muda usiopungua miezi 4.0.

 

1.3.4. Sekta ya Fedha

 

(a)         Mwenendo wa Viwango vya Riba 

Katika kipindi kilichoishia Aprili 2023, riba ya jumla katika soko la fedha baina ya mabenki ilikuwa chini na tulivu japokuwa wastani uliongezeka kidogo hadi asilimia 4.92 kutoka wastani wa asilimia 4.08 kwa kipindi kama hicho mwaka 2022. Aidha, riba ya jumla ya dhamana za Serikali zimeendelea kubaki katika wastani wa asilimia 6.65. Kwa upande mwingine, viwango vya riba za mikopo ya benki za biashara kwa sekta binafsi kwa mwaka 2023 vimeendelea kupungua na  kufikia wastani wa asilimia 15.91 Apili 2023 kutoka ikilinganishwa na asilimia 16.31 Aprili 2022. Mwenendo huu ulichagizwa zaidi na utekelezaji wa sera wezeshi ya bajeti, na hatua zilizochukuliwa na Benki Kuu kuchochea ongezeko la ukuaji wa mikopo kwa sekta binafsi na kupunguza riba za mikopo, hatua ambazo zimesababisha baadhi ya benki kutoa mikopo kwa riba ya chini ya asilimia 10 hususan katika shughuli za kilimo kutokana na hatua za kisera zilizochukuliwa na Benki Kuu kupunguza viwango vya riba katika shughuli za kilimo. Wakati huohuo, wastani wa viwango vya riba za amana za muda maalum na za mwaka mmoja ulipungua  hadi asilimia 6.79 na asilimia 7.70 kutoka asilimia 6.81 na asilimia 8.28 mwaka 2022, mtawalia.

 

(b)         Ujazi wa Fedha

Kwa mwezi Aprili 2023, Serikali kupitia Benki Kuu ilitekeleza sera ya fedha inayolenga kupunguza kasi ya ongezeko la ukwasi kwenye uchumi ili kukabiliana na shinikizo la kuongezeka kwa mfumuko wa bei linalotokana na mitikisiko ya kiuchumi duniani bila kuathiri kasi ya ukuaji wa  shughuli za kiuchumi. Lengo ni kuhakikisha uwepo wa kiwango cha kutosha cha ukwasi kwenye mfumo wa kibenki kuendana na mahitaji halisi ya shughuli mbalimbali za kiuchumi. Kufuatia hali hiyo, ukuaji wa ujazi wa fedha ulikuwa sambamba na malengo ukichangiwa na kuimarika kwa shughuli za kiuchumi zilizokuwa zimeathiriwa na janga la UVIKO - 19 na hivyo kuchochea ongezeko la mahitaji ya  mikopo kutoka sekta binafsi. Katika kipindi kilichoishia Aprili 2023, ujazi wa fedha kwa tafsiri pana zaidi (M3) uliongezeka kwa asilimia 17.2 na kufikia shilingi bilioni 39,961.5 kutoka shilingi bilioni 34,087.8 mwezi mwaka Aprili, 2022. Ujazi wa fedha kwa tafsiri pana (M2) ulikua kwa asilimia 15.6 hadi kufikia kiasi cha shilingi bilioni 31,048.8 mwezi Aprili 2023 kutoka shilingi bilioni 26,861.5 katika kipindi kama hicho mwaka 2022. Aidha, ujazi wa fedha kwa tafsiri finyu (M1) uliongezeka kwa asilimia 14.3 na kufikia shilingi bilioni 19,248.3 Aprili, 2023 kutoka shilingi bilioni 16,843.6 katika kipindi kama hicho mwaka 2022.

 

(c)         Mikopo kwa Sekta Binafsi

Sekta ya benki nchini imeendelea kubaki imara, himilivu na yenye kutengeneza faida ikiwa na mtaji na ukwasi wa kutosha katika kutoa mikopo kwa sekta za uchumi na kupunguza umaskini. Mikopo kwa sekta binafsi imeongezeka kufikia shilingi bilioni 28,702.95 kwa mwaka ulioishia Aprili 2023 kutoka shilingi bilioni 23,422.5 Aprili 2022 sawa na ongezeko la asilimia 22.5. Aidha, ukuaji wa mikopo kwa sekta binafsi ulifikia wastani wa asilimia 15.8 katika kipindi cha Aprili 2022 hadi Aprili 2023 ikilinganishwa na wastani wa asilimia 9.1 katika kipindi kama hicho mwaka 2022 na lengo la asilimia 10.7 kwa mwaka 2022/23.  Ukuaji huu umechochewa na utekelezaji wa sera wezeshi za fedha na bajeti, pamoja na hatua zilizochukuliwa na Serikali ikiwemo ulipaji wa malimbikizo ya madai na  jitihada nyingine za kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji, hali iliyochochea kuimarika kwa shughuli za kiuchumi nchini. 

 

Katika kipindi cha Aprili 2022 hadi Aprili 2023, ongezeko la mikopo kwa sekta binafsi lilikua kwa kasi zaidi kwenye shughuli za kilimo, mawasiliano na usafirishaji, shughuli binafsi na biashara. Ongezeko la ukuaji wa mikopo kwa shughuli za kilimo lilitokana pia na hatua za kisera zilizochukuliwa Julai 2021, kwa ajili ya kuchochea ongezeko la mikopo na kushusha viwango vya riba katika shughuli za kilimo. Hatua hizo ni pamoja na utoaji wa ruzuku ya mbolea na bidhaa za petroli, punguzo la kodi katika uzalishaji wa mafuta ya kupikia na ongezeko la bajeti kwenye sekta ya kilimo. Aidha, sehemu kubwa ya mikopo imeendelea kuelekezwa katika shughuli binafsi (biashara ndogondogo na biashara za kati) kwa asilimia 38.6, ikifuatiwa na biashara kwa asilimia 16.2, uzalishaji viwandani kwa asilimia 9.6 na kilimo kwa asilimia 8.8.

 

(d)         Mwenendo wa Thamani ya Shilingi 

Thamani ya shilingi ya Tanzania dhidi ya sarafu za nchi washirika wakuu wa kibiashara imeendelea kuwa tulivu, licha ya kuwepo kwa changamoto mbalimbali za kiuchumi duniani hususan ongezeko la bei za bidhaa. Hali hii imetokana na utulivu wa mfumuko wa bei nchini ukilinganishwa na nchi washirika wetu wa kibiashara, utekelezaji wa sera thabiti za fedha na bajeti, na uwepo wa chakula cha kutosha nchini. Katika kipindi cha Aprili, 2023 dola moja ya Marekani ilibadilishwa kwa wastani wa shilingi 2,324.07 ikilinganishwa na shilingi 2,322.16 kipindi kama hicho mwaka 2022. Kwa wastani katika kipindi cha Aprili 2022 hadi Aprili 2023 shilingi ya Tanzania ilibadilishwa kwa shilingi 2,310.14. Kutokana na mwenendo huo, thamani ya shilingi imeendelea kupungua kwa kasi ndogo ya chini ya asilimia moja. 

 

(e)         Mikopo Chechefu

Ubora wa rasilimali za benki umeendelea kuimarika kutokana na kupungua kwa kiwango cha mikopo chechefu kufikia wastani wa asilimia 5.5 mwezi Aprili 2023 kutoka asilimia 8.3 Aprili 2022. Hali hii ilichangiwa zaidi na hatua mbalimbali zilizochukuliwa na Serikali kwa kuboresha mazingira ya kufanya biashara na kusimamia ukwasi katika uchumi uliowezesha wateja kulipa mikopo kwa wakati pamoja na hatua mbalimbali zilizochukuliwa na Benki Kuu ikiwemo kuhimiza benki za biashara kuongeza umakini katika kuchakata maombi ya mikopo; kuwaondoa katika sekta ya benki wafanyakazi wa benki wasio waaminifu; kuamuru benki kutumia taarifa za mikopo kutoka katika kanzidata ya taarifa za wakopaji; utekelezaji wa kanuni za kuwalinda walaji wa huduma za kibenki kwa kuhakikisha utunzaji wa haki na usawa wa walaji pamoja na wakopaji; na kuhakikisha kunakuwa na uwazi wa taarifa za kifedha kwa kutoa elimu ya fedha kwa watumiaji wa huduma za kifedha. Vilevile, Benki Kuu ilielekeza  benki na tasisi za fedha kuwa na mifumo ya udhibiti na utawala bora kwa kupitia upya mifumo iliyopo ili kukidhi mabadiliko na maendeleo katika sekta ya benki.

 

(f)          Ukwasi na Faida za Biashara katika Benki

Sekta ya benki imeendelea kuwa imara na kutengeneza faida ikiwa na mitaji na ukwasi wa kutosha. Viwango vya amana na rasilimali vimeendelea kuongezeka na sekta ya benki imeendelea kuwa imara dhidi ya misukosuko ya ndani na nje. Uwiano wa mtaji wa msingi kwa rasilimali zote ulifikia asilimia 19.6 mwezi Aprili 2023, ikilinganishwa na kiwango kinachokubalika kisheria cha asilimia 10. Aidha, uwiano wa ukwasi wa sekta ya benki kiujumla (Liquid Assets to Demand Liabilities) ulikuwa asilimia 25.37 mwezi Aprili 2023 ikilinganishwa na asilimia 27.89 katika kipindi kama hicho mwaka 2022. Uwiano huu ulikuwa juu ya  kiwango cha chini kinachokubalika kisheria cha angalau asilimia 20 na hivyo kuendelea kuwa toshelevu kwa mahitaji ya shughuli mbalimbali za kiuchumi. Sekta ya benki imeendelea kutengeneza faida ambapo faida baada ya kodi (kabla ya ukaguzi wa mahesabu) kwa miezi minne ya kwanza ya mwaka 2023 ilifikia shilingi bilioni 448.5 kutoka shilingi bilioni 374.8 katika miezi minne ya kwanza ya mwaka 2022, sawa na ongezeko la asilimia 19.7

 

(g)         Soko la Upili la Hatifungani 

 

Hatifungani za Serikali

Mauzo ya hatifungani za Serikali zilizoorodheshwa kwenye Soko la Hisa la Dar es Salaam katika kipindi kilichoishia Machi 2023 yalipungua na kufikia shilingi trilioni 2.93, ikilinganishwa na shilingi trilioni 3.21 zilizorekodiwa katika kipindi kilichoishia Machi 2022. Kupungua kwa mauzo ya hatifungani za Serikali kumetokana na marekebisho yaliyofanywa kwenye riba za hatifungani za Serikali, na hivyo kuwafanya wawekezaji kuwa na malengo ya kuendelea na umiliki wa hatifungani zao hadi kipindi zitakapoiva yaani holding to maturity. Marekebisho ya riba za hatifungani za Serikali yaliyofanywa ni kama ifuatavyo: Hatifungani za miaka 25 (kutoka 15.95% hadi 12.56%); Hatifungani za miaka 20 (kutoka 15.49% hadi 12.10%); Hatifungani za miaka 15 (kutoka 13.50% hadi 11.150%); Hatifungani za miaka 10 (kutoka 11.44% hadi 10.25%); Hatifungani za miaka 7 (kutoka 10.08% hadi 9.48%); Hatifungani za miaka 5 (kutoka 9.18% hadi 8.60%); Hatifungani za miaka 2 (kutoka 7.82% hadi 7.60%).

 

Hatifungani za Kampuni (Corporate Bonds)

Mauzo ya hatifungani za kampuni zilizoorodheshwa kwenye Soko la Hisa la Dar es Salaam katika kipindi kilichoishia Machi 2023, yalipungua na kufikia shilingi milioni 850.25 ikilinganishwa na shilingi bilioni 1.14 zilizorekodiwa katika kipindi kilichoishia Machi 2022. Kupungua kwa mauzo ya hatifungani za kampuni kumetokana na sehemu kubwa ya wawekezaji kuwa na malengo ya kuendelea na umiliki wa hatifungani zao hadi kipindi zitakapoiva yaani holding to maturity kutokana na faida na manufaa ya uwekezaji kwenye bidhaa hizi ikilinganishwa na bidhaa zingine kwenye masoko ya fedha.

 

Mifuko ya Uwekezaji wa Pamoja

Mwenendo wa uwekezaji katika Mifuko ya Uwekezaji wa Pamoja (Collective Investment Schemes) katika kipindi kilichoishia Machi 2023 ulikuwa mzuri. Thamani ya jumla ya uwekezaji katika mifuko ya uwekezaji wa pamoja iliongezeka kwa asilimia 69.17 na kufikia shilingi trilioni 1.44 katika kipindi kilichoishia Machi 2023, ikilinganishwa na shilingi bilioni 852.21 katika kipindi kilichoishia Machi 2022. Ongezeko hili limetokana na uhamasishaji pamoja na matumizi ya teknolojia katika utoaji wa huduma kwa wawekezaji. Jedwali lifuatalo linaonesha mwenendo wa uwekezaji katika Mifuko ya Uwekezaji wa Pamoja.

 

Jedwali 4: Mwenendo wa Uwekezaji katika Mifuko ya Uwekezaji wa Pamoja

 

 

31 Machi 2023

 

31 Machi 2022

 

Ongezeko la thamani

Meneja wa

Mifuko 

 

Jina la

Mfuko

Thamani ya Mfuko (TSH)

Bei ya

Kipande

(TSH)

Thamani ya Mfuko (TSH)

Bei ya

Kipande

(TSH)

Ongeze ko la

Thaman i ya

Mfuko

Ongeze ko la

Bei ya

Kipande

(%)

UTT AMIS

Plc

Mfuko wa Umoja 

311,546,992,055.25

903.7726

279,862,683,242.28

808.9271

11.32%

11.72%

Mfuko wa

Wekeza

Maisha 

8,200,947,926.48

772.1019

3,396,285,286.69

680.9052

141.47%

13.39%

Mfuko wa Watoto

9,568,813,873.36

569.5515

5,141,290,669.40

503.8917

86.12%

13.03%

Mfuko wa Jikimu

19,448,126,708.07

162.7009

18,074,006,916.99

154.7339

7.60%

5.15%

Mfuko wa Ukwasi

695,715,800,912.18

352.5116

365,591,173,928.37

312.5168

90.30%

12.80%

Mfuko wa Hatifungani

382,593,090,196.94

115.4184

180,146,881,623.94

113.1666

112.38%

1.99%

Watumishi

Housing Investmen

ts

 

Mfuko wa

Faida

14,634,005,454.77

102.5569

Mfuko wa Faida ulikuwa bado haujapata idhini ya kutoa huduma ya uwekezaji.

Thamani ya Jumla

1,441,707,777,12

7.05

 

852,212,321,667.67

 

69.17%

 

Chanzo: UTT AMIS Plc

 

 

(h)        Mwenendo wa Soko la Hisa

Mwenendo wa biashara katika soko la hisa hupimwa kwa kuzingatia viashiria vya ufanisi wa soko. Viashiria hivyo ni pamoja na: Thamani ya Mauzo ya hisa; Mtaji wa Soko (Market Capitalisation); Fahirisi za Soko (Share Index); na ushiriki kwenye Soko la Hisa. Katika kipindi cha kuanzia Machi 2022 hadi Machi 2023 mwenendo wa Soko la Hisa la Dar es Salaam ulikuwa wa kuridhisha. Ufanisi huu uliotokana na juhudi za Serikali katika kutoa elimu ya masuala ya uwekezaji na fursa na faida za kuwekeza katika masoko ya mitaji na dhamana.

 

Mtaji wa Soko la Hisa

Mtaji wa Soko la Hisa kwa kampuni za ndani yaani Domestic Market Capitalisation katika kipindi kilichoishia Machi 2023 uliongezeka kwa asilimia 16.97 na kufikia shilingi trilioni 10.82 ikilinganishwa na shilingi trilioni 9.25 katika kipindi kilichoishia Machi 2022. Aidha, Mtaji wa Jumla wa Soko la Hisa yaani Total Market Capitalisation katika kipindi kilichoishia Machi 2023 uliongezeka kwa asilimia 2.47 na kufikia shilingi trilioni 15.74 ikilinganishwa na shilingi trilioni 15.36 katika kipindi kilichoishia Machi 2022. Kuongezeka kwa mtaji wa Soko la Hisa kulitokana na kuongezeka kwa bei ya hisa za baadhi ya kampuni zilizoorodheshwa katika Soko la Hisa. Kampuni hizo ni pamoja na CRDB Bank Plc, DSE Plc, National Investment Company Limited (NICO), NMB Bank Plc, Swissport Tanzania Plc, Tanga Cement Plc, na TOL Gases Limited.

 

Mauzo ya Hisa

Mauzo ya hisa katika Soko la Hisa yaliongezeka kwa asilimia 2.90 na kufikia shilingi bilioni 119.21 katika kipindi kilichoishia Machi 2023, ikilinganishwa na mauzo ya shilingi bilioni 115.85 katika kipindi kilichoishia Machi 2022. Kuongezeka kwa mauzo kumetokana na kuongezeka kwa ushiriki wa wawekezaji katika masoko ya mitaji kutokana na elimu inayotolewa na Serikali kupitia Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana kwa kushirikiana na wadau wengine.

 

Fahirisi ya Soko (Market Index)

Fahirisi ya soko kwa hisa za kampuni za ndani yaani Domestic Market Index katika kipindi kilichoishia Machi 2023, iliongezeka kwa alama 573.50 na kufikia alama 4,091.56 ikilinganishwa na alama 3,518.06 zilizorekodiwa katika kipindi kilichoishia Machi 2022. Aidha, Fahirisi ya soko kwa hisa za kampuni zote yaani All Share Index katika kipindi kilichoishia Machi 2023, iliongezeka kwa alama 40.15 na kufikia alama 1,888.79 ikilinganishwa na alama 1,848.64 zilizorekodiwa katika kipindi kilichoishia Machi 2022. Kuongezeka kwa alama za fahirisi kunaashiria ufanisi wa soko hususan kuongezeka kwa bei za hisa za kampuni zilizoorodheshwa DSE, ambazo zinatoa huduma katika sekta za viwanda na fedha.

 

1.3.5. Deni la Serikali

Hadi kufikia mwezi Aprili 2023, deni la Serikali lilikuwa shilingi bilioni 79,100.19 sawa na ongezeko la asilimia 13.9 ikilinganishwa na Shilingi bilioni 69,440.01 kwa kipindi kama hicho mwaka 2022. Kati ya kiasi hicho, deni la nje ni shilingi bilioni 51,162.60 na deni la ndani ni Shilingi bilioni 27,937.59. Ongezeko la deni limetokana na: kupokewa kwa fedha za mikopo kwa ajili ya kugharamia miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa miundombinu ya barabara, reli, viwanja vya ndege, umeme, elimu na afya.Tathmini ya uhimilivu wa deni la Serikali iliyofanyika Desemba, 2022 imeonesha kuwa deni ni himilivu na viashiria vya deni viko ndani ya wigo unaokubalika kimataifa katika kipindi cha muda mfupi, wa kati na mrefu (Jedwali Na. 5).

 

Jedwali 5: Tathmini ya Uhimilivu wa Deni (Asilimia) kwa Mwaka 2022

Viashiria Vya Uhimilivu

Ukom

21/2

2

22/2

3

23/2

4

24/2

5

25/2

26/2

7

27/2

32/3

3

 

 

 

Deni la Nje 

 

 

 

 

 

Uwiano wa thamani ya sasa ya Deni kwa Pato la Taifa 

40

18.1

17.7

17.3

16.4

15.8

15.8

16.3

15.4

Uwiano wa thamani ya sasa ya Deni kwa

Mauzo ya Nje ya Nchi 

180

119.6

113.4

108.1

104.0

101.9

101.3

99.7

92.1

Viashiria Vya Uhimilivu

Ukom

21/2

2

22/2

3

23/2

4

24/2

5

25/2

26/2

7

27/2

32/3

3

Uwiano wa Ulipaji wa Deni kwa Mauzo ya

Nchi 

15

13.5

14.1

9.6

8.9

8.5

8.2

8.8

10.6

Uwiano wa Ulipaji wa Deni kwa Mapato 

18

14.1

14.9

10.4

9.6

9.3

9.3

10.9

12.2

                 Deni la Serikali (Ndani na Nje)

 

 

 

Uwiano wa Thamani ya sasa ya Deni kwa

pato la Taifa 

55

32.5

31.9

30.9

29.5

28.4

27.8

28.6

30.8

Uwiano wa Thamani ya sasa ya Deni kwa Mapato 

N/A 

217

207

202

196

194

195

207.7

207.1

Uwiano wa Ulipaji wa Deni kwa Mapato 

N/A 

34.0

41.6

33.3

30.5

27.6

27.7

30.1

41.0

  Chanzo: Wizara ya Fedha na Mipango, Desemba 2022

 

Katika kuhakikisha kuwa Deni la Serikali linaendelea kuwa himilivu, Serikali inatekeleza mikakati ifuatayo: 

(i)                Kuhakikisha mikopo inayopewa kipaumbele ni ile yenye masharti nafuu kadri inavyopatikana.  Aidha, hali hiyo inajidhihirisha katika bajeti inayopendekezwa ambapo mikopo nafuu imeongezeka kwa asilimia 22.8 na yenye masharti ya kibiashara imepungua kwa asilimia 14.4;

(ii)              Mikopo yenye masharti ya kibiashara itaelekezwa katika miradi inayochochea kasi ya ukuaji wa uchumi na mauzo nje ya nchi; na 

(iii)             Kuboresha mikakati ya kukusanya mapato ya ndani ili kuhakikisha sehemu kubwa ya bajeti inagharamiwa na mapato ya ndani pamoja na kupunguza matumizi yanayoweza kuepukika bila kuathiri uendeshaji wa shughuli za

Serikali.

 

Aidha, mnamo Machi 2023, kampuni za Fitch Ratings na Moody’s Investors Service zilianza zoezi la kuifanyia nchi tathmini ya kukopesheka katika masoko ya fedha ya kimataifa. Zoezi hilo lilikamilika ambapo kampuni ya Moody’s Investors Service ilichapisha matokeo ya tathmini hiyo mwezi Mei 2023 na kampuni ya Fitch Ratings mwezi Juni 2023. Kwa mujibu wa matokeo hayo, Tanzania imewekwa katika daraja la B2 POSITIVE na Kampuni ya Moody’s Investors Service pamoja na daraja la B POSITIVE na Kampuni ya Fitch Ratings ambayo yanaashiria taswira chanya kwa nchi kimataifa. Pamoja na mambo mengine, matokeo hayo yamechangiwa na mwenendo mzuri wa ukuaji wa uchumi, usimamizi makini wa deni la Taifa, kuweka mazingira wezeshi ya uwekezaji kwa sekta binafsi, kuimarisha ushirikiano wa kimataifa pamoja na kuleta maridhiano ya kisiasa ndani ya nchi. Kukamilika kwa zoezi hilo,  kutaiwezesha nchi kutambulika katika masoko ya fedha ya kimataifa na hivyo, kuongeza wigo wa upatikanaji wa mikopo kwa Serikali na sekta binafsi.

 

1.4. Maendeleo ya Watu

1.4.1. Ongezeko la Idadi ya Watu mwaka 2022

Kwa mujibu wa matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022, idadi ya watu Tanzania imeongezeka na kufikia watu 61,741,120 mwaka 2022 kutoka watu 44,928,923 mwaka 2012 sawa na ongezeko la wastani wa asilimia 3.2. Kati ya idadi hiyo, wanawake ni 31,687,990 sawa na asilimia 51.3 na wanaume ni 30,053,130 sawa na asilimia 48.7 ya watu wote. Matokeo ya sensa ni nyenzo muhimu katika mipango jumuishi na maendeleo endelevu ya nchi.

 

Aidha, kwa mujibu wa Utafiti wa Watu Wenye Uwezo wa Kufanya Kazi 2020/21, idadi ya nguvu kazi yenye umri wa miaka 15 na kuendelea imeongezeka kwa asilimia 20.6 kutoka watu 25,750,116 na kufikia watu  31,047,894 sawa na asilimia 54.8 ya idadi ya watu wote mwaka 2020/21. Kuongezeka kwa nguvu kazi ni fursa kubwa nchini katika shughuli mbalimbali za uzalishaji pamoja na sekta za huduma na masoko. Kwa upande mwingine, ongezeko la watu linaweza kuwa na athari hasi ikiwepo ongezeko la bajeti katika utoaji wa huduma mbalimbali za kijamii. 

 

1.4.2. Viashiria vya Maendeleo ya Watu

Katika kuendelea kuboresha maendeleo ya watu, Serikali imeendelea kuchukua hatua mbalimbali ikiwemo: uboreshaji wa huduma za afya; utoaji wa elimu msingi na sekondari bila ada; usambazaji wa umeme mijini na vijijini; utoaji wa huduma ya maji mijini na vijijini; na utoaji wa elimu ya ufundi na mafunzo ya ufundi stadi. Kutokana na utekelezaji wa miradi na programu mbalimbali za maendeleo, kumekua na matokeo chanya katika  viashiria vya maendeleo ya watu ikiwemo:

(i)            Kuongezeka kwa makadirio ya wastani wa umri wa kuishi kutoka miaka 67.8 (2023) hadi miaka 68.3 (2024) na makadirio ya wastani wa miaka 68.8 kwa mwaka 2025. Aidha, wastani wa umri wa kuishi kwa kuzingatia jinsia, unakadiriwa kufikia miaka 70.7 kwa wanawake na miaka 65.7 kwa wanaume mwaka 2024;

(ii)           Vifo vya watoto umri chini ya miaka mitano vimepungua kwa asilimia 36 kutoka vifo 67 kwa vizazi hai 1,000 mwaka 2016 hadi kufikia vifo 43 kwa vizazi hai 1000 mwaka 2022;

(iii)         Kupungua kwa vifo vitokanavyo na uzazi kutoka vifo 432 kwa kila vizazi hai 100,000 mwaka 2014/15 hadi vifo 250 kwa kila vizazi hai 100,000 mwaka 2020/21;

(iv)         Kuongezeka kwa idadi ya watanzania wanaonufaika na huduma za bima za afya kutoka asilimia 21.2 ya Idadi ya watu mwaka 2019/20 hadi asilimia 30.6 mwaka 2021/22;

(v)          Kuongezeka kwa kiwango cha uandikishaji wa wanafunzi wa elimu ya msingi kutoka 1,631,085 mwaka 2021 hadi wanafunzi 1,680,365 mwaka 2022, sawa na ongezeko la asilimia  3.0;

(vi)         Hali ya upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama imeimarika kwa wananchi wa vijijini kutoka wastani wa asilimia 70.1 mwaka 2020 hadi asilimia 77 mwezi Desemba, 2022 na kwa upande wa maeneo ya mijini kutoka wastani wa asilimia 84 mwaka 2020 hadi wastani wa asilimia 88 mwezi Desemba, 2022; na

(vii)        Kuunganishwa kwa jumla ya vijiji 10,127 kati ya vijiji 12,318 vya Tanzania Bara sawa na asilimia 82.21.

 

1.4.2.1. Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini 

Serikali kupitia Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini imeendelea na jitihada za kupunguza umaskini nchini ambapo hadi Machi 2023 jumla ya kaya 1,371,916 zilizokidhi vigezo vya kuingia katika Kipindi cha Pili cha Mpango kutoka maeneo yote ya utekelezaji 186 kwa Tanzania Bara, Pemba na Unguja kwa Zanzibar ambapo jumla ya shilingi bilioni 218 zilitumika. Aidha, kazi nyingine zilizotekelezwa ni pamoja na: jumla ya vikundi 12,054 viliundwa vyenye jumla ya wanachama 165,608 (wanawake 137,451 na wanaume 28,157) kwenye Mamlaka 72 za utekelezaji kwa Tanzania Bara; na na jumla ya miradi 14,236 iliibuliwa na jamii na kuanza kutekelezwa katika mamlaka za utekelezaji 123 ambapo jumla ya kaya za walengwa 660,000 zimeshiriki katika kutekeleza miradi hiyo yenye thamani ya jumla ya shilingi bilioni 40.2.  

 

1.4.2.2. Upatikanaji wa Chakula 

Taarifa ya Tathmini ya Mwisho ya Uzalishaji wa Mazao ya Chakula Msimu wa 2021/2022 inaonesha kuwa, hali ya uzalishaji wa mazao ya chakula umefikia tani 17,148,290 kwa mlinganisho wa nafaka (Grain Equivalent) ambapo mazao ya nafaka ni tani 9,233,298 na mazao yasiyo nafaka ni tani 7,914,992. Aidha, Mahitaji ya chakula kwa mwaka 2022/23 ni tani 15,053, 299 ambapo na ziada ni tani 2,095,256 za chakula. Kiwango cha Utoshelevu wa chakula (Self Sufficiency Ratio – SSR) nchini kinatarajiwa kuwa na ziada kwa uwiano wa asilimia 114 mwaka 2022/23. 

 

SURA YA PILI 

 

MAPITIO YA UTEKELEZAJI WA MPANGO  

 

2.1. Utangulizi

Sura hii inaeleza kwa muhtasari utekelezaji wa Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2022/23 hadi Aprili 2023. Aidha, Sura hii inaainisha bajeti iliyotengwa kwa ajili ya kugharamia miradi ya maendeleo, kiasi cha fedha kilichotumika na hatua mbalimbali zilizofikiwa katika utekelezaji wa baadhi ya miradi ya maendeleo. Vile vile, Sura hii inabainisha changamoto zilizojitokeza katika kipindi cha utekelezaji wa Mpango na mikakati ya kukabiliana nazo. 

 

2.2. Utekelezaji wa Bajeti ya Maendeleo ya Mwaka 2022/23 

Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2022/23 umetengewa jumla ya shilingi bilioni 15,006.0, sawa na asilimia 36.2 ya Bajeti ya Serikali ambapo shilingi bilioni 12,306.9, sawa na asilimia  82.0 ya bajeti ya fedha za maendeleo ni fedha za ndani na shilingi bilioni 2,699.1, sawa na asilimia 18.0 ni fedha za nje.

 

Ridhaa ya matumizi ya fedha za maendeleo iliyotolewa katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Mei, 2023, ni shilingi bilioni 12,885.09 sawa na asilimia 93.67 ya lengo katika kipindi hicho. Kati ya kiasi hicho kilichotolewa, shilingi bilioni 11,145.51 ni fedha za ndani na shilingi bilioni 1,739.58 ni fedha za nje. Aidha, baadhi ya maeneo ya kipaumbele yaliyopatiwa fedha za maendeleo katika kipindi husika ni kama ifuatavyo:

 

(i)            Shilingi bilioni 1,164.34 kwa ajili ya Mradi wa Kufua Umeme wa Maji wa Julius Nyerere katika Mto Rufiji – MW 2,115;

(ii)           Shilingi bilioni 1,289.46 kwa ajili ya ujenzi wa reli ya kati kwa kiwango cha kimataifa (Standard Gauge Railway)

(iii)         Shilingi bilioni 1,151.11 kwa ajili ya ujenzi na ukarabati wa barabara kuu, barabara za mikoa, barabara za mijini na vijijini na madaraja;

(iv)         Shilingi bilioni  652.1 kwa ajili ya kugharamia mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu; 

(v)          Shilingi bilioni  274.71 kwa ajili ya kuimarisha usafirishaji majini ikiwemo ujenzi na ukarabati wa bandari, ununuzi na ukarabati wa meli na vivuko katika bandari za maziwa makuu;

(vi)         Shilingi bilioni 290.14 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maji mijini na vijijini; 

(vii)        Shilingi bilioni 199.29 kwa ajili ya ukarabati wa Reli ya Kati (Mfuko wa Maendeleo ya Reli);

(viii)      Shilingi bilioni 295.3 kwa ajili ya kugharamia elimumsingi na sekondari bila ada ikijumuisha mahitaji ya wanafunzi wote wa shule za msingi na sekondari

za Serikali na posho ya madaraka kwa wakuu wa shule, waratibu elimu kata na walimu wakuu;

(ix)         Shilingi bilioni 202.51 kwa ajili ya mradi wa usambazaji umeme vijijini kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA); na 

(x)          Shilingi bilioni 159.23 kwa ajili ununuzi wa dawa, vifaa, vifaa tiba na vitendanishi pamoja na chanjo za watoto kupitia MSD

 

2.3. Hatua za Utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo

 

2.3.1. Miradi ya  Kielelezo

Hatua iliyofikiwa katika utekelezaji wa miradi ya kielelezo ni kama ifuatavyo:

 

(i)           Mradi Na. 4281: Ujenzi wa Reli ya Kati kwa Kiwango cha Kimataifa (SGR)

Hatua iliyofikiwa ni: Kuendelea na ujenzi wa njia ya reli kwa kipande cha Dar es Salaam – Morogoro (km 300) ambapo utekelezaji umefikia asilimia 98.14 ikiwa ni pamoja na ujenzi wa njia ya kuelekea bandarini (Port link) ambapo utekelezaji umefikia asilimia 34.97; kipande cha Morogoro – Makutupora (km 422) umefikia asilimia 93.83; kipande cha Mwanza - Isaka (km 341) asilimia 31.07; kipande cha Makutupora- Tabora (km 371) asilimia 7.0; kipande cha Tabora - Isaka (km 165) asilimia 2.39; na kusaini mkataba wa ujenzi wa reli ya SGR kipande cha Tabora – Kigoma (km 506).

 

Shughuli nyingine zilizotekelezwa ni: Ununuzi wa vichwa viwili (2) vya treni na mabehewa 30 kwa ajili ya majaribio na uendeshaji wa awali; kufanyika kwa sehemu ya malipo kwa ajili ya ununuzi wa vichwa vya treni 17 vya umeme na seti za treni 10 za kisasa (Electric Multiple Unit - EMU) kwa ajili ya uendeshaji ambapo utengenezaji wa vichwa vya treni umefikia asilimia 42.1 na utengenezaji wa seti za treni umefikia asilimia 38.1; kununuliwa kwa mabehewa 59 ya abiria ambapo mabehewa 14 yamewasili nchini na mabehewa 45 yaliyosalia utengenezaji unaendelea ambao umefikia asilimia 95; na ununuzi wa mabehewa 1,430 ya mizigo ambapo utengenezaji umefikia asilimia 42. Jumla ya shilingi bilioni 1,289.46 zimetumika katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023.

 

(ii)         Mradi Na. 3172: Kufua Umeme wa Maji wa Julius Nyerere (MW 2,115)  

Hatua iliyofikiwa ni: Kukamilika kwa handaki la kuchepusha maji (diversion tunnel); kukamilika kwa ujenzi wa kingo ndogo za juu na chini, ukuta wa bwawa kuu ambapo utekelezaji umefikia asilimia 94.85, handaki la kupeleka maji kwenye mitambo (power waterway) asilimia 99.08, jengo la mitambo (power house) (asilimia 68.30), kituo cha kupokea na kusafirishia umeme (switchyard) (asilimia 98.87), kingo saidizi za kuzuia maji yasitoroke (asilimia 84.47), nyumba za makazi ya watumishi (asilimia

92.69), barabara za kudumu (asilimia 38.71) na daraja la kudumu (asilimia 96.87). Kwa ujumla utekelezaji wa mradi umefikia asilimia  86.89. Aidha, zoezi la ujazaji maji linaendelea ambapo hadi kufikia tarehe 23 Mei, 2023 kina cha maji ya bwawa kimefikia mita 160.51 kutoka usawa wa bahari. Jumla ya shilingi bilioni 1,164.3 zimetumika katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023.

 

(iii)       Mradi Na. 4294: Kuboresha Shirika la Ndege Tanzania 

Hatua iliyofikiwa ni: Kufanyika kwa sehemu ya malipo ya ununuzi wa ndege nne (4) ambazo ni ndege moja (1) aina ya Boeing 767-300F ya mizigo iliyowasili tarehe 03 Juni, 2023, ndege mbili  (2) aina ya Boeing 737-9 Max inayotarajiwa kuwasili mwezi Agosti 2023 na nyingine mwezi Desemba 2023 na ndege moja (1) aina ya Boeing 787-8 Dreamliner inayotarajiwa kuwasili mwezi Februari, 2024; ukarabati wa miundombinu katika karakana ya KIMAFA katika Kiwanja cha Ndege cha Kilimanjaro (KIA) unaendelea ambapo utekelezaji umefikia asilimia 85. Aidha, ununuzi wa vifaa na vipuri kwa ajili ya kuwezesha kufanya matengenezo makubwa na madogo kwa ndege zote katika hanga zote za JNIA na KIA unaendelea; kuanza ukarabati wa nyumba 38 zilizopo KIA na ujenzi wa majengo matatu ya kuhifadhia mizigo katika viwanja vya ndege vya JNIA, KIA na Songwe. Vile vile, ATCL imeendelea kutoa huduma ya usafiri wa anga katika vituo 24 ambapo vituo 14 ni vya ndani ya nchi na vituo 10 nje ya nchi. Jumla ya shilingi bilioni 138.47 zimetumika katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023.

 

(iv)       Mradi Na. 3155: Kuchakata na Kusindika Gesi Asilia kuwa Kimiminika (Liquefied Natural Gas - LNG) – Lindi

Hatua iliyofikiwa ni: Kuendelea na tafiti za kisayansi (geoscience) na tafiti za mitambo itakayosimikwa katika eneo la mradi; na kukamilika kwa majadiliano ya Mkataba Hodhi (HGA) kati ya Serikali na Wawekezaji. Aidha, Mshauri elekezi (Kampuni ya Baker Botts) ambaye anaishauri Serikali kuhusu masuala ya sheria, fedha, biashara, uchumi na masoko ameendelea na kazi kwa kushirikiana na Timu ya Majadiliano ya Serikali (GNT). Jumla ya shilingi bilioni 5.49 zimetumika katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023.

 

(v)         Mradi Na. 3176: Ujenzi wa Bomba la Mafuta Ghafi kutoka Hoima (Uganda) hadi Tanga (Tanzania) lenye urefu wa km 1,443

Hatua iliyofikiwa ni: Kukamilika kwa malipo ya fidia kwa wananchi 387 kati ya 388 waliopisha maeneo 14 ya ujenzi wa kambi zitakazotumika wakati wa ujenzi wa bomba. Aidha, hadi kufikia mwezi Aprili, 2023 wananchi 9,325 kati ya 9,508  wanaopisha eneo la mkuza wa bomba walikuwa wamelipwa jumla ya shilingi bilioni 31.89 na taratibu za malipo kwa waliobaki zilikuwa zinaendelea. Vilevile, Serikali iliendelea kulipia asilimia 15 ya hisa zake katika Kampuni ya EACOP, ambapo jumla ya  dola za Marekani milioni 138.2 zimekwishalipwa. Kazi nyingine zilizotekelezwa ni pamoja na kuendelea na ujenzi wa kituo cha kuweka mfumo wa kupasha joto mabomba (thermal insulation plant) katika kijiji cha Sojo, Nzega Tabora ambapo utekelezaji umefikia asilimia 87 na kutoa Kibali cha Ujenzi wa Mradi, ikiwa ni hatua muhimu katika maandalizi ya kuanza ujenzi wa Mradi. Jumla ya shilingi bilioni 75.48 zimetumika katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023.

 

(vi)       Mradi wa Kiwanda cha Sukari Mkulazi  

Hatua iliyofikiwa ni Kusafishwa kwa eneo lenye ukubwa wa hekta 710 kati ya hekta 790 zilizokuwa zimebaki bila kusafishwa. Eneo la shamba lililolimwa na kupandwa miwa limefikia ukubwa wa hekta 3,011 kati ya eneo la hekta 3,600 linalotarajiwa kulimwa na kupandwa miwa. Kupatikana kwa Mkandarasi wa ujenzi wa bwawa kubwa lenye uwezo wa kujaza maji kiasi cha mita za ujazo milioni 3.5 ambapo ujenzi umefikia asilimia 28; ujenzi wa kiwanda cha sukari Mbigiri umefikia asilimia 90; na kununuliwa kwa mtambo wa kupakia miwa "Cane Loader". Jumla ya shilingi bilioni 39.84 zimetumika katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023.

 

(vii)      Mradi Na. 4015: Daraja la Kigongo – Busisi (Mwanza)

Hatua iliyofikiwa ni: Kuendelea na ujenzi wa daraja pamoja na barabara unganishi zenye urefu wa km 1.66 ambapo ujenzi umefikia asilimia 72. Jumla ya shilingi bilioni 126.7 zimetumika katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023.

 

(viii)    Mradi Na. 4191: Daraja Jipya la Selander (Tanzanite Dar es Salaam) Hatua iliyofikiwa ni: Kukamilika kwa barabara unganishi zenye urefu wa km 5.2. Jumla ya shilingi bilioni 1.74 zimetumika katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023.

 

(ix)       Mradi Na. 1122: Magadi  Soda Engaruka

Hatua iliyofikiwa ni: Kukamilika kwa uthamini wa mradi, vitabu vya uthamini wa fidia vimewasilishwa kwa Mthamini Mkuu wa Serikali na gharama ya fidia iliyohakikiwa ni shilingi bilioni 14.8. Jumla ya shilingi milioni 385.26 zimetumika katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023.

 

(x)         Mradi Na. 3171:  Makaa ya Mawe Mchuchuma

Hatua iliyofikiwa ni: Kukamilika kwa uhakiki wa mali  na kuanza kulipa fidia kwa wananchi wanaopisha mradi katika vitongoji vya Nkomang’ombe, Idusi, Kilomos, Ntiule na Mhambalasi. Aidha, jumla ya shilingi bilioni 5.41 zimetengwa kwa ajili ya kuendelea na zoezi la ulipaji wa fidia. 

 

(xi)       Mradi Na. 3161: Chuma Liganga

Hatua iliyofikiwa ni: Kukamilika kwa uhakiki wa mali na kuanza kulipa fidia kwa wananchi watakaopisha mradi katika katika vitongoji vya Mnyusi, Ilongi na Myorua katika Kijiji cha Mundindi na Kitongoji cha Luhaha katika Kijiji cha Amani. Aidha, jumla shilingi bilioni 10.36 zimetengwa kwa ajili ya kuendelea na zoezi la ulipaji wa fidia.  

(xii)     Kanda Maalumu za Kiuchumi ikiwemo Eneo Maalumu la Uwekezaji Bagamoyo

Mradi Na. 4920: Eneo Maalumu la Uwekezaji Bagamoyo 

Hatua iliyofikiwa ni: Kukamilika kwa kazi ya kuhuisha upembuzi yakinifu na Mpango Kabambe katika eneo husika, kupatikana kwa mkandarasi wa kujenga  barabara kwa kiwango cha lami (Asphalt Concrete) yenye urefu wa kilometa 3 katika eneo lililoanza kujengwa viwanda lililopo Zinga – Bagamoyo. Jumla ya shilingi milioni 103 zimetumika katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023.

 

(xiii)    Mradi Na. 4702:  Ujenzi wa Bandari ya Uvuvi – Kilwa Masoko

Hatua iliyofikiwa ni kukamilika kwa kazi ya usanifu wa kina (Detail Design) na kuanza kazi ya uchimbaji.

 

(xiv)    Mradi Na. 3165: Kufua Umeme wa Maji wa Ruhudji (MW 358) – Njombe 

Hatua iliyofikiwa ni: kukamilika kwa uhuishaji wa Upembuzi Yakinifu; uthamini wa mali za wananchi watakaopisha mradi; na  tathmini ya athari za mazingira na jamii. 

 

(xv)     Mradi Na. 3167: Kufua Umeme wa Maji wa Rumakali (MW 222) - Njombe

Hatua iliyofikiwa ni: kukamilika kwa uhuishaji wa Upembuzi Yakinifu; na  tathmini ya athari za mazingira na jamii.

 

2.3.2. Kuchochea Uchumi Shindani na Shirikishi

2.3.2.1. Uendelezaji wa Miundombinu na Huduma 

A.          Reli

 

(a)         Mradi Na. 4213: Mfuko wa Reli 

Hatua iliyofikiwa ni: Kukamilika kwa ununuzi wa mabehewa 22 ya abiria kwa ajili ya reli ya MGR; kukamilika kwa ukarabati wa mabehewa 52 ya mizigo na mabehewa sita (6) ya abiria na kuanza kutoa huduma; na kukamilika kwa uboreshaji wa mfumo wa mawasiliano na umeme katika njia ya reli ya MGR kutoka Dar es Salaam hadi Mwanza. Jumla ya shilingi bilioni 199.29 zimetumika katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023.

 

(b)         Uboreshaji wa Reli ya TAZARA

Hatua iliyofikiwa ni: Kuunganishwa kwa vichwa vinane (8) katika Mfumo wa Ufuatiliaji wa Mwenendo wa Mabasi ya masafa marefu na treni; usafirishaji wa tani 244,492 za mizigo ikilinganishwa na tani 210,161 zilizosafirishwa katika kipindi kama hicho 2021/22 sawa na ongezeko la asilimia 16.3; kusafirishwa kwa abiria 300,476 hadi Aprili, 2023 ikilinganishwa na 296,307 katika kipindi kama hicho; na kusainiwa kwa mikataba ya kutumia njia ya reli kwa kulipia tozo (Access Fee) na ya kusafirisha mizigo kwa kutumia njia ya reli.

 

B.          Barabara na Madaraja

 

Barabara za Lami Zinazofungua Fursa za Kiuchumi

 

(i)           Mradi Na. 4147: Barabara ya Kidatu – Ifakara – Lupilo - Malinyi – Londo – Lumecha/Songea (km 499)

Hatua iliyofikiwa ni: Kuendelea na ujenzi wa kipande cha Kidatu – Ifakara (km 68) ambapo utekelezaji umefikia asilimia 77. Jumla ya shilingi bilioni 17.74 zimetumika katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023.

 

(ii)         Mradi Na. 4149: Barabara ya Makutano – Natta – Mugumu/Loliondo – Mto wa Mbu (km 235)

Hatua iliyofikiwa ni: Kuendelea na ujenzi wa sehemu ya Sanzate – Natta (km 40) ambapo utekelezaji umefikia asilimia 29; Tarime – Mugumu (km 86) sehemu ya Mogabiri – Nyamongo km 25 (asilimia 8); na kuendelea na maandalizi ya ujenzi wa kipande cha  Natta – Mugumu (km 45). Jumla ya shilingi bilioni 12.69 zimetumika katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023.

 

(iii)       Mradi Na. 4190: Barabara ya Itoni – Ludewa - Manda (km 211) Hatua iliyofikiwa ni: Kukamilika kwa ujenzi wa kipande cha Lusitu – Mawengi (km 50); na kuendelea na ujenzi wa sehemu ya Itoni – Lusitu (km 50) ambapo utekelezaji umefikia asilimia 2. Jumla ya shilingi bilioni 15.26 zimetumika katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023.

 

(iv)       Mradi Na. 4193: Barabara ya Handeni – Kiberashi – Kijungu – Kibaya – Njoro – Olboloti – Mrijo Chini – Dalai – Bicha – Chambalo – Chemba – Kwa Mtoro - Singida (Km 460)  

Hatua iliyofikiwa ni kuendelea na ujenzi wa sehemu ya Handeni – Kiberashi (km 50)  sehemu ya Handeni - Mafuleta (km 20) ambapo utekelezaji umefikia asilimia 11.61 na sehemu ya Mafuleta – Kileguru (km 30) taratibu za manunuzi zinaendelea. Jumla ya shilingi bilioni 2.41 zimetumika katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023.

 

(v)         Mradi Na. 4188: Barabara ya Mbeya – Makongolosi – Manyoni - Mkiwa (km 528)

Hatua iliyofikiwa ni: Kuendelea na ujenzi wa  barabara ya  Noranga – Itigi – Mkiwa (km 56.9) kwa kiwango cha lami sehemu ya Noranga – Itigi (Mlongaji – km 25) ambapo utekelezaji umefikia asilimia 12; ujenzi wa barabara za Itigi Mjini (km 10) umefikia asilimia 70; na sehemu ya Mlongaji - Mkiwa (km 31.9) taratibu za manunuzi zinaendelea. Jumla ya shilingi bilioni 15 zimetumika katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023.

 

(vi)       Mradi Na. 4112: Barabara ya Kigoma – Kidahwe – Uvinza – Kaliua – Tabora (km 389.7)

Hatua iliyofikiwa ni: Kuendelea na ujenzi wa kipande cha Chagu – Kazilambwa (km 36) ambapo utekelezaji umefikia asilimia 74.4; kuendelea kwa ujenzi wa kipande cha Uvinza – Malagarasi (km 51.1) ambapo utekelezaji umefikia asilimia 26; na ujenzi wa

Urambo Roundabout unaendelea na umefikia asilimia 60. Jumla ya shilingi bilioni 29.93 zimetumika katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023.

 

(vii)      Mradi Na. 4041: Barabara ya Kitai – Lituhi (km 90) na Daraja la Mnywamaji

Hatua iliyofikiwa ni: Kuendelea na ujenzi kwa kiwango cha lami wa barabara ya Kitai – Lituhi (km 90) sehemu ya Amanimakoro – Ruanda (km 35) na ujenzi wa daraja la Mnywamaji ambapo utekelezaji umefikia asilimia 22; na sehemu ya Luanda – Ndumbi Port (km 50) taratibu za manunuzi zinaendelea. Jumla ya shilingi bilioni 5.99 zimetumika katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023.

 

(viii)    Mradi Na. 4174: Upanuzi wa Barabara ya Kimara – Kibaha (km 25.7) Ikijumuisha Upanuzi wa Madaraja ya Kibamba, Kiluvya na Mpiji

Hatua iliyofikiwa ni: Kuendelea na ujenzi kwa kipande cha Kimara – Kibaha Mizani (km 19.2) na upanuzi wa madaraja ya Kibamba, Kiluvya na Mpiji ambapo utekelezaji umefikia asilimia 86. Jumla ya shilingi bilioni 5.68 zimetumika katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023.

 

(ix)       Mradi Na. 4024: Barabara ya Nanganga - Ruangwa - Nachingwea (km 145)

Hatua iliyofikiwa ni: Kuendelea na ujenzi kwa kiwango cha lami kwa kipande cha Nanganga – Ruangwa (km 53.2) ambapo utekelezaji umefikia asilimia 59. Aidha, taratibu za manunuzi zinaendelea kwa sehemu ya Ruangwa – Nachingwea (km 57.6). Jumla ya shilingi bilioni 7.87 zimetumika katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023.

 

(x)         Mradi Na. 4101: Barabara ya Tanga - Pangani – Makurunge (km 174.5)

Hatua iliyofikiwa ni: Kuendelea na ujenzi wa kipande cha Tanga - Pangani (km 50) kwa kiwango cha lami ambapo utekelezaji umefikia asilimia 62 na barabara ya Pangani – Mkange (km 214.5), sehemu ya Tungamaa – Mkange (km 95.2)  utekelezaji umefikia asilimia 19.2; na ujenzi wa Daraja la Pangani lenye urefu wa mita 525 na barabara unganishi (km 25.6) umefikia asilimia 3. Jumla ya shilingi bilioni 20.35 zimetumika katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023. 

 

(xi)       Mradi Na. 4014: Barabara ya Kibaoni - Majimoto - Muze - Kilyamatundu (km 152)  

Hatua iliyofikiwa ni: Kuendelea na ujenzi wa barabara ya Ntendo – Muze – Kilyamatundu (km 200) sehemu ya Ntendo – Kizungu (km 25) ambapo utekelezaji umefikia asilimia 14. Jumla ya shilingi bilioni 4.43 zimetumika katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023.

 

(xii)     Mradi Na. 4022: Barabara ya Njombe - Makete - Isyonje (km 157.4) Hatua iliyofikiwa ni: Kukamilika kwa ujenzi sehemu ya Moronga – Makete (km 53.5) kwa kiwango cha lami; na kuanza kwa ujenzi wa barabara ya Isyonje – Makete (km 50) Sehemu ya Kitulo – Iniho (km 36). Jumla ya shilingi bilioni 6.61 zimetumika katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023.

 

(xiii)    Mradi Na. 4123: Barabara ya Dumila – Kilosa (km 141)

Hatua iliyofikiwa ni: Kuendelea na ujenzi wa sehemu ya Rudewa - Kilosa (km 24) ambapo utekelezaji umefikia asilimia 93. Jumla ya shilingi bilioni 1.26 zimetumika katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023.

 

Barabara Zinazounganisha Tanzania na Nchi Jirani

 

(i)           Mradi Na. 4124: Barabara ya Sumbawanga - Matai - Kasanga Port (km 117)

Hatua iliyofikiwa ni: Kuendelea na ujenzi wa barabara ya Matai – Kasesya (km 50) kwa kiwango cha lami sehemu ya Matai – Tatanda (km 25) ambapo utekelezaji umefikia asilimia 12 na sehemu ya Tatanda – Kasesya (km 25) taratibu za manunuzi zinaendelea. Jumla ya shilingi bilioni 5.97 zimetumika katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023.

 

(ii)         Mradi Na. 4115: Barabara ya Marangu - Tarakea - Rongai – Kamwanga/ Sanya Juu (km 271)

Hatua iliyofikiwa ni: Kuendelea na ujenzi wa barabara ya Kiboroloni – Kiharara – Tsuduni – Kidia (km 10.8) kwa kiwango cha lami ambapo utekelezaji umefikia asilimia 46. Jumla ya shilingi bilioni14.69 zimetumika katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023.

 

(iii)       Mradi Na. 4154: Barabara ya Sumbawanga - Mpanda - Nyakanazi (km 432.56)

Hatua iliyofikiwa ni: Kuendelea kwa ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami ya Mpanda – Mishamo – Uvinza Sehemu ya Vikonge – Luhafwe (km 25) ambapo utekelezaji umefikia asilimia 11 na sehemu ya Luhafwe – Mishamo Jct (Bulamata) – km 37.25 taratibu za manunuzi zinaendelea; na kuendelea na ujenzi wa barabara ya Kibaoni – Sitalike (km 71) sehemu ya Kibaoni – Mlele Jct (km 50) ambapo utekelezaji umefikia asilimia 5 na sehemu ya Mlele Jct – Sitalike (km 21) taratibu za manunuzi zinaendelea. Jumla ya shilingi bilioni 27.17 zimetumika katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023.

 

(iv)       Mradi Na. 4141: Barabara ya Nyamuswa – Bunda – Kisorya (km 107.4)

Hatua iliyofikiwa ni: Kukamilika kwa ujenzi wa kipande cha Kisorya - Bulamba (km 107.4) kwa kiwango cha lami. Jumla ya shilingi bilioni 17.96 zimetumika katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023.

 

(v)         Mradi Na. 4162: Barabara ya Mwigumbi Maswa - Bariadi Lamadi (km 121)

Hatua iliyofikiwa ni kukamilika kwa ujenzi wa barabara ya mchepuo wa Maswa (km 11). Jumla ya shilingi bilioni 21.37 zimetumika katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023.

 

(vi)       Mradi Na. 4164: Barabara ya Kidahwe - Kasulu – Kibondo - Nyakanazi (km 341.25)

Hatua iliyofikiwa ni: Kuendelea na ujenzi wa sehemu za Kanyani Junction – Mvugwe (km 70.5) ambapo utekelezaji umefikia asilimia 56, Mvugwe – Nduta Junction (km 59.35) asilimia 66, Kibondo Junction – Kabingo (km 62.5) asilimia 77 na Nduta Junction – Kibondo (km 25.9) asilimia 58. Jumla ya shilingi bilioni 57.7 zimetumika katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023.

 

(vii)      Mradi Na. 4128: Barabara ya Kyaka – Bugene – Kasulo (km 183.1)

Hatua iliyofikiwa ni: Kuendelea na ujenzi wa sehemu ya Bugene – Kasulo –Kumunazi & Kyaka – Mutukula (km 124) sehemu ya Bugene – Burigi Chato National Park (km 60) ambapo utekelezaji umefikia asilimia 12. Aidha ujenzi wa sehemu ya Kyaka – Bugene (km 59.10) umekamilika. Jumla ya shilingi bilioni 14.06 zimetumika katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023.

 

Barabara za Mikoa na Kupunguza Msongamano

 

(a)         Mradi Na. 4138: Barabara za Kupunguza Msongamano Jijini Dar es Salaam (km 138.5) 

Hatua iliyofikiwa ni: Kuendelea na ujenzi  wa barabara ya Goba – Matosa – Temboni (km 6) ambapo ujenzi wa km 1 umekamilika; na kuendelea kwa usanifu wa kina kwa ajili ya ukarabati na upanuzi kwa kiwango cha lami wa barabara ya Mwai Kibaki (km 9.1). Jumla ya shilingi bilioni 1.52 zimetumika katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023.

(b)         Mradi Na. 4145: Kasulu – Manyovu pamoja na barabara za kuingia Kasulu mjini (km 68) 

Hatua iliyofikiwa ni kuendelea na ujenzi kwa kiwango cha lami barabara ya Kasulu – Manyovu pamoja na barabara za kuingia Kasulu Mjini (spur roads) ambapo utekelezaji umefikia asilimia 46. Jumla ya shilingi milioni 329.97 zimetumika katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023.

 

(c)         Mradi Na. 4132: Barabara za Mikoa (km 770.50)

Hatua iliyofikiwa ni: Kujengwa kwa jumla ya kilometa 23.11 za barabara za mikoa kwa kiwango cha lami na jumla ya kilometa 253.67 zilikarabatiwa kwa kiwango cha changarawe. Aidha, utekelezaji wa miradi ya madaraja/makalavati ulifikia asilimia 88.82 ambapo madaraja madogo 40 yalijengwa kwa kutumia fedha za Mfuko Mkuu wa Serikali na madaraja madogo 26 yalijengwa kwa kutumia fedha za Mfuko wa Barabara. Jumla ya shilingi bilioni 27.43 zimetumika katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023.

 

(d)         Mradi Na. 4285 Miundombinu ya Mabasi Yaendayo Haraka (Dar es Salaam)

Awamu ya Pili

Hatua iliyofikiwa ni kuendelea na ujenzi wa Lot 1 inayohusisha barabara zenye urefu wa km 20.3 (Mbagala - Mzunguko wa Bandari (Bendera Tatu) – Kariakoo, Barabara ya Kawawa – barabara ya Morogoro (Magomeni), Barabara ya Chang’ombe – Barabara ya Kilwa) ambapo ujenzi umefikia asilimia 90. Jumla ya shilingi bilioni 179.89 zimetumika katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023.

 

Awamu ya Tatu

Hatua iliyofikiwa ni kuendelea na ujenzi wa barabara za Azikiwe na Maktaba, Bibi Titi, Uhuru na Nyerere hadi Gongo la Mboto zenye jumla ya kilomita 23.6 na kituo kikuu cha mabasi Kariakoo; Shaurimoyo na Uhuru kupitia Buguruni hadi TAZARA umeanza ambapo utekelezaji umefikia asilimia 5. Jumla ya shilingi bilioni 34.75 zimetumika katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023.

 

(e)        Mradi Na. 4146: Barabara ya Mzunguko katika Jiji la Dodoma 

Hatua iliyofikiwa: Kuendelea na ujenzi kwa kiwango cha lami kwa barabara ya mzunguko (Dodoma City Outer Dual Carriageway Ring Road Lot 1 & 2 km 112.3), sehemu za  barabara ya Nala – Veyula – Mtumba – Ihumwa Dry Port (km 52.3) ambapo utekelezaji umefikia asilimia 25; Ihumwa - Dry Port – Matumbulu – Nala (km 60) asilimia 19; Kikombo Jctn – Chololo – Mapinduzi (JWTZ HQ) asilimia 6.5. Jumla ya shilingi bilioni 23.62 zimetumika katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023.

 

Barabara za Vijijini na Mijini

 

Mradi Na. 4170: Matengenezo na Ukarabati wa Barabara

Hatua iliyofikiwa ni: Kukamilika kwa  matengenezo ya  barabara yenye urefu wa km 14,826.35; kukamilika kwa ujenzi wa bararaba kwa kiwango cha lami zenye urefu wa km 163.83 na barabara za changarawe zenye urefu wa km 4,724.15, mifereji ya maji ya mvua yenye urefu wa mita 5,267.85; ujenzi wa madaraja 75 na makalavati 95. Jumla ya shilingi bilioni 420.58 zimetumika katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023.

 

Ujenzi wa Nyumba za Serikali na Madaraja

 

(a)         Mradi Na. 4126: Ujenzi wa Madaraja Makubwa

Hatua iliyofikiwa ni: jumla ya madaraja makubwa nane (8) yamejengwa na kukamilika ambayo ni Daraja la Tanzanite (DSM), Daraja la Gerezani (DSM), Daraja la Mpwapwa (Dodoma), Daraja la Kiegeya (Morogoro), Daraja la Ruhuhu (Ruvuma), Daraja la Kitengule (Kagera) na Daraja la Msingi (Singida). Jumla ya shilingi bilioni 3.9 zimetumika katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023.

 

(b)         Mradi Na. 4020: Daraja Jipya la Wami (Pwani) 

Hatua iliyofikiwa ni kukamilika kwa ujenzi wa daraja la Wami lenye urefu wa mita 510 na barabara unganishi (km 4.3). Jumla ya shilingi bilioni 14.85 zimetumika katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023.

 

(c)         Mradi Na. 6327: Ujenzi na Ukarabati wa Majengo ya Serikali

Hatua iliyofikiwa: Kukamilika kwa ujenzi wa nyumba 20 za Viongozi Jijini Dodoma na kufanya maandalizi ya kuanza awamu ya II; kukamilika kwa ukarabati wa nyumba 66 kati ya 431 zilizohamishiwa TBA kutoka CDA;  kuendelea na ujenzi wa nyumba 150 (Awamu I) za makazi ya watumishi wa umma katika eneo la Nzuguni Jijini Dodoma, ambapo utekelezaji umefikia asilimia 92 na ujenzi wa nyumba 150 nyingine (Awamu ya II) za watumishi wa Umma Jijini Dodoma umefikia asilimia 3; kukamilika kwa ujenzi wa nyumba tano (5) za majaji katika mikoa ya Kilimanjaro, Tabora, Shinyanga na Mtwara na ujenzi wa nyumba moja (1) katika mkoa wa Kagera umefikia asilimia 40; kukamilika kwa ukarabati wa nyumba 40 za viongozi Dodoma eneo la Area D; kuendelea na ukarabati wa nyumba 30 za viongozi mikoani na matengenezo kinga ya majengo ya Magomeni Kota ambapo utekelezaji umefikia asilimia 60; kuendelea na ukarabati wa nyumba zinazomilikiwa na TAMISEMI/NHC katika mikoa 20 zilizohamishiwa TBA ambao umefikia asilimia 67.5; kuendelea na ujenzi wa nyumba za watumishi Temeke Kota ambapo utekelezaji umefikia asilimia 19; na kukamilika kwa ujenzi wa Ghorofa za Watumishi wa Umma katika eneo la Magomeni Kota Awamu ya II “Block” A na ujenzi katika Block B umefikia asilimia 27.

Shughuli nyingine zilizotekelezwa ni: Kukamilika kwa ujenzi wa karakana ya TEMESA katika Mkoa wa Simiyu Awamu ya I na ukarabati wa karakana za Vingunguti na MT Depot Awamu ya I; kuendelea na ukarabati wa karakana za TEMESA mikoa ya Mwanza, Tabora, Kigoma, Mara, Arusha na Mtwara; kukamilika kwa usanifu na usakinishaji (installing) wa Mfumo wa Usimamizi na Ufuatiliaji wa Matengenezo ya Magari, Umeme na Elektroniki na kuanza kwa majaribio ya mfumo katika mikoa ya Iringa, Dodoma na Dar es Salaam; kuendelea na usanifu wa ukarabati wa karakana ya Kisasa katika Mkoa wa Dodoma. Jumla ya shilingi bilioni 17.32 zimetumika katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023.

 

(d)         Mradi Na. 6580: Mradi wa Uendelezaji wa Jiji la Dar es Salaam (DMDP)

Hatua iliyofikiwa ni: Ukamilishaji wa ujenzi wa barabara zenye urefu wa kilomita 5.3 kwa kiwango cha lami; ukamilishaji wa ujenzi wa mitaro ya maji ya mvua kilomita 1.8; na maandalizi ya uendelezaji wa Bonde la Mto Msimbazi. Jumla ya shilingi bilioni

71.38 zimetumika katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023.

 

C.          Usafiri Majini

 

(i)           Mradi Na. 4295: Ujenzi na Ukarabati wa Meli

Hatua zilizofikiwa ni: Kuendelea na ujenzi wa Meli ya MV Mwanza Hapa Kazi Tu umefikia asilimia 83; kuendelea na ukarabati wa meli ya MV Umoja umefikia asilimia 75.8; kuendelea na ukarabati wa meli ya MT Sangara umefikia asilimia 90.7; Kukamilisha taratibu za kupata Mkandarasi ili kuwezesha kusaini mkataba  wa ujenzi wa meli mpya tatu (3) pamoja na chelezo ambapo meli mbili (2) zitajengwa katika Ziwa Tanganyika, meli moja (1) itajengwa katika Ziwa Victoria na Chelezo itajengwa Ziwa Tanganyika. Jumla ya shilingi bilioni 23.19 zimetumika katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023.

 

(ii)         Mradi Na. 4201: Uboreshaji wa Usalama wa Usafiri katika Ziwa Victoria

Hatua zilizofikiwa ni; Kuendelea na taratibu za kumpata Mkandarasi kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha Uratibu wa Masuala ya Utafutaji na Uokozi katika Ziwa Victoria (Maritime Rescue Cordination Centre-MRCC, Mwanza; Kukamilisha ununuzi wa mkandarasi kwa ajili ya ujenzi wa Vituo vidogo vitatu (3) vya utafutaji na Uokozi (Search and Rescue- SARs) katika Ziwa Victoria kwenye eneo la Kanyara-Geita, Ukerewe na Musoma; na Kumpata mzabuni kwa ajili ununuzi wa Boti moja (1) ya matibabu (Ambulance Boat) na boti mbili (2) za Utafutaji na Uokozi. Jumla ya shilingi milioni 751.63 zimetumika katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023.

 

 

 

(iii)       Vivuko

(a)         Mradi Na. 4125: Ujenzi wa Maegesho ya Vivuko

Hatua iliyofikiwa ni: Kukamilika kwa upanuzi wa jengo la abiria katika maegesho ya Magogoni – Kigamboni upande wa Kigamboni Jijini Dar es Salaam; kukamilika kwa ujenzi na ukarabati wa maegesho katika vituo sita (6) vya Magogoni – Kigamboni, Kilambo - Namoto, Utete-Mkongo, Iramba – Majita, Nyakaliro – Kome na Kasharu – Buganguzi; kukamilika kwa ujenzi wa miundombinu ya majengo ya kusubiria abiria, ofisi na fensi katika vituo vya Bugolora – Ukara; kuendelea na ujenzi wa miundombinu ya jengo la abiria na ofisi na uzio katika eneo la Kinesi (Mwigobero) ambapo utekelezaji umefikia asilimia 20 na vituo vya Nyakarilo – Kome na Kisorya – Rugezi vipo kwenye hatua za manunuzi; ujenzi wa maegesho ya Mayenzi – Kanyinya umefikia asilimia 50 ya utekelezaji na maegesho ya Muleba – Ikuza yapo kwenye hatua za manunuzi; ujenzi wa maegesho mapya ya Ijinga – Kahangala (Magu) umefikia asilimia 40 na Bwiro – Bukondo (Ukerewe) umefikia asilimia 80. Jumla ya shilingi milioni 696.17 zimetumika katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023.

 

(b)         Mradi Na. 4139: Ujenzi wa Vivuko Vipya

Hatua iliyofikiwa ni: Kuendelea na ujenzi wa kivuko kipya cha Kisorya – Rugezi ambapo ujenzi umefikia asilimia 57; ujenzi wa vivuko vya  Ijinga – Kahangala (Magu), Bwiro – Bukondo (Ukerewe), Nyakarilo – Kome (Buchosa) umefikia asilimia 35. Aidha, maandalizi ya kuanza ujenzi wa kivuko kipya cha pili kitakachotoa huduma kati  ya Nyamisati – Mafia (Pwani) yanaendelea na taratibu za kumpata Makandarasi wa ujenzi wa vivuko vipya vya Bayugu - Mbalika zimekamilika. Vile vile, ununuzi wa kivuko kipya cha Magogoni - Kigamboni upo kwenye hatua za mwisho za manunuzi. Jumla ya shilingi bilioni 9.41 zimetumika katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023.

 

(c)         Mradi Na. 4144: Ukarabati wa Vivuko

Hatua iliyofikiwa: Kukamilika kwa Ukarabati wa vivuko vya MV Musoma, MV Kazi, MV TEMESA na MV Tanga; na kuendelea na ukarabati wa vivuko vya MV Misungwi ambapo utekelezaji umefikia asilimia 95, MV Nyerere (asilimia 70), MV Kilombero (asilimia 75), MV Ujenzi (asilimia 68), MV Kitunda (asilimia 30),  MV Kyanyabasa (asilimia 30) na ukarabati wa kivuko cha MV Magogoni umeanza. Jumla ya shilingi bilioni 3.83 zimetumika katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023.

 

D.          Bandari

(a)        Mradi Na. 4227: Uboreshaji wa Bandari ya Dar es Salaam 

 

(i)           Bandari ya Dar es Salaam

Hatua iliyofikiwa ni: Kuendelea na awamu ya pili ya utekelezaji wa mradi ambapo shughuli zilizotekelezwa ni: Kuchimba na kupanua lango la kuingilia meli na eneo la kugeuzia meli hadi kufikia kina cha mita 15.5 ambapo utekelezaji umefikia asilimia 96; na kuendelea na ununuzi wa wakandarasi kwa ajili ya kuanza ujenzi wa kuongeza kina kutoka mita 12 hadi kufikia mita 14.5; na kuanza kwa ukarabati Gati Na. 8 – 11. Jumla ya shilingi bilioni 48.83 zimetumika katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023.

 

(ii)         Bandari ya Tanga

Hatua iliyofikiwa ni: Uboreshaji wa Bandari ya Tanga gati namba 1 na 2 umefikia asilimia 99. Jumla ya shilingi bilioni 181.38 zimetumika katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023.

 

(iii)       Bandari Kavu katika Eneo la Ruvu

Hatua iliyofikiwa ni: Kukamilika kwa ujenzi wa mkongo wa Taifa, nyumba za makazi, ofisi na ufungaji wa umeme; kuendelea na ujenzi wa yadi na sakafu ngumu (pavement) yenye ukubwa wa hekta tano (5) kwa ajili ya kuhifadhi shehena za mizigo ambapo umefikia asilimia 90; na kuendelea na ujenzi wa barabara ya zege yenye urefu wa kilomita 15.5 kutoka barabara kuu ya Morogoro hadi Vigwaza/Kwala ambapo umefikia asilimia 99. Jumla ya shilingi bilioni 48.84 zimetumika katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023.

 

(b)        Bandari za Maziwa Makuu 

 

(i)           Ziwa Victoria

Hatua iliyofikiwa ni: Kuendelea na maandalizi ya awali ya ujenzi wa  Bandari za Bukoba na Kemondo Bay; kuendelea na hatua za ununuzi wa Mkandarasi kwa ajili ya ujenzi wa Bandari ya Mwanza South; na kuendelea na hatua za mwisho za kufanya Usanifu wa Kina (Detailed Engineering Design) kwa ajili ya ujenzi wa Mwanza North ikijumuisha miundombinu ya Reli (SGR). Jumla ya shilingi bilioni 3.96 zimetumika katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023.

 

(ii)         Ziwa Tanganyika

Hatua iliyofikiwa ni: Kukamilika kwa ujenzi wa Gati katika Bandari mpya ya Karema; kuendelea na usanifu wa ujenzi wa Passenger Lounge na ukuta wa mizigo wa  Lighter Quay katika Bandari ya Kibirizi na gati la Bandari ya  Ujiji ambapo utekelezaji umefikia asilimia 69; na kukamilika kwa ujenzi wa Ofisi ya Mkuu wa Bandari ya Kigoma. Jumla ya shilingi bilioni 17.5 zimetumika katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023.

 

(iii)       Ziwa Nyasa

Hatua iliyofikiwa ni: Kukamilika kwa ujenzi wa sakafu ngumu katika bandari ya Kiwira na Itungi; kuendelea na ujenzi wa sehemu ya kuegesha meli (ramp) katika bandari ya Kiwira; na kukamilika kwa ujenzi wa sehemu ya kuegesha meli katika bandari ya Ndumbi. Jumla ya shilingi milioni 200 zimetumika katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023.

 

E.          Usafiri wa Anga

 

(a)        Mradi Na. 6267: Institutional Support

 

(i)           Uendeshaji wa Jengo la Tatu la Abiria (JNIA TB III) na Kuboresha

Huduma katika Viwanja vya Ndege  

Hatua iliyofikiwa ni: Kuendelea na uboreshaji wa uzio katika Kiwanja cha Dodoma ambapo utekelezaji umefikia asilimia 75; kazi ya usimikaji wa mfumo wa taa za kuongozea ndege katika kiwanja cha ndege cha Dodoma ilifikia asilimia 40; kuendelea na manunuzi ya gari la Zimamoto; kukamilika kwa uboreshaji wa uzio wa Kiwanja cha Ndege cha Julius Nyerere pamoja na kufunga mfumo ya ufuatiliaji mienendo ya shughuli za kiusalama na uendeshaji (CCTV) katika eneo linalozunguka barabara ya kutua na kuruka ndege katika kiwanja; na kukamilisha ulipaji wa malipo ya fidia kwa wakazi waliopisha upanuzi wa kiwanja cha Ndege cha Dodoma. Jumla ya shilingi bilioni 22.68 zimetumika katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023.

 

(ii)         Mradi wa Ununuzi na Ufungaji wa Rada Nne (4) za Kuongoza Ndege za Kiraia JNIA, KIA, Mwanza na Songwe

Hatua iliyofikiwa ni: Kukamilika kwa ufungwaji wa rada nne (4) za kuongoza ndege za kiraia katika viwanja vya ndege vya Julius Nyerere, Kilimanjaro, Songwe na Mwanza. Jumla ya shilingi bilioni 10.35 zimetumika katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023.

 

(b)         Mradi Na. 4290: Ununuzi wa Rada, Vifaa na Ujenzi wa Miundombinu ya Hali ya Hewa

Hatua iliyofikiwa ni: Kukamilika kwa matengenezo ya rada mbili (2) za hali ya hewa zitakazofungwa katika mikoa ya Mbeya na Kigoma; kuendelea na utengenezaji wa rada mbili (2) zitakazofungwa katika mikoa ya Kilimanjaro na Dodoma ambapo utekelezaji umefikia asilimia 75; kukamilika kwa ununuzi na ufungaji wa vifaa mbalimbali vya hali ya hewa ikiwemo seti tano (5) za vifaa vya utambuzi wa matukio ya radi vilivyofungwa Musoma, Mwanza, Bukoba, Tabora na Kibondo pamoja na vifaa vya kupima hali joto ilivyofungwa katika Kituo cha hali ya hewa kilichopo Singida; kukamilika kwa ununuzi na ufungaji wa  kompyuta maalum “Cluster Computer” yenye uwezo mkubwa wa kuchakata taarifa za hali ya hewa iliyofungwa katika Kiwanja cha Ndege cha Julius Nyerere (JNIA); kukamilika kwa ukarabati wa ofisi ya hali ya hewa na nyumba tatu (3) za wafanyakazi zilizopo Mahenge; na kuendelea na ukarabati wa ofisi ya hali ya hewa katika Kiwanja cha Ndege cha Songea. Jumla ya shilingi bilioni 6.17 zimetumika katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023.

 

(c)         Mradi Na. 6377: Kuboresha Miundombinu na Ununuzi wa Vifaa vya Kufundishia 

(i)           Chuo cha Taifa cha Usafirishaji - NIT 

Hatua iliyofikiwa ni: Kusainiwa kwa mkataba kwa ajili ya ununuzi wa vifaa maalum (Full Motion Cabin Crew Mock-up and Fixed Cabin Crew Mock-up) vya mafunzo kwa Wahudumu ndani ya ndege; kuendelea na ujenzi wa majengo nane (8) kwa ajili ya madarasa, maabara, karakana na ofisi za watumishi ambapo majengo matano (5) yanajengwa katika kampasi ya Mabibo – Dar es salaam na majengo matatu (3) katika Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Kilimanjaro; kununuliwa kwa  Aircraft Engineering System Trainers (runnerable turbo jet engine na motorised cutway piston engine) na Virtual Maintenance Trainer (VMT) for Boeing 737-800 kwa ajili ya mafunzo ya Wahandisi wa Matengenezo ya Ndege. Jumla ya shilingi bilioni 2.50 zimetumika katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023.

 

(ii)         Chuo cha Bahari Dar es Salaam - DMI  

Hatua iliyofikiwa ni: Kuendelea kufanya  sehemu ya malipo kwa ajili ya kununua mtambo (full mission crane simulator) wa kufundishia kwa ajili ya kuongeza ubora na umahiri katika kuhudumia mizigo kwenye meli na vyombo vingine vya usafirishaji. Jumla ya shilingi milioni 275.41 zimetumika  katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023.

 

(d)         Mradi Na. 4209: Kiwanja cha Ndege cha Mwanza

Hatua iliyofikiwa ni: Kukamilika kwa upanuzi wa maegesho ya ndege, uzio wa kiwanja, maegesho ya magari; na kukamilika kwa usanifu wa jengo la abiria. Jumla ya shilingi milioni 27.5 zimetumika katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023.

 

(e)         Mradi Na. 4220: Kiwanja cha Ndege cha Mtwara

Hatua iliyofikiwa ni kukamilika kwa kazi ya upanuzi na ukarabati kwa awamu ya kwanza na mradi upo katika kipindi cha uangalizi. Jumla ya shilingi bilioni 6.05 zimetumika katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023.

(f)          Mradi Na. 4206: Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa Songwe

Hatua iliyofikiwa ni: Kukamilka kwa ukarabati wa tabaka la juu la barabara ya kutua na kuruka ndege, ufungaji wa taa za kuongozea ndege na ujenzi wa uzio wa usalama; kukamilika kwa ukarabati wa eneo la usalama kwenye barabara ya kutua na kuruka ndege na usimikaji wa taa; na kuendelea kukamilisha jengo jipya la abiria pamoja na ufungaji wa mifumo na vifaa vyake ambapo utekelezaji umefikia asilimia 98. Jumla ya shilingi bilioni 4.66 zimetumika katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023.

 

(g)         Mradi Na. 4226: Viwanja vya Ndege vya Mikoa

Hatua iliyofikiwa ni: Kukamilika kwa upanuzi wa njia ya kutua na kuruka ndege, kufungwa kwa mfumo wa kuongozea ndege katika kiwanja cha Ndege Dodoma; kukamilika kwa ujenzi wa barabara ya kutua na kuruka ndege katika kiwanja cha Ndege cha Geita; kukamilika kwa  kazi za upanuzi na ukarabati wa Kiwanja cha Ndege cha Songea na ukarabati wa barabara ya kutua na kuruka ndege kwa kiwango cha changarawe katika kiwanja cha Nachingwea; kukamilika kwa ulipaji wa fidia kwa wananchi waliopisha ujenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Lake Manyara na Tanga; kuendelea na ukarabati wa njia ya kuruka na kutua ndege kwa kiwango cha lami katika kiwanja cha ndege Lindi; na kuendelea na ujenzi na ukarabati wa viwanja vya Ndege vya Iringa (asilimia 50), Musoma (asilimia 47) na Moshi (asilimia 22). Jumla ya shilingi bilioni 18.53 zimetumika katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023.  

 

(h)         Mradi Na. 4286: Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Msalato

Hatua iliyofikiwa ni: Kuendelea na ujenzi awamu ya kwanza inayohusisha ujenzi wa  barabara ya kutua na kuruka ndege, barabara ya viungio, maegesho ya ndege, pamoja na usimikaji wa taa za usalama na kuongozea ndege  ambapo utekelezaji umefikia asilimia 18. Aidha, kwa upande wa awamu ya pili inayohusisha ujenzi wa Jengo la Abiria, Jengo la kuongozea Ndege, Kituo cha Zimamoto, Kituo cha Hali ya Hewa na Vituo vidogo nane (8) vya kufua umeme utekelezaji umefikia asilimia 2. Jumla ya shilingi bilioni 51.44 zimetumika katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023.

  

(i)           Mradi Na. 4221: Kiwanja cha Ndege cha Sumbawanga

Hatua iliyofikiwa ni: Kuendelea na maandalizi ya kuanza ujenzi wa barabara ya kutua na kuruka ndege na viungio vyake, maegesho ya ndege, jengo la abiria, jengo la kuongozea ndege, jengo la uchunguzi wa hali ya hewa, barabara ya kuingia na kutoka kiwanjani na maegesho ya magari pamoja na ufungaji wa taa na mitambo ya kuongozea ndege ambapo kwa sasa taratibu za kusaini Mkataba na Mkandarasi mpya zinaendelea. Jumla ya shilingi milioni 29.14 zimetumika katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023.

 

(j)          Mradi Na. 4222: Kiwanja cha Ndege cha Shinyanga

Hatua iliyofikiwa ni: Kuendelea na maandalizi ya kuanza ujenzi wa barabara ya kutua na kuruka ndege na viungio vyake, maegesho ya ndege, jengo la abiria, jengo la kuongozea ndege, jengo la uchunguzi wa hali ya hewa, barabara ya kuingia na kutoka kiwanjani na maegesho ya magari pamoja na ufungaji wa taa na mitambo ya kuongozea ndege ambapo utekelezaji umeanza na mradi upo katika hatua za maandalizi (Mobilization). Jumla ya shilingi milioni 29.04 zimetumika katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023.

 

(k)         Mradi Na. 4159: Kiwanja cha Ndege cha Tabora

Hatua iliyofikiwa ni: Kuendelea na maandalizi ya ujenzi wa barabara ya kuruka na kutua ndege, jengo jipya la abiria, barabara ya kuingia na kutoka kiwanjani, maegesho ya magari, barabara ya kiungio na jengo la uchunguzi wa hali ya hewa ambapo utekelezaji umeanza na mradi upo katika hatua za maandalizi (Mobilization). Jumla ya shilingi milioni 16.94 zimetumika katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023.

 

F.           Nishati

 

Miradi ya Kufua umeme

 

(i)           Mradi Na. 3164: Kinyerezi I Extension (MW 185)

Hatua iliyofikiwa ni: Kukamilika kwa ufungaji wa mitambo mitambo minne (4) yenye uwezo wa kuzalisha Megawati 185 na mitambo hiyo kuwashwa na umeme unaozalishwa kuingizwa katika Gridi ya Taifa. Jumla ya shilingi bilioni 52.18 zimetumika katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023.

 

(ii)         Mradi Na. 3169: Kufua Umeme wa Maji Rusumo (MW 80)

Hatua iliyofikiwa ni: Kukamilika kwa ujenzi wa bwawa, handaki la kupitishia maji, kituo cha kupoza na kuchochea umeme (switchyard), jengo la utawala na nyumba 24 za kudumu; kuendelea na ujenzi wa jengo la mitambo ambapo utekelezaji umefikia asilimia 98.89 na ufungaji wa mitambo ya kufua umeme asilimia 97. Kwa ujumla mradi umefikia asilimia 99. Jumla ya shilingi bilioni 15.71 zimetumika katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023.

 

Miradi ya Usafirishaji na Usambazaji wa Umeme

(i)           Mradi Na. 3111: Uimarishaji wa Gridi ya Taifa (National Grid Stabilization)

Hatua  iliyofikiwa  ni:  Kuunganishwa kwa Mkoa wa Kigoma pamoja na Wilaya za Ngara na Biharamulo katika gridi ya Taifa kutokea kituo cha Nyakanazi; kuendelea na ujenzi wa njia ya msongo wa kV 132 kutoka Tabora hadi Katavi; na kuwapata Wakandarasi kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya kuimarisha miundombinu ya umeme katika mikoa mbalimbali nchini. Jumla ya shilingi bilioni 88.06 zimetumika katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023.

 

(ii)         Njia ya Kusafirisha Umeme wa Msongo wa kV 220 (Rusumo – Nyakanazi)

Hatua iliyofikiwa ni: Kukamilika kwa malipo ya fidia kwa wananchi wanaopisha eneo la mradi; kukamilika kwa usimikaji wa nguzo na uunganishaji wa nyaya za umeme; na kukamilika kwa ujenzi wa kituo cha kupoza umeme cha Nyakanazi. Kwa ujumla utekelezaji wa mradi umekamilika. Jumla ya shilingi  bilioni 6.94 zimetumika katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023.

 

 

(iii)       Mradi Na. 3175: Njia ya Kusafirisha Umeme wa Msongo wa kV 400 kutoka Singida - Arusha – Namanga

Hatua iliyofikiwa ni: Kukamilika kwa ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme kutoka Singida hadi Arusha; kuendelea na ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme kutoka Arusha hadi Namanga; na kuendelea na ujenzi wa kituo cha kupoza  umeme  cha  Lemugur katika eneo la Kisongo mkoani Arusha.  Kwa ujumla utekelezaji wa mradi  umefikia  asilimia  95. Jumla  ya shilingi bilioni 5.96 zimetumika katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023.

 

(iv)       Mradi Na. 3179: Mradi wa Njia ya Kusafirisha Umeme Msongo wa kV 400 kutoka Rufiji – Chalinze – Kinyerezi - Dodoma

Awamu ya kwanza (Rufiji - Chalinze): Hatua iliyofikiwa ni: Ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme imefikia asilimia 93.5 na kituo cha kupoza umeme asilimia 64. Jumla ya shilingi bilioni 89.41 zimetumika katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023.

 

Awamu ya pili (Chalinze – Dodoma na Chalinze - Kinyerezi): Hatua iliyofikiwa ni: Kuendelea kulipa fidia wananchi wanaopisha mradi kati ya Kinyerezi – Chalinze na Chalinze - Dodoma; na kukamilika kwa tathmini ya Athari za mradi kwa Mazingira na Jamii pamoja na upembuzi yakinifu. Jumla ya shilingi bilioni 9.42 zimetumika katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023.

 

(v)         Mradi Na. 3166: Njia ya Kusafirisha Umeme wa Msongo wa kV 400 - North West Grid Extension (Iringa – Mbeya - Sumbawanga –

Mpanda - Kigoma – Nyakanazi)

 

Awamu ya Kwanza: Iringa – Mbeya – Tunduma – Sumbawanga (TAZA):

Hatua iliyofikiwa ni: Kukamilika kwa taarifa za tathmini (evaluation reports) za zabuni za Wakandarasi Wajenzi wa mradi ambapo taratibu za kupata kibali (No Objection) kutoka kwa Wafadhili zinaendelea; na kuendelea na ulipaji wa fidia kwa wananchi 6,500 wanaopisha mradi ambapo wananchi 4,750 wamelipwa. Jumla ya shilingi bilioni 16.43 zimetumika kulipa fidia hiyo kwa kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023.

 

Awamu ya Pili:Kigoma hadi Nyakanazi: 

Hatua iliyofikiwa ni: Kukamilika kwa asilimia 90 ya ulipaji wa fidia katika eneo la Kidahwe na eneo la mkuza wa njia ya usafirishaji umeme; kukamilika kwa ununuzi wa vifaa vya ujenzi wa miundombinu ya kusambaza umeme; kuendelea na ujenzi wa njia ya kusafirishia umeme ambao umefikia asilimia 53; kuendelea na taratibu za kuwapata wakandarasi wa vituo vya kupoza umeme vya Nyakanazi na Kidahwe pamoja na njia za usambazaji umeme. Jumla ya shilingi bilioni 6.93 zimetumika katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023.

 

(vi)       Mradi Na. 3113: Usambazaji wa Nishati Vijijini

Hatua iliyofikiwa ni: Kuunganishwa kwa jumla ya vijiji 10,127 kati ya vijiji 12,318 vya Tanzania Bara sawa na asilimia 82.21. Jumla ya shilingi bilioni 202.51 zimetumika katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023.

 

Miradi ya Usambazaji wa Gesi Asilia 

(i) Mradi Na. 3162: Usambazaji wa Gesi Asilia Mikoa ya Dar es Salaam, Mtwara, Lindi na Pwani 

Hatua iliyofikiwa ni: Kukamilika usanifu wa mradi; kukamilika Tathmini ya Athari kwa Mazingira; kupatikana kwa Mkandarasi wa ujenzi; kuendelea na ujenzi wa vituo viwili (2) vya CNG, kimoja maeneo ya uwanja wa Ndege mkabala na Terminal III na kingine katika uwanja wa Posta uliopo barabara ya Sam Nujoma mkoani Dar es Salaam; kuendelea na ujenzi wa bomba la usambazaji wa gesi asilia lenye urefu wa kilomita 12.4 kutoka Mwenge hadi Mbezi Beach kupitia barabara ya Bagamoyo ambapo hadi kufikia mwezi Aprili, 2023 umefikia asilimia 44.2; kuendelea na ujenzi wa bomba la kusambaza gesi katika maeneo ya Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam (DUCE) na Mlimani City. Kupitia mradi huu, migahawa mitatu (3) na maabara moja (1) katika chuo cha DUCE pamoja na migahawa 12 iliyopo Mlimani City Mall itaunganishwa ambapo kwa sasa taratibu za kumpata Mkandarasi wa ujenzi zinaendelea; kuendelea na ujenzi wa bomba la gesi asilia kutoka valvu namba tatu (BVS 3) kuelekea Kata za Mnazi Mmoja na Mingoyo mkoani Lindi ambapo utekelezaji umefikia asilimia 60. Aidha, kukamilika kwa bomba hili kutawezesha nyumba 209 za awali zilizounganishwa na miundombinu ya gesi asilia kutumia gesi hiyo.Jumla ya shilingi bilioni 8.89 zimetumika katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023.

 

2.3.2.2.  Kuimarisha Miundombinu na Mifumo ya Kitaasisi 

 

A.          Kuimarisha Shughuli za Mfuko wa Bunge

 

(i)           Mradi Na. 6360: Ujenzi wa Miundombinu ya Bunge

Hatua iliyofikiwa ni: kuendelea ujenzi wa nyumba mbili (2) katika eneo la Kilimani , ambapo hatua ya utekelezaji umefi6103kia asilimia 78.05; kukamilika kwa tathmini ya mahitaji ya mitambo kwa ajili ya ulinzi na usalama na malipo ya awali yamefanyika; na kukamilika kwa ujenzi wa makazi ya Katibu wa Bunge (kilimani – Dodoma). Jumla ya shilingi bilioni 2.54 zimetumika katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023

 

(ii)         Mradi Na. 6318: Ukarabati wa Majengo ya Ofisi 

Hatua iliyofikiwa ni kukamilika kwa ukarabati wa jengo la utawala, ukumbi wa Msekwa, ununuzi na ufungwaji wa vipuri vya mtambo wa kupooza hewa katika ukumbi wa Bunge; na kukamilika kwa ukarabati wa kumbi mbili za Bunge na uzio kwa ajili ya usalama. Jumla ya shilingi milioni 388  katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023.

 

B.          Kuimarisha Uwazi na Uwajibikaji katika Utumishi wa Umma

 

Utumishi wa Umma na Utawala Bora

(i)           Mradi Na. 6315: Ujenzi wa Makazi ya Viongozi Wakuu Wastaafu wa

Kitaifa 

Hatua iliyofikiwa ni: Kuendelea na ujenzi wa nyumba ya makazi ya Rais  wa Awamu ya Tano Hayati Dkt. John P. Magufuli ambapo utekelezaji umefikia asilimia 99; kuendelea na ukarabati wa nyumba ya makazi ya Rais wa Awamu ya Kwanza Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius K. Nyerere ambapo utekelezaji umefikia asilimia 58; na kuendelea na ujenzi wa Klabu ya Viongozi - Makao Makuu eneo la Nzuguni ambapo ujenzi umefikia asilimia 65. Jumla ya shilingi bilioni 4.44 zimetumika katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023.

 

(ii)         Mradi Na. 6284: Programu ya Maboresho katika Utumishi wa Umma Awamu ya Tatu 

Hatua iliyofikiwa ni: Kukamilika kwa ujenzi wa Mfumo wa Taarifa za Kiutumishi na Mishahara (HCMIS) na kuboreshwa kwa moduli ya Watumishi Portal yenye huduma za kielektroniki za uhamisho wa watumishi, mikopo ya watumishi, taarifa binafsi za mtumishi na hati ya malipo ya mishahara; na kuibuliwa na kuboreshwa kwa mifumo mipya ikiwemo mifumo ya e-Mrejesho, e-Mikutano, e-Rufaa, e-Dodoso pamoja na Shared Helpdesk. Jumla ya shilingi bilioni 3.02 zimetumika katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023.

 

C.          Mfuko wa Mahakama

 

(i)           Mradi Na. 6310: Ujenzi na Ukarabati wa Majengo ya Mahakama za Wilaya

Hatua iliyofikiwa ni: Kukamilika kwa ujenzi wa Mahakama ya wilaya ya Manyoni; na kuendelea na ujenzi wa  Mahakama za wilaya za Liwale ambapo utekelezaji umefikia asilimia 70, Kwimba (asilimia 80), na Ulanga (asilimia 35). Jumla ya shilingi bilioni 3.8 zimetumika katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili 2023.

 

(ii)         Mradi Na. 6327: Ujenzi na Ukarabati wa Majengo ya Serikali Hatua iliyofikiwa ni: Kuendelea na ujenzi wa nyumba ya Jaji Mkuu ambapo utekelezaji umefikia asilimia 35; na ujenzi wa jengo la ghorofa sita kwa ajili ya makazi ya Majaji jijini Dodoma ambapo utekelezaji umefikia asilimia 54. Jumla ya shilingi billioni 2.6 zimetumika katika kipindi Julai, 2022 hadi Aprili, 2023.

 

 

(iii)       Mradi Na. 6312: Ujenzi na Ukarabati wa Majengo ya Mahakama za Mwanzo

Hatua iliyofikiwa ni: Kuendelea na ujenzi wa Mahakama za Mwanzo tisa (9) ambapo Mahakama ya Mwanzo Madale (Dar es Salaam) utekelezaji umefikia asilimia 85, Kinesi - Rorya (asilimia 99), Mahenge - Kilolo (asilimia 97), Luilo – Ludewa (asilimia

95), Newala – Newala (asilimia 75) na Usevya – Mlele (asilimia 95); Nyakibimbili - 

Bukoba (asilimia 90), Kabanga – Ngara (asilimia 80) na  Mlimba na Mang’ula – Morogoro (asilimia 85). Jumla ya shilingi bilioni 3.0 zimetumika katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili 2023.

 

(iv)       Mradi Na. 6314: Ujenzi na Ukarabati wa Majengo ya Mahakama Kuu

Hatua iliyofikiwa ni kukamilika kwa ukarabati wa jengo la Mahakama Kuu Tabora na Mahakama Kuu Divisheni ya Kazi. Jumla ya shilingi milioni 370 zimetumika katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili 2023.

 

(v)         Mradi Na. 6215: Mradi wa Uboreshaji wa Huduma za Mahakama (Citizen Centric Judiciary Modernisation Project)

Hatua iliyofikiwa ni kukamilika kwa ujenzi wa Mahakama za wilaya 18 za Kyerwa na Misenyi (Kagera), Mbogwe na Nyang’wale (Geita), Itilima na Busega  (Simiyu), Gairo, Mvomero na Kilombero (Morogoro), Kakonko, Buhingwe na Uvinza (Kigoma), Butiama na Rorya (Mara), Songwe (Songwe), Tanganyika (Katavi), Kaliua (Tabora) na Mkinga (Tanga). Jumla ya shilingi bilioni 17.5 zimetumika katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili 2023.

 

D.          Utawala Bora na Utawala wa Sheria

(a)         Mradi Na. 5501: Kuimarisha Upatikanaji wa Haki za Binadamu

Hatua iliyofikiwa ni: Kuwajengea uwezo watumishi 45 kutoka katika Wizara na Taasisi za Serikali kuhusu uratibu na utoaji wa taarifa za utekelezaji wa mikataba ya kulinda, kuhifadhi na kuendeleza haki za binadamu nchini; na kuandaa rasimu ya mpango kazi wa pili wa kitaifa wa kulinda haki za binadamu nchini kwa kupata maoni ya pande zote mbili za Muungano wa Tanzania. Jumla ya shilingi milioni 78 zimetumika katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023.

 

(b)         Mradi Na. 5502: Mpango Kazi Endelevu wa Kupambana na Rushwa  Hatua iliyofikiwa ni: Kuandaa rufaa za viashiria vya rushwa na kuviwasilisha TAKUKURU; kukamilisha kushughulikia mashauri 15 ya rushwa kubwa katika mahakama ya rushwa na uhujumu uchumi; kufanya mapitio ya majalada 55 ya kesi za rushwa kwa ajili kuwajengea uwezo Wakuu wa Mashtaka wa Mikoa mitano (5) ya Dar es Salaam, Dodoma, Arusha, Mbeya na Mwanza ya Programu ya Kujenga mfumo Endelevu wa Kupambana na Rushwa Tanzania. Jumla ya shilingi bilioni 1.2 zimetumika katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023.

(c)         Mradi Na. 5507: Upatikanaji wa Haki za Wanawake na Watoto wa Kike  

Hatua iliyofikiwa ni: Kuratibu kikao kazi cha wadau wanaotekeleza Eneo Na. 5 la MTAKUWWA la Usimamizi na Utekelezaji wa Sheria ili kuimarisha ulinzi na usalama wa wanawake na Watoto; na Kuzindua Kampeni ya Huduma ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia “Mama Samia Legal Aid Campaign” (2023/24- 2025/26) pamoja na mkakati wake wa utekelezaji inayolenga kutoa elimu ya kisheria, mirathi, ndoa, na taratibu za upatikanaji wa haki na wajibu kwa mujibu wa sheria na katiba ya nchi. Jumla ya Shilingi milioni 135 zilitumika katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023.

 

(d)         Mradi Na. 5508: Upatikanaji wa Haki kwa Maendeleo Endelevu

Hatua iliyofikiwa ni: Kukamilika kwa maandalizi ya mahitaji ya mfumo wa kubadilishana taarifa miongoni mwa Taasisi za Haki Jinai;  na kukamilika kwa andiko la kutungwa kwa Sera ya Adhabu. Jumla ya shilingi milioni 967 zimetumika katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023.

 

(e)         Mradi Na. 6201: Haki Mtandao 

Hatua iliyofikiwa ni: Kuwajengea uwezo washiriki 65 ambao ni Watoa Huduma za Msaada wa Kisheria, Wasaidizi wa Kisheria, Wasajili Wasaidizi, na Madawati ya Huduma za Kisheria kwenye Magereza na Polisi; na kukamilisha mpango wa mawasiliano ya huduma zinazotolewa na Wizara kwa  wananchi. Jumla ya shilingi milioni 225 zimetumika katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023.

 

(f)          Mradi Na. 6207: Kuboresha Uwajibikaji wa Kitaasisi katika Kupambana na Rushwa na Kuongeza wigo wa kuifikia Haki 

Hatua iliyofikiwa ni: kufanyika kwa ukaguzi kwa Taasisi 34 za Watoa Huduma ya Msaada wa Kisheria kutoka wilaya 27 za mikoa tisa (9) ya Tanzania Bara; Kufanya maadhimisho ya Wiki ya Msaada wa Kisheria Mkoa wa Kigoma ambapo wananchi 4,150 (wanaume 1,617, wanawake 2,416 na watoto 117) walipatiwa huduma ya msaada wa kisheria; na kutoa huduma ya msaada wa kisheria kwa mahabusu na wafungwa kwa njia ya huduma ya msadaa wa kisheria inayotolewa na mawakili bila malipo (Pro Bono) katika magereza ya Segerea na ukonga ambapo jumla ya wafungwa 56 walipatiwa huduma ikiwemo wanawake 23 na Watoto 33. Jumla ya shilingi milioni 400 zimetumika katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023.

 

(g)         Mradi Na. 6517: Haki ya Mtoto

Hatua iliyofikiwa ni: Kuandaa taarifa ya utekelezaji wa Mkakati wa Pili wa Haki Mtoto na kuwasilisha kwenye kikao cha Jukwaa la Haki Mtoto; kukamilisha kukusanya maoni ya wananchi kuhusu  maboresho ya Sheria ya Ndoa ya mwaka 1971 na  kuandaa marekebisho ya Sheria husika; kusajili jumla ya watoto 319,624 wenye umri chini ya miaka mitano katika mikoa 23 ya Tanzania Bara inayotekeleza mpango huo; Kukamilisha kuboresha mfumo wa utoaji Haki – Jinai kwa Watoto; kufanya ukaguzi wa watoto wanaokinzana na sheria katika mikoa 26 ya Tanzania Bara na mikoa mitatu (3) ya Kimashtaka ambayo ni Temeke, Kinondoni na Ilala. Jumla ya shilingi bilioni 5.2  zimetumika katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023.

 

(h)         Mradi Na. 6389: Ujenzi wa Majengo ya Ofisi  

 

(i)           Mradi wa Ujenzi wa Majengo ya Ofisi ya Taifa ya Mashtaka

Hatua iliyofikiwa ni: kuendelea na ujenzi wa majengo ya Huduma Jumuishi  za Sheria yanayojengwa na Ofisi ya Taifa ya Mashtaka katika mikoa ya Kimashtaka ya Morogoro (asilimia 75), Ilala (Kinyerezi) (asilimia 98),  Pwani (asilimia 98) na  Mbeya (asilimia 75), Shinyanga (asilimia 35), Manyara (asilimia 35), Njombe (asilimia 10), Katavi (asilimia 10) na Rukwa (asilimia 15). Jumla ya shilingi bilioni 5.56 zimetumika katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023.

 

(ii)      Mradi wa Ujenzi wa Majengo ya Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa

Serikali

Hatua iliyofikiwa ni: kuendelea na ujenzi wa jengo la Huduma Jumuishi za Sheria la  Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali Jijini Mwanza (asilimia 45); Jumla ya shilingi milioni 733.9 zimetumika katika Julai, hadi Aprili, 2023.

 

(iii)    Ujenzi wa Mji wa Serikali Mtumba - Dodoma

Hatua iliyofikiwa katika ujenzi wa majengo ya Serikali ni: Kuendelea na Awamu ya Pili ya ujenzi wa majengo ya Wizara katika mji wa Serikali Mtumba ambapo ujenzi wa majengo 24 umefikia wastani wa asilimia 65 na ujenzi wa jengo moja (1) la Mamlaka ya Serikali Mtandao (eGA) umefikia asilimia 56. Jumla ya shilingi bilioni 93.83 zimetumika katika Julai, hadi Aprili, 2023.

 

(iv)    Ujenzi wa Makao Makuu ya Mahakama Dodoma

Hatua iliyofikiwa ni: Kuendelea na ujenzi wa Jengo la makao makuu Jijini Dodoma ambapo utekelezaji umefikia asimilia 89. Jumla ya shilingi bilioni 16.9 zimetumika katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili 2023.

 

(v)      Ofisi na Makazi ya Viongozi  katika Mamlaka za Serikali za Mitaa Hatua iliyofikiwa ni: Kuendelea na ujenzi wa  majengo 49 ya muda mrefu ya Halmashauri ambapo majengo tisa (9) kati ya hayo yamekamilika; kuendelea na ujenzi wa majengo 30 kwa Halmashauri zilizohamisha Makao Makuu ambapo jengo moja la Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika limekamilika; na kuendelea na ujenzi wa majengo 30 mapya ya utawala na ujenzi wa nyumba 46 za wakurugenzi na  nyumba 78 za wakuu wa idara. Jumla ya shilingi bilioni 87.11 zimetumika katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023.

(vi)    Ofisi na Makazi ya Viongozi katika Sekretarieti za Mikoa

Hatua iliyofikiwa ni: Kuendelea na ujenzi wa Ikulu Ndogo katika Mkoa wa Njombe ambapo utekelezaji umefikia asilimia 98; kuendelea na ukamilishaji wa nyumba za Makatibu Tawala Wasaidizi wa Mkoa wa Njombe (2);  kuendelea na ukamilishaji wa nyumba za Makatibu Tawala wa Wilaya za Momba ambapo utekelezaji umefikia asilimia 95;  kukamilika kwa ukarabati wa nyumba ya Wakuu wa Wilaya za Ludewa na Siha; kuendelea na ujenzi wa nyumba ya Mkuu wa Wilaya Kibiti ambapo uko hatua ukamilishaji; kuanza ujenzi na ukarabati wa nyumba za wakuu wa wilaya za Iramba, Mbinga, Buhigwe, Mbinga na Momba; na kuanza ujenzi wa uzio wa nyumba ya mkuu wa Wilaya ya Same; kukamilika kwa nyumba za Makatibu Tawala wa mikoa ya Katavi na Njombe na kuanza ujenzi wa nyumba za wahudumu na vibanda vya walinzi ambazo zipo hatua za manunuzi; na kuendelea na ujenzi wa nyumba za Makatibu Tawala wa Mikoa ya Ruvuma na Songwe; na kukamilika kwa  nyumba za Wakuu wa Mikoa ya Njombe na Songwe.

 

Shughuli nyingine zilizofanyika ni: Kuanza ujenzi wa Ofisi za Wakuu wa Wilaya za  Kakonko,  Same, Hai,  Gairo, Malinyi na Ulanga; kukamilika kwa ukarabati wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani; kuendelea na ujenzi wa ofisi za wakuu wa Mikoa ya Geita na Songwe ambapo utekelezaji upo hatua ya ukamilishaji; ukarabati wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa wa Dodoma, Iringa, Kigoma, Kilimanjaro, Ruvuma na Rukwa; na upanuzi wa Ofisi za Wakuu wa Mikoa ya Singida na Kilimanjaro; kuendelea na ujenzi wa ofisi za Tarafa katika Mikoa ya Kilimanjaro (8), Arusha (2), Pwani (5), Mtwara (5), Songwe (4), Katavi (3), Dodoma (3), Mwanza (11), Morogoro (5), Ruvuma (2) na Kigoma (1); na kuendelea na ujenzi wa jengo jipya la Soko la kisasa la Kariakoo ambapo utekelezaji uko hatua ya kumwaga zege kwenye ghorofa ya 4. Aidha, ukarabati wa jengo la zamani unaendelea ambapo utekelezaji umefikia asilimia 56. Jumla ya shilingi bilioni 33.26 zimetumika katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023.

 

(i)         Mradi Na. 6209: Mfuko wa Kuchochea Maendeleo ya Jimbo

Hatua iliyofikiwa ni: Kuendelea na utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo katika Mamlaka za Serikali za Mitaa ikiwemo kusaidia ujenzi wa vituo vya afya, vyumba vya madarasa, vyumba vya maabara na miundombinu ya maji na umeme. Jumla ya shilingi bilioni 18.8 zimetumika katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023.

 

E.            Mradi Na. 6501: Vitambulisho vya Taifa  

Hatua iliyofikiwa ni: Kusajiliwa na kutambuliwa kwa  watu 774,594 kati yao wageni 575 na wakimbizi 49 na kufanya jumla ya watu waliosajiliwa kufikia 23,960,323 katika mikoa na wilaya zote Tanzania Bara na Zanzibar; kununuliwa kadi ghafi 6,123,438 za kuzalisha vitambulisho; kuchakatwa kwa maombi na kuzalishwa kwa namba za utambulisho wa Taifa (NIN) 623,247 na kufanya jumla namba za utambulisho wa Taifa (NIN) zilizozalishwa kufikia 20,126,693; kuzalishwa na kusambazwa kwa vitambulisho 1,059,716. kwa wananchi na kufanya jumla ya vitambulisho vilivyozalishwa na kusambazwa kufikia 12,097,933; kuunganishwa na kuboreshwa kwa mifumo na miundombinu ya mtandao wa mawasiliano kati ya Ofisi za Usajili za Wilaya na Makao Makuu ambapo ofisi nne (4) zimeunganishwa na kufanya jumla ya ofisi zilizounganishwa kufikia 143; na kuunganishwa kwa Taasisi 14 katika mfumo wa Usajili na Utambuzi na kufanya jumla ya taasisi zilizounganishwa na mfumo kufikia 75. Jumla ya shilingi billion 4.48 zimetumika katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023

 

F.             Usalama wa Raia  

 

(i)           Mradi Na. 6302: Ujenzi wa Ofisi na Nyumba za Makazi Tanzania Bara

Hatua iliyofikiwa ni: kukamilika kwa ujenzi wa vituo vitatu (3) vya  Polisi vya Daraja “A” Kigamboni, Korogwe na Wanging’ombe, Daraja “B” Ruangwa, Daraja ‘C’ Kirongwe Tarime Rorya; kukamilika kwa ujenzi wa majengo ya Ofisi ya Kamanda wa Polisi wa Mkoa na Mkuu wa Kikosi cha kutuliza ghasia Singida; kukamilika kwa ofisi ya mkoa wa kipolisi Tarime Rorya; kukamilika kwa ujenzi wa majengo mawili (2) ya ghorofa tatu (3) yenye uwezo wa kuishi familia 24 za askari Mabatini – Mwanza; kukamilika kwa ujenzi wa uzio wa kutenganisha eneo la Makao Makuu ya Polisi/CID na eneo la RPC Dodoma; kuendelea na ujenzi wa kituo cha Polisi Daraja ”C” na ujenzi wa nyumba za makazi ya askari Ludewa ambapo utekelezaji umefikia asilimia 65, kituo cha Polisi Daraja “A” katika Mji wa Serikali Mtumba Dodoma (asilimia 80), Daraja “C” Mbande Temeke (asilimia 80), Draja “C” Chang’ombe Dodoma (asilimia 50);  ujenzi wa ofisi za makamanda wa  Polisi za Mikoa ya  Mara (asilimia 95), Katavi (asilimia 75), Njombe (asilimia 60) na ujenzi wa nyumba 3 za kuishi Makamishna wa Polisi  Jijini Dodoma umefikia (asilimia 99). Jumla ya shilingi bilioni 1.39 zimetumika katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023

 

(ii)         Mradi Na. 6303: Ujenzi wa Ofisi na Nyumba za Makazi Zanzibar

Hatua iliyofikiwa ni: kukamilika kwa ujenzi wa kituo cha Polisi Mkokotoni Zanzibar, kukamilika kwa ujenzi wa kituo cha Polisi Daraja “C” Kaskazini – Kusini Unguja; kuendelea na ujenzi wa kituo cha Polisi Kizimkazi ambapo utekelezaji umefikia asilimia 65; kukamilika kwa ujenzi wa ofisi za makamanda wa polisi za mkoa wa Kusini na Kaskazini Unguja; kukamilika kwa majengo manne (4) ya kuishi familia nane (8) za askari Mfikiwa Kusini Pemba; na kukamilika kwa ukarabati wa majengo saba (7) ya ghorofa ya kuishi familia 28 za Askari katika Kambi ya Ziwani – Zanzibar. Jumla ya shilingi milioni 739.3 zimetumika katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023

 

 

G.          Uhamiaji

Mradi Na. 6301: Ujenzi wa Ofisi za Mikoa za Uhamiaji

Hatua iliyofikiwa ni:  Kukamilika na kukabidhiwa kwa Ofisi ya uhamiaji ya Mkoa wa Geita, Manyara na Lindi; kuendelea na ujenzi wa ofisi ya Uhamiaji Mkoa wa Mtwara ambapo utekelezaji umefikia asilimia 75, Lindi (asilimia 90) na Ofisi ya Makao Makuu ya Uhamiaji Dodoma (asilimia 44); kuendelea na awamu ya kwanza ya ujenzi wa chuo cha mafunzo ya uhamiaji cha Raphael Kubaga kilichopo Boma Kichakamiba wilayani Mkinga (Tanga) ambapo utekelezaji umefikia asilimia 94; na ujenzi wa Ofisi ya Uhamiaji Mkoa wa Manyara asilimia 97. Jumla ya shilingi bilioni 5.70 zimetumika katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023.

 

2.3.2.3. Mapinduzi ya TEHAMA

A.          Teknolojia ya Habari na Mawasiliano

 

(i)           Mradi Na. 4283: Ujenzi wa Mkongo wa Mawasiliano wa Taifa

Hatua iliyofikiwa ni: Kukamilika kwa upembuzi yakinifu wa ujenzi mpya wa Kilomita 

1,600 za Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano na vituo 15 vya kutoleo huduma za Mkongo;  kuendelea na kazi za upembuzi yakinifu kwa ajili ya ujenzi wa Kituo cha Taifa cha Data Zanzibar; kukamilika kwa ununuzi wa mitambo kwa ajili ya vituo 112 vya kutolea Huduma (transmission and power equipment)  ambapo usimikaji umefanyika kwenye vituo 61 vya kutolea huduma (Point of Presence-POPs and Optical Line Amplifiers OLA); kuendelea na ujenzi wa njia mpya za Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano wenye jumla ya Kilomita 4,442;  kujengea uwezo kwa wataalamu 114 wa usimamizi na uendeshaji wa Mkongo wa Taifa nchini pamoja na wataalamu wengine 817 katika eneo la usalama mtandao; kukamilika kwa utungwaji wa Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi (Data Protection Act, 2022); na kutoa elimu kwa umma kuhusu usalama wa mtandao kwa wananchi 453, shule za sekondari 3 (wanafunzi  968), vyuo vikuu 8 (wanachuo 656) na wananchi takriban milioni 5.2 kupitia Vyombo vya Habari (TV-9, Redio-8, magazeti-7). Jumla ya shilingi bilioni 54.3 zimetumika hadi Aprili 2023.

 

(ii)         Mradi Na. 4234: Mfumo wa Anwani za Makazi  

Hatua iliyofikiwa ni: Kukamilika kwa uboreshaji wa programu ya Mfumo wa Kidijitali wa Anwani za Makazi; kufanya mapitio ya baadhi ya sheria, Kanuni na Matamko (Establishment order) zinazoguswa na utekelezaji wa Mfumo wa Anwani za Makazi;  kukamilika kwa uhakiki wa taarifa za miundombinu ya Anwani za Makazi pamoja na taarifa za makazi zilizokusanywa katika Operesheni Anwani za Makazi kwenye Halmashauri 23, ambazo ni Majiji ya Dar es Salaam, Mwanza, Dodoma, Arusha, Mbeya na Tanga, Manispaa za Moshi, Kinondoni, Temeke, Ubungo, Kigamboni, Ilemela, Mjini, Magharibi A, Magharibi B pamoja na Halmashauri za Kaskazini A, Kaskazini B, Chakechake, Meru, Mtwara Mikindani, Micheweni, Kusini na Kati; kutoa elimu kwa umma kuhusu Anuani za Makazi kwa wafanyabiashara 166 wa Mkoa wa Dodoma, watumishi 80 kutoka Wizara za Kisekta  na watanzania takribani milioni 4.5 kwa kupitia vyombo vya habari; na kutungwa kwa Kanuni ndogo za Anwani za Makazi ambazo zimetumika katika kutekeleza mradi wa Anwani ya Makazi. Jumla ya shilingi bilioni 16.3 zimetumika hadi Aprili 2023.

 

(iii)       Mradi Na. 4280: Tanzania ya Kidijitali

Hatua iliyofikiwa ni: Kusainiwa kwa mkataba na Mshauri Mwelekezi wa kusanifu na kusimamia ujenzi wa Taasisi ya TEHAMA na vituo vitano vya Ubunifu vya kikanda;  kuboreshwa kwa miundombinu ya intaneti yenye kasi (broadband) na kuunganisha taasisi 18 kwenye mtandao wa Serikali; kuendelea na kazi ya upembuzi yakinifu kwa ajili ya vituo vya huduma pamoja utakaosaidia kurahisisha utendaji kazi wa vituo hivyo (Business Process re-engeering); kusainiwa kwa mkataba baina ya Wizara na Mshauri Mwelekezi kwa ajili ya usanifu wa Mfumo wa Kitaifa wa Usimamizi wa Taarifa za Takwimu za TEHAMA (NISMIS); kuandaa Mpango Mkakati wa Mfumo wa Kitaifa wa Usimamizi wa Taarifa za Takwimu za TEHAMA (NISMIS) unaojumuisha viashiria vya TEHAMA; kukamilika kwa Mpango Mkakati wa Uchumi wa Kidijitali (Digital economy Framework 2023-2033) utakaosaidia kuongeza matumizi ya kidijitali kwa huduma zinazotolewa na Serikali pamoja na Sekta binafsi; kukamilisha upembuzi yakinifu kwa ajili ya kufanya mapitio ya sera na sheria zinazosimamia TEHAMA; na kuwajengea uwezo wataalam wa TEHAMA nchini kwa kuwapatia watalaam 17 mafunzo ya muda mfupi. Jumla ya shilingi bilioni 21.39 zimetumika hadi Aprili 2023..

 

(iv)       Mradi Na. 4279: Upanuzi wa Usikivu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC)

Hatua iliyofikiwa ni: Kukamilika kwa awamu ya kwanza ya ujenzi wa studio za redio (TBC Taifa na TBC FM) na za ukombozi wa Nchi Kusini mwa Afrika katika jengo la utangazaji barabara ya Nyerere; kukamilika kwa taratibu za manunuzi ya kumpata Mzabuni kwa ajili ya Ufungaji wa Mitambo ya redio na TEHAMA katika studio za redio barabara ya Nyerere pamoja na jengo la TBC2 awamu ya pili; kukamilika kwa taratibu za manunuzi za kuwapata wazabuni kwa ajili ya utekelezaji wa Mradi wa Upanuzi wa Usikivu redio za TBC katika maeneo 9; kuendelea na ujenzi wa makao makuu ya TBC Jijini Dodoma;  na kukamilika kwa upembuzi yakinifu wa michoro na mifumo kwa ajili ya ukamilishaji wa jengo la Kituo cha Taifa cha Televisheni (TVT) litakalotumika kwa ajili ya Chaneli ya Utalii ya Tanzania Safari na utawala. Jumla ya shilingi bilioni 6.55  zimetumika hadi Aprili 2023.

 

(v)         Mradi Na. 6567: Habari kwa Umma

Hatua iliyofikiwa ni: Kuandaliwa na kurushwa kwa vipindi ishirini (25) vya Televisheni vinavyohusu utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC1); kuchapisha na kusambaza nakala 5,000 za jarida la NCHI YETU linaloelezea mafanikio ya Serikali ya Awamu ya Sita na utekelezaji wa miradi ya maendeleo ikiwemo ya kimkakati; kuratibu mikutano ya Taasisi za Serikali 48 katika kutoa taarifa za utekelezaji wa shughuli zake kwa umma kupitia vyombo vya habari; na kukamilika kwa malipo ya kifaa cha kurushia matangazo mubashara aina ya Live U. Jumla ya shilingi milioni 876.69 zimetumika hadi Aprili 2023.

 

(vi)       Mradi Na. 6505: Kufunga Mtambo Mpya wa Kisasa wa Uchapaji   

Hatua iliyofikiwa ni: Kuendelea na ujenzi wa kiwanda cha Kupiga Chapa; na kuwasili kwa mitambo tisa (9) ya uchapaji ambapo jumla ya shilingi bilioni 12.41 zimetumika hadi Aprili 2023.

 

(vii)      Mradi Na. 6226: Kujenga Kituo Kikuu cha Kuendeleza Ubunifu wa TEHAMA na Vituo Vidogo vya Kuendeleza Sekta ya TEHAMA Nchini  Hatua iliyofikiwa ni: kusainiwa kwa mkataba na mkandarasi kwa ajili ya kufanya matengenezo na maboresho ya jengo la TEHAMA ziko katika hatua za ukamilishaji; kukamilika kwa upembuzi yakinifu wa kuainisha mahitaji ya vifaa vinavyohitajika kwa ajili ya uundwaji wa bidhaa za TEHAMA hapa nchini; kujenga uwezo kwa wabunifu na watengeneza bidhaa za TEHAMA 165 wa kanda ya Dar es Salaam na Arusha juu ya namna bora ya kukuza bunifu zao ili ziweze kutoa ajira na kuchangia pato la Taifa; na kukamilika kwa matengenezo ya  Portal ya wataalamu wa TEHAMA. Jumla ya shilingi milioni 500 zimetumika hadi Aprili 2023.

 

2.3.3. Kuimarisha Uwezo wa Uzalishaji Viwandani na Utoaji Huduma

2.3.3.1. Uzalishaji Viwandani

 

(i)           Mradi Na. 6103: Kituo cha Kuendeleza Teknolojia ya Magari Tanzania 

Hatua iliyofikiwa ni: Kuanzisha karakana kuu ya kukalibu chuma na kiwanda cha

Metal Galvanization; Kununua mitambo kwa ajili ya Maabara ya Utafiti; na Kujenga uwezo na kuendeleza utafiti na kuhawilisha teknolojia ya magari (kufanya Reverse Engineering ya pampu za magari ya Zimamoto na kufanya utafiti na kuzalisha prototype ya Magari ya Deraya). Jumla ya shilingi bilioni 12.0 zimetumika katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023

 

(ii)         Mradi Na. 4486: Uzalishaji Viwandani kupitia Programu ya Kuendeleza Sekta ya Kilimo Awamu ya Pili (ASDP II)

Hatua iliyofikiwa ni: Kuendelea na mapitio ya mikakati ya sekta ndogo za nguo na mavazi, ngozi na bidhaa za ngozi na kuanza kutengeneza mikakati mipya ya mafuta, korosho na mkakati wa kuvikuza na kuviendeleza viwanda; kuanza kwa uandishi wa mkakati wa bidhaa za nguo na mavazi; kuendelea kufanya tathmini ya uzalishaji wa magunia ya mkonge na biashara ya magunia ya jute; kuendelea na ukamilishaji taratibu za umiliki wa ardhi yenye ukubwa wa ekari 62 iliyoko Kahama mkoani Shinyanga; kukamilika kwa utambuzi na tathmini ya kongano za viwanda vya mazao ya kilimo na sekta nyingine yenye fursa za ukuaji wa jasiriamali ndogo na za kati katika mikoa yote ya Tanzania Bara. Jumla ya shilingi milioni 633.08 zimetumika katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023.

 

(iii)       Mradi Na. 4948: Kuimarisha Uzalishaji Viwandani kupitia Uboreshaji wa Ubora na Tija - KAIZEN

Hatua iliyofikiwa ni: Kuongezeka kwa idadi ya waratibu wa KAIZEN viwandani kutoka 200 hadi kufikia 230 pamoja na idadi ya viwanda vilivyonufaika na huduma hii kutoka 135 ya hadi kufikia 150; kuongezeka kwa idadi ya mikoa iliyofikiwa na huduma za KAIZEN kutoka 8 hadi 12 ambapo takribani viwanda 16 vimenufaika na mafunzo na kufanikisha kuongeza wakufunzi 36 wapya; na kufanyika kwa mafunzo kwa washiriki 20 kutoka Unguja na 70 kutoka Pemba.

 

(iv)       Mradi Na. 6260: Mradi wa Kusaidia Taasisi

 

(a)         Kiwanda cha Mashine na Vipuri KMTC

Hatua iliyofikiwa ni: Kukamilika kwa ununuzi na usimikaji wa mashine ya overhead crane; kukamilika kwa ununuzi wa vifaa vinavyohitajika kwa ajili ya tanuru ikiwemo Induction furnace; kukamilika kwa ujenzi wa msingi na kuendelea na usimikaji wa kinu cha kuyeyushia chuma (induction furnace) ambapo utekelezaji umefikia asilimia 98; na kukamilika kwa ukarabati wa mfumo wa umeme kwa asilimia 99; kukamilika kwa majaribio na mafunzo ya namna ya kutumia kinu cha kuyeyushia chuma kwa awamu ya kwanza, na kuendelea kwa awamu ya pili. Jumla ya shilingi milioni 760.95 zimetumika katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023.

 

(b)         Eneo la Kongano ya Viwanda – TAMCO

Hatua iliyofikiwa ni kupatikana kwa mkandarasi kwa ajili ya ujenzi wa barabara yenye urefu wa mita 320 (China boda road). Jumla ya shilingi milioni 28.7 zimetumika katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023.

 

(c)         Mradi wa kuunganisha Matrekta ya URSUS

Hatua iliyofikiwa ni: Kuendelea kufanya mazungumzo na Serikali ya Poland kupitia wawakilishi wa Timu Maalum ya Serikali ya Majadiliano (GNT); na kuendelea kufuatilia madeni kwa wakulima 716 waliokopa matreka hayo. Jumla ya shilingi milioni 200.0 zimetumika katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023.

 

(d)         Kongane la Viwanda Nyanza

Hatua iliyofikiwa ni: Kukamilika kwa ukarabati wa ghala Na. 1 na kuendelea na ukarabati wa ghala Na. 2 ambapo utekelezaji umefikia asilimia 10. Jumla ya shilingi milioni 84.1 zimetumika katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023.

 

(e)         Mradi wa Kiwanda cha Viuadudu (TBPL)

Hatua iliyofikiwa ni: Kukamilika kwa jaribio la pili la viwatilifu; kuendelea  na ujenzi wa barabara ya ndani (Viuatilifu Road) yenye urefu wa mita 230 ambapo ujenzi umefikia asilimia 75. Jumla ya shilingi bilioni 1.24 zimetumika katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023.

 

(f)          Mradi wa Makaa ya Mawe wa Katewaka

Hatua iliyofikiwa ni: Kukamilika kwa uthaminishaji wa mali za waathirika 689 wa mradi wa makaa ya mawe Katewaka katika Kijiji cha Nkomang’ombe katika Kitongoji cha Nyambalapi na Mhumbi. Jumla ya shilingi milioni 357.1 zimetumika katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023.

 

(g)         Kufanya Maandalizi ya Uchimbaji wa Chuma Ghafi (iron ore) Maganga Matitu

Hatua iliyofikiwa ni: Kukamilika kwa uthaminishaji na uhakiki wa mali za wananchi  381 wanaopisha mradi na maandalizi ya vitabu vya taarifa ya uthaminishaji yanaendelea. Jumla ya shilingi milioni 179.2 zimetumika hadi kufikia mwezi Aprili, 2023.

 

(h)         Kituo cha Zana za Kilimo na Ufundi Vijijini - CAMARTEC 

Hatua iliyofikiwa ni: Kuendelea na ujenzi wa Kiwanda Darasa cha kubangua Korosho katika Wilaya ya Manyoni mkoani Singida kwa kuandaa vifaa na mashine 129; kuanza ujenzi wa Kitivo cha Teknolojia za Kihandisi (KITEKI) wilaya ya Karatu mkoani Arusha kwa kuandaa jumla ya mashine 49 na zana nyingine za kilimo; kufanyika kwa utafiti wa kubaini mahitaji na matumizi ya zana za kilimo, mifugo, uvuvi na teknolojia za vijijini katika Mikoa ya Songwe (Momba), Dodoma (Chemba) na Arusha (Karatu); kufanyika kwa ukarabati wa majengo mawili ya Utawala (Block A na Block B) na nyumba mbili zilizopo katika Kiwanja Na.18 Themi Hill na Kiwanja Na. 83 Kanisa Road (Uzunguni); ununuzi wa mashine tatu (3) kwa ajili ya Karakana ya kituo (mashine  2 za kuchomelea na Gen Set 1 ya kufua umeme). Jumla ya shilingi milioni 873.75 zimetumika katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023.

 

(i)           Shirika la Utafiti na Maendeleo ya Viwanda Tanzania - TIRDO 

Hatua iliyofikiwa ni: Kukamilika kwa zoezi la ukusanyaji wa taarifa za tathmini ya viwanda na kuainisha fursa za uwekezaji katika Kanda ya Kaskazini; kuendelea na ujenzi wa jengo la utawala ili kutoa nafasi ya kuanzisha kituo cha Taarifa za Viwanda na Ubashari wa teknolojia na viatamizi kwa wabunifu wa teknolojia ambapo ujenzi umefikia asilimia 45; kukamilika kwa ununuzi wa vifaa vya upimaji ubora bila kuharibu (Non Destructive Testing - NDT) wa mabomba ya mafuta na gesi ili kuendelea kukidhi viwango vya kimataifa. Jumla ya shilingi milioni 856.13 zimetumika katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023.

(j)          Shirika la Uhandisi na Usanifu wa Mitambo – TEMDO

Hatua iliyofikiwa ni: Kufanyika kwa unakili na kufanya maboresho ya mchoro wa mtambo wa kuchakata mkonge uliopo Tanga; kuendelea na utafiti wa teknolojia ya kutengeneza matofali yanayohimili joto kali kwa awamu ya pili; kukamilika kwa mitambo midogo minne (4) ya sukari; kuendelea na utengenezaji wa Mtambo wa kutengeneza sukari kwa kiwango cha mjasiriamali wa kati (sugar mini-plant, Capacity 200TCD); kuendelea na maboresho ya karakana kwa kuweka mfumo wa upepo na umeme kwenye mashine ya kupaka rangi (painting booth); kuendelea na usanifu na utengenezaji wa vifaa tiba (vitanda, drip stand, examination bed, delivery bed, hospital screens, bed side lockers, biomedical waste incinerators, 6-body Mortuary cabinets na milango ya kuzuia mionzi). Jumla ya shilingi milioni 998.00 zimetumika katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023. 

 

(k)         Uendelezaji wa Viwanda Vidogo (SIDO)

Hatua iliyofikiwa ni: Kukamilika kwa michoro ya majengo ya viwanda (industrial sheds) katika Mkoa wa Iringa na ukarabati katika Mikoa ya Dar es Salaam, Mbeya, Arusha, Tabora na kumalizia jengo la Nyasa Mkoa wa Ruvuma; kukamilika kwa ujenzi wa jengo la kiwanda Tanga na kuendelea ujenzi wa majengo ya viwanda katika mikoa ya Singida - Manyoni (1), Shinyanga – Kahama (2) na Geita - Chato (2); kuandaliwa kwa vipimo vya Mashine ya kukeleza vyuma, kukata na kukunja mabati, kuchomelea na kukata vyuma kwa ajili ya kuimarisha Kituo cha Uendelezaji Teknolojia (TDCs) katika mkoa wa Arusha; kusimikwa kwa mashine ya kukeleza vyuma, kukata na kukunja mabati, kuchomelea na kukata vyuma kwa ajili ya kuimarisha vituo vya Uendelezaji Teknolojia katika Mikoa ya Kilimanjaro na Mbeya; kuzalishwa kwa mashine 228 na vipuli 1,374 za aina mbalimbali kupitia Vituo saba (7) vya kuendeleza Teknolojia (TDCs) kwa ajili ya viwanda vidogo; na kutolewa mafunzo kwa wafanyakazi wa SIDO kuhusu utumiaji wa mfumo wa ofisi mtandao. Jumla ya shilingi bilioni 1.60 zimetumika katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023.

 

(l)           Mchango wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii Katika Uchumi wa Viwanda

 

Kilimanjaro International Leather Industries Co Ltd (KLICL)

Hatua iliyofikiwa ni: Kuendelea na awamu ya pili ya ujenzi wa kiwanda cha kuchakata ngozi ambapo utekelezaji umefikia asilimia 45, maabara na kantini (asilimia 99), Jengo la Jenereta (asilimia 99) na barabara za ndani na mitaro ya maji ya mvua (asilimia 50) ambapo utekelezaji wa jumla wa mradi umefikia asilimia 95; na kuendelea na ujenzi wa miundombinu wezeshi ikiwemo  maji taka, barabara za ndani na uzio katika kiwanda cha ngozi. Jumla ya shilingi bilioni 122 zimetumika katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023

 

Kiwanda cha Nyama cha Nguru Hills Ranch - Morogoro

Hatua iliyofikiwa ni: kukamilika kwa ukarabati wa majengo, mifumo ya umeme na maji, majokofu ya upoozaji, uunganishaji wa umeme mkubwa na ufungaji wa mashine pamoja na majaribio ya mashine na mifumo ya uendeshaji. Jumla ya shilingi bilioni 20.35 zimetumika katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023.

 

Kiwanda cha Kuchakata Tangawizi cha ‘Mamba Ginger Factory Limited

Hatua iliyofikiwa ni: Kukamilika kwa ukarabati wa majengo ya kiwanda; unganishaji wa umeme mkubwa na ufungaji wa mashine, majaribio ya mashine na mifumo ya uendeshaji. Jumla ya shilingi bilioni 1.782 katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023.

 

Kiwanda cha Chai cha Mponde - Tanga

Hatua iliyofikiwa ni: kukamilika kwa ukarabati wa majengo, mitambo, mifumo ya umeme na maji pamoja na majaribio ya mitambo. Jumla ya shilingi milioni 500 zimetumika katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023.

 

(v)        Mradi Na. 4933: Uendelezaji wa Kanda Maalumu za Kiuchumi 

 

Eneo Maalumu la Uwekezaji Mtwara Free Port Zone

Hatua iliyofikiwa ni: Kukamilika kwa ujenzi wa miundombinu ya maji, umeme na barabara za ndani ya eneo la mradi zenye urefu wa km 1.06; na kukamilika kwa usanifu wa jengo la Kituo cha Pamoja cha Huduma (One Stop Center Building). 

 

2.3.3.2. Ubiasharishaji wa Mazao ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi kupitia ASDP II 

A.          Kilimo

 

(a) Mradi Na. 4486: Programu ya Kuendeleza Sekta ya Kilimo Awamu ya Pili - ASDP II

(i)           Ujenzi na Ukarabati wa Miundombinu ya Umwagiliaji 

Hatua iliyofikiwa ni: Kuendelea na ujenzi wa skimu mpya 19 zenye ukubwa wa hekta 45,564 katika mikoa ya Mbeya, Iringa, Dodoma, Mwanza, Tabora, Morogoro, Kilimanjaro, Manyara, Shinyanga, Mara, Simiyu na Rukwa; kuendela na ukarabati wa skimu 19 zenye ukubwa wa hekta 13,243 katika mikoa ya  Mbeya, Iringa, Mwanza, Katavi, Ruvuma, Tanga, Morogoro, Kilimanjaro, Manyara na Tabora; na kuendelea na ujenzi wa mabwawa 10 yenye jumla ya mita za ujazo 122,545,000 ya katika mikoa ya Dodoma, Tabora, Mwanza, Shinyanya, Manyara, Singida na Rukwa. Aidha, jumla ya ajira 298,635 zimezalishwa katika miradi hii. Jumla ya shilingi bilioni 96.43 zimetumika katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023.

 

(ii)         Kuwezesha Uanzishwaji wa Mashamba Makubwa ili kuwa Kitovu Cha Teknolojia Bora kwa Wakulima Wadogo

Hatua iliyofikiwa ni: Kubainisha mashamba makubwa (Block farms) yenye ukubwa wa ekari 264,841.50 kwa ajili ya vijana katika Mikoa ya Kigoma Kigoma (ekari 36,719.75) Mbeya (ekari 52,165), Njombe (ekari 87,000), Dodoma (ekari 33,4543), Singida (ekari 50,000) na Kagera (ekari 5,503.75); kupimwa kwa afya ya udongo wa mashamba hayo na kusafishwa kwa hekta 520 za shamba la Mlazo-Ndogowe; kusafishwa kwa Shamba la Chinangali lenye ukubwa wa hekta 160 kwa ajili ya uwekezaji; kusafishwa kwa mashamba yenye ukubwa wa ekari 77.8 katika Kituo na Vyuo vya Bihawana (ekari 22), Mlingano (ekari 4), Uyole (ekari 3), Mubondo (ekari 10), Ukiriguru (ekari 8.9), NSI - Kidatu (ekari 2.4),  Horti Tengeru  (ekari 4), Mtwara (ekari 10), Ilonga (ekari 3.5) na Tumbi (ekari 10); na kudahiliwa kwa vijana 4,000 kwa ajili ya kupewa mafunzo katika vyuo vya kilimo kuanzia mwezi Machi, 2023 kabla ya kupewa ardhi ya kilimo. Jumla ya shilingi bilioni 3.0 zimetumika katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023.  

 

(iii)       Kuimarisha Vituo vya Utafiti na Utafiti wa Mbegu Bora

Hatua iliyofikiwa ni: Kuendelea na ujenzi wa Ofisi za TARI Makao Makuu - Dodoma ambapo utekelezaji umefikia asilimia 41; kuendelea na ujenzi wa Kituo cha TARI Kihinga – Kigoma ambapo utekelezaji umefikia asilimia 68; kuanza kwa ujenzi wa miundombinu ya umwagiliaji kwenye jumla ya hekta 854 za vituo 16 vya utafiti; kujenga ghala tano  (5) zenye vyumba vya ubaridi (cold rooms) zenye uwezo wa kuhifadhi tani 2,075 za mbegu katika vituo vya TARI Selian, Hombolo, Tumbi,  Naliendele na  Dakawa umefikia asilimia 20; kuanza ujenzi wa uzio katika eneo la kituo cha TARI Uyole lenye hekta 1,042; kununua vifaa na vitendanishi vya maabara ya udongo na bioteknolojia za TARI Mlingano na TARI Mikocheni; kufanya ugunduzi wa teknolojia mbalimbali kwa kukamilisha mapendekezo ya kupitisha aina 15 za mbegu mpya kwa Kamati ya Kitaalam ya Mbegu ambapo mbegu saba (7) ni za maharage, 3 za mtama, 5 za zabibu, na 2 za zao la migomba; kutunza vinasaba 33,332 vya mazao ya mpunga (729), mtama (416), uwele (105), ulezi (3), alizeti (39), zabibu (26), migomba (128), maharage (10), muhogo (20), korosho (30,000), pamba (328), mahindi (250), viazi vitamu (6),  miwa (107), minazi (7), michikichi (3), mkonge (60), na kakao (17) kwa ajili ya utafiti na uhifadhi wa mbegu za asili. Jumla ya shilingi bilioni 15.65 zimetumika katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023. 

 

(iv)       Kuimarisha Huduma za Ugani, Vyuo vya Mafunzo ya Kilimo na Vituo vya Mafunzo ya Wakulima

(a)         Ukarabati wa Vyuo vya Kilimo na Vituo vya Mafunzo ya Wakulima

Hatua iliyofikiwa ni: Kudahiliwa kwa wanafunzi 3,151 wa mwaka wa kwanza na wa pili  katika vyuo 14 vya mafunzo ya kilimo; kutoa huduma ya chakula kwa wanafunzi wa vyuo 14 vya mafunzo ya kilimo; na kuendelea na ukarabati wa miundombinu katika vyuo vya Kilimo Tumbi, Igurusi, Ilonga na National Sugar Institute. Jumla ya shilingi bilioni 7.14 zimetumika katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023.

 

(b)         Kuimarisha Huduma za Ugani 

Hatua iliyofikiwa ni: Kuboresha mazingira ya utoaji huduma kwa kununua na kusambaza pikipiki 5,889 kwa maafisa ugani katika mikoa 25; kununua na kusambaza viti 1,020 na meza 23 katika Vituo vitano (5) vya Rasilimali za Kilimo vya Kata (WARCs) nane (8) katika mikoa ya Dodoma, Singida na Simiyu; kutoa mafunzo kwa maafisa ugani 142 wa Halmashauri 142 kutoka katika mikoa 25 kuhusu matumizi ya vifaa vya kupima afya ya udongo;  na kutoa mafunzo kwa maafisa ugani 203 kuhusu kilimo biashara na matumizi ya mfumo kwa kutumia simu ya mkononi (M – Kilimo). Jumla ya shilingi bilioni 12.78 zimetumika katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023.

 

(v)        Kuongeza Tija na Uzalishaji

 

(a)         Upatikanaji wa Mbegu Bora 

Hatua iliyofikiwa ni: Kuzalishwa na kusambazwa tani 1,004 za mbegu bora za Alizeti kwa wakulima kwa bei ya ruzuku katika wilaya 39 za mikoa ya Dodoma, Kagera, Mbeya, Mwanza na Singida. Kati ya kiasi hicho, tani 300 zimezalishwa na Sekta Binafsi; kuzalisha miche 170,924 ya parachichi na miche 394,000 ya chikichi; kuendelea na ujenzi wa miundombinu ya umwagiliaji katika shamba la Kilimi (Nzega) lenye ukubwa wa hekta 400, Arusha (hekta 200) na Msimba (Kilosa) hekta 200 ambapo utekelezaji umefikia asilimia 25.0; kukamilika kwa upimaji wa maji (geological survey) na kutambua maeneo sita (6) ya kuchimba visima katika shamba la Arusha; kukamilika kwa uchimbaji wa visima virefu sita (6) katika shamba la mbegu la Msimba; kuongeza eneo jipya la  hekta 1,300 kwa ajili ya kuzalisha mbegu bora katika mashamba ya Kilimi - Nzega (hekta 300), Msimba - Kilosa (hekta 400), Mwele - Tanga (hekta 300) na Namtumbo - Ruvuma (hekta 300); kuendelea  na ukarabati wa ghala la kuhifadhi mbegu la msimba ambao umefikia asilimia 90 na usimikaji wa mtambo mpya wenye uwezo wa kuchakata tani tatu (3) za  mbegu kwa saa katika ghala hilo umefikia asilimia 85; ununuzi wa matrekta sita (6) na zana zake kwa ajili ya mashamba ya Msungura, Namtumbo, Msimba, Dabaga, Mbozi na Kilimi na ununuzi wa magari matatu (3) ya kusambaza mbegu. Jumla ya shilingi bilioni 19.68 zimetumika katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023. 

 

(b)         Upatikanaji wa Mbolea ya Ruzuku

Hatua iliyofikiwa ni: Kutolewa kwa ruzuku ya mbolea tani 449,795 na kusambazwa kwa  wakulima katika maeneo mbalimbali nchini; kufanyika kwa usajili wa waingizaji wakubwa wa mbolea 28, mawakala wadogo 3,265 pamoja na wazalishaji wa ndani watatu (3) wa mbolea katika mfumo wa kielektroniki; na kufanyika kwa usajili wa wakulima 3,020,621 kwenye mfumo wa kielektroniki. Jumla ya shilingi bilioni 214.8 zimetumika katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023.

 

(c)         Upatikanaji wa Viuatilifu

Hatua iliyofikiwa ni: Kununuliwa kwa viuatilifu lita 106,000 za kudhibiti visumbufu vya milipuko ya viwavijeshi na lita 82,124 zimesambazwa katika Halmashauri 58 za Mikoa ya Manyara, Singida, Tabora, Katavi, Tanga, Geita, Simiyu, Shinyanga, Ruvuma, Kilimanjaro, Arusha na Dodoma; kununuliwa kwa kilo 2,000 za viuatilifu vya kudhibiti panya  katika mikoa ya Morogoro, Mtwara na Lindi pamoja na lita 300 kwa ajili ya kudhibiti nzi wa matunda katika mikoa ya Tanga, Dar es Salaam na Mwanza; kutoa mafunzo ya matumizi salama na sahihi ya viuatilifu kwa wakulima, wafanyabiashara, maafisa ugani, na wanyunyiziaji katika Kanda ya ziwa (Mwanza na Mara), Kanda ya nyanda za juu kusini (Mbeya na Iringa), Kanda ya mashiriki (Morogoro), Kanda ya kusini (Lindi na Mtwara) na Kanda ya kaskazini (Arusha). Jumla ya shilingi bilioni 34.57 zimetumika katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023.

 

(vi)    Kuimarisha Miundombinu ya Kuhifadhi Mazao ya Kilimo

Hatua iliyofikiwa ni Kuendelea na ukarabati wa ghala tano (5) ambapo utekelezaji katika ghala la Litisha umefikia asilimia 97.67, Lipaya (asilimia 21.58), Liula (asilimia 36.62), Hangangadinda (asilimia 57.80) na Lilondo A (asilimia 33.32) katika halmashauri za Songea na Madaba. Jumla ya shilingi milioni 67.74 zimetumika katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023.

 

(vii)  Upatikanaji wa Masoko ya Mazao ya Kilimo Ndani na Nje ya Nchi Hatua iliyofikiwa ni: Kuwezesha Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula - NFRA kununua mahindi tani 17,257.857 na mtama tani 1,036.457 na Bodi ya Mazao Mchanganyiko – CPB  kununua mahindi tani 34,484, alizeti tani 2,776, mafuta ghafi tani 85.82, mchele tani 1,797, ngano tani 277, maharage tani 406, mtama tani 3,035.06, maharage ya soya tani 393, maharage ya njano tani 30, korosho ghafi 523, na mpunga tani 7,065; na kuendelea na maandalizi ya kuanzisha mnada wa chai kwa njia ya mtandao ambapo utekelezaji wake umefikia asilimia 9. Jumla ya shilingi bilioni 17.31 zimetumika katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023.

 

(viii) Kuboresha Mifumo ya Kitaasisi, Bodi na Sheria 

 

(a)      Mifumo ya Kielektroniki ya kutoa huduma katika Sekta ya Kilimo Hatua iliyofikiwa ni: Kuanza kutumika kwa Mfumo wa M-Kilimo kwa kutoa huduma ya ushauri wa kilimo bora cha mazao mbalimbali ikiwemo kujibu kero zinazohusu utoaji wa mbolea ya ruzuku kwa wadau wa kilimo 4,548; kusajiliwa kwa wakulima 3,050,621 katika Mfumo wa Kielektroniki wa utoaji wa mbolea ya ruzuku; kuendelea na matumizi ya mfumo wa kutoa huduma za biashara ya mazao (Agriculture Trade Management Information System - ATMIS) ambapo jumla ya wakulima 500 wamesajiliwa na kupata huduma. 

 

(b)      Kuimarisha Mifumo ya Upatikanaji wa Mitaji katika Sekta ya Kilimo Hatua iliyofikiwa ni: Kuanzishwa kwa Mfuko wa Maendeleo ya Kilimo; kupungua kwa riba ya mkopo kwa wakulima na kuwa chini ya asilimia 10; kukamilika kwa mapitio ya sera ya mikopo katika mifuko ya pembejeo ambapo hatua za uidhinishwaji zinaendelea na Benki ya Maendeleo ya Kilimo (TADB) imetoa mikopo ya moja kwa moja (direct lending). Jumla ya shilingi milioni 17 zimetumika katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023.

 

(ix)       Kuimarisha Usimamizi wa Maendeleo ya Ushirika 

Hatua iliyofikiwa ni: kukamilika kwa ujenzi wa kiwanda cha TANECU (Newala) cha kubangua korosho chenye uwezo wa kubangua tani 3,500 za korosho kwa mwaka; na  kusajiliwa kwa vyama viwili (2) vya ushirika katika vikundi vidogo vya wakulima 120  wa mazao ya mboga na matunda katika mikoa ya Arusha, Mbeya na Njombe. Jumla ya shilingi bilioni 6.3 zimetumika katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023.

 

(b)         Mradi Na. 4499: Kudhibiti Sumukuvu 

Hatua iliyofikiwa ni: Kuendelea na ujenzi wa  ghala 14 katika mikoa 10 ya Kigoma, Mtwara, Dodoma, Mwanza, Ruvuma, Tabora, Manyara, Geita, Simiyu na Morogoro yenye uwezo wa kuhifadhi tani 21,500 za mahindi na karanga ambapo utekelezaji umefikia wastani wa asilimia 94; kuendelea na ujenzi wa Kituo Mahili cha Usimamizi wa Mazao ya Nafaka (Postharvest Centre of Excellence for Grains) katika Wilaya ya Kongwa ambapo utekelezaji umefikia asilimia 70; kuendelea na ujenzi wa Maabara ya Utafiti wa Magonjwa ya Mimea (Biological Control Unit) Kibaha mkoani Pwani ambapo umefikia asilimia 99; kutoa mafunzo kwa vijana 420 kupitia Chuo cha Mafunzo ya Ufundistadi (VETA) kuhusu utengenezaji wa vihenge vya chuma kwa ajili ya kuhifadhi mazao vijijini; kutoa mafunzo kwa wakulima 60,000 na wafanyabiashara 500 kuhusu udhibiti wa Sumukuvu. Jumla ya shilingi bilioni 17.0 zimetumika katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023.

 

(c)         Mradi Na. 4497: Kuongeza Uhifadhi wa Nafaka 

Hatua iliyofikiwa ni: Kukamilika kwa ujenzi wa vihenge (20) na maghala (4) katika wilaya za Babati, Mpanda na Sumbawanga; kuendelea na ujenzi wa vihenge 36 na ghala nne (4) kwa ajili ya kuongeza uwezo wa kuhifadhi mazao kufikia tani 501,000 katika vituo vya Makambako, Mbozi, Songea, Shinyanga na Dodoma ambapo umefikia wastani wa asilimia 85. Jumla ya shilingi milioni 647.7 fedha za ndani na shilingi bilioni 2.378 fedha za nje zimetumika katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023.

 

 

(d)         Mradi Na. 4427: Kuendeleza Kilimo na Uvuvi - AFDP 

Hatua iliyofikiwa: Kutolewa kwa mafunzo maalum ya kisayansi ya muda mfupi kwa watafiti 21 (breeders) kuhusu teknolojia ya mbegu kwenye mazao ya mahindi, maharage, alizeti na kunde; kukamilika kwa EIA katika miradi ya ujenzi wa miundombinu ya umwagiliaji katika mashamba ya Msimba (Kilosa), Kilimi (Nzega); ujenzi wa maabara ya mbegu katika mkoa wa Morogoro na katika mashamba ya utafiti ya TARI;  na kufanyika kwa usanifu wa ujenzi wa ofisi na ukumbi wa mafunzo, ghala za kuhifadhi mbegu, karakana na nyumba za wafanyakazi katika shamba la Kilimi (Nzega) na Msimba (Kilosa). Jumla ya shilingi bilioni 2.05 zimetumika katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023.

 

B.          Mifugo

 

Mradi Na. 4486: Programu ya Kuendeleza Sekta ya Kilimo Awamu ya Pili

(ASDP II)

 

(i)             Kuimarisha Afya ya Mifugo  

Hatua iliyofikiwa ni: Kukamilika kwa ujenzi wa majosho 97 na kuendelea na ujenzi wa majosho 160 kwenye mamlaka 83 za serikali za mitaa; kununuliwa kwa lita 52,560 za dawa ya kuogesha mifugo kwa ajili ya majosho 2644 na kusambazwa katika mikoa 25 ya Tanzania Bara kwenye mashamba ya Wizara na Taasisi zake; kuwezesha upatikanaji na usambazaji wa chanjo za mifugo dozi 679,827,610 za magojwa mbalimbali ya kipaumbele zikiwemo dozi 160,584,610 zilizozalishwa nchini na kuingizwa jumla ya dozi 519,243,000 kutoka nje ya nchi; kufanyika kwa michovyo 1,040,762,493 (ng’ombe ni 500,572,121 mbuzi 223,982,134, kondoo 250,774,038 na Punda 65,434,200) ya kuogesha mifugo ikilinganishwa na michovyo 446,997,857 iliyofanyika katika kipindi kama hicho mwaka 2022; Jumla ya shilingi bilioni 8.23 zimetumika katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023

 

(ii)           Kuimarisha Huduma za Ugani

Hatua iliyofikiwa ni: Ununuzi wa magari 13 kwa ajili ya uratibu wa ugani na pikipiki 1200 kwa ajili ya kurahisisha utoaji wa huduma za ugani katika Mamlaka za Serikali za Mitaa 184; kupatiwa mafunzo rejea kwa jumla ya maafisa ugani 515 ambapo 487 wa sekta ya umma na 28 wa sekta binafsi kutoka Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka ya Serikali za Mitaa katika kanda zote nane (8) nchini za ambapo jumla ya Halmashauri 119 zimefikiwa; kusajiliwa kwa maafisa ugani 3,018 kati ya 3,201 katika mfumo wa TEHAMA wa utoaji wa huduma za Ugani wa M- Kilimo; na kuendelea na taratibu za uanzishaji wa mashamba darasa  ambapo tararibu za ujenzi na ununuzi wa vifaranga 18,000,000 kwa mashamba darasa matano (5) ya ufugaji kuku imefanyika katika Mikoa  ya Ruvuma (Songea MC – 3) na Shinyanga (Kishapu - 2) kwa ajili ya vikundi vya wanawake vinavyojishughulisha na ufugaji wa kuku.

Shughuli nyingine zilizotekelezwa ni: kukamilika kwa ujenzi wa mabanda 24 kwa ajili ya unenepeshaji wa mifugo katika Vituo Atamizi vya Uwekezaji vya Vijana vya Mabuki (9); Buhuri Tanga (6); TALIRI Tanga (3) na Kikulula (6); kukamilika kwa ujenzi wa zisima viwili (2) vya maji na miundombinu ambata katika Kituo cha TALIRI Tanga na Mabuki, kuandaliwa kwa shamba lenye ukubwa wa ekari 56 la malisho bora kwa ajili ya unenepeshaji wa mifugo katika Vituo Atamizi; na kununuliwa kwa ng’ombe 2,222 kwa ajili ya utekelezaj wa vituo 8 vya vijana na wanawake 238 vya unenepeshaji wa ng'ombe kwa ajili ya kuuza katika viwanda vya kusindika nyama. Jumla ya shilingi bilioni 8.1 zimetumika hadi Aprili  2023. 

 

(iii)         Kuimarisha Huduma za Tafiti

Hatua iliyofikiwa ni: Kununuliwa kwa vifaa shamba vikiwemo matrekta (4), disc plough (3), harrow (2), bailer (1) na forage chopper (1) kwa ajili ya kuwezesha utafiti wa mifugo hususan utafiti wa malisho na kusambazwa katika Vituo vya Utafiti vya TALIRI Tanga, Kongwa, Mabuki, Uyole na Mpwapwa; na kununuliwa kwa mbuzi 2070 aina ya Newala (200) Boers (70), Pare White (225), Gogo White (900), Galla (225) na Sukuma (450) kwa ajili ya shughuli za kitafiti katika vituo vya utafiti wa mifugo; kuanzishwa kwa vituo nane (8) vya uwekezaji vya vijana vyenye uwezo wa kuchukua jumla ya vijana 240 kwa mwaka kwa lengo la kuwawezesha vijana kupata uzoefu katika kuanzisha na kuendeshammiradi ya ufugaji kibiashara, ambapo jumla ya vijana 238 wamesajiliwa katika vituo Atamizi vya LITA na TALIRI; Jumla ya shilingi milioni 800.7 zimetumika katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023

 

(iv)         Uboreshaji wa Mbari kwa ajili ya Uzalishaji wa Maziwa na Nyama 

Hatua iliyofikiwa ni: kununuliwa kwa ng’ombe wazazi 1,160 na kusambazwa katika Mashamba ya Serikali ya kuzalisha mitamba ya Mabuki (500), Sao Hill (307) na Kitulo (160); kununuliwa kwa madume bora 366 ya ng’ombe na kusambazwa kwa wafugaji kupitia vikundi vya wafugaji katika Halmashauri saba (7) za Chamwino

(50), Msalala (50), Maswa (50), Chato (50), Mvomero (40),Mkuranga (50), Buchosa (36) na Mkalama (40); na kuzalishwa kwa mitamba 606 na kuongezwa kwenye kundi la ng’ombe wazazi katika mashamba ya Serikali ya kuzalisha mitamba; Kuzalishwa kwa jumla ya dozi 116,558 za mbegu za mifugo katika kituo cha NAIC kwa ajili ya uhimilishaji; kununuliwa kwa Kimiminika cha Hewa Baridi ya Naitojeni lita 7,000 kwa ajili ya uhimilishaji ng’ombe katika kituo cha NAIC; kununuliwa kwa matrekta 3, Bailer 5, mower 5 na Hay rake 5 na kusambazwa katika mashamba ya Serikali ya kuzalisha mitamba kwa ajili ya kuzalisha na kuvuna malisho; kununuliwa kwa dozi 115,000 za vichochezi vya joto kwa ng’ombe ili kutekeleza shughuli za uhimilishaji katika kambi na kununuliwa kwa  hereni 150,000 kwa ajili ya kuwavalisha ng’ombe watakao himilishwa katika kambi; kuhimilisha ng’ombe 60,697 kupitia kambi za uhimilishaji. Jumla ya shilingi bilioni 6.9 zimetumika katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023.

(v)           Kuimarisha Miundombinu ya Masoko ya Mifugo na Mazao Yake

Hatua iliyofikiwa ni: Kuendelea na ujenzi wa minada minne (4) ya upili ya Mkongeni – Morogoro (70%), Majimoto - Katavi (10%), Utengule – Mbeya (40%) na Lugodalutale – Iringa (40%); kuendelea na ujenzi wa mnada mmoja (1) wa mpakani wa Randa – Mara (20%); na kuendelea na ujenzi wa  vituo 10 vya kukusanyia maziwa vya Kwemakame (65%) na Msomera (80%) – Tanga, Malimbika  - Dar es Salaam (80%), Magogoni  – Morogoro (40%), Lukani – Kilimanjaro (60%), Ngaramtoni – Arusha (60%), Komunge – Mara (27%), Maswa – Simiyu (15%), Karagwe – Kagera (60%) na Mkambako – Njombe (65%).

 

Shughuli nyingine zilizotekelezwa ni: Ukarabati wa minada miwili  (2) ya upili ya Weruweru – Kilimanjaro (98%) na Meserani (98%), ukarabati wa minada miwili (2) ya awali ya Nyanguge (98%) na Buhungulwa – Mwanza (98%); kuendelea na ujenzi wa minada 12 ya awali ya Msomera – Tanga (97%), Lupa – Mbeya (96%), , Kibinda – Simiyu (98%), Nzoka – Songwe (98%), Kilyamatundu – Rukwa (50%), Sikonge (97%) na Urambo (97%) – Tabora na Bukombe (45%) na Kasamwa (40%) – Geita Gwandi (45 %) na Huzi ( 20%) – Dodoma na Kitinku – Singida (20%); kuendelea na ujenzi wa minada miwili (2) ya upili ya  Mhunze – Shinyanga (98%) na Wasso – Arusha (75%); na kununuliwa kwa mizani 82 kusambazwa na kuisimikwa katika minada ya awali, upili na mpakani. Jumla ya shilingi bilioni 3.1 zimetumika katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023.

 

(vi)         Kuimarisha Unywaji wa Maziwa Shuleni

Hatua iliyofikiwa ni: kuendelea na utekelezaji wa Mpango wa Unywaji Maziwa Shuleni ambapo idadi ya shule za msingi zinazoshiriki ziliongezeka kutoka 39 hadi shule 130 na idadi ya shule za sekondari nne (4) zimejiunga na mpango huo na kufanya jumla ya shule zote nchini zinazoshiriki mpango huo kufikia 134; kuongezeka kwa vituo vya kuuzia maziwa katika Ofisi za Serikali kutoka vituo 10 na kufikia vituo 18 katika Mikoa ya Dodoma (9), Mbeya (4), Katavi (1), Tanga (1) na Dar es salaam (3). Jumla ya shilingi milioni 56.1 fedha za nje zimetumika katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023

 

(vii)        Kuimarisha Huduma za Maji, Malisho na Vyakula vya Mifugo

Hatua iliyofikiwa ni: Kukamilika kwa ujenzi wa mabwawa ya Kimambi na Matekwe – Lindi, na Mhanga (Singida); kukamilika kwa uchimbaji wa kisima cha Matanzi (Pwani), Makatapola (Iringa) na Lwami (Kilimanjaro); kununuliwa kwa Mowers tatu (3), Bailers mbili (2), Hay rakes mbili (2), Desktop Computers nne (4) na Printers  mbili (2) na kusambazwa katika mashamba mawili ya Serikali ya kuzalisha mbegu za malisho na malisho ya Vikuge (Kibaha) na Langwira (Mbalali); na kukabidhiwa kwa Mkandarasi wa kusafisha maeneo kwa ajili ya kupanda malisho hekta 175 katika shamba la kuzalisha malisho na mbegu za malisho  la Vikuge.

Shughuli nyingine zilizotekelezwa ni: kuendelea na  ujenzi wa mabwawa 11 ya

Oloirieni (10%) na Naalaram (90%) – Arusha, Kwekikwembe (35%) na Msomera (35%)  – Tanga, Kongwa – Morogoro (10%), Vinyenze – Pwani (10%), Chang’ombe – Mbeya (10%), Kihumbo (20%) na Bukabwa (10%) – Mara, na Kaiwang (05%) na Leralumo (05%) – Manyara na Msaginia – Katavi (60%); kuendelea na uchimbaji wa kisima cha Muhukulu Lilai (Ruvuma) (80%), Kitaraka – Singida (5%), Kapele - Kasinde – Songwe ( 5%) na Maswa – Simiyu (70%); kuingiza umeme na kuendelea na ujenzi wa mfereji wa umwagiliaji ambapo ujenzi umefikia asilima 80 katika shamba la kuzalisha malisho na mbegu za malisho la Langwira; kununuliwa kwa tani 8.56 (Rhodes na Buffel tani 6.105, Juncao tani 2.45) za mbegu za malisho na vipando vya miti malisho 18,025 kutoka mashamba ya Serikali na binafsi na kusambazwa kwa wafugaji kwa vikundi vya uanzishwaji wa  mashamba darasa 100 yenye ukubwa wa ekari 520 katika Mamlaka za Serikali za Mitaa 44. Jumla ya shilingi bilioni 1.5 zimetumika katika kipindi cha Julai hadi Aprili  2023.

 

(viii)      Kuboresha Vyuo vya Mafunzo ya Mifugo

Hatua iliyofikiwa ni: Kuendelea na ujenzi wa kumbi mbili (4) za mihadhara zenye uwezo kuchukua wanafunzi 250 kila moja katika kampasi za Mpwapwa (1), Morogoro (1) na Mabuki (2) ambapo ujenzi umefikia asilimia 30; kuendelea na ujenzi wa hosteli mbili (2) zenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 216 kila moja katika kampasi za Morogoro na Mpwapwa ambapo ujenzi umefikia asilimia 30; na kufungwa kwa samani katika kumbi mbili (2) za mihadhara katika Kampasi ya Tengeru. Jumla ya shilingi milioni 400 zimetumika katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023.

 

C.          Uvuvi

(a)         Mradi Na. 4701:  Mradi wa Kikanda wa Usimamizi Shirikishi wa Rasilimali za Uvuvi Kusini Magharibi mwa Bahari ya Hindi – (South West Indian Ocean Fisheries Governance and Shared Growth – SWIOFish)

Hatua iliyofikiwa ni: Kukamilika kwa ujenzi wa Maabara ya Utafiti wa Uvuvi katika kituo cha TAFIRI - Dar es Salaam; na kuendelea na ujenzi wa jengo la utawala la ofisi ya Hifadhi ya Bahari na Maeneo Tengefu - Mafia ambapo ujenzi umefikia asilimia 90; kuendelea na ujenzi wa awamu ya kwanza ya Kituo cha Ukuzaji Viumbe Maji Bahari – Kunduchi, Dar es Salaam na ununuzi wa samani za ofisi za maabara ya TAFIRI – Dar es Salaam. Jumla ya shilingi bilioni 3.49 zimetumika katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023.

 

(b)         Mradi Na. 4486: Programu ya Kuendeleza Sekta ya Kilimo (ASDP II)

(i)             Kuimarisha na Kuendeleza Ulinzi wa Rasilimali za Uvuvi na Mazingira  

Hatua iliyofikiwa ni: kufanyika kwa kaguzi za jumla ya siku kazi 4,743 za operesheni maalum na doria ambazo ni sawa na asilimia 60.8 ya lengo la mwaka la siku kazi 7,800 katika Ziwa Victoria,Tanganyika, Nyasa na Bahari ya Hindi;; kujengwa na kupatiwa samani kwa Ofisi ya Maeneo ya Pamoja ya Usimamizi wa Uvuvi (CFMA) katika Kijiji cha Karema, Wilaya ya Tanganyika (Katavi); kukamilika kwa ujenzi wa ofisi moja (1) ya ulinzi na usimamizi wa rasilimali za uvuvi ya Busega (Simiyu); kuendelea na ujenzi wa ofisi mbili (2) za ulinzi na usimamizi wa rasilimali za uvuvi za Nyakalilo (Sengerema) ambapo utekelezaji umefikia asilimia 60 na Sota – Rorya (asilimia 50); na kununuliwa kwa pikipiki 50 za maafisa ugani wa uvuvi kwa ajili ya kuimarisha ulinzi na usimamizi wa rasilimali za uvuvi. Jumla ya shilingi milioni 785.0 zimetumika katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023.

 

(ii)           Kujenga na Kuimarisha Miundombinu ya Uvuvi (Mialo na Masoko)

Hatua iliyofikiwa ni: kuendelea na ujenzi ya mialo miwili (2) ya Chifunfu/Kijiweni (Sengerema) na Igabiro (Bukoba) ambapo utekelezaji umefikia asilimia 90 kwa kila mwalo; kuendelea na usanifu wa ujenzi wa soko la Tunduma (Momba); kuendelea na ujenzi wa mashamba darasa mawili (2) kwa lengo la kutoa huduma za ugani katika Halmashauri za Moshi na Mwanga. Jumla ya shilingi  245.3 zimetumika katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023.

 

(iii)         Kuimarisha Wakala wa Elimu na Mafunzo ya Uvuvi (FETA)

Hatua iliyofikiwa ni: Kukamilika kwa ukarabati mdogo wa nyumba tatu (3) za wafanyakazi katika Kampasi ya Nyegezi (Mwanza) na Mbegani (Bagamoyo); kuendelea na ujenzi wa kumbi mbili (2) za mihadhara katika Kampasi ya Nyegezi (Mwanza) ambapo utekelezaji umefikia asilimia 75, ujenzi wa maabara umefikia asilimia 60 na ukarabati wa kitotoleshi katika Kampasi ya Gabimori – Mara (asilimia 15) na ujenzi wa maabara katika Kampasi ya Mikindani – Mtwara (asilimia 40); Jumla ya shilingi milioni 217.4 zimetumika katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023.

 

(iv)         Kuimarisha Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi Tanzania (TAFIRI)

Hatua iliyofikiwa ni: Kukamilika kwa utafiti wa uwingi, bioanuwai na mtawanyiko wa samaki katika Ziwa Tanganyika ambapo jumla ya aina 7 za samaki na sampuli 639 zilikusanywa na kusafirishwa kwenda Uingereza; kufanya utafiti wa majaribio ya matumizi ya mitego/vyungu katika uvuvi wa pweza Tanzania ili kuwezesha uvuvi endelevu wa pweza; kufanya utafiti wa kufuatilia ongezeko la tindikali baharini (ocean acidification) na aina za kaboni (sea water carbonate species) katika maji ya Pwani ya Tanzania. Jumla ya shilingi milioni 599.2 zimetumika katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023.

 

 

 

 

(c)         Mradi Na. 4486: Programu ya Kuendeleza Sekta ya Kilimo (ASDP II ) na Mradi Na. 4429: Programu ya Kuendeleza Kilimo na Uvuvi 

Kujenga na Kukarabati Miundombinu ya Ukuzaji Viumbe Maji

Hatua iliyofikiwa ni: kukamilika kwa ukarabati wa mabwawa makubwa matatu (3) na madogo sita (6) kwa kuotesha nyasi na kujenga mifumo ya kuingiza na kutoa maji katika Kituo cha Rubambagwe (Geita); kukamilika kwa matanki ya maabara (Lab tank), nursery ponds, reservoir na tower pamoja na kuendelea na ujenzi wa Kitotoleshi ambapo utekelezaji umefikia asilimia 60 katika kituo cha kuendeleza Ukuzaji Viumbe Maji Bahari Ruvula – Mtwara; kuendelea na upanuzi wa kituo cha ukuzaji viumbe maji na ujenzi wa ghala moja (1) ambapo utekelezaji umefikia asilimia 60; kuendelea na ujenzi wa Kitotoleshi cha vifaranga vya samaki na upanuzi wa kituo cha Ruhila (Songea) utekelezaji umefikia asilimia 22; kuendelea na upanuzi wa kituo cha ukuzaji viumbe maji na ujenzi wa ghala moja (1) ambapo utekelezaji umefikia asilimia 60; kuendelea na ujenzi wa kitotoleshi, ukarabati na upanuzi wa kituo cha ukuzaji viumbe maji cha Nyengedi – Lindi (asilimia 25); na kuendelea na ujenzi wa mashamba darasa sita (6) ya Ufugaji wa Samaki katika Halmashauri za wilaya za Kongwa, Iringa, Njombe, Songea, Tandahimba  na Ruangwa ambapo utekelezaji umefikia asilimia 15; kutolewa kwa mafunzo kwa vitendo yanayojulikana kama ATAMIZI kwa vijana 200 wanaojishughulisha na uvuvi pamoja na ukuzaji viumbe maji, ili kuzalisha vijana watakaoshiriki katika usimamizi wa rasilimali za uvuvi na utoaji wa huduma za ugani; kukamilika kwa taratibu za ununuzi wa boti za uvuvi 158 ikiwa ni awamu ya kwanza ya ununuzi wa boti 160 zilizotarajiwa kununuliwa kwa ajili ya kukopesha wavuvi. Jumla ya shilingi bilioni 1.12 zimetumika katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023. 

 

(d)         Mradi Na. 4703: Ufufuaji wa Shirika la Uvuvi Tanzania (TAFICO) Hatua iliyofikiwa ni: Kukamilika kwa ukarabati wa Jengo la Utawala la RAS MKWAVI (Block B); na kuandaa na kuhuisha Bussiness Model na Mpango wa Biashara wa miradi itakayotekelezwa na Shirika. Jumla ya shilingi milioni 29.1 zimetumika katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023. 

 

2.3.3.3. Uchimbaji wa Madini, Vito vya Thamani na Gesi Asilia

 

(i)           Mradi Na. 1119: Usimamizi Endelevu wa Rasilimali za Madini (Sustainable Management of Mineral Resources Project - SMMRP)

Hatua iliyofikiwa ni: Kukamilika kwa ujenzi wa vituo vitatu (3) vya umahiri vya Songea, Chunya na Mpanda; kununuliwa na kusimikwa (commissioning) kwa vifaa vya utafiti wa kisayansi (geoscience) na vifaa vya maabara na uchunguzi kwa  ajili ya Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania – GST; kununuliwa kwa mitambo ya uchorongaji (mitambo 5 kwa ajili ya wachimbaji wadogo na mitambo 2 ya uzalishaji wa mkaa mbadala) na utengenezaji wa mkaa unaotokana na makaa ya mawe - STAMICO; na kuendelea na ujenzi wa jengo la kuhifadhia sampuli za miamba choronge eneo la Kizota - Dodoma ambapo utekelezaji wake umefikia asilimia 75. Shughuli nyingine iliyotekelezwa ni kununuliwa kwa mawe mawili (2) makubwa ya madini ya Tanzanite yenye jumla ya uzito wa kilo 5.22 kutoka kwa mchimbaji mdogo. Jumla ya shilingi bilioni 3.5 zimetumika katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023.

 

(ii)         Mradi Na. 1120: Kituo cha Jemolojia Tanzania (Tanzania Geomological Centre)

Hatua iliyofikiwa ni: Kuwawezesha watumishi tisa (9) wa Kituo cha Jemolojia Tanzania (TGC) kupata mafunzo ya muda mfupi na mrefu ndani na nje ya nchi (Thailand, China na India) kuhusu masuala ya uongezaji wa thamani madini. Jumla ya shilingi milioni 716.34 zimetumika zimetumika katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023.

 

2.3.3.4. Huduma

 

A.          Maliasili na Utalii

Hatua iliyofikiwa ni: kuongezeka kwa idadi ya watalii kutoka watalii 922,692 mwaka 2021 hadi kufikia watalii 1,454,920 mwaka 2022 sawa na ongezeko la asimilia 57.7; kuongezeka kwa idadi ya watalii wa ndani kutoka watalii 788,933 mwaka 2021 hadi 2,363,260 mwaka 2022 sawa na ongezeko la asilimia 199.5; Tanzania Kuendelea Kutambulika Kimataifa; Kupandishwa Hadhi Maeneo ya Hifadhi na Misitu; Kuimarika kwa Ulinzi wa Rasilimali za Wanyamapori na Misitu; kuimarika kwa utalii wa urithi wa utamaduni na malikale; kuendeleza Programu za Upandaji Miti na Mashamba ya Miti; na kuongezeka kwa masoko na kiwango cha mazao ya nyuki yanayouzwa nje ya nchi.

 

(a)         Mradi Na. 5203: Mradi wa Usimamizi wa Maliasili na Kuendeleza Utalii Kanda ya Kusini (Resilient Natural Resources Management for Tourism and Growth Project - REGROW) 

Hatua iliyofikiwa ni: ukamilishaji na utiaji saini mikataba nane (8) ya ujenzi wa miundombinu mbalimbali ikiwemo ujenzi wa viwanja vya ndege sita (6) katika hifadhi za Taifa za Ruaha (3), Nyerere (2) na Mikumi (1) na ujenzi wa malango (3), vituo vya kutolea taarifa (2), umeme, kambi (4) za utalii, vituo vitatu (3) vya askari, kituo cha ikolojia (1), hosteli ya wanafunzi (1), malazi ya madereva wa utalii (1), mfumo wa maji safi, na canopy walkway katika hifadhi za Taifa za Nyerere, Ruaha, Udzungwa na Hifadhi ya Mazingira Asilia ya Kilombero. Vilevile, ununuzi wa matrekta saba (7) pamoja na viambata vyake 23 kwa lengo la kuimarisha miundombinu ya barabara katika maeneo ya hifadhi; kuwezesha vijana 120 kutoka wilaya za Kilolo, Iringa, Mvomero, Chamwino na Rufiji kupata mafunzo ya mbinu za kudhibiti wanyamapori wakali na waharibifu; kuwezesha vikundi 159 vyenye jumla ya wanachama 3,816 kwa kuwapatia fedha mbegu jumla ya Shilingi 1,453,272,934 katika vijiji 15 vya awamu ya kwanza vinavyopakana na hifadhi za Taifa Ruaha, Nyerere, Mikumi na Udzungwa; na kuwezesha ufadhili wa masomo ya fani mbalimbali kwa vijana 582 kutoka vijiji 15 katika Wilaya saba (7) za Kilombero, Kilosa, Morogoro, Iringa, Kilolo, Mvomero na Chamwino. Jumla ya shilingi bilioni 29.99 zimetumika katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023. 

 

(b)         Mradi Na. 4812: Mradi wa Kupambana na Ujangili na Biashara Haramu ya Nyara 

Hatua iliyofikiwa ni: kuandaa Mkakati wa Kitaifa wa Usimamizi wa Maeneo ya Jumuiya za Hifadhi za Wanyamapori 2023-2033; kuwezesha kufanyika kwa doria za ki-intelijensia na ushirikiano na nchi jirani katika kanda 10 zilizowezesha kukamatwa kwa vipande 52 vya meno ya tembo, nyamapori aina 101 mbalimbali na majangili 70 ambao wamechukuliwa hatua za kisheria; kuwezesha watumishi 319 kupata mafunzo katika masuala ya intelijensia, operesheni na uendeshaji mashtaka; kufanya tathmini kwa vikundi 155 vyenye wajumbe 2,726 vilivyopo katika mfumo ikolojia wa Ruaha-Rungwa ili kubaini vikundi vinavyokidhi vigezo vya kuwezeshwa na vikundi 45 vilikidhi vigezo na kupewa mafunzo ya ujasiriamali na kuwawezesha kuanzisha umoja wa wafugaji nyuki Manyoni na kuwezesha kuandaliwa kwa Mwongozo wa pamoja wa kubadilishana taarifa za kiintelijensia, uendeshaji wa operesheni za kupambana na ujangili na usimamizi wa wasiri na kuandaa mpango wa kujenga uwezo wa kitaasisi wa kupambana na ujangili na biashara haramu ya nyara. Jumla ya shilingi bilioni 12 zimetumika katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023.

 

(c)         Mradi Na. 4647: Panda Miti Kibiashara (Private Plantation and Value Chain in Tanzania)

Hatua iliyofikiwa ni: kuwezesha kutoa mafunzo kwa viongozi 296 wa Vikundi vya Upandaji miti  ya namna ya kusimamia na kuendesha vikundi; kutoa mafunzo kwa wakulima wa miti 5,689; kutoa misumeno 335 ya kupogolea miti kwa Vikundi  80 vya Upandaji miti ; utambuzi wa wawekezaji 1,335; kuwezesha matukio 768 ya huduma za ugani ambapo wakulima 12,354 walishiriki; kuandaa Mipango ya Usimamizi wa Mashamba ya wakulima 603; kutoa vifaa vya kupambana na majanga ya moto (fire beaters 393 na knapsack fire sprayers 36); uanzishwaji wa Kamati za usimamizi wa moto za vijiji 80 zenye jumla ya watu 2,612; kuanzisha vikosi vya kupambana na moto vyenye jumla ya watu 1,284; kutoa pikipiki 14 katika kongani za Njombe (7), Mafinga (4) na Makete (3) kwa ajili ya kuwezesha utoaji wa huduma za ugani kwenye vijiji 80; na kuwezesha vikundi 39 kuandaa maandiko ya biashara kwa ajili ya kuomba mikopo yenye thamani ya Shilingi 726,335,500. Jumla ya shilingi milioni  959.5 zimetumika katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023.

 

(d)         Mradi Na. 4651: Mradi wa Kuwezesha Mnyororo wa Thamani wa Mazao ya Nyuki - BEVAC

Hatua iliyofikiwa ni: kukarabati ofisi ya mradi iliyopo Pemba; kununua magari matatu (3) na pikipiki 20 kwa ajili ya maafisa; kutoa mafunzo ya mbinu za ufugaji bora wa nyuki kwa vyama vya ushirika 19 vyenye jumla ya wafugaji nyuki 1,204; kukamilisha taratibu za maandalizi ya ujenzi wa bweni la wasichana lenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 350 katika Chuo cha Mafunzo ya Ufugaji Nyuki; kuwajengea uwezo viongozi wa vyama vya ushirika 19 vya ufugaji nyuki; kuwezesha ufanyikaji wa mikutano katika vijiji 297 kwa lengo la kuhamasisha jamii kutenga maeneo kwa ajili ya kufugia nyuki; kuwaunganisha wafanyabiashara sita (6) wanaouza asali nje ya nchi na wafugaji nyuki 296 na vikundi 29; kutoa mafunzo kwa makampuni 30 kuhusu utayari wa usafirishaji wa mazao ya nyuki nje ya nchi; kuwezesha kampuni 10 za uuzaji na usafirishaji wa asali nje ya nchi kupata cheti cha ubora kitakachowezesha kampuni hizo kuuza asali katika masoko mbalimbali duniani. Jumla ya shilingi bilioni 6.21zimetumika katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023.

 

B.          Utamaduni, Sanaa na Michezo

 

(i)           Mradi Na. 6293: Programu ya Urithi wa Ukombozi wa Bara la Afrika

Hatua iliyofikiwa ni: Kukarabatiwa kwa jengo lililokuwa Makao Makuu ya Ofisi ya Kamati ya Ukombozi ya OAU ambapo utekelezaji umefikia asilimia 95;  na kutoa elimu ya uzalendo wa kuenzi na kuhifadhi kumbukumbu za harakati za ukombozi wa Bara la Afrika kwa kuwafikia zaidi ya watu 2,000,000 Afrika kupitia mitandao ya kijamii, makongamano, matamasha, Makala jongefu na mijadala bayana.  Jumla ya shilingi milioni 515 zimetumika katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023.

 

(ii)         Mradi Na. 4353: Ukarabati wa Chuo cha Sanaa Bagamoyo (TaSUBa) Hatua iliyofikiwa ni: Kuendelea na hatua za ununuzi wa wakandarasi kwa ajili ya kuanzisha kituo cha redio na televisheni; kununuliwa kwa vifaa vya kufundishia na kujifunzia; kuendelea na ukarabati wa majengo; na kufanyika kwa Tamasha la 41 la Kimataifa la Utamaduni na Sanaa Bagamoyo. Jumla ya shilingi milioni 550 zimetumika katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023.

 

(iii)       Mradi Na. 6502: Mfuko wa Utamaduni na Sanaa Tanzania

Hatua iliyofikiwa ni: Kutolewa mikopo kwa awamu mbili (2) yenye thamani ya shilingi bilioni 1.07 kwa wasanii na wadau 45 waliokidhi vigezo. Jumla ya shilingi bilioni 1.07 zimetumika katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023.

 

(iv)       Mradi Na. 6385: Ujenzi wa Chuo cha Michezo  cha Malya

Hatua iliyofikiwa ni: Kuendelea na ujenzi wa hosteli ya wanafunzi ambapo utekelezaji umefikia asilimia 27; na kukamilika kwa michoro na kutangazwa kwa zabuni ya ujenzi wa Kituo cha Kukuza na Kuendeleza Vipaji (Sports Academy). Jumla ya shilingi bilioni 1.3 zimetumika katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023. 

 

(v)         Mradi Na. 6523: Ujenzi wa Eneo Changamani la Michezo Dar es Salaam

Hatua iliyofikiwa ni: Kupatikana kwa Mshauri Elekezi wa ukarabati wa viwanja vya Benjamini na Uhuru na kuandaliwa kwa makadirio ya majenzi (BOQ) na michoro; na kukamilika kwa ukarabati mdogo wa miundombinu ya eneo changamani la michezo. Jumla ya shilingi milioni 687 zimetumika katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023.

 

(vi)       Mradi Na. 6521 - Kuimarisha Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA) na Kukiuza Kiswahili Kikanda na Kimataifa

Hatua iliyofikiwa ni: Kushiriki na kutoa mada ya ubidhaishaji wa Kiswahili katika Kongamano la Jumuiya ya Afrika Mashariki (JAMAFEST) lililofanyika nchini Burundi na Kongamano la Chama cha ukuzaji wa Kiswahili Duniani (CHAUKIDU) lililofanyika Chuo Kikuu cha HOWARD nchini Marekani; kufanyika kwa maadhimisho ya kwanza ya Siku ya Kiswahili Duniani; kuanzishwa kwa vituo 30 vya kufundisha Kiswahili katika Balozi za Tanzania Abu Dhabi, Uholanzi, Zimbabwe, Cuba, Ufaransa na Saudi Arabia na ndani ya nchi; na kuendesha darasa la kwanza la Kiswahili nchini Malawi katika Chuo Kikuu cha Hebron. Jumla ya shilingi milioni 300 zimetumika katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023.

 

(vii)      Mradi Na. 6527 - Ujenzi na Uimarishaji wa Miundombinu ya Michezo katika Shule Maalumu  za Michezo

Hatua iliyofikiwa ni: Kufanyika kwa tathmini ya shule 56 za sekondari zilizoteuliwa kuwa shule maalum za michezo; kuanza kwa maboresho ya miundombinu ya michezo katika shule 56 za Sekondari katika mikoa ya Tabora, Tanga, Arusha, Pwani, Dodoma na Mtwara; na kuendelea na maandalizi ya makadirio ya majenzi (BOQ) ili kutangaza zabuni na kumpata Mkandarasi.

 

(viii)    Mradi Na. 6504 - Ujenzi wa Vituo vya Mazoezi na Kupumzikia Wananchi Pamoja na Mradi wa Ujenzi wa Sports Arena (Dar es Salaam  na Dodoma)

Hatua iliyofikiwa ni: Kupatikana kwa mkandarasi wa ujenzi wa vituo vya mazoezi na kupumzikia wananchi katika mikoa ya Dar es Salaam na Dodoma ambapo mkandarasi yupo katika hatua za awali za kuandaa vifaa (Mobilization Stage); na kupatikana kwa eneo la ekari 12 kwa ajili ya ujenzi wa Arena ya Michezo Dar es Salaam lililopo Kawe, Tanganyika Packers. Jumla ya shilingi bilioni 5.8 zimetumika katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023.

 

C.          Sekta ya Fedha, Biashara na Masoko

 

(i)           Benki ya Maendeleo TIB

Hadi kufikia Aprili 2023, Benki ya Maendeleo TIB ilikuwa imetoa mikopo yenye thamani ya shilingi bilioni 370.60 ambayo ipo kwenye sekta mbalimbali za kiuchumi na kijamii zikiwemo kilimo miradi sita (shilingi bilioni 90.85), ujenzi miradi minne (shilingi bilioni 28), elimu miradi miwili (shilingi bilioni 5.19), umeme miradi miwili (shilingi bilioni 6.64), Taasisi za fedha mradi mmoja (shilingi bilioni 0.32), uzalishaji miradi minne (shilingi bilioni 41.38), Madini miradi miwili (shilingi bilioni 97.3), Utalii miradi minne (shilingi bilioni 77.78), Mawasiliano na Usafirishaji mradi mmoja (shilingi bilioni 1.86), Mikopo binafsi mia moja na thelathini na nane (shilingi bilioni 7.02), maji mijini miradi 6 (shilingi bilioni 14.25) na programu ya maji vijijini (shilingi bilioni 4.18).  Kati ya miradi hiyo, asilimia 91.32 ni miradi ya sekta binafsi na asilimia 8.68 ni miradi ya sekta ya Umma.

 

(ii)         Benki ya Maendeleo ya Kilimo – TADB 

Hadi kufikia Disemba 2022 TADB ilikuwa na mtaji (total assets) wa shilingi bilioni 454.351 ikiwa ni ongezeko la asilimia 26 kutoka shilingi bilioni 360.502 zilizokuwepo katika kipindi kama hicho mwaka 2021 kwa hesabu zilizokaguliwa. Hata hivyo, katika kipindi kilichoishia Machi, 2023 mtaji ulipungua kutoka shilingi bilioni 454.351  uliokuwepo Disemba, 2022 hadi kufikia shilingi bilioni 441.039 Machi, 2023. Aidha, katika robo ya kwanza iliyoishia Machi, 2023 TADB ilitoa mikopo ya jumla ya shilingi bilioni 182.87 kwenye mnyororo wa thamani wa mazao ya viwandani (Kahawa, Pamba na Mkonge); mazao ya mbogamboga na matunda (Parachichi, Vanilla, na Zabibu); uzalishaji wa mbegu za mafuta ya chakula (Alizeti na Chikichi); uzalishaji wa nafaka mbalimbali (Mahindi, Mpunga na Maharage) pamoja na ufugaji wa ng’ombe wa maziwa, ng’ombe wa nyama, kuku na samaki. Vilevile, kufikia Machi, 2023 TADB kupitia mfuko wa dhamana kwa wakulima wadogo (SCGS), ulitoa dhamana za jumla ya  shilingi bilioni 56.548 kupitia benki kumi na tano (15) washirika katika mnyororo wa thamani wa mazao mbalimbali katika mikoa 24 ya Tanzania bara na kufanya kiasi cha dhamana kilichotolewa kwa wakulima wadogo kufikia shilingi bilioni 181.567 tangu mfuko ulipoanza mwaka 2018.

 

(a)         Huduma za Bima 

Hatua iliyofikiwa ni: Kuandikishwa na kutolewa kwa leseni 1,196 zikijumuisha Kampuni za bima 32, Kampuni za bima mtawanyo (Reinsurance) 3, madalali wa bima mtawanyo sita (6), madalali wa bima 103, wakala wa bima 1200 na benki wakala (bancansurance) 28, watoa huduma ya bima kidigitali tisa (9) , watakwimu bima wanne (4), Wachunguzi binafsi wa bima (Private Insurance investigators) watatu (3) na wakadiriaji hasara wa bima 56; Kufanya ukaguzi kwa watoa huduma za bima ambao ni makampuni ya bima 18, matawi ya kampuni 18 za bima, madalali wa bima 8; benki wakala 8 na mawakala wa bima 68; kufanya ukaguzi wa bima kwa vyombo vya moto 33,160,000; na kupokea malalamiko 284 ambayo yalishughulikiwa ambapo malalamiko 68 yalipatiwa ufumbuzi na kulipwa, 22 yalikataliwa, 11 yalipelekwa mahakamani, 18 yalipelekwa kwa Msuluhishi wa Migogoro ya Bima na 135 bado yanaendelea katika hatua mbalimbali za uchunguzi.  (b)       Huduma Ndogo za Fedha

Hadi kufikia Machi, 2023, Benki Kuu ya Tanzania ilitoa jumla ya leseni 1,187 kwa Watoa huduma Daraja la Pili, na leseni 780 kwa Vyama vya Ushirika wa Akiba na Mikopo, kusajili Vikundi 37,937 vya Kijamii vya Huduma Ndogo za Fedha. Aidha, Wizara ya Fedha na Mipango imetoa mafunzo kwa waratibu wa biashara ya huduma ndogo za fedha 115 kutoka katika mikoa 13 mwezi Mei, 2023. Vilevile, hadi kufikia Machi, 2023 Watoa huduma ndogo za fedha Daraja la Pili wamekopesha mikopo yenye thamani ya shilingi billioni 870 kwa wajasiriamali wadogo na wa kati nchini.

 

(c)           Huduma Jumuishi za Fedha

Hatua iliyofikiwa ni: kuanzishwa kwa idara ya huduma jumuishi za fedha ndani ya Benki Kuu ili kuchochea mikakati itakayoongeza ujumuishaji wa kifedha nchini na kutoa elimu ya fedha kwa umma kwa kushirikiana na wadau wa sekta binafsi na Serikali ikiwemo kujumisha elimu ya fedha katika sera na mitaala ya elimu ya awali, sekondari, vyuo vya kati na vyuo vikuu nchini. Aidha, katika kuimarisha ulinzi kwa mlaji wa huduma za fedha, Benki Kuu imeandaa rasimu ya Mpango wa Kumlinda Mlaji wa Huduma za Fedha (Bank of Tanzania Financial Consumer Protection Framework). Vilevile, utaratibu wa kuweka mazingira ya kufanya majaribio ya teknolojia za fedha (regulatory sandbox) ili kutambua na kuchochea ubunifu wa aina mbalimbali katika masuala ya fedha unaandaliwa.

 

(d)          Mradi Na. 6251: Programu ya Maboresho ya Usimamizi wa Fedha za Umma (PFMRP)

Hatua iliyofikiwa ni: Kukamilika kwa uandaaji wa Mwongozo wa Ufuatiliaji na Tathmini (Monitoring and Evaluation Guideline) kwa Ofisi ya Msajili wa Hazina pamoja na taasisi anazozisimamia; kufunga na kuunganishwa kwa mfumo wa MUSE na mifumo sita (6) ambayo ni GePG, PlanRep–TR, PlanRep – LGA, ERMS na mifumo ya benki za biashara (CRDB na NMB); kuunganishwa na kufungamanishwa kwa Mfumo wa Ufuatiliaji na Uchambuzi wa Taarifa za Fedha na mifumo ya PlanRep - TR na MUSE; kuendelea na uundaji wa mfumo wa ukusanyaji wa gawio na fedha taslim kutoka Taasisi na Mashirika ya Umma; kuendelea na ujenzi wa Mfumo wa Usimamizi wa Ununuzi wa Umma kwa njia ya mtandao (NeST); Kuandaa Mpango Mkakati wa Utekelezaji wa Programu ya Maboresho ya usimamizi wa Fedha za Umma Awamu ya Sita (PFMRP VI); Kuhuisha Mfumo wa Ukusanyaji wa Mapato katika Serikali za Mitaa (TAUSI) na kuhuishwa kwa Mfumo wa Kihasibu wa Kuripoti Mapato na Matumizi katika Vituo vya Kutolea Huduma (FFARS); Kuandaa Mfumo wa Kusimamia Viashiria Hatarishi (GERMIS); Kuandaa mahitaji ya Mfumo wa Huduma Ndogo za Kifedha; kukamilika kwa ukarabati wa Ofisi za Hazina Ndogo katika mikoa Kigoma, Kagera na Ruvuma. Jumla ya shilingi  bilioni 14.8 zimetumika katika kipindi Julai, 2022 na Aprili, 2023.

 

 

(e)           Mradi Na. 6244: Miradi ya Kimkakati ya Kuongeza Mapato katika Halmashauri

Hatua iliyofikiwa ni: Kuendelea na miradi 26 katika Halmashauri 23 ambapo miradi 19 imefikia hatua ya ukamilishaji (miradi 12 imeanza kutoa huduma) na miradi saba (7) ipo katika hatua mbalimbali za utekelezaji. Jumla ya shilingi bilioni 16.94 zimetumika katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili 2023.

 

D.          Masoko

(a)         Soko la Bidhaa Tanzania – TMX

Hatua iliyofikiwa ni: kutoa elimu, kuhamasisha wadau mbalimbali juu ya manufaa ya Soko la Bidhaa na kuuza Mazao. Soko liliuza Kahawa (Kagera) ambapo jumla ya tani 49,677 ziliuzwa kwa thamani ya shilingi bilioni 110.69. Ufuta uliuzwa tani 136.650 kwa shilingi bilioni 0.44, Kakao tani 909.580 kwa shilingi bilioni 4.31.  Maandalizi ya kuuza Mifugo hai (ngómbe, mbuzi na kondoo) na ngozi zinazotokana na Wanyama hao yanaendelea. Aidha, timu ya wataalam ikijumuisha Soko la Bidhaa, Wizara ya Fedha na Mipango, Tume ya madini na Benki Kuu ya Tanzania ilikutana na kujadili namna Soko la Bidhaa litakavyoshiriki kuuza madini. Tume ya Madini kwa kushirikiana na Soko la Bidhaa Tanzania itafanya utafiti wa aina ya madini yanayoweza kuuzwa kupitia Soko la Bidhaa na kuandaa mkataba wa makubaliano (MOU) kwa maeneo yote ya ushirikiano. Aidha, Soko la Bidhaa kwa kushirikiana na Bodi ya Pamba, Bodi ya Usimamizi Stakabadhi za Ghala na Tume ya Maendeleo ya Ushirika limeanza maandalizi ya kufanya  mauzo ya Pamba katika msimu wa mwaka 2023/24. Hatua za awali ni pamoja na kutoa elimu kwa wadau wa pamba na kuwapitisha katika mfumo wa kielektroniki wa Soko la Bidhaa.

 

2.3.4. Kukuza Biashara na Uwekezaji

 

2.3.4.1. Huduma za Biashara na Masoko

 

(a)         Uendelezaji wa Masoko ya Bidhaa 

Hatua iliyofikiwa ni: Kujengea uwezo wadau wa Mfumo wa Stakabadhi za Ghala na Soko la Bidhaa katika mikoa 12; na kuendelea na taratibu wa kuwa na jengo la Ofisi. Tayari mshauri elekezi amepatikana ambaye ni DIT (Dar es salaam Insitute of Technology) na hatua za  awali zinaendelea katika utekelezaji wa kuwa na jengo la ofisi eneo lililotengwa. 

 

(b)         Kuimarisha Maendeleo ya Soko la Ndani na Nje - TANTRADE

Hatua iliyofikiwa ni: Kuratibiwa kwa Maonesho ya 46 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (DITF) yaliyohusisha washiriki 3,200 (kampuni za ndani 2,975 na kampuni za nje  225 kutoka Nchi 23); kuandaa na kuzinduliwa kwa Mfumo wa TanTrade

Biashara Mobile App unaowezesha wafanyabiashara kupata taarifa za masoko na kubaini fursa za kuweza kuuza bidhaa zao; kuandaliwa kwa Mwongozo wa fursa za Uwekezaji baina ya Tanzania na Marekani; na Kuuzwa kwa tani 147,061 za mazao mbalimbali ikiwemo zabibu, muhogo, mchele, asali, nyama za thamani ya shilingi bilioni 208.2 kwa wanunuzi ndani na nje ya nchi. Jumla ya shilingi milioni 400.00 zimetumika katika kipindi Julai, 2022 na Aprili, 2023.

 

(c)         Kuendeleza Biashara Kupitia Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE)

Hatua iliyofikiwa ni: Kupatikana kwa mkandarasi wa mradi wa ujenzi wa jengo la ghorofa 10 la Vipimo na Viwango katika kampasi kuu ya Dar es salaam; na kukamilika kwa ukarabati wa Kampasi ya Dodoma. Jumla ya shilingi milioni 458.16 zimetumika katika kipindi Julai, 2022 na Aprili, 2023.

 

Kukuza Ushiriki wa Watanzania kwenye Miradi ya Kimkakati na Uwekezaji Hatua iliyofikiwa ni: Kufanyika kwa tathmini ya ushiriki katika miradi ya kimkakati, ambayo ilibainika kuwa kampuni 2,827 za watanzania ziliingia mikataba kwa ajili ya kutoa huduma za ukandarasi ambapo kati ya hizo kampuni 848 ni za ukandarasi, kampuni 83 za ushauri elekezi na kampuni 1,896 za kutoa huduma ya chakula, ulinzi, usafiri, bima na bidhaa za ujenzi. Aidha, miradi hiyo ilizalisha fursa za ajira 72,395.

 

Kukuza Sekta Binafsi

Hatua iliyofikiwa ni: Kuendelea na majadiliano kati ya sekta ya umma na binafsi kupitia mabaraza ya biashara ya ngazi ya Wilaya, Mkoa na Taifa kwa lengo la kutatua chnagamoto zinazokwamisha biashar ana uwekezaji ambapo jumla ya mikutano 10 imefanyika katika ngazi ya mikoa; na kufanyika kwa utambuzi wa muundo wa Sekta Binafsi nchini ambapo jumla ya Kampuni 488 zenye ukomo wa ahadi (Limited by Guarantee) za Sekta Binafsi zimesajiliwa na Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) na Jumuiya za Biashara 22 zimesajiliwa na Ofisi ya Msajili wa Jumuiya nchini. 

 

2.3.4.2. Kuboresha Mazingira ya Kufanya Biashara na Uwekezaji

 

A.            Kuboresha Mazingira ya Uwekezaji 

Hatua iliyofikiwa ni: Kutungwa kwa Sheria ya Uwekezaji namba 10 ya mwaka 2022;  kuendelea kuandaa kanuni za utelekezaji wa Sheria ya Uwekezaji ya mwaka 2022; na kuandaliwa kwa mapendekezo ya maboresho ya sheria na kanuni zenye muingiliano ikiwemo tozo kero, adhabu, leseni na vibali kwenye sekta mbalimbali za biashara na uwekezaji; kuandaa na kushiriki makongamano 10 ndani na nje ya nchi kwa ajili ya kutangaza kwa fursa mbalimbali za uwekezaji kwa ajili ya kuvutia uwekezaji wa mitaji kutoka nje (FDI); kufanya ufuatiliaji wa utekelezaji wa Hati za Makubaliano 50 zilizosainiwa; na kuendelea kuratibu maandalizi ya Kongani za Viwanda. 

B.            Kuimarisha Ushiriki wa Sekta Binafsi

(a) Huduma za Uwekezaji Mahala Pamoja (One Stop Facilitation Centre - OSC)

Hatua iliyofikiwa ni: Kutolewa kwa huduma kwa wateja 13,836 katika kituo cha Huduma za Uwekezaji Mahala Pamoja (OSC) katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023; Kusajiliwa kwa miradi mipya 240 (wazawa - 89, wageni - 94 na ubia - 57) inayotarajiwa kutengeneza ajira 39,245; kutolewa kwa elimu kwa umma kuhusu huduma zitolewazo na OSC kwa njia ya makala (Documentary) na vyombo vya habari; na kutengenezwa kwa Mfumo wa Kielektroniki wa Kuhudumia Wawekezaji Mahali Pamoja (Tanzania Electronic Investment Window - TeIW) ambapo awamu ya kwanza inahusisha kuunganisha Mifumo kutoka Taasisi za NIDA, TRA, BRELA, TIC, Kazi, Uhamiaji na Ardhi.

 

C.          Mahusiano na Nchi za Nje na Uchumi wa Kidiplomasia

 

(a)         Mradi Na. 6391: Ujenzi na Ukarabati wa Majengo ya Vitega Uchumi, Ofisi na Makazi ya Watumishi Balozini  

Hatua iliyofikiwa ni: Kukamilika kwa ukarabati wa makazi ya balozi wa Tanzania

Brussels (Ubelgiji) na nyumba ya mkuu wa utawala Ubalozi wa Tanzania Stockholm (Sweden); kukamilika kwa ukarabati wa jengo linalotumika kama kitega uchumi na jengo la makazi ya watumishi katika Ubalozi wa Tanzania Harare (Zimbabwe); kukamilika kwa ukarabati wa majengo matatu (3) ya makazi ya watumishi katika Ubalozi wa Tanzania Lilongwe (Malawi); kuendelea na ukarabati wa jengo la ofisi za ubalozi wa Tanzania Brussels (Ubelgiji); kuendelea na ukarabati wa makazi ya balozi wa Tanzania Stockholm (Sweden); na kuendelea na ukarabati wa jengo la zamani la ofisi za Ubalozi wa Tanzania Washington D.C (Marekani). Shughuli nyingine zilizotekelezwa ni pamoja na ununuzi wa jengo la Mkuu wa Utawala na Fedha katika Ubalozi wa Tanzania, Berlin (Ujerumani). Jumla ya shilingi bilioni 6.08 zimetumika katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023.

 

(b)         Mradi Na. 6389: Ujenzi wa Majengo ya Ofisi 

Upanuzi wa Uboreshaji wa Miundombinu ya Chuo cha Diplomasia 

Hatua iliyofikiwa ni kuendelea na ujenzi wa vyumba tisa (9) vya mihadhara katika Chuo cha Diplomasia, Kurasini, Dar es Salaam. Jumla ya shilingi milioni 663.0 zimetumika katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023.

 

2.3.5. Kuchochea Maendeleo ya Watu

 

2.3.5.1. Afya

 

(a)         Mradi Na. 5487: Hospitali ya Taifa ya Muhimbili  

Hatua iliyofikiwa ni:  Kuendelea na ujenzi wa Jengo la Wodi Maalum (Private wards) ambao umefikia asilimia 75; kukamilika kwa utengenezaji wa  mfumo mpya wa utoaji huduma kupitia TEHAMA (Health Management Infomation System); kukamilika kwa ukarabati wa vyumba vitano (5) vya ICU na vyumba vya radiolojia  (MRI 1, CT SCAN 1 na X-Ray 2); na kukamilika kwa upanuzi wa jengo la OPD na ukarabati wa Hospitali ya watoto. Jumla ya shilingi bilioni  1.9 zimetumika katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023.

 

(b)         Mradi Na. 6364: Hospitali ya Taifa Muhimbili - Mloganzila  

Hatua iliyofikiwa ni: Kuwezesha mafunzo ndani na nje ya nchi kwa watumishi 82 katika fani mbalimbali za kibingwa katika masomo ya uzamili; kukamilika kwa ujenzi wa kituo cha upandikizaji viungo na sehemu ya kufulia nguo; na kukamilika kwa ukarabati wa wodi za watoto wachanga mahututi (NICU). 

 

Shughuli nyingine zilizotekelezwa ni: Kukamilika kwa ujenzi wa wodi ya kawaida ya watoto, wodi ya mama wajawazito mahututi, wodi ya uangalizi maalumu wa mama wajawazito (HDU) na chumba maalumu kwa ajili ya kufanya matengenezo ya vifaa tiba (biomedical workshop); na kutolewa kwa huduma za uchunguzi za kibingwa ambapo jumla ya vipimo vya maabara 11,096 (Plain X-Ray 3,070, CT Scan 2,601, USS 4,055, MRI 720, Floroscopy 507 na mammography 223) vilifanyika. Aidha, hospitali imetoa huduma mpya za kupunguza uzito kwa kuwekewa Puto (Intragastric balloon) ambapo jumla ya wagonjwa 87 na upandikizaji wa uloto (bone marrow transplant) kwa wagonjwa 11 wamehudumiwa. Jumla ya shilingi bilioni 1.5  zimetumika hadi Aprili 2023. 

 

(c)         Mradi Na. 5491: Taasisi ya Mifupa Muhimbili (MOI)

Hatua iliyofikiwa ni: kuendelea ununuzi wa vifaa tiba na utoaji wa huduma za Tiba kwa njia ya mkoba (Outreach Program) ambapo jumla ya wateja 4,528 walipatiwa huduma hiyo katika Hospitali za Mikoa ya Mtwara, Lindi na Dar es Salaam. Jumla ya shilingi milioni 500 zimetumika katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023.

 

(d)         Mradi Na. 5419: Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI)

Hatua iliyofikiwa ni: Kukamilika kwa ukarabati na upanuzi wa jengo la Wagonjwa mahututi (ICU). Jumla ya shilingi bilioni 2 zimetumika katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023.

(e)         Mradi Na. 5412: Taasisi ya Saratani Ocean Road

Hatua iliyofikiwa ni: Kukamilika kwa ukarabati na upanuzi wa jengo la wagonjwa mahututi; kukamilika kwa ukarabati mkubwa wa chumba cha MRI;  kukamilika kwa ukarabati wa chumba cha tiba mtandao; kufungwa kwa mashine ya PET/CT SCAN; na kununuliwa na kusimikwa kwa mashine mbili (2) za LINAC na mbili (2) za COBALT. Jumla ya shilingi bilioni 4 zimetumika katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023.

 

(f)          Mradi Na. 5424: Hospitali ya Rufaa ya Magonjwa Ambukizi – Kibong’oto (Kilimanjaro)

Hatua iliyofikiwa ni: Kukamilika kwa ujenzi wa jengo la wagonjwa wa nje (OPD) na jengo la utawala; kuendelea na ujenzi wa maabara ya Kisasa (BSL 3) ambapo utekelezaji umefikia asilimia 96; na kuendelea na ujenzi na ukarabati Mkubwa wa jengo la Radiolojia kwa ajili ya kusimika CT Scan ambapo utekelezaji umefikia asilimia 21. Jumla ya shilingi bilioni 1.3  zimetumika katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023.

 

(g)         Mradi Na 5425: Hospitali ya Rufaa ya Afya ya Akili Mirembe

Hatua iliyofikiwa ni: Kukamilika kwa ujenzi wa nyumba ya Mtumishi - Hombolo; kuendelea na ujenzi wa jengo la wagonjwa mahututi (ICU) ambapo utekelezaji umefikia asilimia 99 na jengo la huduma za dharura (EMD) asilimia 98; na  kutoa mafunzo ya muda mrefu na mfupi kwa watumishi 14 katika fani mbalimbali za kibingwa katika vyuo vya ndani na nje. Jumla ya shilingi  bilioni 4 zimetumika katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023.

 

(h)         Mradi Na. 5426: Hospitali ya Rufaa Kanda ya Ziwa, Bugando

Hatua iliyofikiwa ni kukamilika kwa ukarabati na upanuzi wa majengo ya wagonjwa mahututi - Medical ICUSurgical ICU, na Neonatal ICU. Jumla ya shilingi milioni 997 zimetumika katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023.

 

(i)           Mradi Na. 5427: Hospitali ya Kanda ya Kaskazini (KCMC)

Hatua iliyofikiwa ni: Kukamilika kwa ukarabati na upanuzi wa jengo la wagonjwa mahututi (Medical ICU na Surgical ICU); na kuendelea na ujenzi wa jengo la huduma za tiba - mionzi kwa matibabu ya magonjwa ya kansa (Radiotherapy) ambapo utekelezaji umefikia asilimia 53. Jumla ya shilingi bilioni 1.0 zimetumika katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023.

 

(j)          Mradi Na. 5422: Hospitali ya Rufaa ya Nyanda za Juu Kusini Mbeya Hatua iliyofikiwa ni: Kukamilika kwa ukarabati na upanuzi wa jengo la wagonjwa mahututi (ICU), jengo la huduma za dharura (EMD) na chumba cha tiba mtandao; kununuliwa kwa vifaa tiba ikiwemo patient monitors 18, Vitanda, na Bed Lockers; na kuendelea na ujenzi wa jengo kwa ajili ya huduma za uzazi unaofanyika eneo la Meta ambapo utekelezaji umefikia asilimia 99. Jumla ya shilingi bilioni 1.1 zimetumika katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023.

 

(k)         Mradi Na. 5428:  Hospitali ya Benjamini Mkapa

Hatua iliyofikiwa ni: Kukamilika kwa ukarabati wa chumba cha kutolea tiba mtandao na jengo la huduma za CT - Scan; kuanza kutolewa kwa huduma ya upandikizaji wa Uloto (Bone marrow Transplant) ambapo wagonjwa watatu (3) wamehudumiwa; kukamilika kwa upanuzi wa jengo la wagonjwa mahututi (ICU); na na kuendelea na ujenzi wa jengo la Tiba Mionzi (Radiotherapy) ambao umefikia asilimia 15.5. Jumla ya shilingi bilioni 3.1 zimetumika katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023.

 

(l)           Mradi Na. 5408: Ujenzi wa Hospitali ya Kanda ya Ziwa - Burigi

Hatua iliyofikiwa ni: kukamilika kwa awamu ya tatu ya ujenzi wa nyumba 20 za watumishi; kuendelea na ujenzi wa uzio ambao umefikia asilimia 85; kukamilika kwa ujenzi wa njia za kupita wagonjwa na barabara za ndani ya eneo la  Hospitali; na kukamilika kwa ujenzi wa jengo la huduma za uchunguzi kwa njia ya mionzi (Radiolojia).  Shughuli nyingine zilizotekelezwa ni kukamilika kwa ujenzi wa jengo la nyumba ya mashine ya kufua umeme (power house) na kukamilika kwa ujenzi wa jengo la ghorofa mbili (2) la wodi ya wagonjwa. Jumla ya shilingi milioni 461 zimetumika katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023.

 

(m)       Mradi Na. 5423 Hospital ya Rufaa ya Kanda ya Kusini - Mtwara

Hatua iliyofikiwa ni: Kukamilika kwa ujenzi wa jengo la wagonjwa mahututi (ICU), ujenzi wa nyumba ya mtumishi na ukarabati wa chumba cha tiba mtandao; na kuendelea na ujenzi wa Jengo la Huduma za Dharura (EMD) ambapo utekelezaji umefikia asilimia 80 na ujenzi wa jengo la OPD umefikia asilimia 61. Jumla ya shilingi bilioni 3.9 zimetumika katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023.

 

(n)         Mradi Na. 5411: Mradi wa Kuboresha Hospitali za Rufaa za Mikoa 

Hatua iliyofikiwa ni: 

 

(i)           Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Njombe: Kukamilika kwa nyumba ya mtumishi na ukarabati wa jengo la huduma za  CT-Scan. Jumla ya shilingi bilioni 2.2 zimetumika katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023.

 

(ii)         Hospitali ya Mkoa Simiyu: Kuendelea na ujenzi wa jengo la huduma za afya ya uzazi ambapo utekelezaji umefikia asilimia 88; kuendelea na ujenzi wa jengo la wagonjwa mahututi (asilimia 94), jengo la huduma za dharura (asilimia 94) na nyumba ya mtumishi (asilimia 98). Jumla ya shilingi milioni  337 zimetumika katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023.

 

(iii)       Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Geita: Kuendelea na ujenzi wa Jengo la Afya ya Uzazi ambao umefikia asilimia 29, jengo la wagonjwa wa nje (OPD) asilimia 99.5, jengo la wagonjwa mahututi (asilimia 98) na jengo la huduma za dharura (asilimia 98); na kukamilika kwa nyumba ya mtumishi. Jumla ya shilingi bilioni 1.8 zimetumika katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023.

(iv)       Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Songwe: Kukamilika kwa ujenzi wa jengo la OPD; na kuendelea na ujenzi wa jengo la wagonjwa mahututi ambapo utekelezaji umefikia asilimia 90, jengo la huduma za dharura  (asilimia 89) na na jengo la huduma za afya ya uzazi umefikia asilimia 55. Jumla ya shilingi

bilioni 2.6 zimetumika katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023.

 

(v)         Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Katavi: Kukamilika kwa ujenzi wa nyumba ya mtumishi; kuendelea na ujenzi wa majengo ya uchunguzi na afya ya uzazi, miundombinu ya ICT, HVAC, Lift, Hewa Tiba, chumba cha tiba mtandao na jengo la OPD na Ujenzi jengo la huduma za CT-Scan ambao umefikia asilimia 97; na ujenzi wa jengo la huduma za dharura na jengo la wagonjwa mahututi umefikia asilimia 84. Jumla ya shilingi bilioni 12.9 zimetumika katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023.

 

(vi)       Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Singida (RRH): Kukamilika kwa ujenzi wa nyumba ya mtumishi, ukarabati wa jengo la huduma za CT - Scan na chumba cha tiba mtandao; na kuendelea na ujenzi wa jengo la huduma za dharura na Jengo la wagonjwa mahututi ambapo utekelezaji umefikia asilimia 90. Jumla ya shilingi bilioni 7.4 zimetumika katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023.

 

(vii)     Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Shinyanga: Kukamilika kwa ujenzi ya nyumba ya mtumishi na jengo la huduma za CT-Scan; na kuendelea na ujenzi wa jengo la wagonjwa mahututi ambapo utekelezaji umefikia asilimia 97 na jengo la huduma za dharura asilimia 99. Jumla ya shilingi bilioni 3.4 zimetumika katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023.

 

(viii)    Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Mara: Kukamilika kwa ujenzi wa nyumba mbili (2) za watumishi; kuendelea na ujenzi wa jengo la wagonjwa mahututi ambapo utekelezaji umefikia  asilimia 90 na jengo la huduma za dharura asilimia 40. Jumla ya shilingi bilioni 1.0 zimetumika katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023.

 

(ix)       Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Arusha (Mount Meru): Kukamilika kwa ujenzi wa nyumba ya mtumishi, ukarabati na upanuzi wa jengo la wagonjwa mahututi, chumba cha tiba mtandao na jengo la huduma za CT - Scan. Jumla ya shilingi bilioni 3.2 zimetumika katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023.

 

(x)         Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Mwanza (Sekou Toure): Kukamilika kwa ukarabati wa jengo la huduma za CT-Scan, chumba cha tiba mtandao na nyumba ya mtumishi. Jumla ya shilingi milioni 537 zimetumika katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023.

(xi)       Hospitali ya Rufaa ya Mkoa (Mwananyamala): Kuendelea na ujenzi wa jengo la Huduma za dharura ambapo utekelezaji umefikia asilimia 98 na jengo la wagonjwa mahututi (asilimia 90) na ukarabati wa jengo la huduma za CT-

Scan (asilimia  99). Jumla ya shilingi bilioni 3.2 zimetumika katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023.

 

(xii)     Hospitali ya Rufaa ya Mkoa (Temeke): Kukamilika kwa ukarabati na upanuzi wa jengo la huduma za dharura; kuendelea na ujenzi wa jengo la huduma za CT - Scan ambapo utekelezaji umefikia asilimia 95; ukarabati na upanuzi wa jengo la wagonjwa mahututi umefikia  asilimia 96. Jumla ya shilingi bilioni 2.9 zimetumika katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023.

(xiii)    Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Pwani (Tumbi): Kukamilika kwa ujenzi wa nyumba ya mtumishi; kukamilika kwa ukarabati na upanuzi wa jengo la wagonjwa mahututi, jengo la huduma za dharura na jengo la huduma za CT - Scan. Jumla ya shilingi bilioni 2.9 zimetumika katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023.

 

(xiv)    Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Kigoma (Maweni): Kukamilika kwa ujenzi wa jengo la kuhifadhi maiti, nyumba ya mtumishi na ukarabati wa chumba cha tiba mtandao; na kuendelea na ujenzi wa jengo la wagonjwa mahututi, jengo la huduma za   CT-Scan na huduma za dharura ambapo utekelezaji umefikia asilimia 99 na jengo la OPD asilimia 95. Jumla ya shilingi milioni 400 zimetumika katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023.

 

(xv)     Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Kilimanjaro (Mawenzi): Kukamilika kwa ukarabati na upanuzi wa jengo la wagonjwa mahututi, jengo la huduma za dharura na ujenzi wa nyumba ya mtumishi; na kuendelea na ujenzi wa jengo la huduma za afya ya uzazi ambapo utekelezaji umefikia asilimia 85. Jumla ya shilingi bilioni 2.9 zimetumika katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023.

 

(xvi)    Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Manyara: Kukamilika kwa ukarabati wa chumba cha tiba mtandao na nyumba ya mtumishi na ujenzi wa jengo la wagonjwa wa Nje (OPD) umefikia asilimia 99 na kuendelea na ujenzi wa majengo ya huduma za CT - Scan (asilimia 92), Jengo la Damu Salama (asilimia 72), wagonjwa mahututi (asilimia 82) na huduma za dharura (asilimia 70). Jumla ya shilingi bilioni 3.5 zimetumika katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023.

 

(xvii)  Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Mbeya: Kukamilika kwa ukarabati na upanuzi wa jengo la wagonjwa mahututi na ujenzi wa nyumba ya mtumishi; na kuendelea na ujenzi wa jengo la huduma za CT-Sca ambapo utekelezaji umefikia asilimia 87 na jengo la upasuaji (theatre, ICU & CSSD) umefikia asilimia 98. Jumla ya shilingi bilioni 2.0 zimetumika katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023.

(xviii)Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Mtwara: Kukamilika kwa ukarabati wa jengo la huduma za CT - Scan. Jumla ya shilingi bilioni 2.2 zimetumika katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023.

 

(xix)    Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Dodoma: Kukamilika kwa ukarabati na upanuzi wa jengo la huduma za dharura, ujenzi wa nyumba ya mtumishi, ujenzi wa jengo la huduma za CT - Scan na ujenzi wa jengo la wagonjwa mahututi. Jumla ya shilingi bilioni 2.9 zimetumika katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023.

 

(xx)     Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Tanga: Kukamilika kwa ujenzi wa jengo la huduma za CT-Scan, ukarabati na upanuzi wa jengo la wagonjwa mahututi na ukarabati wa chumba cha tiba mtandao. Aidha, ukarabati na upanuzi wa jengo la huduma za dharura umefikia asilimia 99.4 na ujenzi wa nyumba ya mtumishi umefikia asilimia 99. Jumla ya shilingi bilioni 2.6 zimetumika katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023. 

 

(xxi)    Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Kagera: Kukamilika kwa ujenzi wa nyumba ya Mtumishi na jengo la wagonjwa mahututi; na kuendelea na ujenzi wa jengo la huduma za dharura (asilimia 99) na jengo la huduma za CT-Scan (asilimia 98). Jumla ya shilingi bilioni 3.4 zimetumika katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023.

 

(o)         Mradi Na 2208: Taasisi ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu ya Taifa (NIMR)

Hatua iliyofikiwa ni: Kufanyika kwa tafiti za afya za magonjwa 113 ya binadamu; kufanyika kwa utafiti wa kufuatilia hali ya maambukizi ya malaria nchini kwa kutumia mbinu za vinasaba katika mikoa 13 ya Tanzania Bara; kufanyika kwa utafiti kuhusu kutathmini usugu wa vimelea vya ugonjwa wa malaria dhidi ya dawa ya mseto barani Afrika; uimarishaji uwezo wa mfumo wa afya na kupeleka afua ya Praziquantel ya watoto (Pediatric Praziquantel) kwa ajili ya kudhibiti ugonjwa wa kichocho kwa watoto wenye umri chini ya miaka mitano, utafiti wa usalama na ufanisi wa chanjo ya TANCoV 1.3.20 SARS-CoV-2; kufanyika kwa utafiti unaojumuisha uchunguzi wa Kifua Kikuu ili kukomesha Kifua Kikuu katika ukanda wa Afrika Mashariki kwa nia ya kutafsiri shahidi za kitafiti kuwa sera na utendaji (EXITTB); kufanyika kwa utafiti wa kuzuia ugonjwa wa kisukari Afrika; kufanyika kwa jaribio nasibu la awamu ya tatu ya dawa ya Metformin kwa watu walioambukizwa VVU wanaokaribia kupata ugonjwa wa kisukari; na kufanyika kwa utafiti wa vyakula tiba kwa ajili ya afya ya uzazi na kutatua mahitaji muhimu ya virutubisho na madini kabla na wakati wa ujauzito. Jumla ya shilingi bilioni 1.0 zimetumika katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023.

(p)         Mradi Na. 5411: Mradi wa Kuboresha Upatikanaji wa Dawa, Vifaa Tiba na Vitendanishi

Hatua iliyofikiwa ni: Kuendelea na usambazaji wa dawa, vifaa tiba na vitendanishi ambapo kwa zahanati na vituo vya afya umefikia asilimia 45, hospitali za wilaya (asilimia 52), hospitali za rufaa za mikoa (asilimia 87) na Hospitali ya Taifa (asilimia 66); Kuendelea na ununuzi wa vifaa tiba vya afya ya kinywa na macho kwa ajili ya Hospitali za Halmashauri 71 zilizokamilika; na ununuzi wa vifaa tiba vya zahanati 300; na ununuzi wa vifaa tiba katika vituo vya Afya 159 vya tozo. Jumla ya shilingi bilioni 164.0 zimetumika katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023.

 

(q)         Mradi Na. 5432:  Uimarishaji wa Huduma za Chanjo

Hatua iliyofikiwa ni: Kutoa chanjo kwa watoto wa chini ya umri wa mwaka mmoja ambapo chanjo ya Penta3 kwa watoto 397,700 sawa na asilimia 107, chanjo ya Polio ya matone OPV3 asilimia 103, sindano (IPV) asilimia 107, Surua rubella 1 asilimia 109, Surua Rubella 2 asilimia 96, HPV1 asilimia 83 na HPV2 asilimia 62. Jumla ya shilingi bilioni 41.3 zimetumika katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023.

 

(r)          Mradi Na. 5492: Mpango wa Taifa wa Kudhibiti UKIMWI (NACP) 

Hatua iliyofikiwa ni: Kutoa huduma ya tiba na matunzo kwa watu wapatao 1,582,109; kutolewa kwa huduma za  PMTCT, ambapo  vituo 7,120 sawa na  asilimia 95  ya vituo vinavyotoa huduma ya afya ya uzazi na mtoto vinatoa huduma za PMTCT; kutolewa kwa huduma za upimaji VVU kwa wajawazito 1,793,204 kati ya 1,818,147 ya wajawazito wote waliohudhuria hudhurio la kwanza kliniki. Kati yao, wajawazito 52,012 sawa na asilimia 2.9 walibainika kuwa wanaishi na maambukizo ya VVU. Wajawazito 49,953 sawa na asilimia 96 walianzishiwa dawa za ARV na kuzuia maambukizi kwenda kwa mtoto. Watoto 34,364 sawa na asilimia 88 ya Watoto waliozaliwa na akina mama wanaoishi na VVU walipimwa kipimo cha kwanza cha uchunguzi wa maambukizi ya VVU katika umri wa miezi miwili na asilimia 0.7 walibainika kuwa na maambukizi. Jumla ya shilingi bilioni 1.6 zimetumika katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023.

 

(s)         Mradi Na.5498: Mpango wa Taifa wa Kudhibiti Kifua Kikuu na Ukoma

Hatua iliyofikiwa ni: Kununuliwa na kusimikwa kwa mashine za kisasa aina ya Truenut 30 kwenye vituo vya kutolea huduma za Kifua Kikuu; kutolewa kwa huduma za mkoba kliniki tembezi (Mobile Vans outreach services) ambapo jumla ya watu 8,298 walichunguzwa na kupimwa Kifua Kikuu; na kutekeleza shughuli ya tambua TB ambapo jumla ya wagonjwa 155 sawa na asilimia 35 wa Kifua Kikuu Sugu waliogundulika walianzishiwa matibabu. Jumla ya shilingi bilioni 9.0 zimetumika katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023.

(t)          Mradi Na. 5406: Kudhibiti Magonjwa ya Kuambukiza na Yasiyo ya Kuambukiza   

Hatua iliyofikiwa ni:  Kuendelea na ujenzi wa wodi mbili (2) kwa ajili ya matibabu ya magonjwa hatarishi na milipuko katika Hospitali ya Kisopwa ambapo utekelezaji wa umefikia asilimia 60; na kufanya tathmini ya huduma za mionzi nchini katika hospitali tano (5) - BMH, MBEYA, ORCI, KCMC na BUGANDO ili kuangalia huduma zinazotolewa. Jumla ya shilingi  bilioni 4.1 zimetumika katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023.

 

(u)         Mradi Na. 2204: Mafunzo na Maendeleo ya Wataalamu

Hatua iliyofikiwa ni: Kukamilika kwa ujenzi na ukarabati wa wa jengo la wodi maalum (Private wards) katika Chuo cha Tabora Clinical Officers Training Centre; kukamilika kwa ukarabati wa majengo ya vyuo vya Ngudu School of Environmental Health ScienceKilosa Clinical Officers Training CentreKagemu Environmental

Health Science, na Tabora Clinical Officers Training Centre.  Aidha, ujenzi katika Chuo cha Korogwe SON umefikia asilimia 95, Mtwara COTC asilimia 95 na Nachingwea SON asilimia 48; na kutolewa kwa ufadhili wa masomo ya uzamili katika fani mbalimbali za afya kwa watumishi 373 ambapo kati ya hao 318 ni masomo ya kimkakati na 55 ni mafunzo kwa njia ya mafungu. Jumla ya shilingi bilioni 45.5 zimetumika katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023.

 

(v)         Mradi Na. 5416: Mipango ya Afya na Uendeshaji

Hatua iliyofikiwa ni: Kuwekwa kwa mfumo wa tiba mtandao katika hospitali nne (4); na kununuliwa na kuanza kutumika kwa vifaa vya TEHAMA katika hospitali za kanda za Bugando na Benjamin Mkapa na hospitali tatu (3) za kibingwa (Muhimbili, MOI na JKCI) na hospitali maalum moja (1) (Ocean Road Cancer Institute). Jumla ya shilingi bilioni 2.0 zimetumika katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023.

 

(w)       Mradi Na. 5401: Ujenzi wa Hospitali za Halmashauri

Hatua iliyofikiwa ni: Kuendelea na ujenzi wa Hospitali 59 za halmashauri na ukarabati wa hospitali kongwe 19 za halmashauri ambapo utekelezaji wa miradi hiyo ipo katika hatua mbalimbali za utekelezaji. Jumla ya shilingi bilioni 233.4 zimetumika katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023.

 

(x)         Mradi Na. 5429: Huduma ya Afya ya Msingi   

Hatua iliyofikiwa ni: kuendelea na ukamilishaji wa ujenzi wa zahanati 300 katika Halmashauri 184 ambapo utekelezaji upo katika hatua mbalimbali; na ununuzi wa vifaa na vifaa tiba kwa vituo vya afya 150, zahanati 300 na hospitali za Halmashauri 71. Jumla ya shilingi bilioni 69.15 zimetumika katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023.

2.3.5.2. Ustawi na Maendeleo ya Jamii

(i)           Mradi Na. 6330: Ukarabati wa Vyuo vya Maendeleo ya Jamii

Hatua iliyofikiwa ni: Kukamilika kwa ujenzi wa kumbi pacha za mihadhara (lecture theatre two in one) zenye uwezo wa kuhudumia wanafunzi 1,008; kukamilika kwa ujenzi wa bweni la wasichana la ghorofa nne (4) na ununuzi wa samani (viti, vitanda na magodoro) kwa ajili ya kumbi pacha za mihadhara na hosteli iliyojengwa katika Taasisi ya Maendeleo ya Jamii Tengeru; kukamilika kwa ukarabati wa jengo la utawala katika Chuo cha Maendeleo ya Jamii Rungemba; kukamilika kwa ukarabati wa maktaba yenye uwezo wa kuhudumia wanafunzi 120, ukumbi wa mihadhara wenye uwezo wa kuhudumia wanafunzi 260 na mabweni mawili yenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 64 kila moja na kuendelea na ujenzi wa Bwalo la Chakula lenye uwezo wa kubeba wanafunzi 400 ambapo utekelezaji umefikia asilimia 15 katika Chuo cha Maendeleo ya Jamii Ruaha; kukamilika kwa ujenzi wa Jengo la Utawala  lenye vyumba vya ofisi 17 na kumbi mbili (2) ndogo za mikutano zenye uwezo wa kuhudumia watu 40 kwa wakati mmoja katika Chuo cha Maendeleo ya Jamii Mlale; na kuendelea na ujenzi wa hosteli ya ghorofa mbili (2) yenye uwezo wa kuhudumia wanafunzi 600 katika Chuo cha Maendeleo ya Jamii Uyole ambao umefikia asilimia 48; na kuendelea na ukarabati wa nyumba moja ya mtumishi, ufungaji wa mifumo ya TEHAMA na ununuzi wa Lori, gari (pick up) na mashine za kiuhandisi (Poker Machines na Mobile Block Machines) katika Chuo cha Maendeleo ya Jamii Ufundi Mabughai.  Jumla ya shilingi bilioni 3.97 zimetumika katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023. 

 

(ii)         Mradi Na. 6259: Ujumuishaji wa Masuala ya Jinsia katika Mipango ya Maendeleo

Hatua iliyofikiwa ni: kuendelea kufanya mapitio ya Sera ya Maendeleo ya Wanawake na Jinsia (2000) na Mkakati wa utekelezaji wake (2005) ambayo ipo katika hatua ya uidhinishaji; kukamilika kwa tathmini ya utekelezaji wa Mpango Kazi wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto (MTAKUWWA) na kuandaliwa kwa MTAKUWWA Awamu ya Pili; kukamilika kwa maandalizi ya Programu ya miaka mitano (2022 – 2026) ya Utekelezaji wa Ahadi za Nchi kwenye Jukwaa la Kimataifa la Kizazi chenye Usawa; kuanzishwa kwa Dawati la Jinsia katika Chuo Kikuu cha Dodoma na Chuo Kikuu cha Mtakatifu Yohana (Saint John University) na hivyo kufikisha idadi ya madawati 87 ya Jinsia yaliyoanzishwa mpaka sasa katika Vyuo Vya Elimu ya Juu na Kati; kufanyika kwa kampeni maalum ya kupinga ukatili dhidi ya watoto hususan ukeketaji katika mikoa yenye matukio mengi ya ukeketaji ya Manyara ambapo ukeketaji umefikia asilimia 58 na Mara (asilimia 31); kuanzishwa kwa mfumo wa huduma kwa mteja  ambao utatumika kutoa huduma zote za Wizara; kuandaliwa kwa Mwongozo wa Uanzishwaji na Uendeshaji wa Dawati la Jinsia Katika Maeneo ya Umma na kutolewa mafunzo kwa waratibu 216 wa Dawati hilo. Jumla ya shilingi bilioni 2.07 zimetumika katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023.

(iii)       Mradi Na. 5414: Uhai na Maendeleo ya Mtoto

Hatua iliyofikiwa ni: Kuundwa kwa  Madawati ya Ulinzi na Usalama wa Mtoto 1,393 katika shule za msingi na sekondari na Mabaraza ya Watoto 560 katika mikoa 8 (Rukwa, Arusha, Tanga, Dar es salaam, Pwani, Shinyanga, Dodoma na Geita); kutolewa kwa elimu ya uelewa katika jamii kuhusu Programu Jumuishi ya Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto (2021/22 - 2024/25) kwa Waheshimiwa Wabunge 124 na kwenye mikoa 10 ya Tabora, Lindi, Dar es saalam, Morogoro, Arusha, Manyara, Mbeya, Rukwa, Kagera na Dodoma; kuunganisha viashiria vya Mpango wa Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto kutoka kwenye mifumo iliyopo katika Wizara za Kisekta; kutolewa mafunzo kwa wazazi 104 na vijana balehe 94 katika Halmashauri ya Wilaya Mbarali mkoani Mbeya kuhusu Programu ya Malezi Jumuishi kwa Kundi la Vijana Balehe; na kuendelea na maandalizi ya video fupi zenye ujumbe maalum ambazo zitatumika kwenye vyombo vya habari ikiwemo redio na Runinga kwa ajili ya kutoa tahadhari ya matumizi yasiyofaa ya mitandao ya kijamii kwa watoto, wazazi na jamii kwa ujumla. Jumla ya shilingi milioni 662.8 zimetumika katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023.

 

(iv)       Mradi Na. 6290: Uchakataji wa Taarifa na Uandaaji Programu Programming and Data Processing)

Hatua iliyofikiwa ni: Kufanyika kwa ufuatiliaji na tathmini ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika Chuo cha Maendeleo ya Jamii Monduli, Mlale, Ruaha, Uyole, Taasisi ya Ustawi wa Jamii (Kampasi ya Kisangara) na Makazi ya Wazee Kibirizi (Kigoma), Kilima (Kagera) na Nandanga (Lindi).  Jumla ya shilingi milioni 200 zimetumika hadi Aprili 2023. 

 

2.3.5.3. Elimu

(a)           Mradi Na. 4312: Programu ya Lipa Kulingana na Matokeo katika Elimu (EP4R)

Hatua iliyofikiwa ni: Kukarabatiwa kwa majengo yaliyoungua katika Chuo Kikuu Cha Dar es salaam Kampasi ya Zanzibar na ununuzi wa vifaa vya maabara; kuendelea na ujenzi wa Vyuo vitatu (3) vya Ualimu ambavyo ni Sumbawanga (asilimia 80), Dakawa (asilimia 80) na Mhonda (asilimia 80) na shule ya Mfano ya Sekondari Dodoma (asilimia 90); ujenzi wa shule mpya 40, madarasa 96, mabweni 4, nyumba za walimu 7 katika shule za msingi; ujenzi wa mabweni 62, madarasa 46, maabara 16, maktaba 4, nyumba za walimu 13, mabwalo 22  katika shule za sekondari; ujenzi wa ofisi tano (5) za wathibiti ubora wa shule katika halmashauri za Njombe, Tarime, Pangani, Bunda na Ubungo; kuendelea na ujenzi na ukarabati wa miundombinu mbalimbali katika vyuo vya ualimu Mamire (asilimia 90), Vikindu (asilimia 70), Songea (asilimia 5), Singachini (asilimia 5) na Katoke (asilimia 5); kuendelea na ukarabati wa Shule Kongwe 61 (msingi 45, Sekondari 16) ambapo utekelezaji umefikia asilimia 80; na kununuliwa kwa mashine za uchapaji katika kiwanda cha Press A. Jumla ya shilingi bilioni 51.48 zimetumika katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023. 

 

(b)          Mradi Na. 4321: Programu ya Maendeleo ya Sekta ya Elimu ya Msingi (MMEM) LANES II

Hatua iliyofikiwa ni: Kufanyika kwa asilimia 40 ya tathmini ya ubora wa shule kwa shule 5812 Tanzania Bara; kuendelea kwa MEWAKA katika Halmashauri 144 zilizopo katika mikoa 26; kuchapishwa kwa nakala 372,773 ya vitabu vya uchambuzi wa mtihani wa kuhitimu elimu ya msingi – CIRA – PSLE 2021; kuendelea na uchapaji wa nakala 53,510 za vitabu vya uchambuzi wa upimaji wa stadi za kusoma, kuandika na kuhesabu - PIRA – SFNA na nakala 314,700 za vitabu vya uchambuzi wa upimaji wa darasa la IV – PIRA – SFNA ambapo utekelezaji umefikia asilimia 50; kuendelea na ukamilishaji wa ujenzi wa madarasa 128 ya mfano ambapo utekelezaji umefikia asilimia 50. Jumla ya shilingi bilioni 17.64 zimetumika katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023. 

 

(c)           Mradi Na. 4319: Mradi wa Kuboresha Elimu ya Awali na Msingi (Boost Primary Student Learning)

Hatua iliyofikiwa ni: Kufanya tathmini ya mahitaji ya miundombinu kwenye Shule za Msingi 17,182 zilizopo katika Halmashauri zote; Mafunzo kwa Makatibu Tawala wa Mikoa, Wakurugenzi wa Halmashauri, Maafisa Elimu wa Mikoa, timu za utekelezaji wa mradi ngazi za Mkoa na Halmashauri ambapo jumla ya watendaji 2,888 wamepatiwa mafunzo; kutoa Mafunzo ya Walimu Kazini (MEWAKA) kwenye shule za Msingi 2,952 kwenye Halmashauri 26 (Halmashauri 1 kila Mkoa) za majaribio; na kukamilika kwa uaandaji wa miongozo ya utawala bora na kiongozi cha usimamizi wa shule pamoja na moduli 12 za mafunzo endelevu ya walimu kazini. Jumla ya shilingi bilioni 265.08 zimetumika katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023. 

 

(d)          Mradi Na. 3280: Programu ya Huduma ya Maji, Elimu ya Afya na Usafi wa Mazingira Shuleni – SWASH  

Hatua iliyofikiwa ni: Kufanya ufuatiliaji wa awamu ya pili ya ujenzi wa matundu ya vyoo 6,096, vifaa 1,655 vya kunawia mikono na matenki 238 ya kuhifadhia maji katika Shule za Msingi 235 zilizo katika Halmashauri 86; na kuandaa rasimu ya Mpango wa Kitaifa wa Ugharimiaji na Uwekezaji katika Huduma za Maji na Usafi na Mazingira Shuleni (National School WASH Costed Plan and Investment Case). Jumla ya shilingi bilioni 19.02 zimetumika katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023. 

 

(e)           Mradi Na. 4390: Mradi wa Kuboresha Elimu ya Sekondari (SEQUIP) Hatua iliyofikiwa ni: Kuendelea na ujenzi wa shule mpya 232 za Sekondari za kata zenye uwezo wa kuhudumia wanafunzi 400 kila moja katika kata zisizokuwa na shule za Sekondari ambapo utekelezaji umefikia asilimia 75; ujenzi wa shule 10 maalumu za bweni (kidato cha 5 & 6) za wasichana kwa masomo ya Sayansi na upanuzi wa shule 11 umefikia asilimia 50; kukamilika kwa upanuzi wa shule kongwe 18 za sekondari na vituo nane (8) vya Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima ili vitumike kutoa elimu kwa njia mbadala kwa wasichana walio nje ya mfumo rasmi; na kuwezesha na kutoa mafunzo kazini kwa walimu wapatao 736 wa masomo ya Sayansi na Hisabati kama wawezeshaji wa kitaifa. Jumla ya shilingi bilioni 39.72 zimetumika katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023. 

 

(f)            Mradi Na. 6390: Mamlaka ya Elimu Tanzania – TEA

Hatua iliyofikiwa ni: Kuendelea na ujenzi wa ofisi za walimu katika shule saba(7) za sekondari, madarasa 78, (asilimia 28), nyumba 40 za walimu (asilimia 11)na matundu 1,008 (asilimia 13) ya vyoo katika shule 80 za msingi na 22 za sekondari; mabweni 10 ya wasichana katika shule 10 za sekondari (asilimia 10); kutolewa kwa mafunzo kwa wanufaika 5,981 kuhusu ujuzi katika nyanja za Kilimo, Kilimo uchumi, utalii na huduma za utalii, usafirishaji, Nishati na Teknolojia ya habari na mawasiliano; kutolewa kwa mafunzo ya ufundi stadi kwa wananchi 1,627 wanaotoka katika kaya maskini ikiwemo vijana, wanawake na walemavu; na kufikia asilimia 89 ya ununuzi wa vifaa vya kujifunzia na kuboresha miundombinu kwa wanafunzi wenye mahitaji maalumu katika shule tisa (9) za msingi na shule moja (1) ya sekondari. Jumla ya shilingi bilioni 7.0 fedha zimetumika katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023.

 

(g)          Mradi Na. 6363: Ukarabati wa Chuo cha Ufundi Arusha - ATC

Hatua iliyofikiwa ni: Kuendelea na ujenzi wa bweni la wanafunzi wa kike lenye uwezo wa kuhudumia wanafunzi 428 ambapo utekelezaji umefikia asilimia 99.46; kuendelea na ukamilishaji wa ujenzi wa madarasa nane (8) yenye uwezo wa kuhudumia wanafunzi 880 kwa wakati mmoja, maabara sita (6) zenye uwezo wa kuhudumia wanafunzi 270 kwa wakati mmoja na ofisi 26 zenye uwezo wa kuhudumia watumishi 104 ambapo utekelezaji umefikia asilimia 99.4; kuendelea na ukamilishaji wa ujenzi wa hospitali ya taaluma na tiba (polyclinic) ambapo utekelezaji umefikia asilimia 95; na kuendelea na ujenzi wa kliniki itakayohudumia wanafunzi, wafanyakazi na wananchi wa maeneo jirani ambapo utekelezaji umefikia asilimia 24.43. Jumla ya shilingi bilioni 1.0 zimetumika katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023.

 

(h)          Mradi Na. 4397: Ujenzi na Ukarabati wa Vyuo vya Ufundi Stadi

Hatua iliyofikiwa ni: kuendelea na ujenzi na ukarabati wa Vyuo vya Ufundi stadi vya mikoa ya Dodoma (asilimia 90), Mtwara (asilimia 94); ujenzi wa Vyuo vya Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi katika Wilaya 25 (asilimia 98). Aidha, Chuo cha Wilaya ya Mbarali na Chuo cha Wilaya ya Kishapu vimeanza kutoa mafunzo. Jumla ya shilingi bilioni 31.0 zimetumika katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023.

 

(i)            Mradi Na. 4323: Kuendeleza Elimu ya Ualimu - TESP

Hatua iliyofikiwa ni: Kukamilika kwa ujenzi wa Chuo cha Ualimu Kabanga; kuendelea na ujenzi na ukarabati wa maabara za sayansi, maktaba na vyumba vya TEHAMA katika Vyuo saba (7) vya Butimba (asilimia 100), Morogoro (asilimia 90), Tukuyu (asilimia 92), Kasulu (asilimia 90), Patandi (asilimia 91), Mpwapwa (asilimia 70) na Dakawa (asilimia 70); kuendelea na ununuzi wa vifaa vya TEHAMA ambapo kazi ya uunganishaji wa vyuo 35 vya ualimu katika Mkongo wa Taifa umefikia asilimia 40; ununuzi wa vifaa vya kufundishia na kujifunzia kwa vyuo vya ualimu 35; ununuzi wa vifaa na madawa ya maabara katika vyuo 10 vya ualimu vya sayansi; na kuendelea na uundaji wa mfumo wa usahihishaji wa kielektroniki ambapo utekelezaji umefikia asilimia 85. Jumla ya shilingi bilioni 12.35 zimetumika katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023

 

(j)            Mradi Na. 4340: Mikopo kwa Wanafunzi wa Elimu ya Juu

Hatua iliyofikiwa ni: Kutolewa kwa mikopo yenye thamani ya shilingi bilioni 652.1 kwa wanafunzi 202,877 (wanafunzi 72,973 ni wa mwaka wa kwanza na wanafunzi 129,904 ni wanaoendelea na masomo); kuwezesha ukusanyaji wa mikopo iliyoiva ya shilingi bilioni 141.3 sawa na asilimia 61 ya lengo mwaka mzima wa bajeti; kutolewa kwa shilingi bilioni 2.75 kwa ajili ya kudhamini wanafunzi 593 wenye ufaulu wa juu zaidi katika programu za Sayansi, Teknolojia, Uhandisi na Hisabati (STEM) kupitia Samia Scholarship; na kuanzishwa kwa Kituo Mahsusi cha Wateja. Jumla ya shilingi bilioni 655.51 zimetumika katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023.

 

(k)           Mradi Na. 4392: Mradi wa Elimu wa Kukuza Stadi za Kazi na Ujuzi ya ESPJ

Hatua iliyofikiwa ni: Kuendelea na ukarabati na ujenzi wa vyuo 14 vya maendeleo ya wananchi (FDCs) ambapo ujenzi umefikia asilimia 95, vyuo 25 vya Ufundi Stadi vya Wilaya (asilimia 96) na Chuo cha Ufundi cha Dodoma (asilimia 78); kutoa mafunzo ya ujuzi kwa vijana 2,373 walio katika mazingira magumu kupitia mpango wa Bursary Scheme na mafunzo kwa watanzania 5,030 kupitia programu ya mafunzo ya Utarajali na Uanagenzi; na kuwajengea uwezo watumishi 2,400 wa VETA na FDCs kwa lengo la kuimarisha stadi za ujuzi. Jumla ya shilingi bilioni 27.7 zimetumika katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023.

 

(l)            Mradi Na. 4315: Mradi wa Elimu ya Juu kwa Mageuzi ya Kiuchumi (Higher Education for Economic Transformation Project - HEET)

Hatua iliyofikiwa ni: kuendelea na taratibu za manunuzi ya kuwapa wakandarasi na washauri elekezi kwa ajili  ya ujenzi na ukarabati wa miundombinu katika vyuo 22 vya elimu ya juu vinavyonufaika na mradi; kuendelelea na taratibu za kuhuisha na kuandaa mitaala mipya ili iendane na mahitaji ya soko la ajira ikiwemo kutoa mafunzo, kuandaa vigezo vya ulinganifu wa progamu; kutoa mafunzo ya kushughulikia malalamiko (washiriki ), kuimarisha ushirikiano na sekta binasi (Industrial linkages) (washiriki 66); kuendelea kutoa mafunzo ya muda mrefu kwa watumishi 327 (ndani na nje ya nchi) ambapo 220 ni uzamivu (Phd) na 107 ni uzamili (masters); kuanza maboresho ya miundombinu ya TEHAMA kwa kutoa mafunzo ya ufundishaji na ujifunzaji kwa njia ya masafa na kuongeza kasi ya Interneti, kuanzisha madawati ya jinsia 21 katika vyuo vya elimu ya juu 21 vinavyonufaika na mradi. Jumla ya shilingi bilioni 32.3  zimetumika katika kipindi cha nusu mwaka.

 

(m)         Mradi Na. 4314: Upanuzi na Ukarabati wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Mkwawa (MUCE) 

Hatua iliyofikiwa ni: Kuendelea na ujenzi wa maabara ya baiolojia ya viumbe hai ambapo utekelezaji umefikia asilimia 88;na kuendelea na ukarabati wa miundombinu mbalimbali ya chuo (asilimia 75). Jumla ya shilingi milioni 210.2 zimetumika katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023. 

 

(n)          Mradi Na. 6350 Chuo Kikuu cha Dar es Salaam

Hatua iliyofikiwa ni: kuendelea na ujenzi wa jengo la Shule Kuu ya Uchumi (asilimia 46) na maabara kuu ya kemikali kwa ajili ya utafiti na kutoa huduma za kupima sampuli za viwandani (asilimia 20); kuendelea na upanuzi wa hosteli ya Dkt. John Pombe Joseph Magufuli kwa kuongeza ghorofa mbili (2) ambapo utekelezaji umefikia asilimia 15; na kuanza utekelezaji wa mradi wa ubunifu wa utengenezaji wa vifaa vya maabara vya mashuleni (asilimia 50). Jumla ya shilingi bilioni 5.7 zimetumika katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023. 

 

(o)          Mradi Na. 4385: Upanuzi na Ukarabati wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam (DUCE)

Hatua iliyofikiwa ni: Kuendelea na awamu ya pili ya ujenzi wa miundombinu ya maabara za sayansi katika shule ya sekondari ya mazoezi ya Chang’ombe ambapo utekelezaji umefikia asilimia 60; na kuendelea na ujenzi wa Jengo la Kitivo cha Insia na Sayansi za Jamii na Maabara za Sayansi. Jumla ya shilingi bilioni 1.5 zimetumika katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023

 

(p)          Mradi Na. 6353: Upanuzi wa Chuo Kikuu Mzumbe 

Hatua iliyofikiwa ni: kukamilika kwa ukarabati wa jengo la maktaba (wanafunzi 3,000) Kampasi Kuu na Zahanati Kampasi ya Mbeya; kuendelea na ujenzi wa jengo la utawala (asilimia 5) na jengo la madarasa sita (6) lenye uwezo wa kuhudumia wanafunzi 3,129 Kampasi Kuu (asilimia 5); kuendelea na ukarabati wa eneo la mahafali (asilimia 70), viwanja vya michezo (asilimia 44) na madarasa 6 (asilimia 60) katika Kampasi Kuu, bwalo la chakula Kampasi ya Mbeya (asilimia 91); na kuendelea na uwekaji wa taa za barabarani Kampasi Kuu (asilimia 80). Jumla ya shilingi milioni 635.5 zimetumika katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023.

 

(q)          Mradi Na. 6354: Ukarabati na Upanuzi wa Chuo Kikuu Ardhi

Hatua iliyofikiwa ni: Kuendelea na ujenzi wa ukumbi wa midahalo, madarasa, maabara, studio, karakana, jengo la shahada za juu na utafiti pamoja na mabweni; kuendelea na ukarabati wa karakana (asilimia 50), madarasa 15 (asilimia 50), ofisi 5 (asilimia 50), maabara 2 (asilimia 50), mabweni ya wanafunzi 3 (asilimia 50), nyumba 10 za watumishi (asilimia 50) na miundombinu ya TEHAMA (asilimia 50). Jumla ya shilingi milioni 165.68 zimetumika katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023.

 

(r)            Mradi Na. 6365: Upanuzi na Ukarabati wa Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi

Hatua iliyofikiwa ni: kuendelea na ujenzi wa jengo jipya la maktaba (asilimia 8 na ukumbi wa mihadhara ambapo ujenzi umefikia asilimia 28; kuendelea na ujenzi wa jengo la ghorofa lenye kumbi tisa za mihadhara lenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 2,334 kwa wakati mmoja (asilimia 46.6); kuendelea na ukarabati na upanuzi wa jengo la Kurugenzi ya Shahada za Awali (asilimia 95) nakuendelea na ukarabati wa jengo la ofisi za wanataaluma (asilimia 99);, na ofisi 174 za Chuo za mikoani (asilimia 5); na kukamilika kwa ujenzi wa jengo la stoo na choo na ununuzi wa gari moja (1). Jumla ya shilingi milioni 303.8 zimetumika katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023.

 

(s)           Mradi Na. 6364: Ujenzi wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili - Kampasi ya Mloganzila

Hatua iliyofikiwa ni: kuendelea na ununuzi wa vifaa vinavyotumia umeme wa jua ili kukuza matumizi ya teknolojia ya kijani kibichi na kupunguza matumizi makubwa ya umeme (asilimia 85); kuendelea na ujenzi wa tanki kubwa la maji katika na Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (asilimia 40); kuendelea na ukarabati wa Hosteli 4 za wanafunzi na ujenzi wa miundombinu (mihadhara, madarasa, ofisi za utawala na walimu) Kampasi Kuu ya Muhimbili - Upanga (asilimia 50.0); na ukarabati wa awamu ya pili wa miundombinu (nyumba moja ya utafiti na mifumo ya maji na umeme) ya kituo cha kufundishia cha Bagamoyo cha kampasi ya Muhimbili (asilimia 80.6); na ukarabati wa mabweni 6 ya Chole (asilimia 80). Jumla ya shilingi bilioni 1.5 zimetumika katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023.

 

(t)            Mradi Na. 4384: Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaaam – DIT 

Hatua iliyofikiwa ni: Kuendelea na ujenzi wa madarasa matano (5) yenye uwezo wa kuhudumia wanafunzi 200 na mabweni mawili (2) yenye uwezo wa kuhudumia wanafunzi 160 Kampasi ya Myunga ambapo ujenzi umefikia asilimia 95; kuanza ujenzi wa mabweni 2 Kampasi ya Mwanza yenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 300 (asilimia 20); na kuratibu mafunzo kwa washiriki 71 katika TEHAMA, Sayansi ya Maabara na Teknolojia ya Ngozi. Jumla ya shilingi bilioni 2.0 zimetumika katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023.

 

(u)          Mradi Na. 6352: Tume ya Nguvu za Atomiki - TAEC

Hatua iliyofikiwa ni: Kukamilika kwa awamu ya Pili ya Ujenzi wa Maabara na Ofisi zilizopo Arusha na Dodoma; kuendelea na ujenzi wa ofisi na maabara Dar es Salaam (asilimia 63), ujenzi wa ofisi na maabara Mwanza (asilimia 84) na ujenzi wa maabara ya Zanzibar (asilimia 36);  kuendelea na ujenzi wa jengo maalumu la kuhifadhi ya kilimo kwa kutumia teknolojia ya mionzi ambapo utekelezaji umefikia asilimia 34.0; na kuendelea na ujenzi wa jengo maalumu kwa ajili ya kuhifadhi mazao ya kilimo (asilimia 34). Jumla ya shilingi bilioni 2.1 zimetumika katika nusu ya kwanza ya mwaka 2022/23). Jumla ya shilingi bilioni 2.1 zimetumika katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023.

 

(v)           Mradi Na. 6333: Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya - MUST

Hatua iliyofikiwa ni: kuendelea na ujenzi wa hosteli mbili (2) zitakazosaidia wanafunzi wenye mahitaji maalumu (asilimia 44); kukamilika kwa ukarabati wa miundombinu mbalimbali ya Chuo; kuendelea na ununuzi wa vifaa vya kisasa kwa ajili ya maabara na karakana (asilimia 98); na kuendelea na ujenzi wa mabweni mawili (2) yatakayohudumia wanafunzi 800 (asilimia 48). Jumla ya shilingi milioni 84.0 zimetumika katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023.

 

(w)         Mradi Na. 6361: Upanuzi na Ukarabati wa Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine – SUA 

Hatua iliyofikiwa ni: Kuendeleza shamba la miti la Ifinga, kwa kupanda hekta 1,364 za miti; kuendelea na ukarabati wa Hosteli katika Kampasi ya Edward Moringe (asilimia 70); na kununua mtambo wa kisasa wa kuchakata mbao katika kituo cha mafunzo kampasi ya Olmotony na kiwanda cha mbao katika Kampasi ya Mizengo Pinda. Jumla ya shilingi bilioni 7.9 zimetumika katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023.

 

(x)           Mradi Na. 6229: Ukarabati wa Vyuo vya Maendeleo ya Wananchi - FDC 

Hatua iliyofikiwa ni: Kuendelea na ujenzi wa majiko na gesi kwa ajili ya vyuo 54 vya maendeleo ya wananchi (asilimia 93); kuendelea na ununuzi wa vifaa vya karakana katika vyuo 34 vya maendeleo ya wananchi (asilimia 82); na kuendelea na ujenzi na ukarabati wa miundombinu ya vyuo 14 vya maendeleo ya Wananchi (asilimia 90). Jumla ya shilingi bilioni 7.9 zimetumika katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023. 

 

(y)           Mradi Na. 4381: Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere 

Hatua iliyofikiwa ni: kuendelea na ujenzi wa mabweni mawili (2) awamu ya pili  yatakayohudumia wanafunzi 768 kila moja katika kampasi ya Karume – Zanzibar (asilimia 45) na ujenzi wa Jengo la Maktaba na ukumbi wa mihadhara (asilimia 25), kukamilika kwa uwanja wa mpira wa kikapu na ukarabati wa Jengo la Uhuru katika Kampasi ya Kivukoni na jengo la Utawala katika Kampasi ya Karume, vyoo vya wanafunzi katika jengo la utamaduni na ukarabati wa miundombinu na kuweka samani katika mabweni ya Azimio, Kizota, Kawawa na kijichi; na kukamilika kwa   ukarabati wa  kumbi za mihadhara za Garden Hall 3, Garden Hall 4 na Jengo la Uhuru katika Kampasi ya Kivukoni kufanya ukarabati wa mabweni na kuweka samani katika mabweni ya Azimio, Kizota, Kawawa na kijichi  na Jengo la Utawala. Jumla ya shilingi bilioni 4.2 zimetumika katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023. 

 

(z)           Mradi Na. 4306: Wakala wa Maendeleo ya Uongozi wa Elimu (ADEM) Hatua iliyofikiwa ni: kuendelea na ujenzi wa jengo la ghorofa moja (1) lenye ofisi kumi (10) na kumbi nne (4) za mihadhara zenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 500 (asilimia 70); na ujenzi wa kumbi za mihadhara katika kampasi ya Bagamoyo (asilimia 5). Jumla ya shilingi milioni 378.6 zimetumika katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023. 

 

(aa)       Mradi Na. 6345: Mfuko wa Utafiti na Maendeleo wa COSTECH

Hatua iliyofikiwa ni: Kuendelea na ugharamiaji wa miradi 174 (ubunifu 133, utafiti 30 na miundombinu ya utafiti 11;  kutoa mafunzo ya awali ya ubunifu kwa washindi 27 wa MAKISATU; kufanya mafunzo ya kuongeza uelewa juu ya Miongozo ya kutambua, kukuza ubunifu, uvumbuzi na maarifa asilia kwa Halmashauri 23; kuwezesha uanzishwaji wa Kituo cha Ubunifu katika Tume ya Mipango ya Zanzibar (ZPC) na kuzindua kituo cha ubunifu (innovation space) kwa ajili ya  kuwajengea uwezo vijana kitaalamu na pia kutumika kama kituo cha incubation; kutoa mafunzo ya masuala ya baiyoteknolojia kwa washiriki 77 Zanzibar na washiriki 170 katika Mkoa wa Mara na Simiyu; kuandaa mfumo wa uhawilishaji wa teknolojia (technology transfer system) pamoja na mapitio ya teknolojia zinazoibuka (Inventory of emerging technologies); na kuendelea na uboreshaji na uimarishaji wa miundombinu na mfumo wa TEHAMA wa Menejimenti ya Utafiti na Ubunifu ili kuongeza ufanisi na upatikanaji wa taarifa za watafiti na wabunifu. Jumla ya shilingi bilioni 2.4 fedha za ndani zimetumika katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023. 

 

(bb)       Mradi Na. 6327: Ujenzi na Ukarabati wa Majengo ya Serikali

Hatua iliyofikiwa ni kuendelea na ukamilishaji wa maboma: ya madarasa ya shule za msingi 809; vyumba vya maabara za Sayansi 271 katika Shule za sekondari; mabwalo ya chakula manne (4) katika shule za  msingi na mabwalo 74 katika shule za sekondari; na mabweni 64 katika shule za msingi zenye mahitaji maalum na mabweni 115 kwa shule za sekondari. Shughuli nyingine zilizofanyika ni kuendelea na ukamilishaji wa: nyumba za walimu 113  katika shule za msingi; madarasa ya shule kongwe 1,072; uzio shule maalamu 35; vyoo shule shikizi 2,726; kukamilika kwa ujenzi wa madarasa 8,000 ya shule za sekondari katika mikoa yote 26; na ujenzi wa shule sita (6) mpya za Msingi. Jumla ya shilingi bilioni 233 zimetumika katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023.

 

(cc)       Mradi Na. 4322 na 4393: Elimumsingi na Sekondari Bila Ada

Hatua iliyofikiwa ni: Kuendelea kutoa elimumsingi bila ada ikijumuisha ruzuku ya uendeshaji wa shule, posho ya madaraka kwa walimu wakuu 21,335 na maafisa elimu kata 3,921, fidia ya ada kwa shule za bweni kwa wanafunzi 204,439 na kutwa 2,341,438 na kugharamia chakula cha wanafunzi 226,723 wa shule za bweni  na wanafunzi wenye mahitaji maalum 45,366 wa shule za msingi za kutwa. Jumla ya shilingi bilioni 295.3 zimetumika katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023.

 

(dd)       Mradi Na. 4309: Mradi wa Kujenga Ujuzi Afrika Mashariki (EASTRIP) Hatua iliyofikiwa ni: Kuendelea na ujenzi wa Miundombinu (Karakana, Mabweni,

Kumbi za Mihadhara na Nyumba za Watumishi) katika kituo cha Umahili cha Kikuletwa; kuendelea na ujenzi wa majengo nane (8) kwa ajili ya madarasa, maabara, karakana na ofisi za watumishi ambapo majengo matano (5) yanajengwa katika Kampasi ya Mabibo – Dar es salaam na majengo Matatu (3) katika Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Kilimanjaro; na ununuzi wa vifaa maalum vya mafunzo ya wahudumu wa ndani ya ndege (Fixed Cabin Crew Mock – Ups). Jumla ya shilingi 691.5 bilioni zimetumika katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023. 

 

(ee)       Mradi Na. 6321: Ujenzi na Ukarabati wa Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA)

Hatua iliyofikiwa ni: Kuendelea na ujenzi wa jengo la utawala Kampasi ya Babati ambapo utekelezaji umefikia asilimia 60. Jumla ya shilingi bilioni 2.0 zimetumika katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023.

 

(ff)          Mradi Na. 6322: Ujenzi na Ukarabati wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM)

Hatua iliyofikiwa ni: kuendelea na ujenzi wa madarasa, jengo la utawala, bwalo la chakula pamoja na ukumbi wa shughuli mbalimbali (multipurpose hall) ambapo utekelezaji umefikia asilimia 96.7. Aidha, ujenzi wa bweni, nyumba za wafanyakazi, maktaba na maabara za kompyuta umefikia asilimia 47. Jumla ya shilingi bilioni 1.97 zimetumika katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023.

 

(gg)       Mradi Na. 6323: Ujenzi na Ukarabati wa Chuo cha Uhasibu Tanzania (TIA)

Hatua iliyofikiwa ni: Kuendelea na ujenzi wa jengo la utawala, madarasa na maktaba katika Kampasi ya Nyang’homango, Misungwi - Mwanza ambapo utekelezaji umefikia asilimia 73. Jumla ya shilingi bilioni 1.7 zimetumika katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023.

 

(hh)       Mradi Na. 6206: Upanuzi na Ukarabati wa Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini (IRDP)

Hatua iliyofikiwa ni: kuendelea na ujenzi wa ukumbi wa mihadhara awamu ya pili katika Kampasi Kuu Dodoma ambapo ujenzi umefikia asilimia 65; ujenzi wa bweni la wanafunzi katika Kituo cha Mafunzo Kanda ya Ziwa - Magu Mwanza ambapo ujenzi umefikia asilimia 60; na kuanza kwa hatua za awali za ujenzi wa bweni la wanafunzi awamu ya III katika eneo la Miyuji Kampasi Kuu Dodoma. Jumla ya shilingi bilioni 3.32 zimetumika katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023.

 

2.3.5.4. Ardhi, Mipango Miji, Nyumba na Maendeleo ya Makazi

(a)         Mradi Na. 2326: Programu ya Kupanga, Kupima na Kumilikisha Ardhi 

Hatua iliyofikiwa ni: Kununuliwa kwa vifaa vya upimaji vya kisasa (RTK) kwa ajili ya kuharakisha shughuli za upangaji na upimaji katika halmashauri za Manispaa ya Mtwara Mikindani, Njombe Mji, Maswa DC, Tarime TC na Shinyanga Manispaa; kurejeshwa kwa ardhi yenye ukubwa wa ekari 2,385,317 kwa wananchi kutoka katika meneo ya Hifadhi, mapori tengefu, hifadhi za misitu, Ranchi za Taifa na mashamba ya Serikali; na kupimwa kwa viwanja 116,499 na mashamba 401; kazi za uthamini wa ardhi na mali unaendelea katika eneo la Ghuba ya Speke lenye ukubwa wa ekari 14,250 wilayani Serengeti, bonde la mto kilombero na maeneo mengine yenye maslahi kwa Taifa.  Aidha, upimaji ardhi kwa ajili ya maeneo ya vituo vya kusukuma mafuta ghafi vilivyopo Kikagate (Muleba), Lubeho (Mbogwe), Nanga (Igunga), Misindo (Singida), Kimana (Kiteto), Sindeni (Handeni) na Chongoleani (Tanga) pamoja na kupima barabara (access roads) unaendelea; na maandalizi ya mpango kabambe wa Jili la Kibiashara na Uwekezaji Kwala (Pwani) yanaendelea. Jumla ya shilingi bilioni 3.714 zimetumika katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023.

 

(b)         Mradi Na. 2324: Mradi wa Kuimarisha Mipaka ya Kimataifa

Hatua iliyofikiwa ni: Kutekelezwa kwa kazi ya kupima na kujenga alama za mpaka kwenye mpaka wa Tanzania na Kenya. Jumla ya kilomita 110 zimeimarishwa kutoka Ziwa Natroni hadi Namanga na hivyo kufanya kipande cha mpaka kilichoimarishwa kuwa kilometa 348 kati ya kilometa 758 za mpaka wa nchi kavu wa Tanzania na Kenya. Aidha, ukaguzi wa kipande cha mpaka kutoka Namanga hadi Tarakea chenya urefu wa kilomita 110 umekamilika na uimarishaji wa mpaka unaendelea. Jumla ya shilingi milioni 36.0 zimetumika katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023.

 

(c)         Mradi Na. 6327: Ujenzi na Ukarabati wa Majengo  

Hatua iliyofikiwa ni: Ukarabati na ununuzi wa samani za ofisi katika Mabaraza ya Ardhi na Nyumba ya Wilaya matatu (3) Busega, Kishapu na Kyerwa; Kuendelea na ukamilishaji wa jengo la Maktaba katika Chuo cha Ardhi Tabora (ARITA) na ujenzi wa vyumba vya madarasa viwili (2) katika Chuo cha Ardhi Morogoro. Jumla ya shilingi milioni 155.6 zimetumika katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023.

 

(d)         Mradi Na. 4951: Upangaji wa Matumizi ya Ardhi

Hatua iliyofikiwa ni: Kuandaliwa kwa mipango ya matumizi ya ardhi ya Halmashauri za Wilaya tatu (3) za Nsimbo (Katavi), Ngorongoro (Arusha) na Kigoma (Kigoma); kuandaliwa mipango ya matumizi ya ardhi ya vijiji 75 katika Halmashauri za Wilaya sita (6) za Kilosa (13), Rufiji (20), Mkalama (4), Kondoa (6), Bahi (10) na Ngorongoro (22) katika shoroba tatu za mradi wa SGR, Bomba la Mafuta (EACOP) na Mradi wa uzalishaji wa Umeme wa Mwalimu Nyerere (JNHPP); kuandaliwa kwa mipango kina 14 ya vitovu vya vijiji na mashamba katika Halmashauri za Wilaya  za Nzega,  Kondoa, Mkalama, Handeni na Chalinze; kuwajengea uwezo wajumbe 248 kutoka halmashauri za wilaya 31, wajumbe 6,120 wa halmashauri za vijiji 306, wajumbe 2,448 wa Kamati za uandaaji na usimamizi wa mipango ya matumizi ya ardhi ya vijiji 306, wajumbe 2,142 wa Mabaraza ya Ardhi ya Vijiji 306 kuhusu uandaaji na usimamizi wa mipango ya matumizi ya ardhi ya vijiji; na kuhuishwa kwa mipaka ya kiutawala ya vijiji 98 vilivyopo katika Wilaya za Meatu (12), Ngorongoro (36), Kilosa (8), Sumbawanga (4), Kondoa (2), Wanging’ombe (2), Iringa (2), Tanganyika (2), Mpimbwe (3), Bahi (4), Rufiji (8), Mkalama (2), Itilima (10) na Busega (3). Jumla ya shilingi bilioni 1.8 zimetumika katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023.

 

(e)         Mradi Na. 4953: Uboreshaji wa Milki za Ardhi

Hatua zilizofikiwa ni: Kuwajengea uwezo viongozi 44 na watumishi 45 katika jiji la Dodoma kuhusu utekelezaji wa mradi kwa upande wa mjini; kuwajengea uwezo Halmashauri tatu (3) za Chamwino, Longido na Maswa kupitia majaribio ya mradi kwa upande wa vijijini; kuwekwa kwa alama za upimaji katika ardhi za halmashauri za Dodoma Jiji (13), Chalinze (27), Mafinga (14) na Rungwe (14); kuendelea na uandaaji wa Mipango ya Matumizi ya Ardhi ya wilaya sita (6) za Chamwino, Longido, Maswa, Mbinga, Mufindi na Songwe; na kujengwa kwa mtandao kiambo (Local Area Network) katika Ofisi za Ardhi za Mikoa ya Iringa, Lindi, Mwanza na Mbeya na kununua mtambo wa kuzalisha Ramani (DPW). Aidha, Hati za Hakimiliki za Kimila 3,584 zimeandaliwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika. Jumla ya shilingi bilioni 1.1 zimetumika katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023.

 

2.3.5.5. Huduma za Maji na Usafi wa Mazingira

(a)         Huduma za Maji na Usafi wa Mazingira

Hatua iliyofikiwa ni kuimarika kwa hali ya upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama kwa wananchi wa vijijini kutoka wastani wa asilimia 70.1 mwaka 2020 hadi asilimia 77 mwezi Desemba, 2022 na kwa upande wa maeneo ya mijini kutoka wastani wa asilimia 84 mwaka 2020 hadi wastani wa asilimia 88 mwezi Desemba, 2022.

 

(b)         Mradi Na. 3436: Ufuatiliaji na Uratibu wa Programu ya Maendeleo ya Sekta ya Maji (WSDP - II) 

Hatua iliyofikiwa ni: ukarabati wa mabweni matano (5) katika chuo cha maji; ununuzi wa eneo la ekari 41.5 katika Manispaa ya Singida kwa ajili ya ujenzi wa Kampasi ya Singida ya Chuo cha Maji; kugharamia wataalamu washauri wanne (4) kutoa huduma katika maeneo ya usimamizi wa fedha na ununuzi wa mradi wa WSDP II; na kuendelea na ujenzi wa mabweni mawili (2) ambayo utekelezaji umefikia wastani wa asilimia 90. Jumla ya shilingi bilioni 7.39 zimetumika katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023.

 

(c)         Mradi Na. 6545: Kusimamia na Kuendeleza Rasilimali za Maji Nchini  Hatua iliyofikiwa ni: Kukarabati vituo 136 na kujenga vituo sita (6) vya kufuatilia rasimali za maji nchini;  kuanzishwa kwa jumuiya 22 za watumiaji wa maji; kupima na kuweka mipaka katika vyanzo 63 kama hatua ya awali ya kuvilinda na kuvitangaza pamoja na kutangaza vyanzo 41 kwenye Gazeti la Serikali kuwa maeneo tengefu;  na kukamilika kwa ukarabati na ujenzi wa ofisi za mabonde ya Ziwa Nyasa katika Miji ya Njombe, Ziwa Rukwa, Wami - Ruvu na ofisi za Bonde la Ruvuma na Pwani ya Kusini katika miji ya Lindi na Mtwara. Jumla ya shilingi bilioni 29.87 zimetumika katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023.

 

(d)         Mradi Na. 3435: Ufuatiliaji wa Ubora wa Maji na Usimamizi wa Mfumo wa Ikolojia 

Hatua iliyofikiwa: Kufuatilia, kukusanya na kuchunguza ubora wa maji kwenye jumla ya sampuli 4,461 ambapo matokeo yalioneonesha kuwa sampuli 3,190 zilikidhi ubora; na kuendelea kuimarisha maabara za ubora wa maji kwa kuzipatia vitendea kazi, pamoja na kuziwezesha maabara nne (4) kupata ithibati. Jumla ya shilingi bilioni 5.07 zimetumika katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023.

 

(e)         Mradi Na. 3280: Huduma za Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini 

Hatua iliyofikiwa ni kukamilika kwa utekelezaji wa miradi 586 yenye vituo 5,748 vya kuchotea maji vinavyonufaisha wananchi wapatao 4,086,442 kwenye vijiji 1,293. Jumla ya shilingi bilioni 219.88 zimetumika katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023.

 

(f)          Mradi Na. 3306: Ujenzi, Ukarabati na Upanuzi wa Miradi ya Maji katika Miji Mikuu ya Mikoa 

Hatua iliyofikiwa ni: kukamilika kwa uchimbaji wa visima vitano (5) katika jiji la Dodoma; kukamilika kwa ujenzi wa choteo jipya katika mradi wa maji na usafi wa mazingira mji wa Kigoma; kuendelea na utekelezaji wa mradi wa maji na usafi wa mazingira Arusha ambapo utekelezaji umefikia asilimia 92.67; na kuendelea na ujenzi wa miundombinu ya majitaka katika mji wa Musoma ambao umefikia asilimia 13. Jumla ya shilingi bilioni 77.79 zimetumika katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023.

 

 

 

(g)         Mradi Na. 3307: Ujenzi, Ukarabati na Upanuzi wa Miradi ya Maji katika Miji Mikuu ya Wilaya, Miji Midogo na Miradi ya Kitaifa 

Hatua iliyofikiwa ni: kukamilika kwa awamu ya kwanza ya mradi wa uboreshaji maji katika miji ya Tinde na Shelui;  na kuendelea na utekelezaji wa mradi wa Mugango – Kiabakari - Butiama ambapo utekelezaji wake umefikia asilimia 79. Jumla ya shilingi bilioni 103.19 zimetumika katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023.

 

(h)         Mradi Na. 3342: Mradi wa Maji wa Tabora – Igunga - Nzega 

Hatua iliyofikiwa ni: Kukamilika kwa upanuzi wa mradi wa Tabora – Nzega – Igunga kupeleka maji katika miji ya Tinde na Shelui; na kuendelea na ujenzi wa miundombinu ya kusambaza maji katika miji ya Nzega, Uyui, Tabora, Igunga, tinde na Shelui. Jumla ya shilingi bilioni 6.90 zimetumika katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023.

 

(i)           Mradi Na. 3403: Mradi wa Maji wa Ziwa Victoria - Kahama – Shinyanga na Miji Mingine

Hatua iliyofikiwa ni: Kukamilika kwa zoezi la kulipa fidia, usanifu wa bomba kuu na kuhamisha makaburi 78 kwenye eneo la mradi wa kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi katika mkoa wa Simiyu; na kuendelea na usanifu wa miundombinu ya kusambaza maji katika miji na vijiji 147 kandokando ya bomba kuu, mabwawa ya kumwagilia. Jumla ya shilingi bilioni 28.72 zimetumika katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023.

 

(j)          Mradi Na. 3437: Mradi wa Uboreshaji wa Huduma ya Maji eneo la DAWASA

Hatua iliyofikiwa ni: Kukamilika kwa usambazaji wa maji katika maeneo ya Mshikamano, zegereni na Chalinze III; na kukamilika kwa awamu ya kwanza ya mradi wa kutoa maji kutoka kwenye tanki la Chuo Kikuu Ardhi na kupeleka Bagamoyo; na kuendelea na ujenzi wa mradi wa kusambaza maji katika maeneo ya Mbezi - Makabe ambao umefikia asilimia 76. Jumla ya shilingi bilioni 45.46 zimetumika katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023. 

 

(k)         Mradi Na. 3439: Mradi wa Maji wa Mpera na Kimbiji 

Hatua iliyofikiwa ni: Kukamilika kwa ujenzi wa tanki la kuhifadhi maji ujazo wa lita milioni 15 katika eneo la Kisarawe II;  na kuendelea na ujenzi wa miundombinu ya kusambaza maji katika maeneo ya Kigamboni ambapo utekelezaji umefikia asilimia 95. Jumla ya shilingi bilioni 2.82 zimetumika katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023.

 

(l)           Mradi Na. 3438: Mradi wa Bwawa la Kidunda 

Hatua iliyofikiwa ni: Hatua iliyofikiwa ni: kupatikana kwa Mkandarasi wa ujenzi na Mtaalam Mshauri atakayesimamia ujenzi wa bwawa. Jumla ya shilingi bilioni 59.22 zimetumika katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023.

 

2.3.5.6. Hifadhi ya Mazingira na Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi

(a)        Programu Na. 5301: Kuhimili Athari za Mabadiliko ya Tabianchi 

(i)           Mradi wa Kuhimili Athari ya Mabadiliko ya Tabia Nchi Kupitia Mifumo ya Ikolojia 

Hatua iliyofikiwa ni: Kukamilika kwa uchimbaji wa visima virefu 12 vyenye urefu wa mita kati ya 100 hadi 150; kukamilika kwa ujenzi wa majosho sita (6) na majosho saba (7); kukamilika kwa ujenzi wa viwanda vidogo viwili (2) vya bidhaa za ngozi na kimoja (1) cha kuchakata mafuta ya Alizeti. Jumla ya shilingi bilioni 3.8 zimetumika katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023.

 

(ii)         Mradi wa Kurejesha Ardhi Iliyoharibika na Kuongeza Usalama wa Chakula katika Maeneo Kame ya Tanzania  

Hatua Iliyofikiwa ni: kuanzisha mashamba darasa 127 kwa ajili ya kusambaza teknolojia na mbinu bora za kilimo cha mazao ya mahindi, mpunga, mtama, mihogo, alizeti, mwani na migomba; kukamilika kwa ukarabati wa tuta lenye urefu wa mita 850, ujenzi wa spill ways mbili na kukarabati spill way moja katika eneo la Bonde la Ukele - Pemba; upandaji wa miti katika maeneo ya vijiji na shehia za Micheweni (1,967,225), Nzega (8850), Mkalama (3,000), Kondoa (1,100) na Magu (1,500); na kutengeneza na kutundika Mizinga ya Nyuki 3,665 kwa wilaya za Nzega (1,072), Mkalama (1,520), Kondoa (600), Magu (241) na Micheweni (222). 

 

Aidha, shughuli nyingine zilizotekelezwa ni: Kutolewa kwa Hati Miliki za Kimila za ardhi 855 kwa Wilaya za Kondoa (305) na Mkalama (550); kuchimba visima virefu na vifupi 22 katika Halmashauri ya Magu (5), Nzega (6), kondoa (6), Mkalama (3) na Micheweni (2); kujenga maghala matatu (3) ya kuhifadhi mpunga katika Wilaya za Nzega (1) na Mkalama (2); kujenga vituo vitatu (3) vya kukusanya mazao ya nyuki katika Halmashauri za Nzega (1), Mkalama (1) na Magu (1); kukamilika kwa ujenzi wa mabanda 12 ajili ya mifugo katika halmashauri ya Magu (3); Nzega (3), Kondoa (2); na Micheweni (4); kukamilika kwa ujenzi wa majiko banifu 257 kwa kaya 250 na taasisi 7; kutoa mafunzo kuhusu matumizi ya majiko banifu kwa wanufaika 293 katika Wilaya za Micheweni (72), Kondoa (47), Mkalama (65), Magu (63) na Nzega (46) na; kutoa mafunzo ya masoko na ubora wa bidhaa kwa wanufaika 342 katika Wilaya za Micheweni (72), Mkalama (85), Magu (89) na Nzega (96). Jumla ya shilingi bilioni 2.02 zimetumika katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023.

 

(iii)       Mradi wa Majaribio wa Kikanda wa Kuhimili Mabadiliko ya Tabianchi katika Bonde la Ziwa Victoria (ACC - LVB Project)

Hatua iliyofikiwa ni: Kukamilika kwa shuguli za mradi kwa vikundi vya kijamii 16 ambavyo vinafanya shughuli za ufugaji wa Kondoo, Kuku, Nguruwe, unenepeshaji wa Ng’ombe, kilimo bora, ushonaji wa nguo na kuongeza mnyororo wa thamani kwa mazao ya nyuki. Aidha, katika mradi vikundi mbalimbali vimewezeshwa kama ifuatavyo: Vikundi viwili (2) kwa Ng’ombe 30, kujengewa mazizi mawili (2) na kupatiwa vyakula na madawa; Vikundi vitatu (3) kwa kondoo 110, kujengewa mabanda matatu (3) yenye uwezo wa kutunza kondoo mia moja  (100) kwa kila banda na kupatiwa chakula na madawa;  Vikundi vitano (5) vimewezeshwa shughuli za kilimo hususan kilimo cha Choroko, Alizeti, bustani na  malisho kwa kuwezeshwa  mbegu, madawa mbolea ambapo zaidi ya ekari 10 zimelimwa; Kikundi kimoja (1) kimewezeshwa vifaa vya ushonaji nguo ikiwa ni pamoja na vyerehani  sita (6), ukarabati na upanuzi wa chumba cha kufanyia shughuli za ushonaji; Kikundi kimoja (1) kimewezeshwa nguruwe (30) na kujengewa banda ambalo lina uwezo wa kutunza nguruwe (80), Kikundi kimoja (1) kimepewa vifaranga 200 na kujengewa banda la kisasa la ufugaji kuku, madawa na chakula  kwa kipindi cha miezi sita (6). 

 

Shughuli nyingine zilizotekelezwa ni: kukarabati na kuweka vifaa vya kuongeza thamani mazao ya nyuki ambapo chumba hiki kitatumika kama shamba darasa la mafunzo kwa wananchi na wanafunzi kuhusu shughuli za uchakataji wa mazao ya nyuki. Aidha, vitalu nyumba vitatu (3) (greenhouse ) kwa ajili ya kilimo cha mbogamboga vimejengwa. Jumla ya shilingi milioni 355.80 zimetumika katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023.

 

(iv)       Mradi wa Kupunguza Hewa Ukaa inayosababishwa na Ukataji na Uharibifu wa Misitu - REDD

Hatua iliyofikiwa ni: Ununuzi wa vifaa kwa ofisi za Wizara za kisekta za Tanzania Bara na Zanzibar ambazo zinatekeleza Mradi; na kuwezesha ushiriki wa Tanzania Katika Mkutano wa 27 (COP 27) wa Mabadiliko ya Tabianchi uliofanyika Misri; kuandaa mwongozo wa biashara ya Hewa Ukaa na kanuni zake; Kutoa mafunzo kwa wataalamu 30 kutoka katika Wizara za Kisekta na Taasisi kuhusu usimamizi na uratibu wa shughuli za kupunguza hewa ukaa inayotokana na ukataji na uharibifu wa misitu; kujenga uelewa wa Masuala ya Mabadiliko ya Tabianchi na biashara ya Kaboni nchini, Kanuni na Mwongozo wa Biashara ya Kaboni kwa Wajumbe wa Kamati za Maji na Mazingira ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Wizara za Kisekta na Wadau wa Biashara ya Kaboni; na kujenga uwezo wa wataalam 30 katika sekta za Misitu, Maliasili, Nishati, Kilimo, Mifugo, Ardhi na Mamlaka ya Serikali za Mitaa ili kuibua na kuandaa maandiko ya miradi ya kuhimili athari za Mabadiliko ya Tabianchi. Jumla ya shilingi milioni 180.0 zimetumika katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023.

 

(v)         Mradi wa Usimamizi Jumuishi wa Mfumo Ikolojia na urejeshwaji wa Uoto Asili na Hifadhi ya Bioanuai 

Hatua iliyofikiwa ni: Kukamilika kwa Taarifa ya msingi kuhusu Sera, Mipango na Mifumo ya kisheria inayoweza kusaidia/kukwamisha utekelezaji ya mipango ya Urejeshwaji Endelevu wa Mazingira na kupendekeza maeneo yanayotakiwa kufanyiwa maboresho; Kukamilika kwa Mipango ya Matumizi ya Ardhi kwa vijiji 15 vilivyopo kwenye mradi; Kukamilika Tathmini ya Athari za Utekelezaji wa Mradi kwa Mazingira na Jamii; Kukamilika kwa uanzishwaji wa mashamba darasa 31 ya kilimo cha mazao himilivu kwa mabadiliko ya tabianchi katika Halmashauri zinazotekeleza mradi; Kukamilika kwa tafiti 13 za kubaini maeneo yanayofaa kuanzisha skimu ndogo za umwagiliaji; Kutoa mafunzo kwa vikundi 35 vyenye wajumbe 543 kuhusu shughuli mbadala za kiuchumi na rafiki kwa mazingira ikiwemo ufugaji bora wa nyuki, samaki, kuku, mbuzi na ng’ombe na uanzishaji wa vituo vya kukusanyia maziwa; na Kukamilika kwa kisima kimoja katika Halmashauri ya Wilaya Mbarali na upanuzi wa miundombinu ya mabomba yenye urefu wa mita 6,350 na vituo vya kuchotea maji saba (7) katika Halmashauri ya Wilaya ya Mpimbwe. Jumla ya shilingi bilioni 2.53 zimetumika katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023.

 

(b)                              Programu Na. 6571: Programu ya Utekelezaji wa Sheria na

Usimamizi wa Hifadhi ya Mazingira ya Mwaka 2004 

 

(i)           Usimamizi Endelevu wa Matumizi ya Ardhi ya Bonde la Nyasa

Hatua iliyofikiwa ni: kuanzishwa kwa Jumuiya mbili (2) za watumia maji katika Wilaya ya Mbinga na kujenga uwezo kwa Jumuiya tatu (3) katika Wilaya ya Nyasa; kuandaa  mipango shirikishi ya usimamizi wa misitu katika halmashauri tano za Wilaya za Mbinga, Nyasa, Kyela, Ludewa na Makete; kutoa mafunzo ya ujasiriamali kwa vikundi vitatu (3) vya Wanawake na vijana katika halmashauri tano za Wilaya za Mbinga, Nyasa, Kyela, Ludewa na Makete; kutoa mafunzo kwa wanakijiji 300 kuhusu kilimo kinachostahimili mabadiliko ya tabianchi; kukamilika kwa tathmini ya mnyororo wa thamani wa mazao makuu (Mpunga, Ngano, Kakau,  Mahindi, Viazi mviringo, Maharage, Alizeti, Korosho) yanayolimwa katika eneo la mradi wa Bonde la Ziwa Nyasa; na kukamilika kwa taarifa ya tathmini ya mbinu bora za kilimo cha asili zinazohifadhi mazingira katika Bonde la Ziwa Nyasa. Jumla ya shilingi milioni 435.09 zimetumika katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023.

 

(ii)         Mradi wa Kujenga Uwezo wa Kitaasisi wa Kutekeleza Sheria ya Usimamizi wa Mazingira

Hatua iliyofikiwa ni: kuandaliwa kwa taarifa ya ya utekelezaji wa Sheria ya Mazingira Sura 191; kuandaliwa kwa Mwongozo na Kanuni ya Dhamana ya Utunzaji wa Mazingira (Environmental Performance Bond Guidelines and Regulations); na kuandaa Kanuni za Mgao wa Faida zitokanazo na Matumizi ya Rasilimali za kijenetiki (Access Benefit Sharing of Genetic Resources Regulation). Jumla ya shilingi bilioni 1.06 zimetumika katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023.

 

 

 

 

(c)         Mradi Na. 5305: Kutekeleza Mpango wa Kitaifa wa Utekelezaji wa Mkataba wa Stockholm Unaohusu Kemikali Zinazodumu katika Mazingira kwa Muda Mrefu

Hatua iliyofikiwa ni: kuendelea na kuandaa Kanuni ya Udhibiti na Usimamizi wa Kemikali zinazodumu kwenye Mazingira kwa Muda Mrefu kwa lugha ya kiingereza; kubaini Transforma zinazosadikiwa kuwa na kemikali za PCBs, kuchukua sampuli 32 kwa upande wa Zanzibar na kuzisafirisha kwenda Afrika Kusini kwa ajili ya uchunguzi wa kimaabara; na kuanzisha eneo maalumu la muda la kuhifadhi mafuta na Transfoma zilizobainika kuwa na Kemikali za PCBs kabla ya kusafirishwa kwenda Ufaransa kwa uteketezaji. Jumla ya shilingi milioni 171.8 zimetumika katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023.

 

(d)         Mradi Na. 5304: Kudhibiti Kemikali Zinazomong’onyoa Tabaka la Ozoni

Hatua iliyofikiwa ni: kutolewa kwa mafunzo kwa maafisa forodha (40) na wasimamizi wa sheria (20) kuhusu njia za kudhibiti uingizwaji nchini wa kemikali na vifaa vyenye kemikali zinazomong’onyoa tabaka la Ozoni; kutolewa kwa mafunzo kwa mafundi mchundo (60) wa viyoyozi na majokofu kuhusu namna ya kuhudumia vifaa hivyo pasipo kuharibu mazingira; na kuandaa Kanuni za Usimamizi na Udhibiti wa Kemikali zinazomong'onyoa Tabaka la Ozoni za mwaka 2022 kwa lugha ya Kiswahili na Kiingereza na kutangazwa kwenye Gazeti la Serikali (GN No.581 na GN No. 582); Jumla ya shilingi milioni 94.7 zimetumika katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023.

 

(e)         Mradi Na. 6309: Ujenzi na Ukarabati wa Ofisi na Makazi ya Makamu wa Rais 

Hatua iliyofikiwa ni: Kuendelea na ukarabati wa Makazi ya Makamu wa Rais, Kilimani Dodoma na jengo la Ofisi ya Makamu wa Rais Luthuli II - Dar es Salaam. Jumla ya shilingi bilioni 1.079 zimetumika katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023..

 

2.3.5.7. Usimamizi wa Maafa Nchini

(i)         Mradi Na. 6575: Kuimarisha Uwezo wa Kujiandaa na Kukabili Maafa  Hatua iliyofikiwa ni: Kutoa mafunzo kwa Kamati mbili (2) za Usimamizi wa Maafa na waratibu wa maafa katika Mikoa ya Lindi na Mtwara; kuandaa mipango ya kujiandaa na kukabiliana na maafa pamoja na mikakati ya kupunguza madhara katika Halmashauri nane (8); na kutoa misaada ya kibinadamu katika Halmashauri nne (4) zilizoripotiwa matukio ya maafa. Jumla ya shilingi bilioni 1.93 zimetumika katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023.

 

(ii)       Mradi Na. 6327: Ujenzi na Ukarabati wa Majengo ya Serikali

Mradi wa Ujenzi wa Kituo cha Usimamizi wa Maafa Nchini

Hatua iliyofikiwa ni: Kuanza kwa ujenzi wa maghala mawili (2) ya kuhifadhi vifaa vya misaada ya kibinadamu wakati wa maafa ambapo utekelezaji umefikia asilimia 83.  Jumla ya shilingi milioni 490.24 zimetumika katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023.

 

2.3.6. Kuendeleza Rasilimali Watu

 

2.3.6.1. Ujuzi na Uwezeshaji

 

(a)           Mradi Na. 6581: Programu ya Taifa ya Kukuza Ujuzi Nchini 

Hatua iliyofikiwa ni: Kuwezesha vijana 11,973 kupata mafunzo ya kukuza ujuzi kwa njia ya uanagenzi (Apprenticeship) katika fani mbalimbali za ufundi stadi, kuwezesha Wahitimu 1,704 wa ngazi mbalimbali za elimu na mafunzo kupata mafunzo ya uzoefu wa kazi (Internship) katika taasisi mbalimbali  za umma na binafsi, kufadhili vijana 200 kupata mafunzo ya uzoefu katika fani ya ufugaji samaki na mazao ya bahari, kufadhili vijana 234 kupata mafunzo ya kunenepesha mifugo kupitia vituo vy LITA na TALIRI vilivyopo Tanga, Mwanza na Kagera, kuwezesha vijana 74 kushiriki mafunzo ya uzoefu wa kazi (Internship) katika kilimo cha vizimba (Block Farms) kupitia mradi wa Building Better Tomorrow (BBT) katika kituo cha Bihawana, Dodoma, na kuratibu na kuwezesha ushiriki wa wajasiriamali wadogo na wa kati wa sekta isiyo rasmi 250 katika maonesho ya 22 ya nguvu kazi/juakali ya Jumuiya ya Afrika Mashariki yaliyofanyika Jijini Kampala, Uganda. Jumla ya shilingi bilioni 3 zimetumika zimetumika katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023.

 

(b)          Mradi Na. 4952: Mfuko wa Maendeleo ya Vijana  

Hatua iliyofikiwa ni: Kutoa Mikopo yenye  thamani ya Shilingi Billioni 2.82 kwenye miradi ya Vijana 141 yenye vijana 987. Vijana wajasiriamali 1,497 walio katika sekta isiyo rasmi wamefaidika na mafunzo ya kujengewa uwezo katika Ujasiriamali, usimamizi wa biashara , urasimishaji pamoja na kuunganishwa na huduma za kibiashara katika taasisi mbalimbali. Aidha, makampuni 118 ya vijana yameunganishwa na huduma zabuni za ununuzi wa umma. Jumla ya shilingi bilioni 1.88 zimetumika zimetumika katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023.

 

(c)           Mradi Na. 6205: Programu ya Taifa ya Kukuza Kazi za Staha

Hatua iliyofikiwa ni: Kuendelea na mapitio ya Programu ya Kukuza Kazi za Staha; kufanya mapitio ya utekelezaji wa Sera ya Taifa ya Maendeleo ya Vijana ya Mwaka 2007 na kuandaa Rasimu ya mpya ya Taifa ya Maendeleo ya Vijana; kufanya mapitio ya Mwongozo Sanifu na Mfumo wa Uratibu, Ufuatiliaji, Tathmini na Taarifa za Utekelezaji wa Programu ya Stadi za Maisha kwa Vijana walio nje ya Shule; kuandaa Mwongozo wa Stadi za Maisha katika lugha ya Kiswahili; kuandaa Rasimu ya Pili ya Mfumo wa Uratibu, Ufuatiliaji, Tathmini na Taarifa za Utekelezaji wa Programu ya Stadi za Maisha; kufanya uchambuzi wa Sheria Na. 2 ya Baraza la Vijana Tanzania ya Mwaka 2015 pamoja na kanuni zake; na kutengeneza Mfumo wa Kielectroniki wa Kanzi Data kwa ajili ya Watu Wenye Ulemavu Jumla ya shilingi bilioni 1.10 zimetumika katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023.

 

(d)          Mradi Na. 4954: Ujenzi na Ukarabati wa Vituo vya Ufundi kwa Watu Wenye Ulemavu

Hatua iliyofikiwa ni: Kukamilika kwa ukarabati wa vyumba vya madarasa (17), mabweni ya wanafunzi nane (10), nyumba za watumishi (20), karakana sita (7), Majengo ya Utawala (4), majiko (2), na matundu ya vyoo (9) katika Vyuo vya Ufundi Stadi na Marekebisho vya Mtapika (Masasi – Mtwara), Luanzali (Tabora), Sabasaba (Singida) na Yombo (Dar es Salaam). Jumla ya shilingi bilioni 3.46 zimetumika katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023.

 

2.3.7. Uwekezaji katika Taasisi na Mashirika ya Umma

Hatua iliyofikiwa ni: Kuchangiwa kwa jumla ya shilingi bilioni 705.76 katika Mfuko Mkuu wa Serikali sawa na asilimia 75.53 ya Bajeti nzima ya makusanyo ya mapato yasiyo ya kodi. Ongezeko hilo limetokana na kuongezeka kwa makusanyo ya mtaji wa ziada, ulipwaji wa madeni kwa wakati, michango ya asilimia  15 kwenye Mfuko Mkuu wa Serikali na mapato yatokanayo na simu zinazopigwa nje ya nchi. Vile vile, uwekezaji katika Taasisi na Mashirika ya Umma umeongezeka kutoka shilingi trilioni 67.06 mwaka wa fedha 2020/21 hadi kufikia shilingi trilioni 69.91 mwaka 2021/22 sawa na ongezeko la asilimia 4. 

 

2.3.8. Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi

Ubia Baina ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi

Hatua iliyofikiwa ni: 

(i)          Kutangazwa kwa zabuni  ya kupata wazabuni wenye sifa (Request For Qualification) kwa ajili ya  mradi ya ujenzi wa barabara ya tozo kutoka Kibaha - Chalinze - Morogoro (km 205) kipande cha Kibaha – Chalinze (km 78.9) na kuendelea na maandalizi ya taarifa ya Upembuzi Yakinifu ya kipande cha Chalinze – Morogoro (km 126.1);

(ii)         Kukamilisha taarifa ya upembuzi yakinifu ya mradi wa ukaguzi wa lazima wa vyombo vya moto;  

(iii)       Kuendelea na maandalizi ya taarifa ya upembuzi yakinifu wa awali wa mradi wa ujenzi wa kituo cha mazoezi tiba eneo la Mbweni Dar es Salaam;

(iv)       Kuendelea na upembuzi yakinifu wa awali kwa ajili ya ununuzi wa mtoa huduma wa mradi wa mabasi yaendayo haraka Jijini Dar es Salaam Awamu ya Tatu na ya Nne;

(v)        Kuandaliwa kwa mkataba wa ubia na taratibu za kusaini mkataba kati ya mzabuni anayependekezwa ambaye ni mtoa huduma wa kudumu na Mamlaka ya Serikali (Wakala - DART) kwenye mradi wa mabasi yaendayo haraka Jijini Dar es Salaam awamu ya kwanza; 

(vi)       Kuendelea na ununuzi wa mbia wa miradi ya Ujenzi wa hoteli ya Nyota Nne na Jengo la Biashara katika Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere; na

(vii)      Kukamilisha taarifa ya Upembuzi Yakinifu wa mradi wa kuimarisha huduma za Saratani nchini kwa kujenga Kituo cha Ubingwa Bobezi wa Tiba ya Saratani eneo la Mloganzila (Ultra- Modern Oncology Centre - UMOC) na Kituo cha Saratani Mbeya (Mbeya Cancer Centre - MCC) eneo la Iwambi- Mbeya.

 

Aidha, katika kipindi cha Julai 2022 hadi Aprili 2023, maandalizi ya miradi ya PPP yaligharimu jumla ya shilingi bilioni  9.66 kama ilivyoainishwa kwenye Jedwali hapo chini.

 

Jedwali 6: Miradi ya PPP na Fedha na Zilizotumika 

Jina la Mradi

Mamlaka yenye Mradi 

Kiasi cha Fedha Kilichotumika

Mradi    wa     Barabara     ya

Chalize - Kibaha - Morogoro (km 205)

TANROADS

8,940,696,000

Mradi wa Ujenzi wa Kituo cha Mazoezi Tiba Mbweni Dar es Salaam 

Taasisi ya Mifupa ya MOI

171,236,000

Mradi wa Ukaguzi wa Lazima kwa vyombo vya moto

Jeshi la Polisi

134,500,000

Mradi wa Ujenzi wa Hosteli za Wanafunzi 

Chuo cha Elimu ya Biashara

180,000,000

Mradi wa kuimarisha huduma za Saratani nchini kwa kujenga Kituo cha Ubingwa Bobezi wa Tiba ya Saratani eneo la Mloganzila (Ultra- Modern Oncology Centre - UMOC) na Kituo cha Saratani Mbeya (Mbeya

Cancer Centre - MCC) 

Taasisi ya Saratani ya Ocean Road 

230,000,000

JUMLA

 

9,656,432,000

 

2.4.1. Ufuatiliaji wa Miradi katika kipindi cha Mwaka 2022/23

Hadi kufikia Aprili 2023, jumla ya miradi 211 kati ya miradi 300 iliyopangwa kwa kipindi husika ilifuatiliwa na kufanyiwa tathmini. Miradi ya kielelezo iliyofuatiliwa ni: ujenzi wa reli ya kati kwa kiwango cha kimataifa (SGR); kufua umeme wa maji wa Julius Nyerere (MW 2,115); uboreshaji wa shirika la ndege Tanzania; ujenzi wa madaraja ya juu katika jiji la Dar es Salaam (Uhasibu, Chang’ombe na daraja la bandari); ujenzi wa daraja la Kigongo – Busisi; ujenzi wa Kiwanda na Uendelezaji wa Shamba la Miwa Mkulazi – Mbigiri Estate; ujenzi wa Bomba la Mafuta Ghafi Afrika Mashariki (EACOP); ujenzi wa Bandari ya Uvuvi Kilwa; na eneo maalum la uwekezaji Bagamoyo. Miradi ya kimkakati iliyofuatiliwa inatekelezwa katika sekta za kukuza uchumi, huduma za jamii na utawala bora, uwajibikaji na utoaji haki. Kwa upande wa sekta za kukuza uchumi, miradi iliyofuatiliwa ni ya viwanda (17), masoko (1), biashara (1), barabara (3), ujenzi (7), uvuvi (1), uchukuzi (4), kilimo (16), madini (1) na nishati (4). Sekta za Huduma ya Jamii zilizofuatiliwa ni afya (19), elimu (16), na maji (91). Kwa upande wa utawala bora, uwajibikaji na utoaji haki inayojumuisha sheria, mambo ya ndani, habari na mawasiliano na utawala jumla ya miradi nane

(14) ilifuatiliwa. 

Aidha, Serikali inaendelea na maandalizi ya Sera ya Taifa ya Ufuatiliaji na Tathmini ambapo hatua iliyofikiwa ni kukamilika ukusanyaji na uchambuzi wa maoni kutoka kwa wadau na kuanza kwa uandishi wa Taarifa ya Kizio (Baseline Report). Kukamilisha kwa uandishi wa Taarifa Kizio kutajenga msingi wa uandishi wa Sera ambayo inatarajiwa kutatua changamoto za uratibu wa shughuli za ufuatiliaji na tathmini chini.

 

2.4.2. Changamoto za Utekelezaji wa Mpango wa Maendeleo wa Mwaka 2022/23

Katika zoezi la ufuatiliaji na tathmini changamoto mbalimbali zilijitokeza katika utekelezaji wa Mpango. Changamoto hizo zimegawanyika katika makundi mawili ambayo ni changamoto za jumla na changamoto mahsusi za miradi. 

 

Changamoto za Jumla

(i)            Ongezeko la bei za mafuta kutokana na ongezeko la mahitaji lililosababishwa na chumi za nchi nyingi kuanza kurejea katika hali ya kawaida baada ya kuanza kulegeza vikwazo vilivyowekwa kutokana na UVIKO-19 na vita baina ya nchi za Urusi na Ukraine. Ongezeko la bei za mafuta limesababisha kuongezeka kwa gharama na kuchelewa kwa utekelezaji wa miradi; 

(ii)           Ongezeko la bei za bidhaa muhimu kwa ajili ya uzalishaji pamoja na usalama wa chakula nchini ikiwemo mbolea, ngano na kemikali muhimu zinazotumika viwandani kutokana na vita baina ya nchi za Urusi na Ukraine;

(iii)         Kuchelewa kukamilika kwa miradi kutokana na kutokufika kwa wakati kwa vifaa na bidhaa muhimu zinazoagizwa kutoka nje ya nchi kulikosababishwa na kuathirika kwa mnyororo wa ugavi duniani (global supply chain disruptions) kutokana na UVIKO-19 na vita baina ya nchi za Urusi na Ukraine;

(iv)         Kukosekana kwa wabia wa kutekeleza miradi iliyoandaliwa na kutangazwa kwa ajili ya kutekelezwa kwa utaratibu wa Ubia baina ya Sekta ya Umma na Binafsi; 

(v)          Wigo mdogo wa kodi unaotokana na baadhi ya biashara kutokuwa rasmi na hivyo kupunguza mapato ya ndani kwa ajili ya utekelezaji wa Mpango; na

(vi)         Baadhi ya wafanyabiashara kukwepa kodi hususan kupitia njia za magendo, kutokutoa stakabadhi za kielektroniki (EFD receipt) wakati wa mauzo.

 

Changamoto Mahsusi

(i)            Upungufu wa rasilimali watu hususan wahandisi wa kusimamia utekelezaji wa miradi pamoja na wataalamu wa uendeshaji wa mitambo na vifaa vinavyotumia teknolojia ya kisasa; 

(ii)           Watekelezaji wa miradi kuchelewa kukamilisha taratibu za utoaji wa Cheti cha Msamaha wa Kodi  hali inayosababisha kuongezeka kwa gharama za mradi (madai ya riba) na kuchelewa kwa kutekeleza mradi;

(iii)         Usanifu duni wa mradi hali inayosababisha kuongezeka kwa mawanda, gharama na muda wa utekelezaji wa miradi; 

(iv)         Usimamizi usioridhisha katika utekelezaji wa miradi kwa mujibu wa mikataba na mipango kazi kwa baadhi ya watekelezaji wa miradi;

(v)          Kuchelewa kwa malipo ya makandarasi kunakosababishwa na kutowasilishwa kwa nyaraka muhimu za kuwezesha kufanyika kwa malipo kwa wakati hali inayosababisha malimbikizo ya riba na ucheleweshaji wa utekelezaji wa mradi; 

(vi)         Usimamizi na uratibu kwa baadhi ya taasisi kufanyika katika ngazi ya makao makuu bila kushirikisha wasimamizi waliopo katika eneo la mradi hali inayosababisha miradi kuchelewa, kuongeza gharama na kupunguza ufanisi katika malengo ya mradi;

(vii)        Ushirikishwaji mdogo wa wadau muhimu wa mradi katika kipindi cha maandalizi hali inayosababisha kubadilika kwa mawanda ya kazi wakati wa utekelezaji; na

(viii)      Kuchelewa kwa malipo ya fidia kwa wananchi wanaopisha miradi.

 

2.4.3. Hatua Zilizochukuliwa Kukabiliana na Changamoto

(i)            Kuendelea na hatua za kukabiliana na ongezeko la bei za mafuta katika soko la dunia kwa kuchukua hatua mbalimbali ikiwemo kutoa ruzuku, kupunguza viwango na idadi ya tozo na kuogeza jitihada za kuongeza uwezo wa Akiba ya Kimkakati ya Hifadhi ya Mafuta (National Strategic Petroleum Reserves)

(ii)           Kuendelea na hatua za kukabiliana na ongezeko la bei za bidhaa muhimu kwa ajili ya uzalishaji pamoja na usalama wa chakula nchini ikiwemo kupitia sera za kibajeti  mfano; kupunguza tozo na kodi, utoaji ruzuku (mbolea na mafuta) kwa bidhaa muhimu na kuchukua hatua za kuongeza uzalishaji wa bidhaa husika nchini (mfano ngano na mbolea);

(iii)         Kuendelea na utekelezaji wa mikakati mbalimbali ya kuongeza mapato ya ndani na kubuni vyanzo vipya vya mapato ili kuongeza uwezo wa Serikali kugharamia Mpango;

(iv)         Kuendelea kupanga maeneo ya kipaumbele kwa kuzingatia rasilimali fedha zilizopo; 

(v)          Kuendelea kuhakikisha kuwa malipo ya hati za madai yanafanyika ndani ya muda uliokubalika kimkataba;

(vi)         Kuchukua hatua za kisera na kiutawala ili kuendelea kupambana na athari za mgogoro katika mnyororo wa ugavi duniani ikiwemo kutumia zaidi malighafi, vifaa na wataalamu wa ndani kwa maeneo yote ambayo hakuna ulazima wa huduma hizo kutoka nje ya nchi na usimamizi madhubuti wa uagizaji na uhifadhi wa malighafi na vifaa vinavyoagizwa kutoka nje (appropriate investory management); 

(vii)        Kuendelea kujenga uwezo wa Mafungu ili kuyawezesha kuandaa miradi inayokidhi vigezo vya kutekelezwa kwa utaratibu wa PPP ili ijumuishwe katika Mpango;

(viii)      Kuendelea kuajiri wahandisi na wataalamu watakaosimamia utekelezaji na usimamizi wa miradi ya maendeleo;

(ix)         Kuendelea kutekeleza miradi ya kimkakati ya kuongeza mapato ya ndani, kubuni vyanzo vipya vya mapato na kutafuta masoko ya bidhaa nje ili kuongeza uwezo wa Serikali kugharamia Mpango na Bajeti. Aidha, Serikali inaendelea na kufuatilia mikopo yenye masharti nafuu kutoka kwa Taasisi mbalimbali ili kuweza kutekeleza miradi ya kipaumbele; 

(x)          Kuendelea kuimarisha mifumo ya usimamizi na ukusanyaji wa mapato ili kudhibiti ukwepaji kodi pamoja na kuendelea kuhamasisha umma juu ya umuhimu wa kulipa kodi na matumizi ya stakabadhi za kielektroniki; na

(xi)         Kuhamasisha viwanda vya ndani kuongeza uzalishaji wa vifaa vya ujenzi ili kukidhi mahitaji ya soko yaliyoongezeka.

 

SURA YA TATU

 

MIRADI YA KIPAUMBELE KWA MWAKA 2023/24

 

3.1. Utangulizi

Sura hii inaelezea miradi ya kipaumbele itakayozingatiwa katika Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2023/24. Uandaaji wa Mpango umezingatia hatua za kimkakati zilizoainishwa katika Mpango Kazi wa utekelezaji wa Mpango wa Tatu wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano, 2021/22 – 2025/26. Hivyo, utekelezaji madhubuti wa hatua hizo utafanikisha kufikiwa kwa malengo ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025.

 

3.2. Misingi ya Mpango na Shabaha za Ukuaji wa Uchumi

 

3.2.1. Malengo na Shabaha za Ukuaji wa Uchumi

Malengo na shabaha za uchumi jumla ni kama ifuatavyo: 

(i)            Ukuaji wa Pato Halisi la Taifa kufikia asilimia 5.2 mwaka 2023 kutoka ukuaji wa asilimia 4.7 mwaka 2022; 

(ii)           Mfumuko wa bei kubaki kwenye wigo wa tarakimu moja ya wastani wa 

asilimia 3.0 hadi asilimia 7.0 katika kipindi cha muda wa kati; 

(iii)         Mapato ya ndani kufikia asilimia 14.9 ya Pato la Taifa mwaka 2023/24 kutoka matarajio ya asilimia 14.4 mwaka 2022/23

(iv)         Mapato ya kodi kufikia asilimia 12.0 ya Pato la Taifa mwaka 2023/24 kutoka matarajio ya asilimia 11.5 mwaka 2022/23; 

(v)          Nakisi ya bajeti (ikijumuisha misaada) kuwa chini ya asilimia 3.0 ya Pato la Taifa mwaka 2023/24; na 

(vi)         Kuwa na akiba ya fedha za kigeni kwa kiwango cha kukidhi mahitaji ya uagizaji wa bidhaa na huduma kutoka nje kwa kipindi kisichopungua miezi minne (4).

 

3.2.2. Misingi (Assumptions) ya Mpango kwa Mwaka 2023/24

Misingi itakayozingatiwa katika Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2023/24 ni kama ifuatavyo: 

 

(i) Kuongezeka kwa ushiriki wa sekta binafsi kwenye shughuli za uwekezaji na biashara;

(i)   Kuendelea kuhimili athari za majanga ya asili na yasiyo ya asili; 

(ii)  Kuendelea kuhimili athari zitokanazo na kushuka kwa uchumi wa dunia na kuongezeka kwa bei za bidhaa na huduma katika soko la dunia;

(iii)Kuendelea kuimarika kwa utoshelevu wa chakula nchini;

(iv)Uwepo wa amani, usalama, umoja na utulivu wa ndani na nchi jirani; na (v) Kuendelea kuimarika kwa viashiria vya ustawi wa jamii.

3.3. Miradi ya Kipaumbele kwa Mwaka 2023/24

 

3.3.1. Miradi ya Kielelezo

(i)           Mradi Na. 4281: Ujenzi wa Reli ya Kati kwa Kiwango cha Kimataifa (Standard Gauge Railway - SGR) 

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kukamilisha ujenzi wa reli ya Standard Gauge kwa kipande cha Dar es Salaam - Morogoro (km 300) na Morogoro - Makutupora (km 422); kuendelea na ujenzi wa njia ya reli kwa kipande cha Mwanza - Isaka (km 341); Makutupora – Tabora (km 368); Tabora - Isaka (Km 165); na kuanza ujenzi wa kipande cha Tabora - Kigoma (Km 506) na Uvinza (Tanzania) – Musongati – Gitega (Burundi) (Km 282); ununuzi wa injini, mabehewa na mitambo kwa ajili ya matengenezo ya njia; kugharamia uendeshaji wa reli ya Standard Gauge; kuendelea na ugharamiaji wa mafunzo ya wataalamu wa uendeshaji na usimamizi wa treni ya Standard Gauge; kuendelea na taratibu za upatikanaji wa fedha za ujenzi wa reli kwa sehemu za Kaliua – Mpanda - Karema (km 321) na sehemu ya Uvinza – Malagarasi (km 156); Isaka - Rusumo – Kigali (km 495) sehemu ya Isaka – Rusumo (km 371); na ulipaji wa fidia kwa wananchi wanaopisha ujenzi wa reli kipande cha Tabora - Kigoma. Jumla ya shilingi bilioni 1,113.0 fedha za ndani zimetengwa.

 

(ii)         Mradi Na. 3172: Kufua Umeme wa Maji wa Julius Nyerere – MW 2,115

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kuendelea na ujenzi wa bwawa (main dam); ujenzi wa njia kuu za kupitisha maji (tunnels); ujenzi wa kituo cha kuzalisha umeme (power house); ujenzi wa kituo cha kusafirisha umeme (switch yard); na ujenzi wa nyumba za makazi na ofisi. Jumla ya shilingi trilioni 1.5 fedha za ndani zimetengwa.

 

(iii)       Mradi Na. 4294: Kuboresha Shirika la Ndege Tanzania (ATCL)

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kukamilisha malipo ya ununuzi wa ndege nne (4) mpya ambapo ndege moja (1) ni aina ya  Boeing 787-8 Dreamliner, ndege mbili (2) aina ya Boeing 737-9, ndege moja (1) ya mizigo aina ya Boeing 767-300F; ukarabati na ununuzi wa vifaa vya karakana za matengenezo ya ndege (Hangar) za JNIA na KIA; kukamilisha ujenzi wa hanga jipya la kisasa katika kiwanja cha JNIA; kugharamia mahitaji ya awali ya uendeshaji wa ndege tano (5) ambazo ni Boeing 787 – 8, Boeing 737- 9 mbili (2), Boeing 767 - 300F na  Dash 8 Q400 (1); ununuzi wa vifaa vya kuhudumia ndege na abiria viwanjani; ukarabati wa majengo ya ofisi ya ATCL makao makuu na lililopo kiwanja cha ndege cha JNIA Terminal I; ukarabati wa nyumba 38 zilizopo KIA pamoja na ujenzi wa eneo la mafunzo ya awali kwa wanaanga; ununuzi wa ndege aina ya Boeing Business Jet 737 – 7; na ujenzi na ukarabati wa majengo kwa ajili ya kuhifadhi mizigo katika viwanja vya ndege vya JNIA, KIA na Songwe. Jumla ya shilingi bilioni 300.00 fedha za ndani zimetengwa. (iv) Mradi Na. 4015: Daraja la JPM - Kigongo – Busisi (Mwanza) Shughuli itakayotekelezwa ni kuendelea na ujenzi wa daraja pamoja na barabara unganishi (km 1.66). Jumla ya shilingi bilioni 15.16 fedha za ndani zimetengwa.

 

(v)         Ujenzi wa Bomba la Mafuta Ghafi kutoka Hoima (Uganda) hadi Tanga (Tanzania)  

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kukamilisha ulipaji wa fidia kwa wananchi ikiwemo kuhamisha makaburi zaidi ya 400; kukamilisha ujenzi wa nyumba za fidia kwa wananchi; kuanza ujenzi wa bomba; kuendelea na ujenzi wa kambi za wafanyakazi; kuendelea na ujenzi wa kiwanda cha kuunganisha mabomba; kuanza ujenzi wa bandari na matenki ya kupokea mafuta; kuanza ujenzi wa gati; na kuendelea kuchangia hisa za kampuni. Jumla ya shilingi bilioni 65.58 fedha za ndani zimetengwa.

 

(vi)       Mradi Na. 3155: Kuchakata na Kusindika Gesi Asilia kuwa Kimiminika (LNG) – Lindi

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kuanza kazi za awali za maandalizi ya mradi; kuanza tafiti mbalimbali za kitaalamu zikiwemo Usanifu wa Awali wa Kihandisi (Pre-FEED); kuendelea kuwajengea uwezo Wataalamu wa Serikali katika uendeshaji na usimamizi wa Mradi; kuendelea na stadi za kisayansi na stadi za mitambo itakayosimikwa katika eneo la mradi; na kufanya tathmini kuhusu hali za wananchi waliolipwa fidia ili kupisha mradi (post – compensation livelihood study). Jumla ya shilingi bilioni 6.0 fedha za ndani zimetengwa.

 

(vii)      Mradi Na. 3165: Kufua Umeme wa Maji wa Ruhudji (MW 358) – Njombe 

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kulipa fidia kwa wananchi watakaopisha mradi; na kuanza ujenzi wa miundombinu wezeshi. Jumla ya shilingi bilioni 6.27 fedha za ndani zimetengwa.

 

(viii)    Mradi Na. 3167: Kufua Umeme wa Maji wa Rumakali (MW 222) - Njombe

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kulipa fidia kwa wananchi watakaopisha mradi; na kuanza ujenzi wa miundombinu wezeshi ikijumuisha barabara za kufika eneo la mradi. Jumla ya shilingi bilioni 5.25 fedha za ndani zimetengwa.

 

(ix)       Mradi Na. 3115: Uendelezaji wa Sekta Ndogo ya Mafuta na Gesi

Asilia

Eyasi – Wembere: Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kukusanya taarifa za mitetemo za mfumo wa 2D urefu wa kilomita 260; na kutafuta Mbia wa Kimkakati atakayeshirikiana na TPDC katika uendelezaji wa kitalu. 

Mnazi Bay Kaskazini: Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kumpata Mkandarasi atakayechoronga kisima pamoja na watoa huduma nyingine wezeshi; na kutafuta Mbia wa Kimkakati atakayeshirikiana na TPDC katika uendelezaji wa kitalu. Jumla ya shilingi bilioni 24.86 fedha za ndani zimetengwa.

 

(x)         Mradi Na. 4702:  Ujenzi wa Bandari ya Uvuvi – Kilwa Masoko

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kuendelea na ujenzi wa bandari ya uvuvi Kilwa Masoko - Lindi; Ununuzi wa meli tatu (3) za uvuvi wa Bahari Kuu. ambapo jumla ya shilingi bilioni 50.0 fedha za ndani zimetengwa.

 

(xi)       Mradi wa Kiwanda cha Sukari Mkulazi 

Shughuli zitakazotekelezwa ni: kukamilisha matayarisho ya shamba na kupanda miwa katika eneo lililobaki lenye ukubwa wa hekta 589 ili kukamilisha hekta 3,600 zinazotakiwa kulimwa; kuweka mfumo wa umwagiliaji katika shamba lenye ukubwa wa hekta 845; kuendelea na ujenzi wa bwawa la umwagiliaji lenye ukubwa wa mita za ujazo milioni 3.5; kukamilisha ujenzi wa kiwanda kipya cha sukari; na ununuzi wa vifaa vya kupakia na kusafirisha miwa kwenda kiwandani. Jumla ya shilingi bilioni 60.80 fedha za ndani zimetengwa.

 

(xii)     Mradi Na. 1122: Magadi Soda Engaruka

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kulipa fidia wananchi wanaopisha mradi (PAP); kuendelea na hatua za kutafuta mwekezaji wa mradi; Kufanya uhakiki wa taarifa zilipo katika  tafiti zilizofanyika (Brine Resource appraisal and Techno-economic study review); na kulipa leseni za uchimbaji. Jumla ya shilingi bilioni 1.03 fedha za ndani zimetengwa.

 

(xiii)    Mradi Na. 3171: Makaa ya Mawe - Mchuchuma na Chuma – Liganga

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kuendelea na kulipia leseni za uchimbaji nje ya leseni za Kampuni ya ubia; kutafuta mwekezaji mpya, kufanya majadiliano na kuingia mkataba wa ubia; Kufanya ukarabati wa ofisi Ludewa; Kununua gari ya utekelezaji wa shughuli za  mradi; na kulipia leseni. Jumla ya shilingi bilioni 1.15 fedha za ndani zimetengwa.

 

(xiv)    Kanda Maalumu za Kiuchumi ikiwemo Eneo Maalumu la Uwekezaji Bagamoyo na Benjamini William Mkapa

 

Mradi Na. 4920: Eneo Maalumu la Uwekezaji Bagamoyo na Benjamini William Mkapa  

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kuendelea na ujenzi wa miundombinu ya barabara yenye urefu wa kilomita tatu (3) kwa kiwango cha lami katika eneo la mradi wa Bagamoyo SEZ; Kujenga  na kukarabati miundombinu ya ndani katika eneo la uwekezaji la Benjamin William Mkapa SEZ; Kufanya urasimishaji wa makazi yasiyopangwa (Holela) ya  Mlingotini, Zinga na Kiromo kwa kuyapanga ili kuweka miundombinu ya msingi na huduma za jamii. Jumla ya shilingi bilioni 1.90 fedha za ndani zimetengwa.

 

3.3.2. Kuchochea Uchumi Shindani na Shirikishi 

 

3.3.2.1. Kuimarisha Mazingira Wezeshi ya Uwekezaji

 

Uendelezaji wa Miundombinu na Huduma 

 

A.          Reli

 

(i)           Mradi Na. 4216: Ukarabati wa Njia Kuu za Reli

Shughuli zitakazotekelezwa katika awamu ya pili ni: Kukamilisha ukarabati wa maeneo yaliyobaki katika vipande vya Makutupora - Manyoni na Kitaraka – Malongwe - Igalula; na kuboresha vituo vya kuhudumia mizigo vya Ilala na Isaka. Jumla ya shilingi bilioni  11.73 fedha za nje zimetengwa. 

 

(ii)         Mradi Na. 4213: Mfuko wa Reli  

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kuendelea na uundaji wa vichwa viwili (2) vya treni vya njia kuu aina ya 88U na vichwa saba (7) vya sogeza aina ya 64XX; kuanza ukarabati wa njia ya reli ya Tabora - Kigoma (Km 411), Kaliua - Mpanda (Km 210), Tabora – Isaka - Mwanza (Km 385), Tanga - Arusha (Km 470) na Kilosa – Gulwe; ujenzi wa madaraja katika kipande cha Godegode - Gulwe; ufufuaji wa njia za reli zilizofungwa za Kilosa - Kidatu (Km 108) na Manyoni-Singida (Km 115); ukarabati wa mabehewa 120 ya mizigo na 12 ya abiria; ununuzi wa mabehewa ya mizigo 245, mabehewa ya abiria 22 na injini nane (8); kupima na kuweka alama katika maeneo ya reli nchini; na ufufuaji wa mgodi wa kuzalisha kokoto wa Pangani (Tanga) na Tumbi (Tabora) na Mgodi wa Tura. Jumla ya shilingi bilioni  294.80 fedha za ndani zimetengwa.

 

(iii)       Uboreshaji wa Reli ya TAZARA

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Ununuzi wa vifaa na mitambo (Tamping Machine moja, Excavator moja) kwa mgodi wa kokoto wa Kongolo (Mbeya), Mataruma ya Mbao vipande 20,000, Railway Scanner moja, Railway Weighbridge moja na Ujenzi wa njia mbili (2) za reli katika stesheni ya Tunduma. Jumla ya shilingi bilioni 13.19 fedha za ndani zimetengwa.

 

 

 

 

B.          Barabara na Madaraja

 

Barabara za Lami Zinazofungua Fursa za Kiuchumi 

 

(a)           Mradi Na. 4147: Barabara ya Kidatu – Ifakara – Lupilo - Malinyi – Londo – Lumecha/Songea (km 499)

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kuendelea na ujenzi kwa  sehemu ya Kidatu – Ifakara (km 66.9) na maandalizi ya ujenzi wa barabara ya Chalinze – Magindu – Lukenge – Seregete B – Kabwe Jct – Mkulazi (km 77.50). Vilevile, kuendelea na ukarabati kwa kiwango cha changarawe wa barabara ya Dakawa Jct – Mbigiri (km 7) na barabara zenye jumla ya kilometa 50 kuelekea mashamba ya wakulima wa miwa ya Mbigiri. Jumla ya shilingi bilioni 1.25 fedha za ndani zimetengwa. 

 

(b)          Mradi Na. 4113: Barabara ya Ifakara - Kihansi - Mlimba - Madeke –

Kibena (km 346.43)

Shughuli zitakazotekelezwa ni kuanza ujenzi wa barabara za Ifakara – Kihansi (km 124) sehemu ya Ifakara – Mbingu (km 50) na Mbingu – Chita (km 37.5). Vilevile, kuanza upembuzi yakinifu na usanifu wa kina wa sehemu za Njombe (Kibena) – Lupembe – Madeke (km 126) na Kihansi – Mlimba – Madeke (km 95.26). Jumla ya shilingi bilioni 7.56 fedha za ndani na shilingi bilioni 1.82 fedha za nje zimetengwa.

 

(c)           Mradi Na.4149: Barabara ya Makutano – Natta – Mugumu/Loliondo – Mto wa Mbu (km 235)

Shughuli itakayotekelezwa ni kuendelea na ujenzi wa barabara za Sanzate – Natta (km 40), Waso – Loliondo (km 10), Ngaresero – Engaruka (km 39),  Mto wa Mbu – Selila (km 20) na kuendelea na maandalizi ya kuanza ujenzi sehemu ya Natta – Mugumu (km 35) kwa kiwango cha lami. Jumla ya shilingi bilioni 4.02 fedha za ndani zimetengwa. 

 

(d)          Mradi Na. 4190: Barabara ya Itoni – Ludewa - Manda (km 211)

Shughuli itakayotekelezwa ni kuendelea na ujenzi wa barabara ya Itoni – Lusitu (km 50) na kuanza maandalizi ya ujenzi wa barabara ya Nkomang'ombe - Mchuchuma (km 7) kwa kiwango cha lami. Jumla ya shilingi bilioni 4.01 fedha za ndani zimetengwa. 

 

(e)           Mradi Na. 4193: Handeni – Kibaya – Singida (km 424.24)

Shughuli itakayotekelezwa ni kuendelea na ujenzi wa sehemu ya Handeni – Kiberashi (km 50) vipande vya Handeni – Mafuleta (km 20) na Mafuleta – Kileguru (km 30) na kuanza maandalizi ya ujenzi wa sehemu ya Kileguru – Kibaya – Singida (km 410) kwa kiwango cha lami. Jumla ya shilingi bilioni 5.25 fedha za ndani zimetengwa. 

(f)            Mradi Na. 4195: Barabara ya Dodoma – Iringa (km 260)

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kuendelea na ujenzi wa barabara ya mchepuo ya Iringa (Iringa Bypass - km 7.3) kwa kiwango cha lami; kuendelea kuimarisha matabaka ya barabara ya Iringa – Dodoma (km 266); na kuanza kujenga barabara ya Iringa – Pawaga (km 71.93). Jumla ya shilingi bilioni 2.51 fedha za ndani zimetengwa. 

 

(g)          Mradi Na. 4196: Barabara ya Dodoma – Babati (km 263.4)

Shughuli zitakazotekelezwa ni: kuendelea na maandalizi ya ujenzi wa barabara ya Dongobeshi – Dareda (km 60) sehemu ya Dareda mjini – Dareda Mission (km 8), mchepuo wa Babati (Babati Bypass - km 15.5) pamoja na miteremko ya Magara (km 3). Jumla ya s  hilingi bilioni 1.33 fedha za ndani zimetengwa.

 

(h)          Mradi Na. 4188: Barabara ya Mbeya –  Makongolosi – Manyoni (km 479.9)

Shughuli zitakazotekelezwa ni kuendelea na ujenzi wa barabara za Itigi Mjini (km 10), Noranga – Itigi (km 25); kuanza ujenzi wa sehemu ya Itigi – Mkiwa (km 31.6); na kuendelea na maandalizi ya ujenzi wa barabara za Mbalizi – Makongolosi (km 50) na Makongolosi – Rungwa (km 50). Jumla ya shilingi bilioni 6.36 fedha za ndani zimetengwa.                                                                                                                         

 

(i)            Mradi Na. 4112: Kigoma – Kidahwe – Uvinza – Kaliua – Tabora (km 429)

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kuendelea na ujenzi wa barabara ya Kazilambwa – Chagu (km 36); na kuendelea na ujenzi wa barabara ya Uvinza – Malagarasi (km 51.1) na Urambo Roundabout kwa kiwango cha lami. Jumla ya shilingi milioni 840 fedha za ndani na shilingi bilioni 19.27 fedha za nje zimetengwa. 

 

(j)            Mradi Na. 4002: Barabara ya Mtwara – Newala - Masasi (km 210)

Shughuli itakayotekelezwa ni kuanza ujenzi wa barabara ya Mnivata – Tandahimba - Masasi (km 160) sehemu za Mnivata – Mitesa (km 100) na Mitesa – Masasi (km 60); na kuanza maandalizi ya ujenzi ya barabara ya Mangamba – Madimba – Msimbati (km 35) kwa kiwango cha lami. Jumla ya shilingi bilioni 2.41 fedha za ndani na shilingi bilioni 11 fedha za nje zimetengwa.

 

(k)           Mradi Na. 4003: Barabara ya Likuyufusi – Mkenda (km 122.50)

Shughuli itakayotekelezwa ni kuendelea na ujenzi wa barabara ya Likuyufusi – Mkenda sehemu ya Likuyufusi – Mhukuru (km 60) kwa kiwango cha lami. Jumla ya shilingi bilioni 3.0 fedha za ndani zimetengwa.  

 

 

(l)            Mradi Na. 4107: Barabara za Kuelekea kwenye Mradi wa Kufua Umeme wa Maji katika Mto Rufiji (km 406)

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kuendelea na ujenzi wa barabara ya Bigwa – Matombo – Mvuha (km 78) kwa kiwango cha lami; ukarabati kwa kiwango cha changarawe barabara za  Maneromango – Vikumburu – Mloka (km 100) na Kibiti – Mloka – Mtemele – Striggler’s Gorge; na kuendelea na upembuzi yakinifu na usanifu wa kina wa barabara za Chalinze – Utete (km 354.9) na Ngerengere – Mvuha – Kisaki – Mtemele Jct (km 166.4). Jumla ya shilingi bilioni 5.8 fedha za ndani zimetengwa.

 

(m)    Mradi Na. 4174: Upanuzi wa Barabara ya Kimara – Kibaha (Km 25.7) Ikijumuisha Upanuzi wa Madaraja ya Kibamba, Kiluvya na Mpiji

Shughuli itakayotekelezwa ni kukamilisha upanuzi wa barabara ya Kimara – Kibaha Mizani (km 19.2) na madaraja ya Kibamba, Kiluvya na Mpiji. Jumla ya shilingi bilioni 1.5 fedha za ndani zimetengwa.

(n)          Mradi Na. 4024: Barabara ya Nanganga - Ruangwa - Nachingwea (km 108.9)

Shughuli zitakazotekelezwa ni kuendelea na ujenzi wa barabara ya Nanganga – Ruangwa – Nachingwea (km 100), sehemu ya Nanganga – Ruangwa (km 53.20) na Nachingwea – Ruangwa (km 55.7) na kuanza maandalizi ya ujenzi wa barabara ya Nangurukuru – Liwale (km 228), sehemu ya Choya – Liwale (km 72). Jumla ya shilingi bilioni 7.05 fedha za ndani zimetengwa.

 

(o)          Mradi Na. 4041: Barabara ya Kitahi – Lituhi na Daraja la Mnywamaji (km 90)

Shughuli itakayotekelezwa ni kuendelea na ujenzi wa barabara ya Kitahi – Lituhi na Daraja la Mnywamaji sehemu ya Amanimakolo – Ruanda (km 35) na kuanza ujenzi wa sehemu ya Ruanda – Ndumbi Port (km 50). Jumla ya shilingi bilioni 5.50 fedha za ndani zimetengwa.

 

(p)          Mradi Na. 4101: Barabara ya Tanga - Pangani – Makurunge (km 174.5)

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kuendelea na ujenzi wa barabara ya Tanga – Pangani (km 50), Pangani/Tungamaa – Mkange (km 124.5) kwa kiwango cha lami pamoja na Daraja la Pangani (m 525). Kazi nyingine ni kuanza ujenzi wa barabara ya Mkata – Kwa Msisi (km 36). Jumla ya shilingi bilioni 3.50 fedha za ndani na shilingi bilioni 27.56 fedha za nje zimetengwa.            

 

(q)          Mradi Na. 4199: Barabara ya Igawa – Songwe – Tunduma na Mchepuo wa Mbeya (Mbeya Bypass) (km 266.9)

Shughuli zitakazotekelezwa ni: kuendelea na upanuzi wa sehemu ya Uyole – Ifisi – Songwe Airport (km 36). Jumla ya shilingi bilioni 5.15 fedha za ndani zimetengwa.  (r)    Mradi Na. 4022: Barabara ya Njombe - Makete - Isyonje (km 157.4)

Shughuli itakayotekelezwa ni kuanza ujenzi wa barabara ya Isyonje – Makete (km 50) sehemu ya Kitulo – Iniho (km 36.3) na barabara kuelekea hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Njombe (km 3)  kwa kiwango cha lami. Jumla ya shilingi bilioni 4.02 fedha za ndani zimetengwa. 

(s)           Mradi Na. 4194: Barabara ya Makambako – Songea (Songea Bypass) (km 295)

Shughuli zitakazotekelezwa ni kukarabati barabara ya Makambako – Songea sehemu ya Lutikila – Songea (km 95.18) pamoja na mchepuo wa Songea (km 11) kwa kiwango cha lami. Vilevile, kuendelea na maandalizi ya ujenzi wa barabara ya Ramadhani – Ilembula Hospital – Iyayi (km 75). Jumla ya shilingi bilioni 1.32 fedha za ndani na shilingi bilioni 21.42 fedha za nje zimetengwa. 

 

(t)            Mradi Na. 4123: Barabara ya Dumila – Kilosa (km 141)

Shughuli zitakazotekelezwa ni: maandalizi ya ujenzi wa barabara ya Kilosa – Ulaya – Mikumi (km 72) kwa kiwango cha lami. Jumla ya shilingi bilioni 1.32 fedha za ndani zimetengwa. 

 

(u)          Mradi Na. 4023: Barabara ya Omugakorongo - Kigarama - Murongo (km 105)

Shughuli itakayotekelezwa ni kuanza ujenzi wa barabara ya Omugakorongo - Kigarama - Murongo (km 105), sehemu ya Businde – Murongo (km 53.4) na kuanza maandalizi ya ujenzi wa sehemu ya Omugakorongo – Businde (km 51.6) kwa kiwango cha lami. Jumla ya shilingi bilioni 4.0 fedha za ndani zimetengwa.

 

(v)           Mradi Na. 4014: Barabara ya Kibaoni – Majimoto – Muze – Kilyamatundu     (km 189)

Shughuli itakayotekelezwa ni kuanza ujenzi wa barabara sehemu ya Kizungu – Muze (km 12) na maandalizi ya ujenzi wa barabara ya Kibaoni – Majimoto – Inyonga (km 152) na kuendelea na ujenzi wa sehemu ya Ntendo – Kizungu (km 25) kwa kiwango cha lami. Jumla ya shilingi bilioni 4.50 fedha za ndani zimetengwa. 

 

(w)         Mradi Na. 4128: Barabara ya Kyaka – Bugene – Kasulo (km 183.1)

Shughuli itakayotekelezwa ni kuendelea na ujenzi wa barabara za Kamunazi – Kasulo – Bugene na Kyaka – Mutukula (km 133), sehemu ya Bugene – Burigi Chato National Park (km 60). Jumla ya shilingi bilioni 3.01 fedha za ndani zimetengwa. 

 

Barabara Zinazounganisha Tanzania na Nchi Jirani

(a)           Mradi Na. 4124: Barabara ya Sumbawanga - Matai - Kasanga Port (km 107)

Shughuli itakayotekelezwa ni kuendelea na ujenzi wa barabara ya Matai – Kasesya (km 50), sehemu ya Matai – Tatanda (km 25) na kuanza ujenzi wa sehemu ya Tatanda – Kasyesa (km 25); na maandalizi ya ujenzi wa barabara ya Laela – Mwimbi – Kizombwe (km 93) kwa kiwango cha lami. Jumla ya shilingi bilioni 5.01 fedha za ndani zimetengwa. 

 

(b)          Mradi Na. 4115: Barabara ya Marangu - Tarakea - Rongai – Kamwanga/Bomang’ombe - Sanya Juu (km 105.16)

Shughuli zitakazotekelezwa ni kuendelea na ujenzi wa barabara ya Kwa Sadala – Masama – Machame Junction (km 16),  Kiboroloni – Kiharara – Tsuduni – Kidia (km 10.8); Sanya Juu – Kamwanga sehemu ya Elerai – Kamwanga (km 44). Aidha, kuanza ukarabati wa barabara ya Bomang'ombe – Sanya Juu (25 km) na ujenzi wa barabara ya Tarakea – Holili (km 53.0). Jumla ya shilingi bilioni 7.83 fedha za ndani zimetengwa. 

 

(c)           Mradi Na. 4129: Barabara ya Isaka - Lusahunga (km 242.2)

Shughuli zitakazotekelezwa ni: kuendelea na ujenzi wa Kituo cha Pamoja cha Ukaguzi (OSIS) cha Nyakanazi; kuanza ukarabati wa barabara sehemu ya Lusahunga – Rusumo (km 92); na maandalizi ya ujenzi wa barabara ya Nyakasanza – Kobero (km 58). Jumla ya shilingi milioni 560 fedha za ndani na shilingi bilioni 16.72 fedha za nje zimetengwa. 

 

(d)          Mradi Na. 4111: Nyakahura – Kumubuga –Rulenge – Kabanga Nickel – Murugarama (km 141)

Shughuli itakayotekelezwa ni kuendelea na maandalizi ya ujenzi wa barabara za Nyakahura – Kumubuga – Murusagamba (km 34), Kumubuga – Rulenge – Murugarama (km 75) na Rulenge – Kabanga Nickel (km 32) kwa kiwango cha lami. Jumla ya shilingi bilioni 3.0 fedha za ndani zimetengwa. 

 

(e)           Mradi Na. 4154: Barabara ya Sumbawanga - Mpanda Nyakanazi (km 803.6)

Shughuli zitakazotekelezwa ni: kuendelea na ujenzi wa barabara za Mpanda – Mishamo – Uvinza sehemu ya Vikonge - Luhafwe (km 25); Kibaoni – Mlele Jct (km 50); na kuanza ujenzi wa sehemu ya Luhafwe – Mishamo Jct (km 37.70), Mlele Jct – Sitalike (km 23.5) na Kagwira – Ikola – Karema Port (km 112). Aidha,kazi nyingine ni kuanza maandalizi ya ujenzi wa barabara za Kizi – Lyambalyamfipa – Sitalike (km 86.31) na Lyazumbi – Kabwe (km 65) kwa kiwango cha lami. Jumla ya shilingi bilioni

15.54 fedha za ndani zimetengwa. 

 

(f)            Mradi Na. 4155: Barabara ya Nyanguge – Musoma/Kisesa Bypass (Km 202.25)

Shughuli itakayotekelezwa ni kuanza ukarabati wa sehemu ya Nyanguge – Simiyu/Mara Border (km 100.4). Jumla ya shilingi milioni 530 fedha za ndani zimetengwa. 

(g)          Mradi Na. 4162: Barabara ya Mwigumbi Maswa - Bariadi Lamadi (km 171)

Shughuli itakayotekelezwa ni kuendelea na ujenzi wa mchepuo wa barabara ya Maswa (km 11). Jumla ya shilingi bilioni 1.52 fedha za ndani zimetengwa.

                     

(h)          Mradi Na. 4164: Barabara ya Kidahwe - Kasulu – Kibondo - Nyakanazi (km 341.25

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kuendelea na ujenzi wa barabara za Kanyani Junction – Mvugwe (km 70.5), Mvugwe – Nduta Junction (59.35), Kibondo Junction – Kabingo (62.5), na Nduta Junction – Kibondo (25.9); na kuanza ujenzi wa barabara ya Kibondo – Mabamba (km 48) kwa kiwango cha lami. Jumla ya shilingi bilioni 6.52 fedha za ndani na shilingi bilioni 49.50 fedha za nje zimetengwa. 

 

(i)            Mradi Na. 4027: Barabara ya Katumbasongwe – Kasumulu – Ngana – Ileje (km 90.10); 

Shughuli itakayotekelezwa ni kujenga barabara ya Katumbasongwe – Kasumulu – Ngana – Ileje (km 90.10) na sehemu ya Isongole II – Ndembo (km 46) na Ndembo Spur road kwa kiwango cha lami. Jumla ya shilingi bilioni 4.00 fedha za ndani zimetengwa.  

 

(j)            Mradi Na. 4103: Barabara ya Geita - Bulyanhulu - Kahama (km 120)

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kuanza ujenzi wa barabara ya Bulyanhulu Jct – Kahama (km 61.7); na kuanza maandalizi ya ujenzi wa sehemu ya Geita – Bulyanhulu (km 58.3) kwa kiwango cha lami. Kazi nyingine ni kuanza ujenzi wa barabara za Nyikonga – Kashero (km 10.5), Kashelo – Ilolangulu (km 15) na Ushirombo – Kilimahewa – Nanda (km 15.7). Jumla ya shilingi bilioni 1.50 fedha za ndani zimetengwa na shilingi bilioni 5.0 fedha za nje zimetengwa. 

 

Barabara za Mikoa na Kupunguza Msongamano

(a)           Mradi Na. 4138: Barabara za Kupunguza Msongamano Jijini Dar es Salaam (km 138.5) 

Shughuli zitakazotekelezwa ni kuendelea na ujenzi wa barabara ya Goba – Matosa – Temboni (km 6); Mji Mwema – Kimbiji – Pembamnazi (km 27.0); Kibamba – Kisopwa – Kwembe – Makondeko (km 14.66) sehemu ya Mloganzila – Mloganzila Citizen (km 4); na kuanza ujenzi wa barabara za Kongowe – Mjimwema – Kivukoni Ferry Road (One Lane Widening: km 25.1), kuanza upanuzi wa barabara ya Mwai Kibaki (km 9.1) pamoja na kuanza maandalizi ya ujenzi wa barabara za Kipata (m 700), Livingstone (m 350), Msikitini – Sharif Shamba (km 1.0) ), Kibamba Shule – Mpiji Magoe (km 9.2), Mbezi Victoria – Magoe Mpiji (km 9.55); Chanika – Mbande (km 4),

Mbezi – Msakuzi – Makabe Jct (km 8.36) na  Kimara - Bonyokwa  - Kinyerezi (km 6.73). Jumla ya shilingi bilioni 10.19 fedha za ndani zimetengwa. 

 

(b)          Mradi Na. 4132: Barabara za Mikoa

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kukarabati kilometa 544.94 kwa kiwango cha changarawe; kujenga kilometa 50.08 kwa kiwango cha lami; na kujenga madaraja/makalvati 59. Jumla ya shilingi bilioni 61.59 fedha za ndani zimetengwa. 

 

(c)           Mradi Na. 4285: Miundombinu ya Mabasi Yaendayo Haraka 

Shughuli zitakazotekelezwa ni kukamilisha ujenzi wa miundombinu ya Mabasi Yaendayo Haraka Awamu ya Pili. Aidha, shughuli nyingine ni kuendelea na ujenzi wa Miundombinu ya Mabasi Yaendayo Haraka Awamu ya Tatu na Nne na kuendelea na kuanza maboresho ya miundombinu ya Mabasi Yaendayo Haraka iliyojengwa katika Awamu ya Kwanza katika eneo la Jangwani. Vilevile, kuendelea na maandalizi ya ujenzi wa Miundombinu ya Mabasi Yaendayo Haraka Awamu ya Tano na ujenzi wa Daraja la Jangwani. Jumla ya shilingi bilioni 2.26 fedha za ndani na shilingi bilioni 42.63 fedha za nje zimetengwa.

(d)          Mradi Na. 4161: Ujenzi wa Barabara za Juu (Flyover) Jijini Dar es Salaam 

Shughuli zitakazotekelezwa ni: kuendelea na maboresho ya makutano ya barabara katika maeneo ya Magomeni, Mwenge,Tabata/Mandela, Morocco, Buguruni, Mbezi Mwisho, Fire na Makutano ya Barabara za Kinondoni/Ali Hassan Mwinyi na Selander

(Ali Hassan Mwinyi/UN Road Jct); na  kuendelea na maandalizi ya ujenzi wa Mabey

Flyovers katika jiji la Dar es Salaam, Dodoma na Mwanza. Jumla ya shilingi milioni 320 fedha za ndani na shilingi bilioni 1.1 fedha za nje zimetengwa. 

 

(e)           Mradi Na. 4146: Barabara za Mzunguko Katika Jiji la Dodoma 

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kuendelea na ujenzi wa barabara ya mzunguko ya Dodoma (Dodoma City Outer Dual Carriageway Ring Road) sehemu za Nala – Veyula – Mtumba – Ihumwa Dry Port (km 52.3), Ihumwa Dry Port – Matumbulu – Nala (km 60); Upanuzi wa barabara za mzunguko ndani ya jiji: Bahi R/About - Image R/About – Ntyuka R/About – Makulu R/About (km 6.3); Mzunguko wa Kati katika Jiji la Dodoma (Dodoma City Middle Ring Road): Nanenane – Miyuji – Mnadani Sekondari – Mkonze – Ntyuka – Nanenane (km 47.2); na Ujenzi wa barabara ya Kikombo Jct – Chololo – Mapinduzi (JWTZ HQ) Road (km 18). Jumla ya shilingi bilioni 4.0 fedha za ndani na shilingi bilioni 45.08 fedha za nje zimetengwa. 

 

Barabara za Vijijini na Mijini

 

(a)           Mradi Na. 4170: Matengenezo na Ukarabati wa Barabara

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Ujenzi wa barabara zenye kiwango cha lami km 344.6, barabara za changarawe km 8,529.83; madaraja makubwa 239, kalvati 246 na mifereji ya maji yenye urefu wa km 28.13 na matengenezo ya barabara km 21,109. Jumla ya shilingi bilioni 710.31 fedha za ndani zimetengwa.

 

(b)          Mradi Na. 4169: Mradi wa Uboreshaji wa Barabara maeneo ya Uzalishaji wa Mazao ya Kilimo (Agri-Connect Programme)

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kuanza matengenezo ya barabara za lami zenye urefu wa km 63.9 kwa ajili ya uboreshaji wa barabara katika maeneo ya uzalishaji wa mazao ya kilimo (Agri-Connect Programme) cha Kahawa na Mbogamboga katika Mikoa ya Nyanda za Juu Kusini. Jumla ya shilingi bilioni 42.0 fedha za nje zimetengwa.

 

(c)           Mradi Na. 6370: Mradi wa Kuboresha Miundombinu Shindanishi katika Miji Tanzania (Tanzania Cities Transforming Infrastructure and Competitiveness-TACTIC)

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kuendelea na ujenzi wa miundombinu Msingi ya Mijini katika Halmashauri 12 ambazo ni Halmashauri za Majiji ya Dodoma, Arusha, Mwanza na Mbeya; Halmashauri za Manispaa za Kigoma, Ilemela, Kahama, Morogoro, Sumbawanga, Songea na Tabora na Halmashauri ya Mji Geita. Jumla ya shilingi bilioni 74.10 fedha za nje zimetengwa.

 

(d)          Mradi Na. 4021: Programu ya Kuongeza Fursa za Kiuchumi na  Kijamii Nchini (RISE)

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kuendelea na ujenzi wa barabara zenye urefu wa km 400 katika wilaya sita (6) za Iringa, Mufindi, Ruangwa, Mbogwe, Handeni na Kilolo. Jumla ya shilingi bilioni 96.8 fedha za nje zimetengwa.

 

(e)           Mradi Na. 6209: Mfuko wa Kuchochea Maendeleo ya Jimbo

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kuendelea kuchochea maendeleo ya wananchi kwa kuchangia fedha katika miradi inayotekelezwa katika majimbo kupitia mfuko wa maendeleo ya Jimbo. Jumla ya shilingi bilioni 15.99 fedha za ndani zimetengwa.

 

(f)            Mradi Na. 6244: Miradi ya Kimkakati ya Kuongeza Mapato katika Halmashauri

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kukamilisha miradi inayotekelezwa na kuanza ujenzi wa miradi ambayo haijaanza utekelezaji. Jumla ya shilingi bilioni 40.00 fedha za ndani zimetengwa.

 

(g)          Uboreshaji wa Bonde la Mto Msimbazi

Shughuli zitakazotekelezwa ni kuanza ujenzi wa miundombinu ya kupunguza mafuriko katika Bonde la Msimbazi ambapo jumla ya shilingi bilioni 106.7 fedha za nje zimetengwa.

 

 

 

 

Ujenzi wa Nyumba za Serikali na Madaraja

 

(a)           Mradi Na. 4126: Ujenzi wa Madaraja Makubwa

Shughuli zitakazotekelezwa ni: kuanza ukarabati wa daraja la Kirumi (Mara); kuendelea na ujenzi wa barabara unganishi za Daraja la Sibiti (Singida); kuendelea na ujenzi wa Madaraja ya Sukuma (Mwanza), Godegode (Dodoma), Mpiji Chini (Dar es Salaam), Sanza (Singida), Mirumba (Katavi), Simiyu (Mwanza) pamoja na Mitomoni  na Mkenda (Ruvuma). Aidha, shughuli nyingine ni kuanza ujenzi wa Madaraja ya Chakwale (Morogoro), Nguyami (Morogoro) na Mbambe (Pwani). Vilevile, shughuli nyingine ni kuanza maandalizi ya ujenzi wa Madaraja ya Mtera, Nzali, Kibakwe, Mpwapwa, Kerema na Munguli yaliyopo Dodoma, Doma (Morogoro), Mbangala (Mtwara), Kinyerezi (Dar es Salaam), Kisorya/Ukerewe (Mara/Mwanza) na Suguti (Mara), Malagarasi Chini (Kigoma) na kununua Vipuri vya Madaraja ya Dharura. Jumla ya shilingi bilioni 15.43 fedha za ndani zimetengwa. 

 

(b)          Mradi Na.  6327: Ujenzi na Ukarabati wa Nyumba za Serikali

Shughuli zitakazotekelezwa ni: kuendelea na ujenzi wa nyumba 20 za viongozi na nyumba 100 za watumishi jijini Dodoma, nyumba za makazi za watumishi katika eneo la Temeke Kota Dar Es Salaam, nyumba za makazi za watumishi katika eneo la Magomeni Kota; kuendelea na ukarabati wa nyumba za Viongozi pamoja na watumishi wa umma maeneo mbalimbali nchini; ujenzi wa jengo la ofisi ya Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi; ukarabati wa karakana za TBA kwa ajili kutengeneza samani katika mikoa ya Arusha, Mwanza, Morogoro, Tabora, Dar Es Salaam na Mbeya pamoja na karakana 12 za TEMESA zilizopo Tabora, Mwanza, Arusha, Mtwara, Mbeya, M.T Depot Dar es Salaam, Kigoma, Mara, Ruvuma, Dodoma, Pwani na Vingunguti; kuendelea na ujenzi wa karakana za  TEMESA katika Mikoa ya Songwe, Simiyu, Geita, Njombe na Katavi; kusanifu na kusimika mfumo wa usimamizi na ufuatiliaji wa matengenezo ya magari, umeme na elektroniki; na kuendelea na ujenzi wa karakana  mpya ya kisasa ya magari jijini Dodoma pamoja na kuanzisha karakana za wilaya katika wilaya za Simanjiro, Masasi, Ukerewe, Chato, Mafia na Kyela. Jumla ya shilingi bilioni 38.82 fedha za ndani zimetengwa.

 

C.          Usafiri Majini

 

Meli

 

(i)           Mradi Na. 4295: Ujenzi na Ukarabati wa Meli

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kukamilisha ujenzi wa meli mpya ya MV. Mwanza Hapa Kazi Tu; kukamilisha ukarabati wa meli za MV Umoja na MT. Sangara; kuanza ujenzi wa meli mpya (Wagon ferry) yenye uwezo wa kubeba tani 3,000 za mabehewa ya mizigo katika Ziwa Victoria na meli mpya (Barge/Cargo ship) ya kubeba shehena ya mizigo yenye uwezo wa kubeba tani 2,800 na meli mpya ya kubeba abiria 600 na tani 400 za mizigo katika Ziwa Tanganyika; kuanza ujenzi wa chelezo ya kubeba meli wakati wa matengenezo katika Ziwa Tanganyika; kuanza ukarabati wa Meli ya MV Liemba, MV Sengerema, MT. Ukerewe na MT. Nyangumi; na ukarabati wa boti moja (1) ya mwendokasi (Sea Warrios) katika Ziwa Tanganyika kwa ajili ya kusaidia kazi za uokozi sambamba na usafirishaji wa watalii wanaotembelea kisiwa cha Gombe. Jumla ya shilingi bilioni 100.00 fedha za ndani zimetengwa.

 

(ii)         Mradi Na. 4201:  Uboreshaji wa Usalama wa Usafiri katika Ziwa

Victoria 

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kuendelea na uboreshaji wa kituo cha Kanda cha uokozi Mwanza; uboreshaji wa vituo vitatu (3) vya Kitaifa vya Utafutaji na Uokozi vya MRCC-Musoma, Ukerewe na Kanyala; uboreshaji wa Mfumo wa Simu za Dharura; uboreshaji wa vituo vya utafutaji na uokozi; na kuendelea na ununuzi wa vifaa ikiwemo ununuzi wa boti, kamera, samani, X-Band rada, maritime radio - VHF/MHF na HF, GMDSS, LRIT, navigation dividers, vishikwambi na darubini kwa ajili ya vituo na ofisi zilizoanzishwa. Jumla ya shilingi bilioni 1.74 fedha za nje zimetengwa.

 

Vivuko

 

(i)           Mradi Na. 4125: Ujenzi wa Maegesho ya Vivuko

Shughuli zitakazotekelezwa ni: kufanya tathmini kwa ajili ya kulipa fidia kwa wakazi wa Kigamboni watakaoathiriwa na upanuzi wa maegesho Kigamboni; ujenzi na ukarabati wa maegesho 11 (Magogoni – Kigamboni, Kilambo – Namoto, Utete – Mkongo, Iramba – Majita, Nyakarilo – Kome, Irunda - Luchelele, Kisorya – Rugezi, Ilagala – Kajeje, Rusumo - Nyakiziba, Musoma – Kinesi na Kasharu – Buganguzi). Aidha, kazi nyingine ni ujenzi wa maegesho ya Zumacheli (Chato – Nkome) na ujenzi wa maegesho mapya ya vivuko vya Kayenze – Kanyinya, Muleba – Ikuza, Ijinga – Kahangala na Bwiro – Bukondo. Vilevile,  ujenzi/ukarabati wa maegesho ya Buyagu, Mbalika, Ilunda, Luchelele, Bukimwi, Kisorya, Rugezi, Kahunda na Maisome; ujenzi wa ofisi na majengo ya abiria na uzio kwenye vituo sita (06) vya vivuko (Kahunda – Maisome, Msangamkuu – Msemo, Kisorya – Rugezi, Bezi – Bukimwi, Nyakarilo – Kome na Bugolora – Ukara); na kufunga mfumo wa kielektroniki wa usimamizi wa vivuko na mifumo ya tiketi katika vituo 21. Jumla ya shilingi bilioni 2.44 fedha za ndani zimetengwa.

 

(ii)         Mradi Na. 4139:  Ujenzi wa Vivuko Vipya  

Shughuli zitakazotekelezwa ni: kuendelea na ujenzi wa vivuko vipya vya Kisorya –

Rugezi, Ijinga – Kahangala, Bwiro – Bukondo, Magogoni – Kigamboni, Nyakarilo – Kome, Nyamisati – Mafia, Buyagu – Mbalika; kufanya manunuzi ya vitendea kazi vya karakana za TEMESA. Jumla ya shilingi bilioni 5.75 fedha za ndani zimetengwa.

 

(iii)       Mradi Na. 4144: Ukarabati wa Vivuko 

Shughuli zitakazotekelezwa ni kuendelea na ukarabati wa vivuko vya MV Mara, MV Mwanza, MV Ukara I, MV Sabasaba, MV Pangani II, MV Malagalasi, MV Mafanikio, MV Ujenzi, MV Kome II, MV Misungwi, MV Nyerere, MV Kyanyabasa, MV Tanga, MV Kitunda, MV Kazi, MV Magogoni na MV Kilombero II. Aidha, kazi nyingine ni ukarabati wa boti ya Uokozi – MV SAR II. Jumla ya Shilingi bilioni 6.09 fedha za ndani zimetengwa.

 

Bandari 

 

(i)         Mradi Na. 4227: Uboreshaji wa Bandari ya Dar es Salaam

 

(a)         Bandari ya Dar es Salaam

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kuendelea uchimbaji wa kina na upanuzi wa lango la kuingilia na kugeuzia meli hadi kufikia mita 15.5; na uboreshaji wa Gati Na. 8 –11; Kuendelea na utekelezaji wa mradi wa Ujenzi wa Matanki ya kuhifadhia Mafuta; Kufanya upembuzi yakinifu katika bandari ya Dar es Salaam kwa lengo la kupata maeneo ya ziada ya kuhudumia mizigo; na kuendelea na upembuzi yakinifu wa ujenzi wa gati Na. 12 -15. Jumla ya shilingi bilioni  93.80 fedha za nje zimetengwa.

 

(b)         Bandari ya Tanga

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kuendelea na uboreshaji wa awamu ya pili ya kuchimba kina, kupanua lango la kuingilia meli na ununuzi wa “port operational

equipment; na maandalizi ya ujenzi wa miundombinu ya gati la mafuta ghafi kutoka Hoima (Uganda) hadi Chongoleani (Tanga). Jumla ya shilingi bilioni  1.80 fedha za ndani zimetengwa.

 

(c)         Bandari ya Mtwara

Shughuli zitakazotekelezwa ni: ujenzi wa bandari kwa ajili ya kuhudumia bidhaa zinazoweza kuchafua mazingira ikiwa ni pamoja na makaa, clinker, katika eneo la Kisiwa Mgao; kuendelea na ukarabati ya maeneo ya kuhudumia shehena; ukarabati wa miundombinu ya barabara zinazoingia bandarini. Jumla ya shilingi bilioni 5.20 fedha za ndani zimetengwa. 

 

(d)         Bandari ya Bagamoyo

Shughuli zitakazotekelezwa ni: kuhamisha wananchi waliolipwa fidia na wanaotakiwa kupisha ujenzi wa bandari; kuendelea na utekelezaji wa mradi wa Bandari ya Mbegani – Bagamoyo; kuanza maandalizi ya ujenga miundombinu wezeshi (barabara, reli, na umeme) kwa ajili ya bandari ya Bagamoyo. Jumla ya shilingi bilioni 30 fedha za ndani zimetengwa.

 

(e)         Bandari Kavu katika Eneo la Ruvu

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kukamilisha ujenzi wa yadi na sakafu ngumu (pavement) yenye ukubwa wa hekta tano (5) na  barabara ya Vigwaza – Kwala (km 15.5). Jumla ya shilingi bilioni  5.0 fedha za ndani zimetengwa.

 

Bandari za Maziwa Makuu

(a)         Ziwa Victoria

Shughuli zitakazotekelezwa ni: kuendelea na ujenzi wa Bandari za Bukoba na, 

Kemondo Bay; kuendelea na hatua za ununuzi wa mkandarasi kwa ajili ya ujenzi wa Bandari ya Mwanza South; na kuendelea na hatua za mwisho za kufanya Usanifu wa Kina (Detailed Engineering Design) kwa ajili ya ujenzi wa Mwanza North ikijumuisha miundombinu ya Reli (SGR). Jumla ya shilingi bilioni 1.44 fedha za ndani zimetengwa.

 

(b)         Ziwa Tanganyika

 

Bandari ya Kigoma, Kibirizi na Ujiji 

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Uboreshaji wa Bandari ya Kigoma kwa kujenga barabara za kiungo, Cargo Shed, Passenger Wharf and Lounge; kuendelea na ujenzi wa jengo la abiria (Passenger Lounge); na kuendelea na ujenzi wa Passenger

Lounge na ukuta wa mizigo wa  Lighter Quay katika Bandari ya Kibirizi na gati la Bandari ya  Ujiji. Jumla ya shilingi bilioni  12.7  fedha za ndani zimetengwa.

 

(c)         Bandari za Ziwa Nyasa

 

(i)           Bandari ya Ndumbi na Mbambabay

 

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kuendelea na uboreshaji wa Bandari ya Ndumbi kwa kujenga barabara unganishi; na Kuanza uboreshaji wa bandari ya Mbambabay. jumla ya shilingi bilioni 1.462 fedha za ndani zimetengwa.

 

(ii)         Ununuzi wa Mitambo ya Kuhudumia Bandari

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kuendelea na ununuzi wa mitambo na vifaa mbalimbali vitakavyotumika katika Bandari nchini. Jumla ya shilingi bilioni 32.974 fedha za ndani zimetengwa katika mwaka wa fedha 2023/2024

 

D.          Usafiri wa Anga

 

(a)        Mradi Na.6267 : Institutional Support

 

(i)                    Uendeshaji wa Jengo la Tatu la Abiria (JNIA-TB III) na Kuboresha Huduma katika Viwanja Vingine vya Ndege

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kuendelea na uboreshaji wa miundombinu katika jengo la tatu la abiria (JNIA TB III) unaojumuisha matengenezo ya mitambo na mifumo mbalimbali ikiwemo lifti 14, eskaleta saba (7), travelators mbili (2) za abiria, mashine 20 za ukaguzi wa abiria na mizigo, mifumo ya tiketi za abiria na mifumo ya TEHAMA; usimikaji wa mfumo wa taa za kuongozea ndege katika kiwanja cha ndege cha Arusha; ununuzi wa gari moja (1) la Zimamoto na Uokoaji; kukamilisha ujenzi wa jengo jipya la abiria katika kiwanja cha ndege cha Mwanza; kuanza kwa ujenzi wa mnara wa kuongozea ndege katika kiwanja cha ndege Bukoba; na kuanza ujenzi wa jengo la abiria katika kiwanja cha ndege Mtwara. Jumla ya shilingi bilioni  17.30 fedha za ndani zimetengwa..

 

(ii)                  Chuo cha Bahari Dar es Salaam - DMI

Shughuli itakayotekelezwa ni kukamilisha malipo ya ununuzi wa vifaa vya kufundishia (full mission crane simulator). Jumla ya shilingi bilioni 1.0 fedha za ndani zimetengwa

 

(iii)                Mradi wa Ununuzi mitambo ya mawasiliano katika viwanja vya ndege 

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kununua mitambo ya kisasa (Doppler Very High Frequency Omnidirectional Radio Range (DVOR), Distance Measuring Equipment (DME) na Instrument Landing Systems (ILS) ili kuwasaidia marubani kutua kwa usalama katika viwanja vya ndege vya  JNIA, KIA, AAKIA, Mwanza na Songwe. Jumla ya shilingi bilioni 6.50 fedha za ndani zimetengwa.

 

(b)         Mradi Na. 4209: Kiwanja cha Ndege Mwanza 

Shughuli itakayotekelezwa ni: Ujenzi wa jengo jipya la abiria na mifumo yake, upanuzi wa maegesho ya ndege na ujenzi wa uzio wa usalama. Jumla ya shilingi bilioni 5.83 fedha za ndani zimetengwa.

 

(c)         Mradi Na. 4220: Kiwanja cha Ndege Mtwara

Shughuli zitakazotekelezwa ni: kukamilisha ukarabati wa barabara ya kuruka na kutua ndege, viungio na maegesho ya ndege; kufunga taa na mitambo ya kuongozea ndege; na ujenzi wa barabara ya kuingia na kutoka kiwanjani, maegesho ya magari na uzio wa usalama. Jumla ya shilingi bilioni 5.44 fedha za ndani zimetengwa.

(d)         Mradi Na. 4156: Kiwanja cha Ndege Kigoma

Shughuli zitakazotekelezwa ni: kuendelea na ujenzi wa Jengo la Abiria pamoja na miundombinu yake, ukarabati na upanuzi wa maegesho ya ndege, maegesho ya magari na barabara ya kuingia na kutoka kiwanjani, ufungaji wa taa na mitambo ya kuongozea ndege; na ujenzi wa uzio wa usalama, jengo la kuongozea ndege na jengo la uchunguzi wa hali ya hewa (OBS). Jumla ya shilingi bilioni 5.06 fedha za ndani na shilingi bilioni 4.54 fedha za nje zimetengwa.

(e)         Mradi Na. 4221: Kiwanja cha Ndege Sumbawanga

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kujenga barabara ya kutua na kuruka ndege na kiungio, maegesho ya ndege, jengo la abiria, jengo la kuongozea ndege, jengo la uchunguzi wa hali ya hewa, uzio wa usalama, barabara ya kuingia kiwanjani na maegesho ya magari; na kufunga taa na mitambo ya kuongozea ndege. Jumla ya shilingi milioni 726.0 fedha za ndani na shilingi bilioni 4.54 fedha za nje zimetengwa.

 

(f)          Mradi Na. 4222: Kiwanja cha Ndege Shinyanga

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kujenga barabara ya kutua na kuruka ndege na kiungio, maegesho ya ndege, jengo la abiria, jengo la kuongozea ndege, jengo la uchunguzi wa hali ya hewa, barabara ya kuingia na kutoka kiwanjani, maegesho ya magari; kufunga taa na mitambo ya kuongozea ndege; na ujenzi wa uzio wa usalama. Jumla ya shilingi milioni 726.0 fedha za ndani na shilingi bilioni 4.54 fedha za nje zimetengwa.  

 

(g)         Mradi Na. 4206: Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa Songwe

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kumalizia ujenzi wa Jengo la Abiria na mifumo yake; ufungaji wa taa za kuongozea ndege; na ujenzi wa uzio wa usalama. Jumla ya shilingi bilioni 6.12 fedha za Ndani zimetengwa. 

 

(h)         Mradi Na. 4226: Viwanja vya Ndege vya Mikoa

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kuendelea na ujenzi wa viwanja vya ndege katika mikoa ya Geita, Iringa, Ruvuma (Songea), Simiyu, Lake Manyara, Tanga, Moshi, Lindi na Mara (Musoma); ujenzi wa uzio wa usalama katika kiwanja cha ndege cha Dodoma; ujenzi wa barabara ya kuruka na kutua ndege kwa kiwango cha lami kwenye kiwanja cha ndege cha Nachingwea; ukarabati wa kiwanja cha ndege cha Inyonga; na kufanya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina kwa ajili ya ujenzi wa kiwanja cha ndege cha Mkoa wa Manyara. Jumla ya shilingi bilioni 22.48 fedha za Ndani na shilingi bilioni 1.77 fedha za nje zimetengwa.

 

(i)           Mradi Na. 4286: Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa Msalato

Shughuli zitakazotekelezwa ni kuendelea na ujenzi wa kiwanja cha Ndege cha Msalato Jijini Dodoma. Jumla ya shilingi bilioni 1.11 fedha za ndani na shilingi bilioni 28.37 fedha za nje zimetengwa. 

 

(j)          Mradi Na. 4158: Kiwanja cha Ndege Mpanda

Shughuli itakayotekelezwa ni kuanza usanifu wa jengo la abiria. Jumla ya shilingi milioni 13.31 fedha za ndani zimetengwa. 

 

(k)         Mradi Na. 4159: Kiwanja cha Ndege Tabora

Shughuli itakayotekelezwa ni ujenzi wa jengo la abiria, jengo la kuongozea ndege, barabara ya kuingia kiwanjani, maegesho ya magari, uzio wa uwanja na jengo la uchunguzi wa hali ya hewa. Jumla ya shilingi milioni 728.66 fedha za ndani na shilingi bilioni 4.54 fedha za nje zimetengwa.

 

(l)           Kiwanja cha Ndege Bukoba

Shughuli itakayotekelezwa ni kuendelea na maandalizi ya ujenzi wa jengo la Watu Mashuhuri (VIP Lounge), ukarabati wa meta 200 wa barabara ya kuruka na kutua ndege pamoja na ufungaji wa taa za kuongozea ndege. Jumla ya shilingi milioni 10 fedha za ndani zimetengwa.

 

(m)       Mradi Na. 4210: Kiwanja cha Ndege Arusha

Shughuli itakayotekelezwa ni kujenga uzio wa usalama. Jumla ya shilingi milioni 266.22 fedha za ndani zimetengwa.

 

E.          Hali ya Hewa

 

(a) Mradi Na. 4290: Ununuzi wa Rada, Vifaa na Ujenzi wa Miundombinu ya Hali ya Hewa

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Ununuzi wa vifaa na mitambo ya kisasa kwa ajili ya utabiri wa hali ya hewa ikijumuisha rada mbili (2) za kwenye maji zitakazofungwa Tanga na Pemba kwa ajili upatikanaji wa taarifa ya hali ya hewa katika Bahari ya Hindi, mitambo ya kupima hali ya hewa inayojiendesha yenyewe (AWS) na vifaa vya kupima mgandamizo wa hali ya hewa, kiasi cha joto na unyevunyevu; kukamilisha malipo ya rada mbili (2) za hali ya hewa pamoja na ufungaji wake; kuendelea na ujenzi wa kituo cha kanda ya mashariki (Dar es Salaam) na kituo cha kutoa tahadhari ya matukio ya Tsunami; kuendelea na ujenzi wa maabara ya uhakiki wa vifaa vya hali ya hewa; kuanza kwa ujenzi wa ofisi za makao makuu Jijini Dodoma; uboreshaji wa miundombinu ya Chuo cha Taifa cha Hali ya hewa; na ukarabati wa vituo vitatu (3) vya hali ya hewa. Jumla ya shilingi bilioni 13.0 fedha za ndani zimetengwa.

 

F.           Miundombinu ya kujifunzia

 

(a)      Mradi Na.6377 Ujenzi wa Miundombinu na Ununuzi wa Vifaa vya Kufundishia 

(i)         Chuo cha Taifa cha Usafirishaji – NIT 

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Ukamilishaji wa Kituo cha Rasilimali Mafunzo kwa kuendelea na ujenzi wa jengo la ghorofa sita (6) lenye Maktaba yenye uwezo wa kuhudumia wanafunzi 450, madarasa yenye uwezo wa kuhudumia wanafunzi 1,653 pamoja na ofisi za watumishi katika kampasi ya Mabibo – Dar-es-Salaam; kuanza ujenzi wa awamu ya kwanza ya miundombinu ya Kituo Atamizi cha Mafunzo ya kuandaa mafundi mahiri wa teknolojia ya usafiri kwa njia ya Reli Tabora; ununuzi wa vifaa vya kufundishia kwa ajili ya mafunzo ya ufundi na teknolojia ya mafuta na gesi baharini; ujenzi wa jengo la kitaaluma la ghorofa nne (4) lenye uwezo wa kuhudumia wanafunzi 4,500 kwa wakati mmoja katika Kampasi ya Mabibo Dar es Salaam; ujenzi wa miundombinu kwa ajili ya uanzishwaji wa mafunzo na Kituo Atamizi cha kuandaa mafundi mahiri wenye ujuzi kwenye sekta ya usafiri wa majini, mafuta na gesi Kikwetu Lindi; na ununuzi wa vifaa vya mafunzo ya usafiri kwa njia ya maji. Jumla ya shilingi bilioni  2.27 fedha za ndani zimetengwa.

 

G.          Nishati

 

Miradi ya Kufua Umeme

 

(i)           Mradi Na. 3164: Kinyerezi I Extension (MW 185)

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kufanya ununuzi wa vifaa vya akiba (spare parts) na kukamilisha ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme msongo wa kV 132 kutoka kituo cha kufua umeme (Kinyerezi) kwenda Gongo la Mboto hadi Mbagala. Jumla ya shilingi bilioni 40 fedha za ndani zimetengwa.

 

(ii)         Mradi Na. 3168: Umeme wa Maji Kikonge (MW 300 

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kufanya upembuzi yakinifu; kufanya tathmini ya Athari kwa Mazingira na Jamii; uthamini wa mali za wananchi watakaopisha mradi na ulipaji wa fidia; kukamilisha usanifu wa mradi; na kuwapata Mshauri Mwelekezi na Mkandarasi wa mradi. Jumla ya shilingi milioni 500 fedha za ndani zimetengwa.

 

(iii)       Mradi Na. 3174: Umeme wa Maji Malagarasi (MW 49.5) 

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kukamilisha taratibu za kumpata Mkandarasi wa ujenzi wa bwawa; kuendelea na ujenzi wa njia ya kusafirisha  umeme msongo wa kV 132 kutoka kwenye bwawa hadi kituo cha kupoza umeme cha kidahwe; na kukamilisha ununuzi  wa vifaa vya ujenzi wa miundombinu ya kuunganisha wateja. Jumla ya shilingi milioni 350 fedha za ndani na shilingi bilioni 15.17 fedha za nje zimetengwa.

 

(iv)       Mradi Na.3173: Umeme wa Maji wa Kakono (MW 87.8) 

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kulipa fidia kwa wananchi wanaopisha mradi; kukamilisha taratibu za kumpata Mshauri Mwelekezi; kuwapata Wakandarasi wa ujenzi; na kuanza ujenzi wa mradi. Jumla ya shilingi bilioni 2.62 fedha za ndani na shilingi bilioni 36.53 fedha za nje zimetengwa.

 

(v)         Mradi Na. 3182: Kuzalisha Umeme kwa Kutumia Gesi Asilia – Mawe Project (MW 150)

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kukamilisha ununuzi na kusimika mitambo ya kuzalisha umeme kwa kutumia gesi asilia yenye uwezo wa kuzalisha jumla ya MW 150 ambapo MW 90 zitakuwa katika eneo la Tegeta ( Dar es Salaam) na MW 60 eneo la Mwanambaya – Mkuranga (Pwani). Jumla ya shilingi bilioni 345 fedha za ndani zimetengwa.

 

(vi)       Mradi Na.3183: Kuzalisha Umeme kwa Kutumia Gesi Asilia – Mwamba Project (MW 450)

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kufanya Tathmini ya Athari kwa Mazingira na Jamii; kumpata Mshauri Mwelekezi na Mkandarasi; na kuanza maandalizi kwa ajili ya ujenzi wa mradi. Jumla ya shilingi bilioni 1.5 fedha za ndani zimetengwa.

 

(vii)      Mradi wa Kuzalisha Umeme kwa Kutumia Jua wa Shinyanga (MW 150)

Shughuli zitakazotekelezwa ni: kukamilisha malipo ya fidia kwa wananchi wanaopisha mradi na kuanza ujenzi wa mradi. Jumla ya Shilingi milioni 500  fedha za ndani na Shilingi bilioni 27.13 ni fedha za nje zimetengwa.

 

Miradi ya Usafirishaji na Usambazaji wa Umeme 

 

(i)                            Mradi Na. 3111: Uimarishaji wa Gridi ya Taifa (National Grid

Stabilization

Shughuli zitakazotekelezwa ni ujenzi na uboreshaji wa njia za kusafirisha umeme na vituo vya kupoza umeme katika maeneo mbalimbali nchini ikiwa ni pamoja na:  (a) Njia za msongo wa kV 132 za Tabora – Urambo; Tabora – Katavi;  Ilala - Kurasini kupitia ardhini (underground cable); Ubungo – Chalinze - Hale; Kinyerezi - Gongolamboto – Mbagala; Mkata - Kilindi; Kasinga – Lushoto; na Kiyungi – Rombo.

(b)          Njia za msongo wa kV 33 za Mkata - Kwamsisi; Zuzu – Mbande; Nyamongo – Magumu (Serengeti); Nyakanazi – Bulyanhulu; Nyakanazi – Kakonko; na Nyakanazi – Lusahunga.

(c)           Njia za msongo wa kV 220 za Songea – Tunduru; Ibadakuli (Shinyanga) – Bariadi (Simiyu); Kimara – Mabibo – Ilala; Pugu – Dundani; Tunduru – Masasi; na kuongeza uwezo wa njia ya kusafirisha umeme kutoka kV 132 kwenda kV 220 kutoka Ubungo – Kunduchi – Ununio.

(d)          Vituo vya kupoza umeme vya Urambo, Nguruka, Ipole, Inyonga, Mpanda, Tunduru, Kilindi, Songwe Mkwajuni, Zengereni Viwandani, Dege, Ununio, Bariadi, Ukerewe, Mkata, Shinyanga, Lushoto, Rombo, Dundani,  Ilala, Mabibo, Ubungo, vituo vya kuongeza nguvu ya umeme (Regulating Transformer) vya Mbande (Dodoma) na Kasulu (Kigoma) pamoja na ujenzi wa Switching station Msigani (Dar es Salaam) na Mugumu (Serengeti). Jumla ya shilingi bilioni 473.40 fedha za ndani zimetengwa.

 

 

 

(ii)         Mradi Na. 3179: Njia ya Kusafirisha Umeme wa Msongo wa kV 400 Rufiji – Chalinze – Dodoma na Chalinze – Kinyerezi

 

Rufiji – Chalinze kV 400: Kazi zitakazotekelezwa ni kukamilisha ujenzi wa Kituo cha kupoza umeme Chalinze. Jumla ya Shilingi bilioni 20 fedha za ndani zimetengwa.

 

Kinyerezi - Chalinze kV 400: Shughuli itakayotekelezwa ni: Kukamilisha ulipaji fidia wananchi watakaopisha mradi; na kuanza utekelezaji wa mradi.  Jumla ya shilingi milioni 500 fedha za ndani zimetengwa. 

 

Chalinze - Dodoma kV 400: Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kukamilisha ulipaji fidia wananchi watakaopisha mradi na kuanza ujenzi wa mradi. Jumla ya shilingi milioni 500 fedha za ndani zimetengwa. 

 

(iii)       Mradi Na. 3166: Njia ya Kusafirisha Umeme wa Msongo wa kV 400 – North – West Grid Extension (Iringa – Mbeya – Sumbawanga – Mpanda – Kigoma – Nyakanazi)

Awamu ya Kwanza: Iringa – Mbeya – Tunduma – Sumbawanga (TAZA):

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kukamilisha ulipaji fidia kwa wananchi waliopisha mradi; na kuanza ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme na vituo vya kupoza umeme  (Iringa, Kisada, Mbeya, Tunduma na Sumbawanga). Jumla ya shilingi bilioni 3.00 fedha za ndani na shilingi bilioni 53.51 fedha za nje zimetengwa.

 

Awamu ya Pili: Kigoma – Nyakanazi: Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kuendelea na ujenzi wa njia ya kusafirishia umeme; kujenga vituo vya kupoza umeme vya Nyakanazi na Kidahwe pamoja na njia za usambazaji wa umeme katika vijiji vinavyopitiwa na mradi. Jumla ya Shilingi milioni 600 fedha za ndani na Shilingi bilioni 33.4 fedha za nje zimetengwa.

 

Geita – Nyakanazi: Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kukamilisha ujenzi wa miundombinu ya kusambaza umeme katika vijiji 32 vinavyopitiwa na mradi. Jumla ya shilingi bilioni 11.73 fedha za nje zimetengwa.

 

(iv)       Mradi Na. 3181: Njia ya Kusafirisha Umeme wa Msongo wa kV 220 Benaco - Kyaka

Shughuli zitakazotekelezwa ni: kukamilisha uthamini wa mali za wananchi wanaopisha mradi; kulipa fidia wananchi wanaopisha mradi; kuwapata  Mshauri Mwelekezi na Mkandarasi wa ujenzi wa mradi; na kuanza ujenzi wa mradi. Jumla ya shilingi bilioni 5.8 fedha za ndani zimetengwa.

 

 

 

(v)         Njia ya Kusafirisha Umeme wa Msongo wa kV 220 (Rusumo – Nyakanazi) 

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kukamilisha malipo ya fidia kwa wananchi waliosalia na kuendelea na malipo kwa kipindi cha uangalizi (retention money) kwa Mkandarasi wa ujenzi. Jumla ya shilingi milioni 225 fedha za ndani na shilingi bilioni 3.62 fedha za nje zimetengwa. 

 

(vi)       Mradi Na. 3175: Njia ya Kusafirisha Umeme wa Msongo wa kV 400 kutoka Singida – Arusha – Namanga 

Shughuli zitakazotekelezwa ni: kukamilisha kazi za ujenzi wa mradi zikijumuisha kufanya majaribio ya miundombinu iliyojengwa katika mradi huu. Jumla ya shilingi bilioni 15.92 fedha za nje zimetengwa. 

 

(vii)      Mradi Na. 3113: Usambazaji wa Nishati Vijijini

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kuendelea na Awamu ya Tatu Mzunguko wa Pili wa Usambazaji Umeme Vijijini; ufungaji wa mitambo ya umeme wa jua katika maeneo ya vijijini yaliyopo mbali na Gridi ya Taifa; Ujazilizi (Densification) Awamu ya IIB na IIC; kupelekela umeme katika Vitongoji kwa mikoa ya Songwe na Kigoma; kukamilisha ujenzi wa kituo cha kupoza umeme cha wa Ifakara;kuwezesha usambazaji wa mitungi ya gesi na majiko kwa ajili ya kupikia vijijini; kupeleka umeme katika maeneo ya migodi ya wachimbaji wadogo na mashamba ya kilimo cha umwagiliaji; kupeleka umeme kwenye taasisi za afya na pampu za na maji ili kuzuia magonjwa ya kuambukiza ikiwemo UVIKO 19; na kuwezesha ujenzi wa vituo vidogo vya kusambaza bidhaa za petroli vijijini kwa njia ya mkopo nafuu (Credit line facility). Jumla ya shilingi bilioni 59.46 fedha za ndani  na Shilingi bilioni 78.31 fedha za nje zimetengwa.

 

(viii)    Mradi Na. 3180: Usambazaji wa Umeme Katika Vitongoji

Shughuli zitakazotekelezwa ni: kuwapata wakandarasi wa miradi; na kuanza ujenzi katika mikoa mbalimbali nchini. Jumla ya shilingi bilioni 377.05 fedha za ndani zimetengwa.

 

(ix)       Utekelezaji wa Programu ya Nishati Safi ya Kupikia (Clean Cooking Energy)

Shughuli zitakayotekelezwa ni: kuandaa na kuratibu utekelezaji wa Mkakati wa Taifa wa Mawasiliano kuhusu matumizi ya nishati safi ya kupikia; kuhamasisha na kuelimisha wananchi kuhusu matumizi ya nishati safi ya kupikia; kufanya mapitio ya Sera, Sheria, Kanuni na Miongozo inayohusu nishati safi ya kupikia; kusimamia uboreshaji wa miundombinu ya nishati safi ya kupikia; na kujenga uwezo wa wataalamu katika kusimamia masuala ya nishati safi ya kupikia. Aidha, Serikali kupitia REA itatekeleza mradi wa kujenga mifumo ya kuzalisha nishati ya bayogesi kwa ajili ya kupikia katika taasisi takriban 100 zinazohudumia watu zaidi ya 300 katika maeneo mbalimbali nchini. Jumla ya shilingi bilioni 2 fedha za ndani zimetengwa. Jumla ya shilingi bilioni 4.5 zimetengwa, kati ya hizo shilingi bilioni 2.5 zimetengwa na Wizara ya Nishati na shilingi bilioni 2 zimetengwa na Wakala ya

Nishati Vijijini.

 

Miradi ya Gesi Asilia na Mafuta 

 

(i) Mradi Na. 3162: Usambazaji wa Gesi Asilia kwa Mikoa ya Dar es Salaam, Mtwara, Lindi na Pwani 

Shughuli zitakazotekelezwa ni: kuanza ujenzi wa mradi wa bomba la usambazaji wa gesi asilia kutoka Mwenge hadi Mbezi Beach; kuanza ujenzi wa mradi wa bomba la usambazaji wa gesi asilia kutoka matoleo ya bomba kuu (BVS3) hadi Mnazi Mmoja mkoani Lindi; kuingia mkataba na mkandarasi wa ujenzi wa vituo vya CNG pamoja na kuanza ujenzi; kuingia mkataba na mkamdarasi wa ujenzi wa miundombinu ya usambazaji gesi asilia kwenda DUCE na Mlimani City; kuanza ujenzi wa bomba la kusafirisha gesi asilia kutoka Ntorya kwenda Madimba; kuanza ujenzi wa miundombinu ya usambazaji gesi asilia kwa DANGOTE, SAPPHIRE, ANRIC, WU ZHOU na NEELKANTH; na kuanza kwa utekelezaji wa mradi wa usambazaji gesi asilia majumbani kwa mikoa ya Pwani na Lindi. Jumla ya shilingi bilioni 1.05 ya fedha za ndani zimetengwa.

 

3.3.2.2. Mapinduzi ya TEHAMA

 

(i)            Mradi Na. 4283: Ujenzi wa Mkongo wa Mawasiliano wa Taifa 

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kuendelea na  ujenzi wa Kilometa 1,600 za Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano na Vituo vipya 15 vya kutolea huduma za Mkongo; ujenzi wa Mikongo ya Mwisho (last mile connectivity) kwenye taasisi 200 za Kimkakati; kuendelea na ujenzi wa mkongo wa majini kiasi cha kilomita 60 ili kuunganisha Tanzania na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kupitia Ziwa Tanganyika; ujenzi wa Kituo cha Taifa cha Kutunzia Data Zanzibar, kuongeza udhibiti wa matumizi ya taarifa binafsi na kupunguza uhalifu wa mitandao kwa kushirikiana na Vyombo vya Ulinzi na Usalama; kuelimisha umma kuhusu Mkakati wa Usalama Mtandaoni,  na kukamilisha maandalizi ya kanuni na kuanza kwa utekelezaji wa Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi ya mwaka 2022. Jumla ya shilingi bilioni 80 fedha za ndani  zimetengwa. 

 

(ii)           Mradi Na. 4234: Anwani za Makazi 

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kuhakiki taarifa na kuweka miundombinu ya Anwani za Makazi katika Halmashauri 80, maeneo ya makundi maalum ikiwemo vituo vya bodaboda, wamachinga na kwenye maeneo ya Kimkakati nchini; kuboresha programu tumizi kulingana na mahitaji ya watumiaji; kuboresha Sera ya Posta ya Mwaka 2003, na kutunga sheria mahsusi ya Anwani za Makazi; na kujenga uelewa kuhusu namna ya kusimamia na kuendeleza mfumo wa anwani za makazi. Jumla ya Shilingi bilioni 24 fedha za ndani zimetengwa.

 

(iii)         Mradi Na. 4280: Tanzania ya Kidijitali

Shughuli zitakazotekelezwa ni:  Kuanzishwa kwa Taasisi ya TEHAMA na vituo vya  Ubunifu wa TEHAMA; kuanzishwa kwa  vituo vitano (5) vya kanda vya kusaidia kukuza Taaluma ya TEHAMA;  kuendelea na Utekelezaji wa Mradi wa Anwani ya makazi na Postikodi;  utengenezaji wa  Mfumo wa Kitaifa wa Usimamizi wa Taarifa za Takwimu za TEHAMA (NISMIS); kuunganisha Taasisi za Serikali kwenye mtandao mmoja (GoVNET); Usimikaji wa vituo 10 vya Huduma Pamoja Centers; kujenga maabara tatu (3) kwa ajili ya kufufua vifaa vya TEHAMA katika Mikoa ya Arusha, Dar es Salaam na Mwanza;  kuboresha uwezo na Mifumo ya Vituo vya kuhifadhia Data; utekelezaji wa Mkakati wa mawasiliano wa Tanzania ya kidijitali; Elimu kwa Umma; na Kujenga uwezo kwa wataalamu wa TEHAMA 500  Serikalini. Jumla ya shilingi bilioni 35.18 fedha za nje zimetengwa.

 

(iv)         Mradi Na. 4279: Upanuzi wa Usikivu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC)

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kuendelea kujenga na kufunga miundombinu ya utangazaji ya redio na televisheni katika vituo vya TBC1, TBC2 na Tanzania Safari; ununuzi wa magari maalumu mawili (2) ya kurushia matangazo mbashara (Radio na Televisheni); ununuzi wa magari 10 kwa ajili shughuli za utangazaji; kuendelea na ujenzi wa  Makao Makuu ya TBC Jijini Dodoma pamoja na ufungaji wa mifumo ya TEHAMA; na ununuzi wa mitambo na vifaa vya utangazaji wa redio, Televisheni na Mitandao ya kijamii kuunganisha studio tano (5) za Mikocheni, Zanzibar, Barabara ya Nyerere, Dodoma na Arusha. Jumla ya shilingi bilioni 15.0 fedha za ndani zimetengwa.  

 

(v)           Mradi Na. 6567: Habari kwa Umma

Shughuli zitakazotekelezwa ni: kuandaa makala maalumu, kukusanya na kusambaza habari na taarifa kwa wananchi kuhusu mafanikio ya utekelezaji wa miradi na programu mbalimbali za Serikali; ununuzi wa vitendea kazi muhimu kwa ajili ya ukusanyaji, uchakataji na uandaaji wa taarifa vikiwemo kamera na visaidizi vyake, vifaa vya Kurushia Matangazo Mubashara; na kuanzisha Chaneli ya Televisheni ya Serikali itakayokuwa inaonesha habari za Serikali ikijumuisha shughuli zinazotekelezwa na Wizara, Taasisi, Mikoa na Halmashauri.  Jumla ya shilingi bilioni 1.5 fedha za ndani zimetengwa kutekeleza shughuli hizo. 

 

(vi)         Mradi Na. 4383: Kuimarisha uwezo wa Taasisi katika Utekelezaji wa Majukumu

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kuendeleza watalaam wa Sekta na wa nje ya Sekta kwa kutoa mafunzo ya usimamizi na ufuatiliaji wa miradi ya TEHAMA na matumizi ya teknolojia mpya zinazoibukia kwenye sekta nyinginezo; na kuwajengea uwezo waandishi wa Habari na wahariri wa vyombo vya Habari, kuelimisha umma juu ya teknolojia mpya za kidijitali, kutoa elimu kwa umma kuhusu matumizi salama na yenye tija ya TEHAMA huku wakilinda haki za watoto, wanawake, makundi maalum na vijana. Jumla ya shilingi bilioni 4.5 fedha za ndani zimetengwa.

 

(vii)       Mradi Na. 6226: Kuendeleza Ubunifu na Utengenezaji wa Vifaa vya TEHAMA

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Ujenzi wa vituo vitatu (3) vya kanda vya watengeneza bidhaa za TEHAMA; kuendelea na ujenzi wa kituo cha kuwezesha uanzishwaji wa kampuni changa za TEHAMA (ICT startups) cha Dar es Salaam (Soft center); kuendelea na programu ya mafunzo ya kuendeleza wataalam wa TEHAMA waliosajiliwa; kutengeneza mfumo jumuishi utakaounganisha usajili na uendelezaji wa wataalam na wabunifu TEHAMA; na kufanya tafiti za TEHAMA. Jumla ya shilingi bilioni 3.3 fedha za ndani zimetengwa. 

 

(viii)      Mradi Na. 4292: Ujenzi wa Kituo Kikuu na Vituo vidogo vya  Kuendeleza Ubunifu katika TEHAMA

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kujenga kituo cha Kitaifa cha kuendeleza watalaam, tafiti na ubunifu wa TEHAMA jijini Dodoma; kuanzisha vituo atamizi vya TEHAMA katika vyuo vikuu vya umma na maeneo maalum ya kiuchumi kote nchini; na kujenga uwezo kwa wataalam 40 watakaosimamia programu za  anga juu. Jumla ya shilingi bilioni 8.48 fedha za ndani zimetengwa.

 

(ix)         Mradi Na. 6505: Kufunga Mtambo Mpya wa Kisasa wa Uchapaji   

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kuendelea na ujenzi wa kiwanda cha uchapachaji; kukamilisha ufungaji wa mitambo ya kisasa ya uchapaji; na ununuzi wa vitendea kazi ikiwemo magari kwa ajili ya kuongeza uzalishaji. Jumla ya shilingi bilioni 10.0 fedha za ndani zimetengwa.

 

3.3.2.3. Kuimarisha Miundombinu na Mifumo ya Kitaasisi 

 

A.          Kuimarisha Shughuli za Mfuko wa Bunge

(i)              Mradi Na. 6360: Ujenzi wa Miundombinu ya Bunge:   

Shughuli zitakazotekelezwa ni kuendelea na ujenzi wa nyumba mbili (2) za viongozi  wa Bunge (Kilimani - Dodoma), Kununua na kusimika mitambo ya usalama katika majengo ya Bunge. Jumla ya shilingi bilioni 4.161 fedha za ndani zimetengwa. 

 

(ii)             Mradi Na. 6318: Ukarabati wa Majengo ya Ofisi ya Bunge

Shughuli zitakazotekelezwa ni Kuendelea  na ukarabati wa Ofisi ndogo ya Bunge - Dar es Salaam; Ukarabati wa Jengo la Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa

Kimataifa, Utawala Annex na ununuzi na ufungaji wa mitambo ya vipozeo (chiller na AC) kwa ajili  ya kumbi za  Bunge (ukumbi wa Bunge na Msekwa. Jumla ya shilingi milioni 539 fedha za ndani zimetengwa.

 

(iii)           Mradi Na. 6251: Programu ya Maboresho ya Usimamizi wa Fedha za Umma (PFMRP)  

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kukamilisha ujenzi wa jengo la Hazina ndogo Geita; kuandaa Mwongozo wa Ukusanyaji wa Mapato yasiyo ya Kodi kwenye Mashirika Umma; kufanya utafiti unaolenga kuongeza uhiari wa walipa kodi kwa kutumia nyezo ya sayansi ya tabia za binadamu; kuhuisha Kituo Okozi (Disaster Recovery Site) kwa ajili ya mfumo wa Usimamizi wa Serikali na Kufanya Mapitio ya TEHAMA na Miongozo ya Kitaalamu ya Ukaguzi ili iendane na viwango vya kimataifa hasa AFROSAI-E Standard. Jumla ya shilingi bilioni 12.4 fedha za ndani zimetengwa.

 

B.          Maboresho ya Mahakama

(i)           Mradi Na. 6310: Ujenzi na Ukarabati wa Majengo ya Mahakama za Wilaya

Shughuli zitakazotekelezwa ni: kuendelea na ujenzi wa Mahakama za Wilaya za Korogwe, Kibiti, Mbulu, Simanjiro,Tunduru, Kilosa, Chamwino, Nyasa, Mkalama, Ikungi, Momba, Serengeti, Tarime, Masasi, Ulanga, na Nachingwea; kuanza ujenzi wa  jengo la Mahakama ya ujenzi wa majengo mapya ya Mahakama za wilaya za Serengeti, Biharamuro, Uyui, Kishapu, Muleba, Siha, Tarime, na Rombo; na ukarabati wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu. Jumla ya shilingi bilioni 18.5 fedha za ndani zimetengwa. 

 

(ii)         Mradi Na. 6312: Ujenzi na Ukarabati wa Majengo ya Mahakama za Mwanzo

Shughuli itakayotekelezwa ni kuendelea na ujenzi wa Mahakama za Mwanzo za Kinusi (Mpwapwa), Haubi (Kondoa), Magubike (Morogoro), Kitumbeine (Longido), Machame (Kilimanjaro), Ilangala (Ukerewe), Mbalizi (Mbeya), Nanjilinji (Kilwa) na Mkuyuni (Mwanza). Jumla ya shilingi bilioni 4.6 fedha za ndani zimetengwa.

 

(iii)       Mradi Na. 6327: Ujenzi na Ukarabati wa Majengo ya Serikali 

Nyumba za Majaji na Mahakimu

Shughuli zitakazotekelezwa ni: kukamilisha ujenzi wa nyumba ya Jaji Mkuu; ujenzi wa jengo la ghorofa sita (6) kwa ajili ya makazi ya Majaji jijini Dodoma; na kuanza ujenzi wa Nyumba ya Jaji Kiongozi jijini Dodoma. Jumla ya shilingi billioni 20 za fedha za ndani zimetengwa.

 

(iv)       Mradi Na. 6215: Mradi wa uboreshaji wa huduma za Mahakama (Citizen Centic Judiciary Modernisation Project)

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kuendelea na ujenzi wa Vituo Jumuishi vya utoaji haki tisa (9) katika Mikoa ya Pwani, Manyara, Simiyu, Singida, Songwe, Geita, Lindi, Manyara na Katavi;  na Kuendelea na ujenzi wa Mahakama za Mwanzo 60 katika mikoa mbalimbali. Jumla ya shilingi bilioni 40 fedha za nje zimetengwa.

 

C.          Utawala Bora na Utawala wa Sheria

Kuimarisha utawala wa sheria na utawala bora kwa kuboresha miundombinu na uwezo wa utendaji kazi wa vyombo vinavyosimamia utawala bora na utawala wa sheria.

 

(a)         Mradi Na. 5501: Awamu ya Pili  ya Uimarishaji wa Upatikanaji wa

Haki za Kisheria na Haki za Binadamu Tanzania 

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kukamilisha na kuanza kutekeleza Mpango Kazi wa Pili wa Kitaifa wa Haki za Binadamu; kujenga uwezo kwa Taasisi za Serikali 25 na Asasi Zisizo za Serikali 12 kuhusu uzingatiwaji wa haki na ulinzi wa haki za binadamu; kujenga uwezo kwa Mawakili wa Serikali 58 kuhusu uendeshaji wa mashauri ya Jinai;  na kuandaa Sera na miongozo ya Msaada wa Kisheria; kuwajengea uwezo vyombo chunguzi katika kuratibu na kusimamia uchunguzi wa makosa ya Jinai. Jumla ya shilingi milioni 234.5  fedha za nje zimetengwa.  

 

(b)         Mradi Na. 5502: Kujenga Mfumo Endelevu wa Mpango Kazi wa

Kupambana na Rushwa Tanzania

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kuandaa mapendekezo ya Marekebisho ya Sheria ya Kuwalinda Mashahidi na Watoa Taarifa za uhalifu; kuandaa rufaa za viashiria vya rushwa na kuviwasilisha TAKUKURU; kukamilisha kushughulikia Mashauri 15 ya Rushwa Kubwa katika Mahakama ya Rushwa na Uhujumu Uchumi; na kufanya uratibu wa upatikanaji na urejeshwaji wa mali zilizopatikana kwa njia ya Uhalifu. Jumla ya shilingi bilioni 2.5 fedha za nje zimetengwa. 

 

(c)         Mradi Na. 5507: Upatikanaji wa Haki kwa Wanawake na Watoto wa Kike 

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kufanya maboresho Sheria za Kimila ili kuimarisha haki za wanawake na Watoto wa Kike; kujenga uwezo kwa wadau wa Haki 50 kuhusu shughuli za mahakama na ulinzi wa haki za wanawake na watoto wa kike; kujenga uwezo wa Viongozi wa Serikali za Mitaa 45, jamii 1,000 na watoa huduma ya msaada wa kisheria 38 kuhusu haki za wanawake na watoto wa kike, ukatili na unyanyasaji wa kijinsia; kuandaa Sera na  Miongozo ya kuzingatia katika utoaji haki za watoto wa jinsi zote; kutoa mafunzo kwa wadau wa mahakama 52 kuhusu uendeshaji wa mashauri ya jinai kwa kuzingatia usawa wa kijinsia; kuendelea kuratibu mfumo wa utekelezaji wa masuala ya uzingatiwaji na utoaji wa taarifa zinazohusu viashiria vya usawa wa kijinsia. Jumla ya shilingi milioni 442.7 fedha za ndani na shilingi bilioni 3.9 fedha za nje zimetengwa.. 

 

 

(d)         Mradi Na. 5508: Program ya Upatikanaji Haki kwa Maendeleo Endelevu

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kuboresha maboresho ya kisera na kisheria katika kulinda, kukuza na kuhifadhi haki za binadamu na watu za kiuchumi, kisiasa, kijamii na kimazingira; kuboresha Sheria za Uchaguzi na Demokrasia; kufanya kampeni ya huduma ya msaada wa kisheria ya Mama Samia; kuandaa mwongozo wa kuwalinda mashahidi na wahanga wa uhalifu wa jinai; kuratibu vikao vya kuandaa Sera ya Adhabu; kujenga uwezo wa wadau kuhusu kushugulikia viashiria vya Maafa ya Kimbali; kuandaa miongozo ya Kisera ya upatikanaji haki; na kuandaa kituo cha kushughulia viashiria vya mauaji ya kimbali. Jumla ya shilingi bilioni 2.05 fedha za ndani zimetengwa.  

 

(e)         Mradi Na. 6201: Haki Mtandao 

Shughuli zitakazotekelezwa ni: kufanya mapitio ya Mifumo inayotumika na taasisi za haki Jinai na kuandaa mapendekezo ya kuonanisha ili iweze kusomana; kuanzisha mifumo ya kielektroniki kwa taasisi za Haki Jinai; ununuzi wa vifaa na maboresho ya Mifumo ya TEHAMA kwa Wizara na Taasisi za haki Jinai; kuandaa mfumo wa ufuatiliaji na Tathmini wa Majukumu ya Wizara; kuwajengea uwezo watumishi 105 wa Wizara kuhusu mifumo iliyopo Wizarani; na kutoa elimu kwa umma kuhusu mifumo inayotumiwa na Wizara na Taasisi za haki Jinai katika utoaji wa huduma kimtandao. Jumla ya shilingi bilioni 2.6 fedha za ndani zimetengwa. 

 

(f)          Mradi Na. 6207: Kuboresha Uwajibikaji wa Kitaasisi katika Kupambana na Rushwa na Kuongeza Wigo wa Upatikanaji wa Haki 

Shughuli zitakazotekelezwa ni: kuendesha mashauri 58 ya Jinai yanayowahusu Watoto Wanaokinzana na Sheria (pro bono services); kutoa mafunzo kwa kamati za Msaada wa Kisheria Katika Ngazi za Wilaya 85; kuendelea kutoa mafunzo mbalimbali kwa watoa Huduma ya Msaada wa Kisheria kuhusu utekelezaji wa Sheria ya Msaada wa Kisheria na kanuni zake; na kutoa mafunzo kwa viongozi wa kimila 32 na kidini 25 kuhusu haki za watoto, wanawake na Watu Wenye Mahitaji Maalum; na kufanya utafiti na tathmini ya hali ya Upatikanaji wa Msaada wa Kisheria na mchango wa afua za Mradi kwa miaka minne. Jumla ya shilingi bilioni 2.04 fedha za nje zimetengwa.  

 

(g)         Mradi Na. 6517: Kuimarisha Haki za Mtoto 

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kuanza programu ya Pili ya Usajili wa Matukio Muhimu ya Binadamu Tanzania; na kuendelea kuratibu na kusimamia utekelezaji wa Mkakati wa Pili wa Haki ya Mtoto wa mwaka 2020/21-2024/25. Jumla ya Shilingi bilioni 3.38 fedha za nje zimetengwa. 

 

 

(h)         Program ya Usimamizi wa Utajiri Asilia na Maliasilia za Nchi Kijamii na Kiuchumi  Tanzania

Shughuli zitakazotekelezwa ni: kuandaa mafunzo ya kuwajengea uwezo Wadau 55 kuhusu Majadiliano ya Mikataba na Utatuzi wa Migogoro kwa Njia Mbadala; kuanzisha mfumo jumuishi wa uangalizi wa utajiri na maliasilia za nchi; kuanzisha kituo cha Kitaifa cha Utatuzi wa Migogoro; na kuandaa na kusambaza mwongozo wa usimamizi wa Utajiri na Maliasilia za nchi. Jumla ya Shilingi milioni 234.5 fedha za nje zimetengwa..

 

(i)           Mradi Na. 6501: Vitambulisho vya Taifa 

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kuendelea na usajili na utambuzi wa watu 1,597,827 katika Mikoa na Wilaya zote Tanzania Bara na Zanzibar; kuzalisha na kugawa Vitambulisho vya Taifa milioni 10; kuunganisha taasisi 15 za Serikali na binafsi katika Mfumo (Kanzidata) na kuboresha huduma kwa wadau waliounganishwa katika Kanzidata; ununuzi wa kadighafi milioni mbili (2) na malighafi za kuzalisha Vitambulisho vya Taifa; kuunganisha  Ofisi 11 za Usajili za Wilaya na Makao Makuu na mkongo wa Taifa; kuunda mifumo (modules) 11 kwa ajili ya shughuli za usajili na utambuzi; na kufungamanisha kitambulisho cha Taifa na taarifa za mifumo mengine. Jumla ya shilingi bilioni 36.4 fedha za ndani na Shilingi bilioni 4.69 fedha za nje zimetengwa.

 

(j)          Mradi Na. 6209: Mfuko wa Kuchochea Maendeleo ya Jimbo

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kuendelea kuchochea maendeleo ya wananchi kwa kuchangia fedha katika miradi inayotekelezwa katika majimbo kupitia mfuko wa maendeleo ya Jimbo. Jumla ya shilingi bilioni 15.99 fedha za ndani zimetengwa.

 

(k)         Mradi Na. 6389: Ujenzi wa Majengo ya Ofisi

(i)             Ujenzi wa Makao Makuu ya Mahakama Dodoma

Shughuli itakayotekelezwa ni kukamilisha ujenzi wa jengo la Makao Makuu ya Mahakama ya Tanzania jijini Dodoma.

 

(ii)           Ujenzi wa Vituo Jumuishi vya Taasisi za Sheria

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kuanza ujenzi wa vituo 10 jumuishi vya Taasisi ya Sheria katika ngazi ya Mikoa na 20 katika ngazi ya Wilaya; na kuwajengea uwezo wataalamu 32 wa Wizara na Taasisi kuhusu mifumo ya utoaji Huduma katika vituo jumuishi. Jumla ya Shilingi bilioni 10.2 fedha za ndani zimetengwa.

 

(iii)         Ujenzi wa Majengo ya Ofisi ya Mwanasheria Mkuu

Shughuli itakayotekelezwa ni kuendelea na ujenzi wa ofisi za Mwanasheria Mkuu wa Serikali katika mikoa miwili (2) ya Arusha na Mwanza. Jumla ya shilingi bilioni 2.0 fedha za ndani zimetengwa. 

 

(iv)         Ujenzi wa Majengo ya Ofisi ya Taifa ya Mashtaka

Shughuli itakayotekelezwa ni kuendelea na ujenzi wa majengo ya ofisi ya Taifa ya mashtaka katika mikoa sita (6) ya Rukwa, Mwanza, Tanga, Dodoma, Shinyanga na Geita. Jumla ya shilingi bilioni 6.0 fedha za ndani zimetengwa.

 

(v)           Ujenzi wa Majengo ya Serikali 

Shughuli zitakazotekelezwa ni:  Kuendelea na utekelezaji wa Awamu ya Pili ya ujenzi wa Mji wa Serikali Mtumba kwa kukamilisha ujenzi wa majengo ya Ofisi za Wizara na Taasisi; Kukamilisha ujenzi wa miundombinu ya kudumu ya mawasiliano na majitaka; na kusimika kamera za ulinzi. Jumla ya shilingi bilioni 342 fedha za ndani zimetengwa

 

(vi)         Mradi Na. 6339: Ukarabati wa Nyumba za Serikali  

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kuendelea na uboreshaji wa Ikulu ya Chamwino na kuanza ujenzi ukumbi wa madhumuni mbalimbali (multi-purpose hall), ofisi; na kukarabati majengo ya Ikulu Ndogo za Tunguu, Mwanza, Tabora, Shinyanga, Lushoto, Moshi, Arusha na Rest house Zanzibar. Jumla ya shilingi bilioni 11.2 fedha za ndani zimetengwa.

 

(vii)        Ujenzi wa Ofisi na Makazi ya Viongozi katika Mamlaka za Serikali za Mitaa

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kuendelea na ujenzi wa  majengo 71 ya utawala kwenye halmashauri; ununuzi wa samani kwa majengo ya utawala katika Halmashauri 50 yanayotarajiwa kukamilika; na ujenzi wa nyumba za Wakurugenzi 35 na Wakuu wa Idara 25. Jumla ya shilingi bilioni 79.27 fedha za ndani zimetengwa.

 

(viii)      Ujenzi wa Ofisi na Makazi ya Viongozi katika Sekretarieti za Mikoa  Shughuli zitakazotekelezwa ni: Ujenzi, ukamilishaji na ukarabati wa Ofisi za wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya na Maafisa Tarafa; Ujenzi, ukamilishaji na ukarabati wa Nyumba za wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya, Makatibu Tawala wa Mikoa, Makatibu Tawala wasaidizi wa Mikoa na Maafisa Tarafa. Jumla ya shilingi bilioni 28.85 fedha za ndani zimetengwa.

 

Magereza

(a)      Mradi Na. 6103: Mipango ya Ulinzi Magerezani 

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kuweka miundombinu maalum ya usalama na upekuzi katika Magereza matatu (3) ya Lilungu (Mtwara), Lindi (Lindi) na Bukoba (Kagera); kujenga mfumo wa taarifa za wahalifu waliopo magerezani na kuimarisha jukumu la kuwapeleka mahabusu mahakamani katika mikoa minne (4) ya Arusha, Dar es Salaam, Dodoma na Pwani. Jumla ya shilingi bilioni 3.73 fedha za ndani zimetengwa.

(b)      Mradi Na. 6305: Ujenzi na Ukarabati wa Majengo ya Ofisi 

Shughuli zitakazotekelezwa ni: kukamilisha ujenzi wa ukumbi Makao Makuu ya Magereza Msalato Dodoma na viwanja vya michezo Makao Makuu ya Magereza; kuendelea na ujenzi wa Gereza Igunga na kaliua (Tabora), Gairo na Kilosa (Morogoro), Kakonko (Kogoma), Karatu (Arusha), Kwa Mturuki Bagamoyo na gereza maalum Isanga na gereza Msalato (Dodoma) na ukarabati wa Bwalo Kuu la Magereza Ukonga (Dar es Salaam); kuendelea na awamu ya pili ya ujenzi wa hospitali ya Magereza Msalato Dodoma; kuanza ujenzi wa majengo ya kufundishia katika Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji Tanzania (TCTA) Ukonga (Dar es Salaam) na ujenzi wa magereza mapya 12 katika wilaya za Kakonko, Kaliua, Karatu, Msalato, Kilosa, Gairo, Butiamas, Lindi, Mpimbwe, Sengerema, Kyerwa na Mlolo; kuanza ujenzi wa ofisi tano (5) za Wakuu wa Magereza wa Mikoa ya Lindi, Kigoma, Tanga, Songwe na Geita; kuanza ujenzi wa jengo la kuhifadhia nyaraka za Serikali Makao Makuu ya Magereza; kuanza ujenzi wa mifumo ya nishati safi katika magereza 19 ya Arusha (Arusha), Karanga (Kilimanjaro), Maweni (Tanga), Uyui (Tabora), Butimba (Mwanza), Lilungu (Mtwara), Ruanda (Mbeya), Lindi (Lindi), Mbigiri (Morogoro), Ubena (Pwani), Ngara (Kagera), Ukonga, Keko, Segerea, Wazo Hill na Kambi Kimbiji (Dar es Salaam), Isanga, Msalato na King’ang’a (Dodoma; na Kuimarisha matumizi ya nishati jua katika magereza saba (7) ya Lilungu (Mtwara), Isanga na Msalato (Dodoma), Motongo (Simiyu), Mbarali (Mbeya), Kanegele (Geita) na Ngudu (Mwanza). Jumla ya shilingi bilioni 6.12 fedha za ndani zimetengwa.

 

(c)      Mradi Na. 6302: Ujenzi wa Ofisi na Nyumba za Makazi Tanzania Bara Shughuli zitakazotekelezwa ni: kukamilisha ujenzi wa jengo la ghorofa tatu la kuishi familia 12 za Askari Buyekera – Kagera, Ofisi ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara, vituo vya Polisi Daraja “B’’ Bariadi  na Mkuranga, kituo cha Polisi Daraja “C’’ Igoma – Mbeya; jengo la ghorofa la kuishi familia za Askari 12 kambi ya Polisi FFU Dodoma, Rest House ya Polisi Mkoa wa Arusha, jengo la wagonjwa wa nje (OPD) awamu ya pili katika Hospitali ya Polisi Kilwa Road – Dar es Salaam,  na ukuta wa nyumba za Makamishna awamu ya kwanza – Dodoma; kuanza ukarabati wa maghorofa 90 ya kuishi familia za Askari 360 katika Kambi ya Polisi Kilwa Road – Dar es Salaam;  na kuendelea na ujenzi wa jengo la Kamanda wa Polisi Mtwara, kituo cha Polisi Daraja “B” Namtumbo, jengo la RPC Rufiji, bweni la wanafunzi Kidatu, kituo cha Polisi Daraja “C” Kitangari - Newala;  kituo cha Polisi Daraja “B” Misungwi – Mwanza; Kituo cha Polisi Daraja “B” Chang’ombe – Dodoma.  Jumla ya shilingi bilioni

25.54 fedha za ndani na Shilingi milioni 100 fedha za nje zimetengwa

 

(d)      Mradi Na. 6303: Ujenzi wa Ofisi na Nyumba za Makazi Zanzibar

Shughuli zitakazotekelezwa ni: kukamilisha ujenzi wa nyumba 3 za kuishi familia 6 za Askari Tunguu – Kusini Unguja; jengo la Maktaba Chuo cha Polisi Zanzibar, majengo mawili (2) ya ghorofa moja (1) la kuishi askari familia sita (6) na nyumba mbili (2) za kuishi familia za Askari 12 Makunduchi - Kusini Unguja, majengo matatu (3) ya ghorofa moja (1) ya kuishi familia za Askari 12 Wete - Kaskazini Pemba, nyumba saba (7) za makazi ya familia 14 za Askari Polisi Finya – Kusini Pemba, nyumba tano (5) za makazi ya familia 20 za Askari Polisi eneo la Mfikiwa – Kaskazini Pemba na jengo la ghorofa mbili (2) za kuishi familia za Askari 8 Kambi ya Polisi Ziwani - Mjini Magharibi; kuendelea na ukarabati Ofisi ya FFU Kambi ya Polisi Ziwani - Mjini Magharibi, Kituo cha Polisi Daraja “B” Malindi - Mjini Magharibi, kituo cha Polisi 65 Micheweni – Zanzibar na Makao Makuu ya Polisi Zanzibar. Jumla ya shilingi bilioni

1.55 fedha za ndani zimetengwa

 

Huduma za Zimamoto na Uokoaji

 

(i) Mradi Na. 6582: Upanuzi wa Huduma za Zimamoto

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kununua magari matano (5) ya Kuzima moto na Maokozi nchini kwa ajili ya mikoa ya Simiyu, Manyara, Njombe, Songwe na Katavi; kukarabati nyumba 10 za makazi ya askari katika mikoa ya Arusha, Morogoro na Iringa, kununua vifaa vya kuzima moto na uokoaji, kuendeleza ujenzi wa majengo mawili (2) ya ghorofa Kikombo Dodoma, kujenga vyumba vitano (5) vya kuhifadhia silaha katika mikoa ya Kilimanjaro, Rukwa, Mtwara, Kigoma na Shinyanga, kuendelea na ujenzi wa vituo  vinne (4) vya zimamoto na uokoaji katika mikoa ya, Kagera, Katavi, Geita na Njombe, kuendelea na ujenzi wa miundombinu katika Chuo cha Zimamoto na Uokoaji Chogo – Tanga na ukarabati wa visima vya maji ya kuzima moto (Fire Hydrants) katika mikoa ya Pwani, Iringa, Njombe, Katavi, Mtwara, Kagera, Kilimanjaro, Songwe, Ilala, Morogoro na Dodoma. Jumla ya shilingi bilioni 9.93 fedha za ndani zimetengwa.

 

Uhamiaji

 

Mradi Na. 6301: Ujenzi wa Ofisi za Mikoa za Uhamiaji

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kukamilisha ujenzi wa Ofisi ya Uhamiaji Mkoa wa Mtwara; kuanza ujenzi wa ofisi za uhamiaji katika mkoa wa Songwe, ofisi za uhamiaji katika Wilaya ya Mufindi na ujenzi wa Ofisi za uhamiaji katika kituo cha mpakanicha  Kirongwe mkoani Mara, nyumba 12 kwa ajili ya makazi ya wakufunzi katika Chuo cha Raphael Kubaga – Tanga; Kukamilisha ujenzi wa Ofisi ya Uhamiaji Wilaya ya Chato; kuanza ukarabati wa nyumba 12 za watumishi mkoani Tabora na Ofisi za uhamiaji za Kahama na Ifakara; ununuzi wa magari 23 kwa ajili ya kuimarisha shughuli za misako na doria ya wahamiaji haramu. Jumla ya Shilingi bilioni 8.24 fedha za ndani zimetengwa.

 

 

 

 

D.          Utumishi wa Umma 

 

(a)         Mradi Na. 6284: Programu ya Maboresho katika Utumishi wa Umma Awamu ya Tatu 

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kujenga uwezo wa taasisi za umma kuanza kutekeleza Mfumo Mpya wa Kielektroniki wa Usimamizi wa Utendaji Kazi katika Utumishi wa Umma katika taasisi za umma 215 (wizara 26,sekretarieti za mikoa 26, mashirika na taasisi za umma 70 namamlaka za serikali za mitaa 93); Kuendelea kusimamia na kuboresha mifumo ya PEPMIS, PIPMIS, HR Assessment, e-HRP, na Watumishi Portal ili kuendana na mahitaji ya watumiaji na mabadiliko ya teknolojia; kujenga toleo la aplikesheni ya simu za mkononi kwa ajili ya mifumo ya PEPMIS, PIPMIS na Watumishi Portal. Jumla ya shilingi bilioni 8.57 fedha za ndani na shilingi milioni 117.3 fedha za nje zimetengwa.

 

(b)         Mradi Na. 6315: Ujenzi wa Makazi ya Viongozi Wakuu Wastaafu wa

Kitaifa 

Shughuli zitakazotekelezwa ni: kukamilisha nyumba ya Rais wa Awamu ya Tano na kuanza nyumba ya Rais wa Awamu ya Sita; na kuendelea na ujenzi wa Klabu ya Viongozi. Jumla ya shilingi bilioni 3.3 fedha za ndani zimetengwa. 

(c)         Mradi Na. 6282: Mfumo Mpya wa Kielektroniki wa Taarifa za Kiutumishi na Malipo ya Mishahara - Home Grown HCMIS 

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kuwezesha taasisi 50 kutumia Mfumo wa HCMIS na kufanyaufuatiliaji na tathmini kwa Taasisi zilizoingizwa katika Mfumo; Kutoa mafunzo ya matumizi ya Mfumo wa Taarifa za Kiutumishi na Mishahara (HCMIS) kwa watumishi 640 kwa ngazi tofauti ilikuwajengea uwezo wa kutoa huduma bora. Jumla ya shilingi milioni 200 fedha za ndani zimetengwa.

 

3.3.3. Kuimarisha Uwezo wa Uzalishaji Viwandani na Utoaji Huduma

 

3.3.3.1. Uzalishaji Viwandani

 

(a)         Mradi Na. 6103: Kuboresha Kituo cha Kuendeleza Teknolojia ya Magari Tanzania - TATC

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kuendelea na ununuzi wa mashine na mitambo pamoja na kukarabati mashine, mitambo na majengo kwa ajili ya utafiti na uhawilishaji wa teknolojia; kuanzisha Karakana Kuu ya Kukalibu Chuma (Heavy Duty Foundry); kuanzisha kiwanda cha kuunda magari (Nyumbu Brand) na magari ya kuzima moto (Fire Fighting Vehicles) chenye uwezo wa kuunda magari sita (6) hadi kumi (10) kwa mwaka; kuendeleza wataalamu 37 katika fani za uhandisi wa magari na mitambo, mipango, ufundi stadi, masoko, TEHAMA, na ugavi; na kuendeleza utafiti na uhawilishaji wa teknolojia wa zana na vifaa mbalimbali, magari na mitambo. Jumla ya shilingi bilioni 15.375 fedha za ndani zimetengwa.

 

(b)         Mradi Na. 1214: Kuendeleza Programu ya Maendeleo ya Viwanda - PCP 

Shughuli zitakazotekelezwa ni: kuratibu utekelezaji wa programu ya PCP chini ya UNIDO; kuwezesha uanzishaji wa mfuko wa pamoja (Backet fund)  kwa ajili ya maendeleo ya viwanda; kuandaa Mpango kabambe na kutambua maeneo/ardhi kwa ajili ya uwekezaji katika viwanda na fursa za kibiashara; kukamilisha Sera ya Maendeleo Endelevu ya Viwanda(SIDP); kufanya utafiti wa changamoto za  uwekezaji wa ndani katika sekta zote; kufanya uchambuzi wa kiintelijensia ya masoko na mnyororo wa thamani kwa bidhaa muhimu kwa soko la  ndani na nje ya nchi; kufanya sensa ya viwanda na kufanya tathmini ya kisekta ya mnyororo wa thamani kwa ajili ya ushindani wa viwanda katika chuma na bidhaa za chuma, soap na detergent. Jumla ya shilingi bilioni 1.1 fedha za ndani zimetengwa.

 

(c)         Mradi Na. 4486: Uzalishaji Viwandani kupitia Programu ya Kuendeleza Sekta ya Kilimo Awamu ya Pili (ASDP II)

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kufanya utafiti wa kina katika Sekta Ndogo za Pamba, Mafuta, Kahawa, Sukari, Korosho, vinywaji na Vifungashio; kubainisha na kufanya tathmini ya miundombinu ya masoko iliyopo nchini na matumizi yake; kuandaa kanzi data ya biashara za ndani, kikanda na biashara za kimataifa; Kuwezesha mapitio ya mikakati midogo ya Kisekta (Alizeti na Ngozi); kutambua na kujifunza mahitaji ya  Masoko ya Kikanda ikiwemo  EAC, SADC na AfCFTA na kusambaza kwa wazalishaji/ makampuni ya ndani; kufanya tathmini ya hali na mchango  wa Sekta Binafsi nchini na Kuandaa Sera ya Maendeleo ya Sekta Binafsi na Mkakati wake; na kuimarisha Mfumo wa Taarifa za Masoko ya mazao, mifugo, samaki na bidhaa nyingine. Jumla ya shilingi bilioni 2.0 fedha za ndani zimetengwa.

 

(d)         Kuendelea Kueneza Dhana ya KAIZEN Nchini

Shughuli zitakazotekelezwa ni:  Kuendelea kueneza falsafa ya Kaizen kwenye mikoa saba (7) ambayo bado haijapata mafunzo; kuandaa mashindano ya Kaizen kuanzia kwenye mikoa hadi kimataifa kwa wenye viwanda; kushiriki kwenye mafunzo ya Kaizen ndani na nje ya nchi; kushiriki kwenye Maonesho mbalimbali kwa lengo la kueneza falsafa ya Kaizen kwa jamii; kutoa mafunzo kwa vitendo ya dhana ya Kaizen kwenye viwanda; na kuendelea kuvisimamia viwanda ambavyo vimeshapata mafunzo ya Kaizen ili kuendelea kutekeleza dhana hiyo. Jumla ya shilingi milioni 200.00 fedha za ndani zimetengwa.

 

(e)         Mradi Na. 6260: Miradi ya Kusaidia Taasisi

 

(i)            Kiwanda cha Mashine na Vipuri KMTC  

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kununua na kufanya ukarabati wa mashine; kufanya uzalishaji wa mashine na vipuri; na kufanya ukarabati wa majengo matano (5).

Jumla ya shilingi bilioni 1.6 fedha za ndani zimetengwa.

 

(ii)           Eneo la Kongano ya Viwanda – TAMCO – Eneo la viwanda

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kujenga mita 300 za barabara katika eneo la mradi. Jumla ya shilingi bilioni 1.5 fedha za ndani  zimetengwa. 

 

(iii)         Mradi wa Makaa ya Mawe Katewaka

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kufanya majadiliano na mwekezaji na kusaini mkataba wa ubia (JV Agreement); na kulipa leseni za uchimbaji. Jumla ya shilingi milioni 320.69 fedha za ndani zimetengwa.

 

(iv)         Mradi wa Maganga Matitu Sponge Iron

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kukamilisha majadiliano na mwekezaji na kusaini mkataba wa ubia (JV Agreement); na kulipa leseni za uchimbaji. Jumla ya shilingi milioni 238.41 fedha za ndani zimetengwa.

 

(v)           Mradi wa Maka ya Mawe Mhukuru

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kufanya utafiti wa kina wa kijiolojia (geological study); na kulipa leseni za uchimbaji. Jumla ya shilingi bilioni 1.17 fedha za ndani zimetengwa.

 

(vi)         Mradi wa Kiwanda cha Viuadudu (TBPL) 

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kufanya ithibati ya bidhaa za viuadudu na Kiwanda (Pre-qualification); kufanya stadi ya uzalishaji wa mbolea za kibailojia (biofertilizer), na masoko ya viwatilifu vya kibailojia (biopesticides); kuratibu utiaji wa saini mkataba wa manunuzi wa dawa za viuadudu (offtake agreement). Jumla ya shilingi milioni 300 fedha za ndani zimetengwa.

 

(vii)       Kiwanda cha Mang’ula

Shughuli zitakazotekelezwa ni: kufanya Ukarabati wa majengo; kuoneshe mipaka ya eneo la kiwanda na kumtafuta mwekezaji. Jumla ya shilingi milioni 200 fedha za ndani zimetengwa.

 

(viii)      Mradi wa Edible Oil Project ( Palm Oil at Kigoma)

Shughuli zitakazotekelezwa ni: kufanya maandalizi ya awali ya mradi wa mafuta ya kula (edible oil). Jumla ya shilingi milioni 200 fedha za ndani zimetengwa.

 

(ix)         Kituo cha Zana za Kilimo na Ufundi Vijijini - CAMARTEC 

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kufanya utafiti kwa kushirikiana na Taasisi nyingine ili kubaini mahitaji ya teknolojia ya kutenganisha maganda na kiini cha mbegu ya katika Wilaya ya Buhigwe Mkoa wa  Kigoma na Wilaya ya Kyela Mkoa wa Mbeya; kuboresha mashine ya kuvuna chikichi na kufanya majaribio katika Mkoa wa Kigoma; kuimarisha kiwanda darasa cha kubangua korosho katika Wilaya ya Manyoni – Singida, kitovu cha Teknolojia za Kihandisi (KITEKI) wilaya ya  Karatu – Arusha na Maswa - Simiyu; kutengeneza mashine za kubangua korosho kwa ajili ya majaribio ya kuanzisha kiwanda darasa mkoani Mtwara; kuboresha  miundombinu ya eneo la maonesho (ShowGround); ununuzi wa mashine na mitambo ya Karakana na upanunuzi wa karakana iliyoko Makao Makuu (Arusha) na katika Tawi la Nzega (Tabora). Jumla ya shilingi bilioni 1.5 fedha za ndani zimetengwa.

 

(x)           Shirika la Utafiti na Maendeleo ya Viwanda Tanzania - TIRDO 

Shughuli zitakazotekelezwa ni: kufanya mafunzo kwa wataalam na  ununuzi wa vifaa vya upimaji ubora wa mabomba ya mafuta na gesi (Non-Destructive Testing - NDT);  kukamilisha mchakato wa ithibati (Accreditation) na kuboresha maabara ya chakula, mazingira, na vifaa; Kufanya utafiti katika kanda ya ziwa ili kubaini fursa za uwekezaji na maeneo yenye viwanda na rasilimali zilizopo (Industrial Mapping); na kukamilisha ujenzi wa Jengo la Utawala ili kutoa nafasi ya kuanzisha Kituo cha Taarifa za Viwanda na Ubashari wa Teknolojia na Viatamizi kwa wabunifu wa teknolojia. Jumla ya shilingi bilioni 1.5 fedha za ndani zimetengwa. 

 

(xi)         Shirika la Uhandisi na Usanifu wa Mitambo – TEMDO

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kuendeleza na kuhawilisha teknolojia ya mtambo mdogo wa kuchakata miwa na kutengeneza sukari na kukamua mafuta ya alizeti; kuboresha karakana kwa kusimika mashine na vifaa vya kisasa (Heavy duty 6-axes CNC Machines) pamoja na miundombinu; kusanifu na kuendeleza utengenezaji wa vifaa tiba vya hospitali kwa awamu ya III (Autoclave and Laundry machines); na kuendeleza mtambo wa kuteketeza taka ngumu za hospitali mahsusi kwa kuchomea damu isiyofaa, mabaki ya wanyama, na dawa zilizoharibika na kupitwa na muda (incinerating carcass from livestock/cattle abattoir, biomedical waste blood and expired drugs) katika Sekta ya Afya. Jumla ya shilingi bilioni 1.7 fedha za ndani zimetengwa.

 

(xii)       Uendelezaji wa Viwanda Vidogo - SIDO

Shughuli zitakazotekelezwa ni: kujenga Majengo ya Viwanda katika mikoa ya Kigoma, Simiyu na Dodoma; Kununua magari matano (5) kwa ajili ya uendeshaji wa shughuli za  Shirika; kutengeneza Mfumo Mtandao wa Mawasiliano ya Ndani  (LAN) kati Ofisi za mikoa za SIDO; kuimarisha miundombinu ya viwanda kwa kukarabati majengo, barabara, Mifumo ya maji, kujenga uzio katika Mitaa ya Viwanda; kuimarisha Mfuko wa NEDF ili  kuongeza utoaji wa mikopo kwa wajasiriamali na kuunganisha Mfumo wa Mtandao wa Mawasiliano wa Ofisi za Mikoa ya Manyara, Pwani, Simiyu, Katavi na Songwe kwenye Mkongo wa Taifa na SIDO makao makuu. Jumla ya shilingi bilioni 3.14 fedha za ndani zimetengwa.

 

 

(xiii)      Baraza la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi – NEEC

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kuwezesha upatikanaji  kiwanja na hati ya kumiliki ardhi kwa ajili ya  Ujenzi wa Jengo la Ofisi ya NEEC na kuanza kwa hatua za awali za ujenzi; Kubuni, kuanzisha na kujenga  Mfumo wa kielektroniki wa kuratibu, kufuatiliaji na kutathimini  ushiriki wa watanzania katika: uwekezaji; Mifuko na program za Uwezeshaji wananchi Kiuchumi (Economic Empowerment Funds and programs); na  kuanzisha Kanzidata (National Economic Empowerment Database). Jumla ya shilingi milioni 500 fedha za ndani zimetengwa. 

 

(xiv)      Kuendeleza Biashara Kupitia Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE)

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Ujenzi wa jengo jipya la ghorofa kumi (10) la Vipimo na Viwango katika Kampasi ya Dar es Salaam; Ujenzi wa Hosteli za wanafunzi wa kike eneo la Iganzo Kampasi ya Mbeya; Kuboresha miundombinu ya TEHAMA; Kuendeleza rasilimali watu kwa masomo ya muda mrefu; na Ujenzi wa jengo la ghorofa nne (4) kwa ajili ya kujifunzia na kufundishia katika Kampasi ya Dodoma. Jumla ya shilingi bilioni 8.32 fedha za ndani zimetengwa.

 

(f)         Mradi Na. 4933: Uendelezaji wa Kanda Maalumu za Kiuchumi

 

Eneo Maalum la Uwekezaji Tanga 

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kupima na kuweka mipaka kwa ajili ya umilikishwaji; kufanya upembuzi yakinifu; kuandaa mpango kabambe wa uendelezaji katika eneo lililolipiwa fidia la Tanga SEZ. Jumla ya shilingi milioni 100 fedha za ndani zimetengwa.

 

Eneo la Maalum la Uwekezaji Kigoma

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kufanya usanifu wa miundombinu, kuanza ujenzi wa miundombinu ya msingi; na kuendelea na programu za uhamasishaji wa kuvutia wawekezaji. 

 

Eneo Maalum la Uwekezaji Kahama

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kupata hati miliki na kukamilisha ulipwaji wa fidia kwa wananchi waliopisha mradi; kuanza maandalizi ya Upembuzi yakinifu na Mpango Kabambe (Master Plan); kufanya tathmini ya kimkakati ya mazingira (SEA), usanifu wa miundombinu na kuendelea na ujenzi wa miundombinu wezeshi. 

 

Eneo Maalum la Uwekezaji Bunda

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kuandaa upembuzi yakinifu. Jumla ya shilingi milioni 100 fedha za ndani zimetengwa.

 

Eneo Maalum la Uwekezaji Songwe

Shughuli zitakazotekelezwa ni: kuendelea na taratibu za kupata hati miliki; kuanza maandalizi ya Upembuzi yakinifu na Mpango Kabambe (Master plan); na kufanya Tathmini ya kimkakati ya mazingira (SEA) na Usanifu wa Kina wa miundombinu wezeshi. 

 

Eneo Maalum la Uwekezaji Manyara

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kufanya Usanifu wa Kina wa miundombinu ya wezeshi.  

 

Eneo Maalum la Uwekezaji Mtwara Free Port Zone

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kuendelea na ujenzi wa miundombinu wezeshi ili kuhamasisha uwekezaji katika eneo la Bandari huru (Free Port Zone) hususani kwa makampuni ya Mafuta na Gesi.

 

3.3.3.2. Kilimo, Mifugo na Uvuvi

 

A.          Kilimo

(a)           Mradi Na. 4486: Programu ya Kuendeleza Sekta ya Kilimo Awamu ya

Pili - ASDP II

 

(i)            Kuimarisha miundombinu ya utafiti na kufanya tafiti zitakazozingatia ugunduzi wa aina za mbegu bora na mbinu bora za kilimo

Shughuli zitakazotekelezwa ni: kufanya utafiti wa mbegu aina 10 za  mazao ya kimkakati ya nafaka, jamiii ya mikunde na mafuta; kutafiti na kupendekeza teknolojia mpya 10 za kanuni bora za kilimo; kutafiti na kupendekeza teknolojia tano (5) za kuongeza thamani za mazao; kuzalisha mbegu za awali tani 450 za mazao ya kipaumbele ya mahindi, alizeti, soya, ufuta, ngano, maharage, kunde, mpunga, mtama, choroko, dengu, shayiri na karanga; kusafisha na kuzalisha mbegu za asili tani 10 za mazao ya nafaka, jamii ya mikunde na mbogamboga; kuimarisha vituo vyote vya TARI; kuanza kwa ujenzi wa ghala sita (6) zenye vyumba vya ubaridi katika vituo sita (6) vya TARI zenye uwezo wa kuhifadhi tani 2,490 za mbegu za awali; kukamilisha ujenzi wa ghala tano (5) zenye uwezo wa kuhifadhi jumla ya tani 2,075 katika vituo vitano (5) vya TARI; ujenzi wa maabara mpya ya tissue culture katika kituo cha TARI Maruku kwa ajili ya kuzalisha miche bora ya migomba na ujenzi wa maabara ya utambuzi na udhibiti wa visumbufu vya zao la korosho katika kituo cha TARI Naliendele; ukarabati wa maabara ya bioteknolojia ya TARI Mikocheni; kuendela na ujenzi wa maabara ya kuzalisha miche ya mkonge kwa njia ya chupa (tissue culture) katika kituo cha TARI Mlingano; na kuanza ujenzi wa uzio wa mashamba katika vituo vingine 16 vya TARI na vituo vidogo 18. Jumla ya shilingi bilioni 40.73 fedha za ndani zimetengwa.

 

 

(ii)           Kuimarisha upatikanaji wa pembejeo kupitia mpango wa ruzuku (mbegu, mbolea, viuatilifu) na zana za kilimo

 

(a)         Upatikanaji wa mbegu bora

Shughuli zitakazotekelezwa ni; kuendelea na ujenzi wa miundombinu ya umwagiliaji kufikia hekta 3,304.8; kuendelea na ujenzi wa uzio katika mashamba yote ya mbegu ya ASA; kuendelea na ujenzi wa miundombinu ya kuhifadhia mbegu (ghala) katika mashamba ya Mbozi, Namtumbo, Msungura na Kilangali; ununuzi na ufungaji wa mitambo miwili (2) ya kuchakata mbegu katika mashamba ya mbegu ya Mbozi na Namtumbo; kufungua maeneo mapya katika mashamba ya Mwele, Luhafwe, Msimba, Kilimi, Namtumbo na Mbozi; uzalishaji wa tani 1,500 za mbegu za ngano na tani 400 za mbegu za soya; uzalishaji wa miche ya parachichi 450,000; usambazaji wa tani 5,000 za mbegu bora za alizeti na kuzalisha miche/vikonyo/pingili milioni 37.5 na kusambaza kwa wakulima kwa mpango wa ruzuku. Jumla ya shilingi bilioni

43.03 fedha za ndani zimetengwa.

 

(b)         Upatikanaji wa mbolea

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kuendelea kuratibu upatikanaji wa mbolea nchini kwa kutoa ruzuku ya mbolea  tani 750,000; kuimarisha mfumo wa utoaji wa ruzuku ya mbolea kwa wakulima nchini; kuiwezesha Kampuni ya Mbolea Tanzania (TFC) kununua na kusambaza tani 30,000 za mbolea; kukagua na kuthibiti ubora wa mbolea kwa wafanyabiashara na itatoa mafunzo ya ukaguzi wa mbolea; na kusajili aina mpya za mbolea na visaidizi vyake 85 na kutoa leseni 2,100. Jumla ya shilingi bilioni 170 fedha ndani zimetengwa. 

 

(c)         Upatikanaji wa Viuatilifu

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Ununuzi wa viuatilifu lita 101,000 kwa ajili ya kudhibiti visumbufu vya mazao na mimea mbalimbali ikiwemo parachichi na machungwa; kuvijenga uwezo vituo vya kudhibiti visumbufu vya mazao na mimea ikiwemo KILIMO ANGA na kituo cha kudhibiti panya; kudhibiti ubora wa viuatilifu vinavyozalishwa nchini na vinavyoingizwa kutoka nje ya nchi; na kutoa mafunzo ya matumizi bora na sahihi ya viuatilifu. Jumla ya shilingi bilioni 54.7 fedha za ndani zimetengwa. 

 

(iii)         Kuimarisha kilimo cha umwagiliaji 

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kukamilisha ujenzi wa skimu mpya 25 na ukarabati wa skimu 30 zenye jumla ya hekta 95,005 katika mikoa mbalimbali nchini; kuendelea na ujenzi wa mabwawa 14 yenye mita za ujazo 131,535,000; kukamilisha upembuzi yakinifu na usanifu wa kina wa skimu 30 na mabonde ya kimkakati 22; kufanya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina wa  mabwawa mapya 100; kuanza ujenzi wa mabwawa yenye ujazo wa mita 936,535,700; kuanza ujenzi na ukarabati wa skimu 55 zenye jumla ya hekta 142,662; kuanza ujenzi wa miundombinu ya umwagiliaji katika mabonde 22 ya umwagiliaji yenye ukubwa wa hekta 306,361; ujenzi wa miundombinu ya umwagiliaji katika mashamba makubwa yenye jumla ya hekta 91,371.46 kupitia programu ya BBT katika Mikoa  mitano (5); kufanya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina wa skimu mpya 236 zenye ukubwa wa hekta 415,811 na kufanya mapitio ya upembuzi yakinifu na usanifu wa skimu 255 za kukarabati zenye ukubwa wa hekta 290,095. Jumla ya shilingi bilioni 299.96 fedha za ndani zimetengwa.

 

(iv)         Kuimarisha huduma za ugani na mafunzo

(a)         Kuimarisha Vyuo vya Mafunzo

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Ukarabati na ujenzi wa miundombinu ya Vyuo sita (6) ambavyo ni MATI Uyole, KATRIN, Inyala, Igurusi, Mtwara, Mlingano pamoja na Vituo vinne (4)  vya Mafunzo kwa wakulima vya Bihawana, Mkindo, Themi na Ichenga; kudahili wanafunzi 3,000 katika ngazi ya Astashahada ya Awali, Astashahada na Stashahada za kilimo; na kutoa mafunzo ya kilimo biashara kwa vijana 4,000 kupitia programu ya BBT. Jumla ya shilingi bilioni 3 fedha za ndani zimetengwa.  

 

(b)         Huduma za ugani 

Shughuli zitakazotekelezwa ni; Ununuzi wa magari 55 kwa ajili ya maafisa kilimo na Makatibu Tawala Wasaidizi Mkoa wanaoshughulika na kilimo, visanduku vya ugani 4,000, sare 4,000, soil scanner 45 na vishikwambi 1,500 na kusambaza kwa maafisa ugani; kukarabati Vituo vya Rasilimali za Kilimo (WARCs); ununuzi wa magari matatu (3) ya maabara inayotembea kwa ajili ya kutoa huduma za upimaji wa afya ya udongo; na kuimarisha Mfumo wa M-Kilimo na matumizi ya Kituo cha Huduma kwa Wateja. Jumla ya shilingi bilioni 16 fedha za ndani zimetengwa.

 

(c)         Ujenzi na ukarabati wa miundombinu ya hifadhi ya mazao ya kilimo na kuimarisha usalama wa chakula na lishe

Shughuli itakayotekelezwa ni kukamilisha ujenzi wa ghala 38 zenye uwezo wa kuhifadhi jumla ya tani 33,000 katika Mikoa ya Ruvuma (28), Tabora (6), Geita (1) na Shinyanga (3). Jumla ya shilingi bilioni 22.72 fedha za ndani zimetengwa.  

 

(v)           Kuhamasisha na kuanzisha kilimo cha mashamba makubwa (block farming) na kushirikisha vijana katika kilimo  na kuimarisha upimaji wa afya ya udongo

Shughuli zitakazotekelezwa ni;  Kutambua na kuainisha mashamba mapya 30 yenye ukubwa wa hekta 200,000 za kilimo katika mikoa ya Pwani (hekta 60,000), Morogoro (hekta 50,000), Njombe (hekta 30,000), Songwe (hekta 30,000) na Tanga (hekta 30,000); kuanzishwa kwa Mashamba Makubwa ya Pamoja kwa ajili ya kuwawezesha vijana kushiriki katika kilimo; ulipaji wa fidia kwa wamiliki wa ardhi yenye ukubwa wa hekta 370,100 katika Mikoa 14; na kuwajengea uwezo na kuwapatia maeneo ya uzalishaji yenye miundombinu ya umwagiliaji na mitaji kwa vijana na wanawake. Jumla ya shilingi bilioni 14.16 fedha za ndani zimetengwa. 

 

(vi)         Kuimarisha upatikanaji wa masoko ya mazao ya kilimo ndani na nje ya nchi

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kuendelea na  ujenzi wa masoko matano (5) ya kimkakati yaliyokuwa chini ya mradi wa DASIP yaliyopo katika Halmashauri za Kahama MC (1), Ngara (1), Kyerwa (2) na Tarime (1); kuanza kwa ujenzi wa market sheds tatu (3); kuimarisha Mamlaka ya Udhibiti wa Nafaka na Mazao Mchanganyiko (COPRA); ununuzi wa tani 113,435 za mazao ya mahindi, mpunga, alizeti na mtama mweupe kupitia CPB ; ununuzi  na uhifadhi wa mahindi tani 92,500, mpunga tani 6,500 na mtama tani 1,000 kupita NFRA; kuanza kwa ujenzi wa Vituo Jumuishi (common use facilities) vya kukusanya, kuchambua, kupanga madaraja, kufungasha na kusafirisha mazao ya bustani katika Mikoa ya Iringa, Kilimanjaro na Dar es Salaam; na kuanza kwa ujenzi wa kiwanda na kusimika mitambo ya kusindika zabibu ghafi katika Halmashauri ya Jiji – Dodoma. Jumla ya shilingi bilioni 30.27 fedha za ndani zimetengwa.  

 

(vii)       Kuimarisha ushirika 

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kutoa mafunzo ya usimamizi wa Mfumo wa MUVU kwa Vyama vya Ushirika 7,300; kusimamia na kudhibiti Vyama vya Ushirika kwa kukagua vyama 7,300; kutoa Mafunzo kwa vikundi 113 vya mbogamboga;  kukagua Vyama 5,000 vya Ushirika; kuratibu ufufuaji wa vinu vya kuchakata pamba vya Sola, Mugango, Buyagu (Sengerema) na Manawa vilivyopo katika Mikoa ya Simiyu, Mara na Mwanza, mtawalia; ukarabati wa ofisi za COASCO; kuratibu uanzishwaji wa Kiwanda cha kubangua korosho kinachojengwa na TANECU Ltd na Kiwanda cha vifungashio kinachojengwa na SONAMCU Ltd; ukarabati wa Ofisi za Shirika la Ukaguzi wa Vyama Ushirika (COASCO)  katika mikoa ya Dodoma, Iringa, Shinyanga na Dar es Salaam; na ujenzi wa Ofisi katika Mkoa wa Ruvuma.  Jumla ya shilingi bilioni 1 fedha za ndani na shilingi bilioni 1.172 fedha za nje zimetengwa. 

 

(b)         Mradi Na. 4499 Kudhibiti Sumukuvu 

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kukamilisha ujenzi wa Kituo cha Taifa cha Udhibiti wa Kibaiolojia – Kibaha na Kituo Mahili Baada Mavuno (Post Harvest Centre of Excellence) Kongwa - Dodoma; kukamilisha ujenzi wa ghala 14 zenye uwezo wa kuhifadhi tani 21,500 katika Wilaya za Gairo, Chemba, Kiteto, Babati, Itilima, Buchosa, Bukombe, Kibondo, Kasulu, Nzega, Namtumbo, Nanyumbu, Unguja na Pemba;  kuendelea na ujenzi wa Maabara Kuu ya Kilimo; na kutoa mafunzo kuhusu uzalishaji na uhifadhi bora wa mazao ya mahindi na karanga kwa viongozi, waandishi wa habari, wakulima na wasafirishaji wa mazao. Jumla ya shilingi milioni 300.0 fedha za ndani na shilingi bilioni 33.65 fedha za nje zimetengwa 

 

(c)         Mradi Na. 4497 Kuongeza Uhifadhi wa Taifa 

Shughuli itakayotekelezwa ni kukamilisha ujenzi wa vihenge 36 vya kisasa  na ghala tano (5) zenye uwezo wa kuhifadhi jumla ya tani 506,000 katika vituo vya Makambako, Mbozi, Songea, Shinyanga na Dodoma. Jumla ya shilingi milioni 700 fedha za ndani na shilingi bilioni 10 fedha za nje zimetengwa. 

 

(d)         Mradi Na. 4427 Kuendeleza Kilimo na Uvuvi – AFDP

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Ujenzi wa miundombinu ya umwagiliaji katika hekta 198 za mashamba ya  Msimba na Kilimi; ujenzi wa ghala moja (1) la kuhifadhi mbegu, ofisi, jengo la kufundishia wakulima na nyumba 4 za watumishi  katika shamba la Kilimi; ukarabati wa nyumba tano (5) za watumishi na karakana moja (1) katika shamba la Msimba; ukarabati na ununuzi wa vifaa vya maabara ya mbegu katika mkoa wa Arusha; kutoa mafunzo kwa wakaguzi 50 wa mbegu katika ngazi ya wilaya; kuimarisha matumizi ya lebo za kielektroniki na ukaguzi ili kudhibiti uuzaji wa mbegu feki. Jumla ya shilingi bilioni 18.34 fedha za nje zimetengwa.

 

B.          Mifugo

 

(a)           Mradi Na. 4486: Programu ya Kuendeleza Sekta ya Kilimo Awamu ya

Pili (ASDP II)

 

(i)            Kuimarisha upatikanaji wa mbegu bora za mifugo

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kuhimilisha ng’ombe 100,000 katika mikoa 26; kuimarisha Mashamba matano (5) ya Serikali kwa kuyapatia vitendea kazi vikiwemo pikipiki 10 na kununua ng’ombe wazazi 1,200 kwa ajili ya mashamba ya Serikali ya kuzalisha Mitamba; kuzalisha dozi 1,500,000 za mbegu bora za mifugo katika kituo cha NAIC; kuongeza mitamba 1,200 katika mashamba ya Nangaramo na Ngerengere; kukarabati nyumba 20 za watumishi katika mashamba na Kituo cha Taifa cha Uhimilishaji; kununua madume bora ya mbegu 200 ya ng’ombe aina ya Borani na kuyasambaza kwa wafugaji; na kusanifu na kuendeleza mfumo wa kitaifa wa uhimilishaji kwa lengo la upatikanaji na ufuatiliaji wa taarifa za ng’ombe wanaohimilishwa. Jumla ya shilingi bilioni 6.3  fedha za ndani zimetengwa. 

 

(ii)           Kuimarisha Huduma za Maji, Malisho na Vyakula vya Mifugo

Shughuli zitakazotekelezwa ni: kujenga mabwawa matano (5), kuchimba visima virefu sita (6), kuanzisha Mashamba Darasa 150 ya Malisho yenye ukubwa wa ekari tano (5) kila moja katika Mamlaka za Serikali za Mitaa na Taasisi za Serikali; kutoa mafunzo kwa wakaguzi 100 wa maeneo ya malisho na rasilimali za vyakula vya mifugo; kuimarisha mashamba ya Vikuge (Kibaha) na Langwira (Mbarali) yanayozalisha mbegu na malisho kwa kuyapatia vitendea kazi vikiwemo matrekta manne (4); mower mbili (2); hei 59 bailer mbili (2); hay rake mbili (2); forage hervester mbili (2) na forage bailer mbili (2); kuchimba visima virefu vya maji vitatu

(3) na kuweka mfumo wa umwagiliaji; kuzalisha marobota ya hei 200,198 na mbegu za malisho tani 32.08; kuwezesha uzalishaji wa malisho aina ya Napier (Juncao) katika mikoa ya Dodoma, Iringa, Kagera, Katavi, Kigoma, Mbeya, Mtwara, Mwanza na Pwani;  kujenga maghala 15 ya kuhifadhia rasilimali za malisho na vyakula vya mifugo. Jumla ya shilingi bilioni 9.3 fedha za ndani na shilingi bilioni 4.1 fedha za nje zimetengwa.

 

(iii)         Kuimarisha Afya ya Mifugo

Shughuli zitakazotekelezwa ni: kujenga maabara ya virusi na kusimika mitambo ili kuzalisha aina 13 ya chanjo za kipaumbele; kuchanja mifugo 108,000,000 dhidi ya magonjwa mbalimbali; kununua dawa za kuogeshea mifugo lita 56,000; kujenga majosho 246; kukarabati miundombinu ya Kituo cha Karantini cha Kwala ili kuwezesha biashara za kimataifa na na kuwezesha kuongeza udhibiti wa ubora wa viuatilifu vya mifugo kwa kupima, kusajili na ufuatiliaji wake. Jumla ya shilingi bilioni 11.6 fedha za ndani zimetengwa. 

 

(iv)         Kuboresha Huduma za Ugani

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kununua pikipiki 1,200 na magari 3, zana za huduma za veterinari (vet kit) 1,100 na zana za uhimilishaji (AI Kit) katika Mamlaka za Serikali za Mitaa 184; kuwezesha upatikanaji wa vifaa vya komputa, simu kwa Maafisa Ugani kwa ajili ya huduma za ugani katika Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa na kutoa mafunzo kwa Maafisa Ugani (ToT) 1,000 na kutoa mafunzo kwa wafugaji 100,000 juu ya ufugaji bora wa kibiashara katika Sekretariati za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa;. Jumla ya shilingi bilioni 40.01 fedha za ndani zimetengwa. Jumla ya shilingi bilioni 9.2 fedha za ndani zimetengwa.

 

(v)           Kuimarisha Huduma za Utafiti na Mafunzo ya Taaluma za Mifugo

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kuanzisha kituo kipya cha Utafiti wa Mifugo  katika Wilaya ya Nsimbo – Katavi; Kuwezesha Vituo vya Utafiti (TALIRI) kufanya tafiti za mifugo ili kuongeza uzalishaji na tija; kuwezesha mradi wa Maziwa Faida TALIRI Tanga; kuwezesha mradi wa Environment - Cow GHG Emission katika mikoa miwili ya Kilimanjaro na Arusha; kuwezesha mradi wa African Dairy Genetic Gain katika Mikoa saba (7); kujenga jengo la maonesho ya Nanenane katika kiwanja cha John Mwakangale - Mbeya na kuanzisha mashamba darasa 14 ya mifugo katika Mamlaka za Serikali za Mitaa tano (5);   kujenga wa madarasa mawili ya Wakala ya Mafunzo ya Mifugo (LITA)  katika kampasi za Madaba na Buhuri na mabweni mawili katika kampasi za Madaba, Kikulula na Buhuri yenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 100, 100 na 150 mtawalia; kujenga kampasi mpya ya LITA mkoani Songwe; na kujenga miundombinu na kujifunza kupitia mradi wa China-Africa Modern Agricultural Technology Exchange and Training Centre Mkoani Songwe. Jumla ya shilingi bilioni 5 fedha za ndani na shilingi milioni 916.5 fedha za nje zimetengwa.

 

(vi)         Kuwezesha Uongezaji Thamani Mazao ya Mifugo

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kuanzisha vituo atamizi vipya nane (8) vya unenepeshaji wa ng’ombe ili kuongeza maligahafi kwenye viwanda vya kuchakata nyama; kujenga minada ya mifugo mitano (5) ya awali, minne (4) ya Upili  na miwili (2) ya mpakani; kununua nakusimika mizani 70; kujenga miundombinu ya mifugo katika vituo vitatu (3) vya kupumzishia mifugo (Holding Ground) katika vituo vya Kitaraka, Kizota  na Makuyuni; kukarabati Machinjio ya kisasa ya Dodoma; kujenga machinjio ya kisasa ya kuku katika mkoa wa Dodoma; kujenga machinjio ya kisasa ya nguruwe katika mkoa wa Dar es Salaam; kujenga vituo 10 vya kukusanyia maziwa katika mikoa ya Pwani, Iringa, Mbeya, Songwe, Tabora, Mara na Katavi; na kuendeleza programu ya unywaji wa maziwa shuleni kwa kuimarisha mfumo wa upatikanaji wa maziwa na mfumo ukusanyaji taarifa za unywaji maziwa shuleni. Jumla ya shilingi bilioni 17 fedha za ndani na shilingi milioni 290 fedha za nje zimetengwa.

 

(vii)       Kuimarisha Kampuni za Ranchi za Taifa

Shughuli zitakazotekelezwa ni: kuzalisha ndama 5,479 kutokana na majike wazazi 6,849; kuweka uzio wa fensi katika eneo la nyanda za malisho lenye ukubwa wa ekari 2,450 katika ranchi za Kongwa, Mkata, Mzeri, Ruvu na Missenyi; kunenepesha ng’ombe 12,696 katika ranchi za Kongwa, Ruvu na Mzeri; Kujenga ’feedlots unit’’ (3) ‘kwa ajili ya shughuli za unenepeshaji katika ranchi ya Mzeri, Kongwa na Ruvu; kuzalisha marobota ya hei 55,000 katika ranchi ya Kongwa na Mzeri kwenye eneo la Ha.11,000; kuuza madume bora ya ng’ombe aina ya Boran 1,075 kwa wafugaji wa asili kwa ajili ya kuboresha kosaafu ya mifugo yao; kununua madume bora 33 ya ng’ombe aina ya borani kwa ajili ya kuimarisha uzalishaji katika ranchi ya Kalambo; na kutoa mafunzo ya ufugaji bora kwa wafugaji 362 na mafunzo kwa vitendo kwa wanafunzi 500 kutoka katika vyuo mbalimbali nchini. Jumla ya shilingi bilioni 550.8 fedha za ndani zimetengwa.

 

C.          Uvuvi

 

(a)         Mradi Na. 4703: Ufufuaji wa Shirika la Uvuvi Tanzania (TAFICO)

Shughuli zitakazotekelezwa ni: kukarabati gati la kuegeshea meli (Floating Jetty Ras Mkwavi – Dar es Salaam; kununua magari mawili (2) ya ubaridi na kutoa mafunzo kwa Mabaharia 126 kuhusu uvuvi wa Bahari Kuu; kujenga ghala la ubaridi, jengo la mtambo wa kuzalisha barafu na jengo la uhandisi wa mitambo ya uvuvi Ras Mkwavi – Dar es Salaam; Kujenga soko la samaki Kigamboni. Jumla ya shilingi bilioni 3.4 zimetengwa.

 

(b)         Mradi Na. 4486: Programu ya Kuendeleza Sekta ya Kilimo (ASDP II)

(i)           Kujenga na Kuimarisha Miundombinu ya Uvuvi (Mialo na Masoko)

Shughuli zitakazotekelezwa ni: kuendelea na ujenzi wa mialo saba (7) ya Igabiro (Bukoba), Chifunfu (Sengerema), Igombe (Ilemela), Kayenze (Ilemela) Chato Beach (Chato), Karungu (Nkasi), na Ng’ombo (Nyasa); kuendelea na ukamilishaji wa ujenzi wa masoko saba ya (7) ya Tunduma (Tunduma), Kyamkwikwi (Muleba), Masuche (Momba), Manda (Ludewa), Nyamikoma (Busega), Zingibari (Mkinga)  na  Kasanga (Kalambo). Jumla ya shilingi bilioni 13.3 zimetengwa. 

 

(ii)         Kuimarisha na Kuendeleza Ulinzi wa Rasilimali za Uvuvi na Mazingira  

Shughuli zitakazotekelezwa ni: kukamilisha ujenzi wa Vituo vitatu (3) vya Ulinzi na Usimamizi wa Rasilimali za Uvuvi vya Sota (Rorya), Busega (Simiyu)  na Nyakaliro (Sengerema); na kujenga miundombinu katika vituo 8 vya Usimamizi Shirikishi wa Rasilimali za Uvuvi vya Kigoma, Tanga, Mtwara, Muleba, Kagera, Mtera, Ikola, na Singida pamoja na kukarabati vituo viwili vya Kipili na Buhingu; kununua boti 10, mizani tano (5), magari sita (6) na pikipiki 20 kwa ajili ya maafisa ugani wanaotoa huduma katika vituo vituo vya Usimamizi wa Rasilimali za Uvuvi. Jumla ya shilingi bilioni 6.67 fedha za ndani zimetengwa. 

 

(iii)       Kujenga na Kukarabati Miundombinu ya Ukuzaji Viumbe Maji

Shughuli zitakazotekelezwa ni:  Kutambua maeneo ya kuweka vizimba; kuwezezesha vituo vitano (5) vya Ukuzaji Viumbe Maji kufanya kazi zake; Kuanzisha Mashamba darasa 20 ya ukuzaji viumbe maji; kuwawezesha wakulima wa mwani kupata pembejeo na zana za ukuzaji viumbe maji bahari; kujenga na kukarabati mabwawa ya ukuzaji viumbe maji  Kingolwira, Mwamapuli na Rubambagwe. Jumla ya shilingi bilioni 17.2 zimetengwa.

 

(iv)       Kuimarisha Wakala wa Elimu na Mafunzo ya Uvuvi (FETA)

Shughuli zitakazotekelezwa ni: kukamilisha ujenzi wa Madarasa mawili katika Kampasi ya Nyegezi. Jumla ya shilingi milioni 200 zimetengwa.  

 

 

(v)         Kuimarisha Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi Tanzania (TAFIRI)

Shughuli zitakazotekelezwa ni: kuendelea na utafiti wa kujua wingi, aina na mtawanyiko wa samaki katika Ziwa Tanganyika. Jumla ya shilingi Milioni 200 zimetengwa.

 

(c)        Programu 4429: Programu ya Kuendeleza Kilimo na Uvuvi

Shughuli zitakazotekelezwa niununuzi wa meli mbili (2) za uvuvi; Kujenga soko la samaki Kipumbwi (Pangani); kukamilisha utambuzi wa maeneo ya kuweka vifaa vya kuvutia samaki (Fish Aggregate Device – FADs) katika pwani ya bahari ya Hindi na ununuzi wa vifaa hivyo; kufunga mitambo minne (4) ya umeme ya kukaushia dagaa katika mikoa ya Tanga, Lindi, Mtwara na Geita; kujenga mabwawa, mfumo wa umeme na maji, kisima cha maji na kununua gari la ubaridi la kusafirisha samaki katika vituo vya ukuzaji viumbe maji vya Kingolwira, Mwamapuli na Rubambagwe.  Jumla ya shilingi bilioni 23.7 fedha nje zimetengwa.

 

3.3.3.3. Uchimbaji wa Madini, Vito vya Thamani na Gesi Asilia

(i)           Mradi Na. 1119: Usimamizi Endelevu wa Rasilimali za Madini (Sustainable Management of Mineral Resources Project - SMMRP Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kukamilisha ujenzi wa Jengo la ofisi ya makao makuu ya Tume ya Madini - Dodoma; kuimarisha miundombinu ya TEHAMA Mirerani; kuanza kwa ujenzi wa ofisi ya afisa madini mkazi - Geita; kuimarisha kanzidata ya miamba; ununuzi wa vifaa vya utafiti wa jiosayansi, vifaa vya maabara na uchunguzi, magari kwa Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST); kuendelea na  ujenzi wa ofisi na maabara ya GST katika Wilaya ya Chunya (Mbeya); na kuanzishwa kwa minada ya madini ya vito na kujenga uwezo wa usimamizi endelevu wa Sekta ya Madini (Capacity building on sustainable management) kwa Tume ya Madini.

 

Aidha, shughuli nyingine zitakazotekelezwa ni ununuzi wa: magari matatu (3) kwa  Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania – GST; mitambo mitano (5) ya uchorongaji kwa ajili ya wachimbaji wadogo; mitambo miwili (2) ya kuzalisha mkaa mbadala (Coal Briquette) kwa ajili ya matumizi ya nishati rafiki ya kupikia; na mtambo wa kuchenjulia madini ya limestone katika  kituo kipya  cha Mfano cha wachimbaji wadogo mkoani Tanga. Jumla ya shilingi bilioni 16.17 fedha za ndani zimetengwa.

 

(ii)         Mradi Na. 1120: Kituo cha Jemolojia Tanzania (Tanzania Geomological Centre -TGC)

Shughuli zitakazotekelezwa  ni: Kuanza ujenzi na upanuzi wa miundombinu ya Kituo cha Jimolojia Tanzania; kujenga uwezo kwa wataalamu nane (8) wa Kituo cha Jimolojia Tanzania katika shughuli za uongezaji thamani madini; ununuzi wa vifaa vya kufundishia, mashine na mitambo ya kuchakata madini; ununuzi wa vifaa vya maabara; na uwekaji wa samani na vifaa kwenye madarasa na mabweni ya wanafunzi. Jumla ya shilingi bilioni 7.0 fedha za ndani zimetengwa.

 

3.3.3.4. Huduma

 

3.3.3.4.1.       Maliasili na Utalii  

 

(i)           Mradi Na. 5203: Mradi wa Usimamizi wa Maliasili na Kuendeleza Utalii Kanda ya Kusini (Resilient Natural Resources Management for Tourism and Growth Project - REGROW) 

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kuchimba makingio ya maji (weir) manne (4) katika maeneo ya Ngiriama, Telekimboga, Nyamakuyu B na Nyamakuyu C na visima virefu vitatu (3) katika maeneo ya Mbagi, Breakfast Point na Mdonya Falls; na kujenga mabwawa manne (4) katika maeneo ya Ikowoka, Igohuninga, Ilalangulu na Ngalambula kwa ajili ya Hifadhi ya Taifa ya Ruaha; kukarabati miundombinu ya umwagiliaji katika skimu za umwagiliaji za Chosi, Herman, Gonakuvagogolo na Matebete katika bonde dogo la Mto Chimala; kupanda miti 30,000 ili kutunza mabonde ya maji Kanda ya Kusini;  ujenzi wa majengo ya watumishi (8),  malango matatu (3) ya kuingia hifadhini, nyumba za kulala wageni (23), vituo (8) vya watalii na utalii katika hifadhi za Taifa Ruaha, Mikumi, Nyerere, Udzungwa na Msitu wa Asili wa Kilombero; kufanya tafiti mbalimbali zenye lengo la kuhifadhi maliasili na kuendeleza utalii katika Hifadhi za Taifa Ruaha na Nyerere. Jumla ya shilingi milioni 141.0 fedha za ndani na shilingi bilioni 41.7 fedha za nje zimetengwa.

 

(ii)         Mradi Na. 4812: Mradi wa Kukabiliana na Ujangili na Biashara Haramu ya Wanyamapori 

Shughuli zitakazotekelezwa ni: ununuzi wa vifaa vya doria na kufanyika kwa doria; kuandaa kanzidata kwa ajili ya kutunza taarifa na kumbukumbu mbalimbali za ujangili na biashara haramu ya nyara; kununua samani kwa ajili ya chumba maalum cha kuratibu kazi za kudhibiti ujangili Wizarani; na kuandaa kanuni za “compounding”. Jumla ya shilingi bilioni 2.9 fedha za nje zimetengwa. 

 

(iii)       Mradi Na. 4651: Mradi wa Kuwezesha Mnyororo wa Thamani wa Mazao ya Nyuki – BEVAC

Shughuli zitakazotekelezwa ni: kuanzisha hifadhi za nyuki, manzuki na kanda za ufugaji nyuki katika mikoa ya Kusini Pemba, Kaskazini Pemba, Tabora, Katavi na Kigoma; kutoa pikipiki 20 kwa wasimamizi wa mradi katika Wilaya 19; kuandaa mipango ya biashara na ya usimamizi wa vituo sita (6) vya ukusanyaji, uchakataji na usindikaji vilivyowekezwa na Serikali; kuwatafutia fursa ya masoko ya nje wafanyabiashara wa mazao ya nyuki katika mikoa ya Magharibi Pemba; kutoa mafunzo kwa mafundi seremala 95 kuhusu utengenezaji wa mizinga waliopo katika maeneo ya mradi; na kuwezesha uandaaji wa Mkakati wa Ufugaji nyuki Zanzibar. Jumla ya shilingi bilioni 2.9 fedha za nje zimetengwa.

 

(iv)       Mradi Na. 4816: Mradi wa Uendelezaji wa Utalii wa Mikutano na Matukio – MICE 

Shughuli zitakazotekelezwa ni: kuanza kwa maandalizi ya ujenzi wa Kituo cha Kimataifa cha Utalii wa Mikutano na Matukio katika halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni, Jijini Dar es Salaam. Jumla ya shilingi milioni 658.0 fedha za ndani zimetengwa. 

 

(v)         Mradi Na. 4648: Mradi wa Kujenga Uwezo wa Kusimamia Rasilimali za Misitu na Nyuki 

Shughuli zitakazotekelezwa ni: kujenga maabara ya mafunzo na kituo cha kuandaa malkia wa nyuki katika Chuo cha Viwanda vya Ufugaji Nyuki – Tabora (BTI); na kukarabati majengo katika Chuo cha Misitu Olmotonyi. Jumla ya shilingi milioni 141.0 fedha za ndani zimetengwa. 

 

(vi)       Mradi Na.4810: Kujenga Uwezo wa Maeneo ya Hifadhi, Mapori ya Akiba na Kikosi Dhidi Ujangili 

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kuimarisha miundominu (majengo na barabara) katika maeneo ya Hifadhi; kupima eneo na kuandaa michoro kwa ajili ya ujenzi wa ghala la nyara Jijini Dodoma; kununua vitendea kazi (magari, vifaa vya doria na mavazi ya Jeshi la Uhifadhi) kwa ajili ya kuimarisha shughuli za uhifadhi. Jumla ya shilingi milioni 188.0 fedha za ndani zimetengwa

 

(vii)      Mradi Na.4647: Mradi wa Panda Miti Kibiashara (Private Plantation and Value Chain in Tanzania)

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kuwezesha kutoa mafunzo kwa viongozi  wa Vikundi vya Upandaji miti ya namna ya kusimamia na kuendesha vikundi; kuandaa Mipango ya Usimamizi wa Mashamba ya wakulima; kuwezesha vikosi vya kupambana na moto vyenye jumla ya watu 1,284; na kuwezesha vikundi  kuandaa maandiko ya biashara kwa ajili ya kuomba mikopo. Jumla ya shilingi bilioni  3.4 fedha za nje zimetengwa.

 

(viii)    Mradi Na.4650: Mradi wa Kuongeza Thamani kwa Mazao ya Misitu

(Forestry and Value Chain Development Programme (FORVAC) Shughuli zitakazotekelezwa ni: kusimika mitambo ya kukausha mazao ya misitu kwa kutumia teknolojia ya mionzi ya jua; kununua na kusambaza mizinga ya kisasa, jozi  za mavazi ya kurinia asali na vifaa vingine vya kuchakata asali katika vijiji 16 vya kongani ya Ruvuma, wilaya  za Songea,  Mbinga na Nyasa kwa wanufaika vikundi 24; kuanzisha  vikundi vitano (5) vya kukopa katika vijiji vya viwili (2) vya Wilaya ya Ruangwa; na kuwezesha vijiji 13 vya wilaya ya Liwale kupasua mbao na Wilaya ya Ruangwa. Jumla ya shilingi bilioni 3.9 fedha za nje zimetengwa.

 

3.3.3.4.2.       Tasnia ya Utamaduni, Sanaa na Michezo

 

(a)      Mradi Na. 6293: Programu ya Urithi wa Ukombozi wa Bara la Afrika Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kukamilisha ukarabati wa jengo (landscaping) lililotumiwa na Kamati ya Ukombozi ya O.A.U lililopo Jijini Dar es Salaam; kutambua na kukusanya kumbukumbu na taarifa za Urithi wa Ukombozi wa Bara la Afrika ndani na nje ya Nchi; kutayarisha na kuchapisha vitabu vya mashujaa wa ukombozi wa Afrika ujenzi wa minara ya ukumbusho ya mashujaa wawili wa Ukombozi wa Bara la Afrika; na kuadhimisha Siku ya Afrika, Siku ya Ukombozi wa nchi za Kusini mwa Afrika na Maadhimisho ya Siku ya Uanuai wa Utamaduni kwa ajili ya kutoa elimu kuhusu historia ya ukombozi wa Afrika. Jumla shilingi milioni 450 fedha za ndani zimetengwa. 

 

(b)      Mradi Na. 6502: Mfuko wa Utamaduni na Sanaa Tanzania

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kuendelea kutoa mikopo, ruzuku na mafunzo kwa wadau wa sekta ya utamaduni na Sanaa; kuunda Mfumo wa Kielektroniki wa kupokea na kuchakata maombi ya mikopo; kufungua ofisi za kanda ili kuweza kutoa huduma kwa ajili ya kuongeza ufanisi wa kazi na kuwafikia walengwa wengi. Jumla shilingi bilioni 1.6 fedha za ndani zimetengwa. 

 

(c)      Mradi Na. 6521: Kuimarisha Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA) na Kukiuza Kiswahili Kikanda na Kimataifa

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kuandaa maadhimisho ya pili (2) ya Siku ya Kiswahili Duniani; kuwezesha masomo ya wakalimani sita (6) wa lugha za Kispaniola, Kireno na Kifaransa; kuanzisha vituo 15 vya kufundisha Kiswahili kupitia balozi za Tanzania nje ya nchi; kuandaa Kongamano la Idhaa na Televisheni za Kiswahili Duniani; na kufanya Kongamano la Kiswahili nje ya nchi. Jumla shilingi milioni 300 fedha za ndani zimetengwa.

 

(d)      Mradi Na.4353: Ukarabati wa Chuo cha Sanaa Bagamoyo

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kuendelea na ukarabati wa miundombinu ya chuo; kuimarisha miundombinu ya TEHAMA na kununua samani za ofisi;  kununua na kusimika mitambo ili kuanza kurusha matangazo katika Kituo cha Redio na TV; na kuendesha na kuimarisha miundombinu ya Tamasha la 42 la Kimataifa la Sanaa na Utamaduni la Bagamoyo. Jumla ya shilingi milioni 570 fedha za ndani zimetengwa.

 

(e)      Mradi Na. 6385: Ujenzi wa Chuo cha Maendeleo ya Michezo Malya  Shughuli zitakazotekelezwa ni: kukamilisha ujenzi wa hosteli ya wanafunzi; na kuendelea na ukarabati madarasa matatu (3). Jumla shilingi milioni 610 fedha za ndani zimetengwa.

 

(f)       Mradi Na. 6395: Ujenzi wa Akademia ya Michezo Malya 

Shughuli zitakazotekelezwa ni: kumpata mkandarasi na kuanza ujenzi wa akademia itakayojumuisha viwanja vya michezo, mabwawa ya kuongeze, hosteli na vituo vya kufundishia michezo vyenye hadhi ya kimataifa. Jumla shilingi milioni 470 fedha za ndani zimetengwa.

 

(a)         Mradi Na. 6503: Ujenzi wa Eneo Changamani la Michezo Dodoma  Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kupata mshauri Elekezi na kuhuisha upembuzi yakinifu wa mradi utakaohusisha uhuishaji wa michoro, gharama za ujenzi, utafiti wa athari za mazingira na andiko la biashara. Aidha, Serikali itaanza hatua za ujenzi wa uwanja wa Michezo jijini Arusha kama maandalizi ya Tanzania kuwa mwenyeji wa mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika – AFCON 2027. Jumla shilingi milioni 60 fedha za ndani zimetengwa.

 

(b)         Mradi Na. 6504: Ujenzi wa Vituo vya mazoezi na Kupumzikia Wananchi 

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kukamilisha awamu ya kwanza ya vituo vya mazoezi na kupumzika wananchi katika majiji ya Dar es Salaam na Dodoma kwa kujenga hosteli zenye uwezo wa kuhudumia watu 50, viwanja vya michezo ikiwemo uwanja wa mpira wa miguu wa nyasi halisi na nyasi bandia na ujenzi wa viwanja vya mpira wa kikapu, pete na wavu. Jumla shilingi bilioni 4.8 zimetengwa.

 

(c)         Mradi Na. 6527: Ujenzi na Uimarishaji wa Miundombinu ya Michezo katika Shule Maalumu  za Michezo

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kuendelea na ukarabati wa miundombinu ya michezo katika shule 56 teule za michezo. Jumla shilingi bilioni 1.4 fedha za ndani zimetengwa.

 

(d)         Mradi Na. 6523: Ujenzi wa Eneo Changamani la Michezo Dar es Salaam

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kuendelea na ukarabati mkubwa wa uwanja wa Benjamin Mkapa katika maeneo ya uwanja (pitch), mfumo wa umeme, mfumo wa zimamoto, mfumo wa maji, kubadilisha eneo la mashabiki na majukwaa ya watu mashuhuri; na kuendelea kufanya ukarabati mkubwa wa uwanja wa Uhuru katika maeneo ya viti vya watazamaji, kuweka Score Board (Big Screen), mfumo wa zimamoto, kuweka mfumo wa sauti (Sound system) katika uwanja, kuboresha na kujenga vyumba vya kubadilishia nguo na miundombinu ya uwanja ikiwemo mfumo wa Maji taka na mifumo ya Ulinzi. Aidha, Serikali kwa kushirikiana na wadau itaanza ukarabati wa viwanja vya michezo vya majiji ya Mwanza, Dodoma, Arusha, Tanga na Mbeya. Jumla ya shilingi bilioni 1.12 fedha za ndani zimetengwa.

 

(e)         Mradi Na. 6397: Ujenzi wa Arena ya Michezo na Sanaa 

Shughuli zitakazotekelezwa ni: kupata Mshauri Elekezi na kufanya upembuzi yakinifu wa mradi utakaohusisha michoro, gharama za ujenzi, utafiti wa athari za mazingira na andiko la biashara (business plan). Jumla ya shilingi milioni 130 fedha za ndani zimetengwa.

 

(f)          Mradi Na. 6396: Ujenzi wa Jumba Changamani la Filamu 

Shughuli zitakazotekelezwa ni: kufanya upembuzi yakinifu, usanifu wa kina wa mradi na kuandaa andiko la kibiashara (business plan); na kuanza hatua za maandalizi ya ujenzi. Jumla ya shilingi milioni 100 fedha za ndani zimetengwa.

 

(g)         Mradi Na. 6355: Ujenzi wa Ukumbi wa Wazi wa Sanaa

Shughuli zitakazotekelezwa ni: kukamilisha ujenzi wa ukumbi wa wazi wa Sanaa katika eneo la Ilala Shariff Shamba Jijini Dar es Salaam; na kununua vifaa vya sauti na taa kwa ajili ya ukumbi. Jumla ya shilingi milioni 200 fedha za ndani zimetengwa.

 

3.3.3.4.3.       Sekta ya Fedha, Biashara na Masoko

 

(a)           Huduma Ndogo za Fedha

Shughuli zitakazotekelezwa ni: kuandaa na kuchapisha kwenye tovuti za Mamlaka za Usimamizi, Halmashauri na vyombo mbalimbali vya habari, orodha ya watoa huduma ndogo za fedha waliosajiliwa, Kukamilisha maandalizi ya mfumo rasmi wa usimamizi (Supervisory Framework) wa Watoa Huduma Ndogo za Fedha wa daraja la Pili, Kukamilisha mapitio ya Kanuni za Watoa Huduma Ndogo za Fedha wa daraja la Pili ya mwaka 2019; Kuandaa mfumo utakaoweka uwazi wa riba, tozo, ada zinazotozwa pamoja na vigezo na masharti ya Watoa Huduma Ndogo za Fedha wa daraja la Pili; Kukamilisha mifumo ya kupokea na kuchakata taarifa za watoa huduma ndogo za fedha; Kutoa mafunzo kwa Mamlaka za Usimamizi wa watoa huduma ndogo za fedha kuhusu Sera, Sheria na Kanuni za watoa huduma ndogo za fedha; kufanya tathmini za utekelezaji wa Sheria na Kanuni za biashara ya huduma ndogo za fedha. 

 

(b)          Benki ya Maendeleo ya Kilimo – TADB 

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kuzindua utoaji wa mikopo ya ushirikiano na mabenki mengine; kuongeza upatikanaji wa mikopo ya jumla kwa benki na taasisi za fedha, mikopo kupitia mfuko wa dhamana kwa wakulima wadogo, mikopo ya uchakataji na usindikaji wa mazao, Mikopo ya uwekezaji katika miundombinu ya kuzuia upotevu wa mazao ya nafaka, mifugo na uvuvi, mikopo ya ukusanyaji na ununuzi wa mazao kupitia vyama vya msingi, vyama vya ushirika na wasindikaji, mikopo ya ukarabati/ujenzi wa miundombinu ya umwagiliaji, mikopo ya ukusanyaji na ununuzi wa mazao kupitia vyama vya msingi, vyama vya ushirika na wasindikaji, mikopo ya ununuzi wa pembejeo kwa ajili ya uzalishaji wa mazao; na kutoa mafunzo kwa wakulima wadogo.

 

(c)           Benki ya Maendeleo TIB

Shughuli zitakazotekelezwa ni: kutoa mikopo ya takribani shilingi bilioni 51 kwa sekta ya viwanda, maji, nishati, madini, mafuta na gesi, huduma na utalii pamoja na kilimo; kukuza mizania ya benki kufikia shilingi billioni 553 kupunguza ukwasi kwa kuongeza mtaji wa benki kwa shilingi billioni 394; na kubadili amana za muda mfupi za kiasi cha shilingi 166 bilioni kuwa hisa.

 

3.3.4. Kukuza Biashara na Uwekezaji 

 

3.3.4.1. Kuboresha Mazingira ya Uwekezaji na Kukuza Uwekezaji

(a)         Kuboresha Mazingira ya Uwekezaji na Kukuza Uwekezaji 

Shughuli zitakazotekelezwa ni: kuboresha na kuimarisha mfumo wa Dirisha la Pamoja la Uwekezaji (TeIW) kuendelea na awamu ya pili ya ujenzi wa mfumo, kutunga na kuboresha sera, sheria na mikakati mbalimbali inayohusu masuala ya uwekezaji.

 

(b)         Kuratibu, kuhamasisha, kutangaza na kuwezesha uwekezaji 

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kuboresha mifumo ya ukusajili ili kuongeza idadi ya miradi ya uwekezaji inayosajiliwa na Kituo; kuboresha na kuimarisha huduma zitolewazo katika Kituo cha Huduma za Mahali Pamoja (One Stop Facilitation Centre) ili kufanikisha uwekezaji; kuendelea na mkakati wa kufuatilia na kutathmini miradi ya uwekezaji iliyosajiliwa; kuendelea na kutafuta ardhi kwa ajili ya uwekezaji na uanzishwaji wa benki ya ardhi; kuhamasisha uwekezaji ndani na nje ya nchi kupitia makongamano na semina; kutoa elimu kwa wananchi kuhusu masuala mbalimbali ya uwekezaji nchini kupitia vyombo vya habari na mitandao; kutatua migogoro na changamoto za uwekezaji; kufanya tafiti za kuibua fursa za uwekezaji nchini, tafiti za kuboresha mazingira ya uwekezaji, tafiti za kuibua maeneo yenye fursa za uwekezaji; kushirikiana na Balozi za Tanzania katika kuitangaza Tanzania ili kuvutia uwekezaji; na kuwajengea uwezo wafanyakazi wa Kituo ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi. 

 

(c)         Kukuza Ushiriki wa Watanzania kwenye Miradi ya Kimkakati na Uwekezaji

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kuandaa Sera ya Taifa ya Ushiriki wa Watanzania katika uwekezaji na miradi ya kimkakati pamoja na mkakati wake wa utekelezaji; kukamilisha tathmini ya Ushiriki wa Watanzania katika Miradi ya Kimkakati na Uwekezaji.  

 

(d)         Mradi Na. 4901: BEST Programme – BEGIN

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kuboresha sheria, kanuni na taratibu za kisekta zinazoweka vikwazo katika mazingira ya kufanya  biashara; Kufanya tafiti, mapitio na mafunzo mbalimbali ya maboresho ya Sera na mifumo ya udhibiti; kuboresha  Mifumo ya TEHAMA katika taasisi za BRELA, TTLB na Mamlaka ya Serikali za Mitaa na kuandaa kanzidata mbalimbali; kununua  samani , na vifaa vya  ofisi, pamoja na mifumo; na kufanya uratibu na ufuatiliaji wa  utekelezaji wa mradi wa MKUMBI (BEGIN) na kuandaa machapisho mbalimbali ya  kazi za mradi. Jumla ya shilingi bilioni 13.22 fedha za nje zimetengwa.

 

3.3.4.2. Kukuza Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kuimarisha utendaji wa mifuko na programu za uwezeshaji wananchi kiuchumi kwa kuwaunganisha wajasiriamali na fursa za kiuchumi pamoja na kuwawezesha kupata mitaji kupitia mikopo yenye masharti nafuu; kukuza ujuzi na maarifa kwa wajasiriamali wadogo, wa kati na wakubwa ili kukuza biashara zao na kuzalisha kwa tija na ubora; kuimarisha vituo vya uwezeshaji ili kuchochea shughuli za kiuchumi kwa wananchi kwa kujenga vituo vipya katika mikoa 11 pamoja na kufanya ukarabati wa vituo 17 vilivyoanzishwa katika mikoa 6; Kujenga uelewa kwa wananchi kuhusu fursa zilizopo kutoka katika mifuko na programu za uwezeshaji katika kujikwamua kiuchumi;  Kuandaa mfumo wa kidigitali wa ufuatiliaji wa utendaji wa Mifuko na Programu za Uwezeshaji nchini pamoja na kukamilisha mwongozo wa usimamizi wa mifuko na programu za uwezeshaji wananchi kiuchumi.

 

3.3.4.3. Kukuza Sekta Binafsi 

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kuhamasisha Sekta Binafsi kushiriki katika miradi na programu za maendeleo nchini; kufanya tathmini ya mchango wa sekta binafsi katika kukuza uchumi; kuandaa Sera ya Taifa ya Maendeleo ya Sekta Binafsi pamoja na Mkakati wake wa utekelezaji; kuanzisha kanzidata ya sekta binafsi nchini kwa lengo la kuimarisha uratibu wa taasisi za sekta binafsi nchini; kuimarisha majadiliano na mashirikiano kati ya Serikali na sekta binafsi kwa kuandaa zana za kufundishia uendeshaji wa majadiliano kati ya sekta ya umma na sekta binafsi kwa wajumbe wa mabaraza ya biashara ngazi za mikoa (Regional Business Coucils – RBC) na ngazi ya wilaya (Distric Busines Coucils – DBCs) pamoja na wananchi kwa ujumla. Jumla ya shilingi milioni 300 fedha za ndani zimetengwa.

 

3.3.4.4. Huduma za Biashara na Masoko

 

(a)        Mradi Na. 6260: Mradi wa kusaidia Taasisi

 

(i)           Uendelezaji wa Masoko ya Bidhaa 

Shughuli zitakazotekelezwa ni: kuendelea kuongeza wigo wa matumizi ya mfumo wa Stakabadhi za ghala kwa maeneo na kwa mazao yasiyofikiwa na mfumo wa stakabadhi za ghala; kuiwezesha Bodi kupata cheti cha  ithibati ya mfumo wa Ubora ili  kutambulika Kimataifa;  kununua gari kwa ajili ya shughuli za Bodi. Jumla ya shilingi bilioni 1.00 fedha za ndani zimetengwa.

 

(ii)         Maonesho ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam (DTIF) - TANTRADE

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kuimarisha soko la ndani kwa kuratibu matukio ya ukuzaji wa biashara ikiwemo maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Dar es Salaam International Trade Fair - DITF); Kutoa Mafunzo kwa Wafanyabiashara (MSMEs) wenye uwezo wa kuuza mazao na bidhaa soko la nje ya nchi (export potential) wa tasnia ya korosho, zabibu na mafuta ya alizeti na wengine watakaohusika na programu ya BBT ili kuimarisha ushindani katika soko la ndani na kuongeza mauzo nje ya nchi; Kutoa Mafunzo kwa Wafanyabiashara (MSMEs) wenye uwezo wa kuuza mazao na bidhaa soko la nje ya nchi (export potential) wa tasnia ya korosho, zabibu na mafuta ya alizeti na wengine watakaohusika na programu ya BBT ili kuimarisha ushindani katika soko la ndani na kuongeza mauzo nje ya nchi; Kuanzisha Ofisi ya kusimamia biashara ya mipakani hususani Tunduma ili kuimarisha Umoja wa Wafanyabiashara mipakani (CBTAs), na Kamati za Pamoja mipakani JBCs kusimamia na  kuratibu upatikanaji wa taarifa na takwimu za biashara, utatuzi wa kero na kujenga uwezo MSMEs kibiashara;  Kufanya utafiti na intelijensia ya masoko kwa bidhaa na mazao zinazozalishwa nchini katika masomo ya EAC, SADC, AfCFTA  na mengine ili kuongeza mauzo katika masoko ya nje; Kusanifu na kutengeneza mfumo wa kanzidata ya wafanyabiashara pamoja na usajili wa madalali katika masoko nchini; kuandaa programu na kuratibu ushiriki wa Tanzania katika Maonesho ya nje ikiwemo  Expo 2025 Osaka Japan;   Kuratibu programu ya kupata wabia wa uwekezaji  miundombinu ya Maonesho ya Mwl. J. K. Nyerere, Viwanja vya maonesho na vituo vya biashara nchini.  Jumla ya Shilingi bilioni 3.45 zimetengwa kwa mwaka 2023/2024.. Jumla ya shilingi bilioni 3.45 fedha za ndani zimetengwa.

 

(iii)       Udhibiti wa Ubora wa Bidhaa – TBS

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kuendelea na ujenzi wa maabara na ofisi katika Kanda ya Ziwa (Mwanza); na Kuendelea na utafiti wa utengenezaji vinasaba ambavyo vitatumika kwenye mafuta ya petroli, dizeli na mafuta ya taa. Jumla ya shilingi bilioni 10.00 fedha za ndani zimetengwa.

 

(iv)       Kuendeleza Biashara Kupitia Wakala wa Vipimo (WMA)

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kuendelea na ujenzi wa Ofisi ya Makao Makuu ya Wakala Mkoa wa Dodoma, Kununua Flow Meter (3) za kuhakiki Mita za mafuta kwenye Maghala ya mafuta na Migodini, Kununua vifaa (Standards) 30 kwa ajili ya kupima na kuhakiki usahihi wa Mita za Taxi (Taxi Meter) na Kununua Magari matatu (3). Jumla ya shilingi bilioni 3.50 fedha za ndani zimetengwa.

 

(v)         Kuendeleza Biashara Kupitia Tume ya Ushindani (FCC)

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kuanzisha Mfumo wa Kielektroniki kwa ajili ya kutoa huduma zinazotolewa na FCC; kuwajengea uwezo watumishi (5) kuhusu masuala ya ushindani, kumlinda mtumiaji na mapambano dhidi ya Bidhaa Bandia; kufanya utafiti (1) kuhusu masuala ya ushindani; na kununua magari (2) kwa ajili ya kuhudumia ofisi za Kanda. Jumla ya shilingi milioni 500 fedha za ndani zimetengwa.

 

(vi)       Kuendeleza Biashara Kupitia Baraza la Ushindani (FCT)

Shughuli zitakazofanyika ni: Kuweka Mfumo wa kurekodi (automated record equipment system)  kwa ajili ya kuongeza kasi ya usikilizwaji wa mashauri; Kufanya tafiti (1) za kisheria na kiuchumi kuhusu ushindani wa kibiashara;  na kufanya Public Awareness Survey, kuandaa Mkakati wa kujitangaza na kutoa elimu kwa wadau na wananchi wengi kuhusu shughuli za Baraza na haki katika ushindani wa Soko. Jumla ya shilingi milioni 600 fedha za ndani zimetengwa.

(vii)      Soko la Bidhaa Tanzania – TMX

Shughuli zitakazotekelezwa ni: kuuza kiasi cha tani 4,300 za kakao kutoka mkoa wa Morogoro katika wilaya za Ulanga, Kilombero na  Malinyi.  Maandalizi ya kuuza Mifugo hai (ngómbe, mbuzi na kondoo) na ngozi zinazotokana na wanyama hao yanaendelea. Mwaka 2023//24 Soko la Bidhaa kwa kushirikiana na PSSSF ambao ni wahanisa wa Nguru Hills Ranch wanaendelea kutafuta namna ya kuuza mifugo hai na nyama za mifugo.  Kuendelea na majadiliano ya namna Soko la Bidhaa litakavyoshiriki kuuza madini na kufanya utafiti wa aina ya madini yanayoweza kuuzwa kupitia Soko hili na kuandaa mkataba wa makubaliano (MOU) kwa maeneo yote ya ushirikiano. Kufanya maandalizi ya kuuza pamba na kutoa elimu kwa wadau wa pamba na kuwaelimisha kuhusu mfumo wa kielektroniki wa Soko la Bidhaa.

 

3.3.4.5. Mahusiano na Nchi za Nje na Uchumi wa Kidiplomasia

 

(a)         Mradi Na. 6391: Ujenzi na Ukarabati wa Majengo ya Vitega Uchumi, Ofisi na Makazi ya Watumishi Balozini  

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kuendelea na ukarabati wa majengo ya ofisi na makazi ya watumishi pamoja na uendelezaji wa viwanja katika Balozi za Tanzania Washington D.C (Marekani); Brussels (Ubelgiji); Stockholm (Sweden); Pretoria (Afrika Kusini); Uwakilishi wa Kudumu wa Tanzania New York (Marekani); Addis Ababa (Ethiopia); Muscat (Oman); Nairobi (Kenya); Kinshasa (Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo); Lusaka (Zambia) na Abuja (Nigeria). Shughuli nyingine zitakazotekelezwa ni pamoja na: kuendelea na uandaaji wa michoro na nyaraka za miradi ikiwemo upembuzi yakinifu kwa ajili ya utekelezaji wa miradi 14 balozini kwa kushirikiana na sekta binafsi katika Balozi za  Addis Ababa, Ethiopia; Kinshasa, DRC; Kampala, Uganda; Bujumbura, Burundi; Kigali, Rwanda; Maputo, Msumbiji; Lilongwe, Malawi; Abuja, Nigeria; London, Uingereza; na Muscat, Oman. Jumla ya shilingi bilioni 8.65 fedha za ndani zimetengwa.

 

(b)         Mradi Na. 6317: Ujenzi wa Makao Makuu ya Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu

Shughuli zitakazotekelezwa ni ujenzi wa miundombinu na majengo ya Makao Makuu ya Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu katika eneo la Lakilaki jijini Arusha. Jumla ya shilingi bilioni 5.4 fedha za ndani zimetengwa.  

 

(c)         Mradi Na. 6318: Ukarabati wa Majengo ya Ofisi 

Upanuzi wa Uboreshaji wa Miundombinu ya Chuo cha Diplomasia 

Shughuli zitakazotekelezwa ni ujenzi wa vyumba vya mihadhara tisa (9) katika Chuo cha Diplomasia, Kurasini, Dar es Salaam. Jumla ya shilingi bilioni 3.9 fedha za ndani zimetengwa. 

 

(d)         Mradi Na. 4902: Mradi wa kujenga Uwezo kwa Watumishi 

Shughuli zitakazotekelezwa ni pamoja na kuendesha mafunzo kwa watumishi ili kuboresha utendaji kazi. Jumla ya shilingi 187,608,000 fedha za nje zimetengwa.

 

3.3.5. Kuchochea Maendeleo ya Watu

 

3.3.5.1. Afya

 

Hospitali za Kitaifa

 

(a)           Mradi Na. 5487: Hospitali ya Taifa ya Muhimbili 

Shughuli itakayotekelezwa ni kuendelea na ujenzi wa jengo la kutoa huduma kwa wagonjwa binafsi na wagonjwa mashuhuri. Jumla ya shilingi bilioni 4.5 fedha za ndani zimetengwa. 

 

(b)           Mradi Na. 5491: Taasisi ya Mifupa Muhimbili (MOI)

Shughuli zitakazotekelezwa ni: kuendelea na ununuzi wa vifaa tiba (vipandikizi – inplants revolving fund). Jumla ya shilingi bilioni 2  fedha za ndani zimetengwa.

 

(c)           Mradi Na. 5412: Taasisi ya Saratani Ocean Road

Shughuli zitakazotekelezwa ni: kuendelea na ujenzi wa jengo la Oncology na kusimika vifaa vya uchunguzi wa Saratani katika kituo cha Mbeya. Jumla ya shilingi Bilioni 3.0 fedha za ndani zimetengwa. 

 

(d)           Mradi Na. 5419: Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete

Shughuli zitakazotekelezwa ni: kuendelea na upanuzi wa chumba cha kutakasia vifaa ili kuimarisha huduma za upasuaji wa moyo. Jumla ya shilingi Bilioni 2 fedha za ndani zimetengwa.

 

(e)           Mradi Na. 5424: Hospitali ya Taifa ya Magonjwa Ambukizi – Kibong’oto (Kilimanjaro)

Shughuli zitakazotekelezwa ni: kuendelea na ujenzi na ukarabati mkubwa wa jengo la radiolojia kwa ajili ya kusimika CT Scan; kuendelea na ukarabati wa jengo la utawala; kuendelea na ujenzi wa jengo la kuhudumia wagonjwa wa nje na kukamilisha ukarabati na upanuzi wa jengo la wagonjwa mahututi. Jumla ya shilingi bilioni 3 fedha za ndani zimetengwa.

 

(f)            Mradi Na 5425: Hospitali ya Rufaa ya Afya ya Akili - Mirembe

Shughuli zitakazotekelezwa ni: kuendelea na ukarabati wa jengo la wagonjwa wa nje. Jumla ya shilingi bilioni 2 fedha za ndani zimetengwa.

 

(g)           Mradi Na.5445: Hospitali ya Taifa ya Mama na Mtoto - Dodoma

Shughuli zitakazotekelezwa ni: kuendelea na ujenzi wa hospitali ya kibingwa na ubingwa bobezi ya Afya ya Mama na Mtoto – Nala. Jumla ya shilingi bilioni 5  fedha za ndani zimetengwa.

 

Hospitali za Rufaa za Kanda

 

(h)           Mradi Na. 5426: Hospitali ya Rufaa Kanda ya Ziwa, Bugando

Shughuli zitakazotekelezwa ni: kuendelea na ununuzi wa vifaa tiba kwa ajili ya kuimarisha uchunguzi na tiba ya saratani. Jumla ya shilingi bilioni 1 fedha za ndani zimetengwa.

 

(i)             Mradi Na. 5427: Hospitali ya Kanda ya Kaskazini (KCMC)

Shughuli zitakazotekelezwa ni: kuendelea na ununuzi wa vifaa tiba ili kuimarisha huduma. Jumla ya shilingi bilioni 1 fedha za ndani zimetengwa.

 

(j)            Mradi Na. 5422: Hospitali ya Rufaa ya Nyanda za Juu Kusini Mbeya Shughuli zitakazotekelezwa ni: kuendelea na ujenzi wa jengo la huduma za watotoMeta. Jumla ya shilingi bilioni 2 fedha za ndani zimetengwa.

 

(k)           Mradi Na. 5428: Hospitali ya Benjamin Mkapa

Shughuli zitakazotekelezwa ni: kuendelea na ujenzi wa jengo la Radiotherapy na Nuclear medicine. Jumla ya shilingi bilioni 4 fedha za ndani zimetengwa.

 

(l)             Mradi Na. 5408: Ujenzi wa Hospitali ya Kanda ya Ziwa - Burigi

Shughuli zitakazotekelezwa ni: kuendelea na ukamilishaji wa ujenzi wa miundombinu ya jengo la mama na mtoto pamoja na ununuzi wa vifaa. Jumla ya shilingi bilioni 4 fedha za Ndani zimetengwa.

 

(m)         Mradi Na. 5423: Hospital ya Rufaa ya Kanda ya Kusini - Mtwara Shughuli zitakazotekelezwa ni kuendelea na ujenzi wa miundombinu ya hospitali  ikiwemo ujenzi wa jengo la mama na mtoto awamu ya kwanza, sehemu ya kufulia, kichomea taka na nyumba za watumishi. Jumla ya shilingi bilioni 3 fedha za Ndani zimetengwa.

 

(n)           Mradi Na. 5443: Hospital ya Rufaa ya Kanda ya Magharibi – Kigoma Shughuli zitakazotekelezwa ni kuendelea na ujenzi wa majengo ya Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Magharibi katika mkoa wa Kigoma. Jumla ya shilingi bilioni 4.0 fedha za ndani zimetengwa.

Hospitali za Rufaa za Mikoa

 

(o)           Mradi Na. 5411: Mradi wa Kuboresha Hospitali za Rufaa za Mikoa 

Shughuli zitakazotekelezwa ni: kuendelea na ujenzi na ukarabati katika Hospitali za Rufaa za Mikoa ya Katavi, Geita, Songwe, Simiyu, Shinyanga, Singida, Mwl. Nyerere Mara, Bombo, Ligula, Maweni - Kigoma,, Kitete, Sekou Toure – Mwanza, Mawenzi – Kilimanjaro,Songea, Manyara, Sokoine, Kagera, Ukerewe. Miundombinu hiyo inahusisha majengo mbalimbali kama vile ya kutolea huduma za mama na mtoto, majengo ya wagonjwa wa nje, dharura,wodi za upasuaji, radiolojia, vichomea taka na kuhifadhia maiti. Jumla ya shilingi bilioni 60.8 fedha za ndani zimetengwa. 

 

Tafiti na Uboreshaji wa Upatikanaji wa Dawa, Vifaa, Vifaa Tiba na Vitendanishi

 

(p)           Mradi Na 2208: Taasisi ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu ya Taifa (NIMR)

Shughuli zitakazotekelezwa ni: kugharamia utafiti wa magonjwa ya binadamu, tiba asili na tiba mbadala, kuimarisha utengenezaji wa dawa za tiba asili na tiba mbadala na kutoa mafunzo kwa wataalam wa tiba asili na tiba mbadala. Jumla ya shilingi bilioni 3.3 fedha za ndani  na shilingi bilioni 17 fedha za nje zimetengwa. 

 

(q)           Mradi Na. 5411: Mradi wa Kuboresha Upatikanaji wa Dawa, Vifaa Tiba na Vitendanishi

Shughuli zitakazotekelezwa ni: kununua na kusambaza dawa, vifaa, vifaa tiba na vitendanishi kwa vituo vyote vya umma vya kutolea huduma za afya nchini na ugomboaji wa dawa za msaada na kugharamia huduma za uchunguzi. Jumla ya shilingi bilioni 200 fedha za ndani na shilingi biioni 5 fedha za nje zimetengwa.

 

(r)            Mradi Na. 5432: Uimarishaji wa Huduma za Chanjo

Shughuli itakayotekelezwa ni: kuimarisha huduma za kudhibiti magonjwa ya kuambukiza kupitia huduma za chanjo pamoja na kugharamia uchangiaji gharama za chanjo zinazofadhiliwa na Shirika la GAVI (co-financing). Jumla ya shilingi bilioni 38 fedha za ndani zimetengwa na shilingi bilioni 76.3 fedha za nje.

 

(s)           Mradi Na. 5492: Mpango wa Taifa wa Kudhibiti UKIMWI (NACP) 

Shughuli itakayotekelezwa ni kuongeza wigo wa upatikanaji wa huduma kwa watu wenye VVU na UKIMWI ili kufikia malengo ya asilimia 95 – 95– 95 (kutambua - kutumia dawa - kujikinga). Jumla ya shilingi bilioni 65.9  fedha za nje zimetengwa.

 

(t)            Mradi Na. 5498: Mpango wa Taifa wa Kudhibiti Kifua Kikuu na Ukoma 

Shughuli zitakazotekelezwa ni: kuongeza huduma za kinga na kinga ya kifua kikuu kwa vituo vya msingi vya huduma ya afya; kutoa mafunzo kazini ya kuwajengea wafanyakazi uwezo wa kuongeza ufanisi wa uibuaji wa wahisiwa na utoaji wa huduma wa Kifua Kikuu (QI Mentorship); na kutoa huduma za ufuatiliaji na upimaji wa wahisiwa wa Kifua Kikuu magerezani. Jumla ya shilingi milioni 100 fedha za ndani na shilingi bilioni 19.5 fedha za nje zimetengwa.

 

(u)           Mradi Na. 5406: Kudhibiti Magonjwa ya Kuambukiza na Mlipuko Shughuli zitakazotekelezwa ni: kuimarisha huduma za kudhibiti magonjwa ya kuambukiza na ya mlipuko. Jumla ya shilingi milioni 100 fedha za ndani na shilingi bilioni 20.7 fedha za nje zimetengwa

 

(v)           Mradi Na. 5403: Kudhibiti Magonjwa Yasiyo ya Kuambukiza 

Shughuli zitakazotekelezwa ni: kuimarisha huduma za kudhibiti magonjwa yasiyo ya kuambukiza kwa kuwekeza katika elimu kwa umma, upimaji na kujenga uwezo wa vituo vya kutolea huduma kudhibiti magonjwa hayo. Jumla ya shilingi bilioni 2 fedha za ndani zimetengwa na Shilingi bilioni 20 fedha za nje zimetengwa. 

 

(w)         Mradi Na. 2204: Mafunzo na Maendeleo ya Wataalamu

Shughuli zitakazotekelezwa ni: upanuzi, ukarabati na ujenzi wa mabweni, maabara, katika vyuo vya mafunzo ya afya, ujenzi wa maabara za kujifunzia na madarasa na kugharamia mafunzo ya uzamili. Jumla ya shilingi bilioni 27.1 fedha za ndani zimetengwa. 

 

(x)           Mradi Na. 5416: Mipango ya Afya na Uendeshaji 

Shughuli zitakazotekelezwa ni: kuimarisha matumizi ya TEHAMA katika utoaji wa huduma za afya ikiwemo tiba mtandao, mafunzo, utawala, usimamizi wa fedha, dawa na bidhaa zote za dawa pamoja na uboreshaji wa ukusanyaji na matumizi ya takwimu za afya katika ngazi zote za hospitali, vituo vya afya na zahanati. Jumla ya shilingi milioni 121 fedha za nje zimetengwa. 

 

(y)           Mradi Na. 5401: Ujenzi wa Hospitali za Halmashauri

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kuendelea na ujenzi wa hospitali 41 kwa halmashauri ambazo hazikuwa na Hospitali na ukarabati wa hospitali kongwe za halmashauri 31. Jumla ya shilingi bilioni 58.19 fedha za ndani zimetengwa.

 

(z)           Mradi Na. 5429: Huduma ya Afya ya Msingi 

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Ujenzi wa vituo vya afya 16 na ukamilishaji wa vituo vya afya 6 na maboma ya zahanati 376 yaliyoanza kujengwa kwa nguvu za wananchi. Jumla ya shilingi bilioni 28.34 fedha za ndani na nje zimetengwa.

(aa)       Mradi Na. 5411: Mradi wa Kuboresha Upatikanaji wa Dawa, Vifaa Tiba na Vitendanishi

Shughuli zitakazotekelezwa ni: ununuzi wa vifaa na vifaa tiba kwenye hospitali 31 za halmashauri, vituo vya afya 278 na zahanati 364. Jumla ya shilingi bilioni 116.92 fedha za ndani zimetengwa.

 

(bb)       Mradi Na. 5488: Mfuko wa Udhamini wa UKIMWI (AIDS Trust Fund - ATF)

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Ununuzi wa dawa za magonjwa nyemelezi kwa Watu Wanaoishi na Virusi Vya UKIMWI (WAVIU); kutekeleza programu za kinga hasa utoaji wa elimu ya kujikinga na VVU na kubadili tabia; na uendeshaji wa shughuli za Mfuko wa Udhamini wa UKIMWI (AIDS Trust Fund - ATF). Jumla ya shilingi bilioni 3.0 fedha za ndani zimetengwa.

 

3.3.5.2. Ustawi na Maendeleo ya Jamii

 

(a)         Mradi Na. 6330: Ukarabati wa Vyuo vya Maendeleo ya Jamii

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kujenga hosteli (awamu ya pili) yenye uwezo wa kuhudumia wanafunzi 400 katika Chuo cha Maendeleo ya Jamii Misungwi; kuendelea na ujenzi wa hosteli (awamu ya tatu) katika Chuo cha Maendeleo ya Jamii Uyole; kujenga hosteli (awamu ya pili) yenye uwezo wa kuhudumia wanafunzi 600 katika Chuo cha Maendeleo ya Jamii Monduli; na ujenzi wa jengo la utawala katika Taasisi ya Maendeleo ya Jamii Tengeru. Jumla ya shilingi bilioni 3.1 fedha za ndani zimetengwa.

 

(b)         Mradi Na. 6259: Ujumuishaji wa Masuala ya Jinsia katika Mipango ya Maendeleo

 Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kujenga uwezo wa Maafisa Maendeleo ya Jamii, Maafisa Ustawi wa Jamii na Wanasheria kuhusu utoaji wa elimu ya masuala ya ukatili wa kijinsia; kutekeleza afua za MTAKUWA II; kukamilisha mapitio ya Sera ya Maendeleo ya Wanawake na Jinsia (2000) na kutoa uelewa kwa jamii kuhusu Sera hiyo. Jumla ya shilingi bilioni 1.2 fedha za nje zimetengwa.

 

(c)         Mradi Na. 6279: Usawa wa Jinsia na Uwezeshaji wa Wanawake

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kutekeleza Programu ya Jukwaa la Kizazi Chenye Usawa Tanzania (Tanzania Generation Equality Program) kwa: kujenga uwezo wa Madawati ya kuratibu Programu ya Kizazi Chenye Usawa; kutekeleza Mkakati wa mawasiliano wa Programu ya Kizazi Chenye Usawa; kujenga uwezo wa waratibu wa Majukwaa ya Kuwezesha Wanawake Kiuchumi; kujenga uwezo wa Waratibu wa Majukwaa ya Uwezeshaji Wanawake Kiuchumi ngazi ya Mkoa na Wilaya kuhusu utekelezaji wa Programu ya Kizazi Chenye Usawa; kutoa uelewa kwa jamii kuhusu Programu ya Kizazi Chenye Usawa; Kuandaa Mpango wa Ufuatiliaji na Tathmini ya utekelezaji wa Programu ya Kizazi Chenye Usawa; kuwezesha vitendea kazi kwa Waratibu wa Programu ya Kizazi Chenye Usawa; kuwezesha ushiriki wa nchi katika Mikutano ya Kitaifa, Kikanda na Kimataifa kuhusu Jukwaa la Kizazi Chenye Usawa; na kuwezesha shughuli za uratibu wa Programu ya Kizazi Chenye Usawa. Jumla ya shilingi bilioni 4 fedha za ndani zimetengwa.

 

(d)         Mradi Na. 5414: Uhai na Maendeleo ya Mtoto 

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kuanzishwa kwa Dawati la Ulinzi wa Mtoto kwa ajili ya watoto ndani na nje ya shule za msingi na sekondari; kuanzishwa kwa vituo vya kijamii vya malezi, makuzi na maendeleo ya awali ya watoto katika halmashauri 185; kuendelea kuimarisha mabaraza ya watoto kwa kuanzisha mahali ambapo hayapo na kutoa mafunzo kwa wajumbe wa mabaraza hayo kuhusu haki na ustawi wao; na kutoa uelewa kwa jamii kuhusu ukatili dhidi ya watoto mitandaoni. Jumla ya shilingi bilioni 1.2 fedha za nje zimetengwa. 

 

(e)         Mradi Na. 6280: Mfuko wa Kuwezesha Wafanyabiashara Ndogondogo (Machinga)

Shughuli itakayotekelezwa ni kutoa mikopo yenye masharti nafuu kwa Wafanyabiashara Ndogondogo nchini (Machinga). Jumla ya shilingi bilioni 18.5 fedha za ndani zimetengwa. 

 

(f)          Mradi Na. 5451: Kuwezesha Huduma za Ustawi wa Jamii

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kukarabati majengo na miundombinu katika Makazi manne (4) ya Wazee ya Ipuli, Mwanzage, Misufini na Bukumbi; kukarabati majengo na miundombinu katika mahabusu za watoto katika mikoa ya Dar es salaam, Mbeya, Arusha na Moshi; ukarabati wa majengo na miundombinu katika shule ya Maadilisho Mbeya; ujenzi wa mahabusu ya watoto katika mkoa wa Mwanza; na kuimarisha mifumo ya ulinzi na usalama wa watoto walio katika mazingira hatarishi. Jumla ya shilingi bilioni 1.0 fedha za ndani na shilingi bilioni 1.05 fedha za nje zimetengwa.

 

(g)         Mradi Na. 6290: Uchakataji wa Taarifa na Uandaaji Programu (Programming and Data Processing)

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kufanya ufuatiliaji na tathmini ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika taasisi mbili (2), vyuo nane (8) vya Maendeleo ya Jamii, makazi 14 ya wazee, Mahabusu 5 za watoto na Shule ya Maadilisho Irambo); na kuratibu utekelezaji wa Mpango Kazi wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto (MTAKUWWA). Jumla ya shilingi milioni 200 fedha za ndani na shilingi milioni 200 fedha za nje zimetengwa.

 

3.3.5.3. Elimu

 

(a)         Mradi Na. 4340: Mikopo kwa Wanafunzi wa Elimu ya Juu

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kuendelea na ukusanyaji wa mikopo ya shilingi bilioni 230 kutoka kwa wanufaika wa mikopo iliyoiva; kuendelea na ugharamiaji wa mikopo ya wanafunzi 210,169 ambapo wanafunzi 72,361 ni wa mwaka wa kwanza na wanafunzi 136,516 ni wanaoendelea na masomo; kufanya ukaguzi kwa waajiri 8,000 pamoja na kuwabaini wanufaika wapya 40,000; na kutoa mikopo kwa wanufaika 642 wa Samia Scholarship. Jumla ya shilingi bilioni 738.7. 3 fedha za ndani zimetengwa.

 

(b)         Mradi Na. 6363: Ukarabati wa Chuo cha Ufundi Arusha - ATC

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kuendelea na ujenzi wa maktaba ya kisasa yenye uwezo wa kuhudumia wanafunzi 1,200. Jumla ya shilingi bilioni 1.0 fedha za ndani zimetengwa

.

(c)         Mradi Na. 6352: Tume ya Nguvu za Atomiki - TAEC

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kuendelea na awamu ya pili ya ujenzi wa maabara changamano (Arusha); na ununuzi wa samani na vifaa vya maabara. Jumla ya shilingi bilioni 2.2 fedha za ndani zimetengwa.

 

(d)         Mradi Na. 4312: Programu ya Lipa Kulingana na Matokeo katika Elimu (EP4R II)

Shughuli zitakazotekelezwa ni: kuwezesha ununuzi wa samani katika vyuo vya ualimu Sumbawanga, Mhonda na Dakawa ,vifaa vya maabara za shule na wanafunzi wenye mahitaji maalum; kuwezesha ujenzi na ukarabati wa nyumba za walimu katika chuo cha Ilonga, Morogoro, Nachingwea, Vikindu, Korogwe, Patandi, Bustani na Tukuyu; kuwajengea uwezo walimu 12,000 wa shule za msingi katika tathmini ya stadi za Kusoma, Kuandika na Kuhesabu katika mikoa 10 yenye wastani wa chini wa stadi hizo; na kuwajengea uwezo watumishi  774 wakiwemo Maafisa Elimu Mkoa (REOs), Maafisa Elimu Taaluma wa Mkoa (RAOs), Maafisa Elimu wa Wilaya (DEOs), Maafisa Taaluma Wilaya (DAOs) na Maafisa Elimu Takwimu (SLOs) ili kuimarisha mahudhurio ya wanafunzi na waweze kuhitimu hususani wanafunzi wa kike katika Mikoa 13. Jumla ya shilingi bilioni 22.5 fedha za nje zimetengwa.

 

 

(e)         Mradi Na. 4390: Mradi wa Kuboresha Elimu ya Sekondari (SEQUIP)

Shughuli zitakazotekelezwa ni: kuwezesha uchapaji wa moduli tisa (9) za masomo Hatua ya I, II na usambazaji kwa vituo 150 kwa wanafunzi wapya wa Elimu kwa Njia Mbadala na uchapaji na usambazaji wa vitabu 2,000,000 vya Sayansi na Hisabati kwa kidato 1- 4; Kutoa motisha kwa walimu wa Hatua ya II wanaofundisha katika vituo vinavyotoa Elimu kwa Njia Mbadala nchini; kuendesha mtihani wa majaribio (mock) kwa wanafunzi wa kike walio katika mazingira magumu Hatua ya I na II katika vituo 151 vya mafunzo ya Elimu kwa Njia Mbadala; kuwezesha ununuzi wa vifaa vya kujifunzia na kemikali za masomo ya sayansi kwa wanafunzi wa Elimu kwa Njia Mbadala kwa Hatua ya I na II; kuendesha Mtihani wa Kidato cha Nne kwa wanafunzi wa Kike 3,000 na Maarifa (QT) kwa wanafunzi wa kike 3,000 wa Elimu kwa Njia Mbadala walio katika mazingira magumu; kuwezesha ujenzi wa  vituo vinne (4) (Lindi, Songwe, Kagera na Manyara) vya watu wazima; kuwajengea uwezo wawezeshaji 150 wa Stadi za Maisha kwa ajili ya utoaji wa Elimu kwa Njia Mbadala ,wawezeshaji 300 wa masomo ya Hisabati na Fizikia Hatua ya I  na 300 Hatua ya II, walimu 300 kutoka vituo 151 vya Elimu kwa Njia Mbadala kuhusu namna ya ufundishaji wa moduli za masomo tisa (9) ya awamu ya II, waratibu 151 kutoka vituo 151 vya Elimu kwa Njia Mbadala kuhusu matumizi ya TEHAMA, mafunzo kuhusu Programu ya Shule Salama kwa walimu 1,300 na Wakuu wa shule za Sekondari. walimu 10,000 wa masomo ya Sayansi na Hisabati wa shule za sekondari Kidato cha I - 4 kuhusu moduli za Sayansi na Hisabati na mafunzo kuhusu moduli za TEHAMA kwa walimu 4,500 kutoka shule 1,300. Jumla ya shilingi bilioni 29.8 fedha za nje zimetengwa.

 

(f)          Mradi Na. 3280: Programu ya Huduma ya Maji, Elimu ya Afya na Usafi wa Mazingira Shuleni – SWASH

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kuwezesha tathmini ya mahitaji ya miundombinu ya maji, vyoo na vifaa vya kunawia mikono katika shule za msingi 450 zilizokidhi vigezo kwa ajili ya kutekeleza mradi; kuwezesha ufuatiliaji wa ujenzi wa miundombinu ya maji, vyoo na vifaa vya kunawia mikono katika shule za msingi 450; Kuendelea kutoa mafunzo ya Mwongozo wa Huduma ya Maji, Elimu ya Afya na Usafi wa Mazingira kwa waratibu wa Mikoa na Halmashauri 86; kuandaa, kuchapisha na kusambaza michoro na mwongozo wa ujenzi wa miundombinu ya maji, vyoo na vifaa vya kunawia mikono kwa Wahandisi wa Mikoa na Halmashauri; na kuchapisha na kusambaza Mpango wa Kitaifa wa Kugharimia na Kuwekeza katika miundombinu ya maji, vyoo na vifaa vya kunawia mikono shuleni.. Jumla ya shilingi bilioni 1.6 fedha za nje zimetengwa.

 

(g)         Mradi Na. 4315: Mradi wa Kuendeleza Elimu ya Juu Kwa Mabadiliko ya Kiuchumi (Higher Education for Economic Transformation Project - HEET)

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kuanza ujenzi na ukarabati wa miundombinu mbalimbali (mabweni, vyumba vya madarasa, maabara, kumbi za mikutano, ofisi, samani na vituo atamizi) katika vyuo Vikuu na taasisi za elimu ya juu; kutathmini utekelezaji wa Sera ya Taifa ya Teknolojia ya Nyuklia, Sera ya Taifa ya Bayoteknolojia ya Mwaka 2013, na Sera ya Taifa ya Utafiti na Maendeleo ya Mwaka 2010; kuwezesha uandaaji wa Mpango Kabambe wa Elimu ya Juu (2025 - 2035), Mpango Kabambe wa Sayansi, Teknolojia na Ubunifu na Mpango Kabambe wa TEHAMA katika Sekta ya Elimu; kuwezesha Mapitio na Uendelezaji wa Mkakati wa Kitaifa wa Ujuzi (NSDS - 2016), uandaaji wa Mpango Mkakati wa Taifa wa Sayansi, Teknolojia na Ubunifu na Mkakati wa Kitaifa wa usawa wa Kijinsia kwa Elimu ya Juu; kuwezesha uandaaji wa mfumo wa taarifa za Elimu ya Juu kwa ajili ya kufuatilia na kukusanya viashiria vya Ufuatiliaji na tathmini katika Taasisi; kuwezesha uandaaji wa miongozo ya Kitaifa ya kujitegemeza (self-generated income) kwa taasisi zinazotekeleza mradi; kuwezesha uandaaji na ukamilishwaji  wa vipaumbele vya Mpango wa Kitaifa wa Utafiti; kuwezesha uundaji wa utaratibu wa kuimarisha utoaji wa huduma za Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi katika Elimu ya Juu nchini Tanzania; kuwezesha Mapitio ya Mitaala ya Elimu ya Juu na Kuanzisha Mbinubunifu za Ufundishaji; kuwezesha ukuzaji wa majukwaa ya ndani ya kuboresha taasisi mpya na mitaala; Kuwezesha Taasisi ya Elimu ya Juu kuanzisha miundombinu na vifaa vya kisasa vya TEHAMA; na kuwezesha uendelezaji wa elimu-jumuishi inayotoa fursa kwa wanafunzi wenye mahitaji maalum katika programu ya Sayansi Teknolojia na Hisabati. Jumla ya shilingi bilioni 46.6 fedha za nje zimetengwa.

 

(h)         Mradi Na. 4309: Mradi wa Kujenga Ujuzi Afrika Mashariki (EASTRIP) Shughuli zitakazotekelezwa ni: kuwezesha uandaaji wa Mpango Mkakati wa Maendeleo wa Kitaifa wa Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (TVET) na miongozo ya Mitaala na Uhakiki wa Ubora wa Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi; ukwezesha mapitio ya viwango vya ubora wa kazi kwa sekta za kipaumbele za Tanzania - EASTRIP TVET (Nishati - ATC, usindikizaji Ngozi –DIT Kampasi ya Mwanza, Usafirishaji-NIT na TEHAMA - DIT); kuwezesha ujenzi wa Kituo cha Umahiri cha Kikuletwa katika Chuo cha Ufundi Arusha – ATC na Kituo cha Umahiri katika Taasisi ya Teknolojia ya Dar es Salaam kampasi ya Mwanza na Dar es Salaam - DIT; kununua na kufunga mitambo na vifaa katika karakana na maabara; kuwezesha ununuzi wa Zana, Vifaa na Mashine katika Kituo cha Mafunzo Kikuletwa Kilichopo Chuo cha Ufundi Arusha (ATC), Taasisi ya Teknolojia ya Dar es Salaam - DIT Kampasi ya Dar es Salaam na Mwanza; na kujengea uwezo wakufunzi 100 wa Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi katika ufundishaji na upimaji wa wanafunzi. Jumla ya shilingi bilioni 15.1 fedha za nje zimetengwa.

 

(i)           Mradi Na. 4319: Mradi wa Kuboresha Elimu ya Awali na Msingi (BOOST Primary Student Learning)

Shughuli zitakazotekelezwa: Kuwezesha mafunzo ya kifurushi cha TEHAMA kwa walimu wa shule za msingi katika vituo 200 vya walimu, mafunzo kwa walimu wa shule za awali kuhusu ufundishaji na ujifunzaji kwa wanafunzi awali; kuwezesha ujenzi wa darasa mmoja (1) la mfano la awali katika vyuo vya ualimu 17; kuwezesha mafunzo endelevu kazini kwa walimu 3,000; Ujenzi wa vyumba vya madarasa 3,000; kuwezesha mafunzo kwa walimu kazini katika halmashauri 50; ununuzi wa vifaa vya kufundishia na kujifunzia na ufungaji wa vifaa vya TEHAMA katika vituo 200 vya mafunzo ya walimu kazini; kuendelea na mpango salama wa shule katika shule 2000 na kutoa mafunzo ya usimamizi na utawala bora katika utoaji wa elimu msingi. Jumla ya shilingi bilioni 12.7 fedha za nje zimetengwa.

 

(j)          Mradi Na. 6350: Chuo Kikuu cha Dar es Salaam

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kuendelea na upanuzi wa hosteli ya Dkt. John Pombe Joseph Magufuli kwa kuongeza ghorofa mbili (2); kuendelea na ujenzi wa maabara kuu ya kemikali itakayotumika kwa ajili ya utafiti na utoaji wa huduma za kupima sampuli za viwandani, Shule Kuu ya Uchumi na kituo cha wanafunzi na kuwezesha ujenzi wa Kituo cha Wanafunzi kwa awamu ya pili katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam; ununuzi wa samani; na kukarabati nyumba za watumishi. Jumla ya shilingi bilioni 4.0 fedha za ndani zimetengwa.

 

(k)         Mradi Na. 6365: Upanuzi na Ukarabati wa Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi (MOCU)

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kuwezesha ujenzi wa Maktaba yenye uwezo wa kuhudumia wanafunzi 2,500 kwa wakati mmoja, ukumbi wa mhadhara wenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 1,868 na Hosteli yenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 1,500. Jumla ya shilingi bilioni 1.0 fedha za ndani zimetengwa.

 

(l)           Mradi Na. 6345: Mfuko wa Utafiti na Maendeleo wa COSTECH

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kuongeza utafiti wa kimkakati na athari za kitaifa, kuimarisha utamaduni wa STU, kukuza sekta ya viwanda kwa njia ya Teknolojia na kuimarisha uwezo wa Taasisi ya Tume ya Taifa ya Sayansi naTeknolojia - COSTECH. Jumla ya shilingi bilioni 3.5 fedha za ndani zimetengwa.

 

(m)       Mradi Na. 6333: Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya - MUST

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kuendelea na ujenzi wa jengo la utawala na hosteli za wanafunzi katika kampasi Kuu; ununuzi wa samani na vifaa vya kisasa vya maabara, maktaba pamoja na karakana kwa ajili ya kufundishia;. Jumla ya shilingi bilioni 1.3 fedha za ndani zimetengwa.

 

(n)         Mradi Na. 6354: Ukarabati na Upanuzi wa Chuo Kikuu Ardhi

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kuwezesha maendeleo ya Kampasi ya Mwanza, kupata ardhi kwa ajili ya Kampasi ya Dodoma na kujenga Multipurpose pavilion . Jumla ya shilingi bilioni 1.0 fedha za ndani zimetengwa.

 

(o)         Mradi Na. 6361: Upanuzi na Ukarabati wa Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine – SUA

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kuwezesha ujenzi wa jengo  la Ndaki ya Sayansi ya Jamii na Jinsia,  Wodi ya Wazazi na Bwawa la kuvuna maji ya mvua katika Kampasi Kuu.Jumla ya shilingi bilioni 1.0 fedha za ndani zimetengwa.

 

(p)         Mradi Na. 4323: Kuendeleza Elimu ya Ualimu - TESP

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kuwezesha ukarabati wa maabara za Lugha, Sayansi, Chakula na Lishe na Kilimo katika vyuo 7 vya ualimu (Marangu, Songea, Monduli, Korogwe, Klerruu, Tabora na Mandaka); Kuwezesha Kituo cha Hisabati Morogoro kuandaa Programu endelevu kwa walimu ili kuimarisha ufundishaji na ujifunzaji wa somo la Hisabati katika shule na vyuo; kuwezesha uunganishaji wa Vyuo vya Ualimu 11 katika Mkongo wa Taifa (National Fiber Optical); kuwezesha mafunzo kwa wakufunzi 250 wa ajira mpya kuhusu TEHAMA na njia shirikishi za ufundishaji. Jumla ya shilingi bilioni 7.0 fedha za nje zimetengwa.

 

(q)         Mradi Na. 6229: Ukarabati wa Vyuo vya Maendeleo ya Wananchi -

FDC

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kuendelea na ujenzi wa majiko na ununuzi wa vifaa vya karakana kwa ajili ya vyuo 20 vya maendeleo ya wananchi; kuanza kwa ufungaji wa mfumo wa gesi katika majiko kwa vyuo 54 vya maendeleo ya wananchi; na kuendelea na ujenzi na ukarabati wa miundombinu ya vyuo vingine 30 vya maendeleo ya wananchi. Jumla ya shilingi bilioni 1.3 fedha za ndani zimetengwa. 

 

(r)          Mradi Na. 4384: Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam – DIT

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kuendelea kwa ujenzi wa mabweni miwili (2) Kampasi ya Mwanza yenye uwezo wa kuhudumia wanafunzi 300; na kuwezesha uwekaji wa vifaa na ununuzi wa vifaa vya kufundishia na kujifunzia. Jumla ya shilingi bilioni 1.5 fedha za ndani zimetengwa.

 

(s)         Mradi Na. 6364: Ujenzi wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Mloganzila

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kuboresha miundombinu ya MUHAS (maabara ya ustadi, meno, mvua, duka la dawa na maktaba pamoja na kuboresha miundombinu ya kujifunza kielektroniki. Jumla ya shilingi bilioni 1.0 fedha za ndani zimetengwa.

 

(t)          Mradi Na. 4314: Upanuzi na Ukarabati wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Mkwawa (MUCE)

Shughuli zitakazotekelezwa ni: kuwezesha awamu ya II ya ujenzi wa maktaba ya kisasa yenye uwezo  wa kuhudumia wanafunzi 1,500 kwa wakati mmoja na kuwezesha ujenzi Hosteli awamu ya II yenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 300..  Jumla ya shilingi bilioni 1.0 fedha za ndani zimetengwa.

 

(u)         Mradi Na. 4341: Chuo Kikuu cha Mwl. Julius Nyerere cha Kilimo na Teknolojia

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kuwezesha ukarabati wa miundombinu katika kampasi ya Oswald Mang’ombe na kujenga zahanati ya chuo. Jumla ya shilingi bilioni 1.0 fedha za ndani zimetengwa.

 

 

(v)         Mradi Na. 4385: Upanuzi na Ukarabati wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam (DUCE)

Shughuli zitakazotekelezwa ni: kuwezesha ujenzi wa maabaara awamu ya I (Hatua ya II) katika shule ya sekondari ya mazoezi, ujenzi wa madarasa ya shule ya msingi awamu II na ukarabati wa majengo ya chuo pamoja na miundombinu . Jumla ya shilingi bilioni 1.0 fedha za ndani zimetengwa.

 

(w)       Mradi Na. 4322 na 4393: Elimu msingi na Sekondari Bila Ada

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kuendelea kutoa elimu msingi bila ada ikijumuisha ruzuku ya uendeshaji wa shule, ruzuku ya ununuzi wa vitabu, posho ya madaraka kwa walimu wakuu, wakuu wa shule na maafisa elimu kata, fidia ya ada kwa shule za bweni na kutwa na kugharamia chakula cha wanafunzi kwa shule za bweni na kutwa za msingi zenye wanafunzi wenye mahitaji maalum. Jumla ya shilingi bilioni 488.53 fedha za ndani zimetengwa.

 

(x)         Mradi Na. 6390: Mamlaka ya Elimu Tanzania – TEA

Shughuli zitakazotekelezwa ni: kuwezesha ujenzi wa madarasa 90, matundu ya vyoo 336, nyumba za walimu 90, mabweni 11 ya wasichana, maabara za masomo ya sayansi 30, vyumba vya kusomea tisa (9) pamoja na kununua vifaa vya kufundishia na kujifunzia elimu maalum.Jumla ya shilingi bilioni 11.5 fedha za ndani zimetengwa.

(y)         Mradi Na. 4306: Wakala wa Maendeleo ya Uongozi wa Elimu (ADEM) Shughuli zitakazotekelezwa ni: kujenga jengo lenye ofisi 10 na kumbi nne (4) za mihadhara na kuweka samani katika kampasi ya Mwanza na ukumbi wa matumizi mbalimbali na kukarabati majengo matatu (3) katika Kampasi ya Bagamoyo.. Jumla ya shilingi bilioni 10 fedha za ndani zimetengwa.

 

(z)         Mradi Na. 4304: Ujenzi na Ukarabati Chuo Kikuu cha Dodoma

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kuwezesha ujenzi wa maabara (Anatomi – SoMD) ununuzi wa vifaa vya maabara kwa ajili ya wanafunzi wa udaktari na ujenzi wa miundombinu ya maji katika Chuo Kikuu chaa Dodoma.. Jumla ya shilingi bilioni 3.0 fedha za ndani zimetengwa

 

(aa)     Mradi Na. 6353: Upanuzi wa Chuo Kikuu Mzumbe

Shughuli zitakazotekelezwa ni: kuwezesha ujenzi wa jengo la utawala, madarasa nane (8), kumbi mbili (2) za mihadhara, jengo la TEHAMA na Kituo atamizi cha ubunifu (Innovation and Incubation Center) na ukarabati wa miundombinu katika Chuo Kikuu cha Mzumbe. Jumla ya shilingi bilioni 1.0 fedha za ndani zimetengwa.

 

(bb)     Mradi Na. 4381: Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kuendelea na ujenzi wa mabweni mawili (2) ya wanafunzi yenye uwezo wa kuhudumia wanafunzi 1,536  pamoja na nyumba tatu

(3) za wafanyakazi zenye uwezo wa kuhudumia watumishi 30 katika Kampasi ya Karume Zanzibar; kuendelea na ujenzi wa maktaba yenye uwezo wa kuhudumia wanafunzi 2,500 Kampasi ya Kivukoni; ujenzi wa jengo la utawala na madarasa matatu (3) yenye uwezo wa kuhudumia wanafunzi 1,800; kuwezesha ujenzi wa cum theater na madarasa pamoja na kuwezesha umiliki wa majengo ya NSSF kwa ajili ya hosteli za wanafunzi katika Kampasi ya Kivukoni.. Jumla ya shilingi bilioni 2.0 fedha za ndani zimetengwa.

 

(cc)      Mradi Na. 4397: Ujenzi na Ukarabati wa Vyuo vya Ufundi Stadi

Shughuli zitakazotekelezwa ni: kuanza ujenzi wa Ofisi ya VETA Makao Makuu jijini Dodoma na Chuo cha VETA Mkoa wa Dar es salaam Kampasi ya Kigamboni; kufanya upanuzi na ujenzi wa  miundombinu ya mafunzo ya Ufundi Stadi katika vyuo vya VETA Namtumbo, Kanadi (Itilima), Nyamidaho, Ileje, Simanjiro, Kihonda, Arusha, Ngorongoro, Mara, Karagwe na Lindi; kuboresha huduma na miundombinu ya Maktaba katika vyuo vya VETA vya Mikoa ya Pwani, Iringa, Tabora, Kigoma na Mbeya; kukarabati vyuo vya mafunzo vya ufundi stadi katika Mikoa Dar es Salaam, Dodoma, Mwanza, Mtwara, Njombe, Morogoro na Kigoma; na kununua vifaa na mitambo ya kujifunzia na kufundishia; kukamilisha ujenzi wa Vyuo vya Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi katika Wilaya 25 na kuanza ujenzi wa vyuo vya ufundi stadi 64 katika wilaya ambazo hazina vyuo. Jumla ya shilingi bilioni 50.0 fedha za ndani zimetengwa.

 

(dd)     Mradi Na. 4358: Taasisi ya Sayansi na Teknolojia Afrika ya Nelson Mandela

Shughuli zitakazotekelezwa ni: kuwezesha ujenzi wa hosteli yenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 500, jengo la ofisi na ukarabati wa jengo la utawala pamoja na Hosteli.Jumla ya shilingi bilioni 1.0 fedha za ndani zimetengwa.

 

(ee)     Mradi Na. 6321: Ujenzi na Ukarabati wa Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA)

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kuendelea na ujenzi wa bweni la wasichana Kampasi ya Babati – Manyara na ujenzi wa Kampasi Mpya Songea (Ruvuma); kuanza ujenzi wa madarasa na maktaba katika Kampasi ya Babati na Songea. Jumla ya shilingi bilioni 1 fedha za ndani zimetengwa.

 

(ff)        Mradi Na. 6322: Ujenzi na Ukarabati wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM)

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kuendelea na ujenzi wa mabweni, madarasa na ofisi za Kampasi ya Mwanza; na kuboresha mitaala ya elimu, mifumo ya TEHAMA pamoja na ujenzi wa mabweni, maktaba, jengo la kufundishia na jengo la mihadhara katika Kampasi ya Simiyu. Jumla ya shilingi bilioni 3.5 fedha za ndani na shilingi bilioni 12.17 fedha za nje zimetengwa.

 

Afrika (EASTC). Jumla ya shilingi bilioni 36.1 fedha za nje zimetengwa

 

(gg)     Mradi Na. 6323: Ujenzi na Ukarabati wa Chuo cha Uhasibu Tanzania (TIA)

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Ujenzi wa jengo la taaluma Nyang’homango, Misungwi-Mwanza; ujenzi wa jengo la taaluma katika kampasi ya kigoma na ujenzi wa jengo la taaluma lenye ukumbi wa mihadhara, maabara ya kompyuta, Maktaba, ofisi za utawala na ukumbi wa mikutano kampasi ya   Zanzibar. Jumla ya shilingi bilioni 8 fedha za ndani zimetengwa.

 

(hh)     Mradi Na. 6206: Upanuzi na Ukarabati wa Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini (IRDP)

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kukamilisha ujenzi wa jengo la bweni la wanafunzi katika eneo la Miyuji Dodoma; ukamilishaji wa ujenzi wa ukumbi mmoja wa mihadhara awamu ya pili katika eneo la Miyuji kampasi kuu, ukamilishaji wa ujenzi wa bweni la wanafunzi    katika Kituo cha Mafunzo Kanda ya Ziwa eneo la Kitumba Magu Mwanza na Kujengo jengo la Bweni la wanafunzi katika eneo la Kitumba Magu Mwanza. Jumla ya Shilingi bilioni 5 fedha za ndani zimetengwa. 

 

3.3.5.4. Ardhi, Mipango Miji, Nyumba na Maendeleo ya Makazi

 

(a)         Mradi Na. 2326: Programu ya Kupanga, Kupima na Kumilikisha Ardhi

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kutayarisha skimu za uendelezaji maeneo ya mijini kwa majiji ya  Dar es Salaam, Mbeya, Mwanza na Arusha; kupima na kuidhinisha viwanja 300,000; kupanga na kupima maeneo yanazonguka miradi ya kimkakati (SGR, EACOP, JNHPP) na kuandaa mipango kina mitano (5) ya uendelezaji upya wa maeneo ya Visiwa na fukwe na maeneo chakavu katika mikoa ya Dar es Salaam, Mbeya, Mwanza na Arusha kwa ajili ya uwekezaji; na kuendelea kutatua migogoro ya matumizi ya ardhi kwa vijiji 975. Jumla ya shilingi bilioni 4.5 fedha za ndani zimetengwa.  

 

(b)         Mradi Na. 2324: Mradi wa Kuimarisha Mipaka ya Kimataifa

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kuendelea na ujenzi wa alama za mipaka ya kimataifa kati ya Tanzania na Kenya yenye urefu wa kilomita 80 pamoja na mpaka wa Tanzania na Burundi wenye urefu wa kilomita 100 na kufanya utafiti kuhusu teknolojia mpya ya upimaji ndani ya maji. Jumla ya shilingi bilioni 2.5 fedha za ndani zimetengwa.

 

(c)         Mradi Na 2329: Mradi wa Kuimarisha Miundombinu ya Upimaji na Ramani

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kuboresha Mtandao wa Geodetic kwa kusakinisha na kufanya kazi kwa vituo 30 CORS (CORS - Continuously Operating Reference Station) katika miji ya makao makuu ya mikoa yote; kutayarisha ramani za msingi za kidijitali nchini kote; kuanzisha Mfumo wa Wavuti wa usambazaji wa habari za anga; kuwajengea uwezo  wataalam wa GIS (100) kuhusu maendeleo ya National Spatial Data Infrastructure (NSDI); na kuongeza alama za upimaji 357 nchini kwa lengo la kupunguza gharama za upimaji ardhi; na kuwezesha utekelezaji wa shughuli za mradi wa National Spatial Data Infrastructure (NSDI). Jumla ya shilingi  milioni 264 fedha za nadani na bilioni 5.1 fedha za nje zimetengwa.

 

(d)         Mradi Na. 4953: Uboreshaji wa Milki za Ardhi 

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kupima mipaka ya vijiji 200; kuandaa matumizi ya ardhi ya vijiji 200; kuanza ukarabati wa Ofisi za Ardhi za Halmashauri 41; kurasimisha makazi 500,000 katika Halmashauri 23; kujenga vituo 22 vya alama za upimaji na kusimika alama 276 za upimaji; kuandaa na kutoa Hati za haki miliki za Kimila 200,000 (Certificate of Customery of Right of Occupancy (CCROs); kusimikwa kwa Mfumo Unganishi wa Kumbukumbu za ardhi (Intergrated Land Information Management System - ILMIS) katika Halmashauri 132; kubadilisha kumbukumbu za ardhi 1,647, 330 kwenda katika mfumo wa kidigitali; kujenga kumbi nne (4)  za Mihadhara katika Chuo cha Ardhi Tabora (2) Morogoro (2); na usimamizi, ufuatiliaji na tathmini ya mradi. Jumla ya shilingi bilioni 5.7 fedha za ndani na shilingi bilioni 63 fedha za nje zimetengwa.

 

(e)         Mradi Na. 6327: Ujenzi na Ukarabati wa Majengo ya Serikali Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kuwezesha ukarabati wa majengo mawili (2) ya Wizara pamoja na ununuzi wa lifti katika jengo la Wizara - mkoani Dar es Salaam; kuendelea na ujenzi wa majengo ya maabara katika vyuo vya  Ardhi Tabora na Morogoro (Ardhi Institute of Tabora (ARITA) na Ardhi Institute  of Morogoro (ARIMO) na kukarabati miundombinu ya ofisi ya Wizara  na Mikoa (10). Jumla ya shilingi bilioni 1.06 ya fedha za ndani zimetengwa.

 

(f)          Mradi Na. 4951: Upangaji wa Matumizi ya Ardhi

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kuwezesha utayarishaji wa Mipango ya Matumizi ya Ardhi katika Vijiji 333 vilivyopo kando ya  Tanzania Standard Gauge Railway (SGR) (80), The East African Crude Oil Pipeline EACOP (53), Julius Nyerere Hydroelectric Power Plant (JNHPP) (200) na Vijiji 100 vinavyokabiliwa na migogoro ya matumizi ya ardhi; maandalizi ya Mpango wa Mfumo wa Matumizi ya Ardhi wa Wilaya 14; kuwezesha utayarishaji wa mipango 84 ya kina ya matumizi ya ardhi na hati 25,200 za Haki ya hatimiliki ya Kimila (Certificate of Customery of Right of Occupancy (CCROs); kuandaa mipango ya matumizi ya Ardhi ya Wilaya tano (5) na vijiji 210; kuwezesha kufanya ukaguzi na tathimini katika vijiji 100 vilivyofanyiwa mpango wa matumizi. Jumla ya shilingi bilioni 15.73 za fedha za ndani zimetengwa.

 

 

3.3.5.5. Huduma za Maji na Usafi wa Mazingira

(a)         Mradi Na. 3280: Huduma za Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini 

Shughuli zitakazotekelezwa ni: kutekeleza jumla ya miradi ya maji vijijini 1,546; kujenga mabwawa 29 katika maeneo mbalimbali ya vijijini;  na kuunda, kuhuisha na kusajili Vyombo vya Watoa Huduma ya Maji Ngazi ya Jamii (CBWSOs) 111 na kuzijengea uwezo CBWSOs 2,543. Jumla ya shilingi bilioni 212.75 fedha za ndani na shilingi bilioni 60.81 fedha za nje zimetengwa.

 

(b)         Mradi Na. 3306: Ujenzi, Ukarabati na Upanuzi wa Miradi ya Maji katika Miji Mikuu ya Mikoa

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kuendelea na ujenzi na ukarabati wa miundombinu ya huduma za majisafi na usafi wa mazingira katika miji ya Dodoma, Mwanza, Morogoro, Arusha, Shinyanga, Mbeya na Babati; na kuendelea na ujenzi na upanuzi wa miundombinu ya majitaka katika miji ya Musoma, Moshi, Tanga, Babati, Bukoba na Dodoma. Jumla ya shilingi bilioni 32.7 fedha za ndani na shilingi bilioni  76.42 fedha za nje zimetengwa.

 

(c)         Mradi Na. 3307: Ujenzi, Ukarabati na Upanuzi wa Miradi ya Maji katika Miji mikuu ya Wilaya, Miji Midogo na Miradi ya Kitaifa

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kuendelea na utekelezaji wa mradi wa maji Mgango – Kiabakari – Butiama (Mara); kuendelea na ujenzi wa miradi ya kuboresha huduma za maji katika miji 28; na kuendelea na ujenzi wa miundombinu ya majitaka katika miji ya Mheza, Nzega, Chato na Pangani. Jumla ya shilingi bilioni 46.9 fedha za ndani na shilingi bilioni 57.48 fedha za nje zimetengwa.

 

(d)         Mradi Na. 3309: Ujenzi, Ukarabati na Upanuzi wa Miradi ya Maji katika Miji mikuu ya Mikoa mipya

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kuendelea na utekelezaji wa mradi wa maji katika miji ya Vwawa-Mlowo, Njombe na Geita; na kuendelea na ujenzi wa miundombinu ya majitaka katika mji wa Njombe. Jumla ya shilingi bilioni 1.1 fedha za ndani na shilingi bilioni 6.33 fedha za nje zimetengwa.

 

(e)         Mradi Na. 3341: Mradi wa Maji Same – Mwanga – Korogwe

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kukamilisha awamu ya kwanza ya utekelezaji wa mradi inayohusisha ujenzi wa chanzo na mitambo ya kusafisha maji; na kukamilisha ujenzi wa miundombinu ya kusafirisha na kusambaza maji katika miji ya Mwanga na Same. Jumla ya shilingi bilioni 18.0 fedha za ndani na shilingi bilioni 1.3 fedha za nje zimetengwa.

 

(f)          Mradi Na. 3403: Mradi wa Maji wa Ziwa Victoria - Kahama – Shinyanga na Miji Mingine

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kuendelea na utekelezaji wa miradi ya maji katika vijiji  vya karibu na bomba kuu la maji kwenda miji ya Malampaka, Sumve na Malya; kuboresha huduma ya maji katika miji ya Busega, Bariadi, Ligangabilili na Mwanhuzi; na kufanya upembuzi yakinifu na usanifu wa mradi wa kutoa maji Ziwa Victoria kupeleka Singida na Dodoma. Jumla ya shilingi bilioni 5.93 fedha za ndani na shilingi bilioni 10.95 fedha za nje zimetengwa. 

 

(g)         Mradi Na. 3437: Kuboresha Huduma za Maji Katika Jiji la Dar es Salaam

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kuendelea na uboreshaji wa miundombinu ya usambazaji maji na usafi wa mazingira katika maeneo ya Dar es Salaam na Pwani; na kujenga mitambo ya kutibu majitaka, mabomba ya kutolea majitaka kutoka maeneo ya makazi na kupelekwa kwenye mitambo ya usafishaji. Jumla ya shilingi bilioni 2.5 fedha za ndani na shilingi bilioni 32.90 fedha za nje zimetengwa.

 

(h)         Mradi Na. 3439: Mradi wa Maji wa Mpera na Kimbiji

Shughuli zitakazotekelezwa ni kuendelea na ujenzi wa miundombinu ya kusambaza maji kwa wananchi umbali wa kilomita 65 katika maeneo ya Kigamboni. Jumla ya shilingi bilioni 1.5 fedha za ndani na zimetengwa.

 

(i)           Mradi Na. 6545: Kusimamia na Kuendeleza Rasilimali za Maji Nchini Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kukarabati vituo 135 na kujenga vituo 51 vya kufuatilia mwenendo wa rasilimali za maji; kuhuisha na kutoa leseni 50 za uchimbaji visima maeneo mbalimbali nchini; kutoa vibali 450 vya matumizi mbalimbali ya maji; kuunda Jumuiya 10 za Watumia Maji pamoja na kuzijengea uwezo Jumuiya 87 na kuunda kamati tisa (9) za vidakio (Catchment Committees); kutoa vibali 30 vya kutupa majitaka; kufanya utafiti wa maeneo ya kuchimba visima; kuweka mipaka na kutangaza vyanzo vya maji katika Gazeti la Serikali; kuanza ujenzi wa bwawa la Farkwa; kujenga mabwawa 20 ya ukubwa wa kati; kukamilisha ujenzi wa Kituo Mahiri cha Rasilimali za Maji (Water Resources Center of Exelllency) Mjini Dodoma; kuendelea na ujenzi wa majengo ya ofisi Bodi za maji katika mikoa ya Iringa na Songea na kuanza ujenzi wa majengo ya maabara za maji katika mikoa ya Dodoma, Tanga na Arusha. Jumla ya shilingi bilioni 14.5 fedha za ndani na shilingi bilioni 27.0 fedha za nje zimetengwa.

 

(j)          Mradi Na. 3435: Ufuatiliaji wa Ubora wa Maji na Usimamizi wa Mfumo wa Ikolojia 

Shughuli zitakazotekelezwa ni: kuendelea kuimarisha uhakiki na ufuatiliaji wa ubora wa maji katika vyanzo vya maji 2,091; skimu 4,600 za usambazaji maji mijini na vijijini pamoja na mifumo 150 ya majitaka; kuziwezesha maabara tano (5) kupata ithibati; kuhakiki ubora wa madawa ya kusafisha na kutibu maji kabla ya manunuzi na wakati wa matumizi; kuwezesha uandaaji na utekelezaji wa Mipango ya Usalama wa Maji inayohimili mabadiliko ya tabianchi kwa Mamlaka za Majisafi na Usafi wa Mazingira 34 na Vyombo vya Watoa Huduma ya Maji Ngazi ya Jamiii 100; kutoa elimu kuhusu viwango vya ubora wa maji kwa ajili ya matumizi mbalimbali; na kuendelea kuimarisha maabara za ubora wa maji kwa kuzipatia vitendea kazi pamoja na kujenga na kukarabati majengo ya maabara. Jumla ya shilingi bilioni 1.2 fedha za ndani na shilingi milioni 750 fedha za nje zimetengwa.

 

(k)         Mradi Na. 3436: Ufuatiliaji na Uratibu wa Programu ya Maendeleo ya Sekta ya Maji (WSDP II)

Shughuli zitakazotekelezwa ni: kuratibu utekelezaji wa programu ya maji (WSDP III); na kuwezesha uratibu wa masuala ya mazingira katika sekta ya maji. Jumla ya shilingi bilioni 3.98 fedha za ndani na shilingi bilioni 9.67 fedha za nje zimetengwa.

 

(l)           Mradi Na. 3438: Mradi wa Bwawa la Kidunda 

Shughuli zitakazotekelezwa ni kuendelea na ujenzi wa Bwawa la Kidunda. Jumla ya shilingi bilioni 60.43 fedha za ndani zimetengwa.

 

3.3.5.6. Hifadhi ya Mazingira na Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi

(a) Programu Na 5301: Programu ya Kuhimili Athari za Mabadiliko ya Tabia Nchi

 

(i)           Mradi wa Kuhimili Athari ya Mabadiliko ya Tabia Nchi Kupitia Mifumo ya Ikolojia Vijijini

Shughuli zitakazotekelezwa: Uchimbaji wa visima virefu viwili katika Halmashauri za Mpwapwa (1) na Mvomero (1); uchimbaji wa malambo matatu katika Halmashauri za Kishapu (2) na Mpwapwa (1); kuendelea na ujenzi wa kiwanda kidogo cha bidhaa za ngozi katika Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero na ujenzi wa kituo cha kukusanyia maziwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero; ujenzi wa maghala mawili (2) ya kuhifadhia nafaka katika Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro; kuendelea na ujenzi wa kituo cha huduma za mifugo katika Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa; kuendelea na ujenzi wa Skimu ya Umwagiliaji ya Lukenge katika Halmasahauri ya Wilaya ya Mvomero; kuendelea na ujenzi wa majengo matatu (3) ya vikundi vya ushonaji, utengenezaji wa sabuni na ufugaji katika Shehia za Matemwe Kijini, Mbuyutende na Jugakuu Wilaya ya Kaskazini A-Unguja; ujenzi wa vitalu nyumba vitatu (3) Wilaya ya Kaskazini A-Unguja; ununuzi wa Madume aina ya Boran 100 kuboresha kosaafu za ng’ombe katika Wilaya za Kishapu, Simanjiro, Mvomero na Mpwapwa; kuwezesha jumla ya vikundi 25 vya uzalishaji katika Wilaya za Kaskazini A, Kishapu, Mpwapwa, Mvomero na Simanjiro; na kurejesha uoto wa asili katika hekta 9,000 za ardhi iliyoharibiwa katika vyanzo vya maji na kingo za mito katika Wilaya za Kaskazini A, Kishapu, Mpwapwa, Mvomero na Simanjiro. Jumla ya shilingi bilioni 6.63 fedha za nje zimetengwa. 

 

 

(ii)         Mradi wa Usimamizi Jumuishi wa Mifumo wa Ikolojia, Urejeshwaji wa Uoto Asili na Hifadhi ya Bionuai Tanzania

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kuandaa mwongozo wa kitaifa wa kujumuisha masuala ya urejeshwaji endelevu wa mazingira na hifadhi ya bioanuai kwenye sera na mikakati ya kisekta, mipango na mifumo ya kisheria; Kutekeleza shughuli za usimamizi wa rasilimali za misitu na shughuli za uhifadhi wa misitu katika eneo la hekari 20,538 katika maeneo ya mradi; kuandaa mipango ya matumizi bora ya ardhi kwa vijiji 38 ambapo vijiji 12 vitaandaliwa mipango ya matumizi hatua 1 - 6 na vijiji 26 hatua 5 - 6 na kutoa hati miliki za kimila 3,500; kuwezesha utekelezaji wa shughuli mbadala na rafiki kwa mazingira kwa vikundi vya kijamii visivyopungua 35 na kunufaisha watu wasiopungua 20,000 katika maeneo tegemezi sana kwenye maliasili; kutekeleza mbinu za kilimo himilivu kwa mabadiliko ya tabianchi katika eneo lenye ukubwa wa hekta 1,250 na ujenzi wa skimu ndogo za umwagiliaji 7; kuboresha ufugaji endelevu kwa kujenga majosho 14, mabirika ya kunyweshea mifugo 14, mashamba darasa ya malisho 14, na mabanio ya kupandisha ng’ombe 21, ujenzi wa malambo matatu na uchimbaji wa visima virefu 6 katika halmashauri za Wilaya ya Iringa, Wanging’ombe, Mbarali, Mbeya, Sumbawanga, Mpimbwe, na Tanganyika; Kuhamasisha matumizi ya majiko banifu kwa kujenga majiko banifu kwa taasisi 50 zenye matumizi makubwa ya kuni na mkaa, na kujenga majiko banifu kwa kaya 1080. Jumla ya shilingi bilioni 6.74 fedha za nje zimetengwa.   

 

(iii)       Mradi wa Kurejesha Ardhi Iliyoharibika na Kuongeza Usalama wa Chakula Katika Maeneo Kame

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kuendelea na ujenzi wa malambo (2) na ukarabati lambo moja (1), mfumo mmoja wa uvunaji wa maji, ujenzi wa mabirika matatu (3) ya kunyweshea mifugo na ujenzi wa mashojo mawili (2) katika Halmashauri ya Magu; kuwezesha ujenzi  na kukarabati malambo (3) na ujenzi wa bwawa moja (1), mifumo miwili (2) ya uvunaji wa maji ya mvua, ujenzi wa mabirika manne (4)  ya kunyweshea mifugo na ujenzi josho moja (1) na ukarabati wa mashojo mawili (2) katika Halmashauri ya Nzega; na Kuwezesha ujenzi  na kukarabati  mabwawa manne (4) na malambo  mawili (2), mifumo miwili ya uvunaji wa maji ya mvua, ujenzi wa mabirika matano (5) ya kunyweshea mifugo na ujenzi na ukarabati wa mashojo matano (5)  na kukabarati moja (1) katika Halmashauri ya Mkalama. Jumla ya shilingi bilioni 4.31 fedha za nje zimetengwa.

 

(iv)       Mradi wa Kujenga Uwezo wa Taasisi ili Kupunguza Hewa Ukaa Inayosababishwa na Ukataji Miti na Uharibifu wa Misitu 

Shughuli zitakazotekelezwa ni: kuratibu na kusimamia utekelezaji wa shughuli za mradi; kufanya tathmini ya mwisho na kufanya ukaguzi wa mradi. Jumla ya shilingi milioni 324.1 fedha za nje zimetengwa.

 

 

(v)         Usimamizi Endelevu wa Matumizi ya Ardhi ya Bonde la Ziwa Nyasa

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kutoa mafunzo kwa makundi ya wavuvi katika Halmashauri za Kyela, Ludewa na Nyasa; kutoa mafunzo na kuwezesha wanavikundi (375) kuhusu kilimo cha biashara ya miti katika halmashauri zinazotekeleza mradi; na kuwezesha mafunzo kwa wanavikundi (75) kwa kubadilishana uzoefu kwa kutembeleana katika maeneo wanayofanya shughuli za ujasiriamali, kuundwa kwa Jumuiya moja (1) ya watumia maji (Water User Association) katika Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa na kuimarisha jumuiya zilizoundwa awali katika Halmashauri za Wilaya ya Mbinga, Ludewa, Kyela na Makete. Jumla ya shilingi milioni 501.57 fedha za nje zimetengwa.

 

(vi)       Mradi wa Ujenzi na ukarabati wa kingo za fukwe katika Mwambao wa Sipwese Pemba na Mikindani - Mtwara

Shughuli zitakazotekelezwa ni: kuendelea na ujenzi wa kuta za bahari katika maeneo ya Mikindani Mtwara (mita 190) na Sipwese Pemba (mita 290). Jumla ya shilingi billioni 4.2 fedha za ndani zimetengwa.

 

(b)         Programu Na. 6571: Programu ya Utekelezaji wa Sheria na Usimamizi wa Hifadhi ya Mazingira ya Mwaka 2004

Mradi wa Kujenga Uwezo wa Kitaasisi wa Kutekeleza Sheria ya Usimamizi wa Mazingira

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kuandaa kanuni tano (5) na miongozo mitano (5) ya usimamizi wa hifadhi ya mazingira; kanzi data ya tathmini ya mazingira pamoja; na kuanzisha Jukwaa la kitaifa la usimamizi wa mazingira. Jumla ya shilingi billioni 2.6 fedha za nje zimetengwa

 

(c)         Mradi Na. 5305: Kutekeleza Mpango wa Kitaifa wa Utekelezaji wa Mkataba wa Stockholm Unaohusu Kemikali Zinazodumu katika Mazingira kwa Muda Mrefu

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kujenga vituo vitatu (3) vya kuchambua taka zinazorejelezeka katika Manispaa za Kigamboni na Ubungo; na kuratibu ukusanyaji, uhifadhi kwa muda na kuondosha nchini mafuta yaliyobainika kuwa na kiwango kikubwa cha kemikali ya PCBs (above 50ppm) na transfoma zilizokuwa zimehifadhi mafuta husika kwa ajili ya kwenda kuteketezwa kwa njia salama nchini Ufaransa; na Kuandaa Mpango Kazi wa Taifa wa uondoshaji wa Kemikali aina ya PCBs. Jumla ya shilingi milioni 281.41 fedha za nje zimetengwa.

 

(d)         Mradi Na. 5304: Kudhibiti Kemikali Zinazomomonyoa Tabaka la Ozoni

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kutoa mafunzo kwa maafisa forodha (200) na wasimamizi wa sheria (100) kuhusu udhibiti wa uingizaji nchini wa kemikali zinazomong’onyoa tabaka la ozoni; kuwezesha vyuo vyenye fani ya viyoyozi na majokofu kwa utoaji wa vifaa, teknolojia na utaalamu; kutoa mafunzo kwa maafisa ugavi 30 kutoka wizara za kisekta; kutoa mafunzo kwa mafundi 300 wa viyoyozi na majokofu  kuhusu namna bora ya kuhudumia vifaa hivyo kwa kutumia kemikali pasipo kuharibu tabaka la ozoni; na kujenga uelewa kwa walaji wa mwisho na wadau mbalimbali kuhusu matumizi ya teknolojia na kemikali mbadala wa kemikali. Jumla ya shilingi milioni 342 fedha za nje zimetengwa.

 

(e)         Mradi Na. 6309: Ujenzi na Ukarabati wa Ofisi na Makazi ya Makamu wa Rais

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kuendelea na ukarabati wa makazi ya Mhe. Makamu wa Rais Kilimani (Dodoma) na Oysterbay (Dar es salaam); na ukarabati  jengo la Ofisi ya Makamu wa Rais kwenye eneo la  Luthuli II (Dar es Salaam). Jumla ya shilingi bilioni 4.0 fedha za ndani zimetengwa.

 

3.3.5.7. Hifadhi na Kinga  ya Jamii

(a)         Mradi Na. 6575: Kuimarisha uwezo wa kujiandaa na kukabili Maafa 

Shughuli zitakazotekelezwa ni: kuzijengea uwezo Kamati tano (5) za Usimamizi wa Maafa na waratibu wa maafa katika Mikoa mitano; kuandaa na kutekeleza mkakati wa utafutaji wa rasilimali kwa ajili kukabiliana na dharura za Maafa; kuandaa mipango ya kuzuia na kujiandaa na maafa kwenye miradi mikubwa ya kimkakati; kutekeleza mpango wa kutoa elimu kwa umma juu ya masuala ya maafa; na kuratibu shughuli za kuzuia, kujiandaa, kukabili na kurejesha hali baada ya maafa kupitia Mfuko wa Maafa. Jumla ya shilingi bilioni 2.55 fedha za ndani zimetengwa.

 

(b)         Mradi Na. 6327: Ujenzi na Ukarabati wa Majengo ya Serikali

Mradi wa Ujenzi wa Kituo cha Usimamizi wa Maafa Nchini 

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kuendelea na awamu ya pili ya ujenzi wa kituo cha Usimamizi wa Maafa Nzuguni (Dodoma) ambao unahusisha ujenzi wa jengo la utawala, jengo la operesheni na mawasiliano ya dharura, kituo cha matangazo kwa umma na uzio. Jumla ya shilingi bilioni 3.75 fedha za ndani zimetengwa.

 

(c)         Ujenzi wa Kituo cha Taifa cha Utengamao (National Rehabilitation Centre)

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kuanza kwa awamu ya kwanza ya ujenzi wa Kituo cha Taifa cha Utengamao (National Rehabilitation Centre) cha waraibu wa dawa za kulevya eneo la Itega, Dodoma, ujenzi wa karakana mbili (2), ujenzi wa jiko na ukumbi wa chakula, ujenzi wa mabweni mawili (2) na ujenzi wa Ofisi za Wakufunzi; na ununuzi wa vifaa na samani. Jumla ya shilingi bilioni 2.0 fedha za ndani zimetengwa.

 

(d)         Mradi Na. 6220: Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini 

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kufanya zoezi la kuhakiki na kutambua hali za ustawi wa maisha ya kaya za walengwa wa Mpango zipatazo 380,000 iwapo zimeimarika kiuchumi kwa kutumia vigezo vya umaskini na utaratibu uliokubaliwa kitakwimu kwenye maeneo yote ya utekelezaji 186; Kuendelea kuhawilisha ruzuku kwa kaya maskini 972,603 zinazokidhi vigezo vya Mpango; na Kuwezesha uundaji wa vikundi vya kuweka akiba na kuwekeza katika mamlaka za utekelezaji 67 ambapo jumla ya vikundi 16,000 vya jamii vinatarajiwa kuundwa na kuwawezesha walengwa kuanzisha shughuli za kiuchumi na kaya zilizofikia hatua hiyo kupatiwa ruzuku ya kuboresha biashara zao. Jumla ya shilingi bilioni 4.0 fedha za ndani na bilioni 96.79 fedha za nje zimetengwa.

 

3.3.6. Kuendeleza Rasilimali Watu 

3.3.6.1. Ujuzi na Uwezeshaji

(a)         Mradi Na. 6581: Programu ya Taifa ya Kukuza Ujuzi Nchini 

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kukuza ujuzi kwa Wafanyakazi 200 katika sekta mbalimbali (Up-skilling and Re-Skilling), kutoa mafunzo yanayohusu Uchumi wa Buluu kwa vijana 400, kutoa mafunzo ya ujuzi mbalimbali (Apprenticeship) kwa vijana 4,500, kuimarisha vituo vya maendeleo ya vijana kwa kuweka miundombinu muhimu (Common facilities for youth development), kuwezesha wajasiriamali wadogo 300 kuboresha ujuzi wa biashara na kuyafikia masoko ya ndani na kimataifa, kuandaa Mfumo wa Taarifa za ajira (National Labour Market Information System, kufanya ufuatiliaji na tathmini ya utekelezaji wa Mradi wa kukuza ujuzi nchini, kutoa mafunzo ya kutafuta kazi na kutoa ushauri wa ufundi na taaluma kwa wahitimu 20,000 kuhusu matarajio ya waajiri na sifa za ajira, kufanya usaili kuwaunganisha wahitimu 2,000 wa mafunzo kwa vitendo na fursa za ajira, kutoa mafunzo maalum (Tailor made special skill trainings) kwa watafuta kazi 500 ili kuwawezesha kupata kazi maalum nje ya nchi, kutoa mafunzo kwa watafuta kazi 5,000 kwa lengo la kupata kazi nje ya nchi (Pre Departure trainings), na kuwezesha gharama za usafiri kwa Wahitimu 1,000 waliyopo katika sekta za kimkakati. Jumla ya shilingi bilioni 36.0 fedha za ndani zimetengwa.

 

(b)         Mradi Na. 4952: Mfuko wa Maendeleo ya Vijana 

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kuendelea kutoa mikopo kwa vikundi vya vijana vilivyokidhi vigezo kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Vijana (Youth Development Fund – YDF); kutoa mafunzo ya kuwajengea uwezo vijana 1,480 na Maafisa Maendeleo ya Vijana 210 kutoka Sekretarieti za Mikoa na Halmashauri na kufuatilia utekelezaji wa miradi ya vijana ya kimkakati inayopata mikopo kutoka Mfuko wa maendeleo ya Vijana. Jumla ya shilingi bilioni 1.0 fedha za ndani zimetengwa.

 

(c)         Mradi Na. 6205: Programu ya Taifa ya Kukuza Kazi za Staha

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kuratibu na kuwezesha mapitio ya Sera ya watu wenye Ulemavu, Kuwezesha ujumuishwaji wa suala la utumikishwaji wa mtoto katika Mipango na Bajeti katika ngazi ya Halmashauri, kutoa mafunzo kuhusu ujuzi wa usimamizi na uendeshaji wa vyama vya wafanyakazi ili kuimarisha mahusiano mema mahali pa kazi, kutoa mafunzo ya kuwajengea uwezo wa kufundisha elimu ya stadi za maisha maafisa wa maendeleo ya vijana 210 na Waelimishaji rika 150 ambao watatoa mafunzo kwa vijana 23,324 na kufanya Mapitio ya Sera ya watu wenye ulemavu. Jumla ya shilingi bilioni 1.0 fedha za ndani zimetengwa.

 

(d)         Mradi Na. 4954: Ujenzi na Ukarabati wa Vituo vya Ufundi kwa Watu Wenye Ulemavu

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kuendelea na ujenzi wa Kituo cha Ufundi Stadi cha Watu Wenye Ulemavu katika Mkoa wa Mwanza na kuendelea na ujenzi wa vituo vya ufundi Stadi vya Watu Wenye Ulemavu katika Mikoa ya Songwe, Ruvuma na Kigoma. Jumla ya shilingi bilioni 3.41 zimetengwa. 

 

3.3.7. Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi

Katika mwaka 2023/24 kiasi cha shilingi bilioni 2.82 zimetengwa kwa lengo la kufanikisha maandalizi ya miradi ya PPP; kujenga uwezo wa Mamlaka za Serikali katika kuandaa miradi ya PPP; kujenga uwezo wa maafisa wanaosimamia miradi ya PPP nchini; kujenga uwezo wa Wizara, Idara Zinazojitegemea, Wakala wa Serikali, Taasisi na Mashirika ya Umma, Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa kuhusu usimamizi wa miradi ya PPP na kuwezesha utekelezaji wa miradi ya PPP ambayo imefanyiwa uchambuzi na kuonesha ina manufaa makubwa kiuchumi isipokuwa haina faida kibiashara (Viability Gap Funding). 

 

Aidha, shughuli mahsusi zitakazotekelezwa katika baadhi ya miradi mbalimbali ya PPP ni pamoja na:

 

(i)            Kuendelea na majadiliano ya mkataba wa kuwezesha utekelezaji wa mradi wa mabasi yaendayo haraka jijini Dar es Salaam awamu ya kwanza;

(ii)           Kukamilisha  ununuzi wa mbia wa miradi ya ujenzi wa Hoteli ya Nyota Nne na

Jengo la Biashara katika Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere;

(iii)         Kukamilisha taarifa ya upembuzi yakinifu na kuanza ununuzi wa mbia wa mradi wa Ujenzi wa Hosteli za wanafunzi wa Chuo cha Elimu ya Biashara katika Kampasi Dar es Salaam;

(iv)         Kuendelea na maandalizi ya taarifa ya upembuzi yakinifu wa mradi wa Ujenzi wa Hosteli za wanafunzi wa Chuo cha Uhasibu Kampasi za Dar es Salaam na Mbeya;

(v)          Kuanza ununuzi wa mbia wa mradi wa Kuimarisha Huduma za Saratani nchini kwa kujenga Kituo cha Ubingwa Bobezi wa Tiba ya Saratani eneo la Mloganzila (Ultra- Modern Oncology Centre - UMOC) na Kituo cha Saratani Mbeya (Mbeya Cancer Centre - MCC) eneo la Iwambi - Mbeya;

(vi)         Kuendelea na ununuzi wa mbia wa miradi ya ujenzi wa barabara ya tozo kutoka Kibaha - Chalinze - Morogoro (km 205) kwa kipande cha Kibaha – Chalinze (km 78.9) na kuendelea na maandalizi ya taarifa ya upembuzi yakinifu wa kipande cha Chalinze – Morogoro (km 126.1);

(vii)        Kukamilisha taarifa ya upembuzi yakinifu wa awali na taarifa ya upembuzi yakinifu wa mradi wa barabara ya tozo Mbeya By - pass (Uyole – Sogwe 48.9km); 

(viii)      Kukamilisha maandalizi ya nyaraka za zabuni na kuanza  ununuzi wa Mbia wa mradi wa Ukaguzi wa Lazima wa Vyombo vya Moto; na

(ix)         Kukamilisha taarifa ya upembuzi yakinifu wa awali na kuandaa taarifa ya Upembuzi Yakinifu wa mradi wa ujenzi wa Kituo cha Mazoezi Tiba Mbweni Dar es Salaam.

 

3.3.8. Uwekezaji katika Taasisi na Mashirika ya Umma

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kuweka mfumo madhubuti wa ukusanyaji mapato, kusimamia matumizi; kuendelea kufanya ufuatiliaji na tathmini kwenye mikataba ya utendaji kazi ili kuhakikisha Uwekezaji wa Serikali unakuwa na tija zaidi; na kufanya tathmini ya kina kwenye maeneo yaliyobinafsishwa ili kubainisha faida na changamoto kwa wawekezaji pamoja na upande wa Serikali. 

 

 


 


SURA YA NNE

 

UGHARAMIAJI WA MPANGO WA MAENDELEO WA TAIFA 2023/24

 

4.1. Utangulizi

Sura hii inaainisha mikakati ambayo Serikali itachukua ili kuhakikisha kuwa ukusanyaji wa mapato kutoka vyanzo mbalimbali vinafikiwa katika ugharamiaji wa Mpango wa  Maendeleo  wa Taifa wa Mwaka 2023/24 kama ilivyoainishwa katika Mkakati wa Ugharamiaji wa Mpango wa Tatu wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano 2021/22 – 2025/26. Katika kutekeleza vipaumbele vilivyopo katika Mpango, Serikali itahakikisha inatenga  rasilimali fedha za kutosha za kugharamia Mpango ili kufikia malengo yaliyowekwa.

 

4.2. Ugharamiaji wa Utekelezaji wa Mpango wa Maendeleo wa Taifa 2023/24

Katika mwaka 2023/24 Serikali imetenga shilingi bilioni 14,077.2 kwa ajili ya kugharamia shughuli mbalimbali za maendeleo. Kati ya fedha hizo, shilingi bilioni 10,795.1 sawa na asilimia 77.0 ya bajeti ya maendeleo ni fedha za ndani na shilingi bilioni 3,282.1 sawa na asilimia 23 ya bajeti ya maendeleo ni fedha za nje. Fedha hizi zitakusanywa kutoka katika mapato ya kodi na yasiyo ya kodi, misaada na mikopo nafuu, mikopo ya ndani na mikopo ya nje yenye masharti ya biashara. Aidha, Serikali itaendelea kushirikiana na sekta binafsi katika kutekeleza miradi ya maendeleo ikiwemo kupitia utaratibu wa ubia kati ya sekta ya umma na sekta binafsi (PPP) ili kuongeza kasi ya uatekelezaji wa miradi ya maendeleo kupitia ushiriki wa sekta binafsi.

 

4.3. Mikakati ya Vyanzo vya Mapato ya Kugharamia Mpango kwa Mwaka 2023/24

Katika kugharamia Mpango wa  Maendeleo  wa Taifa wa Mwaka 2023/24, vyanzo vya mapato vitakavyotumika ni mapato ya kodi na yasiyo ya kodi, mapato ya Mamlaka ya Serikali za Mitaa, ubia kati ya sekta ya umma na sekta binafsi, mikopo na misaada pamoja na vyanzo mbadala vya ugharamiaji wa  miradi ya maendeleo.

 

4.4. Mapato ya Ndani 

4.4.1. Mapato ya Kodi na Yasiyo ya Kodi

Serikali itaendelea kuimarisha usimamizi wa mapato ya kodi na yasiyo ya kodi kutoka katika vyanzo mbalimbali vya ndani ili kuwezesha kufikia malengo yaliyowekwa kwa kuchukua hatua zifuatazo: 

(i)         Kuimarisha ukusanyaji na usimamizi wa mapato ya kodi kwa kuhakikisha wafanyabiashara wanatoa risiti za kielektroniki wanapouza bidhaa na wateja wanadai risiti wanaponunua bidhaa;

(ii)       Kuendelea kutoa elimu ya kodi kwa mlipakodi kupitia vyombo vya habari, mitandao ya kijamii, semina na warsha; 

(iii)      Kupanua wigo wa kodi kwa kuwatambua na kuwasajili wafanyabiashara katika mfumo rasmi wa ulipaji kodi kupitia kampeni ya Mlango kwa Mlango; 

(iv)      Kuendelea kutumia Mpango wa Usimamizi wa Viashiria Hatarishi (Compliance Risk Management Plan) ili kubaini na kutambua wakwepaji wa kodi; 

(v)       Kuimarisha ushirikiano baina ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na vyombo vya ulinzi na usalama nchini ili kudhibiti bidhaa za magendo na tatizo la ukwepaji wa kodi katika mipaka yote ya Tanzania;

(vi)      Kuimarisha mazingira rafiki ya  ulipaji kodi kwa hiari kwa kuboresha na kuhimiza matumizi sahihi ya mifumo ya TEHAMA ikiwa ni pamoja na kuboresha mifumo itakayosaidia kurahisisha ulipaji kodi; 

(vii)    Kuhamasisha ulipaji  kodi  katika sekta isiyo rasmi  kwa kuijumuisha kwenye mfumo rasmi wa ulipaji kodi; 

(viii)   Kurasimisha shughuli zisizo rasmi zikiwemo shughuli za wajasiriamali wadogo kwa kuwatengea maeneo maalum; 

(ix)      Kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji ili kuvutia wawekezaji wapya, kukuza biashara ndogo na za kati kwa ukuaji endelevu wa uchumi  utakaowezesha kuongeza wigo wa kodi; 

(x)       Kufanya tafiti katika maeneo mapya ambayo yanaweza kuwa vyanzo vya  mapato;

(xi)      Kuimarisha usimamizi wa tozo na ada mbalimbali ili kuhakikisha zinakusanywa na kuwasilishwa kwenye Mfuko Mkuu wa Serikali;

(xii)    Kuimarisha Mfumo wa Kielektroniki wa Kufuatilia Mizigo inayokwenda nchi jirani (Eletronic Cargo Tracking System) ili kuzuia uwezekano wa kuingiza bidhaa hizo katika soko la ndani na kuikosesha Serikali mapato; 

(xiii)   Kuendelea kusimamia Mfumo wa Serikali wa Kielektroniki wa Ukusanyaji wa Mapato (Government Electronic Payment Gateway- GePG) ili kurahisisha ulipaji na kudhibiti upotevu wa mapato; 

(xiv)   Kuimarisha mfumo wa Dirisha Moja la Kielektroniki la Uondoshaji wa Mizigo Bandarini (e-Single Window System) ili kurahisisha uondoshwaji wa mizigo katika vituo vya mipakani pamoja na kupunguza gharama za kufanya biashara nchini; 

(xv)    Kuimarisha na kufungamanisha Mfumo wa Usimamizi wa Mapato ya Ndani (Integrated Domestic Revenue Administration System - IDRAS) utakaounganisha mifumo yote ya ukusanyaji wa mapato ya ndani ya Serikali ili kuimarisha usimamizi wa mapato yatokanayo na kodi za ndani nchini; 

(xvi)   Kuboresha Mfumo wa mawasiliano kati ya NIDA na TRA  ili kurahisisha usajili na ufuatiliaji wa walipakodi; na

(xvii) Kuimarisha usimamizi wa Mashirika, Taasisi za Umma na Wakala za Serikali ili kuongeza ufanisi na kuhakikisha gawio na michango stahiki inawasilishwa kwa wakati.

 

4.5. Mikopo na Misaada

4.5.1. Mikopo ya Nje 

Serikali itaendelea na majadiliano na Taasisi mbalimbali za nje ya nchi ili kuhakikisha  kiasi cha mikopo ya nje kilichopangwa kwa mwaka 2023/24 kinafikiwa. Aidha, Serikali itaendelea kuchukua jitihada za kuongeza ukusanyaji wa mapato ya ndani . Sanjari na hilo, Serikali itaendelea kujikita kwenye Mkakati wa Usimamizi wa Madeni  wa Muda wa Kati 2022/23-2024/25 (Medium Term Debt Strategy-MTDS) kwa kukopa zaidi mikopo yenye masharti nafuu na kuziba pengo la upungufu utakaojitokeza kwa kukopa mikopo yenye masharti ya kati kwa utaratibu wa udhamini kutoka taasisi za udhamini wa mikopo (Export Credit Agencies - ECAs), ambayo masharti yake yana unafuu ikilinganishwa na mikopo ya kibiashara.

 

4.5.2. Mikopo ya Ndani 

Katika mwaka 2023/24, Serikali itaendelea kukopa katika soko la ndani kupitia hatifungani za Serikali kwa kuzingatia Mkakati wa Muda wa kati wa Usimamizi wa Madeni 2022/23-2024/25. Vilevile, katika muda wa kati, Serikali itatumia hatifungani za muda mrefu na mfupi ili kupunguza gharama na viatarishi kwenye deni la Serikali. Serikali itaendelea na mikakati mbalimbali ili kuhakikisha kuwa kiasi kilichopangwa kukopwa katika soko la ndani kinapatikana bila kuathiri ukopaji wa sekta binafsi na kuongeza ushindani. Mikakati hiyo ni pamoja na kutoa elimu zaidi kwa nchi wanachama wa SADC na watanzania waishio nje ya nchi (Diaspora) ili waweze kuwekeza katika dhamana za Serikali.

 

4.5.3. Misaada ya Nje

Ushirikiano baina ya Serikali na Washirika wa Maendeleo utaendelea kuimarika kwa kutekeleza kikamilifu Mwongozo wa Ushirikiano wa Maendeleo (Development Cooperation Framework – DCF) pamoja na Mpango Kazi wake. Serikali itaendelea kuimarisha usimamizi wa matumizi ya fedha kutoka kwa Washirika wa Maendeleo ikiwemo fedha zinazopelekwa moja kwa moja kwa watekelezaji wa miradi ya maendeleo kupitia mfumo wa D-Fund Management Information System. Aidha, Serikali itaendelea kuibua miradi na kufanya majadiliano na Washirika wa Maendeleo ili kuwezesha upatikanaji wa fedha za kufadhili miradi mbalimbali ya maendeleo.

 

4.6. Vyanzo Mbadala na Bunifu vya Kugharamia Miradi ya Maendeleo 

Serikali kwa kutambua umuhimu wa kupunguza utegemezi wa fedha za kutekeleza Miradi ya Maendeleo kupitia bajeti kuu, kupitia Mkakati wa Kugharamia Miradi kwa Njia Mbadala (APF) miradi yenye uwezo wa kujiendesha kibiashara (Commercially Viable project) itawezeshwa kukopa kutoka vyanzo mbalimbali vilivyopo katika sekta ya fedha ikiwa ni pamoja na: benki na taasisi za fedha, hatifungani mbalimbali, na mikopo ya Karadha. Mwongozo wa kuandaa maandiko ya Miradi inayoweza kujiendesha kibiashara kwa kutumia vigezo vya APF wa Mwaka, 2021 (National Guideline for Developing and Financing Income – Generating Infrastructure Investment, 2021) umeandaliwa na Mwongozo za Kusimamia utekelezaji wa Miradi itakayotekelezwa kwa njia ya APF (Special Purpose Vehicles - SPV) utakamilishwa. Katika mwaka 2023/24, Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Tanga (TangaUWASA) itaendelea kukamilisha taratibu za kutoa hatifungani ya kijani (Green bond) kwa ajili ya kugharamia miradi ya miundombinu ya maji ambapo Mshauri Kiongozi wa Miamala (Lead Transation Advisor) Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) inaandaa Hati ya Taarifa kwa ajili ya kutoa hati fungani ya kwanza kwa ajili ya miundombinu ya maji.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

SURA YA TANO

 

UFUATILIAJI, TATHMINI NA UTOAJI WA TAARIFA

 

5.1. Utangulizi 

Ufuatiliaji na Tathmini (U&T) ni nyenzo muhimu ya kuiwezesha Serikali kupima hatua iliyofikiwa katika utekelezaji wa programu na miradi ya maendeleo kwa kulinganisha malengo na vipaumbele vilivyowekwa ili kufanya maamuzi yanayoongozwa na uwepo wa taarifa sahihi na kwa wakati. U&T pia husaidia kupima mwelekeo wa kufikia malengo na matokeo tarajiwa yaliyowekwa katika Mpango wa Tatu wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano (2021/22- 2025/26). Kwa msingi huo, Serikali itaendelea kuimarisha uratibu na usimamizi wa utekelezaji wa Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2023/24 kupitia Mwongozo wa Kitaifa wa Ufuatiliaji na Tathmini ya Miradi ya Maendeleo wa Mwaka 2022; Mkakati wa Ufuatiliaji na Tathmini wa Mpango wa Tatu wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano 2021/22 –

2025/26; Mwongozo wa Maandalizi ya Mpango na Bajeti ya Serikali kwa Mwaka 2023/24; Mwongozo wa Usimamizi wa Uwekezaji wa Umma; Sheria ya Bajeti, Sura 439; Mpango Kazi na Mtiririko wa Mahitaji ya Fedha; Waraka Na. 5 wa Hazina wa Mwaka 2020/21 Kuhusu Matumizi ya Mfumo wa Kitaifa wa Kusimamia Miradi ya Maendeleo (NPMIS); na Waraka Na. 1 wa Hazina kuhusu Utekelezaji wa Bajeti.

 

Ufuatiliaji, tathmini na utoaji wa taarifa utafanyika katika ngazi mbalimbali ambapo katika kila ngazi itaandaliwa taarifa ambayo itawasilishwa kupitia Mfumo wa Kitaifa wa Kusimamia Miradi ya Maendeleo baina ya watekelezaji na waratibu wa miradi na programu za maendeleo. Taarifa hizo zitajumuisha: taarifa za utekelezaji wa miradi za kila robo mwaka; na taarifa za ufuatiliaji na tathmini. Taarifa za ufuatiliaji na Tathmini ziandaliwe kwa kuzingatia viashiria vilivyowekwa katika mfumo madhubuti au bangokitita la mradi (Logframe) na kuziwasilisha kila mwezi kupitia NPMIS. Aidha, watekelezaji wote wa miradi ya maendeleo wanatakiwa kuzingatia maelekezo ya Waraka Na. 5 wa Hazina wa mwaka 2020/21 kuhusu NPMIS.   

 

5.2. Misingi na Mbinu za Ufuatiliaji na Tathmini

Wizara, Idara Zinazojitegemea, Wakala wa Serikali, Taasisi na Mashirika ya Umma, Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa, zina wajibu wa kuzingatia maelekezo kuhusu misingi na mbinu kama zilivyoainishwa katika Mwongozo wa Kitaifa wa Ufuatiliaji na Tathmini ya Miradi ya Maendeleo (National Monitoring and Evaluation Framework) wa Mwaka 2022. Mwongozo wa Ufuatiliaji na Tathmini utawezesha kupatikana kwa taarifa za utekelezaji kwa lengo la kuwezesha watunga sera, wafanya maamuzi na wadau muhimu kufahamu mwenendo wa utekelezaji mipango, miradi na programu za maendeleo kwa kuainisha hatua iliyofikia pamoja na mafanikio na changamoto ya utekelezaji wa malengo.

 

5.3. Matokeo ya Ufuatiliaji na Tathmini 

Matokeo ya ufuatiliaji na tathmini ya utekelezaji wa miradi na programu za maendeleo yatasaidia kubaini hatua iliyofikiwa katika utekelezaji, mafaniko, kuainisha changamoto na mapendekezo ya kuzitatua. Aidha, taasisi zote zinazofanya ufuatiliaji na tathmini zinaelekezwa kutoa mrejesho baada ya kufanya ufuatiliaji kwa wadau wote wanaohusika na utekelezaji miradi kwa lengo la kufuatilia utekelezaji wa mapendekezo yaliyobainishwa.

 

5.4. Muundo wa Taarifa za Ufuatiliaji na Tathmini

Wizara, Idara Zinazojitegemea, Wakala wa Serikali, Taasisi na Mashirika ya Umma, Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa zinatakiwa kuzingatia Mwongozo wa Kitaifa wa Ufuatiliaji na Tathmini ikiwa ni pamoja na: mawanda na malengo ya mradi, hali ya utekelezaji, taarifa za ugharamiaji, taarifa za mikataba, changamoto na mapendekezo ya kukabiliana na changamoto hizo. Aidha, muundo wa Taarifa ya Ufuatiliaji na Tathmini ya Mpango wa Tatu wa Taifa wa Miaka Mitano utatolewa na Idara ya Mipango ya Kitaifa na kujadiliwa na wadau kila mwaka. Vilevile, muundo wa Taarifa hiyo utajielekeza kufanya uchambuzi wa matokeo tarajiwa yaliyoainishwa katika maeneo ya kipaumbele ya Mpango wa Tatu wa Taifa wa Miaka Mitano.

 

5.5. Mgawanyo wa Majukumu

Ufuatiliaji na Tathmini ni suala mtambuka kwa sababu linahusisha wadau mbalimballi katika ngazi tofauti. Ushirikishwaji wa wadau muhimu katika kufanikisha ufuatiliaji, tathmini na utoaji wa taarifa za utekelezaji wa Mpango ni suala la msingi na la kipaumbele kwa Serikali. Aidha, mgawanyo wa majukumu umefafanuliwa vyema katika Mwongozo wa Kitaifa wa Ufuatiliaji na Tathmini ya Miradi ya Maendeleo ambao umeainisha wadau mbalimbali na majukumu yao mahsusi katika ufuatiliaji na tathmini ili  kuhakikisha ufasaha na ufanisi unazingatiwa katika kuhakikisha kwamba utekelezaji wa miradi unafuatiliwa na kufanyiwa tathmini ipasavyo. Kwa upande wa kufuatilia matokeo yaliyoainishwa katika Mpango wa Tatu wa Taifa wa Miaka Mitano, mgawanyo wa majukumu umeainishwa katika Mkakati wa Ufuatiliaji na Tathmini ya Mpango wa Miaka Mitano. Ufuatiliaji huo utafanyika kwa kutumia uchambuzi wa kina juu ya matokeo tarajiwa kupitia tafiti na takwimu zilizozalishwa na wadau mbalimbali ikiwemo  Wizara, Idara Zinazojitegemea, Wakala wa Serikali, Taasisi na Mashirika ya Umma, Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa. 

  

SURA YA SITA

 

VIHATARISHI NA MIKAKATI YA KUKABILIANA NAVYO

 

6.1. Utangulizi

Malengo ya utekelezaji wa Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2023/24 yanaweza yasifikiwe kama ilivyopangwa ikiwa vihatarishi na mikakati ya kukabiliana navyo haitabainishwa na kutekelezwa sanjari kupitia mipango ya Serikali. Vihatarishi vinaweza kusababisha mradi kutotekelezwa, kutekelezwa chini ya kiwango, kuongezeka gharama au kutokamilika kwa wakati. Ili kuhakikisha malengo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2023/24 yanafikiwa kwa ufanisi, Mpango huu umezingatia Mwongozo wa Kuandaa Mfumo wa Usimamizi wa Vihatarishi katika Sekta ya Umma wa Mwaka 2012, ambapo Serikali itahakikisha utekelezaji wa Mpango unaenda sambamba na utekelezaji wa mikakati ya kukabiliana na vihatarishi vinavyoweza kujitokeza. Aidha, vihatarishi vinavyoweza kuukabili Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2023/24 vimegawanyika katika makundi makuu mawili (2). Makundi hayo ni vihatarishi vya ndani vitakavyotokana na utendaji au mifumo ya Serikali na vihatarishi vya nje vitakavyotokana na masuala yaliyoko nje ya udhibiti wa Serikali.

 

6.2. Vihatarishi vya Ndani na Nje na Mikakati ya Kukabiliana Navyo

Vihatarishi vya Ndani: Hivi ni vihatarishi ambavyo nchi ina uwezo wa kuvizuia kutokea. Vihatarishi hivyo ni pamoja na: Ufinyu wa rasilimali fedha kwa ajili ya kugharamia utekelezaji wa miradi ya maendeleo; ushiriki mdogo wa sekta binafsi katika kutekeleza mipango ya maendeleo; upotevu wa mapato ya Serikali yanayotokana na biashara mtandao; mabadiliko ya viwango vya riba katika soko la fedha la ndani; uharibifu wa mazingira kutokana na shughuli za binadamu; vitendo vya rushwa na ubadhilifu wa rasilimali. Serikali ina uwezo wa kudhibiti kutokea au kukabili athari za vihatarishi hivi kupitia utekelezaji wa mikakati iliyowekwa.

 

Vihatarishi vya Nje: Hivi ni vihatarishi ambavyo nchi haina uwezo wa kuvizuia kutokea. Vihatarishi hivyo ni pamoja na: Mabadiliko ya tabia ya nchi, majanga ya asili na magonjwa ya mlipuko; Mdororo na Mitikisiko ya Kiuchumi duniani; kuongezeka kwa kiwango cha riba katika masoko ya kimataifa; Migogoro na hali ya siasa inayojitokeza kwa nchi jirani, kikanda na kimataifa; na Kuongozeka kwa kasi ya mabadiliko ya teknolojia. Mikakati ya kukabiliana na vitaharishi hivi ipo ndani ya uwezo wa Serikali. Serikali haina udhibiti wa kutokea kwa vihatarishi bali ina uwezo wa kupunguza athari zitakazosababishwa kupitia utekelezaji wa mikakati iliyowekwa. Uchambuzi wa vihatarishi vya ndani na nje pamoja na mikakati ya kukabiliana navyo umeainishwa katika Jedwali Na. 7 na 8.

 

 

 

Jedwali 7: Vihatarishi vya Ndani na Mikakati ya Kukabiliana Navyo

NA.

KIHATARISHI

ATHARI 

MIKAKATI

1.

Ufinyu wa rasilimali fedha kwa ajili ya

kugharamia

utekelezaji   wa miradi         ya maendeleo.

(i)      Kutokutekelezwa kwa mradi au kutekelezwa kwa kasi ndogo na hivyo kutokamilika kwa

wakati;

(ii)    Kuongezeka      kwa gharama za mradi; na

(iii)   Kuchelewa kwa upatikanaji wa huduma zilizotarajiwa.

 

 

(i)      Kuimarisha sera za ukusanyaji na usimamizi wa mapato ikiwemo kuhakikisha kila mfanyabiashara anatoa risiti ya kielektroniki anapouza na mnunuzi anadai risiti anaponunua bidhaa au huduma;

(ii)    Kuongeza wigo wa walipa kodi kwa kuhamasisha sekta isiyo rasmi kujumuishwa katika mfumo rasmi wa

ulipaji kodi;

(iii)   Kudhibiti upotevu wa mapato kwa kusimamia ipasavyo mifumo ya ukusanyaji, ikiwemo Mfumo wa Serikali wa Kielektroniki wa Ukusanyaji wa Mapato (Government Electronic Payment Gateway - GePG);

(iv)   Kutekeleza miradi ya maendeleo       kwa

utaratibu wa PPP;

(v)    Kuimarisha utekelezaji wa miradi ya kimkakati yenye kuongeza mapato ya Mamlaka za

Serikali za Mitaa;

(vi)   Kuimarisha sekta ya fedha na kuendeleza soko la fedha la ndani

(domestic debt market)

 

NA.

KIHATARISHI

ATHARI 

MIKAKATI

 

 

 

        ili                kuwezesha

upatikanaji wa mikopo;

(vii) Kupata fedha kupitia mikopo yenye masharti nafuu; na

(viii)       Matumizi ya Vyanzo Mbadala na bunifu vya utekelezaji wa mradi.

2.

Ushiriki mdogo wa Sekta binafsi katika kutekeleza

mipango maendeleo

ya

(i)      Uwekezaji mdogo wa Sekta binafsi katika miradi ya kimkakati; na

(ii)    Kasi ndogo ya utekelezaji wa miradi kutokana na uhaba wa mitaji, teknolojia na mazingira duni ya kufanya biashara;

(i)      Kufanya majadiliano na Sekta binafsi ili kuweka mikakati ya kutatua changamoto

zinazowakabili;

(ii)    Kuendelea kuboresha mazingira wezeshi ya biashara ili kuvutia uwekezaji katika maeneo yanayofaa kwa

Sekta binafsi;

(iii)   Kuendelea kuandaa miundombinu wezeshi katika maeneo mapya  ya uwekezaji; na

(iv)   Kuziwezesha kifedha taasisi za Serikali kupitia Mfuko wa Uwezeshaji  wa Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi kufanya upembuzi yakinifu kwa miradi ya PPP na kuiuza kwa Sekta Binafsi kwa ajili ya uwekezaji.

3.

Upotevu wa mapato ya Serikali yanayotokana na biashara ya

mtandaoni

(i)      Kupungua kwa mapato

ya Serikali; na

(ii)    Kasi ndogo ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo

(i)      Kuongeza matumizi ya kidigitali katika ukusanyaji wa kodi; na

(ii)    Kudhibiti upotevu wa mapato kwa kuboresha usimamizi wa mifumo

 

NA.

KIHATARISHI

ATHARI 

MIKAKATI

 

 

 

ya kisheria iliyopo.

4.

Mabadiliko ya viwango vya riba katika soko la fedha

(i)      Kuongezeka kwa matumizi ya malipo ya riba na nakisi ya bajeti;

(ii)    Serikali kutumia fedha kutoka kwenye vifungu vingine vya bajeti kugharamia malipo ya

riba; na

(iii)   Sekta binafsi kutofikia malengo ya mikopo na hivyo kupungua kwa shughuli za kiuchumi na kusababisha Serikali kukosa mapato.

(i)      Kuendelea    kutekeleza

        Sera        za        fedha

zitakazowezesha viwango vya riba kuwa himilivu;

(ii)    Kuimarisha ukusanyaji wa mapato ya ndani na kudhibiti matumizi yasiyo ya lazima ili kupunguza utegemezi katika misaada na

mikopo kutoka nje; na

(iii)   Kuimarisha       soko   la fedha la ndani.

5.

  Uharibifu         wa

Mazingira

kutokana na shughuli za binadamu.

(i)      Kubadilika kwa hali ya hewa na kusababisha uharibifu wa miundombinu kutokana na mvua nyingi;

(ii)    Kutoweka kwa bioanuai;

(iii)   Kuongezeka kwa gharama za utoaji wa huduma za afya kutokana na kuongezeka kwa magonjwa yanayotokana na uharibifu wa mazingira; 

(iv)   Kuongezeka kwa gharama za kurejesha mazingira katika hali ya awali na hivyo kuathiri utekelezaji wa miradi iliyopangwa; na

(v)    Kupungua kwa uzalishaji wa mazao na bidhaa viwandani.

(i)      Kutoa elimu kwa wananchi juu ya umuhimu wa kutunza mazingira ili kudhibiti uharibifu unaotokana na shughuli za

kibinadamu;

(ii)    Kuhamasisha wananchi kupunguza matumizi ya kuni na mkaa.

(iii)   Kudhibiti uharibifu wa  uoto wa asili na bioanuai;

(iv)   Kuimarisha usimamizi wa mazingira katika maeneo ya vyanzo vya maji na misitu; na

(v)    Kutekeleza ipasavyo miongozo na kanuni za usimamizi wa mazingira.

NA.

KIHATARISHI

ATHARI 

MIKAKATI

6.

Vitendo rushwa ubadhilifu rasilimali 

vya na wa

(i)     Upotevu wa fedha za umma;

(ii)    Miradi kutekelezwa chini ya kiwango; 

(iii)   Kuongezeka kwa muda na gharama za utekelezaji wa miradi; na

(iv)  Kasi ndogo ya ukuaji wa sekta binafsi katika kutekeleza miradi ya Maendeleo.

(i)     Kuimarisha utekelezaji wa sheria ya mapambano dhidi ya rushwa kwa wanaobainika kuhusika na vitendo vya rushwa;

(ii)    Kuimarisha shughuli za ufuatiliaji na tathmini ya miradi;

(iii)   Serikali kuendelea kuweka mazingira wezeshi ya biashara yaliyoboreshwa na yenye uwazi ili kuruhusu sekta binafsi kushamiri na kurasimisha sekta isiyo rasmi; na

(iv)  Kuimarisha mfumo wa utoaji motisha kwa watoaji taarifa zinazohusiana na rushwa.

7.

Uhalifu wa kimtandao wa mifumo ya Serikali

(i)     Kuharibiwa kwa mifumo ya         kielektroniki ya

Serikali; na

(ii)    Upotevu wa mapato na taarifa.

(i)     Kuimarisha utekelezaji wa Sera ya Udhibiti wa Mifumo ya Kielektroniki ya Usimamizi wa Fedha za Umma;

(ii)    Kuimarisha usimamizi na udhibiti wa mifumo ya taarifa ya kielektroniki ya Serikali; na

(iii)   Kuimarisha usalama wa maeneo ya kuhifadhia kumbukumbu mbalimbali (Data recovery sites).

 

 

Jedwali 8: Vihatarishi vya Nje na Mikakati ya Kukabiliana Navyo

NA.

KIHATARISHI

ATHARI 

MIKAKATI

1.

Mabadiliko      ya

tabianchi, 

majanga ya asili         na magonjwa ya

mlipuko

(i)      Kupungua kwa kasi ya

ukuaji wa uchumi;

(ii)    Kuathiri mapato ikiwemo mapato ya kodi yatokanayo na kipato;

(iii)   Raslimali fedha kuelekezwa kukabiliana na majanga badala ya kuelekezwa kwenye miradi ya maendeleo kama

ilivyokusudiwa;

(iv)   Kuathiri ikolojia

(i)      Kuboresha mifumo ya kuzuia na kukabiliana na majanga; 

(ii)    Kuimarisha mifuko ya maafa;

(iii)   Kutekeleza na kuendelea kuridhia itifaki za kimataifa kuhusu utunzaji wa mazingira na mabadiliko ya

Tabianchi; na

(iv)   Kuimarisha utekelezaji wa Sera ya Taifa ya Mazingira ya Mwaka 2021.

2.

Mtikisiko na Mdororo wa

uchumi duniani

(i)      Kuathirika kwa mikopo na misaada kutoka kwa

washirika wa Maendeleo;

(ii)    Kukosekana kwa masoko ya uhakika ya bidhaa nje ya nchi;  

(iii)   Kupungua kwa uwekezaji kutoka nje ya nchi; na

(iv)   Kuongezeka kwa bei za bidhaa muhimu katika soko la dunia zikiwemo bidhaa za mafuta, malighafi na bidhaa za viwandani.

 

(i)      Kuimarisha mikakati ya kisera ili kukabiliana na mabadiliko ya kiuchumi

duniani;

(ii)    Kuendelea kuhamasisha ujenzi wa viwanda vinavyotumia malighafi za ndani na kuzalisha bidhaa zinazotumiwa na watu wengi nchini; na

(iii)   Kuimarisha ubora wa bidhaa zinazozalishwa nchini ili kuhimili ushindani katika masoko ya kimataifa.

3.

Migogoro na hali ya siasa isiyo imara ya nchi jirani, kikanda na kimataifa.

(i)      Kupanda kwa bei ya bidhaa muhimu katika soko la dunia kama bidhaa za petroli, mafuta ya kula, vyakula, mashine na mitambo;

(ii)    Kupungua kwa kasi ya

(i) Kuweka mazingira wezeshi kwa wawekezaji wa viwanda vinavyozalisha bidhaa kwa kutumia teknolojia na malighafi za ndani ili kupunguza

NA.

KIHATARISHI

ATHARI 

MIKAKATI

 

 

utekelezaji wa miradi ya maendeleo;

(iii)   Kuongezeka kwa gharama za utekelezaji wa miradi hususan inayotumia vifaa kutoka nje;

(iv)  Kupungua kwa uwekezaji wa mitaji ya kigeni ya moja kwa moja;

(v)    Kupungua kwa mikopo na misaada kutoka nje; na

(vi)  Kukosekana kwa masoko nje ya nchi kwa ajili  ya kuuza    bidhaa zinazozalishwa nchini.

        uagizaji     wa      bidhaa

kutoka nje; na

(ii) Kuendelea kuimarisha ushirikiano na nchi Jirani, kikanda na kimataifa ili kukuza masoko kwa ajili ya bidhaa zinazozalishwa viwandani.

4.

Kuongozeka kwa   kasi    ya mabadiliko   ya teknolojia

(i)     Mifumo ya kisheria, kisera, na kitaasisi iliyopo  kutoendana na mabadiliko ya teknolojia hivyo kuongezeka kwa gharama za uwekezaji katika mifumo ya teknolojia mpya; na

(ii)    Kupungua kwa uwezo wa kiushindani katika soko la kikanda na kimataifa. 

(i)     Kuendelea kuboresha mifumo ya kisheria, kisera na kitaasisi ili iendane na mabadiliko ya teknolojia duniani; na

(ii)    Kuendelea kuimarisha mikakati ya kuongeza ujuzi, uhawilishaji wa teknolojia na kuhamasisha ubunifu wa teknolojia kwa wataalam wa ndani.

5.

Wadau           wa

maendeleo

kutotekeleza

ahadi kwa wakati na

kiwango kilichoahidiwa

Kuchelewa kwa utekelezaji wa miradi.

Kubuni vyanzo vipya vya mapato kwa ajili ya kugharamia shughuli za maendeleo.

 

Kiambatisho A: Miradi Iliyofuatiliwa katika kipindi cha Julai 2022 hadi

Aprili 2023

 

NA.

SEKTA

MRADI

MKOA

 

1.

UCHUKUZI

UJENZI WA RELI YA KATI KWA STANDARD GAUGE

DAR ES SALAAM, MOROGORO, DODOMA, SINGIDA, TABORA,

SHINYANGA NA MWANZA

2.

UCHUKUZI

KUFUFUA SHIRIKA LA NDEGE TANZANIA (ATCL)

DAR ES SALAAM

3.

UJENZI

UJENZI WA MIUNDOMBINU YA MABASI YAENDAYO HARAKA (BRT) - AWAMU YA II

DAR ES SALAAM

4.

UVUVI

MRADI WA UJENZI WA BANDARI YA UVUVI KILWA

LINDI

5.

UJENZI

UJENZI WA DARAJA LA KIGONGO – BUSISI (M 3,200) NA BARABARA UNGANISHI (KM 1.66)

MWANZA

6.

NISHATI

MRADI WA KUZALISHA UMEME KWA KUTUMIA MAJI WA JULIUS NYERERE - MW 2,115: 

PWANI

7.

NISHATI

MRADI WA UJENZI WA BOMBA LA MAFUTA GHAFI AFRIKA MASHARIKI (EACOP)

TABORA

8.

VIWANDA

 UJENZI WA KIWANDA CHA SUKARI MKULAZI NA UENDELEZAJI WA SHAMBA LA MIWA - MKULAZI - MBIGIRI ESTATE

MOROGORO

9.

AFYA

HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA WA KATAVI

KATAVI

10.

ELIMU

MRADI WA UJENZI WA BWENI LA WASICHANA SHULE YA SITALIKE

KATAVI

11.

MADINI

MRADI WA USIMAMIZI RASILIMALI MADINI

KATAVI

12.

MAJI

UJENZI WA BWAWA LA MAJI KIJIJI CHA NSENKWA

KATAVI

13.

MAJI

MRADI WA MAJI SHANKALA

KATAVI

14.

MAJI

MRADI WA MAJI KIJIJI CHA VIKONGE

KATAVI

15.

UCHUKUZI

UNUNUZI WA RADA, VIFAA NA UJENZI WA

MIUNDOMBINU YA HALI YA HEWA MKOA WA KATAVI

KATAVI

16.

UTAWALA BORA

MAHAKAMA YA WILAYA TANGANYIKA

KATAVI

17.

MAJI

MRADI WA MAJI MKUTANO

LINDI

18.

MAJI

UJENZI WA MRADI WA MAJI MCHANGANI

LINDI

19.

MAJI

MRADI WA MAJI MAKANJIRO - RUANGWA

LINDI

20.

MAJI

MRADI WA MAJI KIWAWA

LINDI

21.

MAJI

MRADI WA MAJI MARENDEGO

LINDI

22.

NISHATI

MRADI WA USAMBAZAJI WA GESI ASILIA MIKOA YA DAR ES SALAAM, MTWARA, LINDI NA PWANI (LINDI)

LINDI

23.

UJENZI

BARABARA YA NACHINGWEA - RUANGWA - NANGANGA (KM 106): LOT 2 RUANGWA - NANGANGA (KM 53.2)

LINDI

24.

UTAWALA BORA

MRADI WA UJENZI WA OFISI ZA UHAMIAJI MKOA WA LINDI

LINDI

25.

UJENZI

UJENZI WA BARABARA YA NYAMUSWA – BULAMBA (KM

56.4) 

MARA 

26.

AFYA

MRADI WA KUBORESHA HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA WA MARA – KWANGWA 

MARA 

27.

ELIMU

UJENZI WA CHUO CHA UFUNDI STADI (VETA) CHA WILAYA YA BUTIAMA KUPITIA PROGRAMU YA ESPJ

MARA 

28.

USTAWI        WA

JAMII

UJENZI NA UPANUZI WA CHUO CHA MAENDELEO YA WANANCHI (FDC)

MARA 

29.

BIASHARA

UJENZI WA SOKO LA KISASA TARIME

MARA 

30.

MAJI

MRADI WA MAJI SUGUTI/KISENYI/KWIKONERO

MARA 

31.

MAJI

MRADI WA MAJI – IRAMBA

MARA 

32.

MAJI

UKARABATI WA MRADI WA MAJI KENYANA - NYAMITITA

MARA 

33.

MAJI

MRADI WA UBORESHAJI WA HUDUMA YA MAJI BUNDA

MARA 

34.

MAJI

UJENZI WA JENGO LA UTAWALA TARIME MJI

MARA 

35.

UTAWALA BORA

UJENZI WA KITUO CHA POLISI DARAJA A – TARIME RORYA, MARA

MARA 

36.

UTAWALA BORA

MRADI WA UJENZI WA OFISI YA KAMANDA WA POLISI

MARA 

 

NA.

SEKTA

MRADI

MKOA

 

 

 

MKOA WA MARA

 

37.

UTAWALA BORA

UJENZI WA MAHAKAMA YA WILAYA BUTIAMA

MARA 

38.

AFYA

MRADI WA UJENZI WA KITUO CHA AFYA MKUNWA

MTWARA

39.

AFYA

MRADI WA UJENZI WA JENGO LA WAGONJWA MAHUTUTI (ICU)

MTWARA

40.

AFYA

MRADI WA UJENZI WA HOSPITALI YA RUFAA YA KANDA YA KUSINI MTWARA

MTWARA

41.

ELIMU

MRADI WA UJENZI WA SHULE YA SEKONDARI YA MFANO LIKOMBE

MTWARA

42.

KILIMO

UJENZI WA GHALA NA MIUNDOMBINU NANYUMBU

MTWARA

43.

MAJI

MRADI WA MAJI - CHEMCHEM

MTWARA

44.

MAJI

MRADI WA MAJI NAMANJELE - NJUMBULI

MTWARA

45.

MAJI

MRADI WA MAJI MKULULU

MTWARA

46.

MAJI

MRADI WA MAJI NAMATUNU

MTWARA

47.

MAJI

MRADI WA MAJI KILOMBERO

MTWARA

48.

MAJI

MRADI WA CHUJIO LA MAJI

MTWARA

49.

NISHATI

MRADI WA USAMBAZAJI WA GESI ASILIA KATIKA MIKOA

YA DAR ES SALAAM, MTWARA, LINDI NA PWANI

(MTWARA)

MTWARA

50.

UJENZI

UJENZI NA UPANUZI WA KIWANJA CHA NDEGE MTWARA

MTWARA

51.

AFYA

MRADI WA UJENZI WA HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA WA NJOMBE AWAMU YA PILI

NJOMBE

52.

ELIMU

MRADI WA CHUO CHA MAENDELEO YA WANANCHI NJOMBE

NJOMBE

53.

MAJI

MRADI WA MAJI KIJIJI CHA NYOMBO

NJOMBE

54.

MAJI

MRADI WA MAJI KIBENA HOWARD

NJOMBE

55.

MAJI

MRADI WA MAJI IGULA

NJOMBE

56.

UJENZI

BARABARA YA NJOMBE – MAKETE – ISYONJE (KM 157.4): KIPANDE MORONGA – MAKETE (KM 53.5)

NJOMBE

57.

UTAWALA BORA

MRADI WA UJENZI WA MAHAKAMA YA WILAYA YA NJOMBE

NJOMBE

58.

UTAWALA BORA

UJENZI WA OFISI YA MKUU WA MKOA NJOMBE

NJOMBE

59.

MAJI

MRADI WA MAJI IDENDE - UNENAMWA

NJOMBE

60.

AFYA

UBORESHAJI WA HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA WA RUKWA

RUKWA

61.

MAJI

MRADI WA MAJI KANOGE II

RUKWA

62.

MAJI

MRADI WA UJENZI WA BWAWA LA MAJI IKOZI

RUKWA

63.

MAJI

MRADI WA MAJI MSANDAMUUNGANO

RUKWA

64.

MAJI

UJENZI WA BWAWA LA MAJI KIJIJI CHA KALEPULA

RUKWA

65.

MAJI

UJENZI WA BWAWA LA MAJI KILEWANI

RUKWA

66.

MAJI

MRADI WA MAJI MATAI

RUKWA

67.

MAJI

MRADI WA MAJI ISALE

RUKWA

68.

MAJI

MRADI WA MAJI MATALA

RUKWA

69.

MAJI

MRADI WA MAJI KASU

RUKWA

70.

MAJI

HOSPITALI YA WILAYA YA SUMBAWANGA - MTOWISA

RUKWA

71.

MAJI

MRADI WA MAJI MUZE GROUP

RUKWA

72.

NISHATI

MRADI WA USAMBAZAJI WA UMEME VIJIJINI (AWAMU

YA PILI YA MRADI WA REA III) KATIKA MKOA WA

RUKWA

RUKWA

73.

UJENZI

BARABARA YA SUMBAWANGA – MATAI – KASANGA (KM 112)

RUKWA

74.

ELIMU

MRADI WA CHUO CHA MAENDELEO YA WANANCHI MPUTA

RUVUMA

75.

ELIMU

CHUO CHA MAENDELEO YA WANANCHI - MBINGA

RUVUMA

76.

KILIMO

USIMAMIZI ENDELEVU WA RASILIMALI ZA MADINI – SMMRP: KITUO CHA UMAHIRI SONGEA

RUVUMA

77.

KILIMO

MRADI WA UJENZI WA GHALA LA KUDHIBITI SUMUKUVU

RUVUMA

78.

KILIMO

MRADI WA KUONGEZA THAMANI KWA MAZAO YA MISITU – FORVAC (RUVUMA)

RUVUMA

79.

MAJI

MRADI WA MAJI RUVUMACHINI

RUVUMA

 

NA.

SEKTA

MRADI

MKOA

 

80.

MAJI

MRADI WA MAJI MANGAMAO

RUVUMA

81.

MAJI

MRADI WA MAJI LIULI GROUP

RUVUMA

82.

MAJI

MRADI WA MAJI MABUNI

RUVUMA

83.

UCHUKUZI

MRADI WA UKARABATI NA UJENZI WA KIWANJA CHA NDEGE SONGEA

RUVUMA

84.

UJENZI

UJENZI WA BARABARA MBINGA - MBAMBA BAY KWA KIWANGO CHA LAMI (KM 66)

RUVUMA

85.

UJENZI

UJENZI WA BARABARA YA KITAI - LITUHI KM 84.5

RUVUMA

86.

UJENZI

UJENZI WA BARABARA YA MWIGUMBI – MASWA (KM

50.3)

SIMIYU

87.

VIWANDA

UJENZI WA VIWANDA VYA CHAKI NA VIFUNGASHIO KATIKA HALMASHAURI YA WILAYA YA MASWA.

SIMIYU

88.

ELIMU

UJENZI WA VYUMBA VYA MADARASA BIASHARA SEKONDARI (EP4R)

SIMIYU

89.

ELIMU

UJENZI WA VYUMBA VYA MADARASA BARIADI SEKONDARI (EP4R)

SIMIYU

90.

KILIMO

MRADI WA KUDHIBITI SUMUKUVU

SIMIYU

91.

MAJI

MRADI WA MAJI NYAMALAPA

SIMIYU

92.

MAJI

MRADI WA MAJI LAMADI – MKULA

SIMIYU

93.

MAJI

MRADI WA MAJI NGULYATI – NYAMSWA

SIMIYU

94.

MAJI

MRADI WA UBORESHAJI WA HUDUMA ZA MAJI – MASWA

SIMIYU

95.

UJENZI

BARABARA YA MASWA BYPASS (KM 11.3)

SIMIYU

96.

UTAWALA BORA

UJENZI WA KITUO CHA POLISI DARAJA B – BARIADI - SIMIYU

SIMIYU

97.

VIWANDA

KIWANDA CHA HESTER BIOSCIENCE AFRICA

PWANI

98.

VIWANDA

KIWANDA CHA VIUADUDU - TANZANIA BIOTECH PRODUCTS LIMITED

PWANI

99.

VIWANDA

MRADI WA KUUNGANISHA MATREKTA YA URSUS

PWANI

100.

VIWANDA

MRADI WA KUUNGANISHA MAGARI – PWANI

PWANI

101.

VIWANDA

KIWANDA CHA KUTENGENEZA VIFUNGASHIO (GLOBAL PACKAGING LTD)

PWANI

102.

VIWANDA

MRADI WA SHAMBA LA MPIRA – KALUNGA

MOROGORO

103.

VIWANDA

KIWANDA CHA NYANZA GLASS

MWANZA

104.

VIWANDA

MRADI WA CHUMA GHAFI NA MAKAA YA MAGANGA MATITU NA MGODI WA KATEWAKA

NJOMBE

105.

VIWANDA

MRADI WA  CHUMA LIGANGA NA MAKAA YA MAWE MCHUCHUMA

NJOMBE

106.

VIWANDA

MRADI WA MAKAA YA MAWE NGAKA

RUVUMA

107.

VIWANDA

MRADI WA MAJENGO - DAR ES SALAAM

DAR ES SALAAM

108.

VIWANDA

ETC CARGO LIMITED

DAR ES SALAAM

109.

VIWANDA

SHAMBA LA MPIRA - KIHUHWI

TANGA

110.

VIWANDA

MRADI WA MAGADI SODA KATIKA BONDE LA ENGARUKA

ARUSHA

111.

VIWANDA

KIWANDA CHA KUTENGENEZA MATAIRI (GTEA)

ARUSHA

112.

VIWANDA

KIWANDA CHA MASHINE NA VIPURI (KMTC)

KILIMANJARO

113.

UJENZI

BARABARA YA KISARAWE – MANEROMANGO (KM 54):

SEHEMU YA KIJIJI CHA KISANGA HADI SUNGWI (KM

3.435) 

PWANI

114.

UJENZI

BARABARA YA NACHINGWEA – RUANGWA - NANGANGA (106KM): LOT 2: RUANGWA - NANGANGA (KM 53.2)

LINDI

115.

UJENZI

MRADI WA UJENZI WA BARABARA YA KALIUA – MALAGARASI – ILUNDE (KM 156): KIPANDE CHA

KAZILAMBWA – CHAGU KM 36

TABORA

116.

TAMISEMI

MRADI WA UJENZI WA JENGO LA UTAWALA LA HALMASHAURI YA WILAYA YA NYANG’HWALE

GEITA

117.

TAMISEMI

MRADI WA UJENZI WA JENGO LA UTAWALA LA HALMASHAURI YA WILAYA YA MBOGWE

GEITA

118.

TAMISEMI

MRADI WA UJENZI WA JENGO LA HALMASHAURI YA WILAYA YA GEITA

GEITA

119.

TAMISEMI

UJENZI WAJENGO LA UTAWALA HALMASHAURI YA

SHINYANGA

 

NA.

SEKTA

MRADI

MKOA

 

 

 

MANISPAA YA SHINYANGA

 

120.

TAMISEMI

MRADI WA UJENZI WA SOKO LA WAFANYA BIASHARA WADOGO (MACHINGA) – NYAMAGANA MWANZA

MWANZA

121.

TAMISEMI

MRADI WA UJENZI WA JENGO LA UTAWALA HALMASHAURI YA WILAYA YA SENGEREMA

MWANZA

122.

MAJI

MRADI WA UBORESHAJI WA MFUMO WA MAJI NYANKANGA - GEITA

GEITA

123.

MAJI

MRADI WA UJENZI WA TANKI NA ULAZAJI WA BOMBA – KIBONDO

KIGOMA

124.

TAMISEMI

MRADI WA UJENZI WA JENGO LA UTAWALA LA HALMASHAURI YA WILAYA YA KAKONKO

KIGOMA

125.

TAMISEMI

MRADI WA UJENZI WA JENGO LA UTAWALA LA HALMASHAURI YA WILAYA YA KARAGWE

KAGERA

126.

MAJI

MRADI WA MAJI MATENDO – SAMWA

`

127.

MAJI

MRADI WA MAJI NYAMIGERE - KALENGE

KAGERA

128.

MAJI

MRADI WA MAJI BUTEMBO

KAGERA

129.

MAJI

MRADI WA UJENZI WA KITEKEO KIPYA CHA MAJI – KIGOMA MJINI

KIGOMA

130.

MAJI

MRADI WA UCHIMBAJI WA VISIMA VIREFU VINNE (4)

KATIKA VIJIJI VYA CHEKENYA, KABULANZWILI, KITEMA

NA RUSESA

KIGOMA

131.

MAJI

MRADI WA MAJI KAMENA

GEITA

132.

MAJI

MRADI WA UTAFITI WA MAJI CHINI YA ARDHI NA UCHIMBAJI WA VISIMA VIREFU 6

GEITA

133.

MAJI

MRADI WA MAJI BISHESHE

KAGERA

134.

MAJI

MRADI WA UPANUZI WA MTANDAO WA MAJISAFI BUKOBA MJINI AWAMU YA PILI

KAGERA

135.

MAJI

MRADI WA MAJI BUSANDA

GEITA

136.

MAJI

UJENZI WA MRADI WA MAJI BUHIGWE, KAVOMO, MULERA NA BWEGA BUHIGWE, KIGOMA

KIGOMA

137.

MAJI

UJENZI WA MRADI WA MAJI KYAMYORWA, KAGERA

KAGERA

138.

MAJI

UJENZI WA MRADI WA MAJI LUGUNGA - LUHALA, GEITA

GEITA

139.

MAJI

MRADI WA MAJI CHILAMBO

KIGOMA

140.

MAJI

UJENZI WA MRADI WA MAJI NJOOMULOLE, KANYONZA NA KINONKO KIGOMA

KIGOMA

141.

MAJI

MRADI WA MAJI KATARE

KAGERA

142.

MAJI

MRADI WA UJENZI WA TANKI LA MAJI NA UPANUZI WA MTANDAO WA MAJI - MJI WA KIGOMA

KIGOMA

143.

MAJI

MRADI WA MAJI NYAKASIMBI

KAGERA

144.

MAJI

MRADI WA MAJI KITOLERWA – ISHOZI

KAGERA

145.

MAJI

MRADI WA MAJI WA KAGURUKA NA SOGEENI KWILIBA

KIGOMA

146.

MAJI

MRADI WA MAJI NYAKASANDA - KIBONDO

KIGOMA

147.

MAJI

MRADI WA UBORESHAJI WA MIUNDOMBINU YA MAJISAFI - CHATO

GEITA

148.

MAJI

UJENZI WA MRADI WA MAJI MSONGA, GEITA

GEITA

149.

MAJI

UJENZI WA MRADI WA MAJI KIZIGUZIGU KAKONKO, KIGOMA

KIGOMA

150.

MAJI

 UJENZI WA MRADI WA MAJI NKOME, KATOMA, NYAMBOGE, NZERA NA LWEZERA, GEITA

GEITA

151.

MAJI

UKARABATI WA MRADI WA MAJI YA MWANSUNGH’HO - MWASHIKU

TABORA

152.

MAJI

UPANUZI WA MRADI WA MAJI KUTOKA ZIWA VICTORIA KWENDA KATA ZA BUKENE NA MWAMALA.

TABORA

153.

MAJI

UPANUZI WA MRADI WA WA MAJI WA ZIWA VICTORIA TOKA ZIBA KWENDA NKINGA.

TABORA

154.

MAJI

UPANUZI WA MRADI WA MAJI KUTOKA MTANDAO WA 

ZIWA VICTORIA KWENDA KATIKA VIJIJI VYA MAYOMBO, KAGERA, MPUTI, HIARIMOYO, KINAMAGI, MBUYUNI NA VUMILIA.

TABORA

 

NA.

SEKTA

MRADI

MKOA

 

155.

MAJI

UPANUZI WA MRADI WA MAJI KUTOKA ZIWA VICTORIA KWENDA KATIKA VIJIJI VYA KONGO NA UHURU MBITI

TABORA

156.

MAJI

UJENZI WA MRADI WA MAJI MWANGONGO, SESEKO NA NGUNDANGALI AWAMU YA II

SHINYANGA

157.

MAJI

MRADI WA UPANUZI WA MRADI WA MAJI WA

NGONGWA KITWANA KWENDA VIJIJI VYA WENDELE NA

TUMAINI

SHINYANGA

158.

MAJI

UJENZI WA MRADI WA MAJI MWANGONGO, SESEKO NA NGUNDANGALI AWAMU YA I

SHINYANGA

159.

MAJI

MRADI WA UPANUZI WA MRADI WA MAJI WA MHANGU

ILOGI KWENDA VIJIJI VYA BUGARAMA, ILOGI,

LWABAKANGA NA KAKOLA NA.9

SHINYANGA

160.

MAJI

MRADI WA UPANUZI WA MRADI WA MAJI WA

ZONGOMELA KWENDA VIJIJI VYA NYANDEKWA, LOWA,

BUDUBA NA BUJIKA

SHINYANGA

161.

MAJI

MRADI WA UPANUZI WA MRADI WA MAJI WA

KAGONGWA ISAKA KWENDA VIJIJI VYA MWALUGULU,

KILIMBU, JANA, BUTONDOLO NA ITOGWANHOLO

SHINYANGA

162.

MAJI

MRADI WA KUSAMBAZA MAJI MAGANZO-MASAGALA

SHINYANGA

163.

MAJI

UCHIMBAJI WA VISIMA VIREFU VITATU VIJIJI VYA IPEJA, ITILIMA NA NHOBOLA

SHINYANGA

164.

MAJI

UKARABATI WA VISIMA KATIKA KATA ZA BUKENE, USULE, ILOLA, IMESELA, MWANTINI, NYAMALOGO, LYABUKANDE NA USANDA.

SHINYANGA

165.

MAJI

MRADI WA MAJI MASENGWA AWAMU YA PILI.

SHINYANGA

166.

MAJI

UPANUZI WA MTANDAO WA USAMBAZAJI WA MAJI KWENDA DIDIA, MWANUBI NA ISELEMAGAZI

SHINYANGA

167.

MAJI

UPANUZI WA MRADI WA MAJI KUTOKA MURITI-IHEBO KWENDA KIJIJI CHA IGONGO

MWANZA

168.

MAJI

UJENZI WA MRADI WA MAJI BUPANDWA

MWANZA

169.

MAJI

MRADI WA MAJI WA KARUMO – SENGEREMA

MWANZA

170.

MAJI

MRADI WA MAJI KIGONGO

MWANZA

171.

MAJI

UJENZI WA MIRADI WA MAJI CHIFUNFU

MWANZA

172.

MAJI

UPANUZI WA MRADI WA MAJI UVINZA

KIGOMA

173.

MAJI

UPANUZI WA MRADI WA MAJI KASELA KATIKA  WILAYA YA SENGEREMA

MWANZA

174.

ELIMU

MRADI WA UJENZI WA SHULE YA SEKONDARI MWILAMVYA MPYA

KIGOMA

175.

ELIMU

MRADI WA UJENZI WA SHULE YA SEKONDARI KITOBO

KAGERA

176.

ELIMU

MRADI WA UJENZI WA SHULE YA MSINGI TRM - NYAKANAZI

KAGERA

177.

ELIMU

MRADI WA MADARASA NA MABWENI KATIKA SHULE YA SEKONDARI NYAKASIMBI - KARAGWE

KAGERA

178.

ELIMU

MRADI WA UJENZI WA SHULE YA SEKONDARI (SEQUIP) – KAHIMBA

KIGOMA

179.

ELIMU

MRADI WA UJENZI WA UJENZI WA SHULE YA WASICHANA KAGERA RIVER - KARAGWE

KAGERA

180.

ELIMU

MRADI WA UJENZI WA SHULE YA SEKONDARI - MIZANI

KAGERA

181.

AFYA

MRADI WA UJENZI YA HOSPITALI YA RUFAA - BUKOMBE

GEITA

182.

AFYA

MRADI WA UJENZI WA HOSPITALI YA WILAYA KIBONDO

KIGOMA

183.

AFYA

MRADI WA UJENZI WA KITUO CHA AFYA IPARAMASA

GEITA

184.

AFYA

MRADI WA UKAMILISHAJI WA UJENZI WA ZAHANATI YA MUBABA

KAGERA

185.

AFYA

MRADI WA UJENZI WA KITUO CHA AFYA KANYIGO

KAGERA

186.

AFYA

MRADI WA UJENZI WA KITUO CHA AFYA KASHAI – BUKOBA MC

KAGERA

187.

AFYA

MRADI WA UKAMILISHAJI WA UJENZI WA ZAHANATI YA IGURWA

KAGERA

188.

AFYA

UMALIZIAJI WA ZAHANATI YA MAKOBELO

TABORA

MKOA NA.        SEKTA MRADI  

189. AFYA UJENZI WA JENGO LA MAMA NA MTOTO KATIKA HOSPITALI YA WILAYA YA NZEGA.       TABORA

UKAMILISHAJI WA JENGO LA ZAHANATI YA KIJIJI CHA            SHINYANGA 190. AFYA      MWASHIGINI-KATA YA MWAKATA.

                                   UKAMILISHAJI WA UJENZI WA ZAHANATI KATIKA KIJIJI      MWANZA

191.     AFYA        CHA LUHAJA

192.     AFYA        UJENZI WA HOSPITALI YA WILAYA MISUNGWI          MWANZA

                                   MRADI WA UJENZI WA OFISI ZA KITUO CHA UTAFITI         KIGOMA

193.     KILIMO     WA KILIMO – TARI - KIHINGA, KIGOMA

MRADI WA UJENZI WA KITUO CHA UTAFITI WA         KIGOMA 194. KILIMO       KAHAWA – TACRI, MWAYAYA

195.                                            KILIMO   MRADI WA UJENZI WA SKIMU YA UMWAGILIAJI ULYANYAMA – SIKONGE TABORA           TABORA

                                   MRADI WA UJENZI WA OFISI YA MAKAO MAKUU YA           TABORA

196.                                            BODI YA TUMBAKU

197.                                            KILIMO   UJENZI WA BWAWA LA GOWEKO    TABORA

198.                                            UKARABATI KATIKA WILAYA YA NZEGA TABORA WA SKIMU YA UMWAGILIAJI YA IDUDUMO           TABORA

                                   MRADI WA UJENZI WA WA MIUNDOMBINU YA                   TABORA

199.                                            KILIMO   UMWAGILIAJI YA KILIMI

MRADI WA UJENZI WA WA SKIMU YA UMWAGILIAJI YA           MOROGORO 200. KILIMO MGONGOLA - MVOMERO

201.     KILIMO     MRADI WA UJENZI WRUDEWA - KILOSA      A WA SKIMU YA UMWAGILIAJI YA   MOROGORO

                                   UJENZI WA MIUNDOMBINU YA UMWAGILIAJI KATIKA         MWANZA

202.     KILIMO     SKIMU YA MAGULUKENDA BUCHOSA - SENGEREMA

203.     KILIMO     UJENZI WA BWAWA LA NYIDA        SHINYANGA

204.     NISHATI    MRADI WA KUZALISHA UMEME KWA KUTUMIA MAJI WA JULIUS NYERERE - MW 2,115     PWANI

205.     UVUVI       UJENZI WA BANDARI YA UVUVI KILWA        LINDI

                                   MRADI WA UJENZI WA MIUNDOMBINU YA MABASI             DAR ES SALAAM

206.     UJENZI     YAENDAYO HARAKA (BRT) - AWAMU YA II

                                   UJENZI WA KIWANDA NA UENDELEZAJI WA SHAMBA LA      MOROGORO

207.     VIWANDA MIWA MKULAZI – MBIGIRI ESTATE

DAR ES SALAAM,

                                   MRADI WA UJENZI WA RELI YA KATI KWA KIWANGO          MOROGORO, DODOMA,

208.     UCHUKUZI             CHA KIMATAIFA (SGR)      SINGIDA, TABORA,

SHINYANGA NA MWANZA

                                   MRADI KUFUFUA SHIRIKA LA NDEGE TANZANIA (AIR          DAR ES SALAAM

209.     UCHUKUZI             TANZANIA COMPANY LIMITED – ATCL)

210.     UJENZI     MRADI WA U(KM 3.2) NA BARABARA UNGANISHI (KM 1.66) JENZI WA DARAJA LA KIGONGO – BUSISI        MWANZA

MRADI WA UJENZI WA BOMBA LA MAFUTA GHAFI      TABORA 211. NISHATI      AFRIKA MASHARIKI (EACOP)

 

 

 





Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post