MCHUNGAJI MATATANI KWA KUMBAKA MUUMINI WA KANISA LAKE


Mchungaji mmoja kutoka katika Kaunti ya Embu nchini Kenya amefikishwa mahakamani Jumatatu Juni 5,2023 kwa tuhuma za kumbaka muumini wa kanisa lake.

Pasta Benson Mwaniki Njuki wa Kanisa la Full Gospel Karurina, ameshtakiwa kwa kumbaka binti mwenye umri wa miaka 22, mnamo Juni 1,2023  katika Kijiji cha Karurina, Embu Magharibi.

Njuki alishtakiwa kwa kuingiza kiwiliwili chake ndani ya mwanamke huyo na pia kumshika sehemu za siri bila idhini yake.

 Kulingana na stakabadhi za mahakama, inasemekana kuwa mwanamke huyo alikuwa katika kikao cha maombi katika kanisa la Njuki, akiwa amepiga magoti, wakati mchungaji huyo alimbaka.

Mahakama ilielezwa kwamba wakati wote huo, mchungaji huyo alikuwa amevaa mavazi yake rasmi ya kanisa.

 Jaribio lake la kupiga mayowe lilisitishwa baada ya mshtakiwa kumshinda nguvu na kumfunga mdomo. 

Mwanamke huyo alimsimulia mama yake tukio hilo na alipelekwa katika Hospitali ya Rufaa ya Embu Level V ambapo ilithibitishwa Njuki alimuingiza kiwiliwili chake na fomu ya P3 na fomu ya Huduma ya baada ya Kumbaka (PRC) zilijazwa. 

Tukio hilo liliripotiwa katika Kituo cha Polisi cha Itabua, ambapo mchungaji huyo alikamatwa. 

Njuki alikana mashtaka hayo alipojitokeza mbele ya Hakimu Mkuu Mwandamizi wa Embu, Robert Gitau.

 Aliachiliwa kwa dhamana ya KSh.100,000 na mdhamini mwenye kiasi sawa au dhamana ya pesa taslimu ya KSh.50,000. 

Kesi hiyo itatajwa tena mnamo Juni 11,2023.

Chanzo - Tuko News

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post