IDADI YA WALIOUAWA UGANDA YAONGEZEKATaarifa zinaonyesha kuwa idadi ya watu waliofariki katika shambulizi la shule mjini Mpondwe magharibi mwa Uganda imeongezeka na kufikia 40, huku idadi ya waliotekwa nyara na waasi bado haijafahamika mpaka sasa
Idadi ya watu waliouawa katika shambulio lililofanywa na waasi katika shule moja nchini Uganda, ambayo ipo karibu na mpaka wa DRC.
Taarifa zinaonyesha kuwa idadi ya watu waliofariki katika shambulizi la shule mjini Mpondwe magharibi mwa Uganda imeongezeka na kufikia 40, huku idadi ya waliotekwa nyara na waasi bado haijafahamika mpaka sasa.

Meya wa Mpondwe-Lhubiriha Selevest Mapoze ameliambia shirika la habari la Associated Press kuwa waliouawa ni pamoja na wanafunzi, mlinzi mmoja wa shule na watu wawili amabao ni wakazi wa maeneo hayo waliokuwa nje ya shule hiyo.

“Wanafunzi waliungua baada ya waasi kuteketeza bweni, wengine walipigwa risasi na wengine kukatwakatwa na mapanga hata hivyo Police hawakuelezea kwa upana tukio hilo,” amesema Mapoze.

Awali polisi nchini Uganda walisema watu 25 walifariki katika tukio hilo na wengine nane walikua na hali mbaya katika Hospitali ya Bwera huku wakililaum kundi la Uganda la Allied Democratic Forces (ADF) lenye makao yake mashariki mwa DRC kwa shambulio hilo.

Msemaji wa polisi wa taifa Fred Enanga amesemwa bweni lilichomwa na duka la chakula kuporwa katika shambulio dhidi ya shule hiyo inayomilikiwa na watu binafsi iliyoko katika wilaya ya Kasese nchini Uganda, takriban kilomita mbili kutoka mpaka wa DRC.

Enanga amesema jeshi na vitengo vya polisi vilikuwan katika msako mkali wa washambuliaji ambao walikimbia kuelekea Hifadhi ya Kitaifa ya Virunga kwenye mpaka wa DR Congo.

“Wanajeshi wa Uganda ndani ya Kongo wanaendelea kuwafatilia waaso ili kuwaokoa waliotekwa nyara," amesema.

Joe Walusimbi, afisa anayemwakilisha Rais wa Uganda Yoweri Museveni amesema, mamlaka inajaribu kuthibitisha idadi ya walipoteza maisha na wale waliotekwa nyara.

CHANZO-MWANANCHI.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments